Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

Waziri Membe KUSHIRIKI MKUTANO WA KUZUIA UHALIFU NA HAKI ZA WAHALIFU Nchini Quatar

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe (Mb.) akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Quatar Mh. Dkt. Khalid Mohamed Al Attiyah, walipokutana na kufanya mazungumzo kuhusu kuendeleza mahusiano kati ya Tanzania na Quatar pia kutangaza Fursa za uwekezaji nchini Tanzania. Waziri Membe yupo nchini Quatar kwa madhumuni ya kushiriki mkutano kuhusu Kuzuia Uhalifu na Haki za Waalifu. 
Mazungumzo yakiendelea
Waziri Membe akiwa Katika picha ya pamoja na Bw. Noel Kaganda Mshauri wa maswala ya kisheria wa Rais wa kikao cha 69 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Mhe. Sam Kahamba Kutesa.

Umuhimu wa kudhibiti matumizi ya vyombo vya elektroniki kwa watoto na vijana

$
0
0

Zaidi ya asilimia 60 ya watoto wenye umri wa miaka 13 hadi 17 wanatumia zaidi ya masaa mawili kila siku kuangalia mitandao ya kijamii pamoja na vipindi mbalimbali vya Televisheni. Hii inaweza kuwa njia kubwa ya kuunganisha, lakini pia kuna hatari zinazohusiana na kutumia muda mwingi sana kwenye vyombo vya habari kijamii.

Leo hii ni nadra kukuta familia ambazo watoto na vijana wake hawajaathirika na vyombo vya habari na elektroniki kama vile televisheni, intaneti na michezo mingine tofauti ya kompyuta.
Hata hivyo utumiaji mkubwa na wa masaa mengi wa vyombo hivyo hauwahusu watoto na vijana tu, bali watu wazima pia wameathirika na jambo hilo.

 Kutokana na sababu kadhaa za kimwili, kisaikolojia na kiroho, kuna udharura kwa watoto kusimamiwa vyema na wazazi, mashirika na taasisi za kielimu na kiutamaduni na kadhalika vyombo vya habari ili kupunguza madhara yanayotokana na matumizi mabaya ya vyombo hivyo vya elektroniki. Licha ya kompyuta kuwa na pande chanya tofauti za kimaendeleo, hasa katika nyanja za kielimu na huduma za mawasiliano, lakini chombo hicho pia kina nafasi hasi kwa watoto na hata kwa watu wazima. 

Utumiwaji usio na udhibiti wa chombo hicho na kadhalika vyombo vingine vya elektroniki kama vile televisheni, unaweza kuyaweka hatarini maisha ya watoto kutokana na athari zake mbaya kwa ustawi wa kiroho, kisaikolojia na kijamii wa watoto hao.

Harakati zetu za kifizikia na miamala yetu tofauti ya kijamii, ni umuhimu yenye taathira kubwa kwa afya na tabia za mtoto. Kinyume chake, ikiwa mtoto atatumia muda wake mwingi katika matumizi ya michezo ya kompyuta, basi hawezi kunufaika na upande chanya wa kujenga akili yake wala harakati bora kwa ajili ya kuufikia ukamilifu wake kijamii. 

Mbali na hayo, watoto pia wanaweza kukabiliwa na hatari ya kutekeleza vitendo vya ukatili na visivyo vya kikatili hata katika umri wao mdogo. Hali hiyo ambayo inaweza kufikiwa ghafla au hata kwa makusudi, huwaletea watoto na vijana madhara yasiyoweza kufidika hasa kuhusiana na masuala ya kiafya, kisaikolojia sambamba na kueneza kwa kiasi kikubwa matatizo ya kimwili na kiakili kama vile utovu wa maadili, vitendo vya ukatili, madawa ya kulevya, tabia mbaya katika jamii, kuzorota thamani za familia na kuenea jinai na uhalifu wa kila aina katika jamii.

Tangazo la Msiba Leicester, Uingereza

$
0
0

Annur Community Centre Leicester, UK,  Inasikitikita kutangaza kifo cha Mume wa Dada Ashura Juma, Bwana Twalib Durrace kilichotokea Jumatatu 13/04/15 Peterborough City Hospital.

Mazishi yatafanya leo Jumanne 14/04/15 hapo Peterborough central Mosque saa Tisa Mchana. Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana na Abdul Dau 07792104495. 
Innaa Lillaahi wa Innaa Ilayhi Rajioon.


Khamis Sahal, 
Mdhamini Jumuia ya  Annoor 
170a Belgrave Gate, Leicester LE1 3XL.

TAMISEMI yatoa ufafanuzi uhaba wa vyakula mashuleni

$
0
0
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu baadhi ya Shule za Sekondari za Bweni  zilizofungwa kutokana na ukosefu wa chakula ambapo alisema shule hizo zimefungwa kimakosa kwani Serikali imeshapeleka fedha za kununulia chakula kwenye halmashauri zote nchini. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Elimu TAMISEMI Bw. Zuberi Samataba.
 Naibu Katibu Mkuu Elimu TAMISEMI Bw. Zuberi Samataba akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam mpango wa Serikali kuajiri waalimu wa shule za msingi wenye elimu ngazi ya Stashahada badala ya Cheti kama ilivyo sasa. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu ajira kwa walimu wapya waliohitimu 2014/2015 na kutoa rai kwa waalimu hao kwenda kuripoti kwenye vituo vya kazi watakavyopangiwa.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini wakati wa mkutano uliofanyika leo kwenye ofisi za TAMISEMI  jijini Dar es Salaam. Picha na Fatma Salum (MAELEZO)

KONYAGI YAWASOMESHA WANAFUNZI WA WAKULIMA WA ZABIBU DODOMA

$
0
0

 Mratibu wa Mpango wa Somesha mtoto wa Mkulima wa zabibu ulidhaminiwa na Tanzania Distillaries LTD (TDL) Saimon Chibehe akizungumza jambo na wakulima wa zabibu pamoja na wanafunzi wa Kata ya Handari wilayani Chamwino, Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.
 Mratibu wa Mpango wa Somesha Mtoto wa Mkulima wa zabibu unaodhaminiwa na Kiwanda cha Konyagi cha  Tanzania Distillaries LTD (TDL), Saimon Chibehe akizungumza jambo akizungumza na Wazazi, Walezi ambao ni wakulima wa zabibu pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mpunguzi iliyopo Manispaa ya Dodoma, mwishoni mwa wiki.
 Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu wa Shule ya Sekondari Mvumi, mkoani Dodoma, Nuru Peter akiwa katika shamba la Zabibu la Wazazi Wake wakati alipofika kumuonesha Mratibu wa Mpango wa Somesha mtoto wa Mkulima wa zabibu ulidhaminiwa na Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distillaries LTD (TDL) Saimon Chibehe (hayupo pichani) mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mpunguzi wanaofadhiliwa na Konyagi kwa kulipiwa Ada, Sale za shule na bweni wakiwa katika picha ya pamoja kwenye kibao cha shule hiyo iliyopo manispaa ya Dodoma.

TAARIFA ZA MICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

$
0
0
KAMATI YA USIMAMIZI NA UENDESHAJI YA BODI YA LIGI.

Kocha Jackson Mayanja wa Kagera Sugar amepigwa faini ya sh. 500,000 na kufungiwa mechi tatu kwa kutoa lugha ya kashfa kwa maneno na vitendo kwa waamuzi wa mechi yao na Mtibwa Sugar kuwa walipewa rushwa.

 Adhabu dhidi ya Kocha Mayanja kwenye mechi hiyo namba 136 iliyochezwa Aprili 1, 2015 kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 40(1) ya Ligi Kuu.

 Klabu ya Mtibwa Sugar imepigwa faini ya sh. 500,000 baada ya timu yake kukataa kuingia vyumbani wakati wa mapumziko katika mechi namba 142 dhidi ya Stand United iliyochezwa Aprili 5, 2015 katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.  Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu.

 Nayo Simba imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa mujibu wa kanuni ya 14(9) ya Ligi Kuu baada ya timu yao kugoma kuingia kwenye vyumba vya kuvalia nguo (changing room) kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakati wa mechi dhidi ya Kagera Sugar. Hatua hiyo ilisababisha wachezaji wakaguliwe kwenye gari lao. 

Pia Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kuzingatia kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu baada ya vilevile kugoma kuingia vyumbani wakati wa mapumziko kwenye mechi hiyo hiyo namba 146 iliyochezwa Aprili 6, 2015. 

Kipa Tony Kavishe wa Polisi Morogoro amepigwa faini ya sh. 500,000 na kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kumpiga ngumi mwamuzi msaidizi namba mbili, Hassan Zani kwa kuzingatia kanuni ya 37(5) ya Ligi Kuu. Alifanya kosa hilo kwenye mechi namba 147 dhidi ya Mgambo Shooting iliyochezwa Aprili 5, 2015 katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.


Mshindi mwingine wa milioni 100 za Jaymillions akabidhiwa kitita chake

$
0
0
 Mshindi wa kitita cha shilingi milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hamisi Khalid (kushoto) mkazi wa Mtwara akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi yake na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kulia) baada ya kuibuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ili  mteja kujua kama  ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
 Mshindi wa kitita cha shilingi milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hamisi Khalid (kushoto) mkazi wa Mtwara akikabidhiwa hundi yake na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi hiyo baada ya kuibuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo. Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo mlimani city jijini Dar es Salaam. Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ili  mteja kujua kama  ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
 Rosalynn Mworia ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania (kulia) akimpongeza kwa kumpigia makofi mshindi wa kitita cha shilingi milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo, Hamisi Khalid (aliyeshikilia hundi) mkazi wa Mtwara wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi hiyo baada ya kuibuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo. Hafla hiyo ilifanyika Makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ili  mteja kujua kama  ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kulia) akisoma tarakimu kwenye hundi yenye thamani ya shilingi milioni 100/- wakati wa hafla ya kumkabidhi hundi hiyo mshindi wa kitita cha shilingi milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hamisi Khalid (aliyeshikilia hundi) baada ya kuibuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo. Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ili  mteja kujua kama  ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.

NEWZZ ALERT :BASI LA KAMPUNI YA GAMET TRANS LAPATA AJALI KIBITI-MKOA WA PWANI

$
0
0
Taarifa zilizoifikia Globu ya Jamii hivi punde kutoka chanzo cha kuaminika,zinaeleza kuwa Basi la kampuni ya GAMET Trans linalofanya safari zake Dar-Lindi-Masasi-Nachingwea limepata ajali maeneo ya Kibiti wilaya ya Rufiji-Utete mkoa wa Pwani baada ya kutaka kumkwepa mtu anayedaiwa kuwa na tatizo la ulemavu wa akili,lakini kwa bahati mbaya likamgonga na kufariki papo hapo,taarifa zaidi zinaeleza kuwa baada ya ajali hiyo basi hilo liliacha njia na kupinduka na kupelekea kifo cha mtu mmoja aliyegongwa na wengine waliokuwemo ndani ya basi hilo (idadi ya abiria haikujulikana mara moja) kujeruhiwa.




WAZIRI CHIKAWE-ASASI KIRAIA ZINAZOJIHUSISHA NA SIASA KUFUTWA

$
0
0
 Waziri wa mambo ya Ndani ya nchi, Mathias Chikawe  akizungumza na waandishi wa Habari ( hawapo pichani) kuhusiana  na Taasisi za Dini na vikundi mbalimbali  kuepuka kushiriki  katika  vitendo ambavyo vinaashilia kuvuruga amani na utulivu nchini jijini  Dar leo.
Baadhi ya Waandishi habari waliohudhuria katika mkutano wa wizara ya Mambo ya Ndani  jijini Dar es salaam leo.Picha Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii.


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.


ASASI za Kiraia  zilizosajiliwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,vinavyojihusisha na siasa na kuacha katiba zao vitaanza kufutwa kuanzia Aprili 30 mwaka huu.


Hayo ameyasema  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mathias Chikawe wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea katika Kura ya maoni pamoja na Uchaguzi Mkuu,Chikawe amesema serikali iko imara katika kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani hivyo watu wanaotaka kuharibu amani  kutumia asasi za kiraia na kuacha katiba zao watafutwa.


Chikawe amesema katika kuelekea uchaguzi kumekuwa na  asasi za kiraia  zikijihusisha na siasa kwa kuchangisha fedha kwa ajili kuwashawishi viongozi wa siasa wagombee hiyo ni kwenda kinyume na katiba zao na kutakiwa kufutiwa usajili.


Amesema katika suala la ugaidi ni tatizo la dunia hivyo kinachofanyika ni kuimarisha ulinzi katika maeneo yetu na kupata taarifa kwa watu wanaoingia nchini na watu wanaobainika kutoa kuwa na taarifa wanawarudisha katika nchi zao.


Chikawe amesema vijana wa kitanzania ambao wamekamatwa nchini Kenya kuhusika na ugaidi hawana taarifa, wanachokifanya ni kupata taarifa kutoka Kenya kama kuna watu wengine wapo katika kundi la al-shabab.


Aidha amesema jeshi liko imara hivyo wananchi waishi kwa amani kwani serikali ina imarisha ulinzi kuhakikisha amani inakuwepo.

BREAKING NEWZZZZZ;RADI YAUA MWALIMU NA WANAFUNZI SITA KIGOMA

$
0
0
 Mwalimu Merina Sekilo aliyenusurika kupigwa na radi wakati akifundisha darasa la kwanza,ambapo wanafunzi 6 walifariki
 Mwalimu Veronika Mtes wa shule ya msingi Kibirizi aliyepata mshtuko baada ya tukio la radi akiwa katika hospitali ya Mawenzi mkoa wa Kigoma  kwa matibabu.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa wa Kigoma,Maweni  akiongeza na Waandishi wa habari juu ya tukio la radi lililotokea hivi punde na kuuwa watu 8

Na Editha Karlo Karlo wa blog ya jamii,Kigoma
WATU wanane wakiwemo wanafunzi sita na mwalimu wa shule ya msingi kibirizi mmoja pamoja na mtu wa kawaida mkazi wa eneo la Bangwe mjini hapa  wamekufa baada ya kupigwa na radi huku wanafunzi wengi 15 wakijeruhiwa na radi hiyo mchana huu.

Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa kigoma(maweni)Dkt Fadhili Kabaya alisema kuwa watu hao walifikwa na mauti hayo kufiatia mvua kubwa zilizonyesha zikiambana na radi zilianza majira ya saa sita mchana.
Dkt Fadhili aliwataja waliokufa katika tukio hilo kuwa ni pamoja na mwalimu wa shule ya msingi kibiriziElinaza Mbwambo(25)mtu mwingine wa kaida ni Forcus Ntahaba(45)mkazi wa eneo la Bangwe mjini hapa.

Aliwataja wanafunzi waliofariki ambao wote ni wa darasa la kwanza kuwa ni Yusuph Ntahoma(8)Hassan Ally(9)Fatuma Sley(7)Zamda Seif(8)Shukranmi Yohana(7) na Warupe Kapupa(10).

Alisema walipokea majeruhi kumi na tano lakini kati yao kumi wametibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumba baada ya hali zao kuwa nzuri na watano wamelazwa wanaendelea na matibabu katika hospital ya Mkoa wa Kigoma.
Akisimulia tukio hilo mwalimu aliyekuwa anafundisha darasani Mwalimu Merina Sililo alisema kuwa akiwa darasani akiendelea kufundisha ghafla aliona wingu zito jeusi limetanda hadi akashindwa kuendelea kuandika ubaoni.

''Manyunyu yalianza kidogo kidogo ikaja mvua kubwa na radi pamoja na miungurumo mikali sana iliyopelekea wanafunzi kuanguka ovyo darasa na kuzima na mara niliona moto umetanda katika chumba kuzima cha darasa na mimi nilianguka chini na kupoteza fahamu''alisema mwalimu huyo
Alisema apozinduka alijikuta katika hospital ya Mkoa wa maweni akipatiwa matibabu baada ya kuletwa kwa msaada wa waalimu wenzie.

''Kwakweli ni mungu tu mwenyewe ndo ameninusuru kwani nilirushwa mmara tatu na radi na watoto wote wote darasani walikuwa wananiangukia mimi wengine walikuwa wanakimbia ovyo nje''alisema Mwalimu huyo

KAMANDA MPINGA-MADEREVA WALIOSABABISHA AJALI KWA UZEMBE KUFUTIWA LESENI ZAO.

$
0
0
 Kamanda wa Polisi wa kikosi cha usalama Barabarani Mohammed Mpinga,akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano  na Kamanda wa Polisi wa kikosi cha usalama  barabarani Mohammed Mpinga  jijini Dar leo.(Picha na Emmanuel Massaka).

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

KIKOSI cha Usalama Barabarani kimesema wanazifuta leseni zote kwa madereva waliosababisha ajali kwa uzembe zikiwemo ajali za hivi karibuni.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam,Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Mohamed Mpinga,amesema katika kukabiliana na wimbi la ajali ni pamoja na kufuta leseni kwa madereva wazembe ambao wanasababisha ajali.

Mpinga amesema ajali za hivi karibuni zimesababishwa na uzembe wa madereva, hivyo ni lazima kufuta leseni zao na hawatakiwi kufanya kazi yoyote ya udereva nchini pamoja na kuweka katika tovuti taarifa zao ili watu wengine wasiwachukue.

Amesema katika usafiri wa mabasi watakuwa wanaangalia muda kutoka sehemu hadi nyingine na basi ambalo litakuwa mbele ya muda uliopangwa katika eneo husika hatua zitachukuliwa.

Mpinga ametoa pole kwa wafiwa waliopoteza maisha katika ajali za hivi karibuni na kusema wale wote waliosababisha ajali hizo watafutiwa leseni na hatua zingine kufuta ili madereva wengine wasifanye makosa hayo.


MKUU WA MKOA DODOM MH.CHIKU GALLAWA AFANYA ZIARA KITUO CHA WAKALA WA TAIFA WA HIFADHI YA CHAKULA - NFRA KANDA YA KATI

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa (mwenye kilemba) akioneshwa chakula kilichohifadhiwa kwenye kituo cha NFRA kanda ya kati mapema leo alipofanya ziara kituoni hapo kukagua akiba ya chakula.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa (mwenye kilemba) akikagua akiba ya chakula kilichohifadhiwa kwenye kituo cha NFRA kanda ya kati mapema leo alipofanya ziara kituoni hapo eneo la kizota.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa (kushoto) akifanya ziara ya ukaguzi kwenye kituo cha hifadhi ya chakula NFRA kanda ya kati mapema leo alipotembelea kituoni hapo eneo la kizota kujionea kiasi cha akiba ya chakula iliyopo, kulia ni meneja wa NFRA Kanda ya Kati Deusdedit Mpazi.
 Sehemu ya chakula cha akiba kilichohifadhiwa kwenye kituo cha hifadhi ya chakula NFRA kanda ya kati, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa amemuagiza Meneja wa NFRA Kanda ya Kati kufanya taratibu zinazohitajika ili kuingiza chakula hiko kwenye masoko kusaidia kupunguza bei ya chakula  sokoni ili wananchi wanufaike.

SIKU YA UCHAGUZI MKUU ITATANGAZWA NA NEC NA SI VINGINEVYO –LIPUMBA

$
0
0
 Mwenyekiti wa taifa wa Chama  cha Wananchi (CUF),Profesa   Ibrahim Lipumba akizungumza na baraza la uongozi wa chama hicho (hawapo pichani) iliyofanyika Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam, wapili kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar,Nassor Ahmed na kushoto ni makamu Mwenyekiti wa chama cha Wananchi (CUF) Taifa,Duni Haji.
 Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad,akisikiliza kwa makini katika ufunguzi wa mkutano Baraza la uongozi wa chama wananchi  (CUF) na kulia ni Naibu Katibu        Mkuu Zanzibar Nassor Ahmed iliyofanyika Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Baraza la Uongozi wa Chama hicho wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa CUF,Profesa Ibrahim Lipumba  (hayupo pichani) iliyofanyika  leo Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam. (Picha na Avila Kakingo)


Na  Avila Kakingo,Globu ya Jamii.


 TUME ya Taifa ya  uchaguzi (NEC) ndiyo inayotakiwa kutangaza siku ya kufanyika kwa uchaguzi Mkuu mwaka huu pamoja na kutangaza matokeo ya viongozi watakao kuwa wameshinda katika uchaguzi huo.


Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama  cha Wananchi (CUF),Profesa  Ibrahim Lipumba wakati akifungua mkutano Baraza la uongozi wa chama hicho  leo jijini Dar es salaam.  Lipumba amesema kuwa  ucheleweshwaji wa  uandikishaji wa daftari la wapiga kura  linatia shaka kutokana na kutokukamilika kwa zoezi hilo mpaka sasa.


Aidha amesema kuna  vifungu vya sheria kwenye katiba pendekezwa virekebishwe hasa kifungu cha Tume ya Taifa  Uchaguzi (NEC) kutangaza Matokeo ya uchaguzi mkuu  ya Rais atayekuwa ameshinda na  awe amepata kura zaidi ya asilimia 50 pia matokeo hayo yahojiwe au  yakikishwe na mahakama.

MAKONDA AKUTANA NA WANANCHI WA KAWE MZIMUNI KUTATUA MGOGORO WA ARDHI

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akizungumza na wananchi wa Kawe Mzimuni alipofika kutatua mgogoro wa ardhi kati yao na taasisi moja ya kiislamu inayomiliki Shule ya Sekondari ya Seminari ya Qiblatain D $B iliyopo eneo hilo Dar es Salaam leo asubuhi.
 Katibu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa eneo hilo Mgili Wambura alimwambia DC Makonda kuwa eneo hilo tangu zamani ilikuwa ni barabara hivyo wanashangaa kuvamiwa hivyo alimuomba Makonda kusaidia kuondoa mvutano huo.


KATIBU WA CHADEMA KANDA YA KASKANI AKIZINDUA MPANGO WA KUICHANGIA CHADEMA

$
0
0
 Katibu wa CHADEMA kanda ya Kaskazini Amani Golugwa akifafanua jambo
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Uzinduzi wa mpango wa
kuchangia Chadema kwa kutumia simu za mikononi kukiwezesha chama hicho kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu.Picha na mahmoud ahmad

TANZANIA KUSHIRIKI MKUTANO WA TATU WA MAENDELEO ENDELEVU YA MIJI NA MAKAZI DUNIANI NCHINI KENYA

$
0
0
Ujumbe wa Tanzania Kwenye Kamati ya maandalizi ya Mkutano wa tatu wa Maendeleo endelevu ya Miji na Makazi Duniani (HABITAT 3) unaofanyija jijini Nairobi nchini Kenya. Ujumbe huo unaongozwa na Naibu katibu Mkuu,Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Dkt.Seleseid D.Mayunga (MBELE KULIA). Wengine pichani ni Maafisa waandamizi wa serikali.

WARSHA YA STADI ZA MAISHA NA AFYA YA UZAZI KWA WARATIBU WA UKIMWI YAFANYIKA LEO JIJINI MWANZA

$
0
0

 Mtaalamu wa Afya ya Uzazi kutoka  chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania Mkoa wa Mwanza  Bi,Jacinta Mutakyawa (Aliyesimama)  akiongea na waratibu wa Ukimwi,Maafisa Vijana na Wadau mbalimbali juu ya haki za Afya ya Uzazi na Ujinsia leo jijini Mwanza.Haki izo zikiwemo haki ya kuwa huru  dhidi ya vitendo vya ukatili na haki ya kuchagua na kupanga uzazi.


Mratibu wa Ukimwi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bw,Musa Varisanga(Aliyevaa Miwani)  akifurahia jambo na Mratibu wa Vijana kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Bi,Grace Kessy(wa Kwanza Kulia)  leo jijini Mwanza inapofanyika Warsha ya Stadi za Maisha na Afya ya Uzazi  katika hoteli ya Midland.
 Washiriki  wa warsha ya stadi za maisha na afya ya uzazi  wakimsikiliza kwa makini mtaalamu wa afya ya uzazi(hayuko pichani)  kutoka Mwanza Bi,Jacinta Mutakyawa alipokuwa akiwapa elimu ya Afya ya Uzazi ikijumuisha Afya ya Ujinsia na Haki zake leo jijini Mwanza  katika hoteli ya Midland.Warsha iyo imefikia siku ya Pili.

MASHINE ZA BVR AWAMU YA PILI KUPELEKWA MIKOA SABA

$
0
0
 Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nchini Tanzania itaanza kusambaza mashine za BVR 248 katika mikoa saba nchni Tanzania Kuanzia katikati mwa wiki ijayo.
Mikoa iliyopangwa kuanza kupokea mashine hizi ni mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa, Wakati zozi likianza mikoa hiyo nyingine zitakuwa zinapelekwa katika mikoa ya Katavi, Mbeya na Dodoma. Mikoa mimgine ni Singida Tabora Geita na Kigoma.

Mkuu wa kitengo cha Ufundi wa idara ya Daftrari/ICT wa NEC Dr Sisit Cariah, Akizungumza na mwandishi wetu amesema kwamba mpaka sasa wanachi wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvumna na Iringa wakae tayari kwani muda wowote watatangaziwa vituo vya kujiandikisha.
 Pamoja na mshine hizo 248 Tume ya taifa ya uchaguzi imewaandaa wataalamu 248 ambao watakuwa na jukumu la kutoa elimu kwa wataalamu wengine 50 kwa kila mmoja nchi nzima kwa ajili ya kuharakisha uandikishaji kwa mfumo wa BVR.
Dr Sisit Ameeleza kwamba wamefanikiwa kufanya maboresho makubwa katika mashine hizi ikiwa ni pamoja na kubadilisha upangaji wa vifaa (settings), mfumo endeshi (Software) na upande wa Vichapishio (printer) ambazo sasa zimetengenezewa Nchini Ufaransa umeboreshwa na nirahisi kusafishwa.

BALOZI SEIF ALI IDDI AWAKUMBUSHA WANANCHI KUWAUNGA MKONO VIONGOZI WANAOWASIMAMIA HARAKATI ZA MAENDELEO YAO.

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi msaada wa Vipaza sauti Amiri  wa Jumuiya ya Sherehe za Siku Kuu ya Iddi Matemwe Ustaadhi Kundi Choum Haji kutekeleza ahadi aliyoip[a Jumuiya hiyo wakati wa sherehe za siku kuu ya Iddi el Hajj iliyopita.
  Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman  Iddi akimkabidhi  mchango wa Shilingi 400,000/-  kwa kila kikundi miongoni mwa  vikundi 14 vya Ushirika wa Akina Mama vilivyomo ndani ya  Wilaya ya Kaskazini “ A “.
 Balozi Seif akikabidhi Seti moja ya Jezi na Mipira kwa kila Timu ya Soka miongoni mwa timu nne zilizomo ndani ya Jimbo la Matemwe.

Usikae kimya! Wafanye wabadilike

Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images