Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

AIRTEL YATOSHA YAINGIA MITAANI

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania,Sunil Colaso akiongea na meneja wa Uhusiano wa Airtel Tanzania,Jackson Mmbando wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembelea wateja wao na kutoa elimu ya huduma zao ikiwemo huduma mpya ya Airtel Yatosha inayompa mteja, Simkadi moja, taifa moja na bei moja.
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Airtel Tanzania,Godfrey Mugambi akimsajili mtenja mpya wa Airtel,Mzee Jumanne Ally mkazi wa Namanga Msasani wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembea wateja wao na kutoa elimu ya huduma zao ikiwemo ya Airtel Yatosha.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya akimpa maelekezo ya huduma ya Airtel Yatosha mmoja wa wateja wa Airtel alietambulika kwa jina la Juliana wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembelea wateja wao na kutoa elimu ya huduma zao ikiwemo huduma mpya ya Airtel Yatosha inayompa mteja, Simkadi moja, taifa moja na bei moja.
Mkurugenzi wa kitengo cha Mauzo Mustapha Kapasi( kushoto) pamoja na Gaspa Mroso waakiongea na wateja wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembea wateja wao na kutoa elimu ya huduma zao ikiwemo Airtel Yatosha.
Afisa Mauzo wa Airtel bi Theresia Kimaro Akiongea na wateja juu ya huduma ya Airtel yatosha wakati Airtel walioko Magomeni na kutoa elimu juu ya huduma mbalimbali ikiwemo ya Airtle yatosha.
Meneja wa kitengo cha network, Emmanuel Luanda akisajili wateja kwenye huduma ya Airtel Yatosha wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembea wateja wake na kutoa elimu ya huduma zao ikiwemo Airtel Yatosha mwishoni mwa wiki hii.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso Akibandika moja ya kipeperushi cha Airtel yatosha wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembea wateja wake na kutoa elimu ya huduma zao ikiwemo Airtel Yatosha inayompa mteja, Simkadi moja, taifa moja na bei moja.

Wateja wa DStv wazidi kujinyakulia Mamilioni

$
0
0
Bwana George Hellar (wa pili kulia) akipongezwa na Meneja Uendeshaji wa DStv Tanzania,Baraka Shelukindo (kushoto) kwa kushinda malipo ya mwezi ya mwaka mzima kwenye shindano la DStv Rewards. Wiki hii wateja wa DStv watapata fursa ya kushinda kitita cha Tshs 10,000,000 katika droo itakayochezeshwa Alhamisi. DStv wamekua wakitoa Tshs 5,000,000 kwa wateja wao waliokuwa wakilipia akaunti zao za DStv kabla ya kumalizika muda wake.Wengine pichani ni Meneja Masoko wa DStv Tanzania,Furaha Samalu (kulia) na Meneja Uhusiano wa DStv Tanzania, Barbara Kambogi.

UMOJA WA MATAIFA WAKUMBUKA UTUMWA NA BIASHARA YA UTUMWA

$
0
0

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza Jumuiya ya Kimataifa kuendelea kupambana na utumwa unaoendelea hivi sasa kila pembe ya dunia.
Professa Ali Mazrui, Mwanazuoni maarufu akisaidiwa kuketi kabla ya kuzungumza katika siku hii ya maadhimisho ya kumbukumbu ya utumwa na biashara ya utumwa .
Professa Mazrui akizungumza ambapo pamoja na mambo mengine alielezea histotia ya utumwa na biashara ya utumwa pamoja na harakati mbalimbali zilizopelekea kukomeshwa kwa biashara hiyo. pamoja na kusisitiza haja na umuhimu wa kuendelea kuwaenzi waathirika wa ukatili huo, alitaka pia kuenzi yale mema ambayo baadhi yake ni matokeo ya historia hiyo ya Utumwa, Professa Mazrui alikuwa mzungumzaji mkuu katika maadhimisho haya ambayo hufanyika Machi 25 ya kila mwaka.
 BANGO  lilombeba ujumba wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya  kumbukumbu ya  utumwa na biashara ya utumwa, maadhimisho ambayo yalifikie kilele Marchi 25 hapa  Umoja wa Mataifa.

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA YAANZA KUWASILISHA TAARIFA YAKE JUU YA UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHI TANZANIA

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mh. Jaji Aloysius Mujulizi akifungua mkutano wa wadau wa sheria ya ardhi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Tume ya Kurekebisha Sheria Bw. Albert Msangi akiwasilisha taarifa ya Utafiti juu ya Mfumo wa Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi Tanzania.
Baadhi ya wadau wa sheria ya ardhi wakiwa katika mkutano.

MKUU WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI, CGP JOHN MINJA AKUTANA NA WAKUU MBALIMBALI WA JESHI HILO BARANI AFRIKA, NCHINI ZAMBIA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali, John Minja (waliokaa wa kwanza kulia) akiwa na wakuu wa jeshi hilo wa nchi mbalimbali barani Afrika (waliokaa) pamoja na maofisa wao (waliosimama) baada ya kufanya mkutano wa Taasisi za Urekebishaji Barani Afrika (ACSA). Wakuu hao wa taasisi hiyo walifanya mkutano wao katika Hoteli ya Sun iliyopo mjini Livingstone, nchini Zambia mwishoni mwa wiki, wakijadili masuala mbalimbali ya kuyaboresha majeshi yao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

KAGASHEKI: TEKELEZENI WAJIBU KWA KUZINGATIA KANUNI NA TARATIBU

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Khamis Kagasheki amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kutekeleza wajibu wa kutekeleza kazi kwa ubunifu na uadilifu huku wakizingatia Sheria, Kanuni na taratibu zinazosimamia utendaji kazi.

Balozi Kagasheki alitoa rai hiyo wakati akifungua rasmi mkutano wa 20 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika jijini Dar es Salam.

Mhe. Waziri aliwataka wajumbe wa wajumbe wa baraza hilo kutambua kuwa Baraza ni chombo muhimu kwa ajili ya kuongeza ufanisi na tija katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara.

“Tumieni vema nafasi mlizonazo kuhakikisha kuwa haki na wajibu wa Mwajiri na Mtumishi vinapewa kipaumbele katika utekelezaji wa majukumu yenu kwa kulinga maslahi ya pande zote mbili kwa manufaa ya Taifa zima.

“Moja ya changamoto mliyonayo kama Baraza hili ni kuhakikisha watumishi wanazingatia nidhamu na maadili katika utumishi wa umma. Ninafahamu mazingira ya kazi na hasa katika vituo vyetu si ya kuridhisha, lakini ni vyema tukahimiza watumishi kufuata kikamilifu Sheria, Kanuni na taratibu za utendaji wa kazi”, anasema Kagasheki.

Anasema wajumbe wakitekeleza wajibu wao kama Wajumbe wa Baraza, watarahisisha kazi ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara. Aidha, aliwataka katika utekelezaji wa majukumu yeao kuhakikisha wanaimarisha ushirikiano, utendaji kazi kama timu moja kwa uwazi na kuaminiana hususan katika maamuzi yanayohusu wengi.

Over 60 delegates from across Tanzania mainland and Zanzibar took part in a Copa Coca-Cola seminar held in Dar today

$
0
0
 Coca-Cola Brand Manager Tanzania Maurice Njowoka delivers his speech at the opening ceremony of the Copa Coca-Cola Directive Seminar held at the National Stadium in Dar es Salaam Tuesday, March 26, 2013.

Tanzania Football Federation (TFF) President Leodegar Tenga emphases a point as he addresses over 60 delegates from across Tanzania at the opening ceremony of the Copa Coca-Cola Directive Seminar held at the National Stadium in Dar es Salaam Tuesday, March 26, 2013.
A section of over 60 delegates from across Tanzania mainland and Zanzibar follow a speech by TFF President Leodegar Tenga at the opening ceremony of the Copa Coca-Cola Directive Seminar held at the National Stadium in Dar es Salaam Tuesday, March 26, 2013.

 Participants to a one-day Copa Coca-Cola directive seminar, including TFF President Leodegar Tenga, take a souvenir picture at the National Stadium in Dar es Salaam Tuesday, March 26, 2013.

26 wajifua Miss Tabata, kupigwa tafu na Miss Mzizima Pasaka

$
0
0
Washiriki wa Miss Tabata 2013 wakipozi kwa picha ya pamoja wakati wa mazoezi yao yanayoendelea kufanyika kwenye ukumbi wa Da'West Park, Tabata jijini Dar es Salaam.
JUMLA ya warembo 23 wamejitokeza kushiriki katika shindano la kumtafuta Miss Tabata 2013 ambalo litazinduliwa siku ya Pasaka kwenye ukumbi wa Da’ West Park Tabata.

Mratibu wa shindano hilo, Godfrey Kalinga amesema leo kuwa warembo hao watatambulishwa pamoja na wale wanaoshiriki Miss Mzizima siku ya sikukuu ya Pasaka Da'West Park.

Kalinga aliwataja warembo waliojitokeza kuwania taji la Miss Tabata 2013 na kuendelea na mazoezi Da West Park ni Martha Gewe (19), Zilpha Christopher (19), Hidaya David (22), Aneth Ndumbalo (19), Amina Ally (18), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Kitereja (19), Angela Fradius (19), Domina Soka (21), Rehema Kihinja (20), Glory Jigge (18) na Sophia Claud (21).

Aliwataja wengine ni Lilian Mpakani (19), Lilian Msanchu (19), Rita Frank (20), Pasilida Mandali (21), Rachel Mussa (19), Jasmin Damian (18), Angelina Mkinga (19), Mercy Mwakasungu (20), Tunu Hamis (19), Blath Chambia (23), Ray Issa (22), Shamim Abass (22) na Shan Abass (22).

Utambulisho wa warembo hao, utasindikizwa na burudani kabambe kutoka bendi ya Twanga Pepeta “Wazee wa Kisigino”. Kapinga alisema wapenzi wa tasnia ya urembo Jijini Dar es Salaam, watapata fursa ya kuwaona warembo kabla ya Miss Tabata kufanyika Mei mwaka huu.

Miss Tabata 2013 imedhaminiwa na Konyagi, CXC Africa, Fredito Entertainment na Saluti5 na kuandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.

Washindi watano kutoka Tabata watafuzu kushiriki Miss Ilala baadaye mwaka huu. Anayeshikilia taji la Miss Tabata ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.

WATEJA WANAOTUMIA HUDUMA YA M-PESA SASA KUTUMIA ATM ZA DTB KUTOLEA FEDHA

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati,(kushoto)akiwaelezea waandishi wa habari,jinsi ya kutoa fedha kwenye mashine za kutolea fedha za DTB kupitia huduma ya Vodacom M PESA ambapo sasa wateja wanaotumia huduma hiyo wanaweza kutoa pesa kupitia mashine hizo popote walipo nchini,huduma hiyo imezinduliwa leo jijini Dares Salaam pamoja nae ni Meneja mahusiano ya nje wa Vodacom Tanzania,Bw.Salum Mwalim.
Meneja mahusiano ya nje wa Vodacom Tanzania,Bw.Salum Mwalim,akitoa fedha kwa mara ya kwanza baada ya kuzinduliwa kwa huduma ya kutoa fedha kupia mashine za kutoa fedha za DTB kupitia huduma ya M PESA, ambapo sasa wateja wanaotumia huduma hiyo wanaweza kutoa pesa kupitia mashine hizo popote zilipo nchini anaeshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati.
Meneja mahusiano ya nje wa Vodacom Tanzania,Bw.Salum Mwalim,pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati.wakifurahia mara baada ya kutoa fedha kwa mara ya kwanza kupitia mashine za kutoa fedha za DTB kwa huduma ya M PESA, ambapo sasa wateja wanaotumia huduma hiyo wanaweza kutoa pesa kupitia mashine hizo popote zilipo nchini.

Ukuaji wa teknolojia ya huduma maarufu ya kutuma, kupokea fedha pamoja na kufanya malipo ya huduma mbalimbali kwa njia ya simu za mkononi ya kampuni ya Vodacom ya M-pesa inazidi kupanuka na hivyo kuongeza kiwango cha matumizi ya huduma hiyo kuzidi kuboresha maisha na kuyafanya kuwa rahisi zaidi.

Katika kufikia mafanikio hayo Benki ya Diamond Trust (DTB) leo imetangaza ubia wa kibiashara na kampuni ya Vodacom Tanzania ubia ambao unawawezesha wateja wa M-pesa kuwa na uwezo wa kutoa fedha kutoka katika akuanti za M-pesa kwa kutumia mashine za kutolea fedha (ATM) za benki ya Diamond Trust.

Wakitangaza na kuzindua huduma hiyo jijini Dar es salaam Mkuu wa Kitengo za Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati, amesema hayo ni mafanikio mengine ya kibishara kwa benki hiyo ya DTB katika kupanua wigo wa huduma na namna benki hiyo inavyoweza kuunganisha teknolojia ili kuleta urahisi kwa watanzania.

"DTB inayo Furaha kubwa kuwa sehemu ya mapinduzi ya kiteknolojia hapa nchini. Hii ni huduma ya kwanza na ya aina yake ambayo hakuna shaka kwamba inaashiria uwezo wa DTB katika kuleta ufumbuzi wa namna bora ya kutumia teknolojia kurahisisha maisha."Amesema Bahati

"Tukishirikiana na Vodacom tunawawezesha wateja wa M-pesa walio karibu na benki zetu na hususan mtandao wa ATM kuwa na uhakika wa kutoa fedha kutoka akaunti zao za M-pesa saa ishirini na nne katika siku zote saba za wiki."

Bahati amesema jambo hilo litasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki sanjari na kuboresha hali ya maisha na uchumi kwa watanzania wote mijini na vijijini.

Hata hivyo hii ni frusa ya kipekee kwa wateja wa benki ya DTB ambao wamejiandikisha kwa ajili ya huduma ya M-Pesa hawana haja tena ya kutembelea matawi ya benki hiyo ili kuweza kuweka amana zao au kuhamisha fedha kwa biashara, marafiki na familia zao. Pia uzinduzi wa huduma hiyo utawezesha kujenga urahisi wa kuruhusu wasiotumia huduma ya benki kupata huduma za kifedha karibu nao.

Azma ya DTB ni kuzidi kuongeza kasi na maboresho ya utoaji wa huduma kwa wateja wake na washirika wake wengine kwa kuhakikisha inaendelea kupanua wigo wa huduma zake ikiwemo kuongeza ATMs, matawi na huduma nyinginezo kwa lengo la kusogeza karibu huduma za kibenki nchi nzima.

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa M- Biashara wa Vodacom Jacques Voogt, amesema, "Hii ni hatua nyingine ambayo tunaifikia leo. Kampuni ya Vodacom inaendelea kupanua mtandao wake wa huduma ya M-Pesa." Voogtz ameongeza kuwa ubia huo ni mwendelezo wa azma ya kampuni ya Vodacom kutumia fursa za teknolojia ya M-pesa kuzidi kuleta amsiha ya watu mikononi mwao kutumia simu za kiganjani.

"Wateja wa Vodacom M-pesa wanayo sababu nyingine ya kujivunia kuwa sehemu ya mtandao mpana wa huduma hii salama, rahisi na yenye kuaminika zaidi nchini wakiunganishwa na makampuni na hata tasisi zaidi ya 200 kufanya malipo ya huduma na manunuzi kwa urahisi na wepesi zaidi kupitia simu za viganjani."Aliongeza Voogtz

Taswirazzz za maeneo mbali mbali ya Kariakoo jijini Dar leo

$
0
0
 Hizi ni Taswira mbali mbali za eneo la Kariakoo kama zilivyonaswa na Kamera ya Mdau wa Blogu ya Jamii leo. 

WAJUMBE WA TUME YA KATIBA WAENDELEA NA UCHAMBUZI WA MAONI YA WANANCHI KUHUSU KATIBA MPYA

$
0
0
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim (kulia) akizungumza wakati wa kikao cha uchambuzi wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya kilichofanyika leo (jumanne Machi 26, 2013) katika Ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam. Wengine ni Wajumbe wa Tume, Prof. Mwesiga Baregu (katikati) na Suleiman Ali.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphery Polepole (aliyesimama) akizungumza wakati wa kikao cha uchambuzi wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya kilichofanyika leo (jumanne Machi 26, 2013) katika Ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam. Wengine ni Wajumbe wa Tume, Simai Mohammed na Dkt. Adrian Sengondo Mvungi.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani (kulia) akizungumza wakati wa kikao cha uchambuzi wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya kilichofanyika leo (jumanne Machi 26, 2013) katika Ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Tume, Dkt. Salim Ahmed Salim.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ULINZI NA USALAMA YAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM KUPOKEA TAARIFA YA HALI YA ULINZI NA USALAMA NCHINI KWA KIPINDI CHA KUANZIA JANUARI – MACHI, 2013

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama Mama Anna Abdallah (mbele katikati) akifuatilia taarifa ya Hali ya Ulinzi na Usalama iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam. Wengine ni wajumbe wa Kamati hiyo na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (wa tatu kushoto) akitoa taarifa ya Hali ya Ulinzi na Usalama kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam. Katika kikao hicho, Dk. Nchimbi alisema hali ya ulinzi na usalama nchini kimsingi imendelea kuwa shwari isipokuwa kwa matukio machahe yaliyogusa hisia za watu kutokana na kutokuwa ya kawaida katika jamii yetu, na kuwa Serikali inayafanyia uchunguzi wa kina matukio hayo.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.

taarifa kutoka Shirikisho la soka Tanzania (TFF) leo

Wazee wa Feva wa Kule Ukweni kwa Ankal wakilisakata Bolingo.

Serena Hotel has recognized Earth hour alongside thousands of people worldwide on the 23rd March

$
0
0
Dar es Salaam Serena Hotel has recognized Earth hour alongside thousands of people worldwide on the 23rd March 2013 by making a significant reduction on energy consumption, the most obvious was switching off most of the lights and using solar power.

This is an initiative that started in Sidney in 2007 with approximately 2.2 million people participating, this event has now got over 1 billion people from different countries participating so as to make a positive impact on climate change, one of the current initiatives is "I will if you will" which encourages people of different calibers to make a positive contribution to the climate and go beyond the 60 minutes.
Mr Seraphin Lusala, Director of Sales and Marketing at the Dar es Salaam Serena Hotel (left) explain to Dr Kanabar, a well know patron who supports positive change the initiative on Climate.
Mr. Seraphin Lusala Director of Sales and Marketing for the Dar es Salaam Serena Hotel (right) explaining the positive impacts of Earth hour and the need to embrace the initiative to some of the staff from the Dar es Salaam Serena Hotel.
Various reused items displayed at the lobby.

WARSHA KUHUSU HALI YA NISHATI JADIDIFU NCHINI TANZANIA 26 MACHi, 2013

$
0
0
Katika nchi ya Tanzania zimekuwepo jitihada nyingi kuongeza upatikanaji na utumiaji wa Nishati jadidifu.Kwa muda mrefu sasa kumekuwa hakuna utaratibu maalum unaoonyesha ukusanywaji wa taarifa juu ya hali halisi ya maendeleo ya sekta ya Nishati jadidifu kama ilivyo katika sekta nyingine mathalani Afya.

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Taasisi ya wadau wa nishati Jadidifu nchini Tanzania(TAREA) wameandaa warsha ambayo wadau mbali mbali wa Nishati watabadilishana mawazo juu ya hali halisi ya Teknolojia ya Nishati jadidifu nchini Tanzania hadi kufikia mwezi Disemba 2002

Mwishoni mwa warsha hii,washiriki watatoa maoni yao juu ya mfumo na mbinu za kuendeleza ukusanyaji taarifa kuhusu maendeleo ya Teknolojia ya Nishati jadidifu.

Katika warsha hii COSTECH na TAREA watabadilishana makubaliano ya ushirikiano kati yao juu ya mambo yote yanayohusu utafiti,uhawilishaji na ukuzaji wa teknolojia ya nishati jadidifu.
MKURUGENZI MKUU WA COSTECH DR HASSAN MSHINDA AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA MAKUBALIANO YA COSTECH NA TAREA KATIKA UTAFITI,UHAWILISHAJI NA UKUZAJI WA TEKNOLOJIA YA NISHATI JADIDIFU.
WASHIRIKI KATIKA WARSHA HIYO.

Uvivu wa kusoma ni kikwazo cha mawasiliano katika jamii yetu

$
0
0

Mkuu wa Kiengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma akizungumza wakati wa Warsha ya siku tatu kwa wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya Kijamii (BLOGS) hapa nchini kuhusu Wizara hiyo inavyoweza kupeleka habari kwa urahisi kwa wananchi wa kawaida iliyofanyia Kibaha mkoani Pwan,hivi karibuni.

Na Othman Michuzi.

Kutokuwa na utamaduni wa kupenda kusoma vitabu, na taarifa mbali mbali zinazohusiana na maendeleo ya nchi imetajwa kuwa ni kikwazo kikubwa katika mawasiliano kati ya wananchi na taasisi mbali mbali za serikali, jambo ambalo ni hatari katika Taifa linaloendelea.

Kwa mujibu wa utafiti usio rasmi uliofanywa na baadhi ya waandishi wa habri za kijamii nchini, ni asilimia tisa tu ya watanzania, ndio wenye utaratibu wa kupenda kusoma, asilimia iliyobakia, hupata habari kwa njia ya kusikia, ama kwenye vyombo vya habari au kwenye maongezi ya kawaida.

Hii ni moja ya taarifa zilizowasilishwa kwenye warsha ya siku tatu iliyoshirikisha baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii na magazeti tando, kwa kushirikiana na Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Fedha, katika kujadili jinsi ya kuboresha mawasiliano kati ya wananchi na taasisi za kimaendeleo ili kurahisisha ufikaji wa taarifa za kimaendeleo kwa wananchi.

Kutokana na tabia hii ya kutopenda kusoma, wananchi wengi wamekuwa wakikosa kujua mambo mengi ya kimaendeleo yanayofanyika nchini kwa sababu taarifa hizi mara nyingi huwekwa katika maandishi.

"Limekuwa ni tatizo kubwa sana hapa nchini, watu hawajui kitu na hawataki kujua kwa sababu hawapendi kusoma", alisema wakati akichangia mada mmoja wa washiriki wa Warsha hiyo,Bw. Josephat Lukaza.

Katika Warsha hiyo ya siku ambayo pia ilihudhuriwa na maafisa habari kutoka sekta mbali mbali za kimaendeleo, wadau walikuwa wakitafuta njia mbadala itakayosababisha wananchi kujua mambo mbalimbali ya kimaendeleo ya nchi ili kujua hali halisi ya uchumi wa nchi inavyoendelea.

Naye Mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha Wizara ya fedha, Bi Ingiahedi Mduma, alisema ipo haja ya kuwa wabuhifu katika kuhakikisha kwamba kwa njia yoyote ile, tunahakikisha kwamba wananchi wa kawaida, hasa wa vijijini, wanapata taarifa husika kwa wakati muafaka.

Amesema taarifa za kimaendeleo za nchi ni haki ya kila mwananchi kujua na ndio maana sasa wameamua kukaa chini na kuumiza vichwa katika kutaka kujua jinsi ya kuwafikia asilimia kubwa ya wananchi, mijini na vijijini. 

Warsha hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro Park Hotel, maeneo ya Misugusugu, wilayani Kibaha, mkoa wa Pwani ambapo pia mikakati mbali mbali ya kimaendeleo ilijadiliwa.

Baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya kijamii (Blogs) wakimsikiliza Mkuu wa Kiengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma (hayupo pichani) wakati wa warsha hiyo ya siku tatu
Baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya kijamii (Blogs) waliohudhulia Semina hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Mhe Lowassa aongoza mazishi ya Nyiti, Arusha

$
0
0
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa ameongoza maelfu ya Wakazi wa mji wa Arusha na mikoa ya jirani katika mazishi ya mfanyabiashara na Kada maarufu wa CCM Mkoani Arusha,Marehemu Henry Nyiti,nyumbani kwake Tengeru Arusha .

Nyiti alifariki ghafla wiki iliyopita akiwa katika mgodi wake wa madini,Mahenge Mkoani Morogoro.

Wengine walioudhuria katika mazishi hayo ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe,Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh. Lazaro Nyalandu,Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dr. Reginald Mengi,Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mh. Magesa Mulongo,Mwenyekiti wa Chadema,Mh. Freeman Mbowe na Ridhiwani Kikwete.
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akiongoza viongozi wenzake kwenda kwenda kuweka udongo kaburini.nyuma yake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe.

Mwenyekiti wa makampuni ya IPP,Dr. Reginald Mengi naye akiweka udongo kaburini.
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akiweka shada la muawa kaburini.

JK AFUNGA MAFUNZO YA JKT KWA VIONGOZI LEO

$
0
0
Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi mbunge wa viti maalum Ester Bulaya leo katika kambi ya RUVU JKT.Rais Kikwete amefunga rasmi mafunzi hayo leo yaliyofanyika kwa wiki tatu.
Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya pamoja na wenzao wakila kiapo wakati wa kuhitimu mafunzo ya muda mfupi yaliyofanyika katika kambi ya jeshi la Kujenga Taifa Ruvu JKT huko kibaha Mkoani Pwani leo.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi kutoka kwa kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu wakati wakimaliza mafunzo ya JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga. 
Zote za Tanga na Hussein Semdoe.
wakwanza katika mstari wa kushoto ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe anayefuata ni Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani, wakiwa kwenye Paredi ya kumaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT Kikosi cha 835 Mgambo JKT kambi iliyopo katika Kata ya Mgambo ilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
wakwanza kushoto ni Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, ZItto Kabwe, wakihitimu mafunzo ya JKT katika kambi ya 835 Mgambo JKT iliyopo Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani, akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Biharamulo, Dk Athanas Mbassa, akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga. 
Mbunge wa Kiwani Pemba, Abdallah Haji Ali, , akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, akiapa mbele ya kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu, hayupo pichani, wakati wakimaliza mafunzo ya JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge Viti maalum Raya Khamis , akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni.
Baadhi ya Wabunge walikuwa wakichukua mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waheshimiwa wabunge waliohitimu mafunzo maalumu ya JKT leo

Mbunge wa Mtera Mh. Livingstone Lusinde 
"Kibajaji"  (wa tatu toka kulia) akipiga kwata leo huko Ruvu

KUTOKA MAKTABA: MAMA MARIA NYERERE AKIWA JKT ENZI HIZO

$
0
0
Mama Maria Nyerere akiwa katika mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa enzi hizo. Kuanzishwa tena kwa mafunzo hayo kwa mujibu wa sheria kumeleta msisimko wa aina yake nchini.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images