Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 78 | 79 | (Page 80) | 81 | 82 | .... | 3282 | newer

  0 0
 • 03/25/13--01:36: In Loving Memory
 • Mzee  Bernardin Lungwa Mwaja
  (05/08/1934  – 25/03/2012)

  _______________

  Daddy,  today it’s exactly a year since you  left us. We are thinking of you, you are always on our minds. We still remember the day, when God Almighty called you Home; He saw you getting tired and a cure was not to be. So He put His arms around you and whispered "Come to Me and Peace be Thine" and gave you wings to fly. With tearful eyes we watched you, and saw you pass away. When we saw you sleeping so calm and free of pain, we would not wish you back to earth to suffer once again. 

  Although  we loved you dearly, we could not  make you stay. A golden heart stopped beating, hardworking hands at rest. You're not around, but your precious memories still remain captured in our hearts. Your love will be our guide, you live on through your children, and you are always by our side. You were like an angel that came and made our lives beautiful, and now that you are in heaven, we know you are doing the same.

  Deeply  missed but always remembered by your children  Pascal, Justina, Severina, Ludovick, Alphonce, Kelvin and Sarah; grandchildren Nuru, Fred, Leah, Salome, Stanford, Kenneth, Viola, Joan, Tonny, Kayla, Chris, Ben and Kamilla; your daughte in-laws; son in-laws; brothers, sisters, all relatives and friends.

  “May God Almighty Rest Your Soul in Eternal Peace.
    Amen!”

  R.  I. P. Daddy!  (Job 1:21)

  0 0

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bibi Rehema Madenge akifunga rasmi mkutano kati ya Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma na Wakurugenzi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa uliomalizika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa St. Gaspar mkoani Dodoma.
  Wakurugenzi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wakimsikiliza Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Bibi Rehema Madenge alipokuwa akifunga rasmi mkutano kati ya Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma na Wakurugenzi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa St. Gaspar mkoani Dodoma.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma (kushoto) Bwana Vincent Mrisho akiteta jambo na Katibu wa Bodi hiyo Bibi Tamika Mwakahesya (kulia) wakati wa mkutano wa siku mbili kati ya Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma na Wakurugenzi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 21-22 Machi katika ukumbi wa St. Gaspar mkoani Dodoma.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma (aliyevaa suti kulia) Bwana Vincent Mrisho akiteta jambo na Katibu wa Bodi hiyo Bibi Tamika Mwakahesya (aliyeshika begi) na baadhi ya wajumbe wa mkutano kati ya Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma na Wakurugenzi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 21-22 Machi katika ukumbi wa St. Gaspar mkoani Dodoma.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bibi Rehema Madenge aliyevaa vitenge (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma Bwana Vincent Mrisho (kulia) na Katibu wa Bodi hiyo Bibi Tamika Mwakahesya (kushoto) pamoja na baadhi ya Wakurugenzi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 21-22 Machi katika ukumbi wa St. Gaspar mkoani Dodoma.

  0 0
 • 03/25/13--02:10: Salamu Kutoka Afrika Kusini
 •  
  Hope all is well.
  Salamu nyingi saaana toka JBG!
  I could not resist! Yes I cried! But Absalom is the same person I knew last two months! Amesimama! Mungu ni Mwema!!!
  Anaomba watanzania wamwombee na amesema anaendelea vizuri kwa sasa…
  Cheers,
  Hoyce Temu.

  0 0

  Salaam Ankal Michuzi,
  Nimeona mvua ilovyoleta matatizo hapo jijini Dar jana katika maeneo mbali mbali.Lakini Matatizo yetu jana hapa Ukerewe (Uingereza) ni kama uonavyo pichani,barafu imejaa kila kona.ama kweli kila mtu na shida zake.

  Mdau Ukerewe 

  0 0

  Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe,akisisitiza jambo kwa Waziri wa Uingereza anaeshughulika na Maswala ya Afrika, Bw. Mark Simmonds(kushoto kwa Waziri Mwakyembe), wakati Waziri huyo alipomtembela ofisini kwake mwishoni mwa wiki kujadiliana maswala mbalimbali yanayohusu Usafiri wa Anga, Reli pamoja na bandari.
  Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe(mwenye suti nyeusi) akimuonyesha Waziri wa Uingereza anaeshughulika na Maswala ya Afrika, Bw. Mark Simmonds Miradi mbali mbali inayofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kwa hapa Tanzania. Waziri Mwakyembe alikutana na Waziri huyo ofisni kwake kujadiliana kuhusu Usafiri wa Anga, Miradi ya Bandari na Miradi mbalimbali ya Reli mwishoni mwa wiki.
  Waziri wa Serikali ya Uingereza anaeshughulika na Maswala ya Afrika, Bw. Mark Simmonds akifafanua jambo kwa Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwkyembe(Mwenye suti Nyeusi), wakati alipomtembelea waziri Mwakyembe ofisini kwake mwishoni mwa wiki. Kulia kwa Waziri Mwakyembe ni Balozi wa Uingereza Tanzania, Dianna Melsone.
  Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Harrison Mwakyembe akishikana mikono na Waziri wa Uingereza anaeshughulika na Maswala ya Afrika, Bw. Mark Simmonds, wakati alipomtembela ofisini kwake leo huu.
  Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Uingereza anaeshughulika na Maswala ya Afrika, Bw. Mark Simmonds(mwenye tai ya blue bahari), Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melsone(kushoto kwa Waziri Mwakyembe) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo(Kulia kwa Waziri Mark).

  0 0

  Baadhi ya wanakamati ya Bunge ya uchumi na viwanda na biashara ambao walihudhuria washa ya maswala ya lishe uhakiki wa chakula na haki za watoto nchini wakioneshwa jinsi virutubisho vinavyochanganywa kwenye chakula na kusagwa na Meneja raslimali watu wa kiwanda cha Azania Bw.Haji Abdallah,jinsi kinavyojishughulisha na kusindika vyakula kwa afya bora kwa jamii, washa hiyo iliandaliwa na taasisi ya chakula na lishe(TFNC)kwa kushirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali ya Helen Keller International(HKI).
  Kaimu mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya chakula na lishe Tanzania Bw.Benedict Jeje akichangia mada katka washa ya uongozaji wa virutubishi kwenye vyakula kwa afya bora na jamii,washa hiyo iliandaliwa na taasisi ya chakula na lishe(TFNC)kwa kushirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali ya Helen Keller International(HKI).
  Mmoja wa wanakamati wa Bunge ya uchumi na viwanda na biashara ambae ni Mwenyekiti wa kamati ya maswala ya ukimwi kwa kikundi cha wabunge maswala ya lishe uhakiki wa chakula na haki za watoto nchini Bi.Lediana Mng'ong'o akitoa mada wakati wa washa ya uongozaji wa virutubishi kwenye vyakula kwa afya bora na jamii,washa hiyo iliandaliwa na taasisi ya chakula na lishe(TFNC)kwa kushirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali ya Helen Keller International(HKI)
  washiriki wa washa ya maswala ya lishe uhakiki wa chakula na haki za watoto nchini wakiwafafanulia jambo baadhi ya washiriki ambao ni wanakamati wa Bunge ya uchumi na viwanda na biashara washa hiyo iliandaliwa na taasisi ya chakula na lishe(TFNC)kwa kushirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali ya Helen Keller International(HKI).

  0 0
 • 03/25/13--02:35: TAARIFA YA MSIBA
 • FAMILIA YA BWANA ATHANAS SHARIFF MUSHI WA URU MAWELLA-MOSHI, INATANGAZA KIFO CHA BABA YAO MPENDWA, ATHANAS SHARIFF MUSHI, KILICHOTOKEA JANA JUMAPILI MACHI 24, 2013 KATIKA HOSPITALI YA MT. JOSEPH, SOWETO-MOSHI. 

  MIPANGO YA MAZISHI INAFANYIKA LEO SAA 10:00 JIONI, KONA BAR MABIBO DAR ES SALAAM NA NYUMBANI KWA MAREHEMU URU, MAWELLA, MOSHI.

   MAZISHI NI JUMATANO, MACHI 27, 2013. HABARI ZIWAFIKIE, MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI (IGP) SAID MWEMA NA WATUMISHI WOTE WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, UKOO WOTE WA MUSHI, UKOO WOTE WA KOMU, FAMILIA YA MPONDA WA MOROGORO, NDUGU JAMAA NA MARAFIKI POPOTE WALIPO. 

  APUMZIKE KWA AMANI.

  0 0

  Na Mwandishi wetu
  KAMPUNI ya Compass Communications imewatahadharisha warembo  na wanamitindo wote nchini kutorubuniwa na genge la watu wanaotumia jina la Flaviana Matata kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai amesema jana kuwa kuna genge la watu wanaotumia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa facebook ujulikano kwa jina la Flaviana Matata’s  na kujipatika fedha kiasi cha sh. 200,000 kwa jila anayejiunga kwa lengo la kutafutiwa kazi au nafasi ya kufanya shughuli za wanamitindo nje ya nchi.
  Maria alisema kuwa watu hao huwarubuni wasichana na kuwaahidi kuwatafutia kazi nje ya nchi kwa mgongo wa Flaviana na mmoja wa vijana hao amejitambulisha kama ‘kaka’ yake mwanamitindo huyo, jambo ambalo si la kweli.
  Alifafanua kuwa baada ya kukutana na wasichana waliongia katika mtego huo, huwa wanaawalaghai kwa njia mablimbali na baadaye kulipa kiasi hicho cha fedha. Alisema kuwa hali hiyo imewaletea usumbufu wasichana wengi na kujikuta wakihaha kutafuta ukweli baada ya kutapeliwa.
  “Compass Communications kama kampuni inayosimamia shughuli za Flaviana Matata inatoa tahadhari kwa umma kuwa Flaviana Matata hahusiki kwa njia yoyote na ukurasa huu au watu hawa.  Pia tunawatahadharisha wananchi kuwa wawe waangalifu kwani Flaviana Matata hayuko katika biashara ya kumtafutia mtu yoyote kazi ya  uanamitindo popote pake,” alisema Maria.
  Maria alisema kuwa ukurasa halisi ya Flaviana Matata kwenye mtandaomwa Facebook ni “Flaviana Lavvy Matata” na kwa sasa wanendelea kushirikiana na vyombo husika kwa kutoa taarifa kuhusu uhalifu huo.

  0 0

  Nawashukuru sana ndg,jamaa na Marafiki kwa jinsi mlivyojitoa na kumuombea Dua mtoto wangu Mpendwa Nuru Abdulaziz katika kipindi chote toka amezaliwa tr 05 march 2013 na alipoanza kuumwa na kuvimba upande mmoja wa kichwa na kulazwa katika hospital ya Mkoa wa Lindi tr 08 march..Hakika mlinifariji sana na kunitia Moyo...Kwa Mapendo ya Mungu yeye alimpenda zaidi na kuweza kumchukua tr 24 march na kuzikwa siku hiyo hiyo

  Kwa Niaba ya Familia yangu nawashukuru sana kwa subira mliyonipa na mnavyozidi kujitokeza kunifariji katika kipindi hiki kigumu..Mungu awape baraka nanyi

  Tuko pamoja kwa kila jambo

  Ahsante........

  Abdulaziz Ahmeid-Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Lindi au maarufu Abdulaziz Video wa Channel ten-Lindi

  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ufunguo kutoka kwa Rais Wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe.Xi Jinping wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Ukumbi huo umejengwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya China na Tanzania.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Xi Jinping wa China wakishangilia jambo wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wageni waliohudhuria sherehe za makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa China Mhe.Xi Jinping wakiangalia picha za matukio mbalimbali yanayohusu historia ya ushirikiano kati ya China na Tanzania katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo wakati wa sherehe za makabidhiano ya ukumbi huo jijini Dar es Salaam leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa katika picha ya Pamoja na Rais wa China Mhe.Xi Jinping pamoja na Mkewe katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere muda mfupi baada ya sherehe za ufunguzi wa ukumbi huo leo.picha na Freddy Maro,Ikulu.

  0 0


  Kaa tayari kipindi chako ukipendacho na gumzo la mji KIJIWE CHA UGHAIBUNI hapo kesho Jumanne March 26, 2013
  Kipindi cha KIJIWE CHA UGHAIBUNI kipo tayari kurushwa kesho Jumanne USIKOSE


  0 0

  Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaundentia Kabaka (Mb) akifungua Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA), mapema leo 25/03/2013, katika ukumbi wa Baraza la Maaskofu Kurasini (TEC) jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa kazi (OSHA), wakimsikiliza kwa makini Mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaundentia Kabaka (Mb) wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi katika ukumbi wa Baraza la Maaskofu Kurasini (TEC) jijini Dar es Salaam.
  Washiriki wa Baraza la Wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaundentia Kabaka.

  0 0


  0 0

  Katibu tawala Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Theresia Mmbando akiwahutubiwa washiriki wa mafunzo ya Uokoaji na Majanga Kutoka taasisi mbalilmbali wakati akifunga mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es salaam, kulia ni Meneja Miradi wa Plan International Wilaya ya Ilala Daniel Kalimbiya.
  Washiriki wa mafunzo ya Uokoaji na Majanga, wakionesha kwa vitendo jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa majeruhi, mafunzo hayo yalifanyika Dar es salaam chini ya ufadhili wa Plan International pamoja na Chama cha Msalaba Mwekundu Red Cross.
  Mshiriki wa mafunzo ya Uokoaji na Majanga, wakionesha kwa vitendo jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa majeruhi, mafunzo hayo yalifanyika Dar es salaam chini ya ufadhili wa Plan International pamoja na Chama cha Msalaba Mwekundu Red Cross.

  0 0

  Naibu Waziri Tamisemi(ELIMU) Ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi ,Kassim Majaliwa Akipokea msaada wa mashuka 100 kwa Mkurugenzi wa Masoko na Elimu kwa Umma toka Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya(NHIF)Raphael Mwamoto kwa ajili ya vituo vya Afya vya wilaya hiyo.
  Mkurugenzi wa Masoko na Elimu kwa Umma toka Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya(NHIF)Raphael Mwamoto akikabidhi mashuka 140 Diwani wa kata ya Singino/Kivinje,Jafari Arobaini shuka ambazo zitasambazwa katika vituo vya Afya vya wilaya hiyo.

  Na Abdulaziz Video,Globu ya Jamii - Lindi

  Imeelezwa kuwa Hospital ya Wilaya ya Kilwa/Kinyonga Mkoani Lindi Inakabiliwa na Upungufu Mkubwa wa Shuka kwa ajili ya Wagonjwa wanaolazwa katika Hospital hiyo pamoja na Vituo Vitano vya Afya Wilayani humo.

  Hayo yamebainishwa na Mganga mkuu wa Wilaya ya Kilwa Dr Mike Mabimbi baada ya kukabidhiwa mashuka 140 na Mkurugenzi wa Masoko na Elimu kwa Umma toka Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya(NHIF)Raphael Mwamoto katika hafla fupi iliyofanyika katika hospital hiyo.

  Amesema kwa sasa hospital yake yenye vitanda 90 kila kitanda kinatumia mashuka mawili tu kwa siku ambayo hayakidhi mahitaji kwa mgonjwa alielazwa ambae anapaswa kuwa na mashuka manne kwa siku Dr Mabimbi amesema kupatikana kwa mashuka hayo kutasaidia baadhi kusambazwa katika vituo vya Afya katika kata za Tingi,Nanjirinji,Pande,Njinjo na Masoko ili kupunguza tatizo hilo sugu kwa Wagonjwa.

  Kwa Upande wake Mkurugenzi Mwamoto amesema msaada huo ni katika Juhudi za Mfuko wake kuhakikisha kuwa Wagonjwa wanaolazwa hospitalini wanapatiwa huduma Muhimu za Kijamii ikiwa ni pamoja na matibabu mazuri .

  Aidha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umekabidhi mashuka 100 kwa ajili ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi katika Hafla fupi zilizofanyika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ruangwa na Hospital ya Wilaya ya Kilwa(KINYONGA)

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping,katika Ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam,walipokutana kwa mazungumzo ya Kiutendaji.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akimtambulisha Waziri wa Fedha,Uchumi na Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf Mzee,kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping,katika Ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam,walipokutana kwa mazungumzo ya Kiutendaji.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping,katika Ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam,walipokutana leo asubuhi ikiwa ni hatua ua ushirikiano katika nchi mbili hizi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiagana na Balozi Mdogo wa China anyeishi Zanzibar Bibi Chen Yiman,baada ya mazungumzo na Rais wa China Xi Jinping,leo asubuhi katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam, [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

  0 0

  Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Bw.Benjamin Michael akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milion moja Bw.Andrew Mwakagenda ambae aliibuka mshindi wa promosheni ya "MAHELA"inayoendeshwa na kampuni hiyo,katikati anaeshuhudia ni rafiki yake mshindi huyo Bw.Patrick Kwai.Mteja anatakiwa kutuma neno"MAHELA"kwenda namba 15544 na kuweza kujishindia.Zaidi ya shilingi Milioni 180 zinaendelea kushindaniwa.
  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu(kushoto)akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni tano,Bw.Clement Semalobe mkazi wa jijini Dares Salaam alijishindia kitita hicho kupitia promosheni ya 'MAHELA' inayoendeshwa na kampuni hiyo,katikati anaeshuhudia ni Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Bw.Benjamin Michael.Mteja anatakiwa kutuma neno"MAHELA"kwenda namba 15544 na kuweza kujishindia.Zaidi ya shilingi Milioni 180 zinaendelea kushindaniwa.
  Bw.Andrew Mwakagenda ambae aliibuka mshindi wa promosheni ya "MAHELA"inayoendeshwa na kampuniya Vodacom Tanzania,akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani baada ya kupokea hundi yake yenye thamani ya shilingi Milioni moja,Kulia ni Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Bw.Benjamin Michael.Mteja anatakiwa kutuma neno"MAHELA"kwenda namba 15544 na kuweza kujishindia.Zaidi ya shilingi Milioni 180 zinaendelea kushindaniwa.
  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu(kulia)akiwasiliana kwa njia ya simu ya mezani na mmoja wa washindi Bw.Alphonce Kusekwa mkazi wa Tanga aliejishindia shilingi million tano kupitia promosheni ya 'MAHELA' inayoendeshwa na kampuni hiyo,wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Bw. Abdallah Hemedy na Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Bw.Benjamin Michael Mteja anatakiwa kutuma neno"MAHELA"kwenda namba 15544 na kuweza kujishindia.Zaidi ya shilingi Milioni 180 zinaendelea kushindaniwa.

  0 0

  Bomba linalotoa maji katika kisima cha kaloleni na hatimaye kuunganishwa katika mtandao wa maji kwa ajili ya wakazi wa Mabogini,Pasua na Bomambuzi.
  Kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dk Ibrahim Msengi akiotesha mti katika chanzo cha maji cha kaloleni wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji iliyofanyika katika kata hiyo.
  Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Bernrdette Kianabo akiotesha mti katika chanzo cha maji cha Kaloleni wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji iliyofanyika katika kata ya Kaloleni.
  Mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingiara mjini Moshi ,Sharry Raymond akiotesha mti katika chanzo cha maji cha Kaloleni.

  Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii ,Moshi

  HALMASHAURI ya Manispaa ya Moshi imewatoa hofu wakazi wa kata za Kaloleni, Pasua na Mabogini wanaotumia maji kutoka kisima cha Kaloleni kwamba ni salama kwa matumizi ya nyumbani licha ya taarifa kuwa yanaathiriwa na dampo lililopo jirani.

  Wakizungumza katika kilele cha wiki ya maji,mkurugenzi wa manispaa,Bernadette Kinabo na kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Moshi (MUWSA),Isa Osena wamesema kisima hicho ni kirefu na hupimwa kitaalamu kila mwezi.

  Kauli hiyo ilifuatia kitendo cha wananchi wa kata hiyo,kumpokea kwa mabango yenye ujumbe mbalimbali,kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Dk Ibrahim Msengi wakilalamikia usalama wa maji hayo lakini pia kutopata maji licha ya kisima kuwapo kwao.

  Mwenyekiti wa mtaa wa Kaloleni,Ndama Bin Ndama,alisema wananchi hawana imani na maji hayo kutokana na majitaka yanayochurizika kutoka katika dampo kuu,lakini pia hawana maji licha ya kuwepo kisima eneo lao huku wakilalamikia maji kupelekwa kata za jirani.

  Katika majibu yao,Kinabo na Osena walisema kisima kina urefu wa mita 100 na hupimwa kila mara na dampo likiwa umbali wa zaidi ya mita 60 na limetengenezwa kitaalamu kwa kuwekewa msingi wa saruji inazozuia maji kuelekea katika kisima.

  Aidha Kinabo alisema MUWSA imetenga zaidi ya Sh Mil 236 kwa mwaka wa fedha 2013/204 kwa ajili ya kuongeza vyanzo vipya huku manispaa ikitarajia kuzindua mpango wa uoteshaji miti Mil 2 katika vyanzo na makazi kuanzia April 10 hadi 16 mwaka huu.

  Awali kaimu mkuu wa mkoa,Dk Msengi akizindua kisima cha Kaloleni kilichoongeza uzalishaji wake kutoka lita za ujazo 71 kwa saa hadi lita 1200 kwa siku na kukarabatiwa kwa Mil 41.2, alitaka wananchi kukilinda na kuotesha miti kwa wingi.

  Dk Msengi alisema hakuna sababu ya wananchi kuilaumu MUWSA au manispaa kuhusu upungufu wa maji wakati wao hawajaotesha miti ambapo alielezea mpango wa wilaya kutenga kila jumamosi ya mwezi kwa ajili ya usafi wa mazingira na upandaji miti.

  0 0


   President Jakaya Mrisho Kikwete listen keenly as  his guest Chinese President Xi Jinping makes  his maiden speech in  Africa during the handing over ceremony of the Mwalimu Julius Nyerere Convention Centre.

  The Visiting Chinese President delivered an important speech, expounding on China-Africa relations and China's Africa policy. 

  President Xi arrived in Dar Es Salaam on Sunday for a state visit to Tanzania, the second leg of his first foreign trip after he assumed presidency earlier this month.

   President Jakaya Mrisho Kikwete and his guest Chinese President Xi Jinping applaud to the mammoth crowd. 
  President Jakaya Mrisho Kikwete speaks as his guest Chinese President Xi Jinping during the handing over ceremony of the Mwalimu Julius Nyerere Convention Centre. For more photos CLICK HERE

  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa China Xi Jinping wakiweka mashada ya maua katika makaburi ya wataalamu wa China waliofariki wakati wa ujenzi wa Reli ya TAZARA.Viongozi hao waliweka mashada hayo ya maua katika makaburi hayo yaliyopo katika kijiji cha Majohe,Ukonga jijini Dar es Salaam.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mke wa Rais wa China Mama Peng Liyuan wakiweka maua katika makaburi ya wataalamu wa China waliofariki wakati wa ujenzi wa Reli ya TAZARA huko katika kijiji cha Majohe,Ukonga nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam huku Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wa Rais Xi Jinping wakishuhudia(picha na Freddy Maro).

older | 1 | .... | 78 | 79 | (Page 80) | 81 | 82 | .... | 3282 | newer