Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 818 | 819 | (Page 820) | 821 | 822 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Balozi Rajabu Hassan Gamaha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi.


   Balozi Gamaha anachukua nafasi ya Balozi Dkt. Mwasi Nzagi ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.
   Kabla ya uteuzi huo Balozi Gamaha alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Uteuzi huo unaanza mara moja.

  Imetolewa na:

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,

  Dar es Salaam


  27 Aprili 2015


  0 0

  Machezaji wa vishale(Darts) wa klabu ya Friedz ya Tiptop Manzese jijini Dar es Salaam wakiwa wameshika kikombe mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya mchezo huo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Friendz walizawadiwa Kikombe na Pesa taslimu Shilingi 100,000/=.
  Bingwa wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) wa mchezo wa Vishale(Darts), Erry Boates kutoka klabu ya Lugalo akishangilia na kikombe mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya kitaifa yaliyofanyika Tiptop Manzese jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Temeke Chang'ombe jijini Dar es salaam jioni ya leo April 27, 2015.  Marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam baada ya Swala ya Alasiri katika msikito wa Mtoro,  baada ya kupata heshima zote za kijeshi asubuhi yake katika makao makuu ya Jeshi Upanga, Dar es salaam.
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia wakati Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Temeke Chang'ombe jijini Dar es salaam jioni ya leo April 27, 2015. 
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma kikwete wakimsikiliza mtoto wa Marehemu Bw. Iddi Mbita (shati jeupe) kuhusu taratibu za mazishi walipokwenda kuifariji familia ya  Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Temeke Chang'ombe jijini Dar es salaam jioni ya leo April 27, 2015.  
  Rais Kikwete akiondoka msibani akiwa ameongozana na mtoto wa marehemu Bw. Iddi Mbita, Balozi Tambwe, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Saidi Meck Sadik na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Sophia Mjema. Picha na IKULU

  0 0

  ·       Iwapo kutakuwepo ushirikishwaji wa wananchi
  ·       Wataalamu nao watoa yao ya moyoni

  KUTOKANA na kugundulika kwa hazina kubwa ya gesi nchini  ambayo inategemewa kukuza pato la taifa zaidi ya mara 15 ya sasa, kiasi cha kuiwezesha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.

  Hata hivyo, dhana ya kwamba Rais ajaye baada ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete kumaliza muda wake, anaweza akaikuta Tanzania ikiwa ni nchi tajiri tayari kutokana na rasilimali hiyo ya gesi asili, inaweza isiwe sahihi kama hautawekwa mfumo madhubuti wa ushirikishwaji wa wananchi katika fursa zilizopo katika rasilimali hiyo, sera, sheria na usimamiaji mzuri wa raslimali hiyo.

  Pia itawezekana tu iwapo viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali hiyo watahakikisha wanaisimamia kikamilifu kwa mujibu wa sera na sheria zitakazotungwa na kusimamiwa na viongozi wenye dhamira ya dhati ya kuwatumikia Watanzania na nchi yao kwanza.

  Hayo pamoja na mengine yalijadiliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Watanzania wapatao 400 kutoka wilaya mbalimbali ambapo walitoa maoni yao kuhusu ni jinsi gani mapato yatakayotokana na gesi yatawanufaisha wananchi wote wa Tanzania.

  Dr Abel Kinyondo & Invited Expert Innocent Bash from TEITI addressing the media .
   Expert Mr Dennis Rweyemamu (Head - Policy and Research, UONGOZI INSTITUTE) answering questions
   January Makamba and Mujobu Moyo listening to participants
  January Makamba answering questions from participants 
  Moderator discussing topics with participants .


  0 0

  Hii ni barabara kuu itokayo Kilwa Masoko kuelekea Nangurukuru, Mkoani Lindi
  Kijani kila kona.
  0 0

   Mratibu Mkuu wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania (Uwawata), Julius Juju (wapili kulia) akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, ripoti inayopinga upigaji wa ramli na mauaji ya albino na vikongwe nchini. Ripoti hiyo iliyoandaliwa na zaidi ya Wajumbe 200 wa Uwawata baada ya kufanya utafiti ya mauaji ya albino katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na kufanya semina ya hitimisho jijini Mwanza kwa kutoa maazimio ya kupinga mauaji hayo. Kulia ni Mkaguzi wa Waganga nchini katika umoja huo, Mohamed Masoud, Kushoto ni Katibu Mkuu wa Uwawata Mkoa wa Dar es Salaam, Swed Omari. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe jijini Dar es Salaam leo.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akiionyesha ripoti inayopinga upigaji wa ramli na mauaji ya albino na vikongwe nchini mara baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo na Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania (Uwawata), ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Ripoti hiyo iliandaliwa na zaidi ya Wajumbe 200 wa Uwawata baada ya kufanya utafiti ya mauaji ya albino katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na kufanya semina ya hitimisho jijini Mwanza kwa kutoa maazimio ya kupinga mauaji hayo. Kulia ni Mkaguzi wa Waganga nchini katika umoja huo, Mohamed Masoud, Kushoto ni Katibu Mkuu wa Uwawata Mkoa wa Dar es Salaam, Swed Omari, na wapili kulia ni Mratibu Mkuu wa Uwawata nchini, Julius Juju.  Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.   
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akiwashukuru viongozi wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili nchini (Uwawata), kwa kumkabidhi ripoti inayopinga upigaji wa ramli na mauaji ya albino na vikongwe nchini, ofisini kwa Waziri Chikawe, jijini Dar es Salaam leo. Ripoti hiyo iliandaliwa na zaidi ya Wajumbe 200 wa Uwawata baada ya kufanya utafiti ya mauaji ya albino katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na kufanya semina ya hitimisho jijini Mwanza kwa kutoa maazimio ya kupinga mauaji hayo. Wapili kulia ni Mratibu Mkuu wa Uwawata nchini, Julius Juju na Kulia ni Mkaguzi wa Waganga nchini katika umoja huo, Mohamed Masoud.(Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)   

  0 0

    Afisa masoko wa Airtel tanzania Prospa Mwanda akionyesha kwa wanafunzi wa chuo Kikuu dodoma (UDOM) jinsi huduma mpya ya Airtel Wi-Fi Intaneti  inavyofanya kazi mara baada ya uzinduzi wa huduma hiyo chuoni hapo jana. Airtel Tanzania chuoni hupo imezindua huduma ya UNI Wi-Fi Intaneti yenye ubora zaidi na itakayopatikana kwa wananfunzi kwa gharama nafuu. 
   Meneja masoko wa Airtel Uni Wi-Fi Bi Aneth Muga anaepiga picha ya selfie ili waitume kwa kutumia huduma ya Airtel Wi-Fi intaneti kwa baadhi ya uongozi wa wanafunzi na mshauri wa wanafunzi chuoni hapo mara baada ya Airtel kuzindua huduma yao ya  intaneti Wi-Fi yenye kasi zaidi  maalum kwa wanafunzi wa chuo hicho jana. 
   Mshauri wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) bw, Dick Manong akiongea na wanafunzi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel UNI Wi-Fi jana chuoni hapo ambapo itawasaidia wanafunzi kupata intaneti kwa gaharama nafuu ya yenye kasi zaidi.
   Wanafunzi 60,000 wa UDOM kufurahia Airtel WI-FI
  • Pia Airtel yazinduzi mnara wa pili UDOM

  Dodoma, Aprili 27, 2015, kutokana na ukweli kwamba Dodoma ni mji mteule na wenye kuendelea kwa kasi hapa nchini na pia ni mji uliobahatika kuwa miongoni mwa mji wenye chuo kikubwa hapa Tanzania, Airtel Tanzania mkoani huko imezindua huduma ya UNI Wi-Fi Intaneti yenye ubora zaidi na itakayopatikana kwa wananfunzi kwa gharama nafuu.

  UNI WI-FI itawezesha wanafunzi zaidi ya 60,000 katika Chuo Kikuu cha Dodoma kupata huduma ya kimtandao ya Intaneti iliyo bora na nafuu pamoja na  kukidhi mahitaji ya wote waishio chuoni hapo.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Airtel Bi , Adriana Lyamba alisema: "Leo hii tunazindua Airtel UNI WI- FI huduma ya internet inayopatikana kwa bei nafuu kwa ajili ya wanafunzi na  pia tumeongeza mnara wa pili  wa simu   ambao tunaamini utaimarisha mtandao wetu hapa UDOM na kuinua uchumi  wa nchi yetu na kwa watu wanaoishi karibu na maeneo haya ".

  Tunafuraha kubwa kwa Airtel kuweza kuboresha Maisha ya wanafunzi hapa chuoni  kwani spidi hii itawawezesha wanafunzi kuweza kufanya utafiti wao, kupata habari mbalimbali za  taaluma au kijamii  kupitia mtandao wetu wa Airtel "

  Meneja Masoko wa Airtel UNI WI-FI, Bi, Aneth Muga, alisema "Airtel wifi itakuwa inapatikana kwa mwanafunzi yoyote hapa  UDOM, kwa kutumia simu zao za mkononi, laptop, kamera na kwa mwanafunzi yoyote aliyepo UDOM bila kujali mtandao wa simu wanaoutumia.

  Wanaweza kununua UNI Wi-FI vocha ambayo inapatikana  masaa 24 , kwa kifurushi cha siku , wiki,  mwezi na kifurushi cha usiku mzima.
  Fikiria! Unaweza kufurahia kifurushi cha 1 GB kwa shilingi  500 tu! Alisisitiza Bi, Muga

  Kwa upande wake mgeni rasmi ambae ni mshauri wawanafunzi chuoni hapo (UDOM) Bw, Dick Manongi   alisema: ". Tunawashukuru sana Airtel Tanzania kwa ajili ya uzinduzi wa huduma hii kubwa na ya bei nafuu hapa chuoni. Nina hakika kwamba, huduma hii itaimarisha uwezo wa kujifunza na kuendelezea wanafunzi  urahisi wa kujipatia Habari mbalimbali zinazoendelea hapa nchini na hata nje ya nchi ".

  Ningependa kuwaomba wanafunzi wote kutumia fursa hii kubwa ili kuweza kuongeza ujuzi wao kitaaluma na katika Maisha yao ya baadae.

  Uzinduzi wa Airtel Uni Wi- Fi katika chuo kikuu cha Dodoma umekuja mara baada ya Airtel Tanzania kuzindua huduma kama hiyo katika chuo kikuu cha Saint Augustine (SAUT) jijini Mwanza na mipango mingine inaendelea kufikia vyoo vingine hapa nchini.

  0 0

   Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kuhusu eneo la hifadhi  lililoombwa kwa ajili ya upanuzi wa manispaa ya Iringa wakati wa ziara ya waziri wa maliasili na utalii mkoani Iringa leo. (Picha zote na Loveness Bernard)
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu  akifafanua jambo katika mkutano wa kutatua mgogoro kati ya wawekezaji na wananchi wanaozunguka hifadhi ya Ruaha (mbomipa). Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

  0 0

  Mkurugenzi msaidizi, Topografia na Jiodesia, wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dr. James Mtamakaya,(katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Mipaka ya Kimataifa, baina ya Tanzania na nchi jirani, katika ukumbi wa HABARI – MAELEZO, (kulia)ni Mpima Ardhi, Geofrey Kameta na (kushoto) kwake ni Mkurugenzi msaidizi, Upimaji Vijijini, Huruma Lugalla.

  Mkurugenzi msaidizi, Upimaji vijijini, Bw. Huruma Lugalla akionyesha kwenye ramani mipaka mbalimbali ya ndani ya nchi na ile ya Kimataifa, baina ya Tanzania na nchi jirani  katika ukumbi wa HABARI – MAELEZO, jijini Dar es Salaam leo.
   Baadhi ya wandishi wa habari waliohudhuria mkutano,kuhusiana na  Mipaka ya Kimataifa, baina ya Tanzania na nchi jirani, katika ukumbi wa HABARI – MAELEZO jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Avila Kakingo, Globu ya Jamii).

  0 0

   Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia.
   Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Ofisi Ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam leo, kuhusu kuporomoka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania.
   Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
  Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
  Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
  (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika jirani na Super Market ya Nakumat.
  Baadhi ya wananchi waliofika katika mkutano huo wakimsikiliza Ndesamburo.
  Baadhi ya viongozi wa Chadema akiwemo mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi ,Jafary Michael wakimsilikiza Ndesamburo.
  Msatahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Jafary Michael akizungumza katika mkutano wa hadhara .

  0 0

   Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mlimani, Mariam Mrisho (kushoto) akisoma ujumbe ulioandikwa kwenye bango kwa ajili ya kutoa elimu kwa madereva wakati wa kuadhimisha siku ya Afya na Usalama Kazini Duniani. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ilifanyika katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
   Mwanaidi Khamis mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mlimani jijini Dar es Salaam (kushoto) akisoma ujumbe ulioandikwa kwenye bango kwa ajili ya kutoa elimu kwa madereva wakati wa kuadhimisha siku ya Afya na Usalama Kazini Duniani. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ilifanyika katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
   Ofisa polisi wa Usalama Barabarani(CPL) Wilbart Binamungwe (kushoto) akiwaelekeza baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mlimani jijini Dar es Salaam jinsi ya kuvuka barabara, wakati wa kuadhimisha siku ya Afya na Usalama Kazini Duniani. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ilifanyika katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
     Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Mlimani jijini Dar es Salaam, wakisoma mabango yaliyoshikiliwa na wanafunzi wenzie yenye ujumbe wa kusisitiza madereva kutokuvunja sheria za barabarani. Wakati wa kuadhimisha siku ya Afya na Usalama Kazini Duniani. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ilifanyika katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
   Ofisa Polisi wa Usalama Barabarani (CPL) Wilbart Binamungwe akifafanua jambo kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mlimani jijini Dar es Salaam jinsi ya kufuata sheria za kuvuka barabara, wakati wa kuadhimisha siku ya Afya na Usalama Kazini Duniani. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ilifanyika katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

   Balozi wa Tanzania Ubeligiji, Laxembourg na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Kutoka Nchi Mbamlimbali Duniani Baada ya Ufunguzi Rasmi wa Kongamano la Biashara la Kimataifa linalofanyika Genval Ubeligiji. Makampuni zaidi ya 500 yakiwemo hamsini kutoka Tanzania yanashiriki Kongamano hilo. 

  Makampuni hapo yanatoka nchi zinazozungumza kifaransa. Tanzania ni nchi pekee inayozungumza kingereza iliyokaribishwa kushiriki. Kesho, Balozi Kamala atawasilisha mada ya kubainisha fursa za uwekezaji na biashara zinazopatikana Tanzania.
   

  0 0
 • 04/28/15--07:12: TWAWEZA: JE, TUKO SALAMA?
 • Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
   WANANCHI watatu kati ya kumi  wameshakumbana na  wizi ndani ya kipindi cha mwaka  jana,na asilimia 84 ya wananchi  wanaamini kuwa kuna uwezekano wa kuathiriwa na makundi ya vijana waharifu kama panya road.

   Hayo yameelezwa kwenye Utafiti umefanywa na Twaweza kwenye utafiti wenye jina la Je, tuko salama? maoni ya wananchi juu ya usalama na haki waliofanya mkutano katika ukumbi wa mikutano  wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam leo.
  Mtafiti wa twaweza Elvis Mushi amesema kuwa licha ya kuongezeka kwa matukio ya vurugu za kisiasa pamoja,wizi na hofu juu ya makundi ya vijana ya wahalifu wananchi wengi  wamekuwa  hawana  usalama wao katika maisha wanayoishi.
   Naye  Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza  Aidani Eyakuze aliongezea kuwa  kwanza wananchi wengi wanahisi kuwa salama maeneo yao lakini bado wanakumbana na vitendo vya wizi, wanaogopa kuvamiwa na panya road na baadhi yao   kushuhudia ghasia na vurugu za kisiasa. 

  Aidha watu wameshuhudia ongezeko la ukatili dhidi vya vituo vya polisi ndani ya miaka miwili iliyopata, jambo hili linapunguza imani yao na vyombo vya usalama.  
   Eyakuze aliongeza kuwa usalama una umhimu wa kipekee katika masuala ya kijamii na kiuchumi akiwa na akiwa na rai kwa serikali  kuyazungatia maoni haya ya wananchi katika utekelezaji wa jukumu lake la kuwahakikishia wananchi usalama wa hali na mali.
  Ofisa masoko wa Twaweza Costantine  Magavilla akizungumza leo na wajumbe kutoka makampuni mbalimbali katika mkutano wa Twaweza uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa  jijini Dar es salaam,(kulia) ni Mtafiti wa Twaweza Elvis Mushi.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza Aidan Eyakuze akiuliza swali kwa wajumbe waliohudhuria katika mkutano wa Twaweza leo katika ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam  kushoto ni Mkurugezi wa Capacitate Consulting, Ngasuma Kanyeka.
   Baadhi ya wajumbe kutoka makampuni mbalimbali waliohudhuria mkutano wa Twaweza katika ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam leo.
   Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Mstaafu) (CAG), Ludovick Uttoh akizungumza na baadhi ya wandishi wa habari katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Avila Kakingo,Globu ya Jamii).

  0 0


  0 0


  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

  TANZANIA inatarajia kushiriki maonyesho ya nchi 149 ya bidhaa za  viungo ambapo watanzania 500 wanatakiwa kushiriki maonyesho hayo yanayotarajia kuanza Mei 1 hadi 31 mwaka huu mjini Milan Italia.

  Akizungumza na waandishi habari ofisini kwake katika  viwanja vya Mamlaka ya Maendeleo ya Tanzania(Tantrade),Jacqueline Maleko,amesema maonyesho hayo ni fursa ya watanzania kujifunza mbinu mbalimbali za kutanua wigo wa biashara.

  Jacqueline amesema kuwa Tantrade imefanya mawasiliano na katika sehemu ya maradhi pamoja na mashirika ya ndege kwa kwa siku tano ambayo itagharimu dola za Kimarekani 1500,hivyo watu mbalimbali wameombwa ili kuweza kusogea mbele kiuchumi kutokana na elimu watakayoipta katika maonyesho hayo.

  Amesema maonyesho haya yatalenga katika sekta ya chakula pamoja na teknolojia mbalimbali duniani zitaendeshwa kwa kauli mbiu ya ,Kulisha Dunia Nguvu ya Uhai. 

  “Hatuwezi  kukua kiuchumi katika biashara za nje kwa kukaa ndani bila kuweza kupata mawazo kutoka kwa nchi zilizo endelea kiuchumi katika nyanja za maendeleo kutokana na biashara za nje”amesema Jacqueline.
  Kwa upande wa Mkurugenzi wa Biashara za Nje,Anna Bulondo,amesema maonyesho ya biashara ya mwaka huu yatakuwa ya aina yake kutokana na mbaoresho mbalimbali na 24 hadi sasa zimedhibisha kushiriki maonyesho hayo.

  Amesema katika mwaka huu watatoa tuzo kwa banda bora hivyo wanatakiwa kufanya maresho ya mabanda hayo ili kuweza kupata tuzo hiyo. Viingilio katika maonyesho ya 39 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam vitakuwa sh.3000 kwa wakubwa na watoto Sh.1000.
    Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE (katikati) akizungumza katika mkutano wa maandalizi ya maonyesho ya 39 ya kimataifa  ulifanyika katika viwanja vya SabaSaba jijini Dar es Salaam leo.
   Mkurugenzi wa Biashara za Nje,Anna Bulondo, akizungumza katika mkutano wa maandalizi ya maonyesho ya 39 ya kimataifa  ulifanyika katika viwanja vya SabaSaba jijini Dar es Salaam leo.
   Baadhi ya wandishi wa habari waliohudhurika katika mkutano wa maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa,ulifanyika katika viwanja vya Saba Saba jijini Dar es Salaam leo. (PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII).

  0 0


  0 0

    Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja (Katikati) akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya Michezo kwa klabu ya Mpira ya Lucenti, itakayoshiriki michuano ya kanda ya Nyanda za juu kusini, itakayofanyika Sumbawanga Mkoani Rukwa. Kushoto ni Meneja Fedha wa Benki hiyo Patrick Kyamba na Mwenyekiti wa Klabu ya Lucent, Yusuph Liambe.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, (Katikati) Mwenyekiti wa Klabu ya Lucenti, Yusuph Liambe, Mkurugenzi wa Bodi ya Benki hiyo Margreth Kyarwenda wakiwa wameshikilia vifaa vya michezo vilivyotolewa na Covenant Bank kwa timu hiyo itakayoshiriki michuano ya kanda ya nyanda za juu kusini itakayofanyika Sumbawanga Mkoani Rukwa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja akimkabidhi Mwenyekiti wa Klabu ya Lucenti, Yusuph Liambe vifaa vya michezo kwa ajili ya maandalizi ya Timu hiyo itakayoshiriki michuano ya kanda ya nyanda za juu kusini itakayofanyika Sumbawanga Mkoani Rukwa. Wanaoshuhudia ni Meneja Fedha wa benki hiyo. Patrick Kyamba na Mkurugenzi wa Bodi Margreth Kyarwenda. 


  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  BUNGE LA TANZANIA
   TAARIFA KWA UMMA
  YAH: UWASILISHWAJI WA MPANGO NA UKOMO
  WA BAJETI KWA MWAKA 2015/16
  _______________

  Kesho Jumatano tarehe 29 Aprili, 2015 Wabunge wote kwa ujumla wao watakutana katika Ukumbi wa Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam kupokea Mapendekezo ya Mpango, Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2015/2016 kwa mujibu ya matakwa ya Kanuni ya 97 ya kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la 2013.

  Shughuli hiyo itaanza rasmi saa tatu na nusu asubuhi kwa Waheshimiwa Wabunge na Washiriki wote kuwasili na kuketi Ukumbini kabla ya ukaribisho utakaotolewa na Naibu Spika amabaye pia atakuwa mwenyekiti wa Mkutano huo na kufuatiwa na neno la utangulizi kutoka kwa Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda.

  Aidha, Uwasilishwaji wa Mapendekezo ya Mpango wa Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016 yatafanyika kuanzia saa nne asubuhi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahususiano na Uratibu) Mhe. Dkt. Mary Nagu (Mb) na kufuatiwa na uwasilishwaji wa mapendekezo ya kiwango na ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (Mb).

  Shughuli hiyo inatarajiwa kumalizika saa sita mchana, na baadae kamati za Bunge kuendelea na utekelezaji Majukumu yake kulingana na ratiba za kamati.


  Imetolewa na:
  Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa,
  Ofisi ya Bunge
  DAR ES SALAAM
  28 Aprili 2015


older | 1 | .... | 818 | 819 | (Page 820) | 821 | 822 | .... | 3284 | newer