Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

TRA yawapa somo wachina kuhusu sheria za ukusanyaji kodi nchini

$
0
0
Mkurugenzi wa JITENG Consultant Company Bw. Andrew Huwang akiongea jumuiya ya wafanyabiashara kutoka China waishio Tanzania kuhusu ushiriki wao katika masuala ya ukusanyaji kodi na kuendelea kuongeza ushirikiano kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa Semina iliyoandaliwa na Jumuiya ya wachina waishio Tanzania na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyolenga kuwaeleimisha kuhusu ukusanyaji na sheria mbalimbali za Kodi Nchini leo Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Bw.Yeremiah Mbaghi.
Afisa Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Rose Mahendeka akiongea na jumuiya ya wafanyabiashara kutoka China waishio Tanzania kuhusu faida za Mfumo mpya wa Uondoshaji Mizigo (TANCIS) unaosaidia kuongeza ufanisi katika uondoshaji wa Mizigo ya wateja na kuondoa malamiko ya ucheleweshwaji wa huduma hiyo pia kuondoa tatizo la upotevu na mizigo pindi inapoingizwa nchini, wakati wa Semina iliyoandaliwa na Jumuiya ya wachina waishio Tanzania na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyolenga kuwaeleimisha kuhusu ukusanyaji na sheria mbalimbali za Kodi Nchini leo Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Hamisi Lupenja akiwaeleza wafanyabiashara kutoka China waishio Tanzania kuhusu umuhimu wa kushiriki katika matumizi ya Mashine za Risiti za Kielektroniki (EFD) katika manunuzi na uuzaji wa Bidhaa mbalimbali ili kuiwezesha serikali kupata mapato stahiki bila udanganyifu wakati wa Semina iliyoandaliwa na Jumuiya ya wachina waishio Tanzania na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyolenga kuwaeleimisha kuhusu ukusanyaji na sheria mbalimbali za Kodi Nchini leo Jijini Dar es Salaam.
4-Wanajumuiya wafanyabiashara kutoka China waishio Tanzania wakimsikiliza Afisa Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Hamisi Lupenja wakati wa Semina iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Picha na HASSAN SILAYO-MAELEZO

NEC:UCHAGUZI MKUU HAUTASOGEZWA MBELE

$
0
0
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Manunuzi na Logistic,Gregory Kaijage na kushoto ni Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya  Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama),Sisti Chriati.
Baadhi ya wandishi wa Habari waliohudhuria katika mkutano wa habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  jijini Dar es Salaam leo.  (Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)


 Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema uchaguzi mkuu utafanyika kama ulivyopangwa na haiwezi kufanya uchaguzi huo usogezwe mbele kutokana na suala hilo kuwa la kikatiba.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa wanasiasa wamekuwa na kauli ambazo zinawafanya wananchi wapate hofu wakati suala hilo kuhairisha uchaguzi halipo katika tume.

Amesema kuwa wanasiasa wametakiwa kuangalia maneno ambayo wanayatoa kwani hayana msingi  kwani wanatakiwa watoe sera zao za vyama kwa wananchi na sio kuisemea tume mambo ambayo hayana ukweli wowote. Amesema zoezi la kuandikisha kwa Mkoa wa Njombe ambalo  linaisha kesho na kuhamia katika mikoa ya Iringa,Lindi,Ruvuma pamoja na Mtwara ambalo litaanza Aprili 24 mwaka huu.


Lubuva amesema wanatarajia kupokea vifaa vya  kuandikisha kwa kuchukua alama za vidole (BVR)1600 ambazo zitafanya kazi katika mikoa hiyo na kuhamia Mikoa ya Dodoma,Mbeya,Katavi pamoja na Rukwa  kuongezeka BVR tena 1600 na BVR 1,152 zitafanya kazi katika mikoa Singida,Tabora,Kigoma pamoja na Kagera na uandikishaji utaanza Mei 2 mwaka huu.

Aidha amesema zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura litamalizika Julai mwaka huu hivyo wananchi wajiandae katika kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Oktoba. Jaji Lubuva amesema Rais Jakaya Kikwete anataka amalize ili apumzike hivyo hakuna mpango wowete wa kuongeza muda wa uongozi kwake,

WARSHA YA WAFANYABIASHARA WA TANZANIA NA CHINA YAFANYIKA JIJINI DAR LEO.

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko Sekta Binafsi Nchini (TPSF),Godfrey Simbeye akizungumza na waandishi wa habari katika warsha iliyowakutanisha wafanyabiashara wa China na Watanzania iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa  Baraza la Biashara la China na Afrika (CABC) Tawi la Tanzania,Xian Ding akizungumza na waandishi wa habari  katika warsha iliyowakutanisha wafanyabiashara wa China na Watanzania iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau katika katika warsha iliyowakutanisha wafanyabiashara wa China na Watanzania iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko Sekta Binafsi Nchini (TPSF),Godfrey Simbeye amesema kukutana na watu wa China ni fursa  nzuri ya watanzania katika kushirikiana katika sekta ya uwekezaji nchini.

Simbeye amesema hayo katika warsha iliyowakutanisha wafanyabiashara wa China na Watanzania iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.

Simbeye amesema wachina hawaji Tanzania kutembea bali wanakuja kwa ajili ya kukuza viwanda vyao vilivyopo nchini ,hivyo ni fursa kwa wawekezaji watanzania kuweza kukutana na wachina hao ili kushirikiana nao.
  
Naye Mwenyekiti wa  Baraza la Biashara la China na Afrika (CABC) Tawi la Tanzania,Xian Ding amewataka wachina pamoja na watanzania kuzidisha ushirikiano ili kupata maendeleo katika biashara.

Rais wa Zanzibar aongoza waombolezaji katika mazishi ya Dkt. Omar Makame Shauri

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia akijumuika na Viongozi na Waislamu mbali mbali katika kumswalia aliyekuwa katibu Mkuu Wizara ya Afya na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar Marehemu Dkt.Omar Makame Shauri katika Msikiti wa Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Unguja kabla ya mazishi yake leo.
Baadhi ya wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislamu wakilibeba jeneza la aliyekuwa katibu Mkuu Wizara ya Afya na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar Marehemu Dkt.Omar Makame Shauri aliyezikwa leo kijijini kwao Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,Makamo wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sherif na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (katikati) wakiwa na Viongozi wengine na Wananchi katika mazishi ya aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar Marehemu Dkt.Omar Makame Shauri aliyezikwa leo kijijini kwao Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein(katikati)akitia udongo kufukia kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar Marehemu Dkt.Omar Makame Shauri aliyezikwa leo kijijini kwao Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Unguja.(Picha na Ikulu.)

MSD YABORESHA HUDUMA ZA UTOAJI TAARIFA KWA WATEJA WAKE.

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda Bohari ya dawa (MSD), Edward Terry,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa habari MAELEZO jijjini Dar es Salaam leo kuhusu utendaji na mipango ya Bohari ya Dawa (MSD) na Ofisa Uhusiano Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),Etty Kusiluka.

Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
 BOHARI ya dawa (MSD) imeboresha huduma  kwa wateja wake kwa kutoa taarifa zinazomhusu mteja kwa kuziweka wazi katika tovuti yao.
 Akizungumza na wandishi wa habari  katika ukumbi wa  Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wateja na Shughuli za Bohari ya Dawa (MSD), Edward Terry,  amesema kuwa taarifa hizo ni za mali inayopatikana gharani, taarifa za kiasi cha fedha za wateja kilichopo katika kila akaunti,fomu za marejesho pamoja na bei za bidhaa na bei zake.

Pia Terry amesema kuwa wateja wenye mahitaji ya dawa au vifaa wanatakiwa kuandika barua kuelezea mahitaji yao pamoja na maelekezo mhimu ya kifaa husika na kutatuliwa na kitengo cha manunuzi ya bohari hiyo.

Waziri Wasira na ujumbe wake ziarani nchini Poland

$
0
0
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Stephen M. Wasira, yuko nchini Poland kwa ziara ya kikazi aliyokaribishwa na Waziri Wa Kilimo wa nchi hiyo Marek Sawicki.

 Pamoja na mambo mengine, ziara hii inahusu Ujenzi wa kiwanda cha Matrekta ya Ursus na Ujenzi wa Maghala ya kuhifadhi chakula chini ya NFRA. 

Katika ziara hiyo Mhe. Wasira ameambatana na Mkuu wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa (NFRA) Charles Walwa, pamoja na Maofisa wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika na SUMA JKT.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Stephen M. Wasira (wa pili kulia) na ujumbe wake wakifanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo wa Poland Mhe. Marek Sawicki.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Stephen M. Wasira (kulia) akifanya mazungumzo na menejimenti ya kampuni inayotengeneza matrekta ya Ursus katika ofisi za Ursus mjini Warsaw, Poland.
Wajumbe wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika wakiwa na mwakilishi wa kampuni ya Ursus Tanzania, Mama Grazyna Tairo.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Stephen M. Wasira pamoja wa ujumbe wake walivyowasili Warsaw, Poland tarehe 16 April 2015.

KIWANDA CHA TUMBAKU MOROGORO CHAFANYA SHERERE KUFUNGA MSIMU NA KUFUNGUA MSIMU MPYA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Tumbaku ya Tanzania Tobacco Procesing Limited (TTPL) na Tanzania Leaf Tobacco Company (TLTC) David Crowhorst Akitoa hotuba yake wakati wa sherehe za kumaliza msimu uliopita na kukaribisha msimu mwingine pamoja na kutoa zawadi kwa wafanyakazi waliotumikia kampuni hizo kwa muda mrefu pamoja na wafanyakazi bora zilizofanyika Kiwandani hapo.Katika Hotuba yake Mkurugenzi Huyo alisema Makampuni hayoyamesaidia Mkoa wa Morogoro kuanza kuinuka kiuchumi kutokana na kutoa ajira za msimu takribani 3000 kila mwaka na kusaidia kupunguza matatizo ya uhalifu yaliyokuwa yakifanywa na vijana wasio kuwa na shughuli  za kujiingizia kipato. 
Mkurugenzi mkuu wa Makampuni ya Tumbaku ya Tanzania Tobacco Procesing Limited (TTPL) na Tanzania Leaf Tobacco Company (TLTC) David Crowhorst Akikabidhi zawadi kwa wafanyakazi waliofanya kazi kwa muda mrefu Ambao wamefanya kazi kwa zaidi ya Miaka 15 Mfululizo.
Mkurugenzi mkuu wa Makampuni ya Tumbaku ya Tanzania Tobacco Procesing Limited (TTPL) na Tanzania Leaf Tobacco Company (TLTC) David Crowhorst Akiwapakulia Chakula waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati wa tafrija hiyo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

UCHAGUZI MKUU HAUTASOGEZWA MBELE - NEC

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema uchaguzi mkuu utafanyika kama ulivyopangwa na haiwezi kufanya uchaguzi huo usogezwe mbele kutokana na suala hilo kuwa la kikatiba.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa wanasiasa wamekuwa na kauli ambazo zinawafanya wananchi wapate hofu wakati suala hilo kuhairisha uchaguzi halipo katika tume.

Amesema kuwa wanasiasa wametakiwa kuangalia maneno ambayo wanayatoa kwani hayana msingi kwani wanatakiwa watoe sera zao za vyama kwa wananchi na sio kuisemea tume mambo ambayo hayana ukweli wowote.

Amesema zoezi la kuandikisha kwa Mkoa wa Njombe ambalo linaisha kesho na kuhamia katika mikoa ya Iringa,Lindi,Ruvuma pamoja na Mtwara ambalo litaanza Aprili 24 mwaka huu.

Lubuva amesema wanatarajia kupokea vifaa vya kuandikisha kwa kuchukua alama za vidole (BVR)1600 ambazo zitafanya kazi katika mikoa hiyo na kuhamia Mikoa ya Dodoma,Mbeya,Katavi pamoja na Rukwa kuongezeka BVR tena 1600 na BVR 1,152 zitafanya kazi katika mikoa Singida,Tabora,Kigoma pamoja na Kagera na uandikishaji utaanza Mei 2 mwaka huu.

Aidha amesema zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura litamalizika Julai mwaka huu hivyo wananchi wajiandae katika kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Oktoba.

Jaji Lubuva amesema Rais Jakaya Kikwete anataka amalize ili apumzike hivyo hakuna mpango wowete wa kuongeza muda wa uongozi kwake.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Manunuzi na Logistic,Gregory Kaijage na kushoto ni Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama),Sisti Chriati.
Baadhi ya wandishi wa Habari waliohudhuria katika mkutano wa habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)

EACJ Judges’ Training on Emerging Trends in Arbitration Sets Off

$
0
0
East African Court of Justice Arusha 17 April 2015:  A two day training for Judges of the EACJ on emerging trends in arbitration set off yesterday  in Arusha. The training is organized by the International Senior Lawyers Project (ISLP) in collaboration with the East African Court of Justice.

In his opening remarks, EACJ Judge President Hon. Justice Dr. Emmanuel Ugirashebuja commended the support of the ISLP in strengthening the Court’s capacity in handling arbitration issues through training of the Judges.

He added that the program has come at a time when the Court is in need of more skills and knowledge in arbitration and that this will benefit East Africans willing to bring matters before the EACJ for Arbitration rather than taking them outside the region.

His Lordship further said that the public is not fully aware of the Court’s jurisdiction on arbitration and this was the right time for the litigants to approach the Court for arbitration. He noted the Court had so far received one (1) arbitration matter but expects more to be filed with the Court in the future as people realize the opportunities available.

The facilitator of the training, Professor Markham Ball, an Arbitrator and Mediator, told the Judges that the purpose of the training was to transform the Court’s ability in handling arbitration matters; where the Court may want to be in future and that arbitration is popular in the business community as well as with investors.

He also emphasized that arbitration is efficient particularly in addressing business matters and the Court plays a big role in enforcing arbitration awards. He said the training will look into modernizing the Court’s existing rules of Arbitration in order to optimize the Court’s efficiency as an arbitration Institution.

The EACJ, ISLP and Professor Ball signed a Memorandum of Understanding on 5th April 2015 with the goal to; assist the Court in its efforts to build the capacity of the Court to further promote the knowledge and practice of arbitration in East Africa as well as become a prominent arbitration center; assess the strengths and weaknesses of the Court and provide guidance on possible modifications of EACJ Rules of Arbitration 2012

In attendance were all Judges of the EAC Appellate and First Instance Divisions accompanied by the Ag. Registrar Ms. Geraldine Umugwaneza.
Judges in training session with Prof. Markham Ball.
Group picture for the Judges with Prof. Markham Ball and Ag. Registrar.

Ujumbe Maalum wa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenda kwa Sultan Qaboos wa Oman

$
0
0
Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania akimkabidhi Mhe. Yousuf bin Alawi bin Abdulla, Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Ujumbe Maalum kutoka kwa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenda kwa Mhe. Sultani Qaboos bin Said Al Said, Mtawala wa Oman.
Makabidhiano yakiendelea huku Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Ali Ahmed saleh akishuhudia.
Waziri Membe akiwa kwenye mazungumzo na Mhe. Alawi bin Abdulla, Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman.

Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa amekabidhi ujumbe maalum kutoka kwa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenda kwa Mhe. Sultani Qaboos bin Said Al Said, Mtawala wa Oman.  

Ujumbe huo maalum ulikabidhiwa kwa Mhe. Yousuf bin Alawi bin Abdulla, Waziri wa Mambo ya Nje na mwenyeji wa ziara ya Waziri Membe nchini Oman, kwenye ofisi za Wizara hiyo jijini Muscat, Oman Alhamisi Aprili 16, 2015.  

Makabidhiano hayo ya kihistoria nchini hapa, yalishuhudiwa na Mhe. Dkt. Mwinyihaji Makame, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Zanzibar , Mhe. Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania Oman, na viongozi wengine wa nchi zote mbili na waandishi wa habari.  

Baada ya makabidhiano, viongozi hao wawili na ujumbe wao walitumia fursa hiyo kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Tanzania na Oman.  

Viongozi hao waliahidi kukuza uhusiano na utamaduni wa nchi hizi mbili ambao unafanana kwa sababu za kihistoria. Mhe. Membe alimuelezea mwenyeji wake nia ya Serikali kujenga Ofisi za Ubalozi  kwenye kiwanja chake hapa Mascut kama sehemu ya utekelezaji wa mpango wa kuwa na majengo ya Tanzania kwenye nchi mbalimbali duniani.  

Aidha mradi mkubwa wa bandari ya Bagamoyo pia ulizungumzwa na viongozi hao ambapo Serikali ya Oman ni mojawapo ya mdau wa mradi huo. Wahusika wengine wa mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni Serikali ya China na Tanzania.  

Mhe. Yousuf bin Alawi bin Abdulla, Waziri wa Mambo ya Nje wa Omani alimuhakikishia mgeni wake ushirikiano wa Serikali yake kwenye hatua zote hizi muhimu za kuendeleza na kukuza uhusiano wa muda mrefu wa nchi hizi mbili.

  Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
17 Aprili 2015

MSD YABORESHA HUDUMA ZA UTOAJI TAARIFA KWA WATEJA WAKE

$
0
0
Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

BOHARI ya dawa (MSD) imeboresha huduma kwa wateja wake kwa kutoa taarifa zinazomhusu mteja kwa kuziweka wazi katika tovuti yao.

Amesema hayo Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wateja na Shughuli za Bohari ya Dawa (MSD), Edward Terry, akizungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.

Terry amesema kuwa taarifa hizo ni za mali inayopatikanagharani, taarifa za kiasi cha fedha za wateja kilichopo katika kila akaunti,fomu za marejesho pamoja na bei za bidhaa na bei zake.

Pia Terry amesema kuwa wateja wenye mahitaji ya dawa au vifaa wanatakiwa kuandika barua kuelezea mahitaji yao pamoja na maelekezo mhimu ya kifaa husika na kutatuliwa na kitengo cha manunuzi ya bohari hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda Bohari ya dawa (MSD), Edward Terry,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa habari MAELEZO jijjini Dar es Salaam leo kuhusu utendaji na mipango ya Bohari ya Dawa (MSD) na Ofisa Uhusiano Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),Etty Kusiluka.

UCHAGUZI MKUU KUBAKI PALEPALE-NEC

DIRA YA DUNIA YA IDHAA YA KISWAHILI BBC LEO

ngoma azipendazo ankal special request from Amb. Cisco Mtiro

$
0
0
Patrick Balisidya & Afro 70 Weekend

Mkutano wa Injili Washington DC...WAZO LA JIONI (April 17, 2015)

$
0
0
Mch Wilbert Nfubhusa
Katika WAZO LA JIONI hii ya leo (Aprili 17, 2015), Mch Wilbert Nfubhusa ameendelea kuzungumzia kuhusu WAZO KUU la Mkutano huu ambalo ni KUFANANA NA YESU
Pia, alielezea ushuhuda aliosimuliwa na wakimbizi toka Burundi
Japo unafurahisha, lakini unafunza sana
KARIBU

Coastal Union yajifua kuikabili Polisi Morogoro

$
0
0
Kocha Mkuu wa Coastal Union,Jamhuri Kihwelu "Julio"akisisitiza jambo kwa wachezaji wa timu hiyo mara baada ya kumalizika mazoezi yao juzi kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani kwa ajili ya kujiandaa na mechi yao ya Ligi kuu dhidi ya Polisi Morogoro itakayochezwa Jumatano wiki ijayo kwenye uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro,Picha kwa Hisani ya Coastal Union.

Innalillahi wa Inna Ilaihi Rajioun: SUPREME Mufti wa Uganda afariki dunia

$
0
0
Innalillahi wa Inna Ilaihi Rajioun:SUPREME Mufti wa Uganda  ambaye pia ni Murshid wa Twariqatus-Shaadhuliy nchini Uganda, Sidi. Sheikh Zubeir Kayongo amefariki dunia katika hospitali ya Agha Khan Jijini , Dar es salaam jana alikokuwa amelazwa muda mfupi akiwa  njiani kuelekeya Kilwa Pande kuhudhuria HAUL na Ziyarah  ya kutimiza  miaka 100 ya Sidi.Sheikh Muhammad Al- Maaruf As-Shadhuly(QAS).

Marehemu aliwahi kuhudhuria Ziyarah ya Mawlid  Jijini  Unguja Mfunguo 6. na Twariqatul Shaadhuliya nchini humo ilimfanyiya hadhra maalum kwa heshima yake katika  Msikiti wa Mwembetanga Jijini Unguja.Ilikuwa ni desturi ya .Al-Marhum SUPREME Mufti wa Uganda  kila mwaka  kuhudhuria Hawl ya Sheikhe Muhammad Al Maarufu aliyeleta Twariqatu Shadhuliyah Afrika ya Masharika mwanzoni mwa miaka ya 1900 toka huko Akka Palestina inayokaliwa kwa Mabavu alipochukua Twariqah hiyo toka kwa Sheikhe lake Sidi Sheikh.

Ali Nurdin Al-Yashurutwi(QAS).Twariqah ya Shadhuli imeenea maeneo mengi duniani ikiwemo Uganda ambapo ilifika miaka ya mwanzoni mwa 1900 chini ya Sidi.Sheikh.Hussein Ibn Hussein wa Kilwa Pande aliyepokea Twariqah toka kwa Sidi Sheikh Muhammad Al-Maarufu wa Ngazija.

Nchi zingine zilizoenea Twariqah hii ni  Misr, Morocco(Maghreb), Algeria,Tunisia, Sudan, Sri-Lanka, India, Pakistani, Jerusalem(Palestina),Libya, Uingereza, America, Canada, Australia, Afrika Mashariki na mwanzilishi wa Twariqah hii akitokea huko Morocco na aliyetawafu huko nchini Misri akielekea safari ya Hajj  kwa umaarufu akiitwa Sidi.


Sheikh Abal Hassan As-Shadhuly, Jina la Shadhuly linatokana na mji wa huko Afriqiyah(Tunis) ambako ndipo harakati za Sheikhe zilipoanzia kueneza Daawah ya Kitwariqah yenye kushikamana na Quraan na Sunnah kwa mujibu wa mafundisho ya Ahlul Sunnah walJamaa..


Watu wengine maarufu waliokuwa wakifuata Twariqah hii ni Imam alHafidh  Jalaludin As-Suyutwi aliyekuwa mufasir maaruf wa Quraan na Hadith (Tafsir Jalalayn),Sidi Sheikh Umar Mukhtar As-Sanusi(mwanaharakati wa Ki-Libya maarufu kama The Lion of The Desert), Shahidi.Sidi.Sheikh Hassan Al-Bannah(Rahimahullah) mwanzilishi wa harakati Ikhwaan Al- Muslimun  ya nchini  Misri, aliyekuwa Mfalme wa Libya Mfalme  Idriss   aliyepinduliwa na Kanali Muammar  Gadafi   Wengine katika karne ya sasa ni wanachuoni wakubwa wa Hadith huko Maghreb wajulikanao kama Saadah al-Ghumari ,, Mwanachuoni wa Hadith wa Alexandria Al-Kahtan, pia aliekuwa Mufti wa nchi ya Misr, Sidi.Sheikh Dr.Ali Gumua na Maulamaa wengine wengi wa Al-Azhari Shariyf na Qarawiyin University  huko Maghreb ni Murshid wa Twariqah hii ya Shadhuly..Tunamuomba Mola Amjaalie Mayiti wetu Sheikhe letu Sidi.Sheikh Zuberi Kayongo msamaha wa mapungufu yake na Amjaalie Mayiti wetu pepo iliyo juu kabisa na tunamuomba Mola amtakase mayiti wetu kama inavyotakaswa nguo nyeupe kutokana na madhambi yake na amjaalie kaburi lake liwe ni katika viwanja vya pepo , Tunamuomba Mola wetu ampe majazo mema kutokamana na amali zinazoendelea na zile zitakazofanywa kwa niaba yake iwe na mimea au viumbe katika wanadamu,Malaika na Majini Yaa Raab.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE NDUGU SOPHIA MJEMA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA SIKU 5 YA KUZUIA MIMBA ZA UTOTONI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI WILAYANI TEMEKE

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu Sophia Mjema akilakiwa na Dkt. Martha Kisanga, Meneja wa Kanda ya Pwani wa Shirika la Engender Health mara baada ya kuwasili kwenye eneo la Shule ya Sekondari Kibasila kwa ajili ya kufunga rasmi mafunzo ya siku 5 yaliyohusu mradi wa kuzuia mimba za utotoni katika Shule za Sekondari katika Wilaya ya Temeke tarehe 17.4.2015. Waliosimama katikati ni Ndugu Donald Siliva, Afisa-Elimu Sekondari, Wilaya ya Temeke na Dkt. Sarah Maongezi, Mkurugenzi wa Afya kutoka Taasisi ya WAMA.
Meneja wa Uragibishi na Mawasiliano kutoka Taasisi ya Wana wake na Maendeleo, Ndugu Philomena Marijani akitoa maelezo ya awali kuhusiana semina ya siku 5 ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari katika Wilaya ya Temeke iliyofanyika huko Kibasila Sekondari tarehe 17.4.2015.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu Sophia Mjema akitoa hotuba ya kufunga rasmi mafunzo ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari za Wilaya ya Temeke yaliyofanyika Kibasila Sekondari.

KILIMO KWANZA

BAGAMOYO JOGGERS SUPPORT ALBINOS

$
0
0
Minister for Education & Vocational Training, Dr. Shukuru J. Kawambwa (centre in white/blue track suit) at the special Bagamoyo jogging session which condemned atrocities against the Albinos. On the Minister's left is Mussa S. Kamota an Albino staying in Bagamooyo. Others are club officers and Counsellors.

Families are encouraged to participate in the Bagamoyo Jogging Sports Club which has, as at today more than 150 members. Children below the age of twelve must accompany their parents. For Source and more...
CLICK HERE
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images