Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 80 | 81 | (Page 82) | 83 | 84 | .... | 3284 | newer

  0 0   Kijana Zuberi Mgeni anayesumbuliwa na maradhi ya moyo yanayopelekea tumbo kujaa maji, anahitaji kiasi cha dola 6000 sawa na shilingi 9.6 milioni kwa ajili ya kwenda India kufanyiwa upasuaji wa maradhi yanayomsumbua.

  Mjomba wa Zuberi, twaha yusuf ugama anasema kulingana na majibu ya madaktari Zuberi anatakiwa kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu ya tatizo lake ikiwa ni pamoja na oparesheni ya kubadili valve za moyo.

  "Vipimo vilifanyika mwezi January, tuliambiwa tuandike barua ya kuomba msaada lakini tangu hapo hatujajibiwa, hivyo tunawaomba wasamaria wema wamchangie kijana huyu ili aweze kufanyiwa upasuaji kuokoa maisha yake.

  Zuberi mwenye umri wa miaka 18 anasema maradhi hayo yamemsababishia maumivu yanayoambata na tumbo kuvimba kupita kiasi pamoja na miguu yake kuvimba ,kushindwa kupumua vizur,kua na mchoko uliopitiliza, hali inayomsababishia karaha na maumivu aliyoyavumilia kwa miaka mitatu sasa.

  "Napumua kwa shida, siwezi kutembea pia ninapata shida wakati wa kulala maisha yangu yamebadilika na wala sina tegemeo kwa maisha yajayo," ni maneno ya kijana Zuberi Mgeni anayesumbuliwa na tatizo la kuvimba kwa tumbo na miguu.

  Hali hiyo imepelekea afya ya kijana huyo kudhorota na tumbo kuwa na ukubwa wa zaidi ya mama mjamzito wa miezi 9, miguu yake kuvimba huku sehemu nyingine za mwili zikionyesha kudhoofu.Inakadiriwa kiasi cha lita za 15 zimerundikana mwilini kwake.

  Akizungumza na Mwananchi juu ya maradhi hayo Zuberi anasema mnamo mwaka 2006 akiwa darasa la tatu katika shule ya Kwale Kizingani Mkoani Tanga, tumbo lake lilivimba kupita kiasi alipelekwa hospitalini na kupewa dawa zilizomrudisha katika hali yake ya kawaida.

  "Ilikuwa likizo, nilikula chakula mchana kwa kuwa sikujisikia vizuri, nilikuwa na homa kali iliyoambatana na mafua nilikwenda kupumzika, nilipoamka jioni saa 12 tumbo langu lilikuwa limevimba sana, nilikwenda hospitali ya Kizingani na kupatiwa dawa, hapo ndipo lilitoweka. Niliendelea na shule hadi mwaka 2010 nilipohitimu darasa la saba," anasema Zuberi.

  Mjomba wa Zuberi, twaha yusuf Ugama anasema baada ya mpwa wake kumaliza darasa ya saba alichaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Kwale ndipo tatizo hilo liliporudi kwa kasi kubwa.

  "Mwanzoni mwa 2011kabla ya kuanza kidato cha kwanza, tatizo lilirudi upya alipopelekwa Kizingani walimwandikia aende hospitali ya Rufaa Bombo iliyopo Tanga mjini. Pale alipewa huduma ya kupunguza maji na kupewa rufaa ya Muhimbili. Aliletwa jijini kwa matibabu," anasema Twaha.

  Anasema tatizo hilo lilianza kuwa sugu na iliwalazimu kuhudhuria kliniki. "Tukiwa Muhimbili tulipatiwa huduma ya kliniki ilikuwa na ugumu kidogo kutokana na mgonjwa kutokuwa na kadi ya matibabu. Ilipofika Septemba 2012 daktari bingwa wa Moyo aliyekuwa akimhudumia alituambia kwamba hali ya mgonjwa itakuwa ngumu kutibika," anasema twaha.
  Anasema Zuberi alisikia kauli ya daktari iliyomfanya akate tamaa ya kuishi "Alirudi Tanga na muda mfupi baadaye alizidiwa tena.

  Ndipo mmoja wa wanafamilia alikutana na tabibu ambaye anatokea Tanga,anaitwa samwel shita ambaye yuko masomoni ya udaktar kwa sasa,aliamua kuchukua jukumu la kumsaidia uchunguzi upya,akisaidiana na daktari bingwa wa moyo dokta henry mayala katika hospital ya Sanitas .

  Waligundua anatatizo la valve za moyo wake hivyo moyo kushindwa kufanya kazi vizur dokta mayala aliandika maelezo yakina na sababu za tatizo la zuberi kiundani nzaidi,Alieleza kutokana na tiba hiyo haipo hapa nchini ,inahitajika kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji kubadili valve zake.

  Baada ya hapo alifanyiwa tena uchunguzi katika hospitali ya regency,baaada ya uchunguz na matibabau sehemu hizi mbili,regency na sanitas ndipo matumini mapya yalirud kwa zuberi. Akiwa Regency Zuberi alifanyiwa vipimo na madaktari

  Twaha anasema kiasi hicho cha fedha kitasaidia matibabu ya Zuberi yanayogharimu kiasi cha dola 2500 sawa na milioni 4 pamoja na fedha zingine kwa ajili ya tiketi ya ndege yeye na msindikizaji wake kwenda na kurudi pamoja na gharama nyingine watakapokuwa huko kwa matibabu.

  Hospitali alizowahi kutibiwa

  Kizingani iliyopo Kwale Tanga
  Hospitali ya rufaa Bombo Tanga mjini
  Hospitali ya taifa ya Muhimbili
  Sandarya Medics Dar
  Sanitaz Hospital Dar
  Temeke Hospitali
  Hospitali ya Regency

  0 0


  Mchakato wa mashindano ya Fifa Copa Coca Cola kwa mwaka 2013 umeanza rasmi leo ambapo Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Leodgar Chilla Tenga alifungua semina elekezi iliyoshirikisha makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa na waratibu wa mikoa wa michezo ya UMISSETA ambao katika ngazi ya wilaya na mkoa wao ndio waendeshaji na wasimamizi wa mashindano hayo. 


  Kikosi cha Timu ya Vijana ya Bifra (BYFT) kilichoshiriki michuano ya Copa Coca Cola (17) mwaka 2012 mkoa wa Kinondoni


  BYFT wakisalimiana na wachezaji wa African Talent - Copa Coca Cola (U17) 2012
  Rais Tenga alitanabaisha kwamba kuanzia mwaka huu, michuano ya FIFA Copa Coca-Cola itakuwa ikishirikisha watoto wenye umri chini ya miaka 15. Hivyo, amewataka viongozi wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kuhakikisha wanaingiza wachezaji wenye umri sahihi katika michuano hiyo. 
  Nahodha wa BYFT (kulia) pamoja na mwamuzi na nahodha ya African Talent
  Rais Tenga alionya kuwa hakuna jambo la kipuuzi kama kuchomekea wachezaji ambao wamezidi umri unaotakiwa kwa vile lengo la michuano ya aina hiyo ni kubaini vipaji na kuwafanya watoto wapende kucheza mpira wa miguu. Pia alisisitiza washiriki wa semina hiyo kuwepo wakati michuano hiyo ikiendelea “Kwanza nawashukuru kwa kutenga muda wenu na kuhudhuria semina. Lakini ni vizuri pia mkahakikisha mnakuwepo kwenye mashindano ili kutekeleza haya ambayo tutakubaliana katika semina hii. Mkileta mtu mwingine anaweza kutuanzishia mambo mengine badala ya yale tutakayokubaliana,” amesema Tenga.
  Baadhi ya wachezaji wa BYFT wakiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Klabu ya Biafra - Michael Silili (mweye fulana ya nyeupe)
   
  Michuano hiyo kwa mwaka huu 2013 inatarajiwa kuanzia katika ngazi ya wilaya mwezi Aprili na fainali zake katika ngazi ya taifa zitafanyika mwezi Septemba.  
   
  Viongozi, wachezaji na mashabiki wa BYFT katika picha ya pamoja
  Klabu ya michezo ya Biafra inatarajia kuingiza timu yake ya vijana katika michuano mara baada ya Kamati ya Utendaji kukutana nakocha, mameneja wa timu pamoja na wachezaji ili kupanga mikakati ya ushiriki wao.


  0 0
 • 03/26/13--12:54: Mambo ya GAdo leo


 • 0 0
 • 03/26/13--13:12: Mambo ya Mnazi Mmoja Lindi
 •  Hapo mmoja buku...anasema mdau 
  Gerson Msigwa aliyekuwa huko majuzi


  0 0

   Mwimbaji wa nyimbo za injili, Solomon Mukubwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu maandalizi yake katika tamasha la Pasaka 2013.
  Mwimbaji wa nyimbo za injili, Faraja Ntaboba akiimba kwa hisia moja ya nyimbo zake mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
  Mwenyekiti wa Kamati Maalumu inayoratibu tamasha hilo la kimataifa, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu maandalizi ya tamasha hilo.

  DAR ES SALAAM, Tanzania

  WAKATI muimbaji Sipho Makhabane wa Afrika Kusini akitarajiwa kutua Ijumaa, waimbaji wa nyimbo za injili kutoka Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wamewasili jana jijini Dar es Salaa, tayari kwa ajili ya kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka, litakaloanza Machi 31 kwenye Uwanja wa Taifa jijini.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Kamati Maalumu inayoratibu tamasha hilo la kimataifa, Alex Msama aliwataja waimbaji waliowasili jana kuwa ni Solomoni Mukubwa (Kenya) na Faraja Ntaboba (DRC).

  Msama aliwataka wapenzi, mashabiki na wadau wa muziki wa injili kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo, ambalo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ili kuunga mkono juhudi za kampuni yake kuandaa tamasha hilo kwa malengo mbalimbali ikiwemo kueneza injili ya Mungu na kusaidia makundi maalumu.

  Kuhusu waimbaji, Msama alisema kuwa hadi kufikia Ijumaa, wakali wote wa nyimbo za injili kutoka nje watakuwa wamewasili jijini tayari kwa tukio hilo linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Dar es Salaam na mikoa yote ambayo tamasha huilo litarindima.

  Aidha, mkali wa aina hiyo ya muziki kutoka Kenya, Mukubwa, alisema kuwa amejiandaa vya kutosha katika tamasha la mwaka huu ambalo limebeba ujumbe wa Upendo na Amani.

  “Wakati wa Uchaguzi wa Nchini Kenya tuliimba na kuhamasisha Amani na Upendo na kwa kupitia tamasha hili tutaimba nyimbo za kuhamasisha Amani na Upendo hapa Tanzania,” alisema Mukubwa. 

  Naye mwimbaji kutoka DRC, Ntaboba alisema kuwa, watu wajitokeze kwa wingi katika tamasha hilo na kupata burudani itakayokwenda sambamba na mafundisho ya dini.

  Msama aliongeza kuwa idadi ya waimbaji imeongezeka baada ya kujitokeza kwa nyota mwingine aliyemtaja kwa jina moja la Ntutuma kutoka Kenya, ambapo baada ya tamasha hilo kutikisa kwenye jijini Dar es Salaam, itakuwa zamu ya Dodoma, Iringa, Mbeya, Mwanza kabla ya mashambulizi kuhimishwa mkoani Mara.

  0 0


  0 0

  Dear Friend,
  I was born intelligent but education has ruined me. May your day be punctuated with a revanchism whose magniloquence can only be theatropistically analysed by the use of a reminiscent excarbation. 

  I hope you don't mind my apostasy. I know your arquistic impedance might not  engulf this kind of debanched pedagogy because of its repuginatious tolecentrism...

  RGDS
  Mimizzz


  0 0


  President Barack Obama appointed the first woman to lead the US secret service in its 148-year-old history. The appointment does not need Senate approval.

  Julia Pierson, a secret service veteran who spent much of her career based in Florida, takes on responsibility for the safety of Obama and his family, the vice-president, other leading Washington figures and visiting international dignitaries. She is at present chief of staff at the secret service.


  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola duniani, Sir Alan Haselhurst(kati) akiwa katika mazungumzo na Mhe.Job Ndugai, Naibu Spika wa Tanzania na Katibu wa Bunge, Dr Thomas Kashililah kwenye Bunge la Uingereza.Naibu Spika anaongoza wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge kwa ziara maalum ya kibunge nchini humo.Mwingine pichani ni Katibu wa CPA Uingereza, Nd.Andrew Tuggey.
  Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge wakipata maelezo kuhusu Bunge la Uingereza wakati wa ziara yao.Ziara hiyo inaendelea ikiwa na lengo la kuwaongezea uwezo wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge namna Bunge la Uingereza linavyofanya kazi. 
  Naibu Spika akipokea zawadi toka kwa Mwenyekiti wa CPA duniani, Sir Alan Haslehurst walipokutana nchini Uingereza.
  Katibu wa Bunge ambae pia ni Katibu wa CPA Afrika, Dr Thomas Kashililah akikabidhi zawadi kwa Katibu wa CPA Uingereza; Nd.Andrew Tuggey wakati wa ziara hiyo.Picha zote na Saidi Yakubu.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji DKT. Mary Nagu (katikati) akifurahia jambo na viongozi wa makampuni ya china (kushoto) ni Mkuu wa chama cha ushirikiano cha China Bw. Charles Li wakiwa wanaonyesha bango lenye maandishi ya lugha ya China kuonyesha ushirikiano kati ya China na Tanzania (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi wa WCUGA International Group Bw. Tiger Liang.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) Bw. Raymond Mbilinyi (kushoto) akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, DKT. Mary Nagu wakielekea katika ukumbi wa kivukoni katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam juzi jioni kuonana na ujumbe wa wawekezaji wa china kwa ajili ya kujadili namna ya kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji hapa nchini. Ujumbe huo wa makampuni kumi na tano toka nchini China uliongozwa na Mkuu wa chama cha ushirikiano cha China Bw. Charles Li.


  0 0


  SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo lilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na baadhi ya wagombea kulalamika kuenguliwa sasa litatuma ujumbe wake nchini katikati ya mwezi ujao.

  Ujumbe huo ambao moja ya shughuli zake kuwasikiliza wote walioenguliwa na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF na hawakuridhika na uamuzi huo, utakuwepo nchini Aprili 16 na 17 mwaka huu.

  Kwa mujibu wa barua ya Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke kwenda kwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga, kazi ya ujumbe huo ni kubaini tatizo lililopo na kutoa ripoti kwa mamlaka zinazohusika ndani ya FIFA kwa ajili ya kutoa mwongozo.

  Ujumbe huo utakutana na pande mbalimbali zinazohusika wakiwemo wagombea, kamati za uchaguzi za TFF. Lakini pia ujumbe huo unatarajia kumtembelea Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara pamoja na watendaji wake wizarani.

  Uchaguzi wa viongozi wa TFF ulikuwa ufanyike Februari 24 mwaka huu, lakini ukasimamishwa na FIFA baada ya baadhi ya wagombea walioenguliwa kulalamika kuwa hawakutendewa haki na wangependa shirikisho hilo liingilie kati.

  Boniface Wambura
  Ofisa Habari
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0

   Mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia,Nyoshi el Sadaat (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo juu onyesho lao maalum litakalofanyika kesho Alhamisi kwenye Ukumbi wa East 24 Bar,uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.Kushoto na kulia ni Maafisa wa Kampuni ya Mabibo,Julius Mapunda na Vailet Otina ambao ndio wadhamini wa Onyesho hilo chini ya Kinywaji chao cha Windhoek Lager.
   Nyoshi el Sadaat akighani moja ya nyimbo zake mpya atakazozitambulisha rasmi kesho.
  Afisa wa Kampuni ya Mabibo,Julius Mapunda akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo juu onyesho la FM Academia litakalofanyika kesho Alhamisi kwenye Ukumbi wa East 24 Bar,uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe.Peter Kallaghe akiwa katika mazungumzo na Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge waliokwenda kumsalimu ofisini kwake jana jioni wakiongozwa na Naibu Spika Mhe.Job Ndugai.
  Picha ya pamoja baina ya ujumbe wa Bunge la Tanzania ulioko Uingereza na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania. Picha kwa hisani ya Ofisi ya Bunge.

  0 0

  Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.

  Askari Polisi Nchini wametakiwa kuendelea kutoa huduma bora kwa Wananchi ili kuendeleza mahusiano mema na Jamii pamoja na kushirikiana katika kuendeleza mpango wa Polisi jamii na Ulinzi shirikishi ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kuwafichua wahalifu hapa nchini tangu kuanzishwa kwake.

  Hayo yalisemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema wakati alipokuwa akizindua Programu za Mafunzo kazini kwa askari Polisi Tanzania nzima katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Jijini Dar es Salaam ambapo uzinduzi huo ulihudhuriwa na Maofisa mbalimbali wa Polisi pamoja na Askari kutoka Makao makuu ya Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam pamoja na Vikosi vilivyopo jijini Dar es Salaam.

  IGP Mwema alisema jambo la kutoa huduma bora kwa wananchi siyo la hiari bali ni la lazima hivyo kila askari anapaswa kuboresha huduma anayoitoa kwa kuzingatia mafunzo aliyonayo ili kuleta ufanisi wa kazi na kuimarisha usalama wa raia na mali zao. Alisema Wananchi nao wanapaswa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa Jeshi hilo ili ziweze kufanyiwa kazi kwa haraka katika kuzuia, kubaini na kutanzua uhalifu hapa Nchini.

  “Usalama unaanza na mimi, wewe na sisi sote hivyo kila mmoja anatakiwa ajiulize anachangia nini katika kuimarisha ulinzi wake binafsi, wa jirani yake na wa taifa kwa ujumla kwa vile suala hili siyo la Jeshi la Polisi peke yake ni wajibu wa kila mmoja” Alisema IGP Mwema.

  Aidha aliwataka Maofisa na Askari kuitumia vyema fursa ya Mafunzo kazini kujiendeleza kielimu ili kuboresha ufanisi wao katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku pamoja na kukabiliana na changamoto mbalimbali za kazi na maisha.

  Mwema alitoa wito kwa kila Askari na Ofisa kuutumia vyema mpango huo wa mafunzo kazini kujitengea muda vizuri kwa ajili ya kujisomea nje na saa za kazi ili kuboresha huduma bora kwa wananchi ambapo alisisitiza suala la kutoa huduma bora kwa wananchi siyo la hiari ni kuto na maboresho ya Jeshi la Polisi yanayolenga kufanya kazi kwa weledi na usasa katika kuihudumia jamii na wananchi ..

  0 0

  mfanyanyazi wa Mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold (ABG) akiwa na tuzo ya ufanyakazi bora kwenye idara ya mahusiano ya jamii kwenye sherehe zilizofanyika mgodini hapo Machi 21, 2013. Shayo na timu nzima ya mgodi huo wamepewa tuzo hiyo kutokana na mradi wa kusaidia kikundi cha wanawake cha Nyabichune kijikwamue kiuchumi.
  Igor Gonzales, makamu wa rais mtendaji na afisa mwandamizi (Executive Vice President & Chief Operating Officer) wa kampuni ya Barrick Gold Corp. (kushoto), akitoa zawadi ya tuzo ya mfanyakazi bora kwa Godfrey Nyabuzoki, mfanyakazi wa kitengo cha ulinzi cha mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold kwenye sherehe iliyofanyika Machi 21, 2013. Godfrey na wafanyakazi wengine watano wa kitengo cha ulinzi cha mgodi huo walionesha ujasiri mkubwa kukabiliana na kundi kubwa la wananchi waliovamia mgodi huo mwezi Machi mwaka huu na wafanyakazi hao wakaweza kumuokoa mwenzao aliyeumia. Kulia ni makamu wa rais wa kampuni ya Barrick Gold Corp. anayeshughulikia masuala ya ulinzi, Mark Wall.
  Marco Zolezzi, afisa mwandamizi (Chief Operating Officer) wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold, akitoa zawadi ya tuzo ya mfanyakazi bora kwa mfanyakazi wa kitengo cha uchunguzi cha mgodi wa Bulyanhulu, Gilbert Kalisa, kwenye sherehe zilizofanyika Machi 21, 2013, kwenye mgodi huo.
  Lolence Kasekenya, mfanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (katikati) akiwa na zawadi yake ya mfanyakazi bora kwenye kitengo cha mahusiano ya jamii katika sherehe iliyofanyika kwenye mgodi huo tarehe 22 Machi 2013. Kulia ni Don Ritz, makamu wa rais mwandamizi wa kampuni ya Barrick anayeshughulikia usalama na uongozi na Kevin D'Souza, Mkurugenzi mwandamizi wa ABG upande wa mahusiano ya jamii na mazingira.

  0 0
 • 03/27/13--07:40: LINDI WAAZIMIA KUJIUNGA CHF
 • Diwani wa Kata ya Kilangala wilayani Lindi Vijijini Somoe Mwaya akihamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
  Meneja wa CHF, Constantine Makalla akimsikiliza mmoja wa wananchi waliohudhuria mafunzo hayo.
  Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma Grace Kisinga akielekeza kauli mbiu ya NHIF/CHF kwa wananchi, kushoto kwake ni Meneja wa NHIF Mkoa wa Lindi Fortunata Raymond.

  BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI

  0 0


  Katika gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno ‘ SIRI YA KUUAWA ZITTO YAFICHUKA’ na vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini’ dk. Slaa atajwa kumtuma Saanane kummaliza’. Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa. Napenda kusema yafuatayo:
  Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.
  Pili, Siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuwawa na mtu mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu. Ndio maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya Zitto yataishi tu. Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari na uaminifu. Siku zote nitasimamia ukweli bila kujali uchungu wa ukweli huo.
  Tatu, nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa. CHADEMA sio pango la watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki. Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.
  Nne, Nawashauri viongozi wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.
  Kabwe Zuberi Zitto, Mb
  Dar-es-Salaam
  Jumatano, Machi 27, 2013

  0 0

  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mh. Jaji Frederick Werema akimkaribisha Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Mathias Chikawe (mwenye miwani) kwenye ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
  Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Mathias Chikawe (watatu kushoto waliokaa) kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Mkurugenzi wa Sayansi ya Uhai, Dkt. Flora Tibazarwa, wakati Makamu alipofanya ziara ya kutembelea katika maonyesho ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Kijitonyama leo Machi 27, 2013 kujionea maendeleo ya tume hiyo inayozalisha vijana wabunifu wa masuala ya kisayansi. Kushoto kwa Makamu wa Rais ni, Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza MMtafiti wa TEHAMA kutoka COSTECH, Rahma Bashary, wakati Makamu alipofanya ziara ya kutembelea katika maonyesho ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Kijitonyama leo Machi 27, 2013 kujionea maendeleo ya tume hiyo inayozalisha vijana wabunifu wa masuala ya kisayansi. Kulia ni, Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya chupa ya dawa ya kuongeza virutubisho mwilini, Juice Lishe,(Morizella Juice) huku akimsikiliza Dkt. Modest Kapingu, kuhusu matumizi ya dawa hiyo, wakati Makamu alipofanya ziara ya kutembelea katika maonyesho ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Kijitonyama leo Machi 27, 2013 kujionea maendeleo ya tume hiyo inayozalisha vijana wabunifu wa masuala ya kisayansi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa namna ya kutumia simu ya mkononi kuunganisha huduma ya mtumiaji simu ili kupata taarifa ya mkulima kutoka kwa Gwaliwa Mashaka wa Kampuni ya Spendid Amos, wakati Makamu alipofanya ziara ya kutembelea katika maonyesho ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Kijitonyama leo Machi 27, 2013 kujionea maendeleo ya tume hiyo inayozalisha vijana wabunifu wa masuala ya kisayansi. Kushoto kwa Makamu wa Rais ni, Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa maonyesho ya Kisayansi yaliyoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia, leo Machi 27, 2013.Picha na OMR.

  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, amemteua Balozi Isaac Abraham Sepetu kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA).

  Kwa mujibu wa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, uteuzi huo umeanza leo Jumatano tarehe 27 Machi, 2013.

  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
  27 Machi, 2013.

older | 1 | .... | 80 | 81 | (Page 82) | 83 | 84 | .... | 3284 | newer