Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 794 | 795 | (Page 796) | 797 | 798 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Na Faustine Ruta, Bukoba
  Kundi zima la Yamoto Band punde walitinga Katika Kituo cha Radio Kasibante 88.5 Bukoba kuongea moja kwa moja na Wakaazi wa Bukoba juu ya Shoo ya yao inayotarajiwa kufanyika Usiku huu katika Ukumbi wa Burudani wa Lina's Night Bukoba. Bendi inayokuja kasi hapa Nchini inayoundwa na Vijana Machachari kama Aslay, Becka, Bella na Maromboso wameteta na Wanabukoba kwamba waje kwa wingi katika Ukumbi huo wa Lina's wajionee walichokuja nacho kipya katika Pasaka hii ya pili maana kwa sasa watawasha Moto wa Uhakika na Watatoa Burudani Live jukwaani na wamekuja wamejipanga wakiwa na Vijana wengine ambao ni Maalum kwa Kuliteka Jukwaa kwa mapigo ya Live"
  Mtandao huu wa jamii murua kwa habari tamu za Michezo na Burudani pia umeweza kuzinyaka za haraka haraka kwamba baada ya Shoo ya leo katika Ukumbi wa Lina's Kesho Jumatatu watatoa Burudani pia huko Biharamulo kwa kiingilio cha 10,000/ siku ambayo ni Karume Day" ya jumanne tarehe 07/04/2015. Kiingilio cha Shoo ya leo ya Lina's kwa kawaida ni Tsh 10,000/ na VIP ni Tsh.15,000/-
  Wasanii wa Kikundi cha Yamoto Band wakiwa Katika Studio za Radio Kasibante 88.5 FM kuteta na Mashabiki wao na kuwajuza Kile walichokuja nacho kwa mara nyingine na kwa mwaka huu mpya wa 2015.


  0 0

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akizungumza katika mkutano wa ujirani mwema kati ya Kata ya Mtoni Wilaya ya Temeka na Wilaya ya Dimani hapo Tawi la CCM Kwerekwe B.
  Mkuu wa Msafara wa Ujumbe wa Kata ya Mtoni Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es salaam Nd.Said Kabuma akitoa shukrani kwa mapokezi mazuri waliyopewa na wenyeji wao Wilaya ya Dimani wakati wa kuagana baada ya kumaliza ziara yao ya ujirani mwema Zanzibar.
  Baadhi ya Viongozi na wanachama wa ujirani mwema kati ya Kata ta Mtoni Wilaya ya Temeka mkoa wa Dar es salaam na Wilaya ya Dimani Mkoa wa Magharibi Zanzibar.


  0 0
 • 04/06/15--14:10: BBC DIRA YA DUNIA LEO

 • 0 0
 • 04/06/15--14:15: IN EVELASTING MEMORY


 • 0 0

  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais -Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya akifungua kisima cha maji cha Mradi wa SEMUSO uliopo Kibandamaiti, Zanzibar.Nyuma yake mwenye mawani ni Mheshimiwa Mussa Mussa Mbunge wa Amani.
  Baada ya kufungulia bomba la maji ya Mradi wa SEMUSO,Kibandamaiti,Zanzibar,Waziri Mwandosya alimtwisha ndoo ya maji Ndugu Ali Magoha, Mjumbe wa Kamati ya Mradi wa SEMUSO, kuashiria kuyafikisha maji kwa watumiaji.
  Tanki la maji la Mradi wa Maji wa SEMUSO lililo Kibandamaiti,Zanzibai,Mradi uliozinduliwa na Waziri Mwandosya.

  0 0


  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi Bandari nchini (TPA), Bw. Awadh Massawe (mwenye koti la bluu kushoto) akiongoza kikao cha wadau wa mamalaka hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Pamoja na kujenga mahusiano ya karibu na wadau wa bandari, vikao hivyo vinalenga kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili bandari hiyo na kuifanya kuwa shindani katika eneo hili la Afrika.

  0 0

   
  Kamanda wa jeshi la zimamoto mkoa wa iringa akikabidhi mbuzi kwa kaimu mkuu wa kituo cha Sister Theresa, Sister Sister Winfrida Mhongole  katika makabidhiano yaliyofanyika kituoni hapo.

  NA DENIS MLOWE,IRINGA

  JESHI la Zimamoto mkoani Iringa limesheherekea sikukuu ya pasaka  na watoto  wanaoishi katika kituo cha kulea yatima cha Sister Theresia  kilichoko Tosamaganga mkoani Iringa kwa kuwapatia misaada mbalimbali.

  Akikabidhi msaada huo Kamanda wa Jeshi la Zimamoto mkoa wa Iringa Inspekta Kennedy Komba alisema lengo kubwa la jeshi hilo ni kuwa karibu zaidi na jamii katika kutoa misaada ambayo itawasaidia yatima walioko katika vituo mbalimbali mkoani hapa.
   
  Alisema yatima wanakabiliana na mazingira magumu katika kupata mahitaji muhimu hasa chakula, afya na malazi hivyo ni jukumu la kila mmoja kuweza kuwasaidia kuondokana na hali ya utegemezi.
   
  “Tumeamua kugawa msaada huu kwa kuguswa na matatizo mbalimbali wanayokabiliana nao vituo vingi vya kulelea watoto hapa nchini katika harakati zetu za kuhahikisha watoto yatima wanapata mahitaji muhimu katika maisha yao ya kil siku huu ni mwanzo tu wa jeshi la zimamoto katika kuwa karibu na jamii na hii tunafanya kila mwaka kuweza kurudisha pia katika jamii kile ambacho jeshi hilo linapata” alisema Komba
   
  Alisema msaada uliotolewa wa mchele kilo hamsini, mbuzi, mafuta ya kupikia, sabuni na kuwapatia kifaa cha kuzimia moto (Fire extinguisher) baada ya kuwapa mafunzo ya jinsi ya kutumia vyote vikiwa na jumla ya thamani ya shilingi laki 250,000.
   
  Komba alisema jeshi la zimamoto litakuwa likitoa msaada wa aina hiyo kila mara ili kujiweka karibu na jamii kuweza kutambua shughuli wanazofanya na kuwataka wadau wengine kuiga jeshi hilo katika kuwasaidia watoto yatima.
   
  “Jamii ya Kitanzania yatakiwa kuunga mkono tabia ya kuwasaidia watoto yatima na kuwaimiza kupenda masomo yao na jamii kutowatumia kama watoto wa kazi za ndani na kuwahudumia kwa kila jambo wanalofanya kuliko kutumia muda mwingi katika matumizi ya anasa” alisema Komba
   
  Kwa upande wake kaimu msimamizi wa kituo hicho Sister  Winfrida Mhongole  alilishukuru jeshi la zimamoto kwa msaada huo na kuwataka wadau wengine wawe na moyo wa kujitolea kwa watoto yatima wanaolelewa katika vituo tofauti mkoani hapa.

  Alisema kituo kina jumla ya watoto 280 ambao mbali na hao watoto 72 wanaishi kituoni hapo na wengine wako katika shule mbalimbali wakisoma zikiwemo za msingi na sekondari.

  Alisema watoto hao wamepokelewa kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo ya Iringa, Mbeya, Njombe, Morogoro, Dar es Salaam na Morogoro.

  “Mbali na mapato yatokanayo na shughuli za kilimo tunazozifanya kama kituo, kituo hiki kinaendeshwa kwa michango ya wahisani mbalimbali wa ndani na nje. Kwa kweli hatuna wafadhili wa kudumu,” alisema na kuomba wahisani waendelee kujitokeza kuwasaidia.

  0 0

  Mshinda wa kitita cha shilingi milioni 10/- kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Shamila Ramadhani(kushoto)akikabidhiwa hundi yake na Balozi wa promosheni hiyo Hillary Daud ‘JayMillions’ baada ya kuipuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo katikati ni mume wa mshindi huyo Abdallah Mahoka.Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Dar Live wakati wa Tamasha la Mwana Dar Live lililofanyika Mbagala jijini Dar es Salaam.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
  Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba akiwapagawisha washabiki wa muziki wake waliofurika katika Tamasha la Mwana Dar Live lililodhamini na Vodacom Tanzania, Katika kuadhimisha sikukuu ya pasaka na kufanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.
  Mamaa Aisha Mashauzi akitumbuza muziki wa Taarabu katika Tamasha la Mwana Dar Live lililodhamini na Vodacom Tanzania, Katika kuadhimisha sikukuu ya pasaka na kufanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.
  Msanii wa nyimbo za mchiriku Sueleman Jabiri”Msaga Sumu”akisaga sumu ipasavyo kwa washabiki wa muziki wake wakati wa Tamasha la Mwana Dar Live lililodhamini na Vodacom Tanzania, Katika kuadhimisha sikukuu ya pasaka na kufanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai maara alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja kubhudhuria katika Hitma ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Iliyofanyika leo asubuhi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) akiwaongoza Viongozi mbali mbali pamoja na Wananchi katika Kisomo cha hitma ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja Iliyofanyika leo asubuhi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi.
  Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilali akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Viongizi wengine wakiitikia Dua iliyoombwa na Mufti Mkuu wa zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (kulia) baada ya kisomo cha hitma iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

  The Chairman of the United Nations High-level Panel on the Global Response to Health Crisis President Jakaya Kikwete on Monday met and held talks with UN Secretary General Ban Ki-moon in New York.

  This was the first time President Kikwete met the UN Chief since he appointed him to chair the panel, whose 0ther members include those from Brazil, Switzerland, Indonesia, Botswana and the United States.

  President Kikwete and Mr Ban Ki-moon reviewed the  terms of reference of the panel which  is mandated  to come up with  recommendations to strengthen  national and international systems to prevent and manage future health crises, taking into account lessons learnt  from the response to the outbreak of  the Ebola virus in West Africa.
  In carrying out its work, the Panel will undertake a wide range of consultations, including with representatives from the affected countries and communities, the UN system, multilateral and bilateral financial institutions and regional development banks, Non-Governmental Organizations, countries supporting the response effort, other member states, health care providers, academic and research institutions, the private sector, and other experts.
  The panel will hold its first meeting in early May and is expected to submit its final report by the end of the year to the UN Secretary General, who will make the report available to the General Assembly, and undertake further action as appropriate.
  President Jakaya Kikwete is received by the UN Secretary General Mr Ban Ki-moon at the UN Headquarters in New York.
  President Jakaya Kikwete in talks with the UN Secretary General Mr Ban Ki-moon at the UN Headquarters in New York.
  resident Jakaya Kikwete and his entourage leave the UN Headquarters in New York, after holding talks with the UN Secretary General Mr Ban Ki-moon at the UN Headquarters in New York. STATE HOUSE PHOTOS

  0 0

  STEVE KANUMBA ENZI ZA UHAI WAKE AKIWA NA ROSE NDAUKA
  Kama wewe ni Mmoja wa Wapenzi wa Filamu za Nchini Tanzania na unafuatilia Vizuri basi utakubaliana na Rose Ndauka Kwamba Baada ya Kufariki STEVEN KANUMBA
  Rose Ndauka Ameongea na @DjHaazu na kusema Steven Kanumba aliipigania sana Tasnia ya Filamu Nchini Tanzania Haswa kwa jitihada zake kukuza Wasanii wenzake ambapo kwa Moyo wake kwa kushirikiana na Wasanii wenzake Waliifikisha Sanaa ya Filamu Tanzania Hapo ilipo ila hadi sasa Hakuna Hatu Nyingine ambayo Wasanii wa Filamu Tanzania Wamepiga Zaidi ni Kuporomoka kwa Kiwanda cha Bongo Movie TZ.
  Hta hivyo Rose ambaye yuko kwenye Tasnia ya Filamu Nchini Tanzania kuanzia Mwaka 2007 Amesema Wao Kama Wasanii kwa sasa wanatakiwa kushikamana na kufanya Mabadiliko ili Kuendeleza Kile alichokuwa anakifanya ambacho ilikuwa Kuhakikisha Sanaa ya Tanzania Inajulikana Kimataifa Zaidi.
  Cha mwisho amewataka Watanzania na Wadau wao Kuendelea Kuwashika Mkono kwa kuwapa Support Japo pia ainawezekana kuna Wakati wamewadissapoint.
  SIKILIZA FULL INTERVIEW YA ROSE NDAUKA click link HII ---> https://www.hulkshare.com/rs95o5svm48w
  Steven Charles Kanumba alizaliwa Tarehe 8 Januari 1984, Shinyanga na Kufariki Tarehe 7 Aprili 2012) alikuwa msanii wa maigizo na filamu kutoka nchini Tanzania. Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania. Hasa walikuwa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi tu. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was Kinigeria nchini

  0 0


  0 0

  The Council of East and Central Africa Football Association (CECAFA) Chairman Leodegar Tenga has retained his seat in the Executive Committee of African Football Confederation (CAF) during the continental Annual General Congress running in Cairo, Egypt April 6-7.

  Tenga of Tanzania will now serve for another four year term as the regional boss at the CAF's decision making body. The CAF congress held every year started in Cairo on Monday and all the 54 African FA's including CECAFA's 12 are in attendance. The CECAFA members are:- Burundi,Kenya, Uganda, Tanzania, Somalia, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Zanzibar, Rwanda, Sudan and South Sudan.

  Tenga was re-elected unopposed after a candidate from Djibouti Hassan Suleiman withdrew from the race and threw his weight behind Tenga, who also served for eight years as Tanzania FA chairman qutting with honour after a two term stint in 2012.

  The CECAFA members and all the other African FA's hailed Tenga for his bold and steadfast leadership. The Tanzanian pledged to conitinue serving CAF and CECAFA with commitment and loyalty.

  Meanwhile on the sidelines of the CAF Congress, CECAFA held its Extra-Ordinary General Assembly and expressed their sympathy with Kenyans following the Garissa massacre that claimed over 147 people.

  Observing a one-minute silence before the meeting, the members expressed shock and disappointment at the macabre of the innocent students. The Council members sent their solidarity to President Uhuru Kenyatta and the people of Kenya during this mourning period.

  Tenga said terrorism must be fought by all people who value life and  mankind.

  During the same CECAFA congress, the 12 member Associations also re-confirmed their commitment to support FIFA President Sepp Blatter ahead of FIFA's congress in Zurich on May 28-29th.

  The CECAFA FA's had made this commitment in Brazil last year during the FIFA Congress


  0 0

  Na  Bashir  Yakub.

  Sheria  ya  ardhi  ni pana   na  ina mambo    mengi.  Kila  nikipata  nafasi  huwa  najitahidi  kueleza  japo machache  ili   watu waweze  kuelewa  masuala  mbalimbali   kuhusu  ardhi.  Ardhi  ni  rasimali  nyeti  mno  na hivyo  ni  tatizo  kubwa   kuishi  bila  kujua mambo  ya msingi  na ya kisheria  kuhusu  ardhi. Kutokujua  ni  moja  ya  sababu inayopelekea  umaskini  wakati  utajiri  upo  mikononi  mwako na  upande  mwingine husababisha migogoro  ya ardhi  inayoongezeka  kila  kukicha  huku   watu  wakizidi  kupata  hasara. 

   Nimewahi kuandika  kuhusu  namna  ya  kisheria ya   kujua  iwapo  ardhi unayonunua  ina  mgogoro  au    hapana,  nikaandika  kuhusu  vitu  gani  viwe  ndani  ya  mkataba  wako  wa  manunuzi  ya  ardhi  ili  usitapeliwe na  mikataba  ya  ardhi  kwa  ujumla,   nikaandika  kuhusu  namna  nyepesi  ya  kubadili/kupata   hati/leseni  ya  makazi  unaponunua  ardhi   na  mengine  mengi  kuhusu  ardhi. Leo  naeleza  kitu  kingine  muhimu  katika  sheria ya  ardhi  ambacho  ni  dhamana(mortgages)    ambazo   unaweza  kutumia   kupatia  mkopo  iwapo  unahitaji  mkopo.   

  1.NINI  MAANA  YA  DHAMANA.

  Kifungu  cha  pili  cha  Sheria Ya  Ardhi   kinasema  kuwa  dhamana ni   hali  ya  mtu, taasisi  au  chombo  chochote  kuwa  na  maslahi  katika  ardhi  inayomilikiwa  na  mtu  mwingine  au  chombo  kingine, maslahi  ambayo   yanatokana  na  deni  au  mkopo.  Maana yake   ni  kuwa  ardhi  ni  yako  lakini  kitendo  cha mtu  mwingine  au taasisi  nyingine  kuwa na  maslahi   ndani  yake  na  maslahi ambayo  yanatokana  na kuwapo  kwa  deni  au  mkopo    basi hiyo  ndiyo  dhamana.  
  Ieleweke  wazi  kuwa  dhamana  haihusishi umiliki  na  wala  haina  uhusiano na  umiliki. Dhamana  ni dhamana  na  mmiliki  anaendelea  kuwa  mmiliki.  Dhamana  haiondoi  haki  ya  umiliki( right  of occupancy).  

  2.VITU  AMBAVYO   WAWEZA  KUWEKA   DHAMANA   NA  KUPATA  MKOPO.

  Watu  wengi  wamekariri   kwa kujua   kuwa  dhamana  katika  masuala  ya  ardhi  ni  lazima  iwe  hati  ya  nyumba, barua  ya  toleo( offer)  au  leseni  ya  makazi.  Ni  kweli  vitu hivi  hutumika  kama  dhamana  lakini  si  hivi  tu  ambavyo  vyaweza  kutumika  kama dhamana.   Vipo  vitu  vingine ambavyo  vyaweza  kusimama  kama  dhamana    na  mtu  akapata  mkopo  kama ambavyo  tutaona  hapa.

  (  A )  MKATABA   WA   PANGO.

  Kisheria  mkataba  wa  pango  ni nyaraka  halali  ambayo  mtu  anaweza  kuitumia  kuombea  mkopo  katika  taasisi  ya  fedha.  Mkataba  wa  pango  ni  yale  makubaliano  ya  kawaida  kati  mwenye  nyumba  na  mpangaji. Mkataba  wa  pango  ni  nyaraka  muhimu  sana  japo  watu  wengi  huwa  hawaipi   uzito  zaidi  ya    kuamini  kuwa  inalinda uhusiano  kati  ya  mwenye  nyumba  na  mpangaji.  Ni  vyema  sasa  kujua kuwa  mkataba  wa  pango  hauishii  kulinda  mahusiano  ya   mwenye  nyumba  na   mpangaji tu  isipokuwa  ni  nyaraka ambayo   ikitumika  vyema  yaweza  kuwa    zana  ya  kukuza uchumi  wako.  


  0 0

  Mchezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona Patrick Kluivert akiwaongoza wachezaji wenzake akiwepo Simao Sabrosa muda mfupi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
  Mchezaji Luis Garcia(kulia) akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro .kushoto ni mratibu wa safari ya wachezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona Royco Garcia.
  Wachezaji wa Barcelona wakielekea upande wa watu mashuhuri katika uwanja wa ndege wa Kiamtaifa wa Kilimanjaro (KIA).

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Habari wadau, 
  Naomba kuwajulisha kuwa mwanafamilia mwenzetu mkongwe katika uandishi wa habari za michezo, Masoud Sanani, amefiwa na mama yake mzazi huko kisiwani Pemba. Msiba ulitokea  hukohuko Pemba na maziko yamefanyika Jana asubuhi.

  Kwa niaba ya TASWA tunampa pole na tupo naye pamoja katika kipindi hiki kigumu kwake. Kwa wanaotaka kumfariji binafsi Masoud Sanani kwa namna mbalimbali namba zake za simu ni 0712 020020 na 0772003377.
   
  Katibu Mkuu TASWA

  0 0

  IMG_2176
  Meneja Mwendeshaji wa kampuni ya Shamy Tours and Travel Agent Zanzibar, Bw. Khamis Mwinjuma Simba akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo katika sekta ya utalii Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wakati wa zoezi la kugawa zawadi za vinyago kwa wageni waalikwa zaidi ya 300 waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mgahawa mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania unaomilikiwa na mpishi maarufu duniani mtanzania, Issa Kasuwi Kapande almaarufu kama ‘Chef Issa’ nchini Sweden katika mji wa Trollhattan.
  Unaweza kutembelea tovuti yao kwa anauni hii www.shamytours.co.tz

  Na Mwandishi Maalumu,
  Trollhattan, Sweden
  KAMPUNI ya kupokea wageni ya Zanzibar ya Shamy Tours and Travel Agent Zanzibar, imefungua ofisi nchini Sweden ambayo itakuwa inashughulikia masuala ya watalii na wageni mbalimbali wanaotaka kuingia Tanzania na visiwani Zanzibar.
  Meneja Mwendeshaji wa Kampuni ya Shamy, Khamis Mwinjuma Simba akizungumza mjini hapa alisema kwamba kampuni yake kupitia Bodi ya Utalii ya Sweden wamepata kibali na leseni ya kuanzishwa kwa branchi ya kampuni hiyo yenye makao makuu yake mjini Zanzibar , mtaa wa Malindi.
  Kampuni hiyo ambayo tangu kuanzishwa kwake ina miaka minne sasa ilifanya uzinduzi wa branchi yake hivi karibuni, kazi iliyofanywa na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dora Msechu wakati akizindua mgahawa wa Mtanzania, Issa Kapande wiki iliyopita.
  Simba alisema kwamba tangu kuanzishwa kwake wamepata maendeleo makubwa hasa katika kukabiliana na changamoto za soko na kwamba kwa kuanzishwa kwa tawi hilo wanaangalia kufikia nchi 30 za Ulaya zinazotumia viza ya Ulaya.
  IMG_2100
  Alisema kuwa na ofisi nchini Sweden kumeamsha mori wa kuongeza mafanikio ya kampuni ili kusaidia juhudi za Wizara ya Utalii Zanzibar katika kuhakikisha kwamba sekta ya Utalii inaendesha uchumi wa Zanzibar.
  Alisema wizara kama wizara imefanya juhudi kubwa kuhakikisha utalii unakua na kuleta mafanikio kwa Zanzibar na hivyo ni wajibu wao kama Shamy Tours kuhakikisha kwamba wanatoa fursa walizowezeshwa na wizara hiyo kutanua shughuli zao ili kuihakikishia mapato serikali kwa kuingiza wageni wengi zaidi.
  "Tumepata faida kubwa kama Shamy Tours kutoka kamisheni ya utalii hasa usajili, kupewa hati za uendeshaji na vipeperushi na machapisho mbalimbali na hasa chapisho la Karibu Zanzibar linalohusu Zanzibar," alisema Simba na kuongeza kuwa kwa kusaidiwa huko wameweza kusonga mbele na katika miaka minne kwa kushirikiana na Issa Kapande, Mtanzania mbaye amefungua mgahawa wa Kitanzania nchini Sweden, wameweza kuanzisha branchi nchini Sweden.
  Alisema pamoja na kuzindua ofisi yao, wameitumia siku ya ufunguzi wa mgahawa wa Issa Kapande kukutana na wadau mbalimbali wa masuala ya utalii nchini Sweden na kuwapatia zawadi halisi za Kitanzania kuwapa ushawishi wa kuja nchini.
  IMG_2182
  Balozi wa Shamy Tours and Travel Agent nchini Sweden, Bi. Anab akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo wakati wa zoezi la kukabidhi zawadi kwa wageni waalikwa zilizotolewa na kampuni hiyo kwenye hafla ya uzinduzi wa mgahawa mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania unaomilikiwa na mpishi maarufu duniani mtanzania, Issa Kasuwi Kapande almaarufu kama ‘Chef Issa’ nchini Sweden.
  Baadhi ya zawadi hizo ni vinyago vya kimakonde taswira za Wamasai na vipeperushi mbalimbali.
  Alisema kuwapo kwa Shammy Tours nchini Sweden kutakuza biashara ya utalii.
  Alisema mipango ya kuanzisha ofisi nchini Sweden ilianza zamani wakati Issa Kapande akifanya shughuli zake katika Hoteli ya African House miaka sita iliyopita na kushika kasi katika miaka miwili iliyopita ambapo Issa Kapande alifika Zanzibar mara mbili kukamilisha ushirikiano uliozaa ofisi hiyo ya Sweden.
  Alisema pamoja na kujitangaza katika nchi zaidi ya 30 za Ulaya kupitia ofisi hiyo ya Sweden Shamy Tours inatarajia kushiriki katika maonesho ya utalii Afrika Kusini yatakayofanyika Mei mwaka huu, Urusi Juni mwaka huu na London, Uingereza Novemba mwaka huu.
  Alisema ushiriki wao ni sehemu ya kutafuta masoko na kuitangaza Tanzania, nchi ya visiwa vya Zanzibar, mlima Kilimanjaro na mbuga ya Serengeti.
  IMG_2194
  Unaweza kutembelea tovuti yao kwa anauni hii www.shamytours.co.tz

  0 0


older | 1 | .... | 794 | 795 | (Page 796) | 797 | 798 | .... | 3272 | newer