Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

KAYA MASIKINI ZATAMBULIWA MUFINDI KUPITIA MRADI WA TASAF

$
0
0
Jumla ya kaya masikini elfu Tisa 277 zimetambuliwa na Halmashauri ya wilaya ya Mufindi, katika utekelezaji wa hatua ya awali ya kuzibaini kaya masikini kwenye vijiji na mitaa ikiwa ni mpango wa awamu ya tatu wakuzinusuru kaya masikini unaoratibiwa na mfuko wa maendeleo ya jamii nchini Tasaf kuputia Halmashauri hiyo.

Taarifa ya Ofisi ya habari na Mawasiliano ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa vyombo vya habari, imetanabaisha kuwa, wawezeshaji wapatao 72 walijengewa uwezo wa kubaini vigezo kwa kaya masikini, ambapo hojaji zilifanyiaka na jumla ya vijiji 82 na mitaa 12 walifanya dodoso na kuzibaini kaya masikini elfu tisa 277.

Taarifa  hiyo imeeendele kubainisha kuwa, tayari kaya hizo zimepelekwa Tasaf makao makuu ili kufanyiwa uchambuzi wa mwisho unaozingatia vigezo kwa njia ya teknolojia ya kompyuta na mara baada ya kurejea kwa kaya teule, zoezi litakalofuata ilitakuwa ni uandikishaji  kabla ya kuziwezesha kifedha, ambapo kila kaya inatarajia kupata shilingi elfu 38 na 100 kila mwezi kwa kipindi cha miaka mitatu.

Pamoja na uwezeshaji huo katika ngazi ya kaya, mpango huo pia unakusudia kuibua na kutekeleza miradi ya msingi ya huduma za kijamii kwenye  sekta za Afya, Elimu na Maji katika maeneo ambayo kaya hizo zimetambuliwa.

Aidha, masharti makuu kwa kaya zitakazo teuliwa na kupatiwa fedha kwa kipindi chote cha miaka mitatu ya mradi zitalazimika kuzizalisha kwa kujiunga kwenye vikundi vya kuweka na kukopa au kuanzisha biashara ya kujiingizia kipato huku wale watakaoshindwa kutekeleza masharti hayo wataondolewa.

Katika hatua nyingine timu ya maofisa iliyokuwa ikiendesha zoezi la hojaji ya kuzitambua kaya hizo lilikabilina na changamoto kadhaa ikiwa ni pamaoja na uwelewa mdogo kuwa fedha hizo ni za bure, kuzihusisha Fedha hizo na Asasi maalufu ya(Free Mason) baadhi ya kaya kupatikana maeneo yasiyofikika kwa urahisi asanjari na baadhi ya wananchi kukana kwamba wao si masikini licha ya kutanjwa na wakazi wenzao.

WARSHA YA STADI ZA MAISHA KINGA DHIDI YA MAAMBUKIZI YA UKIMWI YAFANYIKA JIJINI MWANZA

$
0
0
 Kaimu katibu Tawala mkoa wa Mwanza Bw.Ndaro Kulinjirwa akiongea na Maafisa Vijana,Waratibu wa Ukimwi na Vijana (Hawapo Pichani) kutoka katika Mikoa  ya Simiyu,Shinyanga na Mwanza alipokuwa akizindua rasmi warsha kuhusu Stadi za Maisha kwa washiriki hao leo jijini Mwanza ikishirikisha wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo na Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania .Warsha iyo ya siku nne  inafanyika katika hoteli ya Midland. Kushoto kwake  ni Mratibu wa Vijana kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Bi,Grace Kessy na wa kwanza kulia ni Mtaalamu wa Stadi za Maisha  Bw.Robert Semkiwa.
 Washiriki mbalimbali wa warsha kuhusu Stadi za Maisha wakimskiliza kwa makini Kaimu katibu Tawala mkoa wa Mwanza Bw.Ndaro Kulinjirwa(hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao leo jijini Mwanza.Bw Kulinjirwa aliwasisitiza washiriki hao kutumia vyema mafunzo watakayopata ili kubadili maisha yao na ya jamii nzima kwani Stadi za Maisha ndio kinga dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.
 Mtaalamu wa Stadi za Maisha Bw.Robert Semkiwa(Aliyesimama) akifurahia jambo na washiriki wa warsha ya siku nne kuhusu Stadi za Maisha  kutoka katika mikoa ya Mwanza,Simiyu na Shinyanga leo hii jijini Mwanza.Warsha hiyo imeanza leo ikiwashirikisha Waratibu wa Ukimwi,Maafisa Vijana na Wadau Mbalimbali.Warsha hii inafanyika katika hoteli ya Midland jijini Mwanza.

Waratibu wa Ukimwi,Maafisa Vijana na Vijana wakiwa katika Picha ya pamoja na Kaimu Katibu tawala Mkoa wa Mwanza Bw.Ndaro Kulinjirwa(aliyekaa mwenye suti ya khaki),Mtaalamu wa Stadi za maisha Bw.Robert Semkiwa(wa Kwanza kushoto aliyekaa),Bi Grace Kessy kutoka Tume ya kudhibiti ukimwi Tanzania  (wa pili kutoka kulia waliokaa) na Bw, Godfrey Masawe ambaye ni Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo(wa kwanza kutoka kulia waliokaa).

MSHINDI WA SHINDANO LA AIRTEL TRACE STARS AFRICA KUTANGAZWA RASMI NA AKON APRIL 18, 2015

$
0
0
 Dar es Salaam, 13 April 2015 Finali ya shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika lililoshirikisha washiriki kutoka nchi 13 barani Afrika chini ya majaji mahiri akiwemo  Akon, Devyne Stephens na Lynnsha  mwisho mwa wiki hii watashirikiana kumtanga rasmi mshindi wa Airtel Trace Afrika.
Airtel kupitia taarifa yake iliyotumwa na ofisa uhusiano wake Jane Matinde imesema “Shughuli nzima ya kumtangaza mshindi itaonyeshwa  kupitia chanel ya Trace inayopatikana katika kituo cha DSTV #325  siku ya jumamosi tarehe 18 April 2015

Shindano hilo kabambe la  Airtel Trace music star lilihusisha washiriki wengi  walioshiriki kupitia kupiga simu na kurekodi mojakwa moja ambapo jumla ya simu zaidi ya milioni mbili na laki tatu  za washiriki wote zilipigwa na kufanya namba ya washiriki wa shindano hili kubwa Afrika kuweza kuzidi mashindano ya Ulaya na marekani kama vile ya voice na idols.

Washiriki 13 kutoka nchi za Afrika waliingia katika kinyanganyiro cha kutafuta mshindi tarehe 28 machi 2015.  Usikose kushuhudia shindano hilo la  kusisimua lenye vionjo vya kila aina, mbwembwe na bashasha tele.

Finali hizi za Airtel Trace Stars zitaonyeshwa siku ya Jumamosi ambapo watazamaji na majaji  watachagua na kutangaza mshindi ambaye atapata dili la kurekodi , kupata mafunzo ya muziki kutoka kwa mwanamuziki nguli wa nchini Marekani lenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani 500,000/=

Progam hii ya finali itarushwa siku ya Jumamosi ya tarehe 18 April kuanzia saa tatu Usiku na kurudia siku ya Jumapili tarehe 19 Aprili kuanzia saa kumi jioni katika chaneli ya Trace urban.  Kipindi kitadumu kwa muda wa dakika tisini.

WAMA WAKISHIRIKIANA NA ENGENDER HEALTH WAANDAA SEMINA YA KUZUIA MIMBA ZA UTOTONI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI ZA WILAYA YA TEMEKE.

$
0
0
  Meneja Uragibishi na Mawasiliano wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Ndugu Philomena Marijani (aliyesimama)akitoa maelezo mafupi kuhusu semina ya siku 5 kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari katika Wilaya ya Temeke itayozungumzia uzuiaji wa mimba za utotoni kwa wanafunzi wa wilaya hiyo. Semina hiyo inafanyika katika Shule ya Sekondari Kibasila kuanzia tarehe 13 hadi 17.4.2015.
  Baadhi ya wanafunzi na walimu kutoka Shule 11 za Sekondari katika Wilaya ya Temeke wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi, Afisa Elimu-Sekondari wa Wilaya ya Temeke Ndugu Donald Chavila (hayuko pichani) wakati alipokuwa akifungua rasmi semina ya siku tano inayozungumzia uzuiaji wa mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Wilaya hiyo tarehe 13.4.2015 kwenye ukumbi wa sherehe wa Kibasila Sekondari.
  Afisa Elimu-Sekondari wa Wilaya ya Temeke Bwana Donald Chavila akifungua rasmi semina ya siku 5 ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari katika Wilaya ya Temeke. Semina hiyo inaendeshwa na Taasisi ya WAMA, ikishirikiana na Shirika la Engender Health la Marekani na kufadhiliwa na Shirika la Misaada la Serikali ya Marekani,USAID.
Mwanafunzi mshiriki wa semina ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa shule za sekondari katika Wilaya ya Temeke akiwasilisha majibu ya majadiliano ya kikundi chao katika siku ya kwanza ya semina hiyo. PICHA NA JOHN  LUKUWI.

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YAWAHAKIKISHIA WAFANYAKAZI WA SHAMBA LA MPIRA KICHWELE KULIPWA MISHAHARA YAO

$
0
0
Balozi Seif akiwaahidi Wafanyakazi wa shamba la Mipira Kichwele hatua zitakazochukuliwa na Serikali juu ya matatizo yao likiwemo la kulipwa haki zao.Picha na – OPMR – ZNZ.
 Mmoja wa Wafanyakazi wa shamba la Mipira Kichwele akiwasilisha malalamiko yao mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani wakidai kutolipwa mishahara yao kati ya miezi mitatu hadi Minane.
 Mwakilishi wa Kampuni ya Agro Tec ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bidi ya Uongozi wa Kampuni hiyop Bwana Soud Moh’d Achili akitoa ufafanuzi mbele ya Balozi Seif kuhusu shutuma zilizotolewa  na Wafanykazi wa shamba la Mipira Kichwele dhidi ya Kampuni yake.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Shama la Mipira Kichwele wakifuatilia mkutano wakati wakiwasilisha malalamiko yao kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif dhidi ya muwekezaji wa mradi huo.


MKUTANO WA ACT WAZALENDO JIMBO LA MOROGORO MJINI LEO

$
0
0
Wanachama  ACT  wazalendo la  wananchi  wa   jimbo la  Morogoro  mjini wakiwa katika mkutano  wa ACT wazalendo leo




viongozi  wa  kitaifa  wa ACT  wazalendo  wakiimba  wimbo wa  Taifa  kabla ya  kuanza  mkutano  wa  hadhara  jimbo la  Morogoro  mjini  leo
Wanachama  wa  ACT  wazalendo  wakiimba  wimbo wa  Taifa  leo.
Picha zaidi BOFYA HAPA

huduma bora za ujenzi DMV

$
0
0
Kazi yetu ni kutoa huduma bora za ujenzi katika maeneo ya Washington DC, Maryland na Virginia, kwa huduma za ukarabati wa nyumba yako, kitaalamu na kwa ufanisi zaidi.

Tunaweza kushughulikia mahitaji yote ya matengenezo yanayohusu ujenzi ama ukarabati wa nyumba yako, ili kufanya urahisi wa kile ulichoharibikiwa, kwa uhakika na uwaminifu zaidi juu ya utendaji wa kazi zetu bora kwa ajili ya kusaidiana na mteja kwenye maswala ya ujenzi kwa wamiliki wa nyumba katika maeneo ya hapa DMV.

Tunatoa huduma za vipimo vya nyumba yako bure yani (Free estimate) iwapo mteja ana tatizo lolote lilojiri kwa ukarabati wa nyumba yako .
Tupo DMV kwajili ya kumaliza tatizo la UKARABATI wa nyumba yako endapo utakuwa na tatizo la aina lolote lile.

Tafadhali wasiliana nasi kwa number za simu  202-361-0671 - 301-728-3977
Email: swahilivilla@gmail.com
Professional Handyman Services, wakishirikiana na Abou's Tile Contractors

FAMILIA YA EDWARD MORINGE SOKOINE WAFANYA MISA YA KUMKUMBUKA BABA YAO

$
0
0
Familia aliye kuwa waziri mkuu  wa Tanzania  hayati Edward Moringe Sokoine wakiwa katika ibada maalumu ya maadhimisho ya kifo chake  nyumbani kwake monduli juu, siku ambayo huadhimishwa April 12 kila mwaka
Wake wa  aliye kuwa  waziri mkuu  wa Tanzania  hayati Edward Moringe Sokoine  , wakiweka  mashada ya maua kwenye kaburi la  mume wao nyumbani kwake eneo la monduli Juu wilayani monduli mkoani Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya kifo chake siku ambayo huadhimishwa April 12 kila mwaka.
Watoto wa kiume wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, Kutoka kushoto:  Joseph Sokoine,Tumaini Sokoine na Ibrahimu Sokoine wakiweka shada la maua kwenye kaburi la baba yao nyumbani kwake eneo la Monduli Juu Wilayani Monduli mkoani Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya kifo chake jana.

Watoto wa kike wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, Kutoka kushoto:  Seki Sokoine,Joyce Sokoine ,Mbunge wa Viti Maalum Namelock Sokoine wakiweka shada la maua kwenye kaburi la baba yao nyumbani kwake eneo la Monduli Juu Wilayani Monduli mkoani Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya kifo chake jana.
 Mbunge wa Viti Maalum, Namelock Sokoine akiwa na kaka yake Ibrahim Sokoine katika kumbukumbu ya kifo cha baba yao aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.
 Mbunge wa Viti Maalum na Mtoto wa  aliye kuwa waziri mkuu  wa zamani   hayati Edward Moringe Sokoine, Namilock Sokoine akiongea na baadhi ya wazee wa Kimaasai baada ya misa maalumu ya maadhimisho ya kifo  cha Sokoine amabayo yalifanyika  nyumbani kwa marehemu eneo la Monduli juu wilayani Monduli mkoani Arusha jana.
 Mbunge wa viti maalu, Namelock Sokine akizungumza na wadau waliohudhuria misa hiyo Monduli Juu

Soccer City Mabingwa Safari Nyama Choma 2015 jijini Dar

$
0
0
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa(kushoto) na Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Gerald Ngiichi wakimkabidhi kikombe mchoma nyama mkuu wa Bar Soccer City ya Sinza, Said Dando mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya Safari Lager Nyama Choma jijini Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Leaders mwishoni mwa wiki.
Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Gerald Ngiichi(wa pili kushoto) wakimkabidhi kitita cha Shilingi 1,000 ,000/= mchoma nyama mkuu wa Bar Soccer City ya Sinza, Said Dando mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya Safari Lager Nyama Choma jijini Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Leaders mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa.

Na Mwandishi Wetu.

SOCCER City Bar yenye makazi yake Sinza jijini Dar es Salaam wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Lager Nyama Choma 2015 yaliyofanyiaka mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Leaders Klabu na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi milioni moja na Kikombe.

Nafasi ya pili ilichukuliwa Chamanzi Bar ya Mbagala ambayo ilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 800,000/=,nafasi ya tatu ni Liquid Barya Chang’ombe ambayo ilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 600,000/=,nafasi ya nne ni High Way Bar ya Boko ambayo ilizawadiwa Shilingi 400,000/=, nafasi ya tano ni Amaholo Bar ya Salasala ambayo ilizawadiwa Shingi 200,000/- na nafasi ya sita ni Kilwa road Bar ambayo ilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 100,000/=.

Leo ni siku ya kuzaliwa mwalimu julius kambarage nyerere

$
0
0
Kutoka maktaba: Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa na umri wa miaka 20 (wa tatu kulia waliokaa)  na wanafunzi wenzie wakiwa na Mwalimu Mkuu wa Tabora Boys Bw.  E.S Williams, mwaka 1942.  Mwalimu alizaliwa Aprili 13, 1922 na mwaka huu angekuwa na umri wa miaka 93.

RAIS KIKWETE AZINDUA KOZI MAALUMU YA MAADILI NA UONGOZI, AMSIMIKA MZEE MSEKWA KUWA MWENYEKITI WA KIBWETA CHA MWALIMU NYERERE

$
0
0

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha Programu ya Uongozi na Maadili  katika Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere Kigamoni jijini Dar es salaam leo. Kushoto kwake  ni Waziri wa Elimu Dkt Shukuru Kawambwa na kulia kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsimika rasmi Mzee Pius Msekwa kuwa Mwenyekiti wa Kibweta cha Mwalimu Nyerere cha Uongozi na  Maadili wakati wa uzinduzi wa Kozi Maalum ya Maadili na Uongozi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere Kigamoni jijini Dar es salaam leo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza  Mzee Pius Msekwa akitoa shukurani baada ya kusimikwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa Kibweta cha Mwalimu Nyerere cha Uongozi na  Maadili wakati wa uzinduzi wa Kozi Maalum ya Maadili na Uongozi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere Kigamoni jijini Dar es salaam leo. Kushoto kwake  ni Waziri wa Elimu Dkt Shukuru Kawambwa na kulia kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila.
 Rais Jakaya Mrisho Meza kuu akiwa imesimama na meza kuu  kuimba wimbo wa Taifa baada ya uzinduzi wa Kozi Maalum ya Maadili na Uongozi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere Kigamoni jijini Dar es salaam leo. Kushoto kwake  ni Waziri wa Elimu Dkt Shukuru Kawambwa na kulia kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akielekea kwenye uwanja wa shughuli tayari kuzindua Kozi Maalum ya Maadili na Uongozi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere Kigamoni jijini Dar es salaam leo. Pamoja naye ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila. PICHA NA IKULU

mkutano wa saba wa maji wa dunia seoul, Korea

$
0
0

Spika Anne Makinda na Naibu Waziri wa Maji Mhe. Amos Makalla wakiwa ndani ya treni toka Seoul kwenda Gyeongbuk kushiriki mkutano saba wa Maji wa dunia
Mkutano ukiendelea
Naibu Waziri Maji Mhe Amos Makalla akifuatilia mkutano

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AVALIA NJUGA TATIZO LA UBOVU BARABARA WILAYANI KWAKE

INTRODUCING MIGRSHY FT. WALTER CHILAMBO - MMECHEMKA

DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI LEO JUMATATU 13.04.2015


Article 1

USIKOSE KUANGALIA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA LEO KUPITIA SUPERSPORT NDANI YA DSTV

WANAFUNZI WA CARMAN AINSWORTH HIGH SCHOOL WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON DC

$
0
0
 Wanafunzi wa Carman Ainsworth High School iliyopo Michigan watembelea ubalozi wa Tanzania Washington DC, na kupata fursa ya kuonana na Mhe balozi Liberata Mulamula.
                      Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza kwa makini Mhe, balozi Leberata Mulamula.
                             Mhe, balozi Liberata Mulamula akitoa historia fupi ya Tanzania.

                      Mhe, balozi Liberata Mulamula akiwashukuru wageni wake kwa kuchagua ubalozi wa Tanzania kama sehemu mojawapo ya ziara yao hapa mjini Washington DC.

JE WAJUA UNAWEZA KUNUNUA ARDHI KATIKA MAJENGO MAREFU YANAYOJENGWA SIKU HIZI ?

$
0
0
Na Bashir Yakub
Mara  nyingi  tunapoongelea  umiliki  wa  ardhi  watu  wengi  hukimbilia  kufikiri  kumiliki  ardhi   labda  Pugu,  Bunju, Tegeta, Kimara  na  hata  huko  mikoani.   Wengi  hudhani  kumiliki  ardhi  lazima   iwe  nyumba  hizi  nyumba  za  kawaida   tulizozoea  au  kiwanja    kama  viwanja tulivyozoea au  shamba  kama  shamba.  
Sikatai  kuwa  hizi  sio  ardhi   hapana  hizi  ni  ardhi   ila  ni  vema  sana  kuelewa  kuwa  ulimwengu  umekua  sana  na  kila  kitu  kimepanuka  ikiwemo  dhana  nzima  ya  masuala  ya  ardhi. 
 Leo  tunapozungumzia  suala  la  ununuzi  wa  ardhi   ni  vema  tukapanua    mawazo  yetu  zaidi.  Katika  kupanua  mawazo tutaangalia  kitu  ambacho  ningependa  watu  wengi  wakifahamu.  Kwa    jina  la  kitaalam  kitu hiki  huitwa  ardhi  vipande.  

Ngoma azipendazo ankal kindly sponsored by Isumba Lounge

$
0
0
Evelyn Champagne King - Love Come Down
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images