Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

UTEUZI WA MWENYEKITI NA WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI YA BODI YA KOROSHO TANZANIA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa mamlaka aliyopewa chini  ya kifungu cha 4(1) cha Sheria ya Korosho ya mwaka 2009  (Sura ya 203 ya Sheria za Tanzania), amemteua Mhe. Anna  Margareth Abdallah (MB) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Korosho. 

Aidha, Mhe. Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi hiyo ya Wakurugenzi kwa mujibu wa kifungu  cha 4(1) cha Sheria ya Korosho ya mwaka 2009  (Sura ya 203 ya Sheria za Tanzania):-


1.    Joseph Florian Haule - Mwakilishi wa wabanguaji korosho nchini.

2.    Bw. Thomas Chatanda - Mwakilishi wa wakulima wa korosho 

3.    Mhe. Mudhihir M. Mudhihir- mtaalamu mwenye uzoefu kwenye sekta ya korosho  

4.    Bw. Rashid M. Serungwi- Mwakilishi wa wakulima wa korosho 

5.    Dkt Louis  Kagusa - Mtafiti wa Korosho, anayewakilishwa watafiti wa korosho 

6.    Bw. Mwinyikondo Lila - Mtaalamu mwenye uzoefu kwenye sekta ya korosho  

7.    Bw. Edgar Maokola Majogo - Mwakilishi wa wabanguaji wa korosho 

8.    Bibi Belinda P. Kyesi - Mwakilishi wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika.

Uteuzi huu  ni wa miaka mitatu na unaanza rasmi  tarehe 23 Februari, 2015.

IMETOLEWA NA:

 Sophia E. Kaduma
KATIBU MKUU

MWAROBAINI WA MIGOGORO YA WAFANYABIASHARA WA AFRIKA MASHARIKI WAPATIKANA

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii.

Wadau wa uwekezaji, wanasheria wa Afrika Mashariki wameunda chombo kitakachotatua migogoro mbalimbali kwa njia usuluhishi ili kuweza kukuza biashara kwa nchi wanachama.

Akizungumza leo katika Mkutano wa Kimataifa wa Wadau wa Chombo cha Kutatua migogoro kwa njia ya Usuluhishi (EACIA) uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam, Jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki Kitengo cha Usuluhishi, Fakihi Jundu amesema kila nchi mwanachama wa Afrika Mashariki inasheria zake katika kuweza kutatua migogoro ya mikataba ya kibiashara, kunahitaji chombo cha usuluhishi nje ya mahakama katika kuhakikisha wawekezaji katika nchi mwanachama kutoathirika na uwekezaji sehemu husika.

Amesema kuwepo kwa chombo hicho ni kwa malalamiko mengi ya migogoro ya kimkataba ikiwa ni kuhusisha watalaam kila nchi katika kufanya ufumbuzi wa migogoro.

Naye Balozi wa Namibia nchini, Japhet Isaac amesema amejifunza vitu vingi jinsi na watu watakapotumia fursa hiyo katika uwekezaji katika utatuaji wa migogoro ya uwekezaji kwa nchi mwanachama wa afrika Mashariki.
Jaji Mstaafu,Thomas Mihayo akichangia maada Wadau katika Mkutano wa Kimataifa wa Kutatua migogoro ya Wafanyabiashara wa Nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam.
Jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki,Kitengo Usuluhishi,Fakihi Jundu akizungumza na vyombo vya habari katika Mkutano wa Kimataifa wa Kutatua migogoro ya Wafanyabiashara wa Nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Namibia Nchini,Japhet Isaac akizungumza na vyombo vya habari katika Mkutano wa Kimataifa wa Kutatua migogoro ya Wafanyabiashara wa Nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wadau katika Mkutano wa Kimataifa wa Kutatua migogoro ya Wafanyabiashara wa Nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii).

DCB YAZIDI KUPAA KWA KUINUA WAJASIRIAMALI

$
0
0
Mwenyekiti wa bodi wa Banki ya Wananchi wa Dar es Salaam(DCB),Balozi Paul Rupia akizungumza na waandishia wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuwasilisha matokeo ya uendeshaji wa benki hiyo,amesema kipindi cha uendeshaji wa benki hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa bodi wa Banki ya Wananchi wa Dar es Salaam(DCB),Balozi Paul Rupia akizungumza na waandishia wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuwasilisha matokeo ya uendeshaji wa benki hiyo,amesema kipindi cha uendeshaji wa benki hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Edmund Mkwawa.
Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa bodi wa Banki ya Wananchi wa Dar es Salaam(DCB),Balozi Paul Rupia wakati wa kuwasilisha matokeo ya uendeshaji wa benki hiyo,amesema kipindi cha uendeshaji wa benki hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka)

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

BENKI ya Wananchi ya Dar es Salaam (DCB) imetoa mikopo yenye dhamani ya Sh.Bilioni 363.3 kwa wajasiriamali 362,507 kati ya hao wajasiriamali wadogo kupitia vikundi ni 156,718 katika Manispaa za Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo, Balozi Paul Rupia amesema kipindi cha uendeshaji wa benki hiyo kwa miaka miwili, amana ilifikia sh. bilioni 113 ikiwa ni asilimia tano za amana sh.bilioni 108 ambazo zilipatikana mwaka uliopita.

Rupia amesema mikopo kwa mwaka uliopita iliongezeka kwa asilimia tisa kutoka sh.bilioni 75 hadi kufikia sh.bilioni 82.4 kwa mwaka huu na mali zimeongezeka kwa asilimia 34  kutoka sh.bilioni 117 mwaka jana na kufikia sh.bilioni 157 mwaka huu.

Amesema faida zilizopatikana kwa mwaka uliopita ilikuwa ni sh.bilioni 3.77 baada ya kutolewa kodi ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia mbili  ukilinganiasha na faida ya bilioni 3.71 iliopatikana mwaka 2013.

Rupia amesema katika mikopo yote iliotolewa na benki hiyo asilimia 80 ni wanawake ambao wanajishughulisha na ujasiriamali na idadi ya wanawake imekuwa ikiongezeka kila mwaka.

safari ya mwisho ya Mpiganaji Bernard Rwebangira

$
0
0

Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Bernard Rwebangira likiwa tayari kwa safari ya kwenda kwenye nyumba yake ya milele kwenye Makaburi ya Kawe,Jijini Dar es salaam leo.Marehemu Bernard Rwebangira aliwahi kuwa Mpiga picha wa Kampuni ya TSN wachapishaji wa Magazeti ya Daily News, Sunday News pamoja na Habari leo.Mungu aiweke roho ya Marehemu mahapa pema Peponi, Amin.

Sehemu ya Ndugu wa Marehemu Bernard Rwebangira wakiwa ni wenye huzuni kubwa kuondokewa na Mpendwa wao, wakati wa Ibada ya kuaga mwili iliyofanyika leo Nyumbani kwao, Mbezi Beach jijini Dar es salaam.

Waombolezaji wakiwa Msibani hapo.
Na hii ndio ilikuwa Safari ya Mwisho ya Mpiganaji Bernard Rwebangira kwenye Makaburi ya Kawe, jijini Dar es salaam leo.

TAROWU YAWATAHADHARISHA MADEREVA KUTOJIHUSISHA NA MIGOMO KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama wafanyakazi wa sekta ya usafirishaji
,Sharifu Mohamed akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salam juu ya wafanyakazi wa sekta hiyo kutojihusisha na migomo ,Kuhoto  Katibu Mkuu  Salum Abdallaha TAROWU,kulia Mlezi wa TAROWU,Yakuub Rajabu (Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii)

Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

CHAMA cha  wafanyakazi wa usafirishaji kwa njia ya barabara Tanzania (TAROWU)  kimewatahadharisha  wafanyakazi wa sekta ya usafirishaji  kutojihusisha na mgomo katika sekta ya usafirishaji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chama hicho,Sharifu Mohamed amesema wafanyakazi wa sekta ya usafirishaji wakijihusisha katika migomo watasababisha kushuka kwa uchumi kutokana na sekta hiyo ilivyokuwa muhimu. 

Mohamed amesema serikali inatakiwa kuchukua maamuzi magumu kwa wale ambao watahusika na migomo ambayo inalenga kupoteza haki za wafanyakazi katika sekta hiyo.

Amesema madai yanayotolewa na wafanyakazi wa sekta ya usafirishaji kuwa serikali imeweka sheria ya kuwatoza madereva sh.550,000 hayana ukweli wowote ni viongozi kutaka kuhalalisha mgomo huo.

Mohamed amesema waajiri wanatakiwa kuwalipia gharama za mafunzo kwa madereva wao ili waweze kufanya kazi hiyo kwa ufanisi.

Jumuiya Watanzania wanaoishi Scandinavia yakutana nchini Denmark

$
0
0
Picha ya pamoja ya wana Jumuiya Watanzania wanaoishi nchi za Scandinavia na Ujumbe kutoka Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar na Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania Sweden.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais wa Zanzibar na Utawala Bora, ndugu Salum Maulid Salum akiwa mgeni wa heshima katika mkutano wa mwaka wa wana Diaspora Scandinavia uliofanyika April 4, 2015 nchini Denmark. Kulia ni afisa ubalozi Bw. Jacob Msekwa
Mratabu wa Diaspora,Ofisi ya Rais Ikulu na Ushirikiano wa Kimataifa Zanzibar Ndugu Hassan Hafidh akisikiliza kwa makani maoni ya wana Diaspora Scandinavia.
Mwakilishi mkaazi wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchi za  Scandinavia, ndugu Hamad Hamad akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa miradi mbali mbali ya Jumuiya Zanzibar.

Mangula awataka viongozi wa dini wasiwapotoshe wananchi kuhusiana na kuwapo kwa masuala ya dini katika katiba pendekezwa

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa CCM bara, Philip Mangulla akizungumza na wanafunzi na waalimu wa shule ya Hagafilo mkoani Njombe kuhusiana na katiba pendekezwa na utofauti kati ya katiba pendekezwa na ya sasa.
wanafunzi na waalimu wakimsikiliza Makamu mwenyekiti wa CCM bara Philip Mangula juzi wakati akiwapa ufafanuzi wa katiba Pendekezwa.(picha na furaha eliabu wa www.eliabu.blogspot.com)

Na Furaha Eliab, Njombe

MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) - Bara, Philip Mangula amesema kuwa viongozi wa dini wasiwapotoshe wananchi kuhusiana na kuwapo kwa masuala ya dini katika katiba pendekezwa na kuwataka wamuonyeshe kipengele kinacho taja masuala ya dini na mahakama ya Kadhi.

Akizunzungumza na wanafunzi wa sekondari, Chuo na walimu katika shule ya Hagafilo Mkoani Njombe wakati akitoe elimu ya katiba pendekezwa , amesema kuwa ameisoma katika yote na hajaona kipengele kinacho zungumzia masuala ya udini wala mahakama ya kadhi.

Lakini hata hivyo viongozi wa dini wanapinga mswada wa mahakama ya kadhi kupitishwa bungeni na kuwa sheria.

Amesema kuwa alikuwa katika kanisa moja anako Sali mchungaji wake alisema kuwa waumini wasiipegie kura katiba pendekezwa kwa kuwa ina masuala ya Mahakama ya Kadhi alipo muuliza ni katika kipengele gani kinacho zungumzia mahakama hiyo mchungaji huyo hata kipengele hicho alisema hakifahamu.

 Amesema kuwa katiba hiyo haina kipengele hata kimoja kinachozungumzia dini yoyote na kunakipengele kinacho zungumzia utawala wa sheria na kuwapo kwa mahakama huru

Amesema kuwa katika katiba pendekezwa kuna misingi ya utawala bora na umiliki wa arhi na kuwa ardhi hiyo inatunza na kuwa ni mali ya mtanzania wa kizazi cha sasa na cha baadae.

Katika hatua nyingine Mangula ameungana na kauli ya kiongozi katoriki Kadrinari Polinal Pengo kuhusiana na kuwahusu wananchi kuchukua maamuzi yao wenyewe juu ya kupiga kura ya ndio au hapana.

Amesema kuwa wananchi wakiisoma katiba wao wenyewe wakaielewa kama kuna mapungufu watayaona waikatae wao wenyewe na wanao sema isipigiwe kura wawe na hoja kwanini isipigiwe kura na sio wanasema hivyo bila kuwa na hoja sahihi

USIKOSE KUFATILIA MICHEZO YA LIGI KUU YA UINGEREZA KUPITIA SUPERSPORT NDANI YA DSTV PEKEE


Rais Kikwete afungua Mkutano wa Kimataifa wa Lishe Dar es Salaam

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wanaoshiriki mkutano unaohiusu lishe bora unaoratibiwa na Sun Lead Group's Visioning Sub Group(VSG) uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
Rais Kikwete akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kufungua mkutano unaohusu lishe uliowakutanisha wataalamu wa lishe kutoka mataifa mbalimbali uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam(picha na Freddy Maro).

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA NCHI MAENDELEO NA FRANCOPHONIE WA UFARANSA NA UJUMBE WAKE, LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kumkaribisha Ofisini kwake Waziri wa Nchi Maendeleo na Francophonie wa Ufaransa Mhe. Annick Girardin, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo April 09, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Nchi Maendeleo na Francophonie wa Ufaransa Mhe. Annick Girardin aliyeongoza ujumbe wa watu tisa, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo April 09, 2015.

NexLaw Advocates watembelea Vituo viwili vya kulelea watoto yatima jijini Dar es salaam

$
0
0
Ikiwa moja kati ya huduma zake za ‘Corporate Social Responsibility’ kwa jamii zitolewazo na NexLaw Advocates tarehe 4 April 2015 NexLaw Advocates ilitembelea vituo viwili vya watoto jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka. 
Vituo vilivyotembelewa na kampuni ya NexLaw Advocates ni House of Blue Hope ya Mabibo ambacho ni kituo cha kulelea watoto yatima na wasiojiweza na kituo cha watoto cha Msimbazi Children’s Home Centre cha Msimbazi jijini Dar es Salaam Home Centre. 
 NexLaw Advocates ilitoa mchango wa vifaa vya shule, vyakula pamoja na vifaa vingine vya usafi kwa kituo cha watoto cha House of Blue kilichopo Mabibo, Dar es Salaam. Na katika kituo cha watoto cha Msimbazi Children Home Centre wafanyakazi wa NexLAw Advocates walipata chakula cha mchanapamoja na wafanyakazi wa kituo hicho pamoja na kutoa Zawadi mbalimbali zikiwemo matunda, vyakula na Zawadi zingine ndogondogo. 
 Shughuli hizi mbili zilichochewa na dhima ya NexLaw Advocates kitengo cha ‘Corporate Social Responsibility’ kuhakikisha kuwa inatambua mchango na kuunga mkono shughuli zinazofanywa na taasisi, vikundi na watu binafsi katika kuwasaidia na kuwalea watoto na vijana wasiojiweza na walio kwenye mazingira magumu. 
 Katika vituo hivyo vitu mbalimbali vilitolewa ambapo katika kituo cha Msimbazi Children’s Home Centre kulikuwa na chakula cha mchana pamoja na wafanyakazi wote. Ikiwa ni moja ya sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii , kukumbuka na kuthamini mchango wa wafanyakazi wanaowalea na kuwaangalia watoto katika vituo vyote. 
Pia kama mchango kidogo ofisi ilinunua zawadi mbalimbali kwa ajili ya watoto na wahudumu katika vituo vyote viwili.
 Baadhi ya wafanyakazi wa NexLaw Advocates chini ya jengo  la PPF TOWER (Zilipo ofisi za kampuni hiyo) wakipakia vitu kwenye gari kabla ya kuanza safari kuelekea Vituo viwili vya kulelea watoto ambavyo ni House of Blue Hope kilichopo Mabibo na Msimbazi Children’s Home vilivyopo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa NexLaw Advocates wakielekea kukabidhi bidhaa zilizopelekwa Msimbazi Children’s Home  Centre cha Msimbazi jijini Dar es salaam

 Baadhi ya wafanyakazi wa NexLaw Advocates wakielekea kukabidhi bidhaa zilizopelekwa Msimbazi Children’s Home  Centre cha Msimbazi jijini Dar es salaam

 Sister Anna Francis mlezi wa kituo cha watoto cha Msimbazi Children’s Home wakijadili jambo na wafanyakazi wa NexLaw Advocates.
 Wafanyakazi wa NexLaw Advocates wakipata chakula cha mchana pamoja na wafanyakazi wa Msimbazi Children’s Home Centre. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


DKT. SHEIN AFANYA ZIARA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA ABEID AMANI KARUME, ZANZIBAR

$
0
0
Mkuu wa Kikoso cha Zimamoto Zanzibar Kamishna Ali Abdalla Maalim Ussi akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipotembelea kiyuo cha Zima moato kiliopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume alipofanya ziara maalum leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mshauri mwelekezi wa kampuni ya adpi ya Ufaransa Guillaume VERNA wakati alipofanya ziara maalum ya kutembelea maendeleo ya Ujenzi wa jengo hilo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Abiria Terminal II Yasser De Costa katika Wizara ya Miundimbinu na Mawasiliano wakati alipofanya ziara maalum ya kutembelea maendeleo ya Ujenzi wa jengo la Abiria Terminal II katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume leo.

#TipsForLife by bongo celebrity

$
0
0
 Don't know what to cook but have few stuff in the fridge? On www.supercook.com you can enter the ingredients you have readily available and it will tell you what meals you can make as well as how you can make them.

#TipsForLife: You can go on  www.NameChk.com    to see every website where your username has been used.

#TipsForLife Are Brought To You By www.BongoCelebrity.com

UTT AMIS YATOA ELIMU YA MIFUKO YA UWEKEZAJI WA PAMOJA KWA WASHIRIKI WA MKUTANO MKUU WA 31 WA ALAT

$
0
0
Mifuko ya uwekezaji wa pamoja ni fursa mbadala inayowezasha watu, vikundi,taasisi na kampuni sawa na mahitaji yao kuwekeza pesa zao kwa meneja wa mfuko (UTT AMIS) kisha meneja huwekeza fedha hizo katika masoko ya fedha na masoko ya mitaji kulingana na waraka wa makubaliono. Faida ipatikanayo hugawanywa kwa wawekezaji kulingana na uwiano wa uwekezaji waliofanya katika mfuko husika.


Mifuko hii huwawezesha wawekezaji kuweka akiba na kuwekeza fedha zao na zikakua zaidi.Hatimaye huwawezesha kufanya uwekezaji zaidi katika shughuli za ujasiriamali,kupeleka watoto shule au kufanya shughuli zozote za kiuchumi.

Mpaka sasa UTT AMIS inaendesha mifuko mitano ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi yenye zaidi ya thamani ya Shilingi bilioni 235.

Mifuko yote hii imeweza kukidhi vigezo  muhimu vya uwekezaji ambavyo ni Usalama,Ukwasi na Faida (Safety, Liquidity and Returns).  Wawekezaji wote wananufaika  kwa kupata faida shindani, uwekezaji mseto hufanyika ili kupunguza hatari za uwekezaji,utalaamu wa meneja wa mifuko,unafuu wa mkubwa wa gharama na uwazi kwani bei halisi ya vipande vya mifuko hutangazwa kila siku za kazi.
Ofisa Masoko na Uhusiano UTT AMIS, Rahim Mwanga,  akitoa maelezo kuhusiana na mifuko ya uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa na UTT AMIS kwa Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia (kushoto)  na  Naibu Waziri TAMISEMI, Aggrey Mwanri wakati wa Mkutano Mkuu wa  31 wa ALAT. 
 Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia akisaini kitabu cha wageni katika banda la UTT AMIS.
 Naibu Waziri wa Elimu, Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni.  
Mmoja wa watu waliohudhuria Mkutano Mkuu wa 31 wa ALAT akipata maelezo kuhusiana na mifuko ya uwekezaji wa pamoja kutoka kwa Ofisa Masoko na Uhusiano UTT AMIS, Rahim Mwanga. Katikati ni Ofisa wa UTT AMIS, Waziri Ramadhani.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI TANZANIA BW.JOHN CASMIR MINJA AHUDHURIA MAHAFALI YA KUMALIZA MAFUNZO YA UASKARI MAGEREZA NCHINI UGANDA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania Bw. John .C. Minja wakwanza kushoto akiwaongoza Wakuu wa Magereza Wanachama ACSA (Nchi Wanachama wanaounda Taasisi zinazohusika na Urekebishaji/Magereza )Barani Afrika katika Maadhimisho ya kumaliza Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza Nchini Uganda,sherehe zilizofanyika leo tarehe 9 April,2015 katika Viwanja vya Kololo Kampala Uganda.Wakwanza kulia ni Mkuu wa Magereza Nchini Angola.Maadhimisho hayo yalitanguliwa na Kikao cha siku moja cha Wakuu hao kilichofanyika jana tarehe 8 April,2015.
 Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania mwenye nguo za kijana akisalimiana na Mgeni wa heshima katika sherehe hizo Mhe. Edward Sekandi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Uganda,aliye mwakilisha  Rais wa  Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ambaye ndiye alipaswa kuwa Mgeni Rasmi.
 Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza Nchini Uganda wakipita kwa mwendo wa haraka huku wakitoa heshima mbele ya Mgeni Rasmi katika Sherehe hizo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe.Edward Sekandi,hayupo pichani.
  Makamu wa Rais Jamhuri ya Uganda Mhe.Edward Sekandi wa Nne kulia akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Magereza Nchi Wanachama wa Taasisi zinazohusika na masuala ya Urekebishaji/Magereza Barani Afrika. Wanne Kutoka kushoto ni Kamishna Jenerali Nchini Tanzania Bw. John C.Minja na Watatu kutoka kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Zambia Bw. Percy K. Chato.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Uganda Bw. JohnSon.O.R. Byabashaija Mafunzo hayo yameendeshwa na Chuo cha Mafunzo ya Awali ya Maafisa Magereza  Luzira.Mafunzo hayo yameendeshwa kwa muda wa miezi Tisa (9) na jumla ya Wanafunzi 1228 Wamehitimu Mafunzo na kupasishwa na Mgeni Rasmi kuwa Askari wa Magereza kwa vyeo vya Wdr kwa Wanaume na Wdrs kwa Wanawake.


AIRTEL NA NMB WAZINDUA HUDUMA YA KIFEDHA KWA NJIA YA MTANDAO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Naibu Waziri wa fedha na Uchumi Mh. Mwigulu Nchemba akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya miamala ya kifedha ya Airtel Money na Benki ya NMB katika hoteli ya  Selena jijini Dar es Salaam leo.
 Kaimu mtendaji  mkuu wa Benki ya NMB Tom Borghols akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya miamala ya kifedha ya Airtel Money na Benki ya NMB katika hoteli ya  Selena jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi mtendaji wa  Airtel  Sunil Colaso akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya miamala ya kifedha ya Airtel Money na Benki ya NMB katika hoteli ya  Selena jijini Dar es Salaam leo. 
Naibu waziri wa fedha   na Uchumi Mh. Mwigulu Nchemba (katikati) akizunzindua  huduma ya Airtel money  na Benki ya NMB wanaoshuhudia uzinduzi huo kulia ni  Kaimu mtendaji  mkuu wa Benki ya NMB Tom Borghols,  kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa  Airtel  Sunil Colaso.(Picha zote na Emmanuel Massaka.


Na Avila Kakingo Globu ya Jamii.

Wateja wa benki ya NMB  wamerahisishiwa  kazi kutokana na  benki hiyo kuungana na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel Tanzania  kwenye upande wa miamala ya fedha kwa urahisi na usalama zaidi.

Akizungumza Naibu Waziri wa fedha   na Uchumi Mh. Mwigulu Nchemba katika hoteli ya   Serena jijini Dar es Salaam leo  , amesisitiza kuwa huduma za Fedha kupitia simu za mkononi ni mhimu katika kuliletea maendeleo Taifa. Mwigulu  amesema kuwa ukuaji wa uchumi nchini umewasukuma watanzania kutumia simu zao za mkononi kupata taarifa kuhusu akaunti zao za benki popote pale walipo na wakati wowote.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya simu ya Airtel,Sunil Colaso, alisema kuwa umoja huu ni ishara ya mageuzi katika matumizi ya Teknolojia katika kuboresha masisha ya watanzania kupitia simu za mkononi.

Kwa njia hii wateja wa Airtel na benki ya NMB kwa pamoja wanaweza kuweka na kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti zao za Airtel Money kwenda kwenye akaunti zao za NMB. Alisema  Colaso.

 Pia katika uzinduzi huo utasaidia wateja wa Airtel kuweka na kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti zao za Benki na za NMB.

MALINZI AITAKIA KILA LA KHERI TWIGA STARS

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF Jamal Malinzi, ameitakia kila la kheri timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania (Twiga Stars) katika mchezo wake wa kesho wa marudaino dhidi ya timu ya Taifa ya Zambia (She-Polopolo) utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akiongea na wachezaji wa Twiga Star na benchi la Ufundi katika chakula cha pamoja cha mchana leo katika hosteli za TFF zilizopo Karume, Rais Malinzi amesema watanzania wote wana matumaini na timu yao kufanya vizuri kwenye mchezo huo wa marudiano.

Aidha Rais Malinzi amewaambia bechi la ufundi na wachezaji wa Twiga Stars kuwa pesa zote zitakazopatikana katika mchezo wa kesho baada ya makato ya Uwanja na VAT, wagawane kwa pamoja wachezaji na viongozi.

Naye Mgeni mualikwa Ryhs Torrington ambaye ni Mkurugenzi wa kituo cha Luninga cha Azam, alisema anaitakia kila la kheri Twiga Stars katika mchezo wao wa kesho, na kusema mechi hiyo itaonyeshwa moja kwa moja na Azamtv, hivyo waitumie vizuri nafasi hiyo kujitangaza kimataifa.

Kocha mkuu wa Twiga Stars Rogasian Kaijage na nahodha wake Sophia Mwasikili, wamewahakikishia ushindi katika mchezo wa kesho,  na kuwaomba watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuja kuwashangilia.

Mechi inatarajiwa kuanza majira ya saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, na tiketi za mchezo zitauzwa kesho saa 2 asubuhi eneo la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku viingilio vya mchezo huo vikiwa ni tsh. 5000 kwa VIP na tsh. 2000 kwa majukwaa yaliyobakia.

Twiga Stars ambayo katika mchezo wa awali iliibuka na ushindi wa mabao 4-2, inahitaji sare ya aina yoyote ili kuweza kufuzu kwa fainali za Michezo ya Afrika zitakazofanyika nchini Congo-Brazzavile mwezi Septemba.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

UZINDUZI WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO MKOANI MOROGORO TAREHE 9 APRILI, 2015

$
0
0
Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Dkt. Pindi H. Chana (MB) azindua rasmi Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto mkoani Morogoro tarehe 9 Aprili, 2015. Baraza hili linafanya kikao chake cha siku mbili kuanzia tarehe 9 hadi 10 Aprili, 2015.

Baraza la Wafanyakazi linaundwa na wawakilishi wa wafanyakazi wote wa Wizara na wanachaguliwa kwa mfumo wa haki na uwazi. Baraza hili ni chombo muhimu sana kwani uhalali na uundwaji wake upo kisheria. Madhumuni yake ni kuishauri Serikali katika ngazi ya Wizara na taasisi kuhusu usimamizi wa kazi, mwenendo wa utendaji wa kazi na Rasilimali watu ili kuleta tija katika sehemu ya kazi. Kubwa zaidi ni kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi.

Ni kupitia Baraza hili ambapo mwajiri hupata maoni ya watumishi na kuungana nao katika kujadili na kupitisha kwa pamoja maazimio ya utekelezaji kuhusu masuala yanayoihusu Wizara ili kuleta tija.

Mhe. Dkt. Pindi H. Chana amesisitiza kuwa Sekta ya Maendeleo ya Jamii ni muhimu katika uchumi wa nchi na ustawi wa jamii zetu kwa kuwa shughuli zake zinagusa moja kwa moja maisha ya kila siku ya jamii iwe katika maeneo ya mijini au vijijini.

Kutokana na ukweli huu na umuhimu wa sekta Baraza hili linatakiwa kujua kwa undani mafanikio, fursa na changamoto zinazoikabili Wizara na kushauri njia za kuleta ufanisi na kutatua matatizo yanayojitokeza kwa kutumia sera na sheria za Wizara na za nchi kwa ujumla.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto wakiwa katika Uzinduzi wa baraza hilo mkoani Morogoro tarehe 9 Aprili, 2015.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto katika picha ya pamoja na Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Dkt. Pindi Chana (MB) (waliokaa katikati), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Rajabu Rutengwe (wa pili kulia), Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Bw.Noeli Kazimoto (wa kwanza kulia), katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bibi Anna Maembe na naibu wake Bibi Nuru Millao (kushoto kwa Naibu waziri) mkoani Morogoro tarehe 9 Aprili, 2015. Picha na Hassan Mabuye

KEVERA AJITOA KWA VIJANA KATIKA KUIPIGA JEKI SEKTA YA MICHEZO

$
0
0
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)na Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Scolastica Kevera akikabidhi jezi kwa Nahodha wa Timu ya Twiga,Abuu Nido baada timu hiyo kuzishinda timu katika mechi zilizopigwa katika uwanja wa twiga Tabata Kiswani Jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi wa Globu ya Jamii.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)na Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Scolastica Kevera amesema kuwa yeye ni mwanamichezo ndio maana amejitoa kusaidia vijana katika sekta ya michezo kwa kutambua michezo ni ajira.

Akizungumza hivi karibani,Scolastica amesema ataendelea kujitoa kwa vijana katika michezo ili waweze kufika mbali na kuweza kusaidia watu wengine.

Scolastica amesema vijana wakijituma katika michezo wanaweza kupata mafanikio na kuweza kusaidia nchi kwa uchumi kuptia michezo.

dira ya dunia na BBC SWAHILI

Viewing all 109996 articles
Browse latest View live


Latest Images