Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 799 | 800 | (Page 801) | 802 | 803 | .... | 3285 | newer

  0 0


  Wachezaji wa Yanga wakiwa wameshika zawadi walizopewa na tawi la Facebook lenye makazi yake Buguruni jijini Dar es Salaam, baada ya kukabidhiwa kama shukurani kwa kushika nafasi ya pili kwenye msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam


  Wachezaji wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tawi la Facebook

  Mwenyekiti wa Tawi la Facebok Josephat Sinzobakwilaakiongea na wachezaji na benchi la ufundi la Yanga

  Kocha wa Yanga, Pluijn akikabidhiwa zawadi yake na mlezi wa Tawi la Facebook, Ziota Musisa (kushoto).

  0 0

   Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akifanya ziara ya kutembelea wagonjwa waliojeruhiwa katika vurugu za kisiasa zilizotokea siku ya mkutano wa CUF uliofanyika Makunduchi tarehe 29/03/2015. Baada ya kuwaangalia wagonjwa hao katika mitaa mbali mbali ya Mjini Magharibi ikiwemo mitaa ya Jang'ombe, Muembe Makumbi na Mfenesini, Maalim Seif amesema Chama hicho hakitotoka kwenye mstari na kamwe hakitojitumbukiza kwenye vurugu hizo zilizopangwa kwa malengo ya kukivurugia  malengo yake. (picha na Salmin Said, OMKR),


  0 0

  Jaji mstaafu wa mahakama ya rufaa nchini tanzania mama EUSEBIA MUNUO  ambaye alikuwa ndiye mkufunzi katika mafunzo hayo yaliyoendeshwa leo jijini Dar es salaam
   Rushwa ya ngono pamoja na matumizi mabaya ya madaraka yametajwa kuwa ni moja kati ya matatizo makubwa ambayo yamezidi kuweka mizizi nchini tanzania na kuwaadhiri wasichana wengi huku sheria ikishindwa kuweka wazi adhabu mahususi ili kuwabana wanaohusika katika swala hilo.
  Hayo yamesemwa leo jijini dare s salaam na Jaji mstaafu wa mahakama ya rufaa nchini tanzania mama EUSEBIA MUNUO wakati akiendesha mafunzo maalumu kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam mafunzo yaliyolenga kuzungumzia madhara na jinsi rushwa ya ngono inavyoathiri kizazi kukubwa cha wasichana wa sasa nchini tanzania.
  Wanafunzi mbalimbali kutoka chuo kikuu Dar es salaam waliohudhuria katika mafunzo hayo leo jijini Dar es salaam.
  Amesema kuwa tatizo la ruswa ya ngono limekuwa likiongezeka siku hadi siku nchini kutokana na kutokuwa na sheria mahususi ambayo inawaadhiu moja kwa moja  wahusika katika swala hilo.
    
  Amesema kuwa wasichana wengi wanapokuwa katika harakati za kutafuta ajira katika maofisi mbalimbali wamejikuta wakitumia miili yao kuwashawishi mabosi wao ili waweze kupata ajira jambo ambalo amesema kuwa sio sahihi na wasichana hao wamekuwa wakikosa msaada kuhusu swala hilo.

    Amesema kuwa hata katika maofisi mbalimbali kumekuwa na wasichana ambao hawana vigezi vya kuwa katika maofisi hayo ila wapo tu kwa sababu wanatembea na mabisi wao jambo ambalo limetajwa kuleta madhara makubwa ikiwemo kushusha ufanisi wa kazi pamoja na ofisi husika kwa ujumla.
  Mwanafunzi CATHERIN OLOMY akizungumza na mwandishi wa mtandao huu juu ya mafanikio ya semina hiyo ya siku moja kwao na kwa jamii kwa ujumla
  Baadhi ya wanafunzi ambao wamehuduria mafunzo hayo ya siku moja ambayo yameandaliwa na WILAK kwa kushirikiana na TAWLA mwanafuzni CATHERINE OLIMY ambaye ni mmoja ya washiriki anasema kuwa  mafunzo hayo ni muhimu sana kwa wanafunzi wa sasa hususani wasichana kwa kuwa yatawasaidia kujiamini kujua haki zao kama wanafunzi na watoto wa kike,ikiwa ni pamoja na kujua udhamani wao pindi wanapokutana na swala la rushwa ya ngono.

  0 0

  Kipindi cha mada moto kimeanza rasmi kupitia Channel Ten.Kwa wanaotaka kukiangalia wanaweza kwa kuingia kwenye tovuti ya ww.madamottotvshow.com. kipindi hiki ni live kinarushwa kila jumatau, jumatano na ijumaa saa nne usiku.

  0 0

  Kutoka kushoto ni Reginald Munisi, Mwenyekiti, United Nations Association of Tazania, Mr. Alvaro Rodriguez, Mratibu Mkazi, Umoja wa Mataifa Tanzania, Balozi Dr. Agustine Mahiga, Balozi Mstaafu wa Tazania Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wakiwa katika Maadhimisho ya Miaka 50 Taasisi ya Umoja wa Matifa (UNA) pamoja na maadhimisho ya miaka 70 ya umoja wa Mataifa (UN) yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Reginald Munisi, Mwenyekiti wa UNA Tanzania akitoa maneno ya ufunguzi katika mkutano mkuu wa UNA Tanzania.
  Washiriki katika mkutano mkuu wa UNA Tanzania.

   Washiriki katika picha ya pamoja.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumamosi, Aprili 11, 2015, amekutana na wachezaji nyota wa klabu ya soka la Barcelona ya Hispania katika shughuli iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam. 
  Wachezaji hao wakiongozwa na nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1974 nchini Ujerumani Johann Cruyff pamoja na nyota mwingine wa klabu hiyo na nchi hiyo, Patrick Kluivert wamekaa Ikulu kiasi cha dakika 40 kabla ya kuondoka kwenda Uwanja wa Taifa kwa mchezo wao na nyota wa zamani wa Tanzania. 
  Mheshimiwa Rais Kikwete amewashukuru wachezaji hao kwa kukubali kutembelea Tanzania na kusema kuwa wanakaribishwa tena kuja nchini kwa muda mrefu zaidi.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wachezaji maveterani wa timu ya Barcelona wakati walimpomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
   Mchezaji nyota wa zamani wa Holland  na kocha wa Timu ya veterani ya Barcelona Johann Cruyft akimkabidhi jezi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji maveterani wa timu ya Barcelona walipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam leo. Picha na Fred Maro

  0 0

  Wachezaji wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania wakiongozwa na Patrick Kluivert (aliebeba mtoto) wakiingia uwanjani tayari kwa kukipiga na timu ya Tanzania Veterans katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. hadi mwisho wa mchezo, Barcelona ya Hispania ilishinda bao 2-1.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
  Mchezaji wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania, Patrick Kluivert akifurahia jambo na Mtoto mwenye Ualbino kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Tanzania Veterans uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.
  Mshambuliaji Machacha wa Liverpool na Barcelona enzi hizo, Luis Garcia akionyesha ufundi wake mbele ya wachezaji wa Tanzania Veterans, wakati wa mchezo wao wa kirafiki uliopogwa kwenye uwanja Taifa, Jijini Dar es salaam.  0 0

  Habari zilizotufikia punde zinasema watu kadhaa ambao idadi yao bado haijafahamika wanasemekana wamepoteza maisha baada ya basi la abiria liitwalo Nganga linalofanya safari zake kati ya Iringa na Kilombero kugongana uso kwa  uso na lori aina ya Fuso na kisha magari hayo kuteketea kwa moto  maeneo ya milimani kilomita  kadhaa kutoka Ruaha Mbuyuni kuelekea Morogoro, majira ya saa mbili asubuhi leo. Pichani ni basi hilo la Nganga wakati na bada ya kuteketea kwa moto. Tunaendelea kufuatilia taarifa hizi na tutazileta mara zitapopatikana. 


  0 0

   Kijana Amosi Peter Rwangarya ambaye ni mtanzania mwanafunzi nchini Serbia akiwa anawakaribisha wanafunzi wa Kiserbia (Ulaya Mashariki) kujifunza Kiswahili kwenye ukumbi wa African Museum jijini Belgrade (Serbia).
  Amosi Peter Rwangarya(kulia) na Galina Tudyk (kushoto) ambaye ni Mserbia aliye wahi kukaa East Afrika kama Kenya na Tanzania na anaongea kiswahili na ni mwalimu wa lugha mbalimbali haswa kiingereza na Kiserbia na hapo mbele ni wanafunzi wanaojifunza kiswahili nchini humo.
  Amosi Peter Rwangarya ni mwanafunzi wa Kitanzania nchini  Serbia kwa scholarship ya serikari hizi mbili. Amekuwa nchini Serbia sasa kwa takribani miaka minne akichukua shahada yake  ya kwanza ya uchumi, ambapo katika hii scholarship kuna wanafunzi kutoka nchi takribani 50  za dunia hasa za kiafrika. 
  Yeye amekuwa mmoja ya Watanzania kuchagulia na African Museum nchini humo kufundisha lugha ya kiswahili kwa beginners wa ikiwa ni pamoja na utamaduni wa Waafrika kutambulika duniani na kuwezesha utalii hasa Afrika Mashariki kuwa rahisi kwa watu hao wa Ulaya Mashariki wajapo kutalii.

  0 0

  *Waziri Mkuu aomba Watanzania waiombee nchi yao

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Watanzania waishio ughaibuni hawataweza kupiga kura wakiwa nje ya nchi kwenye uchaguzi wa Oktoba mwaka huu, kwa sababu kuna mambo kadhaa ambayo Serikali inabidi iyatekeleze kabla ya zoezi hilo kufanyika.

  Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumamosi, Aprili 11, 2015) wakati akizungumza na baadhi ya Watanzania waishio Uingereza kwenye makazi ya Balozi wa Tanzania nchini humo, Balozi Peter Kallaghe, yaliyoko Highgate, Kaskazini mwa Jiji la London.

  Akizungumza na Watanzania hao ambao baadhi yao walitoka miji ya Leicester na Manchester, Waziri Mkuu alisema mambo makuu ambayo yanahitaji kuzingatiwa kabla hawajaweza kupiga kura ni pamoja na marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi Na. 1 ya mwaka 1985 pamoja na uandikishwaji wa Watanzania wana-Diaspora kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

  "Najua suala kubwa ambalo mnatamani kulisikia ni hili la Watanzania kuweza kupiga kura kutokea huku mliko. Hili inawezekana lisifanikiwe wakati huu kwa sababu kuna mambo muhimu ya kuzingatia kubwa likiwa ni marekebisho ya sheria na hili zoezi la uandikishaji wapigakura kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura. Ili mwananchi aweze kupiga kura ni lazima awe ameandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura," alisema.

  "Itabidi tuangalie kama mashine za BVR nazo zitapaswa kupelekwa kwenye kila ubalozi ili watu wetu waweze kujiandikisha au itafutwe njia nyingine ya kufanikisha hilo jambo.... lakini watu wa Tume wanaamini kwamba jambo hilo linaweza kufanikiwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2020," aliongeza.

  Waziri Mkuu ambaye aliwapatia nakala zisizopungua 40 za Katiba Inayopendekezwa, alitumia fursa hiyo kuwasisitizia wasome kwa makini Katiba hiyo ili wawe na uelewa mpana na kisha wailinganishe na Katiba ya mwaka 1977 ambayo inatumika hivi sasa ili waweze kubaini kama kweli haina kitu kama ambavyo watu wengine wanadai.

  "Moja ya changamoto zinazotukabili huko nyumbani ni mjadala kuhusu Katiba Inayopendekezwa,wako watu wanaosema kwamba hakuna kitu kipya kabisa kwenye Katiba Inayopendekezwa, lakini mimi nasema hayo ni mawazo yao binafsi," alisema.

  Akifafanua kuhusu Katiba hiyo, Waziri Mkuu alisema: "Mimi nilikuwa sehemu ya Bunge Maalum la Katiba, ni kweli tulibadili baadhi ya vipengele lakini kwa nia ya kuiboresha. Ninawasihi kila mmoja wenu aisome na kuangalia kama kweli hamna kitu au kuna kitu kipya ikilinganishwa na Katiba inayotumika hivi sasa. Angalieni na pimeni, je kuna kitu kimeboreshwa au la?"

  Aliwasihi waendelee kuiombea nchi ya Tanzania ili iendelee kuwa na amani na utulivu na hasa katika kipindi hiki ambacho inakabiliwa na uchaguzi wa madiwani, wabunge na Rais. "Ninawasihi muendelee kuiombea nchi yetu ili ipate viongozi wazuri ambao watajali maslahi ya wengi," aliongeza.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAPILI, APRILI 12, 2015.

  0 0

  Timu ya Tanzania, FC Kilimanjaro ambayo ni mabingwa wa soka la Afrika nchini Sweden imepata ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya watani wao wa jadi Kenya kwenye mechi maalum ya kirafiki ya Amani na Upendo iliyofanyika jijini Stockholm jana tarehe 11 Aprili, 2015

  Mechi hiyo iliandaliwa kwa pamoja na Balozi za Kenya na Tanzania nchini Sweden kwa kushirikiana na wanadiaspora wa nchi hizo kwa madhumuni ya kuonyesha mshikamano na kuziombea nchi zetu amani na upendo kufuatia matukio ya kigaidi yaliyotokea hivi karibuni nchini Kenya.  0 0


  Kambi Mbwana, mwandishi wa kitabu hicho na blogger wa www.handenikwetu.blogspot.com

  0 0

  Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa akiwania mpira wa juu na beki wa Timu ya Mbeya City, Christian Sembuli wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Yanga imeshinda Bao 3 - 1. Picha na Othman Michuzi.
  Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva akiwatoka Mabeki wa Timu ya Mbeya City wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Yanga imeshinda Bao 3 - 1. 
  Kiungo Mchezeshaji wa timu ya Yanga, Haroun Niyonzima akiangalia kwa kupeleka mpira wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Yanga imeshinda Bao 3 - 1.
  Kipa wa Mbeya City, Hanington Kalyesubula akiangalia mpira wavuni huku washabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao.
  Wachezaji wa timu ya Yanga wakisangilia ushindi ushindi na washabiki wao.


  0 0

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dk Shaban Mwinjaka akikata utepe kuzindua safari hiyo
    Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dk Shaban Mwinjaka akiondoa treni kwa kupunga bendera
  Uongozi wa Kampuni  ya Reli Tanzania  –TRL unachukua  fursa hii kuwataarifu wateja wetu wote na Watanzania kwa ujumla na hasa ukanda  wa ziwa kuwa hatimaye ile huduma iliyokuwa ikisubiriwa leo Aprili 12 , 2015 inaelekea Mwanza ‘Rock City’ Ziwa Victoria!

  Safari hii ni ya pili kwa vile ya uzinduzi iliyofanyika Aprili Mosi , 2015 ilielekea Kigoma Ziwa Tanganyika baada ya kuzinduliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dk Shaban Mwinjaka. Aidhaa taarifa zinaeleza kuwa  treni hiyo ilipokelewa kwa furaha na bashasha sehemu zote ilimopita wakati wa kwenda Kigoma na kurudi Dar es Salaam.

  Tayari kuna baadhi ya wakazi wa miji njiani wameutaka Uongozi wa TRL kuiruhusu treni hiyo ya Deluxe isimame katika vituo zaidi vya njiani zaidi ya vile rasmi 14 na vile vitatu vya ufundi.

  Hata hivyo msharti ya uendeshaji wa huduma hii ya Deluxe unaifunga kama ilivyotolewa na Sumtra unaifunga TRL kuchukua uamuzi wa upande mmoja kwa vile uamuzi wowote hautakiwi kuathiri muda wa safari na viwango vya huduma ambazo msafiri wa Deluxe amehakikishiwa kimkataba.

  Aidha safari za deluxe zitakuwa wiki mara moja siku za Jumapili itaondoka Stesheni ya Dar es Salaam saa 2 usiku ikiwa na mabehewa 15, Daraja la kawaida 10 (abiria 80 kila moja) daraja la pili la kukaa 3 (kila moja abiria 60) na daraja la pili kulala 2( kila moja watu 36). Itasimama katika vituo 17 ambavyo ni pamoja na Morogoro, Kilosa, Dodoma, Makutopora, Saranda, Manyoni, Aghondi, Itigi, Tabora, Urambo, Kaliua, Uvinza, Kigoma. Vituo vingine ni Isaka, Shinyanga, Malampaka na Mwanza. Wiki moja ikienda Kigoma wiki inayofuatia itaenda Mwanza

  Kwa wasafiri wa Dodoma na Tabora hawa watatumia huo usafiri wakati wote isipokuwa wale  wanaoishia Kigoma  na Mwanza. Siku za usoni wakati mabehewa mengine ya deluxe yatapatikana safari zitakuwa kila wiki kwenda Kigoma na Mwanza.


  NAULI ZA TRENI YA DELUXE  KWA MUHTASARI  KUTOKA  DAR KWENDA KIGOMA/MWANZA NIA KAMA IFUATAVYO:

  Dar -Dodoma  daraja la kawaida  TZS 18,500, Daraja 2 Kukaa TZS 24, 700 Kulala: 41,200

  Dar -Tabora kawaida 25,400, Daraja la 2 Kukaa 33,900 Kulala 56,500;

  Dar - Kigoma kawaida 35,700, Daraja la 2 Kukaa 47,600 na Kulala 79,400 na

  Dar - Mwanza ;kawaida 35,000, Daraja la 2 kukaa 46,700 na Kulala 77,800.


  Aidha pia tunapenda kutoa wito wa ushirikiano wa wananchi na   wadau wote kutunza vitendea kazi na kwamba kila mmoja awe mlinzi wa mwenziwe. Tujiepushe na vitendo vya makusudi kuharibu mabehewa haya mazuri ndani na nje . Kuna msemo : KITUNZE KIDUMU’! Tukitunza vitendea kazi  vitaweza kutoa huduma kwa muda mrefu na hivyo kuongeza tija na kupunguza matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi. 


  Imetolewa na Afisi ya 
  Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya


   Mkurugenzi Mtendaji 

  0 0

  Abiria zaidi ya 50 wamenusurika leo bada ya basi walilokuwa wakisafiria liitwalo Burudani kugongana uso kwa uso na Lori la tenki la mafuta maeneo ya Soni mkoani Tanga. Mashuhuda wamesema hii ajali imetokea baada ya Lori la mafuta kukatika breki na kuvaana na basi hilo uso kwa uso. Habari zinasema hakuna maafa yaliyoripotiwa hadi sasa ila watu kadhaa wamepata majeraha na kukimbizwa hospitali. 
  Hii ni ajali ya pili ya basi la abiria kutokea leo, ikufuatiwa na ile ya asubuhi maeneo ya Msimba, Mikumi, jirani na milima ya Udzungwa ambapo imeripotiwa kwamba watu 18 wamepoteza maisha hapo hapo na wengine 10 kujeruhiwa baada ya lori aina ya Fuso kugongana uso kwa uso na basi la abiria na yote mawili kushika moto hapo hapo.

  0 0

   Bunnik, the Netherlands, 13 March 2015 – BAM International has been awarded a €37 million design and construct contract for the rehabilitation and extension of Kilimanjaro International Airport (KIA) in Tanzania, which is situated between Moshi and Arusha in northern Tanzania. 

  BAM expects to complete the works for Kilimanjaro Airports Development Company (KADCO) in 2017.

  The scope of work comprises the refurbishment of the terminal building (built in 1971), the construction of a new parallel taxiway, the extension of the existing apron and taxiways, including repairs on the runway, as well as the drainage and sewage works. Furthermore BAM will install new airfield ground lighting and floodlights along the apron.

  Funding was partly granted by the Dutch fund ORIO for the development and implementation of this project. The remaining part is guaranteed by commercial financing arranged by the Government of Tanzania.

  Kilimanjaro International Airport is one of the four international airports in Tanzania and is the second largest airport after Julius Nyerere International Airport in Dar es Salaam for which BAM has completed two rehabilitation projects already and is currently constructing the new Terminal 3 building.  0 0


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Kikombe Mwenyekiti wa Jimbo la Uzini CCM Ali Shaaban wakati hafla ya Sherehe ya kukabidhi vifaa vya Michezo kwa Timu 40 za Jimbo la Uzini vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo Mohamed Raza katika uwanja wa Mpira Bambi leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Mahmoud Ame seti ya jezi wakati hafla ya Sherehe ya kukabidhi vifaa vya Michezo kwa Timu 40 za Jimbo la Uzini vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohamed Raza (kushoto) katika uwanja wa Mpira Bambi leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Kati Unguja Vuai Mwinyi Seti za jezi na vifaa vyengine kwa Timu za Wilaya yake wakati hafla ya Sherehe ya kukabidhi vifaa vya Michezo kwa Timu 40 za Jimbo la Uzini vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo Mohamed Raza katika uwanja wa mpira Bambi leo.


  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Watanzania waishio Uingereza kwenye makazi ya Balozi wa Tanzania nchini humo, Aprili 11, 2015. Kulia kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Peter Kallaghe.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Peter Kallaghe na Binti wa Balozi huyo, Rebecca (katikati) kwenye makazi ya Balozi huyo eneo la Highgate, Londondoni Aprili 11, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Watanzania waishio Uingereza kwenye makazi ya Balozi wa Tanzania nchini humo, Aprili 11, 2015. Kulia kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Peter Kallaghe.


  0 0

  Na Woinde Shizza wa Globu ya Jamii, Arusha
  Serikali imetakiwa kutazama upya uwezekano wa kubadili sheria inayomnyima haki ya kuendelea na masomo mwanafunzi wa kike pindi anapopata ujauzito akiwa shuleni.

  Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Afisa elimu taaluma ,mkoa wa Arusha,Kabesi katundu Kabeja wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa umoja wa wakuu wa shule za msingi kutoka nchi ya Kenya uliofanyika katika hotel ya Leons iliyopo Sakina kwa Idi ,jijini hapa,ambapo walimu zaidi ya 1000 kutoka nchini humo walikutana.

  Alisema hatua ya sasa ya kumfukuza shule mwanafunzi wa kike mwenye ujauzito ni kumnyanyapaa na kumkosesha fursa ya kupata elimu,hivyo alisema ni vema serikali katazama upya sheria hiyo kandamizi.

  Aliitaka serikali kuiga nchi jirani ya kenya ambayo sheria yao inaruhusu msichana huyo kuendelea na masomo pindi anapokuwa amejifungua.

  ‘’Hapa kwetu sheria zinakataza mwanafunzi mwenye ujauzito kuendelea na masomo lakini serikali tumeiomba serikali ibadili sheria hiyo ili kutoa fursa kwa mwanafunzi mwenye ujauzito kuendelea na masomo pindi anapojifungua,alisema Kabeja.

  Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja kutoka nchini Kenya ,Wintred Mbinyasila ,alisema mkutano huo ambao umekuwa ukifanyika kila mwaka unalenga kubadilishana mawazo na mwaka huu lengo ni kujifunza teknolojia ya kufundishia.

  Hata hivyo alisema nchi ya Kenya imepiga hatua kubwa suala la elimu kwa mtoto wa kike baada ya kuruhusu mwanafunzi huyo pindi anapokuwa na ujauzito kuendelea na masomo baada ya kujifungua.

  ‘’Serikali huchukua hatua kali kwa mtu mzima aliyempa ujauzito mtoto wa kike ila kama alipata ujauzito kutoka kwa mwanafunzi mwenzake ,sheria inaruhusu kuendelea na masomo kwa masharti ya kutoa matunzo pindi akifikia umri wa mtu mzima’’alisema

  Naye mjumbe wa shirikisho la walimu wakuu wa nchi za Afrika mashariki ,Anjelina Kitigwa alisema mkutano huo unasaidia sana kubadilishana uzoefu na kujadili changamoto zilizopo hali itakayosaidia kuinua elimu katika nchi za afrika mashariki.

older | 1 | .... | 799 | 800 | (Page 801) | 802 | 803 | .... | 3285 | newer