Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

NSSF Stakeholders meeting - postponed.


jinsi Mayweather alivyomshinda Pacquiao

$
0
0
 Bondia wa Kimarekani,Floyd Mayweather Jr akimrushia konde kali mpinzani wake, Manny Pacquiao wa Philipines wakati wa mpambano wao wa kihistoria na uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na watu wengi Duniani kote, uliopigwa mapema leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa MGM Grand Garden Arena, jijini Las Vegas, Marekani. Bondio Floyd Mayweather ameshinda mchezo huo kwa point 118-110, 116-112, 116-112 kutoka kwa waamuzi wa mchezo huo na kunyakuwa mkanda wa WBO huku akiifanya rekodi yake ya kutopigwa kufikia michezo 48.
Mchezo ulikuwa ni mkali sana na Mabondia wote walikuwa wakirushiana makonde kwa zamu.
haya angalieni wenyewe hasa wale wanaosema jamaa kabebwa.
Mabondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao wakifurahi pamoja mara baada ya mpambano wao wa kihistoria uliopigwa mapema leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa MGM Grand Garden Arena, jijini Las Vegas, Marekani.

Bondia Floyd Mayweather Jr akiwa na mikanda yake na tuzo aliyoshinda katika michezo mbali mbali 

Mwijage afanya kikao na wakandarasi wa miradi ya REA

$
0
0
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage amekutana na Mameneja Tanesco wa mikoa na wilaya katika Nyanda za Juu Kusini Magharibi pamoja na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA ya usambazaji umeme vijijini, Awamu ya pili katika kanda hiyo ili kujadili utekelezaji wa miradi hiyo ya umeme.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (kulia) akizungumza na Mameneja Tanesco wa mikoa na wilaya katika Nyanda za Juu Kusini Magharibi pamoja na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA ya usambazaji umeme vijijini, Awamu ya pili katika kanda hiyo (hawapo pichani). Katikati ni Meneja Mwandamizi wa Tanesco Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Salome Nkondola na kushoto ni Kaimu Meneja wa Tanesco katika mkoa wa Mbeya, Magwila Mbalamwezi.
Meneja Tanesco katika wilaya ya Mbozi mkoa wa Mbeya, Ephraim Cheyo (aliyesimama) akieleza kuhusu utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme vijijini katika wilaya yake, wa kwanza kushoto ni Meneja Tanesco, wilaya ya Kyela, George Fulla na wa pili kushoto Meneja Tanesco katika wilaya ya Mbinga, Kanuti Punguti. Maelezo hayo aliyatoa wakati wa kikao kilicholenga kujadili utekelezaji wa miradi ya usambazaji vijijini katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi kilichofanyika jijini Mbeya.
Mameneja Tanesco wa mikoa na wilaya katika Nyanda za Juu Kusini Magharibi pamoja na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA ya usambazaji umeme vijijini, Awamu ya pili katika kanda hiyo wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (aliyesimama) katika kikao kilichofanyika jijini Mbeya ili kujadili utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme vijijini katika kanda hiyo.
Mameneja Tanesco wa mikoa na wilaya katika Nyanda za Juu Kusini Magharibi, wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA ya usambazaji umeme vijijini Awamu ya Pili katika kanda hiyo pamoja na watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika jijini Mbeya ili kujadili utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme vijijini katika kanda hiyo.

Floyd Mayweather amdunda Manny Pacquiao kwa pointi kibao

$
0
0
Na Sultani Kipingo
Floyd Mayweather ameibuka mshindi katika pambano la karne baada ya kumdunda Manny Pacquiao kwa pointi nyingi alfajiri ya leo huko Las Vegas, Marekani. 
 Mmarekani Mayweather, 38, ametumia mbinu za hali ya juu za kujihami dhidi ya mpinzani wake Mfilipino, akifanya marekebisho muhimu kwenye raundi za awali kabla ya kupotea ulingoni. 
 Mayweather, ambaye ameongeza taji la WBO la uzito wa welterweight juu ya mataji ya WBC na WBA aliyonayo, alipewa ushindi kwa majaji watatu kuamua kapiga 118-110, 116-112 na 116-112. 
Kwa ushindi huo, Mayweather amedhihirisha yeye ni bondia bora wa ngumi-kwa-ngumi wa zama hizi. Bingwa huyu anayeshikilia mataji matano sasa hajashindwa katika mapambano 48 katika miaka 19. 
Akiwa bingwa wa mataji sita, Pacquiao, 36, anaishia ushindi wa mapambano 57, kapigwa mara sita na droo mbili.
 Tiketi kwa mpambano huo wa karne ziliuzwa kwa dola £232,000 na mashabiki wa Marekani walicha dola 66 kuangalia kwenye luninga - kama ilivyokuwa duniani kote.
 Na mshindi kwa pointi 118-110, 116-112 na 116-112... ni Mayweather!!!
Floyd Mayweather alitamba ulingoni hadi dakika za mwisho...
 Floyd Mayweather akidunda Manny Pacquiao
Floyd Mayweather

MAZOEZI YANAJENGA AFYA – IGP MANGU

$
0
0
  Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),Ernet Mangu  akimpa mkono mshindi wa  Kwanza wa Riadha  ya Half May Day Marathon katika kundi la Wanaume,Alphonce Felix wa Club ya Holili,Kilimanjaro yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, wanaoshuhudia ni  Mkurugenzi Mkuu wa Boa  Bank Ammish Owusu, mshindi huyo amejipatia kitita cha Sh. 1100,000.
.Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),Ernest Mangu akimpa mkono mshindi wa  Kwanza  wa  Riadha ya   Half May Day Marathon katika kundi la wanawake,Natalie Elisante Arusha) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, wanaoshuhudia ni Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam (CP),Suleiman Kova ,mshindi huyo amejipatia kitita cha Sh. 1100,000.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),Ernest Mangu akimpa mkono mshindi wa Pili  wa  Riadha ya Half  May Day Marathon katika kundi la wanaume ,Joseph Panga (Arusha) yaliyofanyika leo katika viwanja Polisi Ostebay jijini Dar es Salaam wanaoshuhudia ni ,Mkurugenzi wa Benki ya Boa,Ammish Owusu .

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),Ernest Mangu  amesema michezo inajenga ukakamavu wa mwili hivyo kwa washiriki wa may day marathon wamefanyoa  afya.

Mangu ameyasema aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati  mashindano ya Half May Day Marathon yaliyofanyika katika viwanja vya Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam ,aliwapongeza washindi na kutaka waongeze juhudi ili waweze kufika mbali katika mchezo wa riadha.  Washindi wa May Marathon wamepongeza waandaji wa mashindano hayo kwani yanaongeza chachu ya kupenda mchezo huo.

Washindi hao wameyasema hayo katika mashindano  ya Half May Day Marathon yaliyofanyika katika viwanja vya Polisi Oysterba jijini Dar es Salaam ,wamesema kuwa mashindano hayo yameamsha kupenda mchezo wa riadha kuendelea kupendwa.

Akizungumza  na mshindi wa kwanza katika upande wa wanaume ,Alphonce Felix amesema ameshinda katika mashindano hayo kwani alijituma kutokana na mazoezi ya mara kwa mara na kuwataka watu wengine kushiriki mchezo huo kutokana na kujenga afya zao.

Amesema riadha ni mchezo mmoja mzuri kutokana na utaratibu kujpangia mazoezi  kwa ni riadhia ni ajira kama michezo mingine.

Mshindi wa Kwanza  kwa upande wa Wanawake ,Natalie Elisante (Arusha)amesema amewataka wasichana kushiriki katika riadha mbalimbali kwani wasichana na wanawake wanaoshiriki mchezo huo ni wachache ikilinganishwa na idadi yetu.

WAZAZI WACHANGIA SHULE YA UFUNDI IFUNDA

$
0
0
 Mdau wa maendeleo, Jackson Kiswaga (mwenye skafu) akiwakabidhi moja ya mabati 50 wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ufundi ya Ifunda kwa ajili ya ukarabati wa jengo la taaluma na nidhamu lilounguamwaka 2013 katika shule hiyo.(picha na Denis Mlowe).
 Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini Jackson Kiswaga akizungumza wanafunzi na wazazi wa shule ya shule ya sekondari ya Ufundi ya Ifunda.
 Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini Jackson Kiswaga akikabidhi cheti kwa mhitimu wa shule ya shule ya sekondari ya Ufundi ya Ifunda kidato cha sita.(picha na Denis Mlowe).
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA 

Simba yaifunga Azam FC 2-1

$
0
0
 Mshambuliaji wa Simba, Ramadhani Singano 'Messi" akishangilia kwa staili ya aina yake baada ya kuipatia timu yake bao la pili.
Beki wa Azam FC, Agrey Moris akimiliki mpira mbele ya mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
Raha ya ushindi. 

PINDA ASHIRIKI IBADA YA UZINDUZI WA MAKAO MAKUU YA JIMBO LA MASHARIKI YA KANISA LA MORAVIAN TANZANIA

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika uzinduzi wa Makao Makuu ya Jimbo la Mashariki la Kanisa la Moravian Tanzania eneo la Chamazi jijini Dar es salaam Mei 3, 2015 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MKUU AKABIDHI MADAWATI 45 KIEMBESAMAKI

$
0
0
*Aahidi kuchangia madawati 135 na viti vyake

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameahidi kuchangia madawati 135 na viti vyake kwenye shule ya msingi Kiembesamaki iliyoko wilaya ya Magharibi mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni mwitikio wa maombi aliyopewa na shule hiyo.

Ametoa ahadi hiyo jana (Jumamosi, Mei 2, 2015), wakati akikabidhi msaada wa madawati 45 na viti vyake yenye thamani ya sh. milioni 3.83/- yaliyotolewa na kampuni ya Jambo Plastics ya Dar es Salaam ili kupunguza uhaba wa madawati katika shule za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

“Tatizo la madawati ni la kitaifa… Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali ametuambia kwamba haya ya leo yatatosha darasa moja tu na bado kuna mengine matatu hayana kabisa madawati. Changamoto iliyopo hivi sasa ni kwamba haya madawati yatagawanywa vipi wakati watoto wengine bado hawana mahali pa kukaa?” alihoji Waziri Mkuu.

“Ili kuondoa tatizo hilo, mimi nitachangia madawati yaliyobakia kwa madarasa hayo matatu ili watoto wetu wakae vizuri, wazingatie masomo yao na pia wawe na miandiko mizuri,” alisema huku akishangiliwa na walimu, wanafunzi na baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo waliohudhuria hafla hiyo.

Madawati hayo 135 na viti vyake vina thamani ya sh. milioni 11.5 kwa bei ya sh. 85,000/- kwa kila dawati na kiti chake.

Alipoulizwa ni lini madawati hayo yatakuwa tayari, Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Bibi Rupa Suchak alisema yatawasilishwa shuleni hapo baada ya wiki moja kwa sababu wana madawati ambayo yamekwishatengenezwa kwenye bohari za kiwanda chao.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuongea na jumuiya iliyofika kushuhudia utolewaji wa msaada huo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Bw. Ali Juma Shamhuna alisema yeye alisoma kwenye shule hiyo mwaka 1952 na kuainisha kwamba wana uhaba wa madawati kwa madarasa manne.

“Tunayo madarasa matupu manne na hii ndiyo skuli yangu niliyosoma tangu mwaka 1952. Ni kweli tunakua na tunaongezeka lakini bado tuna watoto wanakaa chini… wananchi wa Zanzibar wanajitolea kujenga shule lakini inapofika kwenye madawati imekuwa ni tatizo. Tunaomba kuungwa mkono zaidi”, alisema.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Magharibi, Bw. Ayoub Mahmoud Jecha alisema shule hiyo ina shule za Serikali 64 lakini ni shule mbili tu ndizo zina madarasa yaliyokamilika na yote yakiwa na madawati. Alisema wilaya hiyo ina jumla ya wanafunzi 114,000 ambapo 79,000 kati yao wanasoma kwenye shule za Serikali na 35,000 wanasoma kwenye shule za binafsi.

“Wilaya hii ina upungufu wa madawati 5,700. Kwa uwiano wa dawati moja kwa kila watoto watatu, ina maana kuwa watoto 17,100 wanasoma wakiwa wamekaa chini. Tunashukuru mchango huu wa Jambo Plastics lakini tunaomba wahisani zaidi wa kutusadia ili watoto wetu wapate mazingira mazuri ya kujifunzia,” aliongeza.

Awali, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Jambo Plastics, Bibi Rupa Suchak katika taarifa yake alisema kampuni yake imeamua kutumia plastiki kutengeneza madawati kwa sababu imedhamiria kuhifadhi mazingira lakini kuokoa kudorora kwa uchumi.

“Haya madawati ni imara na yanadumu kwa muda mrefu tumeshayasambaza kwenye shule zaidi ya 400 huko Tanzania Bara na tumeona matokeo mazuri… pia yanasaidia kuhifadhi mazingira kwa kuzuia ukataji miti ovyo. Takwimu zinaonyesha miti zaidi ya 100,000 inakatwa kila mwaka kwa ajili ya kupata mbao za kuetengezea madawati,” alisema.

“Madawati haya yanaweza kuongezwa au kupunguzwa urefu kulingana kimo cha mtoto lakini pia yana uimara wa pekee ambao unaokoa mamilioni ya fedha ambazo zingetumika kununua madawati mengine pindi yale ya mbao yanapovunjika,” alisema.

Waziri Mkuu alirejea jijini Dar es Salaam jana jioni.

IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMAPILI, MEI 3, 2015.

MAHAFALI YA NANE YA CHUO CHA WAALIMU WA SHULE ZA AWALI CHA NEW MONTESSORI TEACHERS COLLEGE YALIVYOFANA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji na Mkuu wa Chuo hicho, Denis Msangi akizungumza na wahitimu katika mahafali hayo yaliyofanyika Shule ya Msingi ya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana.
 Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Haris Kapiga akisisitiza jambo wakati akizungumza na wahitimu hao wapatao 45.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hildelly Solution (T) Ltd, Hilda Ngaga, akizungumza katika mahafali hayo.
 Wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.
Wahitimu wa Chuo cha Ualimu wa Shule za Awali katika chuo cha New Montesorri wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chuo hicho pamoja na wageni waalikwa huku wakiwa na vyeti vyao kwenye mahafali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam jana.  
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
 

Umoja wa Ulaya, UN; Tutapigania Uhuru wa Habari Siku Zote

$
0
0
Na Joachim Mushi, Morogoro  

UMOJA wa Nchi za Ulaya nchini Tanzania (EU) umepinga vikali vitendo vya kikatili na unyanyasaji wameokuwa wakifanyiwa na vyombo vya dola vya Serikali wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ambapo ilitokea mwanahabari mmoja kuuwawa. Alisema hawatachoka kukemea matukio hayo ya unyanyasaji kwani yanafifisha uhuru wa habari.

Akizungumza leo mjini Morogoro katika Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Kiongozi Mkuu wa Mabalozi hao, Balozi Filiberto Cerianse Bregondi alisema EU itaendelea kupinga namna yoyote ya unyanyasaji kwa wanahabari makundi yote wakiwemo wa mitandao ya kijamii hadi utakapo kuwepo uhuru kamili wa vyombo vya habari. "...Tulifanya hivyo kwa mauaji yalipotokea na tutaendelea kufanya hivyo siku zote watakapo kamatwa na kupigwa wakiwa kazini...Tunajua huenda haitoshi lakini hii ni kutokana na tofauti mbalimbali za kiutendaji," alisema Balozi Cerianse Bregondi. 

Alisema kupinga unyanyasaji kwa wanahabari haina maana wanachoandika wanahabari mara zote ni cha kweli lakini ipo namna nzuri ya kushughulikia mvutano kama huo na kusaidia kupata taarifa za kina zaidi zitakazofikia muafaka. Aidha kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ambaye alikuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo alisema Tanzania inaongoza Afrika kwa kushindwa kuweka utaratibu mzuri wa udhibiti mawasiliano. 

Alisema vyombo vya habari ni muhimu katika taifa na hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Taifa unaotarajia kufanyika Oktoba, alisema vyombo vya habari vinaweza kubomoa au kujenga taifa lolote. "...Waandishi ni watu muhimu katika kudumisha demokrasia nchini hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kujifunza zaidi. 

Maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani kitaifa yamefanyika mkoani Morogoro na kuhudhuriwa na wanahabari mbalimbali, wakongwe, wadau anuai wa vyombo vya habari huku yakiwa na kauli mbiu ya Usalama wa Vyombo vya Habari katika Dijitali: Uhandishi Mzuri unaozingatia, Usawa wa Kijinsia na faragha.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika maadhimisho ya Uhuru wa habari duniani yaliyofanyika mkoani Morogoro. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika maadhimisho ya Uhuru wa habari duniani yaliyofanyika mkoani Morogoro.Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani..Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.

Waziri Tizeba ataka timu za Wizara zishiriki Ligi Kuu

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba ameagiza taasisi zilizo chini ya wizara hiyo ziendeleze michezo kwa wafanyakazi wao makazini na kuhakikisha wanashiriki michuano  ya mashirika ya umma na taasisi zenye uwezo kama Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kushiriki Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara.

Dk. Tizeba amesema hayo mwishoni mwa wiki Jijini Mwanza wakati akiwapongeza wanamichezo wa timu ya Wizara ya Uchukuzi iliyoshiriki michuano ya michezo ya Mei Mosi na kuibuka washindi wa jumla.

“Mnataka kuniambia Bakhressa (Salim Bakhressa, mmiliki wa timu soka ya Azam inayoshiriki Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara) ana fedha kuliko Bandari, “ Waziri Dk. Tizeba aliwauliza wanamichezo hao wakati akitia msisitizo kwa Mamlaka ya Bandari, shirika kubwa, kuwa na timu inayoshiriki Ligi Kuu hiyo nchini.

Alisema timu za taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi na hasa zenye uwezo mkubwa wa kifedha kama Bandari zina fursa ya kushiriki hata Ligi Kuu kama ilivyo Azam ya Bakhressa. Alizitaka zijiandae mapema kwa michezo ya Mesi mosi kwa kuandaa michuano ya ndani na  ya taasisi ili kupata timu bora ya wizara. Alisema vikombe 12 ni vichache sana na akataka mwakani viwe zaidi ya 40 kwani uwezo huo wanao.

Aliwaeleza wanamichezo hao waliotwaa vikombe 12, vitano vya ushindi wa kwanza kuwa, michezo ni sehemu ya kazi na hivyo kumwagiza Mkurugenzi wa Raslimali Watu na Utawala(DAP) wa Wizara ya Uchukuzi, Immaculate Ngwalle kuwaagiza watendaji wa taasisi za wizara hiyo kuipa michezo umuhimu. 

Alisema ni aibu kwa taasisi nane tu kati ya 15 za Wizara hiyo kushiriki Mei mosi kwa madai ya ukata na kuwataka watendaji wa taasisi hizo kuhakikisha wanaweka bajeti ya michezo kwenye bajeti yao kuu vingnevo, hataipitisha kwani wafanyakazi wanapaswa kushiriki michezo kama sehemu ya kazi zao pia.

Aliwataka watendaji wa taasisi ambazo zimeajiri wafanyakazi wa muda kwa muda mrefu ambao ajira zao si za kudumu kuomba kibali cha ikama iii wathibitishwe kazini ili washiriki michezo hiyo bila utata kwani ni haki yao na huchangia ushindi kama walivyofanya kina mama wa Bandari walioshinda mchezo wa kuvuta kamba ingawa ni vibarua. Alihoji kama taasisi hizo haziwahitaji, vipi ziendelee nao muda mrefu.

Wanamichezo  100 wa timu ya Uchukuzi walioshiriki walitoka Bandari (TPA), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA), Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Chuo cha Masuala ya Bahari (DMI) na Wizarani. TAA iliongoza kwa kutoa wanamichezo 56 ikifuatiwa na Bandari 26 na ya mwsho ni NIT (1).

Michezo waliyoshiriki ni soka walioyoibuka washindi wa tatu, baiskeli, netiboli, bao, kuvuta kamba, karata. Mbali ya Waziri, DAP, Mama Ngwalle aliwapongeza kwa ushindi huo mnono na kuwataka waongeze bidiii zaidi mwakani. Manahodha wa timu zilizoshinda walimkabidhi Dk. Tizeba vikombe vyao. IMETOLEWA NA GODFREY LUTEGO, AFISA UHUSIANO, MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA

NAMUOMBA MUNGU ANGEMLETA ROSE NDAUKA MAPEMA - SHETTA

$
0
0
Inline image

Wimbo wa Ruby Na Yule unaweka wazi Vitu ambavyo Vitakufanya uamini kuwa Mama Kaylah Mke wa Shetta Hajarudi nyumbani baada ya Kumwacha Shetta kwa Kile alichokidai kuwa Shetta Amechepuka na Mwanadada wa Bongo Movie Rose Ndauka.
Kwenye mahojiano ya Juzi Tarehe 29 aliyofanya na Kipindi cha DUNDO cha MJ FM ambapo Shetta alikuwa anaizungumzia Ngoma ya mtu mwingine Ambayo anaikubali Kuliko ambapo aliuchagua wimbo wa Ruby Uitwao NA YULE kama Hit On Chart yake na Hapo ndipo akabanwa na DjHaazu Akazungumza KUPITIA DUNDO HIT ON CHART.
Kama unaifahamu vizuri ngoma ya Ruby Na Yule Hutapingana na mimi kuwa ni wimbo ambao unaweza Kuudedicate kwa Mpenzi wako Mpyaaaaaaaaa..... Sasa Shetta na Mkewe wamepeana Likizo Kimpango Flani sasa unajiuliza Mpenzi Mpya kwake ni naniiiiiii?
KILICHOTOKEA HEWANI KISIKILIZE HAPA CHINI NA UJIULIZE JE ANAMMAANISHA ROSE NDAUKA ANGELETWA MAPEMA KWAKE??

Kasi ya Utekelezaji miradi ya NHC Mtwara yafurahisha bodi ya shirika hilo

$
0
0
Mkurugenzi wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, Subira Mchumo akielekeza jambo wakati wa ziara yake aliyoifanya kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu Masasi, mkoani Mtwara ambapo pamoja na mambo mengine amesifu kasi ya ujezi wa nyumba hizo unaozingatia viwango na muda na akawataka wafanyakazi wa NHC kuchapa kazi ili kufikia malengo yao waliyojiwekea. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa NHC, Felix Maagi, wa pili ni Eliaisa Keenja wa NHC, Meneja wa NHC mkoa wa Mtwara, Joseph John na Injinia wa mradi huo Leonard Kazoba.
Mkurugenzi wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, Subira Mchumo akimsikiliza Mhandisi wa mradi huo Leonard Kazoba wakati wa ziara yake aliyoifanya kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu Masasi, mkoani Mtwara.
Mkurugenzi wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, Subira Mchumo akimsikiliza Mhandisi wa mradi huo Leonard Kazoba wakati wa ziara yake aliyoifanya kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu Masasi, mkoani Mtwara.
Baadhi ya Nyumba za gharama nafuu  zilizoko mkoani Mtwara.

MZIIKI KWA KUSHIRIKIANA NA VODACOM TANZANIA YANOGESHA ZARI ALL-WHITE PARTY

$
0
0

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platinumz ambaye ni balozi wa Mziiki ambayo ni program ya simu za mkononi (mobile app) ya Vodacom Tanzania akiimba jukwaani Zari White Party iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. App hiyo inawaletea wateja burudani ya muziki kiganjani. Picha zote na Cathbert Angelo Kajuna wa Kajunason Blog.
Mchumba wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platinum... Bibie Zari the bossylady akiwashukuru Watanzania waliofika katika Zari White Party lililofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Na Cathbert Kajuna 
wa Michuzi Media Group
Mziiki ni huduma ya muziki ya Afrika ambayo inatoa huduma hiyo kwa muziki wa kitaifa na kimataifa, inajivunia kwa kiasi kikubwa kuwa sehemu ya wadhamini wa pati ya Zari All-White party iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mziiki ni sehemu ya kuendeleza wasanii wa ndani na nje ya Afrika ambapo watumiaji wa simu za smartphones za Android, iOS na BlackBerry wanapata nafasi ya kusikiliza nyimbo mbalimbali kwa kupitia simu zao za mkononi.Wateja wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kwa kutumia intaneti ya wi-fi wanaweza kuperuzi na kupata nyimbo ambazo wanaweza pia kuziweka katika miito yao ya simu pia kuzisambaza kwa rafiki zao bure kwa kipindi cha mwezi mzima ambao ni ofa.
Huduma hii inapatikana katika vifurushi vyote vya Lite na Premium, na huduma ya Lite inapatikana pia kwa watumiaji wote wa mtandao wa wi-fi ambao wanaweza pia kuperuzi moja kwa moja bila malipo yoyote kila mahali mtandao wa Vodacom unapopatikana. Tangu Mziiki izinduliwe mwezi Mei mwaka jana, imefanikiwa kuingiza zaidi ya wasanii 1000 wa Afrika ambao wanafanya vizuri mpaka sasa.
Huduma hii imechaguliwa sana kwa ajili ya kuhakikisha Waafrika wanafurahia muziki wao ambapo inaendelezwa na Spice Africa, na ilianzia Tanzania lakini kwa sasa inazidi kukua katika nchi mbalimbali.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Spice Africa, Arun Nagar, alisema ‘Huduma ya hii ya kidijitali inalenga zaidi kuibua vipaji katika nchi za ukanda wa Jangwa la Sahara Afrika ambapo pia ni nafasi nzuri kwa wasanii mbalimbali kutangaza kazi zao’.
‘Tunajivunia kuwa sehemu ya wadhamini wa sherehe za Zari-White Party ambapo pia tuna imani kuwa Watanzania wengi watazidi kufurahia huduma zetu’ Nagar aliongeza kuwa Mziiki ni huduma ambayo inapatikana kirahisi mno kwa kutumia simu za mkononi kwa kupata huduma ya muziki wa wasanii wa ndani na nje ya Afrika.
Diamond Platnumz, ambaye ni balozi wa Mziiki Tanzania, alisema ‘Mziiki imekuwa katika nafasi ya kutoa kipaumbele kwa wasanii mbalimbali kwa ajili ya kupata changamoto kwa wasanii wakubwa kitaifa na kimataifa’
“Muziki wetu umezidi kufanya vizuri katika nchi mbalimbali, na Mziiki inatoa ofa kwa wadau mbalimbali wa muziki kusikiliza nyimbo wanazozipenda kwa kupitia katika viganja vyao,” alisema Diamond Platnumz.
Burudani mbalimbali zilizotolewa katika sherehe hizo za Zari White Party ikiwa ni pamoja na muziki kutoka kwa DJ, muziki wa live kutoka kwa wasanii kama vile Diamond Platnumz na Shetta wakati msanii mwalikwa atakua AKA, kutoka Afrika Kusini.
Zari All-White Party 2015 imedhaminiwa na Vodacom na Mziiki kwa kushirikiana na SK Entertainment, Clouds Entertainment, Prime Time Promotions, Johnny Walker Gold label ( Serengeti Breweries) ambapo ilianza The All-White Parties mwaka 2009 nchini Uganda na Tanzania inafanyika mwaka huu kwa mara ya kwanza.

Simba yaifunga Azam FC 2-1

$
0
0
 Kikosi cha Azam FC kilichoanza leo. 
Kikosi cha Simba.
Waamuzi wa mchezo wa Simba na Azam wakiwa katika picha ya pamoja na manahodha wa timu zote kabla ya mchezo.

mhe mizengo pinda akabidhi madawati skuli ya kiembesamaki, zanzibar

$
0
0
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa ameketi  katika moja ya madawati  yakisasa aliyo  yapokea kutoka kiwanda cha Jambo Plastics Ltd ya Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuisaidia Skuli ya Kiembe samaki Zanzibar anaye shuhudia katikati waziri wa Fedha wa Zanzibar Mhe. Omari Yusufu Mzee. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jambo Plastics Limited Rupa Suchak katika sherehe hizo za kukabidhi zimefanyika katika Skuli ya Kiembesamaki Zanzibar ambako Waziri Mkuu alikuwa Zanzibar kikazi 
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimshukuru Mkurugenzi mtendeji wa Jambo Plastics Ltd Rupa Suchak kwa kwa kuiunga serikali mkono kwa kutoa msaada wa madawati ya kisasa yaliyotengenezwa kwa Plastiki ili kupunguza  tatizo la madawati katika  Skuli ya Kiembesamaki Zanzibar. Katikati wanaoshuhudia kushoto Waziri wa Elimu Zanzibar Alli Juma Shamuhuna na kulia ni Waziri wa Fedha Zanzibar Omari Yusufu Mzee Suchak sherehe hizo za kukabidhi zimefanyika katika Skuli ya Kiembesamaki Zanzibar
Wanafunzi  wa Skuli ya Kiembesamaki wakimfurahia Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye alifika shuleni hapo kuwakabidhi madawati. Picha zote na Chris Mfinanga

Masters Engineering Degree programme in Maintenance Management for the academic year 2015/2016

$
0
0
The Dar es Salam Institute of Technology (DIT), invites applications from qualifield candidates for the admission into the institute's Masters Engineering Degree programme in Maintenance Management for the academic year 2015/2016 scheduled to start in November 2015.


AIMS OF THE PROGRAMME

1.To provide graduate who are technically competent to serve in the proffesion of maintenance  management.

2. To meet the need for locally-trained professional and innovate maintenance management services engineers in consultancy, contracting, maintenance management, recearch and development.

3. To provide an oppoturnity for student to learn through well-designed course, the "art and science" for providing a safe, healthy and energy-efficient built environment impact.

4. To prove students with interectual challenges which will enable them to further self-development towards leadership in the maintenance services engineering profession.


PROGRAMME STRUCTURE

The programme complimice a total of 22 Modules (elective and core Modules) with a minimum of 180 required credits that are spread over two semesters for course work and six months period of dissertation. Each course Module is covered in one semester of 17 weeks. The coursework sessions will be carried out during evening time from 04:00 pm. The Programmeruns for a minimum of 18 months.


Minimun Entry requirements

i.Applicants must be holders of Bacholar of Engineering degree in either  of the following areas of Engineering: Civil, Electrical, Mechanical or equivalent from accredited higher learning institution: with GPA of at least 3.0 OR

ii. Candidets with a Bachelor of Engineering degree in either of the following engineering; Civil; Electrical; Mechanical or equivalent from an accredited higher learning institution; with at least 2.7 GPA may be considered if they have an evidence of not less than 3 years working experience after graduation. OR

iii. Holders of Advance Diploma in Engineering in either of the following areas of Engineering; Civil; Electrical; Mechanical or equivalent from an accredited higher learning institution with PASS and a minimum of five years experience can also be considered.


Fees, application procedures and application forms

Information about fees structure and applications forms (DIT/PS/APPL/01 and DIT/PS/APPL/02) and procedures are available on DIT website (www.dit.ac.tz), research or registrationrs office. The deadline for aplication is on 1th. August 2015

Warning: Any forged certificate submitted by an applicant is a criminal offense and appropriate legal action will be taken against the applicant.

All aplications should be addressed to:


PRINCIPAL

Dar es Salaam Institute of Technology

P.O.BOX 2958

Tel 255-0(22) 2153511 (Registrar)

Fax 255-0(22)222152504


registrar@dit.ac.tz

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
DUNIA NI MSONGAMANO-NDALA KASHEBA

KUMBUKUMBU

$
0
0
MAREHEMU JOACHIM BWANAMPINI LEBABU KIRAMBATA 
 KUZALIWA 02/02/1945 KUFA 04/05/2013

TAREHE 04/05/2015 IMETIMIA MIAKA MIWILI KAMILI TANGU MWENYEZI MUNGU AKUITE.

ILIKUWA SIKU YA MAJONZI MAKUU KATIKA FAMILIA YETU. KIFO KILITOKEA KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI DSM. UNAKUMBUKWA SANA NA FAMILIA YAKO, MKE WAKO BI MARY KIRAMBATA, WATOTO WAKO LILIAN, JOSEPH, FILBERT, FLORENSO, FLORA, JANUARY, OCTAVIAN WAKWE ZAKO ENGELBERT, VIRGINIA, & DEVOTHA WAJUKUU ZAKO CELINE, MARYANNE, MELISA, ROSE, HENRICK, FLORENCE, JEREMIA GABRIELA & JOLENE NDUGU JAMAA MAJIRANI, MARAFIKI ZAKO, NA WENGINE WOTE WANAKUKUMBUKA KILA MMOJA KWA NAMNA YA PEKEE.

MISA YA KUMUOMBEA MAREHEMU ITAFANYIKA TAREHE 03/05/2015 SIKU YA JUMAPILI SAA 3.00ASUBUHI KATIKA PAROKIA YA MT. ANDREA BAHARI BEACH. MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YAKO MAHALI PEMA KWA WATAKATIFU WAKE.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE MILELE.

AMEN.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images