Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 803 | 804 | (Page 805) | 806 | 807 | .... | 3285 | newer

  0 0


  0 0

   Pichani juu ni mmoja wa majeruhi akisaidiwa na msamaria mwema mara baada ya kupata ajali. 

   Mtu mmoja amefariki dunia huku wengine 25 wakijeruhiwa katika ajali ya basi la abiria la Jordan lenye usajili wa namba T 650 AQZ lililokuwa likitokea jijini Mwanza kwenda mkoani Arusha na kupinduka leo wilayani Nzega,Tabora.Mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.
   Baadhi ya Majeruhi mara baada ya ajali hiyo kutokea.
   Baadhi ya Abiria wakiwa nje ya basi la Jordan mara baada ya kupinduka wilayani Nzega mkoani Tabora na kupelekea kifo cha mtu mmoja.
  Mmoja wa abiria akifanya mawasiliano baada ya kunusurika kifo basi la Jordan mara baada ya kupinduka wilayani Nzega mkoani Tabora na kupelekea kifo cha mtu mmoja.

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Uingereza na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe, jijini Dar es Salaam leo.  Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
   Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe, jijini Dar es Salaam leo.  Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimkaribisha ofisini kwake, Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose, wakati balozi huyo alipomtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kujadiliana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Uingereza na Tanzania. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb),akimkaribisha Wizarani Waziri wa Mambo ya Nje wa Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe El-Anrif Said Hassane kwa mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Comoro.
  Balozi wa Comoro hapa Nchini Mhe.Dr.Ahamada El Badaoui Mohamed(kushoto)akisalimiana na Naibu Waziri Dkt.Mahadhi huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro Mhe.El-Anrif Said Hassane(katikati) akishuhudia.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb),akifurahia jambo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro wakati wakiendelea na mazungumzo yao.
  Katibu wa Naibu Waziri, Bw.Adam Misara (kulia) pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bw.Mudrick Soragha wakinukuu mazungumzo kati ya mhe. Mahadhi na Mhe. Hassane (hawapo pichani).
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb),akifafanua jambo katika kikao hicho.Picha na Reuben Mchome

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Mhe. Skeikh Sabah Al-Khalid Al-Sabah,  Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait. Waziri Membe alifanya ziara ya siku moja nchini humo tarehe 14 Aprili, 2015 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.
   Waziri Membe akimtambulisha kwa Mhe. Skeikh Sabah Al-Khalid Al-Sabah,  Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya.
  Mazungumzo ya ushirikiano yakiendelea.


  0 0

  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Rajab Gamah akifungua kikao  kati ya Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar inayosimamia Ofisi za Viongozi za Kitaifa  kushoto ni Mwenyekiti wa Jimbo la Kwamtipura Mhe. Hamza Hassan Juma kulia ni Mwenyekiti wa Jimbo la Wawi, Mhe. Saleh Nassor Juma. 

  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za Viongozi wa Kitaifa wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Gamaha (hayupo pichani).
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara za Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo (kushoto) akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bi. Bictoria Mwakasege (katikati)  na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw. Elibariki Maleko  wakati wa kikao kati ya  Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
  Kikao kikiendelea.Picha na Reginald Philip 

  0 0

    Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA),Gilliard Ngewe akizungumza na waandishi wa habari  kuhusiana na ushushwaji wa nauli za mabasi ya masafa marefu ofisini kwake jijini Dar es salaam leo.
   kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Udhibiti usafiri wa barabara,Geffrey Silinda akifafanua jambo kwa waandishi wa habari  katika ofisi za Mamlaka ya Uthibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) leo jijini Dar es Salaam,kulia ni  Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA),Gilliard Ngewe. 
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii)

  Na Bakari Issa,Globu ya jamii.

  Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) imeshusha nauli za mabasi ya masafa marefu huku nauli za daladala  viwango vyake vikibaki kama kawaida.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA),Gilliard Ngewe wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam leo.

  Ngewe amesema uamuzi huo umekuja baada ya mamlaka hiyo kufanya utaratibu wa kupitia kanuni kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali ikiwemo watoa huduma ili kutoa maoni yao,kutokana na ongezeko la msongamano wa magari mijini.

  Viwango vilivyobainishwa kutokana na ukokotoaji wa nauli mpya za mabasi ya mijini ni pamoja na;

   0-10km nauli ya sasa ni Sh.400 sawa na asilimia 5.8
  11-15km nauli ya sasa ni Sh.450 sawa na asilimia 0.3
  16-20km nauli ya sasa ni Sh.500 sawa na asilimia 2.9
  21-25km nauli ya sasa ni Sh.600 sawa na asilimia 2.8
  26-30km nauli ya sasa ni Sh.750 sawa na asilimia 1
  Huku nauli ya Mwanafunzi ikibaki palepale sh.200

  Wakati viwango vipya  vya nauli za mabasi ya masafa marefu ni pamoja na;
  Daraja la kawaida la chini kwa Barabara za Lami ,viwango vipya vilivyoridhiwa ni 34.00 TZS/Abiria/km sawa na 7.8%
  Daraja la kawaida la chini kwa Barabara za vumbi ,viwango vipya vilivyoridhiwa ni 42.50 TZS/Abiria/km sawa na 7.8%
  Daraja la kawaida la juu, kiwango kilichoridhiwa ni 44.96TZS/Abiria/km
  Daraja la kati,viwango vilivyoridhiwa ni 50.13TZS/Abiria/km sawa na 5.81%
  Aidha,Bodi hiyo ya Wakurugenzi imeamua kwamba nauli za mabasi ya hadhi ya juu (Luxury bus) hazitadhibitiwa ili kuchochea ubunifu katika utoaji huduma na ushindani kati ya huduma za barabara na njia njinginezo za usafiri.

  0 0
  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, akiwaonesha waandishi wa habari ( hawaonekani pichani) milipuko hatari  aina ya ' Water explosives gel ' iliyokamatwa jana usiku kutoka kwa watuhumiwa  tisa waliokuwa wamehifadhiwa ndani ya  msikiti wa  Suni uliopo Tarafa ya Kidatu, wilayani Kilombero mkoani Morogoro.

  0 0

  TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo kwa watumishi wa wa umma na kampuni zilizoidhinishwa, mwishoni mwa wiki ilizindua tawi lake jipya la 80 wilayani Ileje, mkoani Mbeya, huku Mkuu wa wilaya hiyo, Rosemary Staki Senyamule, akiwataka wananchi wake kukopa kwa sababu maalum.
  Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Mheshimiwa Rosemary Senyamule kulia, akionyeshwa nyaraka za ofisi ya Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, inayojihusisha na mambo ya mikopo katika uzinduzi wa taasisi hiyo katika wilaya hiyo ya Ileje, mkoani Mbeya. Kushoto ni Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Alpha Akim. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wilayani humo. 

  Kufunguliwa kwa tawi hilo si kutainua uchumi wa wananchi wa Ileje watakaotumia fursa ya uwapo wa ofisi hiyo, bali pia kutarahisisha utoaji wa huduma wa taasisi hiyo ya Bayport nchini Tanzania.

  Wageni mbalimbali wakiangalia shughuli za uzinduzi wa tawi jipya la taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, wilayani Ileje, mkoani Mbeya, mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya hiyo, Rosemary Senyamule.

  Akizungumza katika uzinduzi wa tawi hilo jipya, Mkuu huyo wa wilaya Ileje, Rosemary alisema kuwa wananchi wakiitumia fursa ya tawi hilo kutainua pia kiwango cha uchumi cha watu wake.
  Baadhi ya wageni waalikwa wakisoma vipeperushi vya taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, wilayani Ileje, mkoani Mbeya.
  Alisema suala la mikopo ni jambo jema kutokana na uwezo mzuri unaoweza kuwaendeleza wananchi, wakiwamo watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zote zilizoidhinishwa, ambao kimsingi ni watu wanaotakiwa kuendelezwa kwa mambo mengi.
  Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa Bayport Financial Services, Alpha Akim, akizungumza jambo katika uzinduzi wa tawi lao la 80 wilayani Ileje, mkoani Mbeya, mwishoni mwa wiki iliyopita na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
  HABARI ZAIDI INGIA HAPA

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Uongozi wa Mamlaka zinazohusika na  uwekezaji Tanzania na Wawekezajia kutoka Egypt wakati ujumbe huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo April 15, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wawekezajia kutoka Egypt baada ya mazungumzo yao wakati ujumbe huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo April 15, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wawekezajia kutoka Egypt baada ya mazungumzo yao wakati ujumbe huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo April 15, 2015.


  0 0

  Mwakilishi wa Vijana kutoka kamati ya kudhibiti Ukimwi manispaa ya Shinyanga Bw,Rigobert Rwehumbiza akielezea wajibu binafsi kwa kijana kwa washiriki wenzie katika warsha ya siku nne ya stadi za maisha na afya ya uzazi.
  Katibu asasi ya Vijana ya Boys & Girls Bw,Johnson Jacob kutoka Bariadi akionyesha igizo lilikuwa likionyesha wajibu wa Vijana  kwa Familia ikiwamo kuwalinda na kuwapatia mahitaji yao muhimu.
  Mtaalamu wa Stadi za Maisha Bw,Robert Semkiwa akiwafundisha waratibu wa ukimwi na maafisa Vijana wanaohudhuria Warsha ya siku tatu inayohusu Stadi za maisha na Afya ya uzazi jinsi ya kukabiliana na Msongo wa Mawazo na njia gani za kutumia kukabiliana nao.
  Waratibu wa Ukimwi na maafisa Vijana wakiwa katika mjadala wa pamoja wakipambanua kwa kina stadi mojawapo katika stadi tatu za maisha ya kujitambua leo jijini Mwanza.kundi ili lilikuwa likijadili jinsi ya kukabili mihemko kwani ni  hatua mojawapo kijana anayoipitia katika maisha yake.


  0 0

  Mafundi wakiendelea na kazi za ujenzi wa daraja kubwa la Kolo lenye urefu wa mita 60 katika barabara ya Dodoma-Babati sehemu ya kipande cha barabara ya kutoka Mela kwenda Bonga chenye urefu wa km 88.8. Ujenzi wa daraja hilo unatarajiwa kukamilika mwezi Mei mwaka huu.
  Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Dodoma, Eng. Leonard Chimagu (watatu kutoka kushoto) akiwa na wahandisi wa barabara ya kutoka Mela-Bonga mara baada ya ukaguzi wa daraja la Kolo.
   Kazi za ujenzi zikiendelea kwenye tuta la barabara ya Mayamaya-Mela km 99.35.

  Ujenzi wa Barabara ya Dodoma (Mayamaya) hadi Babati km 188.15 katika sehemu ya Mayamaya-Mela  km 99.35  pamoja na kipande cha Mela Bonga km 88.8 unaendelea vizuri na unatarajiwa kukamilika mwaka 2017.

  Kauli hiyo ilitolewa na Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoani Dodoma Eng. Leonard Chimagu wakati akifanya ukaguzi wa ujenzi wa barabara hiyo inayojulikana kama barabara kuu ya Kaskazini  iliyoanzia Cape town nchini  Afrika Kusini hadi Cairo nchini Misri

  “Katika barabara kuu hiyo sehemu yetu ya Tanzania ndio ilikua haina lami ila kwasasa ujenzi umeanza na unaendelea vizuri, ujenzi wa barabara katika sehemu ya kwanza ya Mayamaya-Mela km 99.35  umefikia asilimia 18 na ule wa Mela Bonga km 88.8 umefikia asilimia 20 ya ujenzi wake” alisema Eng. Chimagu.

  Eng. Chimagu aliongeza kuwa  mkandarasi yupo katika hatua za mwanzo na anaendelea vizuri na  kama hakutakuwa na vikwazo vyovyote basi ataikamilisha barabara hiyo kwa wakati”, alisema Eng. Chimagu.

  Kwa upande wa Mhandisi Mshauri katika sehemu ya barabara ya Mayamaya-Mela km 99.35   Eng. Godfrey Kombe alisema kuwa kazi za ujenzi zinaendelea vizuri na tayari mkandarasi ameshasafisha eneo la barabara lenye urefu wa km 70.

  “Tayari Mkandarasi ameshasafisha eneo la barabara lenye urefu wa km 70 kwa kuondoa miti mikubwa, pia ameweza kujenga jumla ya makalavati 52 ya duara pamoja na 12 ya boksi”, alibainisha Eng. Kombe.


  0 0

  Na. Wambara Mayori, Pwani.
     
  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Bi Subira Khamis Mgalu, amewasihi wananchi wa  Kisarawe kulinda ardhi yao kama mboni ya jicho  na kuwataka kuacha tabia ya kuuza ardhi yao kiholela na badala yake wajikite katika kuyaendeleza maeneo yao. 

  Bi Subira, amesema kuwa, kuna watu hutumia kofia ya uwekezaji katika nchi hii kujitwalia ardhi katika maeneo mbalimbali  na kisha kuyatelekeza bila ya kufanyiwa kazi kwa muda mrefu na kuleta usumbufu mkubwa kwa wananchi wanaoishi kuzunguka maeneo hayo kwa kugeuka kuwa  mazalia na makazi ya nyoka , maficho ya wahalifu na baadaye kuwa chanzo cha migogoro ya ardhi alisema.

  Alisema, hatuhitaji wawekezaji wasio na tija kwa wananchi wa wilaya ya Kisarawe, na kusisitiza kuwa muda wa wawekezaji hewa umekwisha na wala hatuhitaji wawekezaji wanaokuja na mikoba bali tunawakaribisha wawekezaji wenye tija wanaoweza kutoa fursa ya ajira kwa wananchi na vijana wa wilaya ya Kisarawe.

  Hata hivyo, ametoa wito kwa wenyeji na wakazi wa wilaya hiyo kutokuwa wepesi kununulika kwa watu wajanja wachache wanaojiita wawekezaji na badala yake wawe macho na watu hao ili wasijikute wanapoteza ardhi yao.

  Aidha, Mkuu huyo wa wilaya, amewaonya viongozi wanaokumbatia wawekezaji hewa katika wilaya hiyo na   amewataka wananchi kushikamana na  kushirikiana na viongozi wao wa vijiji na mitaa katika kupanga na kusimamia  mipango yao ya maendeleo kwenye maeneo yao kwani maendeleo yao ni maendeleo ya wilaya ya Kisarawe, alisema.

  Alisema, Bi Subira, ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Homboza        kilichopo Kata ya Msimbu Tarafa ya Sungwi wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, huku akiwatahadhalisha kuwa, hakuna mtu yeyote anayeweza kumkataza ama kumnyima mtu haki yake ya kikatiba ya kuchagua kiongozi anayemtaka kwa kuwa hiyo ni haki yake na hivyo si haki kwa baadhi ya wananchi wa kijiji cha homboza, kunyimwa haki ya kuchagua kiongozi wanayemtaka katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni.

  Mkuu wa wilaya ya Kisarawe  Bi Subira Khamis Mgalu  amewataka wananchi wanaokidhi vigezo kutumia haki yao ya kikatiba kujitokeza na kujiandikisha kwa wingi wakati wa uandikishaji kwenye daftari la wapiga kura na siku ya kupiga kura wajitokeze kwa wingi ili kuwachagua viongozi wanao wataka bila bughudha yoyote.

  0 0
 • 04/15/15--10:44: KUMBUKUMBU
 • Miaka sita imepita toka ulipotuaga tarehe 15 April 2009 na kuzikwa nyumbani kijiji cha Buhangaruti, Mugana Catholic Parish, Bukoba. 

   Unakumbukwa daima na mume wako Dr.F.C.Kahabuka, wanao Anna, Oliva, Mary, Prim, Pelagia pamoja na wakwe zako na wajukuu, ndugu, majirani na marafiki na wote tunazidi kukuombea upumzike mahali pema huko peponi, Amina.

  0 0

  Meneja Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa GEPF, Bw. Aloyce Ntukamazina (kushoto) akimkabidhi rasmi kadi ya uanachama, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh. Chiku Gallawa mara tu baada ya kujiunga na Mfuko huo akionyesha ni jinsi gani Mfuko umejipanga vyema kuwahudumia wanachama wake kwa wakati. 
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Chiku Galawa akijaza fomu na kujiunga rasmi na Mpango wa hiari wa kujiwekea akiba ulianzishwa na GEPF (VSRS) akishuhudiwa na meneja wa GEPF mkoa wa Dodoma Bw Josephat Mshana.
  Meneja Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa GEPF, Bw. Aloyce Ntukamazina (kushoto) akimkabidhi cheti cha ushiriki mmoja kati ya wadau wa mkoa wa Dodoma.
  baadhi ya wadau wa mikoa ya Dodoma na Singida wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa (hayupo pichani) wakati akitoa nasaha zake.
  washiriki wa semina hiyo maalum wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mara baada ya ufunguzi wa semina hiyo.

  0 0

   Biashara ya kuuza chenji za sarafu imezidi kutoga katika maeneo mengi hapa jijini Dar, kama inavyoonekana pichani. Hapo ukitoa Buku unapata sh. 700 inayobaki inakuwa imekatwa.Upo hapoo???

  0 0
 • 04/15/15--13:06: SHIMOZZZ
 • Mkazi wa Jiji la Dar es salaam akikatiza kando ya shimozz la chemba lisolokuwa na mfuniko, lilipo katika makutano ya Mtaa wa Mkwepu na Sokoine Drive, Katikati ya Jiji.

  0 0
 • 04/15/15--13:16: YALE YALEEEE........

 • 0 0


  Balozi Henry Mdimu akiongea na vyombo vya habari


  Taasisi isiyo ya ki serikali ya Imetosha Foundation inayopinga unyanyapaa, ukatili na mauaji dhidi ya watu wenye ualbino kwa njia ya elimu, inatarajia kutuma ujumbe mzito kanda ya ziwa hapo kesho kwa maandalizi ya ujio wa timu nzima ya taasisi hiyo iliyojikita kwenye kubadilisha mtazamo (mind set) wa watu juu ya janga hili. Ujumbe huo utaongozwa na mwenyekiti wa taasisi hiyo Bw Masoud Kipanya, Balozi Henry Mdimu Mgaya na katibu Salome Gregory,wajumbe watakaongozana na viongozi hao ni pamoja na Mkala Fundikira, Isaya Mwakilasa (wakuvwanga aka Baba Andunje) Zaytun Biboze, Kelvina John na msanii wa muziki wa reggae Jhikoman Manyika.
  Mwenyekiti Masoud Kipanya akiongea katika kilele cha matembezi ya hamasa yaliyofanyika jijini Dar.

  Dhumuni la safari hiyo itakayoupeleka ujumbe huo mpaka mkoani Shinyanga ni kwenda kujitambulisha kwa viongozi wa serikali na usalama wa mikoa na za kanda hiyo iliyoathiriwa sana na janga la ukatili na mauaji ya watu wenye ualbino. Taasisi ya Imetosha imepanga kwenda kanda ya ziwa baadaye mwezi ujao ambapo timu itaenda maeneo yaliyoathiriwa na kutoa elimu kwa wakazi wa maeneo hayo kuwa si kweli kwamba ukiwa na kiungo cha mtu mwenye ualbino utapata mafanikio, elimu hizo zitatolewa kwa njia ya filamu mbali mbali, michezo ya kuigiza na matamasha ya muziki.
  Hoteli ya Green Palm utakapofikia ujumbe wa Imetosha Foundation jijini Mwanza aka the Rock City.
  Ujumbe huu ukiwa mjini Mwanza utakuwa chini ya udhamini wa hoteli ya Green Palm iliypo maeneo ya Bwiru, vile vile kampuni ya Mwananchi communication ltd (MCL) inayozalisha gazeti bora la Mwananchi na mengineyo itachapisha habari zote kuhusiana na msafara huo wa Imetosha kanda ya ziwa. Meneja wa hotel 

  Isaya Mwakilasa wa (Orijino komedi) Henry Mdimu na familia ya Isaya aka Wakuvwanga
  ya Green Palm Bw Juma Herman ameuambia mtandao huu kuwa "imekuwa rahisi kwetu (Green Palm Hotel) kudhamini makazi na usafiri kwa taasisi hiyo kwa kuwa inachofanya ni kitu chema basi nasi tumeona ni vema tuwatie nguvu kwa kuwapatia malazi na usafiri wa ndani kwa kipindi chote watakachokuwa jijini Mwanza, kwa kweli sasa imetosha ukatili na mauaji dhidi ya watu wenye ualbino" aliongeza.
  Wakiongea na mtandao huu kwa nyakati tofauti Mwenyekiti Masoud Kipanya na Balozi Henry Mdimu walisema  wanashukuru sana kwa kitendo cha Green Palm na Mwananchi communictaion na kuwa ni vya kuigwa na makampuni mengine ili kuiwezesha taasisi hiyo kufikia malengo yake. Taasisi ya Imetosha haina vyanzo vya fedha hivyo kutegemea wahisani kama Green Palm Hotel na Mwananchi communication.
  Maktaba Baadhi ya wajumbe wa Imetosha wakijiandaa kwenda katika mchezo wa Simba na Yanga

  0 0

  Na   Bashir  Yakub.

  Upangaji  kama  upangaji  una  mambo  mengi.  Hii  ndio  sababu sheria  imegusa  eneo  hilo  pia.  Kila  mtu  anajua  kuwa upangaji  si  lazima  uwe  wa  nyumba  ya  kuishi tu bali  hata  ule  wa  maeneo  ya  biashara  pia.  Ipo  misuguano  mingi  ambayo  hutokea   katika  miamala  ya  upangaji  na upangishaji. Ipo  misuguano  inayotokana  na  ukorofi  tu  lakini  ipo  misuguano  inayotokana  na  kutojua  baadhi  ya  mambo  ya  msingi  na  ya  kisheria  kuhusu  dhana  nzima  ya  upangaji  na upangishaji . Leo  nitaeleza  mambo  mawili  tu   kuhusu  upangaji  na  upangishaji.

  1.INARUHUSIWA  KUPANGA  NA  WEWE UKAMPANGISHA  MWINGINE.

  Sheria  haimkatazi  mtu kupanga  sehemu  halafu   naye akaamua  kumpangisha  mwingine.  Hili  lipo  na  si  kinyume  cha  sheria  kufanya  hivi.  Na  zaidi  hata  huyu  aliyepangishwa  naye  anaweza  kumpangisha  mwingine  wa  tatu.  Yaani  ikawa  A  amempangisha  B  na  B  amempangisha  C   na  C  amempangisha  D  na  wote katika  eneo  hilohilo.  
  Hii  yote  inaruhusiwa  na   upangaji  wa  kila  mmoja  unalindwa  na  sheria    na  kila mmoja  anapata  haki  zake kwa  nafasi  yake.  Kwa  mfano  kila mpangishaji  ataitwa  mwenye  nyumba  yaani  A  ataitwa  mwenye  nyumba  na  B  na  B  ataitwa  mwenye  nyumba  na  C  na  C  ataitwa  mwenye    nyumba  na  D.  Halikadhalika  kila  aliyepangishwa  ataitwa  mpangaji. 

  Suala  la  msingi  sana  katika  upangaji  wa  namna  hii  ni  kuwa  ule  mkataba  wa  mwenye  nyumba  halisi  ambaye  ni mmiliki  kabisa  yule  A   uwe  unatoa  ruhusa  kwa    mpangaji aliyempangisha naye kuruhusiwa  kupangisha  mwingine   na  yule  mwingine  naye  mkataba  wake umruhusu  kumpangisha mwingine  na  mwingine  naye  mkataba  wake  umruhusu  kumpangisha  mwingine  iwe  hivyohivyo.   Ikiwa  mkataba  wa  mmoja haumruhusu  kupangisha zaidi  basi  huyo  asiyeruhusiwa   hawezi  kumpangisha  mwingine  na  akifanya  hivyo  itakuwa  kinyume    cha  sheria. Kisichowezekana  ni  kuwa huwezi kuwa  mpangaji  halafu  ukampangisha  mwingine  bila  kuwa  umeruhusiwa  kufanya  hivyo  na  mwenye  nyumba  katika  mkataba  wenu. older | 1 | .... | 803 | 804 | (Page 805) | 806 | 807 | .... | 3285 | newer