Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 797 | 798 | (Page 799) | 800 | 801 | .... | 3270 | newer

  0 0


  0 0

  IMG-20150410-WA0026
  Artist:Lady jaydee Ft Mazet&UhuruSong: Give me loveProducer:Uhuru
  Support Jaydee, Support Our Own

  0 0

  Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue jana imesema uteuzi huo ulianza Machi 27.Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amemteua Hemed Iddi Mgaza kuwa Balozi wa Tanzania Saudi Arabia.
  Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue jana imesema uteuzi huo ulianza Machi 27.Kabla ya uteuzi huo, Mgaza alikuwa Ofisa Mambo ya Nje Mkuu, Daraja la Pili na Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
  Mgaza anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Abdillah Omar ambaye mkataba wake wa utumishi umekwisha.

  0 0
 • 04/10/15--03:38: In Loving Memory


 • 0 0

  Napenda kumshukuru Mungu kwa kunifikisha leo Aprili 10 siku yangu ya kuzaliwa... Hakika Mungu ni mwema kwa kila jambo. Pia napenda kuishukukuru familia yangu, ndugu jamaa na marafiki kwa kuwa pamoja nami mpaka leo. Asanteni sana.

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kuchezesha droo ya 55 ya promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo iliyofanyika leo,ambapo Habibu Saidi(19)ambaye ni mkazi wa Kabale Bukoba vijijini anayesubiria kuanza kidato cha tano hivi karibuni kwa kujishindia kitita cha shilingi milioni 10.Kutoka kushoto ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha,Mrisho Millao na Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo Mathew Kampambe.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544 au AUTO kwenda namba hiyo iwapo simu haina fedha ambapo  mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-tu.

  Zaidi ya milioni 300/-zimesha nyakuliwa na wateja walioshinda
  Watanzania wapatao 44  maisha yao yameweza kubadilika kutoka hali ya kawaida na kuwa mamilionea kutokana na kujishindia fedha taslimu kupitia promosheni ya siku 100 ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania ambayo ilianza katikati ya mwezi Februari na inatarajia kufikia ukingoni mapema mwezi ujao.
  Hadi kufikia sasa wateja wa Vodacom walioshinda wamejinyakulia shilingi milioni 278 huku mamilioni mengine ya fedha yakisubiri kunyakuliwa na washindi watakaobahatika katika siku chache zilizobaki kabla ya promosheni kufikia tamati.
  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amesema promosheni bado inaendelea na kuwataka watanzania waendelee kuangalia  namba zao kama zimeshinda kwa kutuma neno JAY kwenda namba 15544. Aliitaja njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo  mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-

  “Promosheni ya Jaymillions inaendelea hivyo tunawakumbusha wateja wetu kuwa bado kuna mamilioni ya kujishindia hivyo wachangamkie kwa kujaribu bahati zao katika siku hizi ambazo promosheni inaelekea ukingoni.Tunajivunia kwa kufanikiwa kubadilisha maisha ya baadhi ya wateja wetu walioshinda wengi wakiwa ni wateja wenye maisha ya kawaida na hii ndio dhamira yetu kubwa inayoendana na kauli mbiu yetu ya “ukiwa na Vodacom maisha ni murua”. Nkurlu alisema hayo wakati wa kuchezesha droo ya 55 iliyomwibua Habibu Saidi(19)ambaye ni mkazi wa Kabale Bukoba vijijini anayesubiria kuanza kidato cha tano hivi karibuni kwa kujishindia kitita cha shilingi milioni 10.
  Baadhi ya wateja waliobahatika kushinda wanasema kuwa promosheni hii imewafanya kutimiza ndoto zao zilizoshindwa kutimia kwa muda mrefu kwa kuwa maisha yao yamebadilika kutoka hali duni kuwa bora zaidi.
  Upendo Madengenya kutoka wilayani Kilolo ambaye alikuwa mhudumu katika nyumba ya kulala wageni wilayani humo ambaye alijishindia milioni 100 anasema“Jaymillions naifananisha na methali ya Kiswahili ya kulala maskini ukaamka tajiri kwa kuwa nilikuwa nakabiliwa na changamoto nyingi za maisha pamoja na familia yangu ,Mungu kaniona nikafanikiwa kushinda hivi sasa maisha yangu yamebadilikakutoka hali duni kuwa bora na bado safari ya kuelekea kwenye maisha bora zaidi inaendelea.
  James Mangu kutoka Mwanza ambaye alijishindia milioni 10 anasema kuwa kwa muda mrefu alikuwa anawaza kupata mtaji wa kuendeleza biashara zake ndogo ndogo na kwa bahati nzuri ameweza kuibuka na ushindi na kupata mtaji ambao anakiri kuwa utabadilisha maisha yake na familia yake kwa  ujumla kutoka maisha duni kuwa bora.
  Hynes Petro Kanumba mkazi wa Rukwa anasema:”Katika maisha yangu sitaisahau Vodacom Kwa kuwa kupitia promosheni yake ya Jaymillions imeniwezesha kunitoa katika hali duni na kuwa na maisha bora pamoja na familia yangu na natoa wito kwa watanzania kutozipuuza promosheni hizi kwa kuwa ni za kweli na zinalenga kutukomboa sisi wanyonge”
  Kwa upande wake Deborah Stanley mshindi wa milioni 10 anasema: “Nimefuatilia Promosheni ya Jaymillions naona inalenga kuwakomboa kimaisha watanzania hususani wenye kipato cha chini hasa  wajasiriamali wadogo wadogo kama vile; wamachinga, mama ntilie, wanafunzi na wazee wastaafu ambapo kwa kiasi kikubwa tunajua watu wa aina hii wanahitaji msaada ili kujiendeleza kiuchumi. Kwa fedha ambazo baadhi ya washindi tayari wamezipata wengi zimewasaidia kujikwamua na kujiendeleza kimaisha,".

  0 0

  Madereva wa Vyombo vya Usafirishaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini, leo wameingia katika Mgomo wa kutotoa huduma hiyo, kwa kile kinachoelezwa Madereva hao kutakiwa kurudi vyuoni kwa mafunzo zaidi ya usalama barabarani.

  Hali ya mgomo huo, umepelekea adha kubwa kwa abiria wa vyombo hivyo, hasa wale waliokuwa wakielekea mikoani, kwani katika Stendi kuu ya Mabasi ya Ubungo jijini Dar es salaam, hakuna basi hata moja lililoondoka huku daladala nazo zikiwa hazionekani kabisa vituoni.

  Uongozi wa Madereva hao umeomba kukutana na Uongozi wa Juu Serikalini ili kulizungumzia swala hilo la kuwataka Madereva hao kurudi mafunzoni, kwani wao wanadai kuwa kazi wazifanyazo si za kudumu na hivyo watakaporudi mafunzoni hali ya maisha yao itatetereka.
  Mabasi ya Abiria yaendayo Mikoani yakiwa yameegeshwa tu kwenye maeneo yake katika Kituo kikuu cha Mabasi Ubungo jijini Dar.
  Wakina mama hawa wakiwa wamemshikilia Mgonjwa wao waliekuwa wakimsafirisha kwente mkoani, wakiondoka stendi ya kuu ya Mabasi Ubungo baada kukosa usafiri kutokana na mgomo wa vyombo hiyo leo.
  Huku Ubungo mambo yako namna hii, ni mwendo wa kupiga mguu tu.
  Mijadala ikiendelea kwa wadau mbalimbali wanaofanya shughuli zao katika kituo kikubwa cha Mabasi cha Ubungo jijini Dar.
  Mara lori likazuiliwa na watu hawa, wakidai kuwa amepakia abiria hivyo anatakuwa kuwashusha kama anataka kuendelea na safari yake.

  KUONA PICHA ZAIDI 
  BOFYA HAPA AU BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudencia Kabaka amekutana na uongozi wa juu Madereva wa Vyombo vya Usafirishaji nchini na amefanikiwa kumaliza mgomo wa madereva hao baada ya kutangaza kufuta agizo lililokuwa likiwataka madereva wa mabasi na malori kwenda kusoma tena udereva katika chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). (picha na Maktaba)

  0 0  0 0

  Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

  Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene amesema kuwa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) lina mpango wa kufunga mita za LUKU katika ofisi za taasisi zote za serikali kama moja ya mikakati yake katika ukusanyaji wa mapato.

  Simbachawene aliyasema hayo wakati wa kikao chake na Balozi wa Marekani Nchini, Mark Childress aliyemtembelea ofisini kwake lengo likiwa ni kujadili hatua iliyofikiwa ya utekelezaji wa mpango wa kuboresha sekta ndogo ya umeme na miradi ya Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC).

  Alisema kuwa kama mkakati wa kuhakikisha kuwa shirika la Tanesco halijiendeshi kihasara, shirika hilo limeweka mkakati wa ukusanyaji wa mapato, moja ya mkakati ikiwa ni kufunga mita za Luku kwenye Taasisi za Serikali, Binafsi na wateja wa kawaida.

  “Tunaamini shirika likitekeleza mkakati huo, litapunguza hasara na kuwa tegemezi kwenye serikali kupitia ruzuku.” Alisema Simbachawene. Alisema pia Tanesco itaingia mkataba na Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco) kwa ajili ya ukusanyaji wa madeni yake ya nyuma na kuendelea kulipia ankara zake za kila mwezi.

  Akizungumzia hatua iliyofikiwa ya utekelezaji wa miradi ya MCC Awamu ya Pili , Simbachawene alisema kuwa kazi ya uandaaji wa miradi imekamilika na kuwasilishwa katika Bodi ya MCC nchini Marekani kwa ajili ya kupata idhini ya kufadhili miradi Alitaja mikoa itakayofaidika na miradi ya MCC Awamu ya Pili kuwa ni pamoja na Pwani, Tabora, Shinyanga na Morogoro pamoja na kuboresha utendaji kazi wa Tanesco.

  Wakati huohuo Balozi wa Marekani Nchini, Mark Childress alisema kuwa amefurahishwa na hatua ya utekelezaji wa miradi ya MCC Awamu ya Pili na kusisitiza kuwa Marekani ipo tayari kushirikiana na nchi ya Tanzania kupitia miradi ya umeme ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata umeme wa uhakika ambao una mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
  Balozi wa Marekani Nchini, Mark Childress (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene (kulia) kwenye Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini .
  Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akiagana na Balozi wa Marekani Nchini, Mark Childress (kushoto) mara baada ya mazungumzo kwenye ofisi za Wizara ya Nishati na Madini.

  0 0

  Katika siku za hivi karibuni kumeibuka tabia ya baadhi ya watu wachache wasiofahamika kutunga na kusambaza ujumbe kupitia simu za mikononi na mitandao mbalimbali ya kijamii wenye lengo la kuwatia hofu wananchi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria. Aidha, watu hao wanaosambaza taarifa hizo wanajifanya kwamba taarifa hizo zimetoka kwenye taasisi za kimataifa na taasisi zingine zinazoaminika jambo ambalo siyo kweli.

  Jeshi la Polisi nchini linawataka wote wenye tabia hiyo kuacha mara moja na badala yake, endapo mtu yeyote anayo taarifa ya uhalifu wa aina yoyote ama kikundi chochote cha uhalifu atoe taarifa hiyo katika kituo chochote cha Polisi au kupitia simu za makamanda wa polisi wa mikoa ama vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili taarifa hizo ziweze kufanyiwa kazi haraka.

  Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa taarifa zote zinazopokelewa ili kuhakikisha kwamba usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika. Hata hivyo, Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kusambaza ujumbe wenye mlengo wa upotoshaji, uchochezi ama kuwatia hofu wananchi.

  Imetolewa na:-
  Advera Bulimba -SSP
  Msemaji wa Jeshi la Polisi.

  0 0

  Na Avila Kakingo,Globu ya jamii

  MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA), kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita imekusanya zaidi ya Sh. Bilioni 258 zilizotokana na faini ya bidhaa mbalimbali za magendo.

  Hayo ameyasema leo Mkurugenzi huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es salaam,amesema TRA inaungana na jeshi la Polisi katika kukamata watu wanaojihusisha na usafirishaji na uuzaji wa bidhaa za magendo ambazo zinaisababishia serikali kukosa mapato.

  Amesema kwa Mkoa wa Kagera zaidi ya Sh.milioni 120 zilizotokana na pombe ya aina ya signature Vodka katoni 2043 kutoka nchini Uganda sawa na lita 24,516 yenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 61, zilizosafrishwa kwa jahazi la MV Tabasamu lenye namba za usajili MTZ 0541.

  Hata hivyo amesema Mkoa wa Morogoro kodi ya zaidi ya Sh.milioni 66 ilipatikana baada ya kukamata madumu 1599 ya lita 20 za mafuta ya kupikia yenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 65 ambapo wakwepa kodi hao walilipa faini pamoja na kodi waliyokuwa wakikwepa na Mkoa wa Tanga madumu 888 ya mafuta ya lita 20 yalikuwa na thamani ya zaidi ya sh.milioni 15 yaliyokamatwa eneo la Kwame katika bandari bubu ya wilayani Mkinga.

  Kayombo amesema katika Mkoa wa Arusha jumla ya lita 2290 za mafuta ya taa zenye thamani ya zaidi ya sh.milioni mbili,mafuta hayo yalikuwa yakisafirishwa kwa gari aina ya Toyota hiace iliyokuwa ikisafirishwa kutoka Holili Kwenda Mkoani Moshi.
  Mkurugenzi huduma na elimu kwa mlipa kodi,Richard Kayombo akizungumza leo na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akiwataka wananchi kutoa taarifa ya bidhaa zinazosafirishwa kwa njia za magendo, katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO,jijini Dar es Salaam. kushoto ni Meneja elimu kwa mlipa kodi,Diana Masala na kulia ni Mkurugenzi msaidizi Idaya ya habari Maelezo Zamaradi Kawawa.(Picha na Avila Kakingo).

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi kuhusu operesheni tokomeza Jaji(Mstaafu) Balozi Hamisi Amiri Msumi akimkabithi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ripoti ya Uchunguzi wa Tume hiyo katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Rais Kikwete aliiteua tume hiyo mwaka jana kuchunguza tuhuma za uvunjifu wa sheria katika utekelezaji wa operesheni hiyo.
  Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya Uchunguzi wa operesheni Tokomomeza ikulu leo. picha na Freddy Maro.

  0 0
 • 04/10/15--10:00: DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI

 • 0 0

  Mashabiki wa soka kesho watawashuhudia wachezaji wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania, Patrick Kluivert, Gaizka Mendieta, Anderson de Sousa “Deco” Francesco Coco na Luis Garcia wakionyeshana kazi na wakali wa Tanzania kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
  Hii itakuwa mara ya pili kwa Watanzania kushuhudia mastaa hao wa zamani wakikipiga kwenye uwanja huo baada ya wale wa Real Madrid waliokuwa chini ya Luis Figo, Christian Karembeu na Fabio Cannavaro wakicheza kwenye uwanja huo kwa mara ya kwanza na kushuhudiwa na Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete. 
  Kikosi cha FC Barcelona kimesheheni wachezaji nyota wengi mbali ya Kluivert na wenzake ambao kwa mashabiki wa soka ni majina maarufu. Wachezaji wengine ambao wanatarajia kushuka leo uwanjani chini ya kocha maarufu, Johan Cruyff ni pamoja na makipa nyota, Jesus Mariano Angoy Gil na Robert Oscar Bonano. 
  Wengini ni Sergi Barjuan Esclusa, Albert Toams Sobrepera, Luis Milla Aspas, Lluis Carrreras Ferrer, Miguel Angel Nadal Homar, Ion Andoni Goikoetxea Lasa, Oscar Arpon Ochoa, Santiago Ezquerro Marin, Javier Villena Mulero, Magin Civantos Martinez, Mateo Segura Capellades na Simao Sabrosa. 
  Kocha wa timu hiyo, Cruyff alisema kuwa wamekuja kuonyesha vipaji vyao vya zamani vilivyotukuka na hakuna wa kuwazuia kushinda katika mechi hiyo. Alisema kuwa wachezaji wake wegi japo wameacha soka, bado wanajihusisha kwa kufundisha na wengine kufanya mazoezi kwa ajili ya timu yao “FC Barcelona Legends”. 
  “Tupo vizuri, tumejiandaa kwa ajili ya kuweka historia, tunajua wenyeji wataleta upinzani, lakini sisi ndiyo tutakuwa washindi,” alisema Cruyff kwa kifupi. Mratibu wa mechi hiyo kutoka kampuni ya Primetime Promotion, Stuart Kambona alisema kuwa maandalizi yamekamilika na kikosi cha Tanzania Stars kitakuwa na nyota kama Manyika, Kaseja Shadrack Nsajigwa, Abubakari Kombo, Mustapha Hozza, Salvatory Edward, Amour Aziz, na Yusuph Macho. Wengine kwa mujibu wa Kambona ni Shaban Ramadhan, Dua Saidi, Nassoro Bwanga, Mohamed Hussein, Steven Nyenge, Mwanamtwa Kihwelu, Edibily Lunyamila, Henry Morris, Haruna Moshi, Bitta John, Madaraka Selemani, Deo Lucas, Bakari Malima, Thomas Kipese, Khatibu Sinapo na Nico Nyagawa. Kambona alitaja viingilio katika mchezo huo kuwa ni Sh 7,000 kwa viti vya kijani, Sh10,000 (blue), Sh20,000 (Orange), Sh30,000 (VIP C), Sh50,000 (VIP B) na SH300,000 for VIP A.
    Kocha wa magwiji wa Barcelona Johan Cryuff mwenye shati nyeupe akishuka kwenye ndege ya serikali tayari kwa mechi dhidi ya magwiji wa tanzania itakayopigwa kwenye uwanja wa taifa.
   Mchezaji wa zamani wa Liverpool na Barcelona, Luis Garcia mwenye fulana nyeupe akishuka kwenye ndege 
  Msafara wa wachezaji na viongozi wa hotel ya Ledger Plaza bahari beach wakiwa na wachezaji wa barcelona wakielekea kwenye chumba maalum tayari kuzungumza na waandishi wa habari
   Meneja mkuu wa hotel ya Ledger Plaza bahari beach, Wissem Souifi (mwenye tai) akibadilishana mawazo na kocha wa barcelona Johan cryuff huku wakielekea kwenye mkutano na waandishi wa habari
  Luis garcia ( kulia) akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari. wengine katika picha ni Kocha Johan Cryuff (katikati) na kiungo machachari, Gaizka Mendieta

  0 0  0 0  0 0


  0 0

  Mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma na mikoa ya jirani juzi jumanne tarehe 7 /04/2015  karume DAY walijitokeza kwa wingi kwa semina kuhusu biashara ya mtandao ambayo ni biashara ambayo ya karne ya 21 na kuendelea kukua kwa kasi duniani pia hapa nchini na kuwezesha kutengeneza mamilionea kwa wingi bila kujali kiwango chao cha elimu wala kipato na pia huanza kwa mtaji kidogo na bila mkopo toka benki.

  Mfanyabiashara wa kimataifa na mjasiriamali aliyefanikiwa katika biashara ya mtandao dada Mariam Njemu alikuwa ni mmoja wa wazungumzaji waliotoa hamasa kubwa kwa umati wa wakazi wa Dodoma na mikoa ya jirani  uliojaa kupata mafunzo ya kuweza kutimiza ndoto zao kwa kufanya biashara hii iliyoaminika na kufanikisha kuwezesha kupatikana mamilionea wengi ndani na nje ya Tanzania 

  \Mmoja ya wafanyabiashara  wakubwa waliofanikiwa katika biashara ya mtandao toka mkoa wa Dodoma Ndg George akipozi na wadau wengine wakati semina ikiendelea 

  Mkurungezi wa MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA na  KAJO ITECH Ndg Krantz Mwantepele ambaye mtaalamu wa biashara ya mtandao na mhamasishaji wa mafanikio akipata taswira na mfanyabishara aliyefanikiwa kwa biashara hiyo toka mkoa wa Dodoma ndg Patrick komba  na mdau mwingine.


  Mfanyabiashara wa kimataifa na mjasiriamali aliyefanikiwa katika biashara ya mtandao dada Mariam Njemu alikuwa ni mmoja wa wazungumzaji waliotoa hamasa kubwa kwa umati wa wakazi wa Dodoma na mikoa ya jirani  uliojaa kupata mafunzo ya kuweza kutimiza ndoto zao kwa kufanya biashara hii iliyoaminika na kufanikisha kuwezesha kupatikana mamilionea wengi ndani na nje ya Tanzania Semina ilifanyika jumanne wiki hii katika hoteli ya Dodoma hotel. Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   
  Rais wa Heshima wa Timu ya Barcelona Kocha Johan Cruyff, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar alipofika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.

  Kikosi cha Wachezaji wa Zamani wa Timu ya Barcelona wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwasili Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakitokea Arusha , wakiwa Zanzibar kwa Mualiko wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, kutembelea Zanzibar kujionea Vivutio vya Utalii na kujionea Vipaji vya Wachezaji Vijana wanaocheza katika timu mbalimbali za Watoto.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein akipokabidhiwa Jezi ya Bacelona namba 14 ya mchezahji wa zamzni akiwa kocha Johan Cruyff (kushoto)wakati wa hafla fupi ya chakula jioni  iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar timu hiyo ilipokutana na Rais.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 797 | 798 | (Page 799) | 800 | 801 | .... | 3270 | newer