Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

Rais Mstaafu Mkapa atoa elimu ya uchumi kwa Mabalozi, maofisa na wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje

$
0
0
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb) akimpokea Rais wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin William Mkapa mara baada ya kuwasili Mwalimu Nyerere kwa ajili ya semina hiyo. 

 Rais Mstaafu Mkapa akiteta jambo na Mhe. Membe wakati wa semina hiyo ambapo alizungumzia changamoto za ushirikiano wa kiuchumi na diplomasia nchini Tanzania, na nje ya nchi na Jumuiya za Kimataifa. Andiko la mada hii litapatikana baada ya muda mfupi kwenye tovuti ya Wizara.

 Mabalozi, Maofisa na Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Walimu na Wanachuo cha Diplomasia wakimsikiliza kwa makini Mhe. Benjamin W. Mkapa.
 Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akitoa mada katika semina ya masuala ya diplomasia ya kiuchumi kwa Mabalozi, Maofisa na Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (hawapo pichani). Semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 9 Aprili 2015.


 Mabalozi, Maofisa na Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Walimu na Wanachuo cha Diplomasia wakimsikiliza kwa makini Mhe. Benjamin W. Mkapa.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma wa Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga akiuliza swali kufuatia mada iliyotolewa na Rais Mstaafu Mhe. Mkapa katika hiyo semina hiyo.

KUMBUKUMBU

$
0
0
MAREHEMU BERNARD THOMAS NDERUMAKI

Ni miaka miwili imepita tangu mungu alipokuchukua mnamo tarehe 10 Aprili, 2013. Si rahisi kumpata mbadala wako, kwani ulikuwa Mume, Baba, Babu, Mwalimu, Rafiki na zaidi ya yote mtu mwenye upendo wa kweli kwa jamii. Kumbukumbu zako hazitakaa zitutoke kirahisi, na tutakua tukikukumbuka milele. Pumzika kwa amani.

Misa ya kumbukumbu itafanyika Parokia ya St. Thomas More, Mbezi Beach siku ya Jumapili tarehe 12 Aprili, kuanzia saa 2.30 asubuhi.

Wote mnakaribishwa.

Mfumo mpya wa upokeaji wa maombi ya kazi kwa njia ya mtandao kuzinduliwa hivi karibuni.

$
0
0
Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa umma inatarajia kuzindua mfumo mpya wa utumaji na upokeaji wa maombi ya kazi kwa njia ya mtandao kupitia “Recruitment portal” hivi karibuni baada ya hatua za majaribio ya mfumo huo kuonyesha mafanikio.
Sababu za kuanzisha mfumo huu mpya zinalenga kuboresha utendaji kazi wa taasisi katika kufikisha huduma kwa wateja, kuongeza ufanisi katika mchakato wa ajira, Kupunguza muda wa mchakato wa Ajira ili kukidhi mahitaji ya wadau, kuwafikia waombaji wa nafasi za kazi wengi zaidi, kudhibiti udanganyifu wa sifa toka kwa waombaji wa fursa za Ajira kwa kurahisisha ukaguzi na uhakiki wa taarifa za waombaji  kazi kwa kuunganishwa na mifumo ya taasisi mbalimbali lakini pia kukidhi maelekezo ya Sera mbalimbali za utumishi wa umma pamoja na dira ya Taifa ya mwaka 2025 kuhusiana na umuhimu wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika kutimiza malengo ya Taifa.

Hadi sasa Sekretarieti ya ajira imefanya majaribio ya kupokea maombi ya kazi kwa kutumia mfumo wa “Recruitment Portal” kwa matangazo ya kazi matano ambayo yaliyowahusu waajiri mbalimbali serikalini na muitikio umeonekana kuwa mzuri.

Matangazo hayo yalihusu Wakala wa serikali mtandao lililotolewa tarehe 22 Aprili, 2014 ambapo kati ya nafasi 12 zilizotangazwa idadi ya maombi yaliyopokelewa yalikuwa 1,158, Tangazo la nafasi za Mkemia mkuu wa Serikali lililotolewa tarehe 4 Desemba, 2014 lenye nafasi 11 jumla ya maombi ya kazi 119 yalipokelewa kwa njia ya mtandao.

Matangazo mengine ni ya  Mamlaka ya Hali ya hewa la tarehe 4 Desemba, 2014 lililokuwa na nafasi  moja na idadi ya maombi ya kazi matatu yaliyopokelewa, tangazo la tarehe 16 Januari, 2015 la Wizara ya Ardhi lililokuwa na nafasi 51 ambalo jumla ya maombi ya kazi 738 yaliwasilishwa na tangazo la mwisho lilitolewa tarehe 10 Machi, 2015 kwa niaba ya taasisi mbalimbali Serikalini jumla ya maombi ya kazi 2,567 yalipokelewa kutumia mfumo huu. Idadi hii inaonyesha kuwa watu wengi wameanza kuhamasika na matumizi ya mfumo huu.

Taratibu za uzinduzi rasmi wa mfumo huu inatarajiwa kufanyika hivi karibuni ambapo sekretarieti ya ajira inatarajia kupunguza muda wa uendeshaji wa  mchakato wa ajira kwa asilimia 34%. Aidha mfumo pia utapunguza changamoto kadhaa zikiwemo baadhi ya barua kutofika kwa wakati au kupotea kwa kutumia njia ya posta, Mrundikano wa barua na nyaraka nyingine zinazohusiana na maombi ya kazi  kutokana na matumizi ya karatasi, Barua za vibali vya ajira kuwasilishwa wakati vimechelewa na kusababisha mchakato kuchelewa na gharama inayotokana na uendeshaji wa mchakato mzima wa ajira kuwa juu.

Pia mfumo huu utakuwa rafiki na rahisi kwa watumiaji kwa kuwa wataweza kutumia simu zao za kiganjani kupata taarifa za mchakato wa ajira kila wakati kwa kupiga *152*00#

Tunatoa rai na kusisitiza kuwa waombaji kazi na wale wanaotarajia kuingia katika soko la ajira wajisajili katika mfumo huu kwa kufungua http://portal.ajira.go.tz ili kuingiza taarifa zao za kitaaluma, wasifu binafsi (CV) pamoja na vyeti.

Matarajio ya Sekretarieti ya ajira ni kuona kuwa mara baada ya mfumo huu kuzinduliwa rasmi utaongeza ufanisi, ubora, uwazi na uwajibikaji wa huduma zinazotolewa, kupunguza muda unaotumika sasa wa kuendesha mchakato wa ajira, Gharama za uendeshaji zitapungua kwa kiasi kikubwa na mfumo utawafikia waombaji wa fursa za kazi wengi zaidi na kwa haraka.

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwasisitiza wananchi hususani waombaji kazi kuwa inaendelea na uimarishaji wa mfumo mpya wa kutuma maombi ya kazi kwa njia ya mtandao (recruitmemnt portal) ili kuondoa baadhi ya changamoto zilizojitokeza baada ya majaribio kabla ya uzinduzi wake na tunasisitiza na kuhimiza waombaji kazi pamoja na wanafunzi wanaotarajia kumaliza vyuo waendelee kujisajili katika mfumo huo mpya.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma. 

Mambo ya Sister Fay

Sheikh Maxamed Cali Mowllid

DIRA YA DUNIA NA BBC SWAHILI LEO

ziara ya kikazi ya profesa mark mwandosya zanzibar

$
0
0
Kwa mwaliko wa Waziri wa Ardhi, Makaazi,Maji na Nishati wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Mheshimiwa Ramadhan Abdallah Shaaban, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Mark Mwandosya ametembeleaZanzibar kwa ziara ya kikazi. Pamoja na mambo mengine,Waziri Mwandosya amefungua rasmi Mradi wa maji wa Sebleni-Muungano-Sogea,SEMUSO.
 Tanki la maji la Mradi wa Maji wa SEMUSO lililo Kibandamaiti,Zanzibai,Mradi uliozinduliwa na Waziri Mwandosya.
Waziri Mwandosya amepata nafasi ya kuhudhuria na kuhutubia mkutano wa wanachama wa CCM Wilaya ya Amani,mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa CCM Mkoa wa Mjini. Kulia kwa Waziri Mwandosya ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini, Ndugu Borafia Silima Juma.Kushoto kwa Waziri Mwandosya ni Ndugu Abdi Ali Mzee,Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Amani.
 Waziri Mwandosya akifungua kisima cha maji cha Mradi wa SEMUSO.Nyuma yake mwenye mawani ni Mheshimiwa Mussa Mussa Mbunge wa Amani.
Baada ya kufungulia bomba(mfereji) la maji ya Mradi wa SEMUSO,Kibandamaiti,Zanzibar,Waziri Mwandosya amtwisha ndoo ya maji Ndugu Ali Magoha, Mjumbe wa Kamati ya Mradi wa SEMUSO, kuashiria kuyafikisha maji kwa watumiaji.Nyuma ya Waziri Mwandosya kutoka kushoto ni ;Mheshimiwa Muhammad Seif Khatib,Mbunge wa Uzini;Mheshimiwa Ramadhan Abdallah Shaaban,Waziri wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishsti wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;na Mheshimiwa Mussa Hassan Mussa,Mbunge wa Amani.

TANZANIA YATIA FORA KATIKA MAONESHO YA UTAMADUNI NA UTALII CANADA

$
0
0
Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Canada kwa ushirikiano na The Canadian Comprehensive Auditing Foundation - La Fondation Canadienne Pour la Verification Integree (CCAF - FCVI Inc.), kwa pamoja wameandaa hafla ya kutangaza vivutio vya utalii vya nchi za Tanzania, Senegal na Ghana. 
 Hafla hiyo iliyofanyika katika Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Canada pia imedhaminiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Canada. 
 Katika hafla hiyo ambayo iliambatana na utoaji wa mada juu ya utamaduni na utalii, Tanzania iliwakilishwa na Bi. Ndyanao Mgweno na Bwana Andrew Kellei ambao wanatoka katika Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Tanzania. 
Maafisa hao wako nchini Canada kwa mafunzo ya Ukaguzi wa ufanisi (performance Audit) ambayo yanatolewa na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Canada. Shughuli za kutangaza utamaduni wa Utalii wa Tanzania ilisimamiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Canada ambapo Mheshimiwa Balozi wetu huko Canada Mhe. Jack Zoka aliwakilishwa na Kaimu wa Kitengo cha Utalii na Mwambata wa Fedha wa Ubalozi huo Ndg. Richard Masalu. 
 Banda la Tanzania limetia fora kwa vielelezo na vivutio vya utalii kati ya mabanda mengine kama inavyoonekana katika picha.
Kutoka kulia  ni Bi. Ndyanao Mgweno kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali Tanzania akiwa amebeba mtoto wake ambaye ni mualikwa katika shughuli hiyo, katika ni Ndg. Richard Masalu aliyemwakiliswa Balozi wetu nchini Canada, akifuatiwa na Ndg. Andrew Kelei ambaye pia anatoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania. 


UVUVI ENDELEVU UTAWASAIDIA WAVUVI KUONDOKANA NA UMASKINI - BALOZI MANONGI

$
0
0
Na Mwandishi Maalum, New York 
 Tanzania, kupitia Mwakilishi wake wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, imeelezea kuridhishwa kwake na namna ambavyo Mashirika ya Kimataifa naTaasisi binafsi zinavyoshirikiana na kwa karibu na serikali na taasisi zake kuimarisha sekta ya uvuvi. 
Ushirikiano huo umeifanya sekta ya uvuvi nchini kuwa wenye tija na hivyo kuchangia katika ongezeko la kupato na kuwaondoa katika umaskini jamii ya watanzania ambao maisha yao ya kila siku yanategemea sana uvuvi, na pia kuimarisha utuzaji wa mazingira ya pwani na viumbe hai. 
Balozi Tuvako Manongi ameyasema hayo wakati wa mkutano wa pembezoni ( side event) uliokuwa umeandaliwa na Mpango wa Chakula Dunia ( FAO). Mkutano huo umefanyika sambamba na mkutano usio rasmi ambapo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, wakutana ana kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya bahari na uwiano wake katika utekelezaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu baada ya 2015. 
Balozi Manongi alikuwa mmoja wa wazungumzaji katika mkutano huo ambapo majadiliano yalilenga zaidi katika suala zima la uwezeshwaji wa wataalamu wa sekta ya uvuvi na wavuvi wadogo na wakati kwa kuwapatia mbinu na maarifa ya kisasa ya uvuvi endelevu na unaozigatia utuzaji wa mazingira ya bahari na viumbe hai. 
Katika mchango wake, Balozi ameeleza kuwa uchumi na ustawi wa wavuvi wengi wanaoishi pembezoni mwa bahari (pwani) nchini tanzania unategemea sana shughuli za uvuvi na kutoka na ukweli huo, Serikali ya Tanzania, licha ya kukaribisha wabia katika kuiendeleza sekta ya uvivu pia inawashukuru wale wote ambao hadi sasa wametoa mchango wao wa hali na mali katika eneo hilo. Akaongeza kuwa mafunzo na utaalamu ambao wadau hao wamekuwa wakiwapatia wataalam wa kitanzania kwa kuwashirikisha pia wavuvi ambao ndio wahusika wakuu, umesaidia sana katika kuwainua kiuchumi lakini pia kuwapatia mbinu endelevu za uvuvi na utunzaji wa mazingira. 
Wadau ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kusaidia maendeleo endelevu ya sekta ya Uvuvi ikiwamo misaada ya kiufundi ni FAO na EAF- Nansen Project ya Norway. Tanzania ni kati ya nchi 32 ambazo zinashirikiana kwa karibu na EAF –Nansen Project katika miradi mbalimbali inayohusu uwezeshwaji wa wavuvi wadogo na wakati. 
Aidha Tanzania ni kati ya nchi 10 za mwanzo zilizochaguliwa kutekeleza mpango huo. Amesema Balozi Manongi, uvuvi endelevu na matumizi salama ya Bahari ni moja ya ajenda za Malengo Mpya ya Maendeleo Endelevu baada ya 2015 (SDGs). 
 Ajenda ambayo kwayo inasisitiza usimamizi endelevu na ulinzi wa bahari na mazingira ya pwani na viumbe hai ili kuepusha athari mbalibmali. Vile vile ajenda hiyo ambayo ni namba 14 inasisitiza pia uwepo kwa kanuni bora zinazosimamia uvuvi ikiwa ni pamoja na kudhibiti uvuvi wa kupita kiasi na uvuvi haramu, na utoaji wa huduma za kisasa kwa wavuvi wadogo na fursa za masoko. 
 Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzani katika Umoja wa Mataifa ameeleza zaidi kwamba, zao la samaki pamoja na kuwa kuchanzo cha kipato kwa watanzania wengine na taifa kwa ujumla, lakini pia samaki wanachangia katika kuwapatia lishe bora watanzania na kwa sababu hiyo matumizi endelevu ya mazao ya bahari na bahari ni jambo muhimu sana. 
Katika majadiliano hayo, Dr. Gabriella Bianchi ambaye ni mtaalamu wa masuala ya utafiti wa samaki kutoka ofisi za FAO yeye katika mchango wake, ameelezea baadhi ya mambo ambayo wanatarajia kuyafanya katika kuzisaidia nchi za Afrika Mashariki Tanzania ikiwamo na kwingineko Afrika katika masuala ya usimamizi, mafunzo na utaalamu zaidi kwenye masuala ya samaki na bahari kwa ujumla. 
 Akasema mabadiliko ya tabia nchi, shughuli za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi, na uchafuzi wa bahari ni baadhi ya changamoto ambazo wataalamu na watafiri wa masuala ya bahari na viumbe hai wa baharini kuamua kupanua wigo wa kazi zao za utafiti ikiwa ni pamoja na mafunzo na uwezeshaji. 
Naye Dr. Alf Hakon Hoel ambaye ni mkurugenzi wa masuala ya utafiti, amesema Norway inakamilisha ujenzi wa meli mpya na ya kisasa ya masuala ya utafiti inayotarajia kuanza shughuli zake mwaka 2016. 
Kwa mujibu wa Dr. Hoel meli hiyo itakuwa na vyumba vya kufundishia, maabara za picha na maabara ya tabia nchi
 Wavuvi wakirejea pwani baada ya shughuli ya kuvua samaki. Inaelezwa kwamba wavuvi wadogo kama hawa wakiwezeshwa   siyo tu wanajiongezea kipato chao lakini pia  inawasidia  katika utunzaji wa mazingira ya  bahari .
 Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi akizungumza wakati wa mkutano wapembezoni kuhusu masuala ya uvuvi endelevu, katika mchango wake, Balozi ameeleza  kuridhwa  kwa Tanzania namna ambavyo wadau mbalimbali wamekuji wakijitokeza kusaidia sekta ya uvuvi na wavuvi nchini Tanzania
 Balozi Manongi akibadilishna  mawazo na Dr. Alf Hakon Hoel ambaye ni mtaalamu wa masuala ya  utaifiti na ambaye alieleza kwamba Norway iko katika maandalizi ya mwisho ya kukamilisha meli mpya  na ya kisasa zaidi ya utafiti itakayoanza kazi mwakani.
 Hapa Balozi  akibadilishana mawazo na Dr. Gabriella Bianchi ambaye pia ni  mtaalamu wa masuala ya  utafiti wa samaki,  Dr   Gabriella na Dr, Hoel wamefanya kazi kwa karibu sana na wataalamu wa Tanzania katika kuendeleza sekta ya  uvuvi.
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo wa pembezoni

Rais ateua Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma, Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Biashara ya Fedha Haramu.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Kissiok Ole Mbille Lukumay kuwa Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma.

Aidha, Rais Kikwete amemteua Bwana Onesmo Hamis Makombe kuwa Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Biashara ya Fedha Haramu.

Taarifa iliyotolewa Alhamisi, mjini Dar es Salaan na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa maofisa hao wawili ulianza Ijumaa ya Machi 27, 2015.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Lukumay ambaye ana diploma in Materials Management na niCertified Supplies Professional na pia ana MBA (Procurement and Logistics) alikuwa Ofisa Ugavi Mkuu na Kaimu Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma.

Naye Bwana Makombe kabla ya uteuzi wake alikuwa Kaimu Kamishna, Kitengo cha Kudhibiti Biashara ya Fedha Haramu. Kielimu, Bwana Makombe ana shahada za B.Com, CPA na MBA (Finance and Human Resources Management).


Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu – Dar es Salaam.


10 Aprili,2015

Zanzibar International Film Festival mourn Garissa attack victims

$
0
0


As Chair of the Zanzibar International Film Festival I would like to convey our heartfelt condolences and Pole to the people and relatives of those directly affected by the shocking massacre in North Kenya. 
ZIFF stands together with the people of Kenya and condemn this heinous attack on the peace loving neighbours and East African Community partners. 
As an arts organisation our duty has always been to promote enduring peace and exchange between cultures and we have gained enormously from our communion with filmmakers from Kenya. 
ZIFF would not be what it is if it had not been for the support and belief that the people and government of Kenya has in our organization and our role in the region. 
We therefore pledge to redouble our efforts at working closely with the people of Kenya to pursue a better future for all the people of the region. 
Through film we shall continue to educate our populations to understand and have respect for freedom, tolerance, human rights, responsibility and accountability. 

 Poleni sana Ndugu zetu. 
 Mahmoud Thabit Kombo (MP) 
Chair ZIFF

Maalim seif azindua msikiti wa Ijumaa MASJIDIL AQSAA katika kijiji cha Kiboje Mkwajuni, Zanzibar

$
0
0
Na Hassan Hamad (OMKR) 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amewasisitiza waislamu nchini kuachana na tabia ya kugombania misikiti, kwani haisaidii kuendeleza dini hiyo. 
Amesema misikiti ni nyumba za Mwenyezi Mungu, hivyo hakuna sababu kwa waislamu kulumbana kwa sababu za kugombea uongozi au kutokana na tofauti ya kimadhehebu. 
Maalim Seif ametoa nasaha hizo wakati akifungua msikiti wa Ijumaa MASJIDIL AQSAA katika kijiji cha Kiboje Mkwajuni, Wilaya ya Kati Unguja. 
Amesema Uislamu ni dini yenye nidhamu kamili, na kuwataka waumini wa dini hiyo kufuata nidhamu hizo katika kuendesha mambo yao bila ya kukaribisha malumbano na mifarakano baina yao. 
Amewahimiza waislamu wa eneo hilo kuuimarisha na kuuendeleza msikiti huo kwa kuendeleza harakati za darsa, sambamba na kuwaandalia watoto muda wa kutosha kuweza kuhudhuria katika darsa hizo ili kuwajenga kimaadili. 
Amesema madrasa zina mchango wa kipekee katika kuwaandaa watoto na kuwakuza kuwa raia wema walioleleka katika maadili ya Kiislamu, na kwamba waislamu bado wana jukumu la kuzianzisha madrasa kwa wingi na kuhakikisha kuwa watoto wanapita katika darsa hizo kupata malezi sahihi. 
Amefahamisha kuwa hivi sasa Zanzibar inahitaji malezi mazuri kwa watoto na vijana kuliko wakati mwengine wowote, kutokana na matishio makubwa yanayojitokeza na kuvurugika kwa maadili mema. 
 Amewakumbusha waislamu kuchangia harakati za dini hiyo kwa kujenga na kuimarisha misikiti na madrasa, kwani kila mmoja ana wajibu wa kutoa mchango wake katika kuziendeleza nyumba hizo za Mwenyezi Mungu. 
Aidha Maalim Seif amewakumbusha waislamu kuendeleza umoja, maelewano, na mshikamano miongoni mwao, na kujiepusha na chuki miongoni mwa waumini wa dini hiyo na dini nyengine. 
Amesema serikali imefanya juhudi kubwa kuiwezesha jamii kuondokana na hasama, chuki na kudharauliana na badala yake kujenga mazingira ya umoja, mshikamano na maelewano, mambo ambayo yanapaswa kuungwa mkono kwa vitendo. 
Katika hatua nyengine Maalim Seif ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwa waangalifu katika kuwachagulia vyuo vijana wao, ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza ikiwa ni pamoja na kuporomoka kwa maadili . 
Amesema baadhi ya vyuo hasa vilivyoko nje ya nchi havina misingi mizuri ya malezi, na kwamba bila ya kuwa waangalifu jamii inaweza kupoteza wengi ambao hatimaye wanaweza kujitumbukiza katika vitendo viovu. 
“Chagueni vyuo vitakavyo wanufaisha vijana, sio kijana kwa sababu anakwenda kusoma nje ya nchi umkubalie tu, wazazi na walezi ni lazima mufuatilie kujua uhakika wa vyuo hivyo” alisisitiza. 
Akizungumza kabla ya hotuba ya Ijumaa, Sheikh Thabit Noman Jombo kutoka ofisi ya Mufti wa Zanzibar amewahimiza waislamu wa eneo hilo kuutumia msikiti huo kama sehemu ya kutolea taaluma. 
Amesema Zanzibar ilikuwa kitovu cha elimu katika nchi za Afrika Mashariki, na hakuna budi kuienzi historia hiyo kwa vizazi vya sasa na vijavyo. 
Mapema akisoma risala ya wazee wa msikiti huo Sheikh Abdalla Rajab, amewashukuru waliojenga msikiti huo mkubwa katika kijiji chao, na kuahidi kuutunza na kuweka darsa ambazo zitakuwa endelevu. 
Amesema uwepo wa msikiti huo ni faraja kwa wanakijiji na maeneo jirani, kwani pia wameweza kuondokana na shida ya maji safi na salama iliyokuwa ikiwakabili kwa kipindi kirefu.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akifungua pazia kuashiria ufunguza rasmi wa MASJID AQSAA katika kijiji cha Kiboja Mkwajuni, Wilaya ya Kati Unguja.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akipena mikono na  Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, baada ya ugunguzi wa MASJID AQSAA na sala ya Ijumaa katika kijiji cha Kiboja Mkwajuni.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, viongozi wa dini ya kiislamu nchini pamoja na waislamu mbali mbali wakisikiliza hotuba ya Ijumaa iliyotolewa na Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraha (hayupo pichani) katika msikiti mpya wa  MASJID AQSAA ulioko Kiboja Mkwajuni. Kushoto ni Kadhi Mkuu Sheikh Khamis Haji akifuatiwa na Mufti Mkuu Sheikh Saleh Omar Kabi
 Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, akitoa nasaha baada ya uzinduzi wa MASJID AQSAA Kiboje Mkwajuni.
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu walioshiriki katika ufunguzi wa MASJID AQSAA, Kiboje Mkwajuni.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria  ufunguza wa MASJID AQSAA katika kijiji cha Kiboja Mkwajuni, Wilaya ya Kati Unguja. 
Picha na Salmin Said, OMKR

Promosheni ya Jaymillions yaendelea kuongeza mamilionea nchini: Zaidi ya milioni 300/-zimeshanyakuliwa na wateja walioshinda

$
0
0
Watanzania wapatao 44  maisha yao yameweza kubadilika kutoka hali ya kawaida na kuwa mamilionea kutokana na kujishindia fedha taslimu kupitia promosheni ya siku 100 ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania ambayo ilianza katikati ya mwezi Februari na inatarajia kufikia ukingoni mapema mwezi ujao.
Hadi kufikia sasa wateja wa Vodacom walioshinda wamejinyakulia shilingi milioni 278 huku mamilioni mengine ya fedha yakisubiri kunyakuliwa na washindi watakaobahatika katika siku chache zilizobaki kabla ya promosheni kufikia tamati.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amesema promosheni bado inaendelea na kuwataka watanzania waendelee kuangalia  namba zao kama zimeshinda kwa kutuma neno JAY kwenda namba 15544.
Aliitaja njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo  mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/- 
“Promosheni ya Jaymillions inaendelea hivyo tunawakumbusha wateja wetu kuwa bado kuna mamilioni ya kujishindia hivyo wachangamkie kwa kujaribu bahati zao katika siku hizi ambazo promosheni inaelekea ukingoni.
Tunajivunia kwa kufanikiwa kubadilisha maisha ya baadhi ya wateja wetu walioshinda wengi wakiwa ni wateja wenye maisha ya kawaida na hii ndio dhamira yetu kubwa inayoendana na kauli mbiu yetu ya “ukiwa na Vodacom maisha ni murua”. 
Nkurlu alisema hayo wakati wa kuchezesha droo ya 55 iliyomwibua Habibu Saidi(19)ambaye ni mkazi wa Kabale Bukoba vijijini anayesubiria kuanza kidato cha tano hivi karibuni kwa kujishindia kitita cha shilingi milioni 10.
Baadhi ya wateja waliobahatika kushinda wanasema kuwa promosheni hii imewafanya kutimiza ndoto zao zilizoshindwa kutimia kwa muda mrefu kwa kuwa maisha yao yamebadilika kutoka hali duni kuwa bora zaidi.
Upendo Madengenya kutoka wilayani Kilolo ambaye alikuwa mhudumu katika nyumba ya kulala wageni wilayani humo ambaye alijishindia milioni 100 anasema“Jaymillions naifananisha na methali ya Kiswahili ya kulala maskini ukaamka tajiri kwa kuwa nilikuwa nakabiliwa na changamoto nyingi za maisha pamoja na familia yangu ,Mungu kaniona nikafanikiwa kushinda hivi sasa maisha yangu yamebadilikakutoka hali duni kuwa bora na bado safari ya kuelekea kwenye maisha bora zaidi inaendelea.
James Mangu kutoka Mwanza ambaye alijishindia milioni 10 anasema kuwa kwa muda mrefu alikuwa anawaza kupata mtaji wa kuendeleza biashara zake ndogo ndogo na kwa bahati nzuri ameweza kuibuka na ushindi na kupata mtaji ambao anakiri kuwa utabadilisha maisha yake na familia yake kwa  ujumla kutoka maisha duni kuwa bora.
Hynes Petro Kanumba mkazi wa Rukwa anasema:”Katika maisha yangu sitaisahau Vodacom Kwa kuwa kupitia promosheni yake ya Jaymillions imeniwezesha kunitoa katika hali duni na kuwa na maisha bora pamoja na familia yangu na natoa wito kwa watanzania kutozipuuza promosheni hizi kwa kuwa ni za kweli na zinalenga kutukomboa sisi wanyonge”
Kwa upande wake Deborah Stanley mshindi wa milioni 10 anasema: “Nimefuatilia Promosheni ya Jaymillions naona inalenga kuwakomboa kimaisha watanzania hususani wenye kipato cha chini hasa  wajasiriamali wadogo wadogo kama vile; wamachinga, mama ntilie, wanafunzi na wazee wastaafu ambapo kwa kiasi kikubwa tunajua watu wa aina hii wanahitaji msaada ili kujiendeleza kiuchumi. Kwa fedha ambazo baadhi ya washindi tayari wamezipata wengi zimewasaidia kujikwamua na kujiendeleza kimaisha,"
.Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kuchezesha droo ya 55 ya promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo iliyofanyika leo,ambapo Habibu Saidi(19)ambaye ni mkazi wa Kabale Bukoba vijijini anayesubiria kuanza kidato cha tano hivi karibuni kwa kujishindia kitita cha shilingi milioni 10.Kutoka kushoto ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha,Mrisho Millao na Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo Mathew Kampambe.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544 au AUTO kwenda namba hiyo iwapo simu haina fedha ambapo  mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-tu.

WORLD MALARIA DAY 2015 - SHARE YOUR PLANS TO COMMEMORATE WORLD MALARIA DAY !!

$
0
0
cid:image007.jpg@01D06C9B.DB110200

World Malaria Day 2015:
Invest in the Future, Defeat Malaria

The World Malaria Day theme provides a common platform for all malaria partners to showcase their successes in malaria control and unify diverse initiatives in the changing global context. Malaria-endemic countries have made incredible gains in malaria in the last decade, but sustaining them will take extra efforts until the job is finished and malaria is eliminated worldwide. The theme for 2015 is Invest in the future, Defeat malaria calling attention to the need to increase commitments in the new era of development, with Sustainable Development Goals..
Post your event on the World Malaria Day website!
·        Share your event with everyone and post it on the World Malaria Day website !

INTRODUCING new single from Lady Jaydee ft. Mazet & Uhuru - GIVE ME LOVE


MKOA WA KAGERA NA UTAMADUNI WA KUWAENZI VIONGOZI WAKUU WALIOUONGOZA MKOA HUO KWA NYAKATI TOFAUTI TANGU UHURU MWAKA 1961

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kagera wa sasa Mheshimiwa John V.K. Mongella ukimuaga aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Kagera wa 20  Kanali Mstaafu Fabian Inyasi Massawe kwa jina maarufu Mulokozi.
Tangu uhuru  wa iliyokuwa Tanganyika sasa Tanzania  mwaka 1961 miaka 53 ya uhuru mkoa wa Kagera umekuwa ukiongozwa na viongozi mbalimbali hasa katika nafasi ya  ukuu wa mkoa na kwa kipindi hicho chote hadi sasa tayari mkoa umeongozwa na wakuu wa mikoa wapatao 21 kwa vipndi  tofauti.

Viongozi hao  (Wakuu wa Mkoa)  waliowahi kuuongoza mkoa wa Kagera kwa nyakati  tofauti  waliweza kuisogeza Kagera kutoka katika hali fulani na kupiga hatua kimaendeleo katika nyanja  mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchumi, elimu,  siasa, utamaduni, miundombinu, na nyanja mbalimbali za ustawi wa jamii.

Mkoa wa Kagera chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa wa sasa Mheshimiwa John V.K. Mongella ulimuaga aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Kagera wa 20 na aliuongoza  mkoa  kwa miaka mitatu akiteuliwa kutoka katikanafasi ya Ukuu wa Wilaya ya Karagwe naye ni Kanali Mstaafu Fabian Inyasi Massawe kwa jina maarufu Mulokozi.
Kama walivyokuwa watangulizi wake Mhe. Kanali Mstaafu Massawe alifanya mengi katika mkoa wa Kagera na kuweka rekodi ya mambo mengi aliyoyafanya yakiongozwa na kaulimbiu yake ya “Amani na Maendeleo” kubakia katika kumbukumbu za mkoa wa Kagera na wananchi wake kwa ujumla.

Kupata historia ya Kanali Mstaafu Fabian Inyasi Massawe BOFYA HAPA

PWANI WAINGIZA MABILIONI YA FEDHA KUPITIA MISITU

$
0
0
Na John Gagarini, Bagamoyo
MKOA wa Pwani umefanikiwa kukusanya kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni nane kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika kipindi cha mwaka 2013/2014.

Hayo yalisemwa juzi wilayani Bagamoyo na Ofisa Misitu wa mkoa huo Daniel Isara, wakati wa maadhimisho ya upandaji miti kimkoa iliyofanyika kwenye eneo la la Gareza la Kigongoni ambapo ilipandwa zaidi ya miti 3,000.

Isara alisema kuwa fedha hizo zimetokana na kukabiliana na uharibifu wa rasilimali misitu na mazingira ambapo doria ziliimarishwa na ukusanyaji wa mapato kufikia kiasi hicho.

Alisema kuwa hadi kufikia mwezi Januari 2014/2015 makusanyo yalifikia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni sita baada ya wakala hao kuongeza watumishi kwenye ngazi za wilaya.

“Mbali ya mafanikio ya ukusanyaji wa mapato hayo ya Serikali pia mkoa umehamasisha na mwamko umekuwa mkubwa na kuongeza uanzishwaji wa vitalu vya miche na upandaji wa miti kwe taasisi za serikali na zisizo za serikali na watu binafsi kutoka miche ya miti milioni 2,253,136 mwaka 2013/2014 na kufikia milioni 2,663,202 mwaka 2014/2015,” alisema Isara.

Aidha alisema kuwa pia wakala imeweza kuwaondoa wavamizi kwenye misitu ya Ruvu Kaskazini, Ruvu Kusini, Kiloka, Kazimzumbwi na wavuvi kwenye Delta ya Rufiji pia kuweka mipaka ya misitu ya hifadhi kiasi cha kilometa 640 katika hekta 10,704.

“Changamoto zinazoikabili rasilimali ya misitu ni pamoja na ongezeko kwa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam ambalo huongeza mahitaji ya mkaa na kuni hivyo kuongezeka kwa ukataji na ufyekaji wa misitu na mapori,” alisema Isara.

Alibainisha kuwa kuna wafanyabiashara 320 waliosajiliwa kufanyabiashara ya kuvuna mazao ya misitu mkoani Pwani kwa  mwaka 2013/2014 na 336 mwaka 2014/2015 na zaidi ya asilimia 90 wanatoka nje ya mkoa.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Pwani  Evarist Ndikilo ambaye aliwakilishwa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga alisema kuwa taasisi zinazotumia kuni kwa wingi kwa ajili ya kupikia na shughuli nyingine zinapaswa kupanda miti kwa wingi.

Ndikilo alisema kuwa zinapaswa kutumia majiko sanifu yanayotumia kuni au mkaa kidogo ili iwe sehemu ya ubunifu wa kupunguza matumizi makubwa ya nishati ya miti.

Aliwataka wananchi kila mtu kupanda miti ili kulinda mazingira pia mamalaka za serikali za mitaa kuomba vibali vya kuajiri watumishi kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa rasilimali misitu na misitu iliyohifadhiwa inatunzwa na kuzuia wavamizi wanaoingiza mifugo, uchimbaji wa mchanga, kilimo na makazi kwenye misitu.

Mkoa wa Pwani una misitu 34 ya hifadhi yenye jumla ya hekta 335,712 iliyohifadhiwa kisheria na hekta milioni 2.2 ya misitu kwenye ardhi huria ambayo hutegemewa na mikoa ya Pwani na Dar es Salaam kwa ajili ya matumizi ya nishati za magogo, mbao, samani na matumizi mengine.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akipanda mti kuashiria maadhimisho ya upandaji miti kimkoa yaliyofanyika katika eneo la Gereza la Kigongoni wilayani Bagamoyo. (Picha na John Gagarini).

MKUTANO NA TAMASHA LA CHAUKIDU... Mzee Ali Hassan Mwinyi Mgeni Rasmi

$
0
0
MKUTANO KUANZA ASUBUHI, HOWARD UNIVERSITY (9:00AM-5:00PM)  NA TAMASHA JIONI HOLLYWOOD BALLROOM (7:00PM-12:00 AM))
Njoo ujumuike na wapenzi wa Lugha ya Kiswahili na kupata chakula cha Kiafrika, vinywaji, burudani ya muziki kutoka kwa gwiji Master DJ Luke na maonyesho kadhaa ya wasanii, wakiwemo Anna Mwalaghona AJ Ubao, katika Tamasha la kipekee Washington DC, April 23, 2015.
Nunua tiketi yako mapema kwa kutembelea Tovuti ya CHAUKIDU <www.chaukidu.org>, au piga simu namba 301-433-3411 (Tumaini), 301-793-2833 (Asha) na 202-830-6555 (Dr. Magembe) kununua tiketi yako mkononi.
 Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi
Njoo ujumuike na wapenzi wa Lugha ya Kiswahili pamoja na kupata chakula cha Kiafrika, vinywaji, burudani ya muziki kutoka kwa gwiji Master DJ Luke na maonyesho kadhaa ya wasanii, wakiwemo Anna Mwalagho na AJ Ubao, katika Tamasha la kipekee Washington DC, April 23, 2015.

Nunua tiketi yako mapema kwa kutembelea Tovuti ya CHAUKIDU <www.chaukidu.org>, au piga simu namba 301-433-3411(Tumaini), 301-793-2833 (Asha) na 202-830-6555 (Dr. Magembe) kununua tiketi moja kwa moja mkononi.

TIKETI HAZITAUZWA MLANGONI.

Mkurugenzi wa Mwananchi Communications Limited Francis Nanai azindua asasi ya TAYL

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, Francis Nanai akizungumza wakati akizindua asasi ya kuendeleza vijana katika masuala ya uongozi ijulikanayo kwa jina la Tanzania- Asia Young Leaders (TAYL).
Mjumbe wa Kamati Kuu na mmoja wa muasisi wa asasi ya TAYL, Ismail Biro akizungumzia historia na malengo ya asasi hiyo wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye hotel ya New Africa jijini.
Wajumbe na wanachama wa asasi hiyo walifuatilia uzinduzi. 

Balozi Seif Idd afungua Mafunzo ya Miezi Mitatu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mkuu wa Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar Nd. Abdullah Othman Ali wakati wa hafla ya kuyafunga mafunzo hayo hapo Skuli ya Sekondari Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja. Kati kati yao ni Mbunge wa Jimbo la Donge Mheshimiwa Sadifa Juma Khamis, na nyuma ya Balozi Seif ni Mratibu wa Mradi unaoondesha mafunzo hayo Nd.Abdi Hamid Abeid.
Mkuu wa Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar Nd. Abdullah Othman Ali akimpatia maelezo Balozi Seif wakati alipotembelea Darasa la mafunzo hayo hapo Skuli ya Sekondari Donge.
Baadhi ya Wanafuzi wa Darasa la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar wakishuhudiwa na Balozi Seif wakiendelea kufanya mazoezi ya vitendo katika kukabiliana na matatizo madogo madogo yanayojichomoza wakati wa matumizi wa kompyuta zao.

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images