Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110109 articles
Browse latest View live

WORKSHOP: WEBSITE / BLOG DESIGN & MAINTENANCE USING JOOMLA!

$
0
0
 

DUDUMIZI TECHNOLOGIES LTD, Leading Website design and Development Company in Tanzania is organizing 6 days Workshop to equip participants with the skills, knowledge and techniques of designing, developing and maintaining good websites / blog by using Open source Content Management System called Joomla!
Joomla is an award-winning content management system (CMS), which enables people to build Websites and powerful online applications. Joomla the most popular Websites software in the world. Almost 80% of Websites in Tanzania are designed using Joomla. For Full Details CLICK HERE

wilaya ya ilala yaadhimisha siku ya mazingira na elimu

PSPF YAZINDUA HUDUMA YA WANACHAMA WAKE KUWASILISHA MICHANGO KUPITIA MAXMALIPO

$
0
0
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Vvijana na Michezo, Juma Nkamia, (wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (wapili kushoto), na Afisa Mtendaji Mkuu wa Maxcom Africa, Juma Rajabu, wakizindua huduma mpya ya wanachama wa Mfuko huo, kuwasilisha michango yao kupitia Maxmalipo. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye ofisi za makao makuu wa PSPF, Golden Jubilee, katikati ya jiji leo Alhamisi Aprili 16, 2015. Kulia ni Mkurugenzi Mtendajiwa Glob al Publisher, Erick Shigongo, ambaye ndiye aliyebuni na kushawishi PSPF kutumia huduma hiyo kurahisishia wanachama wake.
Kutoka kushoto kwenda kulia, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Zamaradi Kawawa, Afisa Mtendaji Mkuu wa Maxcom Africa, Juma Rajabu, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Myingu, Naibu Waziri Juma Nkamia, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publisher, Erick Shigongo, wakishikana mikono baada ya kuzinduz huduma hiyo

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Maxcom Africa, na wenzao wa PSPF, katika uzinduzi

Baadhi ya maafisa wa PSPF

Wafanyakazi wa PSPF. Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

BRIGEDIA JENERALI SARA THOMAS RWAMBALI ATEULIWA KUWA MWAKILISHI MAALUM WA AU SUDAN YA KUSINI

$
0
0
Na Mwandishi Maalum, New York 
 Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Dr. Nkosanzana Dlamini Zuma, amemteua, Brigedia Jenerali Sara Thomas Rwambali kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ),kuwa Mwakilishi Maalum na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Afrika Sudan ya Kusini . 
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na AU na nakala yake kutumwa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, inaeleza kwamba makazi ya Brigedia Jenerali Sara Thomas Rwambali yatakuwa Juba. 
 Pamoja na uteuzi wa Brigedia Jenerali Sara Rwambali, Dr. Nkosazana Dlamini Zuma pia amewateua Madame Josephine- Charlotte Mayuma Kala kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, anayekuwa Mwakilishi Maalum na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Afrika huko Cote d’Ivoire na makazi yake yakiwa Abidjan, 
Wengine walioteuliwa ni Madame Nyiramatama kutoka Rwanda, anayekuwa Mkuu wa Ofisi ya AU huko Chad , makazi yake yakiwa Ndjamena na Dr. Arvin Boolel kutoka Mauritius anayekuwa Mwakilishi Maalum na Mkuu wa Ofisi ya AU katika Maziwa Makuu Burundi na makazi yake yakiwa Bujumbura. 
Taarifa kwa vyombo vya Habari kutoka AU inaeleza zaidi kwamba uteuzi huo ni sehemu ya AU ya kuhakikisha uwepo wake katika kila eneo na vile vile kuunga mkono juhudi zinazolenga katika kukuza Amani na Usalama Barani Afrika “Ninatoa pongezi zake za dhati kwa wateuliwa ambao ni viongozi wa ngazi za juu na wenye sifa za kutukuka katika utumishi wa umma wakiwa na uzoefu mkubwa katika eneo la amani na usalama. Si jambo la ajabu kwamba wateule watatu kati ya wanne ni wanawake” anasema Dr. Zuma 
Na kuongeza, “katika mwaka huu wa 2015, ambao Umoja wa Afrika umejikita katika uwezeshwaji wa wanawake. 
"Ninayo matumaini makubwa kwamba AU na Afrika kwa ujumla itanufaika na utaalamu na uzoefu mkubwa na uwezo wa kiuongozi kutoka kwa wateuliwa hawa”. 
Mwenyekiti wa Kamishna ya AU pia ametoa wito kwa wadau wote kuwapatia ushirikiano wateuliwa hao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ukamilifu kwa maslahi ya Bara la Afrika, huku akitoa shukrani kwa wawakilishi ambao wanamaliza muda wao.
Katika picha hii ya Maktaba,  Amiri Jeshi Mkuu , Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku  nishani ya kumbukumbu ya  miaka 50 ya Jeshi la  Wananchi wa Tanzani ( JWTZ) Brigedia Jenerali Sara Thomas Rwambali ambaye hivi karibuni,  Mwenyekiti  wa  Kamisheni ya  Umoja wa Afrika,  Dr. Nkosazana Dlamini Zuma amemteua kuwa Mwakilishi Maalum na Mkuu wa Ofisi ya  Umoja wa Afrika  nchi  Sudani ya Kusini.

SafariTV Show - Zanzibar & Arusha

How the Cyber Crime Law will affect E-commerce in Tanzania.

$
0
0

The recently introduced Cybercrime Act bill of 2015 by the parliament of Tanzania promises to provide security to all citizens from any sort of cyber-attack that may come their way as they are surfing on the internet. For a developing country like Tanzania this is a big step in trying to make sure justice is served and that all those that are using the internet as a medium to take advantage of people’s rights, privacy and that of the state are dealt with accordingly.

A report by the Tanzania Communication Regulatory Authority (TCRA) shows that internet services in Tanzania commenced from the year 1995. There has been a steady growth of internet users from 3.5million people in 2008 to over about 11 million out of the 32 million Tanzanians with access to mobile phones by the end of 2014.

This growth shows that our lives currently depend on the wind of info- technology.  We use it for healthcare, transport and most especially for communication. It has made life much easier than it was before, in every sense. There are now several websites that can help one get any product or service simply by the click of a button.

E-commerce in Tanzania is growing fast due to the increasing number of internet users and service providers in the country. The country is at a stage where it is vital that its people feel secure when buying products or booking tickets through the internet via websites like Kaymu or Travel start.

KaymuTanzania’s Country Manager Mr. Erfaan Mojgani says that “E-commerce in Tanzania is very exciting. The country has about 49 million people and the number of internet users is still growing very fast.” He added that “Tanzanians shouldn’t be afraid of using online services for fear of conmen as Kaymu is a genuine website for sellers to meet their buyers and this law will definitely help eradicate this fright. “

Mr. Richard Maguluko, one of the Tanzanians with online shopping experience, tells us his thoughts on cybercrime, “In the recent years we Tanzanians have been hesitant in using E-commerce sites because there are a lot of conmen out there trying to deceive the citizens and they get away with it many times.”


The bill is a sign that Tanzania as a developing country is heading in the right direction, like other European and western countries already has; this is a positive step that the country is taking in catching up with the rest of the world. If the new bill passes, using the internet will very much be more enjoyable and comfortable and additionally problems associated with internet scams can be dealt with accordingly and all those who are responsible for misconduct, will be punished as required.

News alert: Serikali kuwarudisha nchini Watanzania waliopo Yemen

Tanzania Ijayo: Nini Maana Ya Uchumi Wa Gesi Asilia - Prof Dr Sospeter M. Muhongo


DIRA YA DUNIA YA IDHAA YA KISWAHILI BBC LEO

VIJANA WA CCM IRINGA WAMPA NGUVU KATIBU WA MKOA HASSAN MTENGA KUKOMBOA JIMBO, LA IRINGA MJINI

$
0
0
Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga katika kikao na baadhi ya vijana hao












KIU ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Iringa kukomboa jimbo la Iringa Mjini katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu inazidi kuongezeka, baada ya umoja wake wa vijana (UVCCM Manispaa ya Iringa) kuahidi kuongeza nguvu ili kuufanikisha mkakati huo.



CCM ililipoteza jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 kwa Mchungaji Msigwa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anayekaribia kumaliza muda wake.



Katika kikao kilichozikutanisha sekretarieti za umoja huo kutoka katika kata zote 18 za manispaa ya Iringa, Mwenyekiti wa UVCCM wa manispaa hiyo, Kaunda Mwaipyana alisema; “katika kukisaidia chama kushinda uchaguzi huo, kauli mbiu yetu ni chama kwanza mtu baadaye.”



“Tutapita katika matawi na kata zetu zote, tutafanya vikao, mikutano ya hadhara na kuwakumbusha vijana wajibu wa kukipigania chama chao ili mkakati wa kulikomboa jimbo ufanikiwe,” alisema.

INTRODUCING KNOWLEDGE ZA KITAA BY JCB FT. NIKKI WA II, MO PLUS, JOES

Jarida la Wiki la Wizara ya Nishati na Madini, Toleo Namba 63

BREAKING NYUZZZZZ....: AJALI NYINGINE YATOKEA JIJINI MBEYA LEO, ZAIDI YA WATU 20 WADAIWA KUPOTEZA MAISHA

$
0
0
Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde toka Wilayani Rungwe, Jijini Mbeya inaeleza kuwa Basi dogo aina ya Toyota Hiace imetumbukia kwenye Mto Kiwira mapema leo na inadaiwa kuwa zaidi ya watu 20 waliokuwepo kwenye basi hilo wamepoteza Maisha.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, amesema kwamba ajali hii imetokea wakati Mabasi yafanyayo safari zake kati ya Mbeya na Kyela (maarufu kama Coaster) kugoma kutoa huduma ya kusafirisha abiria katika maeneo hayo, hivyo baadhi ya hiace za mjini kuamua kubeba abiria, hali iliyopelekea hiace hizo kubeba abiria wengi zaidi ya uwezo wake.

Inaelezwa kuwa gari hiyo ilipoteza muelekea na kuingia mtoni, baada ya dereva wake kushindwa maarifa kutokana na mwendo aliokuwa nao.

Mungu aziweke pema roho za marehemu hao,Amin.
Pichani ni Baadhi ya wakazi wa maeneo ya jirani na ilipotokea ajali hiyo wakiiangalia basi hiyo ikiwa kando kando ya mto Kiwira.
Wananchi wa Mji wa Kiwira wakienda kuangalia ajali hiyo.
Sehemu ya wananchi wa Mji wa Kiwira wakiangalia Baadhi ya Miili ya Watu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.

Benki ya Exim yatangaza ongezeko la asilimia 35 la faida ya kabla ya kodi

$
0
0
 Kaimu Afisa Mkuu wa fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Issa Hamisi (wa kwanza kutoka kulia) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari  wakati akitoa  taarifa ya mapato ya mwaka 2014 ya benki ya hiyo jana jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa kitengo cha rasilimali watu wa benki hiyo , Frederick Kanga (wa pili kulia) na Mkaguzi mkuu wa ndani wa hesabu za benki hiyo, George Binde (kushoto) .
 Meneja Mwandamizi utafiti na Uchambuzi wa Biashara wa Benki ya Exim Tanzania,  Joseph Mrawa (wa pili kulia) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari  wakati akitoa  taarifa ya mapato ya mwaka 2014 ya benki hiyo  jana jijini Dar es Salaam. Wengine ni Kaimu Afisa Mkuu wa fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Issa Hamisi (wa kwanza kutoka kulia) Mkuu wa kitengo cha rasilimali watu wa benki hiyo , Frederick Kanga (wa pili kulia) na Mkaguzi mkuu wa ndani wa hesabu za benki hiyo, George Binde (kushoto) 
 Mkuu wa kitengo cha rasilimali watu wa benki ya Exim Tanzania, Frederick Kanga (katikati ) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari  wakati akitoa  taarifa ya mapato ya mwaka 2014 ya benki hiyo  jana jijini Dar es Salaam. Wengine ni Kaimu Afisa Mkuu wa fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Issa Hamisi (wa kwanza kutoka kulia) naMkaguzi mkuu wa ndani wa hesabu za benki hiyo,George Binde (kushoto) 

BENKI ya Exim Tanzania imepata ongezeko la faida (kabla ya  kodi) kwa mwaka 2014 la asilimia 35 kufikia shilingi bilioni 24.1 kutoka shilingi bilioni 17.9 kwa mwaka 2013. Benki imeendelea kuwa na mali za shilingi tilioni 1 na kuweza kukuza pato la wenyehisa kwa asilimia 23 kufikia shilingi bilioni 190 ikilinganishwa na shilingi bilioni 154 iliyorekodiwa mwaka Jana.

 "Tunafuraha kubwa kuitangaza kwenu mafanikio makubwa ya kifedha ya mwaka 2014 Desemba,” alisema Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha Bw. Issa Hamisi, akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam Jana.

Alisema kuwa benki hiyo imefanikiwa kupata faida (baada kodi) kiasi cha sh bilioni 57.3 kutoka sh billion 44.2 iliyopatikana mwaka 2013 ikiwa ni ongezeko la asilimia 30, ikilenga zaidi katika ongezeko la amana zenye gharama nafuu.

Kwa mujibu wa Bw. Hamisi, pia masuala ya ada, kamisheni na mapato ya fedha za kigeni yaliongezeka kwa asilimia 25 hadi kufikia shilingi bilioni 38 kutoka shilingi bilioni 30.4  kwa mwaka uliopita. Ukuaji huu kwa kiasi kikubwa umechangiwa na kasi ya ukuaji katika shughuli ya za biashara za fedha za kigeni, bidhaa za biashara ya fedha na ada kutoka kwenye  utoaji wa huduma  mbadala.

Mali za benki zimekuwa wakati ‘Gross NPA ratio’ ikishuka kutoka asilimia 9.60 kwa mwaka 2013 kufikia asilimia 6.83 mwishoni mwa mwaka uliyolipotiwa.

Benki hiyo pia iliweka mkakati wa miaka mitatu mwanzo kabisa wa mwaka huo 2014 ambao ulilenga kujiongezea soko lake la amana sambamba na kufikia nafasi ya uongozi katika malipo.

Bw. Hamisi aliongeza kuwa benki imeweka mkakati wa kuzidi kujiimarisha na kuimarisha watu wake, shughuli zake pamoja na teknolojia. Alisema benki imeweza kufanyakazi na makampuni bora ya kimataifa katika utoaji ushauri kwenye masuala yajulikanayo kama Enterprise-wide Risk Management, na pia kuweza kurahisisha zaidi ufanyaji wa shughuli zake kwa mwaka huo.

Aidha Bw Hamisi aliongeza kuwa benki imendelea jitihada za kupanua wigo wa huduma zake kwa kuongeza idadi ya matawi mawili kwenye nchi tatu ambazo inatoa huduma zake vikiwemo visiwa vya Comoro na nchini Djibouti.

“Mafanikio haya ni mwangaza tosha katika utendaji wetu wa sasa na siku zijazo….kwa sasa Exim imejenga msingi imara kitu ambacho kinatuhakikishia mafanikio zaidi kwa mwaka huu 2015,’’ aliongeza Bw Hamisi.

Benki imeendelea kujidhatiti katika urejeshaji wa kile ikipatacho toka kwa jamii. Katika mwaka huo benki ilijikita zaidi katika kusaidia taasisi za elimu, hospitali na taasisi nyinginezo.

MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI(MUWSA) YAKAMATA WEZI WA MAJI

$
0
0
Watumishi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA,wakiwa katika nyumba moja ambayo inadaiwa mmiliki wake alikuwa akiiba maji baada ya kujiunganishia kinyemera licha ya kukatiwa huduma hiyo kwa muda mrefu.
Wafanyakazi hao wakiongozwa na afisa uhusiano wa mamlaka hiyo ,Frolah Nguma na mkuu wa kanda ya Rau ,Selemani Zabron na fundi Aminiel Swai baada ya kufuatilia katika eneo hilo walibaini wapi wizi wa maji unafanyika.
Hivi ndivyo ilivyooonekana katika mauongio ya mteja wa mamlaka hiyo ambaye mtuhumiwa wa wizi wa maji alifanya usanii wa kujiungia maji bila ya kulipia huku mzigo wa kulipia ankala ya maji ikibaki kwa jirani yake aliyeunganisha bomba kwenye line yake.
Fundi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA,Aminiel Swai akiondoa bomba liliunganishwa kwa wizi .
Mkuu wa kanda ya Rau wa mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi Selemani Zabron akifukia eneo ambalo hujuma ya kujiunganishia maji ilikuwa imefanyika.
Mmiliki wa nyumba hii ndiye line ya kupeleka maji kwake imekutwa ikiwa imefanyiwa hujuma na kulazimika kulipa bili ya matumizi ya maji kwa nyumba mbili.
Watumishi wa MUWSA wakitazama kama maji yanatoka katika nyumba hiyo mara baada ya kuondoa bomba ambalo lilikuwa likitumika kupeleka maji katika nyumba nyingine kwa njia ya wizi.Hata hivyo katika operersheni hiyo Mtuhumiwa pamoja na mkewe walilazimika kuikimbia nyumba yao na kutelekeza watoto wao wawili wakiume wenye umri wa kati ya miaka miwili na minne.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI(MUWSA) YAKAMATA WEZI WA MAJI

$
0
0
Watumishi wa MUWSA wakitizama kama maji yanatoka katika nyumba hiyo mara baada ya kuondoa bomba ambalo lilikuwa likitumika kupeleka maji katika nyumba nyingine kwa njia ya wizi.Hata hivyo katika operersheni hiyo Mtuhumiwa pamoja na mkewe walilazimika kuikimbia nyumba yao na kutelekeza watoto wao wawili wakiume wenye umri wa kati ya miaka miwili na minne.
Mmiliki wa nyumba hii ndiye line ya kupeleka maji kwake imekutwa ikiwa imefanyiwa hujuma na kulazimika kulipa bili ya matumizi ya maji kwa nyumba mbili.
Fundi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA,Aminiel Swai akiondoa bomba liliunganishwa kwa wizi .

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

WAZIRI CHIZA AKUTANA NA KAMPUNI YA UJENZI MRADI WA KUZALISHA UMEME KINYEREZI III

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Eng. Christopher Chiza (Mb), (katikati) akiwa na ujumbe wa kampuni ya Shangai Electic Power ya nchini China inayokusudia kujenga Mradi wa Uzalishaji umeme wa Kinyerezi III, walipokutana ofisini kwake kuzungumza masuala ya uwekezaji katika mradi huo, tarehe 17 Aprili 2015, (kushoto) ni Makamu wa Rais wa kampuni hiyo Bw. Guo Baohong.

APPLICATION FOR TRAINING AND EMPLOYMENT OPPORTUNITIES

$
0
0
The Director General of the Tanzania Meteorological Agency wishes to re-announce availability of training opportunities for Meteorological Technicians within the Agency. This announcement was earlier made on 12 December 2014. For those who have already applied are not supposed to re-apply.

Qualifications:

  1.  Form six leavers with two principal passes in mathematics and physics. Passes in chemistry and geography will be an added advantage.

  2.  Should be not more than 22 years of age by 12 December 2014.

  3.  Women are highly encouraged to apply.


Mode of application:

Applicants are required to pay a non-refundable processing fee of TShs. 10,000 through NMB Bank, A/C Name-Tanzania Meteorological Agency, A/C No. 20101000013.


Duly filled application forms with detailed curriculum vitae, copies of certified academic certificates, three referees, a recent photograph, daytime telephone numbers and bank pay in slip should be mailed to:


Director General,

Tanzania Meteorological Agency,

P.O. Box 3056,

Fax: + 255-22-2460735

Dar es Salaam.

Email:met@meteo.go.tz


Deadline : 22/April/2015


Please note that application forms may be downloaded from the TMA website wwww.meteo.go.tzor obtained from Tanzania Meteorological Agency Headquarters, 3rd  floor,  Ubungo Plaza, Morogoro Road, Dar es Salaam


It should be noted that applications sent without application forms will not be considered and only short listed candidated will be contacted.



Successfully candidates will be required to undergo one year training course at the Agency’s National Meteorological Training Centre, Kigoma. Employment will only be granted after successful completion of the Course.

MABARAZA YA WAFANYAKAZI TAASISI ZA ELIMU YA JUU YATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha (Sera) Mhe. Mwigulu Nchemba (katikati) akiwa ameambatana na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt. Joseph Kihanda (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara Prof. Isaya Jairo kabla ya kuzindua Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) lililojumuisha wawakilishi kutoka matawi 6 ya taasisi hiyo katika mikoa ya Kigoma, Singida, Mwanza , Mtwara, Dar es salaam na Mbeya.
Naibu Waziri wa Fedha (Sera) Mhe. Mwigulu Nchemba wakati akizindua Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) leo mjini Bagamoyo.
Wajumbe wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakiimba wimbo wa mshikamano daima kabla ya kuanza kwa mkutano wao leo mjini Bagamoyo.

SOMA ZAIDI HAPA

NEWS ALERT: WACHIMBAJI WA DHAHABU ZAIDI YA 20 WADAIWA KUFARIKI DUNIA KWA KUFUKIWA KIFUSI HUKO KAHAMA

$
0
0
Wachimbaji wadogo wadogo wapatao 20 wa dhahabu katika machimbo ya madogo yaliyopo kwenye kijiji cha Kalole kata ya Runguya tarafa ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, wamedaiwa kufariki dunia baada ya kufunikwa na kifusi kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha maeneo hayo.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha amesema kuwa usiku wa kuamkia leo kuna wachimbaji ambao walivamia machimbo hayo ambayo yaliachwa kuchimbwa muda mrefu na ndipo wakaanza shughuli ya uchimbaji kutokana na machimbo hayo kuonekana kutokuwa uimara na mvua iliyokuwa ikinyesha ndipo mashimo hayo yakaporomoka na kuwafukia na kusababisha vifo vyao.
 Sehemu ya shimo hilo la dhahabu katika kijiji cha Kalole wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

TAARIFA KAMILI ITAWAJIA BAADAE KIDOGO
Viewing all 110109 articles
Browse latest View live




Latest Images