Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

News alert: Mama Hillary Clinton kuwania urais wa marekani mwakani

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje wa Zamani wa Marekani  Mama Hillary Clinton akiwa na wenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa Ikulu Dar es salam wakati alipotembelea Tanzania June 13, 2011.
Imetangazwa leo kuwa Mama Clintoameamua kujitosa katika kuwania nafasi ya Urais wa nchi hiyo mwakani. John Podesta, Meneja wa kampeni wa Clinton leo katuma email kwa wanaomuunga mkono, kwamba  Clinton yumo katika mbio hizo,
Podesta amesema  Clinton anaelekea Iowa kukutana na wapiga kura na kwamba sherehe rasmi ya kutoa tamko itafanyika mwezi ujao.
Akiongea kwenye video fupi iliyo kwenye tovuti yake rasmi ya kampeni, amesema" Mimi natagombea urais, Wamarekani wamepigana na kigingi cha hali ngumu ya uchumi lakini karata  bado iko mikononi mwa walio juu. Kila siku Wamarekani wanahitaji bingwa, nami nataka kuwa huyo bingwa ili tuweze kufanya zaidi ya kupita tu. Inawezekana kuwa mbele na kubakia mbele, Sababu pale familia zinapokuwa na nguvu, Marekani ina nguvu.
"Hivyo naingia barabarani kupata kura zenu, Sababu huu ni muda wenu na namini mtaungana nami katika safari hii" amesema kwenye video hiyo ambayo ukitaka kuiona kwenye tovuti yake.... 


TAARIFA YA MAFUNZO YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI KUHUSU MTAALA MPYA WA ELIMU YA MSINGI DARASA LA I NA LA II

Lt.Col PASCAL STEPHEN HAULE (Rtd) WA KILUVYA GOGONI AFARIKI DUNIA

0
0
Familia ya Haule wa Kiluvya Gogoni Inasikitika kutangaza kifo cha Mpendwa wao Lt. Col. Pascal Stephen Haule(mstaafu)  Kilichotokea tarehe 10/4/2015 katika Hospitali ya Jeshi Lugalo.
Mazishi yatafanyika nyumbani kwa marehemu Kiluvya Gogoni siku ya Jumanne 14/4/2015 Habari ziwafikie Ndugu  jamaa majirani na marafiki Popote pale walipo.

Bwana Ametoa Bwana Ametwa
 Jina la Bwana Lihimidiwe

TANGAZO LA MSIBA WA MAMA FLORA KAAYA

0
0


Familia ya Marehemu Freddrick Nicholaus Kaaya wa Mikocheni  Dar es Salaam, wanasikitika kutangaza kifo cha mama yao mpendwa Flora Kaaya (pichani) kilichotokea 11/04/2015 katika Hospitali ya TMJ.

Mwili wa Marehemu utaagwa nyumbani kwake Mikocheni siku ya Jumatano Aprili 15,2015 kuanzia saa 4 asubuhi.

Mazishi yatafanyika kijiji cha Akheri –Arumeru, Arusha suku ya Alhamisi Aprili 16,2015 saa 4 Asubuhi.



 BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, 
JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

JK ahudhuria ibada ya kusimikwa askofu Mpya wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu

0
0
ais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza askofu Mpya wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu wakati wa ibada ya kumweka wakfu iliyofanyika katika kanisa kuu la Parokia ya Mama mwenye Huruma, Ngokolo, mjini Shinyanga leo.
---------------------------------
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumapili, Aprili 12, 2015 ameungana na maelfu ya waumini wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Shinyanga, kuhudhuria Ibada rasmi ya kumweka wakfu na kumsimika Askofu mpya wa Jimbo hilo, Mhashamu Baba Askofu Liberatus Sangu.

Rais Kikwete amewasili kwenye Kanisa Kuu la Mama Mwenye Huruma, Ngokolo, mjini Shinyanga kiasi cha saa sita unusu mchana kwa ajili ya Ibada hiyo iliyohudhuriwa pia na maaskofu wakuu, maaskofu na maaskofu wasaidizi 38, akiwamo Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na Rais wa Mabaraza ya Kipapa na Katibu Mwambata wa Uenezaji Injili Ulimwenguni Askofu Mkuu Protase Rugambwa kutoka Makao Makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican.

Askofu Sangu ambaye amewekwa wakfu na kusimikwa kwenye Siku ya Huruma ya Mungu Duniani anakuwa Askofu wa nne wa Jimbo la Shinyanga na anachukua nafasi iliyoachwa wazi tokea Novemba 6, 2012, wakati aliyekuwa Askofu wa Jimbo hilo, Baba Askofu Aloysius Balina alipofariki dunia.

Kwa miaka karibu mitatu, jimbo hilo limekuwa chini ya Usimamizi wa Kitume wa Askofu Mkuu Yuda Tadei R’uaichii wa Jimbo Kuu la Mwanza.

Askofu Sangu mwenye umri wa miaka 52 baada ya kuwa amezaliwa Februari 19, mwaka 1963, katika Kijiji cha Mwazye, Jimbo Katoliki la Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa, alipata daraja la upadrisho Julai 3, mwaka 1994. Wakati anateuliwa na Baba Mtakatifu Francesco kuwa Askofu Februari 2, mwaka huu wa 2015, alikuwa na daraja la Mosinyori.

           Akikabidhi Jimbo hilo kwa Askofu mpya, Askofu Mkuu R’uaichii amesema kuwa Jimbo la Shinyanga ni moja ya majimbo makubwa zaidi ya Kanisa Katoliki nchini, likiwa na kilomita za mraba karibu 30,000 na waumini Wakatoliki wanaokaridiwa kufikia 300,000 katika Mkoa ambao idadi kiasi ya wakazi wake bado wanaamini  imani za jadi.

Amesema kuwa Jimbo hilo lina parokia 29, mapadre wa Jimbo 52, mapadre wa Kitawa 18 na hivyo kulifanya jimbo hilo kuwa na jumla ya mapadre 70 na “jeshi kubwa” la watawa 70.

Kwenye sherehe hizo zilizohudhuriwa na viongozi wengi wa Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Ali Lufunga, Askofu Sangu amepewa zawadi ya sh milioni 18, fimbo ya kiuchungaji na ng’ombe 10 wa maziwa na Wakatoliki wa Jimbo hilo.


Rais Kikwete amerejea Dar es Salaam jioni ya leo baada ya kumalizika kwa Ibada hiyo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa salamu zake za pongezi muda mfupi baada ya kumalizika kwa ibada ya kumweka wakfu askofu mpya wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu katika Kanisa Kuu Parokia ya Mama Mwenye Huruma Ngokolo Mjini Shinyanga.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na maaskofu wa Katoliki muda mfupi Baada ya ibada ya kumweka wakfu askofu mpya wa jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Baba Askofu Liberatus Sangu(wapili kulia pembeni ya Rais) huko Ngokolo mjini Shinyanga leo. Picha na Freddy Maro

msaada tutani: mwalimu wa kiswahili sweden anatafuta mwalimu mwenzie kubadilishana nondo

0
0
Mimi ni mwalimu wa Kiswahili Sweden natafuta mwalimu yoyote anayefundisha kiswahili hapa ili tuweze badilishana materials. Nashindwa kufundisha kwa ufasaha vile sijapata mwenzangu.

Kwa mawasiliano nitumie email.

MEYA WA MANISPAA YA KINONDONI ASHINDA TUZO YA MEYA BORA TANZANIA

0
0
Rais Jakaya Kikwete akikabidhi tuzo ya Meya Bora Tanzania kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda baada ya kushinda tuzo hiyo kitaifa iliyoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa nchini (ALAT) katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Kulia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Agrey Mwanri.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza baada ya kukabidhi Tuzo ya Meya Bora Tanzania, Yusuph Mwenda (kulia) baada ya kushinda tuzo hizo zilizoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa nchini (ALAT) katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB, Tom Boghols na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia (wa pili kushoto).
Rais Jakaya Kikwete akitoa maelekezo kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kulia) kuhusu namna bora ya matumizi ya trekta baada ya kumkabidhi Meya huyo baada ya kushinda Tuzo ya Meya Bora Tanzania kwenye hafla iliyofanyika Dar es Salaam hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki na Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB, Tom Boghols (wa pili kulia).
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akijaribu kuendesha trekta alilokabidhiwa na Rais Jakaya Kikwete baada ya kushinda tuzo ya Meya Bora Tanzania.

Na Mwandishi Maalum,
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda ameshinda Tuzo ya Meya Bora Tanzania na kuzishinda Halmashauri 168 zote nchini.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na Rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda amesema siti ya kushinda tuzo hiyo ni kufanya kazi kwa pamoja kati yake Madiwani, Watendaji na kuwahsirikisha wananchi wake.

Meya Mwenda alisema kuwa Halmashauri yake imekuwa ikifanya kazi kwa uwazi zaidi kwa kuwashirikisha wananchi wake katika mikakati ya kimaendeleo ikiwemo kuwashirikisha katika miadi mbalimbali ya Halmashauri hiyo na hivyo kujikuta kazi yake inakuwa rahisi na kupata mafanikio makubwa kwa muda mfupi.

Mwenda alisema kuwa Manispa yake imekuwa mstari wa mbele katika kusimamia na kuitekeleza miradi yake kwa bidii kubwa ikiwemo ukusanyaji mapato na usimamizi mzuri wa matumizi ya mapato hayo katika miradi hiyo.

“Ushirikiano ‘team work’ kati yangu na madiwani, Madiwani na Watendaji, Ofisi ya Mkuu wa Wialaya na Mkuu wa Mkoandio siri ya mafanikio. Lakini kubwa zaidi ni wananchi wenyewe, kupitia wao tumeweza kuwa na mendeleo zaidi.” Alisema Mwenda.

Aidha Meya Mwenda alisema kuwa Halmashauri yake imefanikiwa kufikia malengo yake kutoka na kuongezeka kwa mapato ya ndani kwa aslimia 360 kutoka shilingi Bilioni 10 mwaka 2011/ 2011 mpaka kufikia Bilioni 36 mwaka jana na kuiwezesha Manispaa hiyo kusimamia vema miradi yake yenyewe.

Aliitaja miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa Barabara, Madara, Zahanati, Shule, matumizi ya Teknohama pamoja na ujenzi wa Kituo kikubwa cha daladala cha kisasa cha Sinza ambacho ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 4.06.

Aidha alisema Halmashauri yake imeweza kuongeza fedha za miradi yake ya maendeleo kutoka Bilioni 3.2 kwa mwaka 2011 mpaka kufikia Bilioni 16 na hivyo kuifanya kuwa ya kwanza nchini kusimamia miradi yake kwa fedha za mapato ya ndani kwa asilimia kubwa.


Hii ni mara ya kwanza kufanyika kwa shindano la Tuzo za Meya Bora Tanzania chini ya Jumuiya ya Serikali za Mitaa nchini (ALAT) ambazo zilikuwa katika makundi mawili makuu ambayo ni Tuzo ya Maendeleo ya Halmashauri na Tuzo ya Jumla ambazo zilifanyika juzi na kuhudhuriwa na Rais Jakaya Kikwete. 

Only lady driver Shazia Khatau wins MMSC Rally Queen trophy in Bagamoyo as Jamil Khan grabs overall trophy

0
0
STORY BY ABDUL HAI & PICTURES BY  SAYED FAIQ 
Machine and drivers’ skills were put to rigorous tests in a sprint rally organized by Mzizima Motor Sports Club in Bagamoyo on Sunday afternoon. Although the dusty track length was only 1.5 kms but it was up and down the hill with tricky turns and twists to be covered in less than ninety seconds.
Out of 37 entries, less than ten drivers just managed to cover the track in less than ninety seconds, one car experienced front wheel tyre burst (the only car driven by a lady driver), two breakdown which needed to be towed away and one almost went topsy- turvy just when the driver was negotiating a left turn. 
No one was hurt as volunteers and track officials used human power to put it aright. Hundreds of motor rally enthusiasts almost forgot to breathe when the teenager Jamil Khan driving his Subaru all-wheel-drive twice covered the track in less than 170 seconds and snatched the Best Overall Trophy in the Sprint Rally. He also received the first trophy in his class of four-wheel vehicles. 
 The only Lady Driver, Shazia Khatau in Nissan Xtrail, despite having got a burst front tyre, quickly came back in high spirits and managed to finish the track but speed-wise not as good as her competitors. She was awarded a “MMSC Rally Queen” trophy. 
The Chairperson of Mzizima Motor Sports Club, also a Lady, Hidaya Thabit Kamanga worked tirelessly with event Secretary Azim Somji and Clerk of the Course Jabu Maalim and Faheem Aloo to keep the crowd on their toes. 
 All the participants were awarded participating certificates and about seven Sponsors were well applauded and awarded recognition certificates. The event was divided in five categories namely Rally Cars; Two wheel drive cars; All wheel drive cars; Sports Utility Vehicles and 4x4 wheel vehicles. 
Three best winners from each category were awarded trophies by Sponsors and veteran rally drivers. 

The only lady driver Shazia Khatau winner of MMSC Rally Queen trophy being presented by veteran rally driver Kirit Pandya.

 4WD Polaris Driver Ebrahim Bockle from Bagamoyo after having a roll-over on the first turning with co-driver Denis from KTM Polaris Dar es salaam.

The overall winner Jamil Khan receiving trophies from veteran rally driver Kirit Pandya. 


April 2015 Night Sky for Tanzania

0
0
Inline image



Venus is extremely bright, noticeable immediately from sunset about 30 degrees above the west horizon.  It will continue to rise higher and reach maximum of 40 degree elevation at sunset in mid-June and after that it will come down again and disappear below the west horizon by the beginning of August.

Jupiter is also very bright high in the sky and is slowly shifting westwards day by day and by 1st July will meet up with Venus for a very close encounter in the sky - a spectacle worth seeing.  Especially on 18th July a thin crescent Moon will join them to produce a remarkable sight not to miss.

Saturn is also poised to come into the evening skies by the middle of next month (i.e. mid-May).  Its sharp shine can be confused with stars but remember that stars twinkle while planet's light is steady.

Among the constellations, the big horizontal rectangle of Orion with its three stars middle stars lined up close together is seen in the west soon after sunset and is worth catching its view.

The Southern Cross, pointing south and the Big Dipper pointing north are also clearly visible for you to find your directions.

In city skies it can be difficult to make out overhead the shape of Leo (the lion) constellation but with some concentration and clear skies you can make it.  In rural skies with no light pollution, stars are clearly visible and numerous fainter stars become visible and pose their own challenge to identifying the constellations shown. 


Happy viewing....


Dr. Noorali Jiwaji

The Open University of Tanzania

Faculty of Science Technology and Environmental Studies

Lecturer in Physics

Head of Department of Physical Sciences



Sababu za Jose Mourinho kuzuru Angola ni zipi?

maalim seif ziarani Wilaya ya Kaskazini B unguja

0
0
Na Hassan Hamad, OMKR
 Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameweka mawe ya msingi na kupandisha bendera katika matawi na barza sita za CUF ndani ya Jimbo Kitope Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja. 
 Matawi na barza alizoweka mawe ya msingi ni pamoja na Kiombamvua, Mkaratini, Mgambo, Kilombero, Kipandoni na Kiwengwa Cairo. 
Hata hivyo, mkutano wa hadhara uliokuwa ufanyike katika viwanja vya Kipandoni umehairishwa, kwa madai kuwa haukupata kibali kutoka kwa jeshi la polisi.
 Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika barza ya CUF ya WENYE WIVU WAJINYONGE katika eneo la Kitope Mkaratini.
.Vijana wa barza ya HATUDANGANYIKI  ya Kiwengwa Cairo wakimsikiliza Maalim Seif wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika barza hiyo (Picha na OMKR)

DIAMOND PLATNUMZ UK CONCERT TOUR TICKETS NOW ON SALE!!!!!

0
0
ZURII HOUSE OF BEAUTY AND BONGO DEEJAYS PRESENT!!
Londons Rugby 7's After Party, Appearing Live, Bongo Flava recording artist from Tanzania most famous for his song "Number One". Diamond Platnumz will be preforming with his WCB dancers and special guests at the Royal Regency Banquet Hall for one night only.
THE ROYAL REGENCY
501 HIGH STREET NORTH
MANOR PARK 
For Front Row V.I.P Tables and Info Please Contact our Ticket Hotline: 07853482158 or 07421167123
Dont be left out, tickets are running out quickly. We are counting down to the most Epic event of the Year!!
IN SUPPORT OF ALBINO CRUELTY IN TANZANIA. TOGETHER WE SAY: "IMETOSHA"
Follow the link below or clck "Buy Tickets" to get your tickets A.S.A.P


Buy tickets for Diamonds are forever UK live concert

Wizara ya Afya yaridhishwa na viwango TBL

0
0

 Meneja Mdhibiti Viwango wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Conchesta Ngaiza (kulia) akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe wakati wa ziara ya Kiwanda cha Dar es Salaam cha TBL kilichopo Ilala. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usalama na Chakula wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Raymond Wisenge. Wizara ilionesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake.
Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Calvin Martin akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe wakati wa ziara ya Kiwanda cha Dar es Salaam cha TBL kilichopo Ilala. Wizara ilionesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake.
 Mshauri wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Phocus Lasway akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe (kulia) wakati wa ziara ya Kiwanda cha Dar es Salaam cha TBL kilichopo Ilala. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usalama na Chakula wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Raymond Wisenge. Wizara ilionesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake.

BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI

MWISHO WA ZIARA YA SWAHILI BLUES BAND WAFANA VILIVYO- JUMA SETUMBI ANG'ARA

0
0

Mkongwe Dr Mulatu akijituma


Dr Mulatu akikong'ori vigoma vyake

Dr Mulatu na Leo wakishebedue

Ziara ya Swahili Blues Band mjini Addis Ababa ilimalizika rasmi siku ya Jumamosi ya tarehe 11 April 2015 katika klabu mpya na maarufu ya African Jazz Village.

Kama ilivyo kawaida, shoo ilianza rasmi saa tatu na nusu usiku pale Swahili Blues Band ilipopanda jukwaani na kuanza kuporomosha nyimbo zao mfululizo. Waliendelea na midundo hiyo kwa muda wa saa moja na ilipotimia saa nne na nusu ndipo Leo Mkanyia alipowaita stejini mpiga zeze la kihabeshi (krar) maarufu wa Ethiopia anayejulikana kwa jina la Mesele na gwiji mwenyewe wa miondoko ya Ethio Jazz Dr Mulatu Astakte.

Hapo ndipo lile vuguvugu maalumu linalojulikana kama Ethio- Tanzanian Fusion lilipoendelea kushika kasi. Bendi ilipiga nyimbo zao nane mfululizo huku vionjo vya kihabeshi vikiingizwa ndani kupitia kwenye krar, vigoma vidogo na vibraphone vilivyokuwa vikicharazwa kwa umahiri mkubwa na Dr Mulatu Astakte. Nyimbo zilizopigwa zilikuwa ni Aichelelo, Seychelles, Wazazi Wangu, Afrika, Dar es Salaam, Sawa Saware, Haki na Shikandambwe. Shoo hiyo pia ilipambwa vilivyo na wasichana wawili wanenguaji wa Kihabeshi ambao walibamba vizuri kwa kucheza kihabeshi midundo ya kiswahili.


Jioni hiyo pia ilikuwa maalumu kwa wageni waalikwa kutoka balozi mbalimbali ambao walifika kuja kuunga mkono vugu vugu la kutambulisha muziki wa Afrika Mashariki kimataifa. Wageni hao maalumu walijumuisha mawaziri waandamizi wawili kutoka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mabalozi kutoka nchi za Senegal, Ubelgiji, Mexico, Togo, Uturuki, Georgia, Uholanzi na Afrika ya Kusini. Vilevile walihudhuria maofisa waandamizi kutoka ubalozi wa Marekani, Ufaransa na Umoja wa Afrika yaani AU.

Ethio- Tanzanian Fusion iliendelea kuwashikilia vilivyo waalikwa hao hadi saa tano na dakika arobaini na tano pale Leo Mkanyia alipowatambulisha wanamuziki wote walioshiriki katika shoo hiyo kabambe na maalumu kabisa. Mara baada ya Leo kutambulisha wanamuziki, Dr Mulatu Astakte alichukua kipaza sauti na kuwashukuru wote waliohudhuria na kuelezea umuhimu wa vuguvugu hili linalojumuisha muziki wa kweli kutoka Afrika ya Mashariki. Aliendelea kwa kutoa rai kwa wadau wote wa kimataifa kutoa ushirikiano kwa juhudi za pamoja zakuufanya muziki wa Afrika ya Mashariki ufike mbali na mipaka ya nchi hizo kama ilivyo kwa pande nyingine za Afrika kama vile Kusini, Magharibi na Kaskazini. Vile vile alitoa pongezi kwa Swahili Blues Band kwa kuwa na ushupavu wa kuthubutu kupiga muziki usiotharika na utamaduni kutoka sehemu nyingine tofauti na Afrika Mashariki. Aliendelea kuwasisitiza kuwa wako kwenye njia sahihi kwa kupiga muziki wenye mizizi ya kiutamuduni ya Kiswahili yenye ladha na mchanganuo wa kimataifa.

Shoo hiyo maalumu ilimalizika rasmi saa sita kasoro dakika tano kwa tukio la kihistoria pale mpiga tumba na Marimba wa Bendi Juma Setumbi alipompa zawadi ya Marimba Bendi Dr Mulatu Astakte. Juma Setumbi alidai kuwa lengo la kumpa zawadi ya Marimba Dr Mulatu ni kutambua juhudi zake za zaidi ya miaka 50 katika muziki wa ki Ethiopia. Vile vile ni kumshukuru kwa kutoa wazo na kuanzisha Ethio-Tanzanian Fusion pamoja na kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu alioonyesha kwa Bendi ndogo kama hii wakati yeye ni mwanamuziki mkubwa sana wa kimataifa.

Lilikuwa ni tukio kubwa na la kihistoria ukizingatia kuwa Dr Mulatu hajazoea kupokea bali yeye siku zote amekuwa mtu wa kutoa tu. Alimshukuru sana Juma kwa zawadi hiyo na kuahidi kuendeleza ushirikiano huu muhimu sana.

JUST IN: BASI LA PRINCES MUNAA LAPIGA MWELEKA MKOANI DODOMA LEO

0
0
 
 Muda mfupi uliopita, kumetokea ajali ya Basi la Princes Munaa lililokuwa likitokea Jijini Dar es Salaam kwenda Mwanza, katika kijiji cha Mtanana Kibaigwa Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma. Hakuna aliepoteza maisha katika ajali hii, watu kadhaa wamejeruhiwa.

MAALIM SEIF ATINGA KIZIMBANI KUSIKILIZA KESI YA LIPUMBA

0
0
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad leo amehudhuria katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kusikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba na wenzake 30 wa chama hicho.

Maalimu Seif alifika na msafara wake wa magari matatu Mahakamani hapo  majira ya saa nne asubuhi.

Hakimu wa Makakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Cyprian Mkeha amesema washitakiwa hao wanadaiwa kufanya kosa la jinai la kufanya mkusanyiko usio halali kwa mujibu wa sheria za nchi.

Hakimu huyo ametoa dhamana kwa watu wote kutokana na maelezo yao kama masharti ya dhamana yalivyokuwa yakihitajika 

Hakimu huyo, amesema kuwa  kesi inayomkabili Profesa Lipumba na wenzake 30 ni ya kufanya mkusanyiko usio halali kwa mujibu wa sharia za nchi mnamo januari 22 na 27 maeneo ya Temeke jijini Dar es Salaam na upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika.

Jopo la mawakili wa kesi hiyo likiongozwa na Wakili,Job Karario awali walipeleka pingamizi la mashtaka dhidi ya Profesa Lipumba na wenzake 30.

Hakimu  Cyprian aliahirisha kesi hiyo mpaka itakapotajwa tena Mei 6 mwaka huu na washitakiwa wote katika kesi hiyo wamepewa dhamana.

 Akizungumza baada ya kutoka Mahakamani hapo ,Maalimu Seif Sharif Hamad amesema anashukuru wanachama kwa kujitokeza kwa wingi pamoja na kuwatolea washitakiwa dhamana.

Amesema wanachama waendelee kuwa na moyo wa kujitoa katika matatizo kwani wote wako katika safari moja katika chama.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF)Profesa Ibrahim Lipumba akiingia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo jijini Dar es Salaam kwa kutuhumiwa kufanya kukosa la jinai kwa kushawishi wafuasi wa cha hicho kufanya mkusanyiko usio halali.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Maalim Seif Shariff Hamad (mwenye suti ya kijivu)akiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo jijini Dar es Salaam, akisikiliza kesi inayomkabili wa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Liipumba na wenzake 30 wakituhumiwa kufanya mkusanyanyiko usio halali. (Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii).

CHAMA KIPYA CHA SIASA CKUT CHAPATA USAJILI JIJINI DAR LEO.

0
0
 Mwenyekiti  na Muasisi wa Chama cha  Kijamaa na Uzalendo Tanzania (CKUT),Ramadhani  Semtawa  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupata usajili wa muda wa chama hicho uliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa leo jijini Dar es Salaam,Kushoto ni katibu Mkuu wa Chama hicho,Noel  Antapa.
 Mwenyekiti  na Muasisi wa Chama cha  Kijamaa na Uzalendo Tanzania (CKUT),Ramadhani  Semtawa  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupata usajili wa muda wa chama hicho uliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa leo jijini Dar es Salaam,Kushoto ni katibu Mkuu wa Chama hicho,Noel  Antapa.
Mwenyekiti  na Muasisi wa Chama cha  kijamaa na uzalendo Tanzania,Ramadhani  Semtawa  akiwa ameshika katiba ya chama hicho  na Kushoto  ni Katibu Mkuu wa Chama hicho Noel Antapa akiwa katika viwanja va ofisi ya msajili wa vyama vya siasa leo jijini Dar es Salaam.PICHA NA EMMANUEL MASSAKA.

Jipatie Vodacom ZTE kwa Sh 40,000 Tu

Uzinduzi wa Mfuko wa Uchaguzi wa Mkoa wa Mjini.

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  (katikati) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif ALi Iddi (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,Mama Mwanamwema Shein (kushoto) na Mwenyekiti wa Mkoa Mjini kichama Borafya Silima Juma (wa pili kushoto) wakiwa katika uzinduzi wa mfuko wa Maendeleo ya Mkoa wa Mjini sambamba na Chakula cha kuchangia Mfuko huo katika ukumbi wa Salama Bwawani jana.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar (kulia) alipokuwa akitoa nasaha zake wakati wa Chakula cha hisani cha kuchangia  Mfuko wa maendeleo ya Mkoa wa Mjini uliofanyika jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja na kuwajumuisha wafanyabiashara mbali mbali na Viongozi wa CCM wa Mkoa huo.
  Baadhi ya wajumbe wa kamati Maalum ya mfuko wa maendeleo ya Mkoa wa Mjini wakielekezana jambo wa uzinduzi wa Mfuko huo sambamba na Chakula cha hisani cha kuchangia  Mfuko huo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja jana mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.
 Viongozi mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi CCM wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Mfuko wa Uchaguzi wa Mkoa wa Mjini Kichama sambamba na chakula cha kuchangia mfuko huo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja jana. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

TIMU YA UTUMISHI YAENDA MWANZA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MEIMOSI 2015

0
0
 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais-Utumishi Mhe.Celina O.Kombani (Mb) akiwa katika hafla fupi ya kuwaaga wanamichezo wa ofisi yake wanaoelekea katika mashindano ya Meimosi 2015 mkoani Mwanza.
 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais-Utumishi Mhe.Celina O. Kombani (Mb)akiagana na wachezaji  wa Ofisi ya Rais-Utumishi wanaokwenda katika mashindano  ya Meimosi 2015 yatakayofanyika jijini Mwanza.
Kaimu Katibu Mkuu-Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kushoto) akiagana na wachezaji  wa Ofisi ya Rais-Utumishi wanaokwenda kuiwakilisha ofisi katika mashindano  ya Meimosi 2015 yatakayofanyika jijini Mwanza.
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images