Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 789 | 790 | (Page 791) | 792 | 793 | .... | 3272 | newer

  0 0
 • 04/01/15--02:25: Motown KunaMambo event
 • Motown Club - Morogoro (formerly 4Stars) present Motown KunaMambo starting 3rd of April 2015 and every Friday from 7:00pm; come dine and dance to the live sounds of Afro Jazz, Salsa, Rhumba,Charanga, Raggae and much more!...with a gate contribution of 10,000tsh per person; Cash bar, delicious food and snacks Respect yourself, do not miss this! Karibu

  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu za makazi za Kibada, Kigamboni alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akisikiliza maelezo ya Injinia wa NHC, Elisante Ulomi anayesimamia Mradi wa Mwongozo Housing Estate mchana wa leo. Nyumba za mradi mkubwa wa NHC Morocco Square, Dar es Salaam zikiwa zinajengwa katika hatua ya msingi, zinavyoonekana leo wakati Waziri Lukuvi alipozitembelea.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Anitha Jonas – MAELEZO,Dodoma.

  Serikali inatarajia kuanzisha Baraza la Vijana litakalo kuwa chombo cha vijana kitakacho waunganisha Kitaifa bila kujali itikadi zao za Kisiasa,Imani zao za Kidini wala tofauti zao za Rangi,hayo yamesemwa na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe.Fenella Mukangara alipokuwa akisoma Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana Tanzania Bungeni Mjini Dodoma.

  Mheshimiwa Mukangara aliendelea kusema Baraza hilo litaisaidia Serikali kuweza kuwafikia vijana kwa urahisi na kusikiliza shida zao pamoja na kutoa ufumbuzi wa hoja mbalimbali za vijana.Hata hivyo chimbuko la Muswada huo ni katika kutekeleza Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya 2007,Ibara ya 3 Sehemu ndogo ya 11 inayosema kwa uwazi Serikali itawezesha kuundwa kwa Baraza Baraza la Vijana na kuanzisha mfumo wa kisheria ili kuliwezesha kufanya kazi.

  “Madhumuni ya Muswada huu ni Kutunga Sheria ya Baraza la Vijana Tanzania(The Youth Council of Tanzania 2015) ili kuwa na chombo cha Kitaifa cha kuwewezesha vijana kujadili masuala yao,kutambua majukumu yao,kukuza maadili mema,kukuza moyo wa umoja ,uzalendo,uwajibikaji na kujitolea kwa malengo chanya miongoni mwao katika nchi yetu,”alisema Mhe.Mukangara.

  Mbali na hayo katika sehemu ya pili kifungu cha 4-15 cha Muswada huo unaeleza juu ya masharti mbalimbali kuhusu Uanzishwaji,Uanachama,Muundo na kazi za Baraza.Pia sehemu hii imefafanua Mamlaka ya Baraza na vyombo vya utendaji katika ngazi ya Taifa,Mkoa na Wilaya.


  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano unaozungumzia jinsi ya kupata Maendeleo endelevu kwa kukuza ajira na kazi zenye utu (Achieving sustainable development through employment creation and decent work) tarehe 30 Aprili, 2015 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York, Marekani.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiondoka baada ya yeye kuhutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano unaozungumzia jinsi ya kupata Maendeleo endelevu kwa kukuza ajira na kazi zenye utu (Achieving sustainable development through employment creation and decent work) tarehe 30 Aprili, 2015 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York, Marekani.

  =====  ======  ======
  Kuna Umuhimu mkubwa wa kuweka suala la Ajira  katika  ajenda   ya maendeleo,  mipango na progamu ya Mataifa yote duniani.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo tarehe 30 Aprili, 2015 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York wakati wa ufunguzi wa Mkutano  unaozungumzia jinsi ya kupata Maendeleo endelevu kwa kukuza ajira na kazi zenye utu  (Achieving sustainable development through employment creation and decent work).

  Rais Kikwete amesema tatizo la ajira lina pande mbili, kwanza linaweza kutumika vizuri pale  wawekezaji wanapokuja  barani Afrika, wanaweza kupata nguvu kazi iliyopo tayari,  ikiwa inakidhi matakwa ya kazi na pili ni changamoto kubwa pale ambapo ajira hazipatikani kwa kundi kubwa la vijana ambao wanaongezeka kila mwaka.

  "Hivyo ni muhimu ukuzaji wa ajira kuwa kipengele muhimu katika ajenda ya maendeleo, mipango na programu mbalimbali katika Mataifa yote" Rais amesema na kuelezea kuwa pamoja na ukweli uliopo kuwa nchi mbalimbali barani Afrika ikiwemo Tanzania, zimeonyesha hali nzuri ya uchumi kwa miongo miwili mpaka mitatu iliyopita, na kuonyesha kuwa bara la Afrika ni moja ya mabara yanayokua kwa kasi kiuchumi duniani, bado bara linakabiliwa na tatizo kubwa la ajira. 

  "Natarajia  tutabadilishana mawazo ya jinsi gani Afrika inaweza kutatua tatizo hili na pia kupata mawazo ya nini kifanyike kuweza kuvutia wawekezaji zaidi". Rais amesema. 


  "Pia nitapenda kupata mawazo na ikiwezekana kuunga mkono katika kusaidia vijana wetu katika suala la kujiajiri" ameongeza na kusema suala hili linahitaji programu maalum na miradi. 

  Rais Kikwete amezungumzia suala la ajira barani Afrika kuwa la kutia mashaka na hivyo kuhitaji hatua za haraka. Takwimu zinaonesha kuwa Afrika ilitengeneza ajira 37 million  pekee kwa kipindi cha muongo uliopita, kati ya hizi asilimia 28 zilikuwa ajira zenye utu, na wakati huo huo inakadiriwa kuwa, soko la ajira barani Afrika linapokea watu milioni 122 katika ajira mpya kila mwaka. 

  "Hii inatisha sana kwa vile karibu watu 200 barani Afrika ni wake wenye miaka 15 na 24 na kwamba idadi hii itaongezeka mara mbili ifikapo mwaka 2045" 
  Rais amefafanua na kuonyesha wasiwasi wake kwamba bara la Afrika litakumbwa na idadi kubwa ya ukosefu wa ajira, na kibaya zaidi idadi kubwa kuwa ya vijana.

  Imetolewa na; 
  Premi Kibanga,
  Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
  New York - USA
  31 Aprili, 2015

  0 0

  IT SEEMS LIKE YESTERDAY THOUGH IT IS TWO YEARS SINCE OUR LORD TOOK YOU HOME, OUR LOVELY DAD, THE FACT THAT YOU ARE NO LONGER HERE WILL ALWAYS CAUSE US PAIN, HOWEVER WE TAKE REFUGE IN THE LOVE THAT BOUND US FOREVER.

  OUR HEARTS ARE FULL OF FOND MEMORIES; YOU GAVE US SO MUCH TO REMEMBER.

  WE REMEMBER ALL THE SUPPORT AND GUIDANCE YOU PROVIDED THAT HAS BUILT A SOLID FOUNDATION IN OUR LIVES AND HAS MADE US WHAT WE ARE TODAY. 

  WE CHERISH THE GOOD TIMES WE HAVE HAD TOGETHER AND THE LOVE THAT YOU GAVE US SO UNCONDITIONALLY. YOU WILL REMAIN FOREVER IN OUR HEARTS. YOU ARE DEEPLY MISSED BY Ma GLORY, Ma THECLA YOUR CHILDREN MERCY, DICKSON, NEEMA AND MVANO, YOUR GRANDCHILDREN JOYCE, ESTHER, FAITH-FATUMA, LINDA-RACHEL, TALLE, IBRAHIM, MONICA AND JAMES; YOUR IN-LAWS AND RELATIVES.

  THANKS GIVING MASS WILL BE HELD AT ST. THOMAS ANGLICAN CHURCH, YOMBO KIWALANI ON SATURDAY, 4TH APRIL, 2015 FROM 08:00am.

  THE LORDGAVEANDTHE LORDHASTAKENAWAY; MAYTHENAMEOFTHE LORDBE PRAISED, AMEN.

  0 0

  Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii

  KIKOSI cha polisi usalama barabarani kimewataka madereva wa mabasi ,magari makubwa pamoja na daladala kwenda kusoma ili kuongeza ujuzi wa kazi zao kutokana na kuwepo kwa teknolojia za kisasa katika magari hayo.

  Hayo ameyasema,Ofisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Johansen Kahatano wakati wa semina ya kuwajengea uwezo madereva katika kukabiliana na ajali za barabarani iliyofanyika jana katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

  Alisema sheria ya madeva wa mabasi ya abiria na magari makubwa kwenda kujiendeleza kimasomo pamoja na kupata ujuzi  kwa kila baada ya miaka miwili pamoja na kupewa leseni mpya  kwa sababu leseni zote zinakaribia kuisha muda wake.

  Kahatano, alisema kuwa madereva wote wa malori wanatakiwa kusoma, kujikumbushia vitu mbalimbali na kuongeza ujuzi wao kwa kila baada ya miaka 3, ilikupunguza ajari za barabarani.

  Katika semina hiyo waendesha daladala wamesema kuwa kama serikali imeamua madereva twende darasani tena,  tunaomba gharama zote za mafuzo hayo ziwe za waajili wetu au serikali.


  0 0

  Na John Nditi, Morogoro

  MKUU  wa wilaya ya Mvomero, mkoa wa Morogoro, Festo Kiswaga, Machi 31, 2015,  amefungua mkutano wa siku mbili wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli Oasis , mjini Morogoro.

  Mkuu huyo wa wilaya alimwakilisha mkuu wa mkoa, Dk Rajab Rutengwe ,na  katika hotuba yake ya ufunguzi wa Baraza hilo ,amewapongeza wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kwa kuendeleza na kuitangaza taaluma yao vizuri ya utabiri wa  hali ya hewa ikiwa na  kuelimisha umma wa watanzania.

  Pamoja na hayo alisema , Mamkala hiyo  imekuwa mstari wa mbele kutoa taarifa za hali ya hewa zitolewazo kila siku, siku kumi na zile za msimu pamoja na tahadhari kutokana na hali mbaya ya hewa , kutokana na hali hiyo TMA imeendelea kuaminika katika macho ya mii ya watanzania na kuweza kuchangia kuinua uchumi wa nchi yetu.

  Kwa upande wake , Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi, mbali na kuelezea changamoto kubwa ya ufinyu wa bajeti, amesema kuwa , wataendelea kutoa tabiri wa kila siku ambao ni muhimu kwa wananchi na wakulima kuutumia katika kilimo ili kupata mazao mengi yenye kuwaletea tija .

  Alisema , utabiri huo inaonesha mifumo ya hali ya hewa na kutokea kwa mvua na kukosekana kwa mvua za kutosha , hali inayowawezesha kutumia muda mupi wa hali ya hewa na mvua kupanda mazao ambayo nayakomaa kwa muda mfupi na kuvuna mazao mengi, ambapo pia amewataka maofiza ugani kusambaza matokeo ya utabiri kwa wakulima vijijini .
  Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Festo Kiswaga akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Kijazi katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi.
  Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi ( kulia) akinukuu jambo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi DC wa Mvomero (kati kati), Festo Kiswaga.


  0 0

  Na Editha Karlo, Globu ya Jamii - Kigoma

  MKAZI wa Kijiji cha Buzebazeba katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, Zuwena Abdu (29) jana amejifungua watoto mapacha wanne kwa mkupuo katika Hospital ya Mkoa  wa Kigoma (Maweni).

  Zuwena alisema kuwa watoto aliojifungua wenye jinsia ya kiume ni  watatu na  mmoja ambaye ni wa mwisho ana jinsia ya kike ,wa kwanza akiwa na uzito wa kilo 1.8,pili 2.5 wa tatu 1.7 na wanne 1.7.

  Alisema watoto hao alijifungua jana majira ya saa kumi na mbili jioni salama  kwa njia ya kawaida 

  Zuwena alisema huo ni uzazi wake wa tano ambao awali alijifungua wanne kwa njia ya kawaida kwahiyo jumla anaidadi ya watoto nane.

  ''Kwanza nina mshukuru mungu kwa kuniwezesha kujifungua salama watoto wote na wakiwa hai kutokana na hali duni ya  kiuchumi ya familia yetu mimi na mume wangu tunaomba Watanzania wenye mapenzi mema watusaidie ili tuweze kuwalea hawa watoto,mume wangu hana kazi na mimi sina kazi''alisema mama huyo

  Muuguzi wa zamu katika wodi  ya wazazi  Agness Nguvumali alisema kuwa alifikishwa mama huyo alifikishwa hospitalini hapo siku ya jumatatu saa kumi jioni akiwa na uchungu na ilipofika saa kumi na mbili akawa amejifungua mapacha wanne kwa njia ya kawaida salama.

  Muuguzi huyo alisema kuwa watoto wote wana afya njema alisema wataendelea kubaki hospitalini hapo kwaajili ya uangalizi wa karibu wa madaktari.

  Agness amewaomba Watanzania,mashirika mbalimbali kujitokeza kumsaidia mama huyo ili aweze kuhudumia watoto wake hao kwakuwa hali yake ya uchumi na mume wake siyo nzuri na utunzaji wa mapacha hao unahitaji uwezo wa nguvu ya ziada.
   YEYOTE MWENYE MSAADA KWA WATOTO HAO ANAWEZA KUWASILIANA KWA KUTUMIA NAMBA 0752202783
  Mama wa watoto mapacha wanne, Bi. Zuwena Abdu akiwa wodini baada ya kujifungua.
  Muuguzi wa zamu katika Wodi ya wazazi ya Hospital ya Mkoa wa Kigoma (Maweni), Agness Nguvumali akiwaangalia mapacha wanne waliozaliwa hospitalini hapo.

  0 0

  Uelewa finyu juu ya masuala ya utoaji wa mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu umeendelea kuwa chanzo cha baadhi ya wahitaji wa mikopo kulalamika bila kuanza kutafuta chanzo cha wao kutopata mikopo hiyo.

  Hayo yamebainika hii leo katika ziara ya mafunzo ya wanachuo 147 kutoka Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) unaoendeshea shughuli zake Bagamoyo mkoani Pwani waliofika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa ziara ya mafunzo.

  Miongoni mwa maswali yaliyoulizwa na wanachuo hao ni pamoja na uwezekano wa wafanyakazi kupatiwa mikopo, vigezo vya utoaji mikopo na jinsi ya kubaini waombaji wa mikopo wenye sifa za kupata mikopo hiyo. Maswali mengine yalilenga kujua jinsi Bodi inavyowatambua wanufaika wa mikopo ambao mikopo yao imeiva tayari kurejeshwa.

  Awali, Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano Bw. Cosmas Mwaisobwa aliwasilisha mada iliyojumuisha historia fupi ya Bodi, Sera ya Uchangiaji, Muundo wa Uongozi, Utaratibu wa Utoaji Mikopo na Utaratibu wa Urejeshwaji wa mikopo ya elimu ya juu.

  Akitoa shukrani kwa niaba ya wanachuo hao, Mkufunzi aliyeandamana nao Bibi Rhoda Samwepa, ameelezea kufurahishwa kwake na jinsi Bw. Mwaisobwa ambaye pia ni Msemaji wa Bodi, alivyotolea ufafanuzi kwa ufasaha masuala yanayoonekana kuwa na utata kuhusu mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na kwamba anaona umuhimu wa wanufaika kurejesha mikopo hiyo ili wahitaji wengine waweze kunufaika.

  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imekuwa ikipokea makundi mbalimbali ya wadau wa elimu wanaofika kwa lengo la kujifunza masuala ya utoaji mikopo, vigezo na masharti ya utoaji mikopo na utaratibu wa kurejesha mikopo hiyo na hivyo kuendelea kuongeza uelewa wa mikopo ya wanafunzi kwa idadi kubwa zaidi ya wadau.
  Sehemu ya wanachuo wa ADEM wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano Bw. Cosmas Mwaisobwa (haonekani kwenye picha hii).
  Baadhi ya wanafunzi wa ADEM wakifuatilia kwa makini mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano Bw. Cosmas Mwaisobwa.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Pangani, Saleh Pamba bungeni mjini Dodoma Aprili 1,2015.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Naibu Waziri Wizara Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe.Pindi Chana akijibu swali la msingi la Mhe.Kidawa Salehe (Mb) Viti Maalum CCM lililohoji juu ya Serikali imefanya utafiti gani juu ya sababu za ukatili kwa watoto,bungeni Mjini Dodoma 1 Aprili,2015.
  Mbunge wa Kisarawe (CCM) Mhe.Seleman Jafo akiwasilisha hoja binafsi kuomba tarehe ya kura ya maoni isogezwe mbele na kupendekeza Serikali ipeleke Muswada Bungeni wa hati ya dharura kupitisha Katiba ya mpito,Bungeni Mjini Dodoma 1 Aprili,2015 .
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitoka nje ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma mara baada ya kuhairisha bunge kutokana na fujo zilizozuka ndani ya bunge kutoka na kuwepo kwa mwingiliano wa hoja binafsi kati ya Mhe.Seleman Jafo (Mb) CCM Kisarawe na Mhe.John Mnyika (Mb)Ubungo CHADEMA Bungeni Mjini Dodoma 1 Aprili,2015.


  0 0

  Uongozi wa Klabu ya Simba umepanga kumpa gari mchezaji bora wa klabu hiyo katika sherehe za Simba maarufu 'Simba Day' inayofanyika kila mwaka Agosti 8.

  Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Rais wa Simba Evans Aveva alisema kuwa chini ya uongozi wake wameanzisha tuzo hizo kwa wachezaji wa Simba ili kuibua morali ya wachezaji na kuthamini mchango wao na hiyo imekuja baada ya klabu hiyo ya wekundu wa Msimbazi kuingia mkataba wa miaka mitano na Kampuni ya EAG ambao watakuwa na jukumu la kuiwezesha Simba kupata mapato kwa njia mbali mbali ikiwemo udhamini kutoka makampuni mbali mbali.

  Aveva alisema pia mbali na kumpa gari mchezaji bora wa klabu hiyo pia kutakuwa na tuzo ya mchezaji bora anayechipukia, kiungo, mshambuliaji bora na mchezaji mwenye nidhamu.

  "Mchezaji bora atapata gari, mchezaji bora chipukizi atapata Sh5 milioni waliosali watapata Sh2 milioni ikiwemo mwenye nidhamu.

  Aveva alisema pia mbali na tuzo hizo pia watatoa tuzo ya mchezaji aliyetukuka 'All Fame' ambaye nae atapata kiasi hicho cha fedha na pia mbali na zawadi hizo wachezaji hao watapewa simu aina ya Huawei.

  Mbali na tuzo hizo Aveva alisema pia Kampuni hiyo ya EAG itakuwa pia na jukumu la kuhakikisha Simba inafanikiwa mikakati yake ya kuongeza mapato, kukuza namba ya wanachama, kuongeza na kuwapa faida wanachama wa Simba kupitia huduma za Bima, kuongeza ari ya wachezaji Simba, kuwaenzi na kukumbuka wachezaji wa zamani.

  "Lengo la utekelezaji wa mikakati hii ni kukuza ajira kutokana na biashara zitakazoanzishwa, tunaamini tukitumia bidhaa za Simba ambazo tunalenga kuzifikisha kila sehemu Tanzania na kutengeneza mfomo wenye lengo la kuuipatia mapato stahiki tofauti na sasa.

  "Kupitia mkakati huu Simba itakuwa na uwezo wa kujenga uwanja wake na kuwa na vyanzo endelevu vya mapato vitakavyoiwezesha kuboresha kiwango cha timu na kuifanya iwe bora si Tanzania pekee bali Afrika nzima....: "Kwa timu yenye mamilioni ya washabiki hili si jambo lisilowezekana bali linalowezekana, ni jambo la kufurahisha na kuona uongozi wa Simba umetambua hili."alisema Aveva.

  Naye mkurugenzi wa EAG Group Iman Kajura akizungumzia suala hilo alisema "Kupitia  mkataba huu nataka kuona Simba inapata mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa kuitafutia vyanzo vingi vya mapato, ili iache kutegemea mapato ya  mlangoni na ada za wanachama pekee."

  Kajura alisema mipango yote ya kuendesha zoezi hilo anaipata kutoka klabu ya Arsenal ya England ambayo anafanya nayo kazi katika kukuza na kuingiza wabia wa biashara.

  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (Kushoto) na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia) wakiingia kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini unaoanza tarehe 01 hadi tarehe 02, Aprili 2015 wenye lengo la kujadili mafanikio na changamoto katika utendaji kazi wa Wizara pamoja na taasisi zake.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu (TUGHE) Wizara ya Nishati na Madini, Marcelina Mshumbusi akisoma hotuba ya kumkaribisha Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (hayupo pichani) katika mkutano huo. Kushoto ni Katibu wa TUGHE Wizara ya Nishati na Madini, Assa Mwakilembe.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini.
  Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (hayupo pichani).


  0 0

  Head of Public Relations & Promotions of Social Security Regulatory Authority (SSRA), Mrs. Sarah Kibonde Msika (left) inviting delegates from Public Service Commissions of Zimbabwe & Tanzania
  Head of Public Relations & Promotions of Social Security Regulatory Authority (SSRA), Mrs. Sarah Kibonde Msika making presentation regarding Social Security Sector in Tanzania.


  0 0

   Awali ya yote nirudie kutoa pongezi kwa serikali kwa hatua hii muhimu waliyofikia ya kuwasilisha mswada wa sheria mtandao ambao naimani kubwa itakua na majibu mazuri ya kudhibiti na kuhimili vishindo vya uhalifu mtandao nchini. Naomba itambulike Tanznaia si ya kwanza kuwa na sheria za usalama mitandao na ukweli ni kwamba tumechelewa kwa kiasi Fulani. Nchi nyingi tayari zinasheria za usalama mitandao na zimeendelea kuboreshwa kadri teknolojia inavyo endelea kukua na kubadilika.

  Nitaanza na mifano michache kunasheria mitandao zilizopendekeza kifungo cha maisha kwa wahalifu mtandao nchini Uingereza. Na katika Kikao cha usalama mitandao kilichopita mshiriki aliyekua nami meza kuu katika kuongoza moja ya kikao aliyetokea “US Secret service” alipata kuainisha adhabu ya miaka kumi na sita bado imeonekana ni ndogo na inashauriwa kuongezwa makali.


  Aidha, Nieleze ushauri wa kuhakiki sheria mitandao zinaboreshwa na kuwa kali zaidi ni kutokana na athari ya uhalifu mtandao kua kubwa sana na imekua ikimgusa kila mmoja wetu – Kwan nje ya nchi kila siku tumekua tukipata habari mpya ya matukio ya kiuhalifu mtandao ambapo maelfu wamekua wakipoteza maisha, fedha na pia ufaragha wao umekua ukitumiwa vibaya na wahalifu mtandao.


  Tanzania pia hatuko salama – Nimekua nikipata malalamiko mengi ya watu kudukuliwa faragha zao, kuibiwa fedha nyingi sana na wengine kufikia hata kujitoa maisha kwa kudalilisha mitandaoni.

  Hayo yote yamekua yakisukuma wataalam usalama mitandao kuumiza vichwa kuhakiki wanakuja na mwarubaini wa uhalifu huu mtandao unaozidi kuota mbawa kila kukicha. Hapo ndipo mengi yakawekwa sawa katika kukabiliana na hali hii ikiwa ni pamoja na kukuza uelewa kwa watumiaji mtandao (Matumizi salama ya mitandao), Kuzalisha na kuongezea uwezo kwa wataalam wa usalama mitandao, kuwa na sharia stahiki za uhalifu mitandao, kukuza ushirikiano kutokana na uhalifu huu kutokua na mipaka, kuhimiza kupatikana kwa takwimu sahihi za uhalifu mitandao ili kuweza kutambua maeneo athirika zaidi.


  0 0

  Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Jumbe Mangu akitoa heshma za mwisho kwa miili ya askari wawili waliouawa na watu wasiojulikana huko vikindu wilaya ya mkuranga, mkoani Pwani hivi karibuni. Shughuli za kuiaga miili hiyo zilifanyika jana katika maeneo hospitali ya barabara ya kilwa jijini Dar es Salaam . Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
  nspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Jumbe Mangu akitoa heshma za mwisho kwa miili ya askari waliouawa na watu wasiojulikana huko vikindu wilaya ya mkuranga, mkoani Pwani hivi karibuni. Shughuli za kuiaga miili hiyo zilifanyika jana katika maeneo hospitali ya barabara ya kilwa jijini Dar es Salaam.

  0 0
 • 04/01/15--13:23: BBC DIRA YA DUNIA LEO

 • 0 0

  Marehemu Dkt. Alec 
  Chemponda enzi za uhai wake

  Mwenyekiti Mtendaji wa Michuzi Media Group anaungana na familia, ndugu, jamaa, jirani na marafiki wa  Chemponda katika kuomboleza kifo cha Dkt Alec Che Mponda kilichotokea juzi Machi 30, 2015 katika hospitali ya Massana jijini Dar es salaam kutokana na saratani (cancer) ya mifupa iliyokuwa ikimsumbua kwa muda mrefu. Alikuwa na umri wa miaka 80.

  Tunatoa mkono wa pole kwa binti mkubwa wa marehemu na blogger na mwanahabari mwenzetu, Bi Chemi Che-Mponda pamoja na wadogo wake wote na wajukuu wa marehemu ambaye atakumbukwa kuwa mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini aliyepata kuanzisha na kuongoza chama cha Tanzania People'e Party (TPP).

  Mbali na siasa pamoja na kuwa mmoja wa watangazaji wa kwanza wa Idha ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika (VOA) Marehemu Dkt Che-Mponda pia aliandika thesis ya shahada ya uzamivu (PhD) juu ya mzozo wa mpaka wa Tanzania na Malawi ambayo imesimama kama kimoja ya kielelezo muhimu katika swala hilo nyeti.

  Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mbezi (mbele ya Massana Hospital) jijini Dar es salaam.

  Mola aiweke roho ya marehemu 
  mahala pema peponi
  Amen  0 0  0 0


  Katika jitihada za kupambana na uhalifu wa kimtandao ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kibenki katika mazingira salama zaidi, Benki ya Exim imetoa wito kwa wateja wake kuchukua kadi zao za ‘Faida chip and pin Debit Card’ zilizotambulishwa mapema mwezi Januari mwaka zilizochukua nafasi ya ‘Magnetic Stripe Faida Debit Card’.

  Kadi za ‘Faida chip and pin Debit Card’ hutoa usalama wa hali ya juu kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’ inayodadavua taarifa za mteja ikiwa na mfumo madhubuti wa kiusalama hivyo kutoruhusu unakili wa taarifa za mteja husika.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa Benki ya Exim, Bw. Eugen Masawe jijini Dar es Salaam jana, mwisho wa kuchukua kadi hizo ni tarehe 15 Aprili, hivyo wateja wamebakiwa na siku zipatazo 13 kuanzia leo.

  “Tunatoa wito kwa wateja wetu kuchukua kadi zao za ‘Faida chip and pin Debit Card’ ambazo ni salama zaidi ukilinganisha na ‘Magnetic Stripe Faida Debit Card’ zilizokuwa zikitumika hapo awali.

  “Wateja hawatakuwa na uwezo wa kutumia kadi zao za zamani kuanzia tarehe 15 Aprili, kwani kadi hizo zitafungiwa. Hivyo wateja wanapaswa kutembelea matawi yao ili kuchukua kadi mpya,” alisema Bw. Masawe.

  Bw. Masawe alisema kuwa benki yake imedhamiria kutoa huduma bora kwa wateja na kusisitiza juu ya uchukuaji wa kadi hizo ambazo zitawasaidia wateja kufanya miamala yao ya kila siku katika mazingira salama zaidi.

  “Kwa kutumia kadi hii mpya ya kimataifa kutoka Benki ya Exim, mteja anaweza kuwa na uhakika kwamba miamala yake inafanyika katika mazingira salama kabisa,” alisisitiza.

  Aliongeza kuwa, Kadi hiyo mpya ya kimataifa inamuwezesha mteja kufanya miamala duniani kote katika mashine za ATM na POS zilizothibitishwa na MasterCard.


  0 0

  Mfalme wa Masauti Christian Bella ameachia Track yake mpya Nashindwa Audio pamoja na Video, Audio ya wimbo huo imefanywa chini ya Studio za Combination sound chini ya Producer man Walter na Video imefanyika Africa ya Kusini na director kutoka Bongo Adam Juma, Christian Bella amesema kuwa lengo la kwenda South Africa ilikua ni kufata location tu na pia amesema kuwa madirector wa Bongo wanauwezo mkubwa sana wa kufanya video nzuri kwa sasa isipokuwa hawana connection za TV kubwa za Africa na Nje ya Africa tofauti na Madirector wa SA ambao wana connection kubwa ya TV Kubwa hivyo wakikufanyia Video inafika Mbali zaidi.
  Mbali na hilo Bella anatarajia kufanya show kubwa siku ya tarehe 18/4 na inategemea kufanyika pale escape one huku msanii Alice mwenye asili ya Kiganda lakini anaishi Sweden anatarajiwa kuwepo siku hiyo, Alice amefanya Track kama Mpita Njia na Juliana lakini pia amefanya Yabolingo Track ambayo imefanya vizuri sana hapa Tanzania na Est Africa kwa ujumla. Wasanii wengine watakao shiriki siku hiyo bado hawajajulikana lakini bella amesema kuwa anatarajia kufanya na wasanii wa THT na wengine ambao bado wako kwenye mazungumzo na haitokuwa band yeyote ya dance.


older | 1 | .... | 789 | 790 | (Page 791) | 792 | 793 | .... | 3272 | newer