Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

Mama wa Mitindo Asya Idarous, Gusagusa Min band kufanya maonyesho Uingereza

$
0
0
11169017_958488377518759_1048095244_n
Bana ya shoo hiyo ya Gusagusa Min band na Asia Idarous Khamsin itakayofanyika nchini Uingereza

London, Uingereza
Mbunifu wa mavazi nchini ‘Mama wa Mitindo’, Asia Idarous Khamsin yupo nchini Uingereza akiwa ameambatana na magwiji wa muziki wa taarab kutoka Tanzania, Gusagusa Min Band ambao watafanya maonyesho makubwa ndani ya miji ya nchi hiyo ikiwemo London na Northampton.
Kwa mujibu wa wandaaji wa shoo hiyo nchini humo, Kampuni ya Didas Entertainment ya Uingereza walieleza kuwa, shoo ya kwanza itakuwa Mei 2, katika viunga vya mji wa London na shoo nyingine ni Mei 3 katika mji wa Northampton ambapo kutakuwa na fashion shoo ‘Divas Catwalk’ itakayopambwa na Mama wa Mitindo, Asia Idarous.
11069501_10152884668557684_7139946682781219300_n
Magwji Afua, Mwanahawa, Asya Idarous na Achun Baa meneja wa Gusagusa min Band ndani ya UK.

“Gusagusa Min Band na Mama wa Mitindo, Asia Idarous, Tayari wapo ndani ya viunga vya Uingereza na wapo kamili kwa shoo kabambe Mei 2 ndani ya Empire Suite, London na shoo ya Mei 3, ndani ya Academy, mji wa Northampton. Gusagusa ipo full band nzima ikijumuisha wapiga vyombo wao” ilieleza taarifa hiyo kutoka Didas Entertainment.

Aidha, katika safari hiyo, Asia Idarous ameongozana na wadau wengine wakiwemo Mkurugenzi wa Gusagusa Mind Band, Hasan Farouk, gwiji wa taarab, Bi Afua Suleiman (muimbaji), Bi Mwanahawa Ally (muimbaji), Jaffer bhai (muimbaji), Khamis Chizi (master keyboard ) na Abdulla Ngonda (mpiga base) na wengineo wengi.
11178372_957991814235082_5347065811729573025_n
Mama wa Mitindo, Asya Idarous Khamsin (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Gusagusa Min Ban, Achun Baa na Hamis chizi 'Master keyboard' ndani ya viunga vya Milton Keynes UK (Uingereza).
Didas Entertainment imekuwa ikifanya shughuli mbalimbali za burudani ikiwemo kupeleka wasanii kutoka Tanzania na kupiga shoo nchini Uingereza pamoja na shughuli zingjne za Sanaa ikiwemo filamu, wasanii wa filamu na uandaaji wa filamu, ambapo hadi mwaka huu imeweza kutimiza miaka 10, tokea kuanzishwa kwake.



MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KWA MWAKA 2015

$
0
0
 
 Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (kulia)akishaurina na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(katikati) leo mjini Songea wakati wa mazoezi ya mwisho ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2015.Wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi(mwenye kofia nyeupe) na Katibu wa Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Juma Mswadiki(mwenye tshirt ya bluu bahari)
 Naibu Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia  (wa pili kulia)akishaurina na Katibu Mkuu wa Mkuu wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga leo mjini Songea wakati wa mazoezi ya mwisho ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2015.Wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi(mwenye kofia nyeupe) na Waziri wa Uwezeshaji , Ustawi wa Jamii , Vijana ,wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Zainabu Omary Mohamed(kushoto)
 Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (katikati)akishaurina na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kushotoi)  na Waziri wa Uwezeshaji , Ustawi wa Jamii , Vijana ,wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Zainabu Omary Mohamed(kulia) leo mjini Songea wakati wa mazoezi ya mwisho ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2015, utakaozinduliwa tarehe 29.4.2015 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
 Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangaraakizunguza na wandishi wa habari leo mjini Songea.
Kikundi cha sanaa cha Mlale JKT mkoani Ruvuna kikitumbuiza leo mjini Songea wakati wa mazoezi ya mwisho ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2015 ,utakaozinduliwa tarehe 29.4.2015 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

Sherehe ya mtoto wa Mpiganaji Rhoda Danford Mpumilwa ya Kupokea Komunyo

$
0
0
 Jumapili iliyopita ilikuwa siku maaalum kwa Binti Rhoda Danford Mpumilwa ambapo alipokea Holy Communion hapo kwenye kanisa la Katoliki la Holy Family Njiro mjini Arusha. Katika sherehe hiyo alisindikizwa na familia yake wakiwamo dada zake,Leah Danford Mpumilwa (mkubwa) na Tuli Danford Mpumilwa. (mdogo wake).
Rhoda na dada zake mkubwa Leah (kushoto) na Tuli.
 Rhoda (kulia) akisindikizwa na mdogo wake Tuli   kwenda kanisani.

NHIF YAENDELEA KUWAHAMASISHA WANANCHI WA KILWA KUJIUNGA NA CHF

$
0
0
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),  Rehani Athumani (kulia) akikabidhi baadhi ya mashuka kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Chumo, Khatib Riwanda kwa matumizi ya Zahanati ya Kijiji hicho cha Chumo, wakati wa muendelezo wa Kampeni yake iliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Chumo, Kata ya Chumo, Kilwa Mkoani Lindi. Katikati ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Lindi, Fortunata Raymond.Picha na Othman Michuzi, Lindi.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),  Rehani Athumani akizungumza na Wakazi wa Kijiji cha Chumo juu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inayofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF, wakati wa muendelezo wa Kampeni yake iliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Chumo, Kata ya Chumo, Kilwa Mkoani Lindi.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Lindi, Fortunata Raymond akieleza jambo kwa Wakazi wa Kijiji cha Chumo juu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inayofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF, wakati wa muendelezo wa Kampeni yake iliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Chumo, Kata ya Chumo, Kilwa Mkoani Lindi.
Mwakilishi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Mtandao wa Mifuko ya Afya ya Jamiii nchini (TNCHF), Kidani Mhenga akiwapa somo Wakazi wa Kijiji cha Chumo juu ya umuhimu wa wananchi hao kujua taratibu zote zinafanywa katika vituo mbalimbali vya Afya na kuhoji mapato na matumizi ya fedha za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inafanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF, wakati wa muendelezo wa Kampeni yake iliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Chumo, Kata ya Chumo, Kilwa Mkoani Lindi.

MICHEZO YA MEI MOSI YAPAMBA MOTO CCM KILUMBA, MWANZA

$
0
0
 Timu ya Wanaume Wavuta Kamba wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakivutana na Timu pinzani ya Uchukuzi (hawapo pichani) wakati wa fainali ya michezo ya Mei Mosi iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa CCM Kilumba Mkoani Mwanza leo.
 Timu ya Wanawake Wavuta Kamba wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakipambana na Timu pinzani ya Uchukuzi (hawapo pichani) wakati wa fainali ya michezo ya Mei Mosi iliyofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza leo.
 Meneja wa Timu za Michezo ya Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Suleman Kifyoga (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Wavuta Kamba Wanaume wa Ofisi hiyo wakati wa Mshindano ya Michezo ya Mei Mosi yaliyofanyika Viwanja vya CCM Kilumba Mwanza
Timu ya Wavuta Kamba Wanawake kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Michezo ya Mei Mosi Viwanja vya CCM Kilumba Mwanza Aprili, 2015.
Picha na Nyamagory Omary, Afisa Habari-PMO

Mhe Pindi Chana atembelea kituo cha kulelea Watoto

$
0
0
Habari na picha na Hassan Mabuye 
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mheshimiwa Dkt. Pindi Chana amefanya ziara ya kutembelea kituo cha kulelea Watoto Wilayani Kibaha mkoa wa Pwani kwa lengo la kuangalia maeneo ambayo yanahitaji maboresho pamoja na kujionea hali halisi ya uendeshaji wa vituo vya kulelea Watoto. 
Katika ziara hii Mheshimiwa Naibu Waziri alitembelea kituo cha Malezi na Makuzi ya watoto Kilichopo katika kata ya Mtambani Mlandizi jumatatu tarehe 27 Aprili 2015, ambapo aliongea na Walezi na wasimamizi kukienzi na kukitunza kituo hicho. 
Aidha Mheshimiwa Pindi Chana amewahusia wasimamizi na wazazi kuyapa kipaumbele mambo yanayohusu Watoto kuanzia kwenye familia na kuyaweka katika bajeti za kila siku za familia kwani taifa la kistaarabu linajengwa kuanzia kwa watoto wadogo. 
Mheshimiwa Naibu Waziri alifanikiwa pia kukutana na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha ambapo aliwahusia vijana kuzingati masomo yao wakati wazazi bado wana nguvu za kuwasomesha. 
"Unadhani siku hizi ukikimbia shule au kutoroka masomo unamkomoa nani, mzazi au mwalimu? Unajikomoa mwenyewe sababu baadae wewe ndo utabeba majukumu na pengine ndio utakuwa mzazi na maisha ya sasa ni elimu na ujuzi" alisisitiza Mhe. Pindi Chana. 
Aidha Mheshimiwa Pindi Chana katika ziara hii alikutana na vikundi vya Wanawake walionufaika na mikopo inayotolewa na Benki ya Wanawake Tanzania eneo la Picha ya Ndege Kibaha.
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mheshimiwa Dkt. Pindi Chana akisisitiza jambo wakati akiongea na watoto pamoja na walezi wa kituo cha Malezi na Makuzi ya Watoto cha Mtambani, Mlandizi wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwan
 Baadhi ya watoto wa kituo cha Malezi na Makuzi ya Watoto cha Mtambani wakiwa katika kikao hicho.

 Baadhi ya watoto wa kituo cha Malezi na Makuzi ya Watoto cha Mtambani wakiwa katika kikao hicho.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mheshimiwa Dkt. Pindi Chana akisisitiza jambo wakati akiongea na wanachuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha.
Wanachuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mheshimiwa Dkt. Pindi Chana.

Dkt. Shein mgeni rasmi uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Ruvuma.

$
0
0
Na: Frank Shija, WHVUM

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2015 ambazo Kitaifa zinafanyika Mkoani Ruvuma.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waizri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara wakati wa mazoezi ya ya mwisho yaliyofanyika katika Uwanja wa mpira wa Majimaji mjini Songea.

Waziri Fenella amesema kuwa maandalizi yameenda vizuri na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika sherehe hizo za uzinduzi wa mbuio za Mwenge na kutoa hamasa zaidi kwa Vijana wotye nchini kushuhudia uzinduzi huo ata kwa vile utaonyeshwa moja kwa moja kupitia Televisheni ya Taifa (TBC).

"Nisema tu kuwa maandalizi yamekwenda vizuri sana mmejionea vijana wa Halaiki walivyo onyesha umahiri wao, niwatate tu wakazi wa mjini wa Songea mjitokeze kwa wingi kuja kushuhudia sherehe hizi za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru lakini pia VIjana nchini kote shuhudieni tukio hili muhumu kwa kuwa litaonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa TBC" Alisema Dkt.Fenella

Aidha Waziri Fenella alitoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma kujitokeza kwa wingi katika zoezi a kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura na baadaye watumie demokrasia kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka 2015 zinazindulia rasmi tarehe 29 Aprili 2015 mkoani Ruvuma na kilele chake kitakuwa tarehe 14 Oktoba mkoani Dodoma ambapo mbo hizo kwa mwaka huu zimebeba kauli mbiu ya "Tumia Haki yako ya Kidemokrasia" Jiandikishe na kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. 

Mwenge huo wa Uhuru unatarajiwa kukimbizwa katika halmashauri 168 za mikoa 30 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

AMIRI JESHI MKUU NA RAIS WA TANZANIA DKT. JAKAYA KIKWETE AZINDUA MELI VITA ZA JESHI LA WANAMAJI

$
0
0


1
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa amri kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015
2
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mara baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015
34
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na makamanda wa meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015
5
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Chifu Edward Wanzagi wa kabila la Wazanaki (kati) pamoja na Mbunge wa Afrika Mashariki Mhe Makongoro Nyerere baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015. PICHA NA IKULU
---------------------------------
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,  Jumanne, Aprili 28, 2015, ametoa kamisheni na kuruhusu kuanza kutumika kwa Melitiva mbili kwa ajili ya ulinzi wa pwani ya Tanzania.


Rais Kikwete ametoa kamisheni hiyo na kuruhusu kuanza kutumika kwa meli hizo, Melivita P77 Tanzania Navy Ship Mwitongo na Melivita P78 Tanzania Navy Ship Msoga katika Sherehe ya Utoaji Kamisheni iliyofanyika Makao Makuu ya Kamandi ya Jeshi la Maji la Tanzania Navy Base, Kigamboni, mjini Dar es Salaam.


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Davis Mwamunyange na Balozi wa China katika Tanzania, Balozi Lu Youching walikuwa miongoni mwa waliohudhuria sherehe hizo pamoja na wawakilishi wa kijiji cha Mwitongo, Butiama Mkoani Mara na Kijiji cha Msoga, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani ambavyo majina yake yametolewa kwa meli hizo mbili.


Akizungumza katika sherehe hizo, Jenerali Mwamunyange amesema uongozi wa Jeshi umeamua kuziita meli hizo mbili kubwa zaidi za kivita zilizopata kununuliwa nchini majina ya vijiji walikozaliwa viongozi wakuu wawili wa Tanzania, Mwalimu Nyerere na Rais Kikwete.


Rais Kikwete ameambiwa katika shehere hizo kuwa meli hizo kutoka Jamhuri ya Watu wa China, zitaongeza kwa kiwango kikubwa uwezo wa JWTZ kulinda mpaka wake ulioko katika Bahari ya Hindi na kuweza kukabiliana zaidi na vitendo vya uharifu, ugaidi na  kulinda vizuri zaidi shughuli za utafutaji gesi na mafuta katika pwani hiyo ya Tanzania.


Akizungumza kabla ya kutoa kamisheni kwa meli hizo, Rais Kikwete ameishukuru Jamhuri ya Watu wa China kwa kuendelea kuiunga mkono Tanzania katika Nyanja ya kijeshi na Nyanja nyingine nyingi.


“Marafiki zetu wa China wamekuwa nasi kwa muda mrefu, wametuunga mkono tokea kuanzishwa kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tokea Mwaka 1964. Kwa upande wa ulinzi wa majini, wamekuwepo tokea Mwaka 1971 walipotusaidia kuanzishwa kituo hiki cha Tanzania Naval Base hapa Kigamboni na kutoa boti 13 za ulinzi.”


Ameongeza Rais Kikwete: “Wamesaidia vifaa, wamesaidia utaalam na wataalam, wametoa mafunzo katika Chuo chetu cha Ubaharia cha hapa hapa. Kwa hakika hakuna marafiki kama wenzetu wa China, wananchi wake na Serikali yake kwa sababu wamesaidia sana maendeleo ya Jeshi letu. Karibuni wametusaidia kuanzisha kombania mbili za majeshi maalum ya majini na sasa meli hizi mbili ambazo zina uwezo wa kwenda kasi zaidi, uwezo wa kubeba silaha nyingi na kubwa zaidi na uwezo zaidi wa kulinda mipaka yetu”.


“Wako watu wanasema kuwa vifaa vya jeshi na ulinzi wa nchi yetu ni ghali. Ni kweli. Lakini sasa nani atatulindia nchi yetu? Ni sisi wenyewe na kazi ya ulinzi wa nchi haiweza kuwa kazi rahisi, wala nyepesi, wala isiyokuwa na gharama.”


Akifafanua hali ilivyo katika Pwani ya Tanzania, Rais Kikwete amesema: ”Miaka ya karibuni hapa yaliwahi kutokea majaribio 28 ya kuteka nyara meli katika eneo la maji la Tanzania, matano yalifanikiwa na mengine yakashindikana. Tuna shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi, maharamia  hufanya jitihada za kuzivuruga, lazima tuzilinde.”


Akitoa kamisheni hiyo, Rais Kikwete amesema:  “Kwa kutumia nafasi yangu kama Amiri Jeshi Mkuu, natoa kamisheni na kuruhusu kuanza kutumika kwa melivita P77 Mwitongo na P78 Msoga. Mwenyezi Mungu azibariki melivita hizi pamoja na wafanyakazi wake wote.”


Wakati wa ukaguzi wa meli hizo, Rais Kikwete ameambiwa kuwa kila moja ya meli hizo ina uwezo wa kukaa baharini kwa muda wa siku saba bila kuhitaji kuongeza mafuta wala diseli na bila kuhitaji msaada wa huduma yoyote kwa ajili ya watumishi wake.


Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu – Dar es Salaam.


28 Aprili,2015




Fight of the Century only on DStv's SuperSport

Makala ya JK alipozindua Tuzo ya Meya katika Maadhimisho ya miaka 30 ya Jumuiya ya Serikali za Mitaa ALAT

BALOZI WA UMOJA WA AFRIKA AMINA SALUM ALI ATOA RAMBI RAMBI KWA KIFO CHA BRIGEDIA JENERALI HASHIM MBITA

$
0
0
Balozi Amina Salum Ali

Na mwandishi wako, Washington, DC.

Balozi wa kudumu wa Umoja wa Afrika, Mhe. Amina Salum Ali leo ametoa salamu za rambi rambi kwa Brigedia Jenerali mstaafu Hashim Mbita aliyefariki siku ya siku ya Jumapili April 26, 2015 asubuhi na kuzikwa siku ya Jumanne April 28, 2015 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Balozi Amina Salum Ali alisema amepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa za kifo cha mmoja wa watumishi wa miaka mingi wa Serikali, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF), aliendelea kwa kusema Brigedia Jenerali msataafu Hashim Mbita atakumbukwa Tanzania, bara nzima la Afrika na dunia kwa jumla kama mmoja wa makamanda mahiri aliyeshiriki kikamilifu katika uondoshaji wa utawala wa ukoloni barani Afrika, hususan utawala wa kidhalimu wa makaburu Zimbabwe na Afrika ya Kusini na hatimaye kuachiwa huru kwa aliyekuwa Rais mzawa wa kwanza nchini Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela.

Mzee Mbita alijitoa mhanga kuongoza mapambano ya ukombozi wa Afrika, Atakumbukwa milele kwa kurudisha heshima ya Muafrika.

Brigedia Jenerali msataafu Hashim Mbita ni mfano uliotukuka kwa watanzania na Afrika.Aliiongoza vizuri sana kamati ya ukombozi ya Umoja wa Afrika Mungu amlaze pema peponi, Amin.

Balozi Amina Salum Ali yupo safarini kuelekea Tanzania.

OFISI YA WAZIRI MKUU, YATEMBELEA MAENEO YALIYOPATA MAAFA MTWARA.

$
0
0
Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig. Jen. Mbazi Msuya akioneshwa na Kiongozi wa Matengenezo wa Kampuni ya kuzalisha umeme M&P mkoani Mtwara, Musa Kongola, eneo lililoathiriwa na mvua karibu na kiwanda hicho kwa kusababisha udongo kushuka zaidi ya mita mia kutoka usawa wa bahari
 Eneo la nchi kavu ambalo udongo umeshuka zaidi ya mita mia kutoka usawa wa bahari, karibu na bomba la kusafirisha gesi na kiwanda cha kuzalisha umeme  cha M&P   Mnazi bay Msimbati Mkoani Mtwara. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa shughuli za Kuratibu Maafa, Brig. Jen,  Mbazi Msuya akikagua maafa yaliyosababishwa na mvua katika kalvati la barabara ya mbae inayounganisha vijiji vya Mbae na Mbawala, Mtwara Mikindani, Aprili 2015.(katikati) ni Mhandisi msaidizi wa Halmashauri hiyo, Is-haka Mpaki
 Sehemu ya Barabara ya Mbae ambayo kalvati lake limebomolewa na mvua, barabara hiyo inaunganisha vijiji vya Mbae na Mbawala, Mtwara Mikindani.
 Mkurugenzi wa Idara ya Kuratibu shughuli za Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya akiwaonesha viongozi wa Kampuni ya Kuzalisha umeme mkoani Mtwara M&P jinsi ya kuzuia udongo usishuke zaidi kutoka usawa wa bahari.
Muonekano wa Alama lilipo bomba la kusafirisha gesi, Kiwanda cha kuzalisha umeme cha M&P na sehemu ya nchi kavu ambayo udongo umeshuka zaidi ya kilomita mia kutoka usawa wa bahari katika eneo la Msimbati Mkoani Mtwara

Rais Kikwete atoa heshima za Mwisho kwa Brigedia Jenerali Hashim Mbita

$
0
0
Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa Katibu Mkuu mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Afrika (OAU) marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
Rais Kikwete akiifariji familia ya Marehemu muda mfupi baada ya kutoa heshima za mwisho(picha na Freddy Maro).
 Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakiuwasilisha mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita kwenye Msikiti wa Mtoro, Kariakoo tayari kwa kuswaliwa mwili na kwenda kuuhifadhi kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo
 Waumini wa Kiislam kwenye Msikiti wa Mtoro, Kariakoo wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita tayari kwa kuswaliwa mwili na kwenda kuuhifadhi kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo
 Sehemu ya waumini wa Kiislam wakisoma dua ya kumrehemu Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita aliezikwa jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam.

DKT. MAGUFULI AMWAGIZA MTENDAJI MKUU TANROADS KUKABIDHI BARABARA YA “DART”

$
0
0
Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amemwagiza  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale, kukabidhi barabara  ya magari yaendayo kasi kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo kasi(DART) ili zianze kutumika wakati sehemu zilizobaki zikiendelea kukamilika.


Hayo ameyazungumza Waziri wa Ujenzi Dkt. Magufuli katika hafla uzinduzi wa barabara ya Uhuru ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam iliyofanyika leo katika viwanja vya Karume.


Pia Dkt. Magufuli amemwaagiza  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo kasi(DART), Bi. Asteria Mlambo aharakishe kutafuta mabasi yaendayo kasi ili ifikapo Octoba Mwaka huu yawe yameanza kufanya kazi katika barabara ya Morogoro Road,jijini Dar es Salaam.


Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick, amekemea vitendo vyote vya uhujumu wa miundombinu na uchafuzi wa mazingira ambavyo vinaathiri taswira ya jiji la Dar es salaam.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick, amekemea vitendo vyote vya uhujumu wa miundombinu na uchafuzi wa mazingira ambavyo vinaathiri taswira ya jiji la Dar es salaam.


“Tatizo la wananchi wa Dar es salaam ni kutokutunza miundombinu pamoja na kutupa taka ovyo hali inayosababisha uharibifu wa miundombinu na kupelekea mafuriko wakati wa mvua”, alisema Meck Sadick.

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mitambo ya ujenzi wa barabara ya Uhuru km 3 huku akiwa pamoja na viongozi wengine wa mkoa wa Dar es Salaam leo jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mitambo ya ujenzi wa barabara ya Uhuru km 3 huku akiwa pamoja na viongozi wengine wa mkoa wa Dar es Salaam jijini Dar es Salaam leo.

Sehemu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika uzinduzi wa barabara ya Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya Pamoja ya Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali wa Dar es Salaam pamoja na wananchi wa Manispaa ya Ilala waliohudhuria katika uzinduzi wa barabara ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.

Picha zote na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

DKT.SHEIN AZINDUA MBIO ZA MWENGE MKOANI RUVUMA LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein (kushoto)akimkabidhi Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa Juma Khatibu Chum (kulia) Mwenge wa uhuru leo mjini Songea baada ya uzinduzi wa mbio hizo Kitaifa mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Songea Profesa Norman Sigalla King(kulia) Mwenge wa Uhuru uhuru kwa ajili ya kuanza mbio wilayani humo baada ya uzinduzi ulifanywa leo mjini Songea na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihotubia leo mjini Songea.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihotubia leo mjini Songea wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa uhuru zilizofanyika kitaifa mkoani Ruvuma.


SHINDANO LA MAMA SHUJAA LAZINDULIWA WILAYANI KISARAWE

$
0
0

Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh.Subira Mgalu amezindua Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloendeshwa na Shirika lisilo la kiserikali la Oxfam kupitia kampeni ya Grow lenye lengo la Kumuwezesha Mwanamke katika kilimo na kumkwamua kiuchumi.

Subira ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kumwezesha mwanamke katika kilimo na kumkwa mwanamke kiuchumi iliyofanyika  katika kijiji cha Kisanga wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

Subira amesema kufanyika kwa mashindano wilayani kwake ni fursa kwa wanawake kushiriki  kuchukua fomu za ushiriki na kuacha uvivu  na kutaka zawadi ya mshindi wa kwanza itokee wilyani humo.

 Aliongeza kuwa shindano hilo linawapa mwanamke uwezo wa kutambua haki zao umiliki wa ardhi na kuwa na ubunifu wa kuweza kubadilisha mbinu za kisasa za kilimo bora.

Nae Mwakilishi kutoka Oxfam Eluka Kibona amesema  kijiji cha Kisanga ndicho kitakuwa wenyeji wa shindano hivyo wanawake wa kisarawe wanahitaji kujituma katika kuchangamkia fursa hiyo.


Pia Diwani wa Kata ya Masaki Mh. Pily Chamnguhi aliwasihi akina baba wa Kisarawe kuwaruhusu wake zao na watoto wao wa kike kuchukua fomu kwa wingi na kushiriki katika shindano hilo kwa kuwa hiyo ni moja ya fursa ambazo watazipata kupitia Shindano la  Mama Shujaa wa Chakula.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu  akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo wakati uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 akizindua Rasmi Mashindano hayo katika kijiji cha Kisanga Mashindano yatakapofanyikia.
  Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam,Eluka Kibona akielezea Shindano la Mama Shujaa wa Chakula.
 Diwani wa Kata ya Masaki Mh. Pily Kondo Changuhi akizungumza na Wakazi wa Kisarawe pamoja na wageni waalikwa katika Sherehe hizo za uzinduzi wa Shindano la Mama  Shujaa wa Chakula.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

NEWS ALERT: WATUHUMIWA WATATU WA UJAMBAZI WAUWAWA MKOANI KIGOMA

$
0
0
Na Editha Karlo,Kigoma

JESHI  la Polisi Mkoani Kigoma limefanikiwa kuuwa majambazi watatu baada ya kurushiana risasi na kukamata silaha mbalimbali za kivita.

Akizungumzia tukio hilo ofisini kwake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Frednand Mtui alisema kuwa majira ya saa nane usiku katika eneo la  mto kahabwe mpakani mwa Wilaya ya Kakonko na Kibondo, askari Polisi wakiwa doria walirushiana risasi na majambazi ambao idadi yao haijajuikana na kufanikiwa kuwauwa majambazi watatu.

Alisema wamefanikiwa kukamata silaha moja aina ya AK.47 yenye namba 10363 ikiwa na risasi 11 ndani ya magazine na risasi 22 za SMG ndani ya mfuko wa rambo pamoja na mabomu 2 ya kutupa kwa mkono .

Kamanda Mtui alisema kuwa aina ya mabomu waliyokutwa nayo majambazi hao ni offensive handgrenade namba Y.3PM-2 na jingine ni aina  ya deffensive handgrenade ambalo namba zake hazisomeki.

''Leo ilikuwa ni siku ya mnada hivyo inaonekana majambazi hao walijipanga wenda kupora mali na pesa katika mnada wa leo,tunawashukuru raia wema kwa kutoa taarifa mapema na kufanikiwa kuwanasa majambazi hao na kuwauwa''alisema Kamanda Mtui

Alisema maiti za majambazi wote watatu ambao majina yao hayajafahamika ila wote wana umri kati ya miaka 25-35 zimehifadhiwa katika Wilaya ya Kibondo na upelelezi wa tukio hilo unaendelea.

KITABU KIPYA CHA MHAMASISHAJI MAHIRI ZAIDI AFRIKA, ERIC SHIGONGO KUZINDULIWA MEI 30, 2015 ALISA HOTEL, ACCRA

BENKI YA POSTA YAJIVUNIA UTENDAJI BORA KWA MWAKA 2014 ULIYOIPA FAIDA NONO

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Sabasaba Kitewita Moshingi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza utendaji wa benki hiyo kwa mwaka 2014 ambapo TBP walipata faida ya shilingi 10.28 bilioni kabla ya kodi. Pamoja nae ni Mkurugenzi Fedha, Regina Samakafu (katikati) na Mkurugenzi wa Sheria, Mystica Mapunda Ngongi
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Sabasaba Moshingi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza utendaji wa benki hiyo kwa mwaka 2014 ambapo TBP walipata faida ya shilingi 10.28 bilioni kabla ya kodi. Katikati ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa benki hiyo, Peter Mapigano na kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji na Teknolojia , Jema Msuya.
Mkurugenzi wa Mipango wa Benki ya Posta Tanzania (TPB)Bernadethe Joseph Gogadi (kushoto) akifuatilia mkutano huo leo ambapo waandishi wa habari nao walikuwepo kuchukua taarifa kama wanavyoonekana pichani.

BASATA, TCRA WATAKA MATUMIZI SAHIHI YA MITANDAO YA KIJAMII KWA WASANII

$
0
0
Na Mwandishi Wetu

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) mapema wiki hii wamelaani matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii miongoni mwa wasanii wakati wa programu ya Jukwaa la Sanaa iliyofanyika makao makuu ya Baraza hilo yaliyoko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.

Akiongea wakati akiwasilisha mada iliyohusu ‘Matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa wasanii’, Meneja mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy alisema kuwa wasanii ni kioo cha jamii hivyo kwa namna yoyote ile hawapaswi kuwa sehemu ya uharibifu wa jamii inayowazunguka au kuharibu wajihi (taswira) yao kwa jamii yao.

“Unapokuwa kioo cha jamii, unategemewa kuishi kwa kuwa mfano katika jamii yako. Vijana wengi wanaiga kutoka kwa wasanii ambao ni maarufu. Tunatarajia wasanii wawe mfano kwao” alisisitiza Mungi.

Aliongeza kwamba, msanii anapotumia mitandao ya kijamii kwa kuweka picha chafu, zisizo na maadili au kitu chochote kisicho na staha ni kuchafua wajihi wake mbele ya jamii na hili linampotezea fursa nyingi za kibiashara na kiuchumi maana hakuna kampuni au asasi itakayopenda kufanya kazi na msanii mwenye sifa mbovu.

“Wasanii wanapotumia hovyo mitandao ya kijamii wanachafua wajihi wao katika jamii. Wanajikosesha fursa za kimapato. Mfano; mfanyabiashara anapotaka kutangaza shule yake ya watoto wa awali hawezi kutumia msanii mwenye wajihi mchafu na unaoharibu watoto” aliongeza Mungy.

Alizidi kueleza kwamba wasanii hawana budi kutumia mitandao hii ya kijamii hususan facebook, twitter, instargram, u-tube na kadhalika katika kujitangaza na kuuza kazi zao na zaidi kutenga muda mwingi kutumikia jamii.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Sanaa na Masoko wa BASATA, Vivian Shalua alisema kwamba Baraza hilo muda wote limekuwa likisisitiza maadili mema miongoni mwa wasanii maana vijana wengi huwaangalia kama mfano katika maisha yao.

“Kila mara BASATA limekuwa likisisitiza maadili kwa wasanii wote. Kazi hii ni ngumu na inataka wadau wote kushiriki katika kunyoosha maadili ya wasanii na vijana kwa ujumla” alimalizia Shalua
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Innocent Mungy (Kulia) akiongea na wadau wa Sanaa (hawako pichani) wakati akiwasilisha mada kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa wasanii kwenye Jukwaa la Sanaa lililofanyika Jumanne ya wiki hii makao makuu ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ilala, Sharif Shamba. Kushoto ni Mwanasheria wa BASATA Deogratius Nchimbi.
Mwanasheria wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Deogratius Nchimbi (Kushoto) akiongea jambo na wadau wa Sanaa (hawako pichani) mapema wiki hii wakati akihitimisha mjadala kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa wasanii uliowasilishwa na Meneja Mawasiliano wa mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia programu ya Jukwaa la Sanaa ya Baraza hilo kwenye Ukumbi wa BASATA ulioko Ilala, Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wadau wa Jukwaa la Sanaa akiuliza swali kwa Meneja mawasiliano wa TCRA juu ya athari za sheria mpya ya mitandao ya kijamii kwa wasanii na waandishi wa habari.
Sehemu ya wadau wa Sanaa waliohudhuria programu ya Jukwaa la Sanaa ya Baraza la Sanaa la Taifa mapema wiki hii.
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images