More Channels
Showcase
Articles on this Page
(showing articles 16221 to 16240 of 65641)
- 04/21/15--03:03: _BREAKING NYUZZZZZZ....
- 04/21/15--03:08: _MAKALA YA SHERIA: H...
- 04/21/15--03:23: _TAARIFA YA JESHI LA...
- 04/21/15--03:30: _MAELFU YA RAIA WAPY...
- 04/21/15--04:02: _bei ya Madafu leo
- 04/21/15--04:17: _BORA KUFIKA
- 04/21/15--04:22: _YANGA, ETOILE ZAING...
- 04/21/15--04:28: _UNICEF PAYS TRIBUTE...
- 04/21/15--04:45: _KAMPUNI ZA SIMU ZAS...
- 04/21/15--06:58: _MAABARA YA BRN KUCH...
- 04/21/15--07:16: _Mahafari ya 11 ya L...
- 04/21/15--07:36: _Mrema aunguruma Vunjo
- 04/21/15--07:45: _BALOZI WA MALAWI N...
- 04/21/15--08:33: _SHIRIKA LA BIMA LA ...
- 04/21/15--08:44: _TAARIFA YA JESHI LA...
- 04/21/15--08:50: _WAZIRI WA UCHUKUZI ...
- 04/21/15--08:59: _JKT YAZIDI KUIBUA M...
- 04/21/15--13:02: _MFUKO WA LAPF WATOA...
- 04/21/15--13:10: _mikataba ya mabilio...
- 04/21/15--13:14: _Watanzania 18 warej...
(showing articles 16221 to 16240 of 65641)
Channel Description:
Most read Swahili blog on earth
0 |
|
0 |
|
Watuhumiwa wa Ujambazi wakiwa wamewekwa chini ya Ulinzi mara baada ya kutiwa mbaroni kwenye mataa ya Red cross katikati ya jiji Dar es salaam muda huu. inaelezwa kuwa Majambazo hao walimvamia na kumpora raia mmoja wa kigeni (Mzungu) maeneo ya Kinondoni na kufanikiwa kukimbia, lakini kumbe wakati wanafanya tukio hilo kuna raia aliwaona na alijitolea kuwakimbiza kwa gari na kuwanikiwa kuwablock maeneo hayo ya Red Cross ambapo huwa na askari wengi wa doria, wamekamatwa na bunduki mbili.
Watuhumiwa hao wakiwa chini ya ulinzi, huku wengine wakijaribu kuficha nyuso zao.
0 |
|
0 |
|
Na Bashir Yakub.
Kuna malalamiko katika baadhi ya maeneo na zaidi malalamiko haya yamekuwa yakielekezwa kwa mamlaka za serikali za mitaa. Nimewahi kuandika kuhusu ukiukaji wa taratibu mbalimbali ambao hufanywa na serikali za mitaa katika maeneo au ardhi za watu. Pia niliandika kuhusu upotoshi wa mamlaka za serikali za mitaa katika kuwaandalia watu mikataba ya mauzo ya ardhi wakati wakijua kuwa hawaruhusiwi kufanya hivyo jambo ambalo huwasababishia wananchi usumbufu mkubwa wanapoamua kutafuta hati au kubadili majina kwakuwa mikataba hiyo ya serikali za mitaa huwa haikubaliki kisheria na hivyo watu hurudishwa kuibadili.
Leo tena nazungumzia ubabe walionao serikali za mitaa wa kutwaa maeneo ya watu na kuyapangia shughuli mbalimbali za mtaa huku yakiwa ni maeneo ya watu binafsi. Kugeuza maeneo ya watu njia bila fidia ni moja ya uonevu mkubwa ambao wamekuwa wakiupata wananchi kutoka serikali za mitaa. Kwa ufupi tutaangazia jambo hilo likoje kisheria.
1.SERIKALI ZA MITAA HAWARUHUSIWI KUTANGAZA ENEO FULANI KUWA NI NJIA.
Serikali za mitaa hawana mamlaka kisheria kuchukua eneo la mtu kulitangaza kuwa njia. Kinyume na ilivyozoeleka ambapo viongozi wa serikali za mitaa hutembea maeneo mbalimbali ya mtaa na kuchukua maeneo ya wananchi kwa madai kuwa yanapaswa kuwa njia. Sheria ya ardhi inasema kwamba serikali kuu au serikali ya mtaa au chombo chochote hakiruhusiwi kutenga maeneo kuwa njia isipokuwa lazima watume maombi kwa kamishna wa ardhi ambaye ndiye atakuwa na mamlaka ya kutangaza eneo fulani kuwa ni njia.
Sheria inaendelea kusema kuwa maombi hayo yatakuwa yamewekwa katika fomu maalum na kujazwa katika namna inayokubalika. Kwa hiyo kumbe hali haiko kama tulivyozoea ambapo serikali za mitaa huamua kuchukua eneo la mtu na kulifanya njia bila ruhusa ya kamishna wa ardhi. Ieleweke kuwa utaratibu ndio huo wa kutuma maombi kwa kamishna wa ardhi na si kuamka asubuhi na kulifanya eneo la mtu kuwa ni njia.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 19.04.2015 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA NAMTAMBALALA, KATA YA NZOKA, TARAFA YA NDALAMBO, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA WIZI WA VIATU, SIMU NA NGUO. WATUHUMIWA WAMEKAMATWA NA UCHUNGUZI ZAIDI WA TUKIO HILI UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI KUFANYA HIVYO NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWANAMKE MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA IYENGA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA PILLY MGALA ALIMUUA MUME WAKE AITWAYE AMADI MWASHAMBWA, (42) MKAZI WA KIJIJI CHA IYENGA KWA KUMCHOMWA KISU KIFUANI.
AWALI MNAMO TAREHE 19.04.2015 MAJIRA YA SAA 21:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA IYENGA, KATA YA ISANSA, TARAFA YA IGAMBA, WILAYA YA MBOZI MWANAMKE HUYO ALIMJERUHI MUME WAKE KWA KUMCHOMA KISU KIFUANI NA KUPELEKEA KUKIMBIZWA KATIKA ZAHANATI YA KIJIJI CHA IYENGA KWA MATIBABU. KUTOKANA NA MAJERAHA ALIYOYAPATA MNAMO TAREHE 20.04.2015 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU.
CHANZO CHA TUKIO HILO NI UGOMVI ULIOTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI BAADA YA MAREHEMU KUMTUHUMU MKE WAKE KUWA SIO MWAMINIFU KATIKA NDOA YAO. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO NA MSAKO MKALI UNAENDELEA WA KUMTAFUTA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANDOA KUTATUA MIGOGORO YAO KWA KUKAA MEZA MOJA NA KUFIKIA SULUHISHO ILI KUEPUKA VITENDO VYA KUJICHUKULIA SHERIA VINAVYOWEZA KUSABABISHA MADHARA NA MATUKIO KAMA HAYA YA MAUAJI.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA KIJANA MMOJA MKAZI WA FOREST YA ZAMANI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EMANUEL SAMWEL (28) AKIWA NA NOTI BANDIA AMBAZO KAMA ZINGEKUWA HALALI ZINGEKUWA NA THAMANI YA TSHS 325,000/=.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 20.04.2015 MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI HUKO ENEO LA ISYESYE, KATA YA ISYESYE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA MBEYA AKIWA KWENYE HARAKATI ZA KUJARIBU KUWEKA PESA HIZO KWENYE AKAUNTI YAKE YA TIGO-PESA KWENYE DUKA LA MARY PATRICK (32) MFANYABIASHARA NA MKAZI WA ISYESYE.
NOTI HIZO ZILIKUWA NA NAMBA DT. 2937833 NOTI 6, BV 2937839 NOTI 10, DT 4243042 NOTI 4, BF 1547948 NOTI 5, BV 4243044 NOTI 8, AA 4243045 NOTI 18, DT 1547949 NOTI 5 NA BC 2937831 NOTI 10. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA PINDI WAONAPO VIASHIRIA VYA UHALIFU AU WANAPOMTUHUMU MTU/WATU ILI HATUA STAHIKI ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imesainiwa na:[AHMED Z. MSANGI – SACP]KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
0 |
|
0 |
|
Mkuu wa Makazi ya Mishamo, Fredrick Nisajile akizungumza na maofisa wake (kushoto) kabla ya kuanza kugawa vyeti vya uraia kwa raia wapya wa Tanzania kijijini Ilangu katika Makazi ya Mishamo, yaliyopo wilayani ya Mpanda Vijijini, Mkoa wa Katavi. Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania.
Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo kuwawiwa ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Afisa Uhamiaji, Philimon Msenya (kushoto) akichukua alama ya vidole kwa raia mpya wa Tanzania, Bukuru Yohana kabla ya kupewa cheti chake cha uraia katika ugawaji wa vyeti hivyo kwa raia wapya zaidi ya 52,565 katika Makazi ya Mishamo yaliyopo wilayani ya Mpanda Vijijini, Mkoa wa Katavi.
Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania. Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo kuwawiwa ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Makazi ya Mishamo, Fredrick Nisajile akizungumza na wazee wa Kijiji cha Ilangu katika Makazi hayo, ambao ni raia wapya wa Tanzania wakati wakisubiria kupewa vyeti vyao vya uraia. Wazee hao wametengewa sehemu maalum ili kupewa kipaumbele kutokana na umri wao ili waweze kupewa vyeti hivyo kwa uharaka zaidi.
Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania. Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo kuwawiwa ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Raia wapya wa Tanzania wa Kijiji cha Ilangu katika Makazi ya Mishamo, wakiwa wameweka foleni ndefu ili waweze kugawiwa vyeti vyao vya uraia kijijini hapo, wilayani Mpanda Vijijini, mkoani Katavi, leo. Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania.
Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo kuwawiwa ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Raia wapya wa Tanzania wa Kijiji cha Ilangu katika Makazi ya Mishamo, wakiwa wameweka foleni ndefu ili waweze kugawiwa vyeti vyao vya uraia kijijini hapo, wilayani Mpanda Vijijini, mkoani Katavi, leo. Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania.
Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo kuwawiwa ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Afisa Operesheni wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Stephen Daniel (kushoto) akiwaelekeza raia wapya wa Tanzania katika Kijiji cha Ilangu, Makazi ya Mishamo, kuwasilisha vyeti vya kliniki vya watoto wao ili waweze watoto wao kuwekwa kwenye kumbukumbu ya Serikali. Watoto wote waliozaliwa baada ya mwaka 2010 ni raia wa Tanzania wa kuzaliwa, hivyo hawatapewa vyeti vya uraia kama wanavyopewa wazazi wao.
Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania.
Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo kuwawiwa ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mchezo no.91 wa Kombe la Shirkisho barani Afrika (CC) hatua ya 16 bora uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam, kati ya wenyeji timu ya Young Africans dhidi ya Etoile du Sahel kutoka Tunisia umeingiza jumla ya sh. 223,135,000.
Jumla ya watazamaji 36,105 walikata tiketi kuhudhuria mchezo huo, huku VIP A zikikatwa tiketi 68, VIP B tiketi 869, VIP C tiketi 582, Orange tiketi 1,955 na viti vya rangi ya Bluu na Kijani tiketi 32,631 ziliuzwa.
Mgawanyo wa mapato ni VAT 18% sh. 34,037,542.37, Gharama ya tiketi sh. 11,462,000, Gharama ya Uwanja 15% sh. 26,645,318.64, Gharama za mchezo 15% sh. 26.645,318.64, CAF 5% sh. 8,881,772.88, TFF 5% sh. 8,881,772.88 na Young Africans 60% sh. 106,581,274.58.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
NAIROBI, 21 APRIL 2015 - With great sadness, UNICEF can now release the names of the four colleagues who were killed in a horrific attack as they travelled to work yesterday in Garowe, northern Somalia.
Those who lost their lives were:
· Mr. Payenda Gul Abed, who had been coordinating UNICEF’s polio immunization efforts in Garowe since May 2014.
· Ms. Brenda Kyeyune, who had managed social mobilization and communication initiatives in support of polio eradication in Somalia since 2014.
· Ms. Woki Munyui, who had been supporting UNICEF’s education work in Somalia since 2007.
· Mr. Stephen Oduor, who had been undertaking vital administrative work for UNICEF Somalia since 2010.
These heroes were dedicated to building a better world for children – today, all of us at UNICEF honour their sacrifice.
Five other UNICEF colleagues are being treated for injuries sustained in the attack, and we hope for their speedy recovery.
Two local security personnel, unrelated to UNICEF, were also killed as a result of the attack, and four others injured.
Our thoughts are with the families of all who died, with those who were injured, and with all our staff who continue to work tirelessly in Somalia to support women and children.
Ofisa Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (kulia) akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa MIC Tanzania (Tigo), Cecilia Tiano (kushoto) wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya miradi miwili ya upelekaji mawasiliano vijijini awamu ya 2A kati ya Mfuko Wa Mawasiliano Kwa Wote (UCSAF)na kampuni za simu za mkononi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Miradi hiyo ni upelekaji wa mawasiliano mipakani na maeneo maalum na mradi wa kuunganisha Intaneti kwenye Shule za Umma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Wa Mawasiliano Kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya miradi miwili ya upelekaji mawasiliano vijijini awamu ya 2A kati ya Mfuko Wa Mawasiliano Kwa Wote (UCSAF)na kampuni za simu za mkononi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Miradi hiyo ni upelekaji wa mawasiliano mipakani na maeneo maalum na mradi wa kuunganisha Intaneti kwenye Shule za Umma.
Ofisa Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (wa kwanza kulia) akisikiliza kwa makini wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya miradi miwili ya upelekaji mawasiliano vijijini awamu ya 2A kati ya Mfuko Wa Mawasiliano Kwa Wote (UCSAF)na kampuni za simu za mkononi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Pamoja naye ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi ya MIC Tanzania (Tigo) Cecilia Tiano (wa pili kutoka kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Tanzania (TTCL) Kamugisha Kazaura (wa tatu kutoka kulia).
Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), imealika wataalamu wa kilimo ili kuchambua na kutoa mapendekezo juu ya namna bora nchi inavyoweza kutatua changamoto ya masoko kwa wakulima. Ili kufikia lengo hilo, maabara ndogo ya siku tano imeandaliwa ili kutathmini mifumo ya sasa ya masoko kwa mazao ya mahindi na mpunga.
Akifungua maabara hiyo jijini Dar es Salaam, Jumatatu, Mtendaji Mkuu wa PDB, Bw. Omari Issa amewataka wadau wote husika kufanya kazi hiyo kwa pamoja katika kuleta majibu yanayolenga mikakati ya muda mfupi na mrefu ili kuwapatia nafuu wakulima.
Alisisitiza kuwa nidhamu ya kiutendaji ya BRN inawataka wadau wa sekta za umma na binafsi kufanyakazi kwa pamoja ili kutatua changamoto zinazozikabili sekta muhimu; ikiwemo ya kilimo na kuongeza kuwa majibu ya changamoto za masoko kwa wakulima yatakoka kwenye pande pande hizo mbili. Maabara hiyo ndogo inajumuisha wawakilishi 50 kutoka sekta za umma, binafsi, taasisi za kimataifa na wakulima wenyewe.
Tanzania nzima, na hususani miradi ya kipaumbele ya kilimo iliyo chini ya BRN, ilishuhudia uzalishaji mkubwa wa mahindi na mpunga katika msimu wa 2013/14; jambo ambalo limeleta fursa nzuri lakini pia lilikuja na changamoto zake. Kwa mfano katika msimu huo, uzalishaji wa mahindi ulifikia tani milioni 6 ikilinganishwa na uzalishaji wa tani milioni 4.5 kwa wastani katika miaka mitano ya nyuma. Mpunga ulifikia tani milioni 1.7 kutoka tani milioni 0.85 mwaka uliotangulia.
Mwisho wa maabara hii, washiriki wataibua mapendekezo na mpango wa utekelezaji utakaoainisha mfumo madhubuti wa masoko ya mahindi na mpunga. Inatarajiwa kwamba mapendekezo haya yataweza kutumika kwa mazao mengine pia.
0 |
|
0 |
|
Apostle Onesmo Ndegi kiongozi wa huduma ya Living Water Centre Ministry Kawe ambaye ndio kiongozi wa kozi hiyo alikuwepo kuhudhuria mahafali hayo, ambayo kozi hiyo ilianza mwaka 2004 ikiwa na wanafunzi wachache ambapo kadri miaka inavyokwenda idadi imekuwa ikiongezeka, na tangu chuo kianze mwaka huu ni mahafali ya 11.
Mahafari hayo yalipambwa na Uimbaji,Maigizo,dance na shuhuda za kile ambacho Mungu amewatendea wanafunzi hao katika kipindi chote walichosoma.Wengi wao katika shuhuda wamesema darasa hilo limewafundisha kumtumikia Mungu zaidi
Wakitoa shukrani zao kwa Mungu na mtumishi wamesema kuwa wamefundishika vyema kwa sababu wapo tofauti sana na walivyokuwa awali kabla ya kuanza darasa na wamefanyika utu upya na kwao hadi jana wanahitimu darasa wamepata mabadiliko makubwa.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Kata ya Makuyuni, Badi Mandali akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi ya uanachama wa Tanzania Labour Party (TLP) katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kata ya Makuyuni, Himo mkoani Kilimanjaro, juzi. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho, Augustine Mrema na mkewe Rose Mrema.
Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema akiongoza maandamano ya wakazi wa Kijiji cha Lole, Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara ikiwa ni shemeu ya ziara yake jimboni humo juzi.
Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema akiwa na wanachama wapya wa chama hicho waliotoka NCCR-Mageuzi, CCM na Chadema mara bada ya kuwakabidhi kadi mpya mara baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Kata ya Makuyuni, Himo mkoani Kilimanjaro, juzi.
0 |
|
0 |
|
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta akimsikiliza Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Hawa Ndilowe alipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake. Waziri wa Uchukuzi na Balozi huyo wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya Uchukuzi na Balozi huyo aliipongeza Wizara kwa kutekeleza vyema miradi inayotekelezwa chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa sasa(BRN).
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta akisisita jambo kwa Balozi wa Malawi, Hawa Ndilowe, alipomtembelea ofisini kwake leo mchana kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya Uchukuzi. Wa pili kutoka kulia ni Afisa Usafirishaji Mwandamizi,kutoka Wizara ya Uchukuzi, Bw. Biseko Chiganga.
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, akimuonyesha mafanikio ya sekta ya Uchukuzi, Balozi wa Malawi, Hawa Ndilowe, alipomtembelea ofisini kwake leo mchana. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw. Sam Kamanga (kushoto) akimkabidhi mikataba ya mauziano ya nyumba zilizopo Buhire wilayani Musoma Mkurugenzi wa wakala wa majengo ya serikali, Bw. Bartazar Kimangano, katika ofisi za shirika hilo leo jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Mwanasheria wa Shirika Bima la Taifa (NIC) Bi. Verdiana Macha,Kaimu Mkurugenzi wa Shirika Bima la Taifa (NIC), Bw. Sam Kamanga, Mkurugenzi wa wakala wa majengo ya serikali, Bw. Bartazar Kimangano na Mkurugenzi wa utafiti na Maendeleo Bi. Asha Myanza wakisaini mikataba ya mauziano ya nyumba zilizopo eneo la Buhire wilayani Musoma leo jijini Dar es Salaam.PICHA NA AVILA KAKINGO WA GLOBU YA JAMII.
0 |
|
0 |
|
Watuhumiwa wanne wamekamatwa jijini Dar es Salaam katika makutano ya barabara ya Bibi Titi na Ohio karibu na Hotel ya Serena baada ya kumpora raia wa kigeni wakiwa na gari dogo rangi ya kijivu yenye nambari za usajili T787 DBU Toyota Cienta.
Hivi karibuni kumeibuka wimbi la wahalifu kuwapora pesa na vitu vya thamani kama mikufu, bangili, hereni pia pete na vitu mbalimbali vya thamani raia wa kigeni na akina mama ambao hupenda kutembea na pochi. Wahalifu hawa hutumia gari dogo ambalo mara kwa mara hubadilishwa namba zake za usajili na wakati mwingine gari hili wanalitumia kama Tax bubu.
Leo tarehe 21/04/2015 majira ya saa 09:00 asubuhi katika eneo la Posta Mpya watuhumiwa hawa walimdangavya bwana CEES S/O JAN CONIJN, Miaka 27, raia wa Uholanzi aliyetaka kufika Klabu ya Leaders kwamba wangempeleka eneo hilo kwa kutumia gari tajwa hapo juu. Baada ya kuondoka na dereva kila baada ya mita 200 dereva huyo alikuwa anasimamisha gari na kuongeza mtu mwingine kama abiria hadi walipotimia wote wane.
Walimpeleka hadi maeneo ya Kinondoni kwa Manyanya na walipofika eneo hilo walimweleza wazi kuwa wao ni wahalifu na walimtaka awapatie pesa vinginevyo wangemuua. Aliwapatia pesa zote alizokuwa nazo Tshs 75,000/= lakini hawakuridhika ndipo walipomtaka awapatie kadi ya benki (ATM CARD) na nambari za siri (Pass Word).
Baada ya tukio hilo wakamtupa karibu na Hospitali ya Mwananyamala na wao wakageuza gari kurudi katikati ya mji. Wakati tukio hilo linatokea raia wema walishuhudia na kutoa taarifa kwa Polisi. Polisi walifuatilia haraka na kuweka mtego uliowanasa watuhumiwa wote katika eneo la makutano ya barabara ya Bibi Titi na Ohio karibu na Hotel ya Serena.
Majina ya watuhumiwa waliokamatwa ni:
1.SALUM S/O SAID MTUMWA @ MARO, Miaka 25, Mkazi wa Chang’ombe Bora.
2.ALEX S/O INNOCENT MANGUKA @ MAKA, Miaka 30, Mkazi wa Kimara Temboni.
3.MOHAMED S/O ALLY ABDALLA @ MEDY, Miaka 27, Mkazi wa Mwananyamala.
4.STEPHANO S/O ALBERT KIKINDI @ KING, Miaka 32, Mkazi wa Mwananyamala.
Walipopekuliwa watuhumiwa hawa walikutwa na simu mbalimbali za mkononi zipatazo 11 ambazo zinachunguzwa kuhusiana na mbinu ya uhalifu wanaoutumia. Pia ilikamatwa ATM CARD iliyochukuliwa kwa mlalamikaji kabla watuhumiwa hao hawajaitumia. Aidha gari namba T787 DBU Toyota Cienta linashikiliwa kwa uchunguzi zaidi.
Miongoni mwa watuhumiwa waliokamatwa, wawili ambao ni MOHAMED S/O ALLY ABDALLA @ MEDY, na STEPHANO S/O ALBERT KIKINDI @ KING, tayari wanazo kesi nyingine mahakamani na wako nje kwa dhamana.
Sambamba na tukio hili oparesheni ya kuwakamata wahalifu wengine wenye mtindo huu wa kuwapora wageni au wakina mama wenye mikoba inaendelea na tunawaomba wananchi waonyeshe ushirikiano wa kutosha ili kutokomeza vitendo hivyo viovu. Aidha hakuna silaha yoyote iliyotumika au kukamatwa kama ilivyoripotiwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM.
0 |
|
0 |
|
Waziri wa Uchukuzi, Samweli Sitta (wa pili kutoka kulia) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Awadh Massawe, wakati akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Mamlaka hiyo leo mchana. Wa kwanza Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka.
Mbunifu majenzi kutoka kampuni ya K &M Acrplans (T) ltd, ambao ndio washauri wa ujenzi wa Jengo hilo, Arch. Albert Mwambafu, akitoa maelezo kwa Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta ya sehemu mbalimbali za jengo hilo, leo mchana wakati Waziri huyo alipotembelea jengo hilo kuona maendeleo ya Ujenzi wake. Jengo hilo litakuwa na ghorofa 35, lakini litakuwa na ofisi mbalimbali na Ukumbi utakaoweza kuchukua watu 1,200 kwa wakati mmoja.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Awadhi Massawe (wa tatu kutoka kushoto), akitoa maelezo ya namna ukumbi ulioko kwenye jengo utakavyokuwa kwa Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, leo mchana wakati Waziri huyo alipotembelea jengo hilo kuona maendeleo ya ujenzi wake.
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta akiangalia Boya ya Kupakulia mafuta la SPM, kupitia juu ya jengo jipya la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA),leo mchana wakati alipotembelea jengo hilo kuona maendeleo ya ujenzi wake.Jengo hilo linatarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwaka huu.
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, akitoa maelekezo kwa viongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wakandarasi na viongozi kutoka Wizara ya Uchukuzi, baada ya kuangalia maendeleo ya jengo jipya la leo mchana. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi).




0 |
|
0 |
|
Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Mfuko wa LAPF, Yesaya Mwakifulefule (wa pili kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, Christina Mndeme, msaada wa rangi zenye thamani ya sh. milioni 3 kwa ajili ya umaliziaji wa ujenzi wa maabara katika shule za Ulanga Mashariki.
0 |
|
0 |
|
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (Universal Communications Service Access Fund - UCSAF) Eng Peter Ulanga (Katikati) akiwa na Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa, Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka Ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma, CEO wa TTCL Dr. Kamugisha Kazaura wakiweka sahihi mikataba ya mabilioni kupelekea mawasiliano vijijini.
Afisa Mtendaji Mkuu WA Mfuko WA Mawasiliano kwa Wote (Universal Communications Service Access Fund - UCSAF) Eng Peter Ulanga (Kulia) akitia sahihi mikataba ya mabilioni kupelekea mawasiliano vijijini pamoja na CEO WA TTCL Dr. Kamugisha Kazaura.
Afisa Mtendaji Mkuu WA Mfuko WA Mawasiliano kwa Wote (Universal Communications Service Access Fund - UCSAF) Eng Peter Ulanga (WA pili kulia) akibidilishana mawazo na Waziri WA Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa baada ya kutia sahihi mikataba ya mabilioni kupelekea mawasiliano vijijini.
Afisa Mtendaji Mkuu WA Mfuko WA Mawasiliano kwa Wote (Universal Communications Service Access Fund - UCSAF) Eng Peter Ulanga (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na (Kutoka Kushoto) Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia John Mngodo, Mkurugenzi mkuu WA Mamlaka Ya Mawasiliano Tanzania Prof. John Nkoma,Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa, (Kutoka Kulia) CEO WA TTCL Dr. Kamugisha Kazaura, mwakilishi kutoka kampuni ya mtandao ya simu za mkononi Airtel Ronald Mitti pamoja na wawakilishi wengine wa mitandao ya simu za mkono pamoja na wafanyakazi wa Mfuko huo.
Bw. Sabri Hery Omari ambaye ni miongoni mwa Watanzania waliorejea nae akizungumza na Waandishi wa Habari huku sehemu nyingine ya Watanzania hao wakionekana kwa nyuma.
Watanzania waliurudishwa Nchini wakitokea nchini Yemeni kutokana na machafuko yanayoendelea huko wakifurahi kuwa nyumbani salama |
=================================
Na Reuben Mchome
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imefanikiwa kuwarejesha nyumbani jumla ya Watanzania kumi na nane kutoka nchini Yemen kufuatia mapigano yanayoendelea nchini humo ya wenyewe kwa wenyewe.
Watanzania hao ambao wamewasili nchini leo kwa ndege ya shirika la emirates namba EK 725 wameishukuru serikali kutokana na jitihada za haraka zilizofanywa kupitia ubalozi wa Tanzania nchini Oman na kufanikiwa kuwarejesha salama pasipo gharama zozote .
Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Watanzania hao Bw. Sabri Abeid Almaghi ambaye alikua anafanya biashara nchini Yemen amesema kuwa anaishukuru Serikali ya Tanzania kwa namna ya pekee kwa kuwajali wananchi wake bila kujali wapo nchini au nje ya nchi na kutoa msaada kwa wakati.
“Tunaishukuru sana serikali yetu ya Tanzania kwa jinsi ambavyo wanajali wananchi wake bila kujali wapo ndani au nje ya nchi, kweli kama sio jitihada za ubalozi wetu pale mjini Muscat, sijui leo tungekua katika hali gani, tunaomba shukrani zetu mzifikishe kwa Rais Kikwete, Waziri Membe na wahusika wengine wote waliofanikisha kuturejesha nyumbani” alisema Mzee Saleh Mbaraka Jabri mmoja wa watanzania hao waliorejea kutoka Yemen.
Aidha, akizungumzia hali ya usalama ilivyo nchini Yemen, Bw. Almaghi amesema kuwa hali ni mbaya sana kufuatia mapigano ya anga yanayoendelea hivi sasa na muda wowote yataanza mapigano ya ardhini. Aidha amesema kuwa kufuatia hali hiyo huduma zote za kijamii pamoja na biashara zimesimama.
Akizungumza mara baada ya kuwapokea watanzania hao Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini Bi. Mindi Kasiga amesema mpaka hivi sasa watanzania ambao wamesharejeshwa nchini kutoka Yemen ni 23, kati ya Watanzania 69 ambao wamejiandikisha na jitihada zinaendelea.
“Awamu ya kwanza ya Watanzania waliorejeshwa na serikali kutoka nchini Yemen ni familia moja ya watu watano ambao walirudi wiki chache zilizopita” alimalizia Bi. Mindi Kasiga.
Hivi karibuni Serikali kupitia Waziri wa Mambo na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe ilitangaza kuwarejesha nchini Watanzania waliopo Yemen kufuatia machafuko yanayoendelea nchini humo.