Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Kipindi kipya cha TV cha Plants


Xenophobia in South Africa from the horse's mouth

Kipindi cha "UBISHI" na Constantine Magavilla

Killer Bi: Remembering Bi Kidude, the Taboo-Busting Queen of Taarab

$
0
0
Andy Jones’s music documentary As Old as My Tongue is subtitled “The Myth and Life of Bi Kidude,” an apt addendum for a film about a larger-than-life performer who came to global attention only when she was well into her 80s. 

Or so it was thought; when the reigning queen of Taarab died two years ago this week, she was thought to be several years past 100 but no one knew her age for sure – not even Bi Kidude, which only added to her allure when she was discovered by the growing international audience for African music, including Jones, at the time an up-and-coming British filmmaker.
For More CLICK HERE

DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI LEO

Mkutano wa kundi la Afrika wafanyika mjini Washington DC

$
0
0
Shirika la fedha la kimataifa (IMF) hujishughulisha na kutoa ushauri wa kisera kwa nchi wanachama na kutoa mikopo na misaada ya kifedha. Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum aliyaeleza hayo mjini hapa. 

Akishiriki kikao cha kundi la Africa(African Group one Constituency). Kundi hili hukutana kila kunapokuwa na mikutano ya Shirika la Fedha la Kimataifa na Benki ya Dunia kwa lengo la kuwezesha nchi za Afrika kuwa na sauti moja na kujua hatua ambazo Nchi za Afrika zimefikia kuhusiana na Taasisi zake za kifedha.

  Mhe. Mkuya alichangia mada mbalimbali zilizohusu kundi hilo akilenga zaidi maendeleo na muelekeo mzuri wa mafanikio ya kifedha katika nchi ya Tanzania. 

 Waziri wa Fedha  wa Tanzania Mhe. Saada Salum Mkuya ni Gavana katika mkutano huu akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile ambaye ni  Gavana msaidizi kwa upande wa Benki ya Dunia (WB), aidha  Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu ni Gavana msaidizi kwa upande wa Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF).

 Katika Mkutano huu Magavana hawa ndio wenye maamuzi ya juu na nguvu kubwa ya kuweza kuyashawishi mashirika  ya kifedha kuhusu nini kifanyike.  Mkutano huu uliofanyika leo, umeangalia uhalisia na vigezo vinavyotolewa na Shirika la Fedha la kimataifa katika kuimarisha taasisi za kifedha katika nchi wanachama Afrika.  

Katika mkutano huu, mambo muhimu yaliyojadiliwani pamoja na maendeleo katika kundi hilo na mabadiliko ya maboresho katika Benki ya Dunia. Wakijadiliana katika mkutano huo wajumbe hao wameshauri Shirika la fedha la kimataifa pamoja na taratibu zake, liangalie namna ya kulegeza masharti ya mikopo ili nchi wanachama ziweze kufanya mabadiliko ya kifedha kwa urahisi.

 Mikutano hiyo bado inaendelea hapa mjini Washington DC. na nchi wanachama wanaendelea kufika kwa wingi.
 Ujumbe kutoka Tanzania ukifuatilia kwa karibu mkutano huu. (African Group one Constituency
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya  akishiriki katika mkutano huu wa kundi la Afrika. (African Group one Constituency)
 Ujumbe kutoka Tanzania ukifuatilia kwa karibu mkutano huu. (African Group one Constituency)

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

TANZIA: CHE MUNDUGWAO AFARIKI DUNIA LEO

$
0
0
Mwanamuziki Mkongwe wa Nyimbo za Asili hapa nchini, Chigwele Che Mundugwao (pichani) amefariki Dunia mapema leo asubuhi kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es salaam.

Kabla ya kufikwa na mauti, Che Mundugwao aliugua na kulazwa katika hospitali ya Muhimbili kwa muda mrefu. 

Che Mundugwao alikuwa anashikiliwa katika gereza la Segerea kwa kukosa dhamana ya kesi yake,  ya kukutwa na pasi za kusafiria 12 za watu tofauti tofauti bila kuwa na maelezo yake.

Taarifa zaidi zitawajia baadae kidogo.

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDORI EFATHA WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO VODACOM TANZANIA

$
0
0
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Efatha iliyopo Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wakimsikiliza Ofisa Rasilimali Watu wa Vodacom Tanzania, Ndihagati Biduga (kulia) akiwafafanulia jambo wakati walipofanya ziara ya kimafunzo makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Mlimani City jijini Dare s Salaam hivi karibuni.
Ndihagati Biduga, Ofisa Rasilimali Watu wa Vodacom Tanzania (kulia) akiwaelezea jambo kuhusiana na mnara wa mawasiliano baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Efatha iliyopo Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wakati walipofanya ziara ya kimafunzo makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Mlimani City jijini Dare s Salaam hivi karibuni.
Ofisa Rasilimali Watu wa Vodacom Tanzania Ndihagati Biduga (kulia )akiwa ameambatana na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Efatha iliyopo Bagamoyo Mkoa wa Pwani, walipofanya ziara ya kimafunzo makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Mlimani City jijini Dare s Salaam hivi karibuni.

DRFA YAIPA MBINU YANGA KUINYOA ETOILE DU SAHEL

$
0
0
Kuelekea mchezo wa michuano ya kombe la shirikisho barani afrika kati ya Yanga dhidi ya Etoile Du Sahel ya Tunisia utakaopigwa jumamosi hii April 18 katika uwanja wa taifa,Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimeitabiria makubwa klabu hiyo ya Jangwani kuvuka katika kizingiti hicho kigumu kwa mchezo wa nyumbani na ugenini dhidi ya wababe hao wa Tunisia.

Mwenyekiti wa chama hicho Almasi Kasongo,amesema ili yanga ifanye vizuri katika mechi hiyo na kuwapa raha mashabiki wake na watanzania kwa ujumla,ni lazima icheze kwa uangalifu mkubwa na kukwepa kuendana na style ya kupoozesha mpira wanayoitumia wapinzani katika mechi za ugenini.

kasongo amelishauri benchi la ufundi la Yanga chini ya makocha Hans Pluijm na msaidizi wake Charles Mkwasa,kutumia mbinu ya kushambulia kwa muda wote ili kuwaduwaza wapinzani ambao wakati mwingine hutumia mbinu ya kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

Ametoa wito pia kwa mashabiki wa soka mkoa wa Dar es salaam na maeneo ya jirani, kujitokeza kwa wingi siku ya jumamosi kuishangilia Yanga ambao wanaliwakilisha taifa katika mashindano hayo ya vilabu barani afrika.

Hata hivyo DRFA inaamini kuwa Yanga ambayo ni moja ya timu zake zilizopo katika mkoa wa Dar es salaam haina sababu ya kutofanya vizuri katika mchezo huo, kutokana na kuwa na kikosi kizuri kilichovisambaratisha katika michuano hiyo vilabu vya BDF ya Botswana pamoja na Platinum ya Zimbabwe.

Imetolewa na 
Omary Katanga,Mkuu wa Habari 
Chama Cha Soka Mkoa wa Dar es salaam,DRFA.

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LEO

IGP NA MASHEIKH WAUNGANA KUKEMEA UHALIFU NCHINI

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akitoa hotuba yake katika Mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa dini ya Kiislam katika kuimarisha usalama nchini yakiwa na kauli mbiu isemayo “Amani na usalama ndio maisha yetu”.

Na Frank Geofray- Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu pamoja na viongozi wa dini ya Kiislamu nchini wameungana kwa pamoja kukemea vitendo vya uhalifu hapa chini pamoja na kuzitaka familia kutoa malezi bora kwa watoto wao ili kuondokana na wimbi la watu wanaojiingiza katika vitendo hivyo.

Rai hiyo ilitolewa leo jijini Dar es salaam na IGP Ernest Mangu pamoja na Viongozi mbalimbali wa dini ya kiislamu katika muendelezo wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa dini hiyo katika kuimarisha usalama nchini yakiwa na kauli mbiu isemayo “Amani na usalama ndio maisha yetu”.Mafunzo ambayo yaliratibiwa na Taasisi ya Mwinyi Baraka na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini ya kiislamu hapa nchini.

IGP Mangu alisema Viongozi wa dini wanadhamana kubwa katika kuhakikisha kuwa vitendo vya uhalifu vinadhibitiwa nchini kwa kuwaelimisha waumini wao na jamii kwa ujumla juu ya madhara ya uhalifu pamoja na kuwapa mafundisho yatakayojenga na kuimarisha ulinzi na usalama nchini.

Alisema wahalifu wa sasa wana mbinu nyingi hivyo kitu kikubwa kitakachoweza kusaidia katika mapambano hayo ni mshikamano wa dhati kutoka kwa viongozi hao katika kuwafichua ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Naye Mwakilishi wa Sheikh Mkuu wa Tanzania katika kikao hicho ambaye ni Mjumbe wa Baraza kuu la ulamaa BAKWATA, Sheikh Abubakar Zuber alisema kuna haja ya kuziba nyufa za uvunjifu wa amani ambazo zimeanza kujitokeza hapa nchini.

Alisema ni muhimu kuziba nyufa hizo kwa kuanzia kwenye misikiti, familia zao na hatimaye katika jamii zinazowazunguka ili kuhakikisha kuwa nchi inaendelea kubaki salama kwakuwa amani tuliyo nayo ni neema ambayo tunapaswa kuilinda kwa nguvu kubwa.

“Vilevile hatuna budi kuimarisha malezi katika familia zetu mana tunaposhindwa kuwalea watoto wetu vizuri ndio chimbuko la kushamiri kwa vitendo vya uhalifu wa aina mbalimbali hivyo tujielekeze katika kutoa mafunzo bora katika familia”Alisema Sheikh Zuber.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu Sheikh Khamis Mataka alisema uhalifu unaweza kujitokeza sehemu yeyote na hata ndani ya msikiti hivyo ni jukumu la viongozi wa misikiti kuwafichua wahalifu walio ndani ya misikiti.

Akizungumzia mafunzo hayo Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwinyibaraka Sheikh Issa Othman alisema wataendelea kutoa mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo viongozi wa dini waweze kuwaelimisha waumini wao juu ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu ili kuimarisha ulinzi na usalama.

MKURUGENZI MTENDAJI TRL ASIMAMISHWA KAZI KWA TUHUMA ZA MALIPO KINYUME CHA MKATABA

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Reli nchini(TRL),Mhandisi Kapallo Kisamfu amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa malipo ya Sh. Bilioni 230 ya mabehewa ya Mizigo yenye kasoro pamoja na kufanya malipo ya mabehewa yote kabla ya kukamilika.

Akitangaza maamuzi hayo ya kusimimishwa kwa Mkurugenzi huyo leo jijini Dar es Salaam baada ya ripoti ya kamati iliyoundwa na Waziri wa Uchukuzi (ambaye sasa ni Waziri wa Afrika Mashariki), Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta amesema ameshtushwa na malipo hayo kwani yamekiuka manunuzi ya umma kwani mkataba wake ulikuwa TRL ilipe nusu ya asilimia 50 lakini matokeo yake mabehewa yamelipwa yote.

Amesema mabehewa 120 yaliyofika nchini yakiwa yana kasoro aliyazuia baada ya kubaini hivyo lakini TRL ilikuwa imeshalipa fedha yote katika mazingira hayo yanaonyesha mkataba una dalili ya hujuma.

Waliosimamishwa wengine ni Mhandisi Mkuu wa Mitambo TRL,Ngosomwile Ngosomiles,Mhasibu Mkuu,Mbaraka Mchopa ,Mkaguzi Mkuu wa Ndani Jasper Kisiraga pamoja na Meneja Mkuu Ferdinand Soka.

Kamati ya uchunguzi kwa watendaji hao kwa kuidhinishwa kwa kulipwa kwa mabilioni ya Shilingi itaongozwa na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru),Mamlaka ya udhibiti wa Ununuzi katika sekta ya Umma (PPRA),pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana kuwasimamisha baadhi ya watendaji wakuu wa kampuni ya Reli hapa nchini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta akionyesha baadhi ya Ripoti za uchunguzi za mamlaka ya Bandari,TPA na Ripoti ya shirika la Reli jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Waandishi wa Habari walio hudhuria katika mkutano wa Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta katika wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo.(Picha na Avila kakingo)

BENKI YA DCB YAKABIDHI MSAADA WA KOMPYUTA KWA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI ARNAUTOGLU

$
0
0
    Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe.Dkt.Pindi Chana akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Kompyuta katika  Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu  kilichopo Manispaa ya Ilala,leo jijini Dar es Salaam.
    Meneja Masoko na Maendeleo ya Bidhaa wa DCB Commercial Bank,Bw.Boyd Mwaisame akifafanua jambo  wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Kompyuta katika  Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu  kilichopo Manispaa ya Ilala,leo jijini Dar es Salaam.
    Baadhi ya Wanafunzi wa  Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu wakisikiliza kwa makini risala iliyo kuwa ikisomwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe.Dkt.Pindi Chana leo Jijini Dar es Salaam.
0  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe.Dkt.Pindi Chana (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu  kilichopo Manispaa ya Ilala,leo jijini Dar es Salaam.( Picha na Emmanuel Massaka)




Na Bakari Issa,Dar es Salaam.

Benki ya Biashara ya DCB imetoa msaada wa Kompyuta kwa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu  kilichopo Manispaa ya Ilala,kwa lengo la kutoa elimu katika Chuo hiko chenye wanafunzi wenye ulemavu.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo wa Kompyuta kwa Chuo hicho,Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe.Dkt.Pindi Chana amesema  umuhimu wa Vyuo hivi unatokana na lengo la kuanzishwa kwake aambalo ni kutoa maarifa na stadi zitakazowawezesha wananchi kujiajiri,kujitegemea  ili kuondokana na ujinga,umaskini na maradhi hatimaye waweze kuchangia kuinua uchumi wa taifa.

Pia,Dkt.Chana amewahasa wazazi kuacha kuwaacha watoto wao kukaa nyumbani bila kujishughulisha na shughuli yeyote pindi wanapomaliza masomo yao na badala yake kuwashughulisha watoto hao ili kujiepuka kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa.

Kwa upande wake,Meneja Masoko na Maendeleo ya Bidhaa wa DCB Commercial Bank,Bw.Boyd Mwaisame amesema  Benki imekabidhi msaada huo kutokana na kuguswa na matatizo mengi yanayojitokeza katika jamii likiwemo la ukosefu wa vitendea kazi . kwa watoto wenye Ulemavu.

Naye, Mkuu wa  Chuo hiko,Bi.Pulcheria M. Ndamgoba ametoa  shukrani kwa msaada huo wa Kompyuta katika Chuo hiko na kuahidi kukitumia vizuri katika kutoa elimu chuoni hapo,huko Kiongozi wa  Wanafunzi wa Chuo hiko,Ridhwan Omary akitoa msisitizo kwa Benki hiyo kuwasaidia kujengea viwanja vya michezo.

NEC YAANZA MAFUNZO YA UCHAMBUZI WA MIFUMO YA COMPUTER

$
0
0
Afisa Mchambuzi wa Mifumo ya Computer wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Amos Madaha akizungumza katika semina ya siku nne ya matumizi ya fomu mbalimbali za uandikishwaji wa wapiga kura (BVR) ya mafunzo kwa zaidi ya wachambuzi 500 yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mchambuzi wa Mifumo ya Computer wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Adolf Kinyero akizungumza katika semina ya siku nne ya matumizi ya fomu mbalimbali za uandikishwaji wa wapiga kura (BVR) ya mafunzo kwa zaidi ya wachambuzi 500 yanayofanyika jijini Dar es Salaam. 
Zaidi ya wachambuzi 500 wamekutanishwa na NEC kwa ajili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya mfumo wa BVR.

USAFI WA MAZINGIRA UENDANE NA UTOAJI WA ELIMU BORA KWA WANAFUNZI-DC.MUSHI.

$
0
0
Mkuu wa Wilaya Ilala, Raymond Mushi (katikati) akizungumza katika siku ya kilele cha maadhimisho ya uboreshaji mazingira ya shule za msingi na sekondari za halmashauri ya manispaa ya Ilala, yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam leo. (kushoto) Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mugurumu(kulia) ni Mwenyekiti kamati ya uchumi na huduma za Jamii Manispaa ya Ilala  Angelina Malembeka.
0Kikundi Mganda cha shule ya Msingi Umoja ya Manispaa ya Ilala kikitoa burudani katika maadhimisho ya uboreshaji mazingira ya shule za msingi na sekondali za halmashauri ya manispaa ya Ilala.
Baadhi ya Waalimu na Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari wakiwa na kombe lao la ushindi wa utunzaji wa mazingira, katika maadhimisho ya uboreshaji mazingira ya shule za msingi na sekondali za halmashauri ya manispaa ya Ilala.PICHA NA EMMANUEL MASSAKA.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

MKUU wa Wilaya Ilala Raymond Mushi ametaka usafi wa Mazingira uendane na utoaji wa elimu bora kwa kuweka mazingira rafiki ya kufundishia wanafunzi

Mushi  aliyasema hayo leo wakati wa maadhimisho ya uboreshaji wa Mazingira katika Shule Msingi na Sekondari kwa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam,Mushi amesema mazingira rafiki  kwa wanafunzi yanawafanya kupenda shule na kuachana na utoro pamoja kuongeza ufaulu katika mitihani ya taifa.

Mushi amesema asasi pamoja na idara za sekta ya umma kuhakikisha suala la elimu ya mazingira na usafi linapewa kipaumbele katika maeneo yao ya kazi . Aidha amesema kila mtu kwa nafasi yake anatakiwa kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wa mazingira kulingana na sheria  zinavyoelekeza na watu waliopewa mamlaka ya kusimamia mazingira kuhakikisha zinafanya kazi kwa bidii.

Mushi amesema madhara yakitokea kutokana na uchafu wa mazingira  waadhirika ni wote hivyo ni vyema kila mtu afanye usafi kwa nafasi yake bila kumsubiri mtu mwingine.

IGP MANGU AKUTANA NA MASHEIKH JIJINI DAR LEO

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akiongozana na viongozi wa dini ya kiislamu (kulia) Mwakilishi wa Mufti wa Tanzania katika Mafunzo hayo Sheikh Abubakar Zuber na kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwinyibaraka Sheikh Issa Othman wakati akilelekea kufungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo Viongozi wa dini ya Kiislamu ili kuimarisha usalama nchini.Mafunzo hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Mwinyibaraka na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.(Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi)
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, akizungumza na  viongozi wa  dini ya kiislamu waliohudhuria katika mafunzo ya kuwajengea uwezo Viongozi wa dini hiyo.Mafunzo hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Mwinyibaraka na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akizungumza  na Katibu wa Jumuiya ya Wanazuoni wa kiislamu Sheikh Khamisi Mataka katika Mafunzo ya kuwajengea uwezo Viongozi wa dini ya Kiislamu ili kuimarisha usalama nchini.Mafunzo hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Mwinyibaraka na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.

ZANZIBAR INAHITAJI KUENDELEA KUWA SALAMA NA TULIVU-BALOZI SEIF ALI IDDI

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kati Kati akisindikizwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Said Mohd Dimwa Kulia yake mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa pamoja  kati ya Uongozi wa Kampuni inayohusika na masuala ya Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini  { SRT } na watendaji wa sekta ya Habarini hapo Zanzibar Ocean View.
  Afisa Mkuu wa Mradi wa Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini  wa Kampuni ya { SRT } kutoka Nchini Uingereza  Bwana Simon Tucker akielezea umuhimu wa kifaa cha mawasiliano kinachotumika katika vyombo vya usafiri Majini kwenye Mkutano wa pamoja na watendaji wa Sekta ya Baharini hapa Zanzibar.

Wa Pili kutoka Kulia waliokaa ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Kulia ya Balozi ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Said Mohd Dimwa na wa kwanza kulia ni Bwana Lazaria Moh’d Said.
Balozi Seif akizungumza na Wanahabari   mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa pamoja kati ya Uongozi wa Kampuni inayohusika na masuala ya Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini  { SRT } ya Nchini Uingereza na  watendaji wa Taasisi zinazohusika na sekta hiyo hapo Zanzibar.

SHUKURANI

$
0
0

Familia ya Kanali mstaafu Julius L. Mugeko ya Kibaha kwa Mathias, inapenda kutoa shukrani za dhati kwa  ndugu jamaa na marafiki walioshirikiana nasi katika kufanikisha  shughuli za msiba wa kijana wetu mpendwa GODFREY MWITA MUGEKO aliyefariki dunia tarehe 22 February, 2015 katika hospitali ya Tumaini Dar- es- salaam na kuzikwa tarehe 28  February,  2015 katika makaburi ya PAROKIA YA NYAMIONGO - MAKOKO MUSOMA.

Familia inatoa shukrani za dhati kwa Daktari Malikita na wauguzi wa hospitali ya Tumaini, Paroko wa parokia ya Mkuza Kibaha na jumuiya ya Mt. Andrew Mtume - kigango cha Nyumbu. Paroko na jumuiya ya Mt. Yuda Thadei Parokia ya Nyamiongo Makoko Musoma, kamati za maandalizi za shughuli za mazishi Kibaha na Musoma.
Tunashukuru kwa jinsi mlivyokuwa karibu nasi kwa maombi na dua wakati wote wa kumuuguza hadi tulipompumzisha ndugu yetu.
Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru kila mtu kipekee, tunaomba shukrani hizi mzipokee kwa mikono miwili kutokana na jinsi mlivyohusika kwa njia moja ama nyingine katika kufanikisha shughuli nzima ya msiba wa mpendwa wetu GODFREY MWITA MUGEKO.

Bwana alitoa na bwana ametwaa,
Jina lake lihimidiwe.
AMINA

KUELEKEA SIKU YA HEDHI DUNIANI, MTANDAO WA HEDHI SALAMA WAENDESHA SEMINA SHULE YA SEKONDARI ST. ANTHONY

$
0
0
 Daktari Edna Kiogwe akieleza juu ya umuhimu wa elimu ya Hedhi kwa jamii nzima wakati wa semina na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Anthony.
Mkurugenzi mtendaji wa Kasole Secrets Hyasintha Ntuyeko ambeye pia ni muandaaji wa siku ya Hedhi Duniani kwa Tanzania akielezea umuhimu wa kutunza Mazingira wanapokuwa Hedhi na kuithamini miundombinu.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Anthony wakiwa wanafuatilia kwa makini Semina hiyo.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Anthony wakifurahia Pads za Glory walizopewa ikiwa ni ishara ya kusherehekea sikukuu ya Hedhi Duniani. Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

mazishi ya Chigwele Che Mundugwao kufanyika kwao wilayani masasi, Mtwara, kesho

$
0
0

MAZISHI ya aliyekuwa msanii wa muziki wa asili Chigwele Che Mundugwao, 46, aliyefariki dunia jana asubuhi katika hospitali ya taifa Muhimbili, yanatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa  Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara.

Rais
 wa Shirikisho la Muziki Tanzania Ado Novemba, alisema marehemu alifikwa na umauti huo baada ya kufikishwa hospitalini akitokea Keko gerezani ambako alikuwa mahabusi.
“Marehemu Che Mundugwao alikuwa akisumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu miezi miwili iliyopita, akiwa huko alipelekwa katika hospitali ya Amana na kugundulika na tatizo hilo. Mpaka sasa bado hatujafahamishwa chanzo cha kifo chake,” alisema Novemba.
Naye Makamu wa shirikisho hilo Samuel Mbwana alisema, “Che Mundugwao alilazwa katika hospitali ya Amana kwa kipindi cha miezi miwili kabla ya kurudishwa mahabusu na baadaye alipelekwa katika hospitali ya Muhimbili ambako alilazwa kwa muda kabla ya umauti kumfika leo saa moja asubuhi. Taarifa za mwisho za marehemu bado hatujazipata. Na ukizingatia alikuwa chini ya ulinzi hivyo bado hatujajua.”
Chigwele Che Mundugwao aliyekuwa ofisa Manunuzi  wa Idara ya Uhamiaji na wenzake watatu walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam mapema mwaka jana, wakikabiliwa na mashtaka manne likiwemo kosa la wizi wa  Pasipoti 26.


Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images