Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 795 | 796 | (Page 797) | 798 | 799 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Na Mwandishi Wetu

  Kampuni ya Kimataifa ya Zest imezindua simu mpya zenye huduma zote muhimu kwa bei nafuu.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa simu hizo jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Salum Awadh amesema kuwa simu hizo ambazo ni imara zitauzwa kwa bei nafuu ili kila mtu aweze kununua.

  "tumeingiza sokoni simu mpya aina ya 7 Mobile ambazo zina huduma za mitandao ya kijamii ikiwemo Internet, Whatsap pamoja na Facebook huku bei yake ikiwa ni 35,000, aina nyingine ni Tablet inayojulikana kwa jina la ZestPad Tango ambayo inauzwa sh. 165,000.

  Aidha aliongeza kuwa mbali ya huduma muhimu za kijamii kama facebook pamoja na whatsap simu hizi pia wakati unachaji zinapojaa zinajizima zenyewe.

  "Tunameamua kuingiza sokoni simu zenye ubora wa hali ya juu ili kila mtu aweze kutumia simu za kisasa zenye gharama nafuu" alisema Mkurugenzi huyo".
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zest International, Salum Awadh akionyesha Tablet wakati wa uzinduzi wa aina mpya za simu  uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Kampuni ya Jumia, Michael Ryoba na Meneja Maendeleo ya Biashara, Rajab Smith. (Picha na Francis Dande).
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zest International, Salum Awadh akionyesha Tablet ambayo inauzwa kwa shilingi 165,000.
  Meneja wa Kampuni ya Jumia, Michael Ryoba akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.

  0 0

  Hayati Dkt. Mohamed Mhita

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt. Agnes Kijazi anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu (mstaafu) Dkt. Mohamed Mhita kilichotokea siku ya Jumatatu tarehe 06 Aprili 2015 katika hospitali ya Agakhan jijini Dar es Salaam.

  Dkt. Mhita alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa iliyokuwa Idara Kuu ya Hali ya Hewa kwa kipindi cha miaka 8 kuanzia 1992 hadi 1999 na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kwa kipindi cha miaka 9 kuanzia 1999 hadi 2008. Dr. Mhita kwa kushirikiana na uongozi wa iliyokuwa idara Kuu ya Hali ya Hewa alishiriki katika kuishauri Serikali kuhusu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kutoka iliyokuwa Idara Kuu ya Hali ya Hewa.

  Pamoja na nafasi ya Mkurugenzi Mkuu pia alikuwa Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani kuanzia mwaka 1992 hadi 2008. Alichaguliwa kuwa Mjumbe katika Baraza Kuu la Shirika la Hali ya Hewa Dunia kuanzia mwaka 1995 hadi 2007. Alichaguliwa kushika nafasi ya Rais wa Jumuiya ya Hali ya Hewa katika Bara la Afrika (RA 1) kuanzia mwaka 1998 hadi 2007. Dkt Mhita alikuwa Rais wa ‘Tanzania Meteorological Society’ sambamba na nafasi nyingine nyingi mbalimbali alizoshika ndani na nje ya nchi.

  Akielezea baadhi ya mambo makubwa yatakayomfanya Dkt. Mhita aendelee kukumbukwa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Dkt. Agnes Kijazi alisema ‘Dkt. Mhita atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika kuendeleza sayansi ya hali ya hewa hapa nchini, katika Bara la Afrika na Duniani kwa ujumla hususani katika ushiriki wake wa kuianzisha Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini kwa kuandaa dira (vision) na dhamira (mission) ya Mamlaka kwa kipindi cha miaka kumi na tano (15) kuanzia mwaka 2000 hadi 2015’.

  Dkt. Mohamed Mhita ni mmoja kati ya wanasayansi waliokuwa zao la chuo kikuu cha Stolkholm, Sweden ambako alitunukiwa shahada ya hali ya hewa (BSc. Met) mwaka 1977. Kuanzia mwaka 1981 hadi 1984 alikuwa mafunzoni katika chuo Kikuu cha Reading, Uingereza ambako alitunikiwa shahada ya uzamivu (PhD). Hapa nchini alipata mafunzo ya Sekondari katika shule za Tanga na Kamrimjee zote zikiwa mkoani Tanga.

  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inajumuika na familia, ndugu, jamaa na marafiki katika kuomboleza msiba huu. 

  Innalilah Wainnailaih Rajiun.

  IMETOLEWA NA: MONICA MUTONI

  AFISA MAHUSIANO MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

  0 0

  Neema Herbalist & Nutritional Foods Clinic ni wauzaji wa dawa mbalimbali za asili. Tunayo dawa nzuri ya asili inayo ondoa kitambi na kulifanya tumbo lako kuwa flat kabisa ndani ya siku kumi na nne.

  Dawa ni ya asili kabisa " Pure Herbal", haijachanganywa na kemikali yoyote na haina side effects kwa mtumiaji.

  BEI YAKE NI SHILINGI ELFU HAMSINI TU ( Tshs.50,000/=)

  Kwa wasio weza kufika ofisini kwetu tunawapelekea dawa moja kwa moja mahali walipo (DELIVERY)

  Kwa wateja wa mikoani, tunawatumia dawa kwa njia ya mabasi, kwa wateja waliopo Zanzibar tunawatumia dawa kwa njia ya meli na kwa wateja waliopo nje ya Tanzania, tunawatumia dawa kwa njia ya posta au DHL.

  Pia tunayo dawa bora kabisa ya nguvu za kiume iitwayo JIKO ambayo inatibu na kumaliza kabisa tatizo la nguvu za kiume ndani ya siku thelathini.

  Vile vile tunayo dawa ya asili inayosaidia kurudisha afya na mwili kwa mtu aliye dhoofika kwa magonjwa mbalimbali.

  Tunapatikana jijini DarEs salaam,katika eneo la Changanyikeni karibu na Chuo Cha Takwimu.

  Kufika ofisini kwetu, panda daladala za UBUNGO-CHANGANYIKENI kisha shuka kituo cha TAKWIMU halafu tembea hatua ishirini mbele kisha tazama upande wako wa kulia.

  Kwa maelezo zaidi,wasiliana nasi kwa simu 0766538384 na kwa taarifa zaidi kuhusu huduma zetu, tembelea website yetu kwa kubofya hapa.

  0 0

  Kilimo na Ufugaji wa Kisasa kwa maendeleo ya Jamii na kukataa umasikini kwa kujiajili ndiyo kauli kuu iliyotawala katika Semina ya Kilimo na Ufugaji wa kisasa iliyofanyika Jijini Dar es salaam ambapo washiriki walipata mafunzo na Elimu Bora juu ya Kilimo bora cha kisasa pamoja na ufugaji Semina iliyo ongozwa na Mjasiriamali mwanamke ambaye amethubutu Bi. Mary David Kinong'o.

  Katika Semina hiyo kulikuwa na mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kilimo cha kisasa cha kutumia Green houses ambapo , wanasemina walipata elimu ya umuhimu wa kilimo hicho ambacho hakichukui nafasi kubwa na kinaweza kufanyika mahali popote na kwa gharama nafuu ambapo kilimo kama cha Nyanya, Matunda na Mboga mboga kinaweza kikafanyika katika Green Houses.

  Pia walipata elimu juu ya ufugaji wa Samaki, Kuku, Kware pamoja na Matumizi ya Mashine za Kisasa za Kutotolea mayai Incubator, Chicken Cages za kisasa ambazo zinasaidia kuwatunza kuku vizuri na kupata faida zaidi, Mashine za kunyonyolea kuku na kutengenezea chakula cha kuku ili mfugaji asipate shida wakati wa kutafuta wapi apate mahali pa kufanya hayo na badala yake kuwa nayo mwenyewe nyumbani.

  Mwisho Mwendesha semina Bi. Mary David Aliwasisitiza watanzania kuwa wanaweza kuwa wajasiliamali na kujitegemea pia kupata kipato kikubwa kama wakifuata hatua bora za kilimo na ufugaji wa kisasa.


   Mjasiriamali na Muandaaji wa wa Semina ya Kilimo na Ufugaji wa Kisasa Bi. Mary David Kinong'o akitoa Maelezo juu ya Kilimo na Ufugaji wa kisasa ambapo aliwasisitiza Vijana na watu wote kujiunga na ujasiliamali na kuunda vikundi mbalimbali ili kujiendeleza kiuchumi.
  Wa kwanza Kulia ni Stella mmoja wa akina dada  ambaye amekuwa mfano mzuri wa kuigwa katika semina hiyo akieleza ujuzi  wake umuhimu wa mikutano kama hii ambapo yeye anafanya kilimo cha Mpunga ambapo alianza na kuvuna Gunia Mbili na sasa amefikisha mpaka Tani 100 na zaidi baada ya kupata elimu Bora ya Kilimo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  MWANAHABARI WA SIKU NYINGI NA ALIYEWAHI KUWA MPIGA PICHA WA KAMPUNI YA TSN (WACHAPISHAJI WA MAGAZETI YA DAILY NEWS,SUNDAY NEWS NA HABARI LEO), BW. BERNARD RWEBANGIRA (PICHANI) AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO NA MSIBA UPO NYUMBANI KWAO MBEZI BEACH, JIJINI DAR ES SALAAM.

  MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMINA
  0 0


  0 0
 • 04/08/15--03:38: bei ya Madafu leo

 • 0 0


  0 0

  East African Community Headquarters, Arusha, 8 April, 2015: The EAC Secretariat together with the East African Business Council (EABC) and CEOs of Media Houses are finalizing preparations for the 7th EAC-EABC Media Summit, which is to be held from 14 to 15 May 2015, at the Hyatt Kilimanjaro Hotel Dar es Salaam, Tanzania.  

  The 7th EAC-EABC Media Summit will bring together over 250 Media owners, CEOs, Publishers, Editors, prominent Media personalities and practitioners on a round table discussions under the theme: The Role of the Media in Deeping Democracy in the Region, with sub-themes on Democracy in the EAC: Achievements and Challenges; The Role of Media in Electoral Processes, and Regional Security, Business Environment and Media: Towards a Common Goal.

  “We see the Summit as a vehicle to increase the visibility of EAC’s flagship in the integration process and EAC-EABC joint activities through the media is commendable,” comments Mr. Kajubi Mukajanga, Chair of the Regional Preparatory Committee of the 7th Media Summit and also the Executive Secretary of Media Council of Tanzania (MCT).  “This will also be a time to network with and update the Media industry on the latest developments in the East African regional integration process,” he said.

  The Head of Corporate Communications and Public Affairs at the EAC Headquarters Owora Richard Othieno notes that the Media Summit is designed to, among others; advance the relationship between the EAC/EABC and the media, who have long been recognized as strategic partners for the Community in achieving its key objective of deepening and widening regional integration and development process.

  Launching the EAC Media Scholarship Fund sponsored by EAC-KfW-AKU, and announcing and recognizing Winners of the EAC Media Award Competition 2013/14 are expected at the Media Summit over a Gala Dinner.

  The East Africa Media Awards were originally launched during the 3rd Media Summit in Kampala, Uganda in 2009.  The first Awards ceremony was held during the 4th Summit in Nairobi, Kenya in 2011. This Media Awards are currently in the fourth year running. The judging process for 2013/14 concluded on 26th February, 2015. Twenty three winners have been identified for the Awards in different categories.

  Presentation on the first-ever EAC Media Caravan and a Field Visit to one of the upcoming local media houses in Dar es Salaam, Tanzania is set for the second day of the Summit. The Media Caravan is an EAC-GiZ initiative which will engage regional journalists on a road trip to each Partner State to independently report on the achievements of the Common Market Protocol since its launch in 2010.

  Online registration is now open at; http://www.mediasummit.eac.int/ or at the EAC Media Centre: mediacentre@eachq.org.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi cheti mwanafunzi mmojawapo katika mahafali hayo.
  Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kazi ya uchanaji wa mbao katika Shule ya Sekondari Chato. Mbao hizo hutumika katika kazi mbalimbali za ujenzi wa shule hiyo. Pia Dkt. Magufuli ameichangia shule hiyo kiasi cha Shilingi Milioni tano.
  Waziri Magufuli akikagua moja ya computer katika shule hiyo.kushoto kwake ni Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Mahendeka Mafele.


  0 0

   Makamu Mkuu wa Chuo cha Bagamoyo.Profesa Costa Mahalu akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya utumiaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika semina iliyofanyika leo katika hoteli ya New Afrika,Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi,Teknolojia na Mawasiliano,Profesa Patrick Makungu akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya utumiaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika semina iliyofanyika leo katika hoteli ya New Afrika,Jijini Dar es Salaam.
  Meneja Mradi wa Idara ya Uchumi na Mendeleo ,Mazingira na Utalii wa Afrika Kusini,Rolda Rapotu akizungumza na  katika semina ya wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano iliyofanyika  leo katika hoteli ya New Afrika ,Jijini Dar es Salaam.PICHA NA EMMANUEL MASSAKA

  =========  ==========  ===========

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
   
  Wizara ya Sayansi,Teknolojia na Mawasiliano imesema itaendelea kudhibiti matumizi ya mtandao katika kuhakikisha hayatumiki vibaya kwa watumiaji.

  Hayo ameyasema leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi,Teknolojia na Mawasiliano,Profesa Patrick Makungu wakati wa Semina ya Maendeleo ya Jamii na Utumiaji Teknolojia ya Habari na Mawasiliano iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya New Africa,Jijini Dar es Salaam.
   
  Makungu amesema kuwa Wizara ya Sayansi,Teknolojia na Mawasiliano imepitisha sheria ya matumizi ya mitandao katika kulinda ili kulinda matumizi hayo yasitumike vibaya na kuharibu sura ya nchi.Amesema kuwa tafiti mbalimbali za mitandao  zimeanza 2010 hali ambayo zinaendelea na kufanya hivyo itasaidia nchi kupata maendeleo katika sekta ya mawasiliano.
   
  Naye Mratibu wa Semina ya Maendeleo ya Jamii na Utumiaji Teknolojia ya Habari na Mawasilino,Profesa Benson Nindi amesema kuwa wanaufanya mradi huo katika suala zima la kutoa elimu juu ya utumiaji wa mitandao na serikali ya Tanzania inatakiwa kutunga sera ambayo itasaidia wananchi kwenda kasi na teknolojia ya habari na mawasiliano.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kulia), wakati kiongozi huyo alipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN) nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi wa Wizara hiyo, Harrison Mseke, anayefuata ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, Joyce Mends-Cole.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania. Rodriguez alimtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

   Mhadhiri wa Chuo Cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere,Shadrack Mwakalila akizungumza na waandishi wa habari  (hawapo pichani) juu ya kozi ya uongozi na maadili ya chuo hicho ,Kushoto ni Mhadhiri Msasidizi wa Chuo Cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere,Amon Katunzi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka)
   
  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

  Rais Dk.Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kozi ya uongozi na maadili iliyoanzishwa na Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere itayofanyika Aprili 13.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo,jijini Dar es Salaam,Mhadhiri w Chuo Kumbukumbu Cha Mwalimu Nyerere,Shadrack Mwakalila,amesema kozi hiyo watasoma kwa muda wa miezi mitatu na itakuwa endelevu.

  Mwakalila amesema  kozi hiy ni kujenga watu kuwa na maadili ya kutokana na jinsi alivyowajibika Mwalimu wakati wa uhai wake.

  Amesema watu wajitokeze katika kusoma kozi hiyo ambayo itasaidia kuwa viongozi na wenye maadili kutokana na kozi hiyo iliyoandaliwa.

  0 0

  Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mheshimiwa, Stephen M. Wasira (Mb), ametangaza kuwasimamisha kazi watendaji watatu wa Mamlaka ya Kuendeleza Bonde la Mto Rufiji (Yaani Rufiji River Basin Development Authority – RUBADA) kutokana na tuhuma mbalimbali za ubadhirifu wa fedha za umma na matumizi mabaya ya madaraka.

  Akitoa agizo hilo leo mbele ya Waandishi wa Habari, Waziri Wasira aliwataja Watendaji hao kuwa ni Bwana Aloyce L. Masanja – Kaimu Mkurugenzi Mkuu; Bibi Tabu Ndatulu – Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji; na Bwana Filozi John Mayayi – Mkurugenzi wa Fedha na Utawala.

  Taarifa ya Mheshimiwa Wasira imeanisha kuwa kati ya shilingi 2.748 billion zilizokuwa zimekusanywa kwa ajili uwekezaji, ni shlingi 714.606 milioni tu ndizo zimetumika kihalali wakati kiasi kilichobaki kimetumika bila kuzingatia sheria na kanununi za fedha za umma.

  Aidha, Bodi ya RUBADA imetakiwa kuteua Maafisa watakaokaimu nafasi za viongozi hao wakati mchakato wa kuwapata viongozi wa kudumu ukiendelea.

  Vilevile, mamlaka zingine ikiwa ni pamoja na vyombo vya dola kama vile TAKUKURU na Polisi wanaendelea na taratibu za kuwachukulia hatua viongozi hao kwa mujibu wa sheria za nchi.
  Mheshimiwa Wasira (kulia) akiongea na Waandishi wa habari (hawapo pichani). Katikati ni Katibu Mkuu Bibi Sophia Kaduma (katikati), na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Dkt. Yamungu Kayandabila.

  0 0

  Balozi Mdogo Mpya wa India Hapa Zanzibar Bwana Satendar Kumar akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
  Balozi Mdogo Mpya wa India Hapa Zanzibar Bwana Satendar Kumar akijitambulisha rasmi kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
  Balozi Seif akibadilishana mawazo na Balozi Mdogo Mpya wa India Hapa Zanzibar Bwana Satendar Kumar Ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akipokea zawadi kutoka kwa Balozi Mdogo Mpya wa India Hapa Zanzibar Bwana Satendar Kumar. Picha na – OMPR – ZNZ.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  ameyashauri  Makampuni  na Taasisi za uwekezaji  kutoka Nchini India kuwekeza miradi yao katika Visiwa vya Unguja na Pemba  ili kuitikia wito wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kukaribisha wawekezaji  mbali mbali kuwekeza hapa Nchini.

  Alisema India  bado ina nafasi pana  kwa Makampuni yake kuwekeza miradi yao ya Kiuchumi hasa katika Sekta ya Viwanda kama ilivyowahi kutumia fursa hiyo hapa Zanzibar katika miaka ya 80.

  Akizungumza na Balozi Mdogo  Mpya wa India hapa Zanzibar  Bwana  Satendar Kumar hapo Ofisini kwake Vuga  Mjini Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Sekta ya Viwanda  ni eneo muhimu katika kukuza uchumi na kupunguza Umaskini.

  Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa na malengo la kuimarisha sekta hiyo kwa azma ya  kulisaidia kundi kubwa la Vijana wasio na ajira ambalo limekuwa likiongezeka kila mwaka baada ya kumaliza masomo yao.

  Akizungumzia miradi mengine ya Kiuchumi na Maendeleo ya Kijamii Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliiomba Serikali ya India kupitia Balozi wake Mdogo  huyo kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika harakati za Maendeleo kwenye sekta hizo.

  Mapema Balozi Mdogo Mpya wa India hapa Zanzibar Bwana Satendar Kumar alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba uhusiano wa Kidiplomasia kati ya India na Tanzania ikiwemo Zanzibar utaendelea kuimarishwa siku hadi siku.

  Balozi Satendar alisema uhusiano huo umejengwa katika mpango Maalum wa Maendeleo wa India – Afrika  uliojikita kwa Wataalamu wa Nchi hiyo kusaidia taaluma katika sekta za afya, elimu, miradi ya Kazi za amali pamoja na Teknolojia ya Mawasiliano na Habari.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Afrika, Karibiani na Pacific, Balozi Patrick Gomes (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania katika Jumuiya ya Ulaya, Balozi Dk. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) baada kumaliza kikao cha kushauriana masuala mbalimbali ofisini kwa Balozi Kamala Brussels. Kulia ni Balozi Jagne msaidizi wa Balozi Gomes.

  0 0


  0 0

   Basi la Ngorika likiwa halitamaniki baada ya kugongana uso kwa uso la basi lingine la Kampuni ya RATCO katika ajali iliyotokea mapema leo kwenye eneo la Kijiji cha Mbweni, Mkata mkoani Tanga. kwa mujibu wa Ripota wetu aliopo eneo la tukio,inadaiwa kwamba mpaka sasa ni Watu kumi wamepoteza maisha katika ajali hiyo, akiwepo Dereva wa Basi la Ratco.Chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika mpaka sasa. Globu ya Jamii inafanya jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga kwa maelezo zaidi.
   Hivi ndivyo lionekanavyo Basi la Ratco baada ya kupata ajali hiyo leo.
   Basi la Ngorika lionekanavyo baada ya ajali hiyo.
   Askari Polisi walifika eneo la tukio kwa Wakati ili kuhakikisha usalama unapatikana eneo hilo.
  Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa, na inasikitisha sana.


  0 0

  Meneja Utawala wa Bayport Financial Services aliyezibwa macho, Evalyine Hall, akichagua koponi ya mmoja wa washindi wa Kopa Bayport kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, inayoendeshwa na taasisi hiyo ambapo washindi watatu ambao ni Hyasint Mbunda (Songea), Phaustine Mbilinyi (Dar es Salaam) na Allen Bishubo (Bukoba), walipatikana na kila mmoja kushinda Sh Milioni moja. Kushoto ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport, Ngula Cheyo na kushoto ni Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha, Humud Abdulhussein.

  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
   
  WASHINDI watatu waliokopa fedha kwa njia ya Mtandao wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, wamejishindia Sh Milioni moja kila mmoja, kutokana na shindano hilo lililoanzishwa maalum kwa ajili ya wateja wao waliomua kuutumia mtandao wao wa www.kopabayport.co.tz kupata huduma mbalimbali.

  Washindi hao wamepatikana kutoka kwenye droo ya mwezi wa Aprili, iliyoendeshwa na Bayport Financial Services kwa kusimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

  Meneja Utawala wa Bayport Financial Services Evelyine Hall katikati akisoma koponi ya mmoja wa washindi wa Kopa Bayport kwa njia ya Mtandao inayoondeshwa na taasisi hiyo ya kifedha. Kulia kwake ni Msimamizi wa Michezo ya Kubatisha Tanzania, Humud Abdulhussein na kushoto ni Ngula Cheyo, Meneja Masoko na Mawasiliano wa taasisi hiyo ya Bayport Financial Services.

  Akizungumza katika droo hiyo, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kwamba washindi hao watatu wamepatikana baada ya kuamua kukopa kwa njia ya mtandao wao waliyouzindua mwezi uliopita.
  Ngula Cheyo (katikati) ambaye ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services akizungumza jambo katika droo ya kutafutwa washindi watatu wa bahati nasibu inayoandaliwa na taasisi hiyo ambao kila mmoja alishinda Sh Milioni moja.

  “Tuliamua kuanzisha huduma ya kukopa kwa njia ya mitandao tukiamini ni huduma rahisi inayoweza kuwafanya Watanzania wote wafurahie kwa pamoja na kukuza uchumi wetu, hivyo tukaona tufike mbali zaidi kwa kuchezesha droo yetu ya kuwapatia Sh Milioni moja washindi watatu kila mwezi.
  Ngula Cheyo (katikati) ambaye ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services akizungumza jambo katika droo ya kutafutwa washindi watatu wa bahati nasibu inayoandaliwa na taasisi hiyo ambao kila mmoja alishinda Sh Milioni moja. Kulia ni Humud Abdulhussein kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha na kushoto ni Meneja Utawala wa Bayport Financial Services, Evalyine Hall.
  Shughuli ya kutafutwa washindi wa Kopa na Bayport kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz inaendelea.
  Jamani huyu ndiye mshindi. Ndivyo anavyoenekana kusema Meneja Utawala wa Bayport Financial Services katika droo ya kutafutwa washindi watatu waliokopa kwa njia ya mtandao.

  Washindi hao ni Phaustine Mbilinyi (Dar es Salaam), Hyasint Mbunda (Songea) na Allen Bishubo (Bukoba)ambao kila mmoja amejinyakulia Sh Milioni moja baada ya kushinda katika bahati nasibu yetu hii, huku tukiamini kuwa wateja wengine wanao uwezo wa kushinda katika droo nyingine ijayo, ukizingatia kuwa Bayport ipo kwa ajili yao katika kutoa huduma bora zinazoweza kuwakwamua, ikiwamo ya mikopo isiyokuwa na dhamana wala amana,” alisema Cheyo.

  Naye Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka kwenye Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein alisema washindi hao baada ya kupatikana walipigiwa simu ili wataarifiwe ushindi wao na jinsi ya kupata zawadi zao za Sh Milioni moja kila mmoja.

  “Huduma ya kukopa kwa njia ya mtandao inayoendeshwa na Bayport Financial Services ni nzuri na rahisi, ambapo pia ipo fursa ya kushinda pesa taslimu kwa wale watakaoamua kukopa kwa njia hiyo,” alisema.

  Bayport Financial Services ni taasisi ya kifedha inayoongoza kutoa mikopo isiyokuwa na dhamana wala amana kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa na taasisi hiyo.  0 0

  Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Beijing China wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo na kuwapata Viongozi wapya baada ya kuchagulia kwa kuongoza Jumuiya hiyo kwa mwaka 2015/2016.
  Viongozi Wapya waliochaguliwa katika Mkutano Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja ikiwa ni kumbukumbu ya Uchaguzi huo.

older | 1 | .... | 795 | 796 | (Page 797) | 798 | 799 | .... | 3284 | newer