Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110144 articles
Browse latest View live

Mtandao wa mawasiliano wa seacom wapata kwikwi, wadau wahaha afrika mashariki

$
0
0
Kwa siku nzima ya leo, mawasiliano ya mtandao katika nchi za Afrika Mashariki yamepatwa na kwikwi kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni  matatizo ya kiufundi yaliyoikumba mitambo ya kampuni ya Seacom, inayotoa huduma  hiyo kwa njia ya mkongo upitao chini ya bahari.

Tayari Seacom, kupitia mtandao wake, imeomba radhi kwa kwikwi hiyo iliyosababisha tafrani kila mahali, ikiwemo Tanzania, na kuahidi kuirekebisha  haraka iwezekanavyo.

Globu ya Jamii inaomba Kunradhi wadau kwa kukumbwa pia na kwikwi hiyo ambayo iko nje ya uwezo wetu. Tunaahidi kundeleza Libeneke mara tu mambo yatapotegamaa.

Kwa kuwa hii si kwikwi ya kwanza, tungependa kujua endapo kama hatua mbadala za makusudi zimewekwa ama zipo kukabiriana na kwikwi kama  hii, ambayo kwa kweli inatoa raha kwa kukosesha wadau mawasiliano haya muhimu.

ANKAL


ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Franklin BOUKAKA anatamba hadi leo na ngoma yake ya 'AFRICA'

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Ngoma ya 'Cool It Now' ya New Edition ilitutoa jasho enzi hizo

Novelist Chinua Achebe dies, aged 82

$
0
0

Chinua Acebe
Chinua Achebe: 'grandfather of African fiction'.
Chinua Achebe, the Nigerian novelist seen by millions as the father of African literature, has died at the age of 82.
African papers were reporting his death following an illness and hospital stay in Boston this morning, and both his agent and his publisher later confirmed the news to the Guardian.
Simon Winder, publishing director at Penguin, called him an "utterly remarkable man".
"Chinua Achebe is the greatest of African writers and we are all desolate to hear of his death," he said.
In a statement, Achebe's family requested privacy, and paid tribute to "one of the great literary voices of all time. He was also a beloved husband, father, uncle and grandfather, whose wisdom and courage are an inspiration to all who knew him."
A novelist, poet and essayist, Achebe was perhaps best known for his first novel Things Fall Apart, which was published in 1958. The story of the Igbo warrior Okonkwo and the colonial era, it has sold more than 10m copies around the world and has been published in 50 languages. Achebe depicts an Igbo village as the white men arrive at the end of the 19th century, taking its title from the WB Yeats poem, which continues: "Things fall apart; the centre cannot hold."
"The white man is very clever. He came quietly and peaceably with his religion. We were amused at his foolishness and allowed him to stay. Now he has won our brothers and our clan can no longer act like one," says Okonkwo's friend, Obierika, in the novel.
The poet Jackie Kay hailed Achebe as "the grandfather of African fiction" who "lit up a path for many others", adding that she had reread Things Fall Apart "countless times".
"It is a book that keeps changing with the times, as he did," she said.
Achebe won the Commonwealth poetry prize for his collection Christmas in Biafra, was a finalist for the 1987 Booker prize for his novel Anthills of the Savannah, and in 2007 won the Man Booker international prize. Chair of the judges on that occasion, Elaine Showalter, said he had "inaugurated the modern African novel", while her fellow judge, the South African Nobel laureate Nadine Gordimer, said his fiction was "an original synthesis of the psychological novel, the Joycean stream of consciousness, the postmodern breaking of sequence", and that Achebe was "a joy and an illumination to read".
Nelson Mandela, meanwhile, has said that Achebe "brought Africa to the rest of the world" and called him "the writer in whose company the prison walls came down".
The author is also known for the influential essay An Image of Africa: Racism in Conrad's Heart of Darkness (1975), a hard-hitting critique of Conrad in which he says the author turned the African continent into "a metaphysical battlefield devoid of all recognisable humanity, into which the wandering European enters at his peril", asking: "Can nobody see the preposterous and perverse arrogance in thus reducing Africa to the role of props for the break-up of one petty European mind?"
According to Brown University, where Achebe held the position of David and Marianna Fisher university professor and professor of Africana studies until his death, this essay "is recognised as one of the most generative interventions on Conrad; and one that opened the social study of literary texts, particularly the impact of power relations on 20th-century literary imagination".
Born in 1930 in Ogidi, in the south-east of Nigeria, the author won a scholarship to the University of Ibadan, and later worked as a scriptwriter for the Nigeria Broadcasting Service. He chose to write Things Fall Apart in English – something for which he has received criticism from authors including Ngugi wa Thiong'o – but Achebe said he felt "that the English language will be able to carry the weight of my African experience. But it will have to be a new English, still in full communion with its ancestral home but altered to suit its new African surroundings".
His fourth novel, 1966's A Man of the People, anticipated a coup that took place in Nigeria just before the book was first published. "I'd ended the book with a coup," Achebe told the Guardian, "which was ridiculous because Nigeria was much too big a country to have a coup, but it was right for the novel. That night we had a coup. And any confidence we had that things could be put right were smashed. That night is something we have never really got over."
His most recent work was last year's mix of memoir and history There Was a Country, an account of the Nigerian civil war of 1967 to 1970.
Achebe was a supporter of Biafran secession, but after the end of the civil war in 1970 he took what he described as a "sojourn" in politics. There he found that "the majority of people … were there for their own personal advancement", deciding instead to devote himself to academia.
He went on to write what he called a "limited harvest" of five novels – the most recent of which was 1987's Anthills of the Savannah. "I go at the pace of inspiration and what I can physically manage," he said.
In 1990 a car accident in Nigeria left him paralysed from the waist down, and forced his move to the US. "I miss Nigeria very much. My injury means I need to know I am near a good hospital and close to my doctor. I need to know that if I went to a pharmacist, the medicine there would be the drug that the bottle says it is," he said in 2007.
Achebe has twice rejected the Nigerian government's attempt to name him a Commander of the Federal Republic – a national honour – first in 2004, and second in 2011. In 2004 he wrote that "for some time now I have watched events in Nigeria with alarm and dismay. I have watched particularly the chaos in my own state of Anambra where a small clique of renegades, openly boasting its connections in high places, seems determined to turn my homeland into a bankrupt and lawless fiefdom. I am appalled by the brazenness of this clique and the silence, if not connivance, of the presidency … Nigeria's condition today under your watch is, however, too dangerous for silence. I must register my disappointment and protest by declining to accept the high honour awarded me in the 2004 honours list."

MAPATO YA TAMASHA KUJENGA KITUO CHA YATIMA DAR

$
0
0

 Mwenyekiti wa Maandalizi ya Tamasha la Pasaka Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo kuhusu maandalizi ya tamasha hilo lenye kauli mbiu ya Amani na Upendo. Kulia ni Mdau wa muziki wa Injili, Mcharo Mrutu. 
WARATIBU wa tamasha la Pasaka litakalofanyika kwenye Uwanja
wa Taifa, jijini Dar es Salaam hapo Machi 31, wamepanga kutumia sehemu ya
mapato ya kiingilio kujenga kituo cha watoto yatima kama
ishara ya shukrani kwa jamii.(Picha na Francis Dande) 
======  ======  ======
Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati
maalumu inayoratibu tamasha hilo la kimataifa, Alex Msama, alisema kituo hicho kitakachokuwa chini ya kampuni ya Msama Promotions kitajengwa eneo la Pugu. 
Alisema uamuzi huo umefikiwa kwa lengo la kuwapa faraja
watoto yatima ambao nao wana haki ya kupatiwa matunzo na mahitaji muhimu katika makuzi yao ikiwemo elimu katika kujenga taifa bora la kesho.

“Tangu kuasisiwa kwa tamasha la Pasaka mwaka 2000, tumekuwa
tukirejesha sehemu 
ya mapato ya viingilio kwa jamii kwa njia ya misaada kwa 
yatima, wajane na walemavu, lakini safari hii tumeona twende zaidi ya hapo kwa kujenga kituo cha watoto,” alisema. Alisema lengo ni kujenga kituo hicho cha kisasa ambapo kama mipango itakwenda vizuri, kitakamilika kabla ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza muda wake kwani wangependa ndiye akizindue kwa kutambua mchango wake kwa tamasha hilo.

“Mwaka 2011, Rais Kikwete ndiye alikuwa mgeni rasmi wa
tamasha letu pale 
Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam. “Kitendo cha Rais kuacha kazi nyingi na kuja kutuunga mkono kwenye shughuli hii  ya kiroho, kwetu ni jambo kubwa sana ambalo kamwe hatutalisahau, hivyo tumeona tumpe heshima hiyo ya kuzindua kituo hicho akiwa bado madarakani,” alisisitiza.

Msama ametoa wito kwa wapenzi, mashabiki na wadau wa muziki
wa injili kujitokeza kwa wingi kuunga mkono juhudi za kampuni yake kuandaa tamasha hilo kwa malengo mbalimbali ikiwemo kueneza injili ya Mungu na kusaidia makundi maalumu. 
Kuhusu waimbaji, Msama alisema wale wa nje wataanza kuwasili wiki ijayo na kuongeza kuwa hadi kufikia Ijumaa, waimbaji wote  watakuwa wamefika tayari kwa tukio hilo mbalo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Aliongeza kuwa idadi ya waimbaji imeongezeka baada ya kujitokeza
kwa mwingine aliyemtaja kwa jina moja la Ntutuma kutoka nchini Kenya.
Baada ya kishindo cha tamasha hilo kutikisa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, itakuwa zamu ya Dodoma, Iringa, Mbeya, Mwanza kabla ya mashambulizi kuhimishwa mkoani Mara.

JAMBO LEO, BTL MABINGWA NSSF MEDIA CUP 2013

$
0
0
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala akimkabidhi kombe la Ubingwa wa michuano ya NSSF Media Cup 2013 kwa naodha wa timu ya Jambo Leo, Said Mwishehe katika baada ya kuifunga Changamoto bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika leo kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam. (Picha na Habari Mseto Blog)
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala akimkabidhi kombe la Ubingwa wa michuano ya NSSF Media Cup 2013 kwa naodha wa timu ya Business Times Queens, Lulu Habibu baada ya kuifunga TBC 39-18 katika mchezo wa fainali uliofanyika leo kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

 Wachezaji wa Jambo Leo wakifurahia ushindi wa timu yao.
Beki wa Changamoto John Robert akichuana na mshambuliaji wa Jambo Leo, Rogatius Katyali katika mchezo wa fainali ya michuano ya NSSF Media Cup 2013.
=======  ======  ======
TIMU za Jambo Leo na Business Times (BTL), zimefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya NSSF Media Cup 2013, baada ya kushinda mechi zao za fainali ya soka na netiboli dhidi ya Changamoto na TBC.

Katika fainali ya soka, bao pekee la kipindi cha kwanza la mshambuliaji Julius Kihampa, lilitosha kuwapa Jambo Leo ubingwa wa pili wa michuano hiyo iliyofanyika kwa mwaka wa 10 na harakati za Changamoto kusawazisha hazikuzaa matunda.

Kwa upande wa Netiboli, Business Times Queens ‘The Bize,’ ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mchezo huo kwa ushindi wa magoli 39-18 dhidi ya TBC, huku nyota wake Lulu Habibu akifunga mara 27.

Lulu alitwaa tuzo ya mfungaji bora wa michuano hiyo upande wa netiboli kwa kufikisha magoli 153 katika mechi nne alizocheza, huku tuzo hiyo kwa upande wa soka ikitwaliwa na Nurdin Msindo wa Tumaini Media, aliyefunga mabao manne.

Lulu na Nurdin kila mmoja alizawadiwa kiasi cha shilingi 300,000 ambayo ni zawadi kwa wafungaji bora, huku Sahara Media ikitwaa tuzo ya timu yenye nidhamu, ambapo walizawadiwa kikombe.

Kwa kutwaa ubingwa soka, Jambo Leo walizawadiwa kikombe na shilingi mil. 4, huku Changamoto wakitwaa shilingi mil. 3 kwa kushika nafasi ya pili na TBC wakizoa shilingi mil. 2 kwa kutwaa nafasi ya tatu - baada ya juzi Ijumaa kuwalaza IPP kwa penati 4-3.

‘The Bize Queens’, wamebeba kombe na shilingi mil. 3.5 za ubingwa wa netiboli, huku mshindi wa pili TBC wakilamba shilingi mil. 2 na mshindi wa tatu NSSF wakibeba kombe pekee na kitita chao cha shilingi mil. 1 wakikitoa kwa Tumaini iliyoshika nafasi ya nne.

NSSF Media Cup 2013 ni michuano iliyofanyika kwa wiki mbili kwenye viwanja vya TCC na DUCE vilivyoko Chang’ombe jijini Dar es Salaam, ikihusisha timu 17 za soka na 15 za netiboli zilizoundwa na wafanyakazi wa vyombo vya habari nchini.

Baada ya michuano hiyo kuzinduliwa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaundencia Kabaka Machi 9, ilihitimishwa leo kwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makalla kukabidhi zawadi kwa washindi wapya.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Makandarasi waliofutiwa usajili watakiwa kurejesha vyeti, kutofanya kazi

$
0
0
Na Ripota Wetu , Dar es Salaam
Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) imesisitiza kuwa wakandarsi 1110 waliofutiwa usajili hivi karibuni waharuhusiwi kufanya kazi yoyote hapa nchini kwa vile kuendelea kufanya kazi hivyo kutapelekea adhabu kali zaidi za kisheria.
Msajili wa Bodi hiyo, Eng. Boniface Muhegi aliwaambia waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kuwa wale wote waliofutiwa usajili hivi karibuni wanatakiwa kurudisha vyeti vya usajili wao kwenye bodi ya makandarasi kwa sababu kubaki navyo na kuendelea kufanya kazi ni kinyume na sheria.
Akitoa sababu za kufutiwa kwa usajili kampuni hizo alisema kampuni 10 zimefutiwa sababu majina yao yalitumiwa na kampuni nyingine zisizo na sifa; na kampuni 34 kwa kushindwa kutimiza masharti ya usajili katika mamlaka husika.
Alisema kampuni mbili zilishindwa kusimamia vizuri kazi; tano ziliomba zenyewe zifutwe na kampuni 1059 zilishindwa kulipa  ada ya usajili kwa muda unaotakiwa.
Hatua hii ya kufuta usajili wa idadi hii ya makandarasi imepata baraka za kibali toka kwa waziri wa ujenzi, Dkt. John Magufuli.
Alieleza kuwa kwa kampuni 1059 zilizoshindwa kulipa ada zao kwa wakati, wanaweza kulipa ada hiyo na faini ili bodi iweze kuangalia taratibu za kuwarudishia tena usajili wao.
“Kwa mujibu wa sheria mkandarasi aliyefutiwa usajili haruhusiwi kufanya kazi tena…hata kama alikua na kazi anaendelea nayo,” alisema, na kufafanua kuwa waajiri waliokuwa na wakandarasi waliofutiwa usajili wanatakiwa kutafuta wengine kwani wenye sifa zinazotakiwa wako wengi nchini.
Alisema mkandarasi aliyefutiwa usajili na kugundulika anafanya kazi atakabiliwa na kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya asilimia 10 ya mradi wote anaoutekeleza.
Alisema bodi kupitia ofisi zake za kanda itaendelea kuwafutia usajili wakandarasi nchini ambao wanashindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Alitoa wito kwa wanaotoa kazi kwa wakandarasi kushirikiana vyema na bodi hiyo kuhakikisha kuwa taratibu zinafuatwa na mafanikio yanapatikana katika sekta ya ujenzi nchini.
Alisema kuanzia mwaka 2000, kampuni za kizalendo zimekuwa zikiimarika na kufanya vizuri na kwamba bodi itaendelea kuzipatia mafunzo na uwezeshaji wa aina mbalimbali katika kiziimarisha na kuzijengea uwezo.
Alisema waajiri wote wanaotumia kazi za wakandarasi nchini wanahitajika kupata ushauri kutoka bodi hiyo ili kupata wakandarasi bora na kupata huduma iliyo bora na salama.

WFP, IFAD NA FAO ZAAHIDI USHIRIKIANO NA TANZANIA

$
0
0
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekutana na wakuu wa taasisi za kimataifa za WFP, IFAD na FAO na kufanya nao mazungumzo kuhusu namna ya kuendeleza kilimo nchini Tanzania.
 
Waziri Mkuu amekutana na viongozi hao Alhamisi (Machi 21, 2013) alipowatembelea kwenye ofisi zao jijini Roma, Italia kila mmoja kwa nyakati tofauti.
 
Mkurugenzi Mtendajiwa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Bi. Ertharin Cousin, alimweleza Waziri Mkuu kwamba shirika lake litaendelea kutumia bandari ya Dar es Salaam kusafirishia vyakula kwenda nchi zenye uhitaji wa chakula ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa ununuzi wa bidhaa kwa maendeleo (Purchase for Progress Programme).
 
“Tumekubaliana na wadau tunaoshirikiana nao, tuendelee kutumia bandari ya Dar es Salaam kupeleka mizigo Sudan ya Kusini na Uganda kwa sababu ya amani iliyopo nchini Tanzania. Kwa hiyo muamini kwamba sisi ni wadau wenu wa karibu na wa kuaminika,” alisema Bi. Cousin.
 
Akitoa mfano, Bi. Cousin alisema: “Kuna wakati kulikuwa na njaa kubwa kule Somalia na Zambia wakawa na hifadhi kubwa ya mahindi, lakini tulishindwa kusafirisha mahindi kutoka huko na kuyapeleka yanakohitajika kwa sababu ya hali mbaya ya usalama kwenye ukanda wa magharibi,” alisema.
 
Akizungumzia kuhusu ukuaji wa miji na kasi ya watu kuhamia mijini, Bi. Cousin alionya kwamba kuna haja ya kuwianisha uendelezaji wa miundombinu kwenye maeneo ya mijini na yale ya vijijini ili kuepuka tatizo la msongamano mkubwa wa watu mijini linalozikabili nchi nyingi zinazoendelea.
 
Alisema shirika lake limefanya utafiti nchini India na kubaini kuwa kadri kiwango cha ukuaji wa miji kinavyoendelea ndivyo kasi ya wakazi kuongezeka inavyozidi. “Tumeziainisha nchi za Kenya, Tanzania na Ethiopia na kuziweka kwenye mpango maalum ili zijipime jinsi zitakavyokuwa katika miaka 20 ijayo ili zisije kuwa na hali kama ya India hivi sasa,” aliongeza.
 
Naye, Rais wa Shirika la Kimataifa Kuendeleza Kilimo na Chakula (IFAD), Dk. Kanayo Nwanze alimweleza Waziri Mkuu kwamba shirika lake limeandaa mpando wa miaka mitatu ambao utazihusisha nchi 30 ikiwemo Tanzania ambazo zitafanyiwa impact evaluation kulingana na misaada ambayo zimekuwa zikipatiwa na shirika hilo.
 
“Tunataka tuangalie hali halisi kule Vijijini, je maisha ya wananchi yamebadilika kulingana na misaada ambayo tumekuwa tukiitoa? Je, wakulima wameongeza uzalishaji? Je wakulima wameunganishwa na masoko? Je, taasisi za kifedha zinawajali wakulima wadogo?” alifafanua Rais huyo wa IFAD.
 
Alisema hivi sasa wameanza kukusanya takwimu za awali (baseline data) katika nchi husika kabla ya kuanza kufanya tathmini itakayoanza mwaka huu hadi mwaka 2016.
 
Mapema, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), Bw. Jose Graziano da Silva alimweleza Waziri Mkuu kwamba shirika lake limetiliana saini makubaliano na benki ya Rabo (Rabobank) ili iweze kuwasaidia wakulima waliojiunga kwenye vyama vya ushirika.
 
“RaboBank imekubali kufanya kazi hiyo na imeichagua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zitakazokuwa waanzilishi wa mpango huo (pilot project)… watawasiliana nanyi muda si mrefu kuhusiana na suala hili,” alisema.Aliomba wakati mpango huo utakapoanza, wakulima wa Tanzania wawe tayari kushiriki kwenye mpango huo.
 
Waziri Mkuu Pinda kwa upande wake, katika nyakati tofauti aliwaarifu wakuu wa taasisi hizo za kimataifa juu ya hali ya uchumi wa Tanzania, Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP), Ukanda wa Kilimo wa Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT) na mchakato wa kuandaa Katiba mpya.
 
Alisema ili kuendeleza kilimo, ipo haja ya kushirikiana na wadau kutoka sekta binafsi kama njia ya kuleta maendeleo ya haraka nchini Tanzania. Bado tunayo changamoto ya kukabiliana na umaskini, lakini tunaamini kuwa kilimo ndiyo jawabu la tatizo hili,” alisema.
 
Waziri Mkuu alikwenda Roma, Italia kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete kwenye ibada maalum ya kumsimika Papa Francis iliyofanyika Jumanne, (Machi 19, 2013) kwenye viwanja vya Kanisa Kuu la Mt. Petro mjini Vatican, kisha akaamua kukutana na viongozi wa taasisi hizo.
 
Waziri Mkuu alirejea nchini Ijumaa, Machi 22, 2013).
 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
JUMAMOSI, MACHI 23, 2013.


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA SERIKALI YA UINGEREZA NA UJUMBE WAKE

$
0
0

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Serikali ya Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mark Simmonds (kulia kwake) aliyeongozana na ujumbe wake baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 22, 2013.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri wa Serikali ya Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mark Simmonds (kushoto) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 22, 2013.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Serikali ya Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mark Simmonds (kushoto kwake) aliyeongozana na ujumbe wake wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 22, 2013 kwa amazungumzo. Picha na OMR
======= ====== ======
MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKUTANA NA WAZIRI WA UINGEREZA ANAYESHUGHULIKIA MASUALA YA AFRIKA
DAR ES SALAAM, MACHI 22, 2013
 Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo Ijumaa, amekutana na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika Bwana Mark Simmonds ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo sambamba na masuala mengine akaelezea shukrani zake kwa serikali ya Uingereza kwa kuwa na mahusiano mazuri na Tanzania na kwa kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
 Mheshimiwa Makamu wa Rais aliyekuwa anamuwakilisha Rais katika mapokezi hayo alisema, Tanzania inathamini mchango wa Uingereza katika sekta za elimu na afya na sasa ambapo kampuni za Uingereza hasa British Gas inajihusisha katika utafutaji wa Gesi katika bahari ya kina kirefu Kusini mwa Tanzania. Pia alizungumzia kuhusu mchango wa Uingereza kimataifa hasa katika masuala ya Mazingira na akamueleza Waziri Simmonds kuwa, Uingereza inaweza kusaidia nchi zinazokabiliwa na athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa yenyewe kushirikiana na nchi kubwa duniani katika kuhakikisha kuwa zinatimiza wajibu wao katika kulinda mazingira.
 Kwa upende wake Waziri Simmonds yeye alimshukuru Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa mapokezi mazuri na kisha akaelezea furaha yake kwa mchango wa Tanzania katika kusaka amani katika nchi za Maziwa Makuu hasa DRC, Madagasca na Zimbabwe na kisha akafafanua kuwa, Tanzania ni mshirika mzuri wa Uingereza na kwamba nchi hii ni mfano wa kuigwa kutokana na ushiriki wake katika kusaidia amani kwa majirani zake sambamba na hatua zake za kuwapatia maendeleo wananchi wake.
 Waziri huyo alibainisha kuwa Uingereza iko tayari kuendelea kusaidia katika suala zima la uwazi na uwajibikaji na hasa katika maeneo ya Kodi na akashauri juu ya kuzidi kuwa na mashirikiano baina ya serikali na sekta binafsi katika shughuli za maendeleo.
Waziri Simmonds anakaa nchini kwa siku mbili na katika mkutano huu na Mheshimiwa Makamu wa Rais alifuatana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Diana Melrose.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam, Tanzania

Ras Inno kutambulisha rasmi bendi yake

$
0
0

MWANAMUZIKI nguli wa miondoko ya reggae hapa nchini, Ras Inno Nganyagwa,anatarajia kuitambulisha rasmi bendi yake katika onesho mahsusi linalotarajiwa kufanyika katikati ya mwezi ujao jijini Dar es Salaam.

Akizungumza hapa Globu ya jamii, Ras Inno alisema kwamba huo ni mwanzo wa kutimiza mikakati yake ya harakati za kurudi kwenye fani baada ya kujiweka pembeni kwa muda mrefu. Alisema kwamba, onesho hilo licha ya kuitambulisha bendi hiyo, lakini pia litakuwa mahsusi kwa ajili ujio wake mpya wenye mbinu za kisasa za kiweledi za kufanya kazi.

Nguli huyo ambaye pia ni mtafiti wa masuala mbalimbali ya kijamii na mwandishi maarufu wa safu mbalimbali katika magazeti ya hapa nchini, alibainisha kuwa baada ya kuwa nje ya ulingo kwa muda mrefu.

“Nimeamua kurudi rasmi kivingine kwenye fani baada ya kuusoma muziki wa reggae nikiwa pembeni na kubaini mapungufu kadhaa niliyotathmini, hivyo nimebuni mikakati mbadala tofauti ya namna bora ya kurudi jukwaani kwa dhamira ya kuipaisha reggae, pia kukonga nyoyo za mashabiki wake ambao hawajamuona jukwaani kwa muda mrefu,” alisema.

Akifafanua zaidi alisema kuwa licha ya kuitambulisha bendi yake ya kudumu atakayokuwa akitumbuiza nayo, tofauti na zamani ambapo alitumbuiza zaidi kama mwanamuziki huru anayepiga na kundi la wapiga vyombo bila jina rasmi la bendi.

Onesho hilo mahsusi pia litakuwa maalum katika kuitambulisha taasisi yake aliyoiunda itakayosimamia kazi zake ikiwemo bendi, pamoja na miradi aliyoibuni yenye lengo la kuupromoti muziki wa reggae ili kuhakikisha vijana wengi wanavutika na kujitosa kwenye miondoko hiyo, ili kupanua wigo wa idadi ya wanamuziki wa reggae kwa kuibua vipaji vipya.

Alisema onesho hilo litakalohudhuriwa na wadau wa muziki watakaoalikwa ambao taasisi yake inatarajia kushirikiana nao siku za usoni, litatumika pia kuitambulisha rasmi albamu yake mpya ya nne aliyoirekodia katika studio za Soundcrafters zilizopo Temeke hapa jijini, anayotarajia kuizindua hivi karibuni.

“Katika onesho hilo nitapiga nyimbo zangu zilizonipatia umaarufu miaka ya nyuma ukiwemo wimbo wa ‘Gila’ kutoka albamu ya Money-Pesa (1994), pamoja na nyimbo nyingine kutoka albamu zangu mbili zilizofuata na nyimbo mpya kutoka katika albamu mpya ya ‘Kwa Nini’.”

Utambulisho huo ni mwanzo wa maandalizi ya uzinduzi utakaofuatiwa na ziara ya maonesho yasiyopungua 10 katika awamu ya kwanza, itakayoanzia hapa jijini kabla ya kuelekea nyanda za juu Kusini na baadaye awamu ya pili itahusisha kanda ya Kaskazini na ziwa katika mfululizo wa maonesho ya kupromoti albamu yake mpya na muziki wa reggae kwa ujumla.

Katika onesho la utambulisho atasindikizwa na kundi la Kizazi Kipya cha Reggae, bendi ya Fimbo inayopiga miondoko ya asili, mwimbaji wa muziki wa gospo Mrs Annette Mwasambogo na Dj maarufu wa disco la reggae hapa nchini Aluta Warioba kutoka redio ya Times FM. 

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMJULIA HALI MZEE KINGUNGE NYUMBANI KWAKE

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, wakati alipofika kumjulia hali nyumbani kwake Victoria jijini Dar es Salaam jana Machi 23, 2013 baada ya mzee Kingunge kulazwa Hospitali ya Muhimbili kwa uangalizi hivi karibuni alipougua ghafla.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, wakati alipofika kumjulia hali nyumbani kwake Victoria jijini Dar es Salaam jana Machi 23, 2013 baada ya mzee Kingunge kulazwa Hospitali ya Muhimbili kwa uangalizi hivi karibuni alipougua ghafla. Kulia ni Mke wa Mzee Kingunge
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, wakati alipofika kumjulia hali nyumbani kwake Victoria jijini Dar es Salaam jana Machi 23, 2013 baada ya mzee Kingunge kulazwa Hospitali ya Muhimbili kwa uangalizi hivi karibuni alipougua ghafla. Picha na OMR

WAKAZI WA ARUSHA KULIPIA ANKARA ZA MAJI SAFI NA MAJI TAKA KUPITIA M-PESA SASA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya jiji la arusha, John Mongella,akiongea wakati wa uzinduzi rasmi wa jinsi ya kulipia Ankara ya maji safi kupitia huduma ya M-PESA,kwa wakazi wa mkoa wa jiji la Arusha,kutoka kushoto ni Mwenyekiti kamati ya mawasiliano na ujenzi Zanzibar Bw.Makame Mshimba Mbaruk,Mwenyekiti wa bodi ya (AUWSA) Bw.Felix Mrema.
Mkuu wa Wilaya ya jiji la arusha, John Mongella,wanne toka kushoto akifatilia maelekezo toka kwa Mkuu wa Vodacom kanda ya kaskazini Bw.Philemon Chacha jinsi ya kulipia Ankara ya maji safi kupitia huduma ya M-PESA,mara baada ya kuzindua huduma hiyo mkoani humo ambapo wakazi wa jiji la arusha watakuwa wakilipia Ankara za maji safi na maji taka kwa kupitia huduma hiyo,wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Mwenyekiti kamati ya mawasiliano na ujenzi Zanzibar Bw.Makame Mshimba Mbaruk,Mwenyekiti wa bodi ya (AUWSA) Bw.Felix Mrema naMkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja wa (AUWSA) Masoud Katiba.
Mkuu wa Wilaya ya jiji la arusha, John Mongella,watano kutoka kushoto waliokaa,akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom na wa mamlaka ya maji safi na maji taka ya Arusha (AUWSA) mara baada ya hafla fupi ya uzinduzi wa kulipia Ankara za maji safi na maji kupitia huduma ya Vodacom M-PESA kwa wakazi wa jiji la arusha.

Nancy Sumari: Nililipwa Mshahara wa 120,000 Kwa Mwezi

$
0
0
Katika kipindi cha Makutano kinachoendeshwa na Fina Mango wiki hii alifanya mahojiano na Miss Tanzania na Miss World Africa 2005, Nancy Sumari kuhusu mambo mbalimbali yanayomhusu katika maisha ya kabla na baada ya kutwaa mataji hayo makubwa na kuingia katika historia kama Miss Tanzania aliefanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya ulimbwende duniani.

Nancy ambaye hivi karibuni amezindua kitabu cha watoto alichokipa jina la Nyota Yako alielezea nini hasa kilichomsukuma hadi kuamua kuandika kitabu hicho na kusema ilitokana na baada ya kuwa mama na kujikuta kila akienda maduka ya vitabu anakosa vitabu vya watoto vilivyoandikwa na waandishi wa Tanzania na kukuta vingi ni kutoka nje ya nchi, hivyo kuamua kuandika kitabu ambacho watoto wa kike wa Tanzania wataweza kukisoma na kuvutiwa kufanya kile ambacho muandishi amekielezea. “Kwa hivi sasa kitabu kinapatikana maduka ya Scholastica Mlinani City na pia Novel Idea Masaki na Ohio kwa shilingi 5,000 tu” alisema Nancy.

Lakini Nancy alikuwa na stori ya kusisimua kwani anasema kabla ya kuingia kwenye mashindano ya urembo alilazimika kufanya kazi kama muuzaji katika duka la fenicha kwa mshahara wa shilingi lakini moja na ishirini kwa mwezi. Hii ilitokana na kukwama kupata nafasi ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kitivo cha Sheria kutokana na chuo hicho kutoruhusu mwanafunzi aliemaliza kidato cha nne kwa elimu ya Kenya kujiunga moja kwa moja kwa ajili ya shahada.

Nancy amesema alifanya kazi hiyo kwa moyo wote hadi alipopata nafasi ya kushiriki taji la Miss Dar Indian Ocean baada ya kuonwa na wandaaji wa shindano hilo na kuibuka mshindi wa pili na baadae kuibuka Miss Kinondoni na hatimaye Miss Tanzania huku akisema kufanya kila kitu bila kuogopa kushindwa ndio siri hasa ya kufanikiwa licha ya kutokuwa na uzoefu wowote katika suala la urembo wa wakati huo na kusema hatimaye alifanikiwa kupata nafasi ya kuingia chuo kikuu cha Dar es salaam na atatarajia kumaliza masomo yake mwezi Julai.

Alipoulizwa nini ushauri wake kwa vijana wanaochipukia alisema “Let’s all try to become better people, everyone makes mistake no one is perfect lakini ni muhimu kama binadamu kujitahidi kufanya vitu sahihi sawa na unapoona ua linafifia linamwagilizie maji likue na unapomuona mwenzio anahitaji msaada na unayo nafasi ya kumsaidia usisite”

Mahojiano yote yanapatikana katika:


Muendeshaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango akimsikiliza Nancy Sumari
Nancy Sumari akijibu moja ya maswali aliyoulizwa na Fina Mango

hoja ya haja........

$
0
0
Kaka Michuzi Salaam Aleuikum,

Baada ya salaam, napenda kulizungmzia ili swala au kero linalowasumbua watanzania wengi. Kwa kweli, kwenda kupumzika au kula Sea-Cleaf ni tatizo ambalo uongozi wa jiji au serikali inabidi iingilie kati kwani tunakoelekea ni kubaya zaidi, kwani itafika hatua kila mtu atajichukulia hatua ya kufanya kila atakalo kwa manufaa yake Kwa muda mrefu nimekuwa mteja wa eneo la Sea-Cliff hasa sehemu ya Karambezi restaurant. 

Napenda sana kwenda pale na familia yangu. Kwa bahati mbaya kwenda pale sasa hivi na gari ni tatizo. Chakula ni ghali kuliko sehmu ya kula ulaya. Mbaya zaidi, wanachaji kupaki gari. Yaani licha ya kwamba chakula ni ghali mno, bado unalazimishwa kulipia kupaki vinginevyo hautoki Majuzi nilipoenda pale, nililalamika sana kuhusiana na hii tabia. Nikamwambia mkuu mmoja mwenye asilia ya Ki-Asia kwamba huu ni unyang’anyi. 

Yeye badala ya kunielewesha, aliniporomoshoea tusi la nguoni.Sikuwa na la kujibu. Tunaiomba serikali iingilie kati kuisaidia umma wa kitanzania. Vinginevyo tutawaomba wanchi waanze kuisusia hii sehemu kutokana na mwendelezo wa hii tabia. Serena, Kilimanjaro hata na Double tree ambazo ni za daraja za juu kupaki ni bure, lakini Se-Cleaf wanachaji kupaki. Uongozi wa Sea-Cleaf tunaomba muingilie kati hili tatizo la kuwachaji wateja wenu kupaki gari ili kuja kula. 

Nawakilisha 
Mdau

Taifa Stars yaihadhilisha Morocco leo Uwanja wa Taifa,Yaitungua Bao 3-1

$
0
0
 Ubao wa Matokeo unavyosomeka mara baada ya kumalizika kwa mechi kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Timu ya Taifa ya Morocco uliochezwa jioni hii kwenye uwanja wa Taifa wa Jijini Dar es Salaam.
 Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars),Thomas Ulimwengu akiwatoka Golikipa na Beki wa Timu ya Taifa ya Morocco wakati wa Mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu kucheza Kombe ya Dunia Mwaka 2014 kule nchini Brazil,uliochezwa jioni hii kwenye uwanja wa Taifa wa Jijini Dar es Salaam.Taifa Stars imeshinda Bao 3 - 1,mabao yaliyotiwa kimiani na Mshambuliaji Machachari,Mbwana Samatha.

PICHA ZAIDI ZITAKUJIA MUDA MFUPI UJAO.

Habari za Tanzania toka TBC

PLOT FOR SALE IN ZANZIBAR

$
0
0
                   A huge lovely Beach plot with newly built VILLA cottage in MARUMBA/ UROA ZANZIBAR  for sale                




 Plot   Number 211

                Measuaring   5091,40 square meters
                Survey  plan Number   5.88/2009
                            For more Information please contact the following  
Emails IN Zanzibar   salimmasoud05@hotmail.com
               Tel   0773 925860
Germany   gombani@sinntal.net                
Zanzibar   Salum  Mohd                

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Gloria Esteffan na miami sound machine walitisha na ngoma yao ya 'dr beat'

Stanbic Bank Tanzania encourages women to use land as collateral

$
0
0
Stanbic Bank Tanzania Home Loan Manager Miranda Lutege, makes a presentation on how bankers avail opportunities to women to use land as collateral investment through Mortgage, during 2013 Annual General Meeting for Tanzania Women Lawyers Association (TAWLA) and Continuing Legal Education sponsored by Stanbic Bank Tanzania, held at Bank of Tanzania hall at the weekend. The meeting had the theme; from being defensive to being proactive: Women, Land and Investment.

DC ILALA AWAFUNDA VIJANA KUHUSU UJASIRIAMALI

$
0
0
Baadhi ya Vijana waliopata mafunzo ya  jinsi ya kutengeneza mkaa mbadala wakionyesha jinsi ya kutengeneza mkaa huo wakati wa ufungaji wa Mafunzo ya Ujasiriliamali kwa vikundi vya Vijana kutoka Kata za Vingunguti na Buguruni jijini Dar Es Salaam.Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa Ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Plan.

Mmoja wa wahitimu akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Raymond Mushi wakati wa ufungaji wa Mafunzo ya Ujasiriliamali kwa vikundi vya Vijana kutoka Kata za Vingunguti na Buguruni jijini Dar Es Salaam.Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa Ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Plan.Kushoto ni Meneja Miradi wa Plan Wilayani Ilala Bw.Daniel Kalimbiya.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Raymond Mushi akimsikiliza mmoja wa Vijana waliopata mafunzo ya  jinsi ya kutengeneza mkaa mbadala wakati wa ufungaji wa Mafunzo ya Ujasiriliamali kwa vikundi vya Vijana kutoka Kata za Vingunguti na Buguruni jijini Dar Es Salaam.Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa Ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Plan
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Raymond Mushi akiangalia mkaa mbadala wakati wa ufungaji wa Mafunzo ya Ujasiriliamali kwa vikundi vya Vijana kutoka Kata za Vingunguti na Buguruni jijini Dar Es Salaam.Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa Ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Plan.
Vijana  waliopata mafunzo ya  jinsi ya kutengeneza mkaa mbadala wakimsikiliza Mgeni Rasmi wakati wa ufungaji wa Mafunzo ya Ujasiriliamali kwa vikundi vya Vijana kutoka Kata za Vingunguti na Buguruni jijini Dar Es Salaam.Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa Ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Plan.(Picha na Demetrius Njimbwi-Jeshi la Polisi).
===============  =========  ==============
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi
Vijana nchini wameshauriwa kuacha kubweteka na kuonekana mzigo kwa familia na badala yake wajikite katika ujasiriamali ili kupambana na hali ngumu ya maisha hatua itakayo wasaidia kuongeza kipato na kuinua uchumi wao.
Wito huo umetolewa mapema jana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi wakati akifunga mafunzo ya siku tano ya ujasiriamali wa kutengeneza mkaa unaotokana na mabaki ya takataka za majumbani na viwandani kwa Vikundi vya Vijana kutoka Kata za Vingunguti na Buguruni yaliyofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Plan na kuendeshwa na Wakufunzi kutoka Shirika la Kuhudumia viwanda vidogo (SIDO).
Mh. Mushi amesema kuwa, moja ya changamoto zinazowakabili vijana wengi ni kutokupenda kujishughulisha na badala yake hutumia muda wao mwingi katika kufanya mambo yasiyo na faida hali ambayo imekuwa ikichangia kurudisha nyuma jitihada zao za kujiletea maendeleo.
Alisema kuwa pamoja na mafunzo yaliyotolewa kwa vijana hao, bado wanajukumu la kutambua maendeleo yanaletwa na wao wenyewe kwa kuutumia ipasavyo ujuzi walioupata hatua itakayo saidia kufungua fursa ya ajira.
Aidha  aliwataka vijana kuzingatia maadili ikiwa pamoja na kuthamini mafunzo waliyoyapata na kuwa na tabia ya kushirikiana  katika mambo yatakayo  wasaidia kuongeza ujuzi  pamoja na kutanua wigo wa kibiashara.
Kwa upande wake Meneja Miradi wa Shirika  Plan Wilayani Ilala Bw. Daniel Kalimbiya amesema kuwa, bado wataendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali ili kuboresha maisha ya Watanzania ikiwa  pamoja na kuwataka vijana kutokujiingiza katika vitendo viovu vya uhalifu ikiwemo kujiuza katika madanguro kwa kisingizio cha kukosa ajira.
 “Tumieni fursa vyema mliyoipata hapa ili mjiletee maendeleo na sisi tutaendelea kushirikiana na kuviwezesha vikundi vya Vijana ambavyo vimekuwa vikifanya vizuri katika kujiletea maendeleo kwani malengo ya shirika letu ni kutetea haki za Watoto na Vijana”Alisema Kalimbiya
Naye Meneja wa SIDO Mkoa wa Dar Es Salaam Hamwel Meena aliahidi kuwapatia vijana hao mikopo itakayowawezesha kununua mashine zitakazowawezesha kufanya kazi ya kutengeneza Mkaa mbadala kwa ufanisi ili kuokoa mazingira na kuufanya mji kuwa msafi kwakuwa mkaa huo unatengenezwa kutokana na takataka.
Viewing all 110144 articles
Browse latest View live




Latest Images