Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 779 | 780 | (Page 781) | 782 | 783 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Tanga
  KAMPUNI ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, imemjaza noti kiungo Joseph Mahundi wa Coastal Union baada ya mwishoni mwa wiki kumkabidhi Sh. Milioni 1/-kutokana na kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu.

  Mahundi, kiungo fundi aliyekulia kwenye kituo cha Azam FC jijini Dar es Salaam, aliibuka Mchezaji Bora wa Mwezi Desemba 2014 wa VPL akiwa ni mchezaji wa nne kutwaa tuzo hiyo tangu ianzishwe msimu huu na kampuni hiyo.

  Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia aliyekuwa amefuatana na Ofisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude, ndiye aliyekabidhi zawadi hiyo kwa Mahundi dakika chache kabla ya kuanza kwa mechi ya VPL ya Coastal dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini hapa Jumapili.

  Baada ya mechi hiyo kumalizika huku Azam FC wakiibuka na ushindi wa bao 1-0, Mahundi aliipongeza Vodacom Tanzania kwa kuanzisha tuzo hiyo.

  "Ninawashukuru na kuwapongeza Vodacom kwa kuanzisha tuzo hii kutambua mchango wa wachezaji wanaofanya vizuri VPL. Ninawashukuru pia TFF kwa kuona kutambua uwezo wangu na kunitangaza mshindi wa Desemba. Nitaendelea kujituma zaidi ili nikuze soka langu na kuisaidia Coastal Union," alisema Mahundi.

  Matina Nkurlu, Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, alisema kuwa kampuni hiyo itaendelea kutoa zawadi kwa wachezaji wanaofanya vizuri ikiwa ni sehemu ya mikakati na mchango wake katika kuinua kiwango cha michezo, hususan mpira wa miguu nchini.

  Tangu tuzo hiyo ianze kutolewa Septemba mwaka jana, ni Coastal Union pekee iliyofanikiwa kutoa wachezaji wawili walioitwaa hadi sasa.

  Washindi wa tuzo hiyo tangu ianzishwe ni Antony Matogolo wa Mbeya City (sasa yuko kwa mkopo Panone FC ya Kilimanjaro) aliyeitwaa Septemba, Salum Abubakar 'Sure Boy' wa Azam FC (Oktoba), Rashid Mandawa wa Kagera Sugar (Novemba), Mahundi, Said Bahanunzi wa Polisi Moro (Januari) na Godfrey Wambura wa Coastal Union (Februari).
  Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia(kushoto)akimkabidhi kombe na hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 1/- Joseph Mahundi wa Coastal Union kwa kuibuka mchezeji bora wa Mwezi Desemba 2014 wa(VPL) kabla ya mechi kati ya timu yake na Azam FC iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini hapa Jumapili.Aliyeshikilia hundi kulia ni Ofisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude.


  0 0


  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Jasmine Tiisekwa aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, akikata utepe kama ishara ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa kijiji cha Mseta wilayani Kongwa wakati wa kilele cha maadhiisho ya wiki ya maji Mkoa wa Dodoma Machi 22, 2015.
   Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Jasmine Tiisekwa aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa kijiji cha Mseta wilayani Kongwa wakati wa kilele cha maadhiisho ya wiki ya maji Mkoa wa Dodoma Machi 22, 2015.
   Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Jasmine Tiisekwa aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, akifungua bomba la maji kama moja ya zoezi lililofanyika wakati wa kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa kijiji cha Mseta wilayani Kongwa wakati wa kilele cha maadhiisho ya wiki ya maji Mkoa wa Dodoma Machi 22, 2015.


  0 0

  Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mrimia Mchomvu (aliyesimama), akisisitiza jambo kwa Wafanyakazi wapya wa Wizara hiyo (hawapo pichani), wakati wa ufunguzi wa Mafunzo Elekezi uliofanyika Jumatatu - Machi 23, 2015, katika Ukumbi wa Elimu ya Watu Wazima – Dar es Salaam. Mkurugenzi Mchomvu alifungua rasmi mafunzo hayo kwa niaba ya Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara husika, Mhandisi Ngosi Mwihava.
  Mmojawapo wa Washiriki wa Mafunzo Elekezi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Ester Njiwa (aliyesimama), akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Washiriki wenzake kwa Uongozi wa Wizara husika, kwa kuandaa mafunzo hayo. Mafunzo hayo ya siku tano (5), yalifunguliwa rasmi Jumatatu – Machi 23, 2015 na Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi, Mrimia Mchomvu kwa niaba ya Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Ngosi Mwihava.


  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Prime Minister of Singapore, H.E. Lee Hsien Loong
   PRESS RELEASE
  H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a condolence message to H.E. Lee Hsien Loong, Prime Minister of Singapore following the death of his father and founding Prime Minister of Singapore, the late Mr. Lee Kuan Yew.

  The message reads as follows:

  “H.E. Lee Hsien Loong,

  Prime Minister of Singapore,

  SINGAPORE.

  Your Excellency and dear brother,

  I am writing to extend my deep condolences and that of the government and the people of the United Republic of Tanzania following the death of your father and founding Prime Minister of your nation Mr. Lee Kuan Yew.

  The demise of Prime Minister Yew is a great loss not only to Singapore but also to all who saw in him an example of a nation builder. The late Yew was admired by the people of Tanzania as a leader whose input in building Singapore is immeasurable, a selfless leader and a friend of all.

  May sincere wish in remembering the late Yew is to emulate him in practice and always embracing his contribution as a leader and role model.

  The People and the Government of the United Republic of Tanzania                        will continue to pray for peace, compassion and strength for the family and the People of Singapore in the time of sorrow and also for the nation as ending’s demise is an immense loss to all Singaporeans.

  Your Excellency,

  Please accept my condolences and may the Almighty God rest his soul in eternal peace.

  Please accept, Your Excellency the assurances of my highest consideration”.

  Issued by: The Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam

  23rd March 2015


  0 0

  Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam limetoa misaada ya kibinadamu kwa watoto yatima wa kituo cha Msimbazi centre ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Maji yaliyoanza mapema tarehe 16 na kufika kilele 22 machi mwaka huu.

  Akiongea na vyombo vya habari, Afisa Uhusiano wa DAWASCO, Bi Everlasting Lyaro alisema msaada huu ni sehemu ya jamii wanayotoa huduma hiyo kila siku.

  “sisi kama DAWASCO tumeguswa na mahitaji ya watoto hawa na kama sehemu ya Jamii na katika kuadhimisha wiki ya Maji tumeona tutoe msaada wa hali na mali kwa watoto hawa ili kuwakumbusha jamii umuhimu wa kukumbuka jamii kama hizi” alisema Lyaro

  Nae mlezi wa watoto hao sister Anna Francis alishukuru kwa msaada huo na kuitaka jamii kukumbuka watu wenye mahitaji mbalimbali kama sehemu ya ibada na utu katika sehemu ya maisha ya binadamu.

  Maadhimisho ya wiki ya Maji yalianza mapema wiki iliyopita na yalifika kilele Jumapili hii ambako kitaifa yalifanyika mkoani Musoma.
  Ofisa Uhusiano DAWASCO, Everlasting Lyaro (kushoto) akikabidhi msaada wa chakula kwa mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Msimbazi Opharn Centre, sista Anna Francis katika kuhitimisha wiki ya Maji kwa kutoa msaada kwa jamii inayowazunguka jijini Dar es salaam.

  0 0

  BENDI ya muziki wa dansi hapa nchini,Mashujaa Band 'Wana Kibega' leo imemtangaza Aliyekuwa mwanamuziki na mtunzi wa bendi ya Ruvu Stars, Rogert Hegga 'Katapila' kujiunga rasmi katika bendi hiyo.

  Mkurugenzi wa bendi ya Mashujaa, Maximilian Luhanga, alisema kuwa Hegga amejiunga rasmi na bendi hiyo na watamtambulisha katika onyesho maalumu litakalofanyika Aprili 5.

  Luhanga alisema kwamba kujiunga kwa msanii huyo ni moja ya mikakati ya kuiimarisha Mashujaa ili iweze kuwa bendi bora hapa nchini kama ilivyoweza kung'aa kwenye tamasha la tuzo za muziki la Kilimanjaro.

  Alisema kuwa ujio wa msanii huyo utaongeza changamoto kwenye bendi yao ambayo imelenga kufanya vizuri zaidi kwenye safu ya muziki wa dansi hapa nchini.

  Hegga alisema kwamba ameamua kujiunga na Mashujaa kwa sababu anataka kufanya kazi katika bendi yenye wasanii wenye uwezo ambao watatumia vipaji vyao kuwafurahisha mashabiki wao.

  Aliahidi kutowaangusha mashabiki wa bendi hiyo na mashabiki wake binafsi ambao wanakubali uwezo alionao kwenye sanaa hiyo.

  "Nimekuja kuongeza chachu, nimejiunga Mashujaa kwa sababu nafahamu wasanii walioko kwenye bendi hii ni bora, naahidi kuwapa furaha na raha mashabiki wa bendi hii, hawatajutia ujio wangu ndani ya Mashujaa", alisema mwanamuziki huyo ambaye amewahi pia kufanya kazi katika bendi ya Mchinga Sound na African Stars 'Twanga Pepeta'.

  Akizungumzia ujio wa mwanamuziki huyo Rais wa bendi hiyo Charles Gabriel 'Chalz Baba Kingunge' alisema kwamba amefurahia ujio wa Hegga ambaye anamuamini na kuufahamu uwezo wake wa kazi.

  Alisema kwamba ushirikiano atakaouonyesha yeye na Hegga utasaidia kuinyanyua bendi na kuendelea kutamba hapa nchini.

  "Moyo wangu umejaa furaha, nasema karibu sana Mashujaa, najua uwezo wangu na wako utatoa matunda mazuri na yenye kulifunuka jiji", aliongeza Chalz. Moja ya nyimbo ambazo zilipata umaarufu na kutamba zilizotungwa na Hegga ni Fadhila kwa Wazazi ambayo aliiandaa akiwa na Twanga Pepeta.

  0 0

  Camera ya Globu ya Jamii imeinasa taswira hii ya samaki wakikaushwa tayari kwa matumizi mengine ikiwemo kitoweo,taswira hiyo imenaswa katika kitongoji cha Kiyungi katika kijiji cha Mijongweni,wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
  Sehemu ya soko ndani ya mji wa Machame wilayani Hai.
  Moja ya Daraja maarufu sana wilayani Hai,liitwalo Daraja la MNEPO linalopatikana katika kitongoji cha Kiyungi, kijiji cha Mijongweni,wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
   Shamba la Migomba ndani ya Machame wilayani Hai,kama lionekavyo mara baada ya kunaswa na kamera ya Globu ya Jamii. 

  0 0

  Freddy Malima from Dar Es Salaam is the first winner in theongoing #MakeitHappenEAcompetition and will get the chance to take his girlfriend for an all-expenses paid trip to the Mikumi National Park this Easter season as Lumia continues to reward consumers.
  Launched in January 2015, the #MakeItHappenEA aims to empower customers to share their life long desires, and 4 lucky winners will be selected and get a rare opportunity of bring their dream to life.
  Meanwhile, the main prize is only one week away as one lucky consumers stands a chance to win a life changing all expenses paid Experience with friends toCape Town, South Africa courtesy of Lumia.
  To participate, buy any Lumia device*, visit the www.lumialiving.com page where you enter your details and share your dream!
  Winners will be announced on the official Microsoft Lumia social media pages and will be contacted by the Microsoft team to plan how to bring their dream to reality!To learn more about the campaign, follow the #MakeItHappenEA conversations on:

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Utafiti unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 30 ya vifo vya watu walioathirika na Ukimwi vinatokana na Ugomjwa wa Kifua Kukuu na inakadiriwa  kuwa tangu kuanza  kwa ugonjwa wa ukimwi, kati ya asilimia tano (5) hadi 10 ya watu wenye VVU wana ugonjwa wa kifua kikuu  na takribani ya asilimia 40 wanaouguwa  kifua kikuu  wana maambukizo ya VVU.

  Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Dk.Donan Mmbando wakati akitangaza maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani kwa waandishi wa habari ofisini kwake jijni Dar es Salaam ambayo hufanyika Machi 24 kila  mwaka .

  Dk.Mmbando amesema, Tanzania ni nchi ya Sita katika bara la Afrika kwa kuwa na wagonjwa wengi wa kifua kikuu na takwimu za Wizara ya Afya ziligundua kuwepo kwa wagonjwa wa Kifua Kikuu zaidi ya 65,000 kwa mwaka 2013,utafiti wa mwaka 2012  wa kutathimini kiwango cha ugonjwa huo,ulionyesha kuwa idadi kubwa ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 wapo katika hatari ya kupata ugonjwa huo.

  Aidha amesema Kifua Kikuu ni ugonwa unaoambukiza na unasababishwa na vimelea aina ya bacteria na mtu anayeugua ugonjwa huo ni rahisi kuambikiza kwa watu wengine  kwa kukohoa au kupiga chafya.

  Dk.Mmbando aliendelea zaidi kwa kumesema kwa sasa takribani zaidi ya watu milioni 1.5 duniani  wanafariki kwa ugonjwa wa kifua kikuu kila mwaka na asilimia kubwa ya vifo hivyo vinatokea katika  nchi za Kusini  mwa Jangwa la sahara na Tanzania ni kati ya nchi 22 yeye idadi kubwa ya wagonjwa wa kifua Kikuu Duniani.

  nchi hizo zinachangia asilimia 80 ya wagonjwa wa kifua kikuu ulimwenguni.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt.Donan Mmbando akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Wizarani hapo leo Machi 23,2015.Kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali,Dkt. Margaret Mhando.
  Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma,Dkt. Beatrice Mutayobya akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika kwenye ofisi ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,leo Machi 23,2015 jijini Dar es salaam.Picha na Emmanuel Massaka.

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji,Dk. Diodorus Buberwa Kamala akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu wa Serikali ya Wabelgiji Wanaozungumza Kijerumani,Mhe. Oliver Paasch,wakati alipokutana nae leo ofisini kwake jijini Eupen Ubelgiji.
  Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji,Dk. Diodorus Buberwa akimkabidhi zawadi Waziri Mkuu wa Serikali ya Wabelgiji Wanaozungumza Kijerumani,Mhe. Oliver Paasch baada ya kumaliza mazungumzo naye ofisini kwake Eupen Ubelgiji.

  0 0

  Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Lindi,Fortunata Raymond akitoa elimu ya umuhimu na faida ya kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF),kwa viongozi wa chama cha mpira wa miguu na vilabu vilivyopo Manispaa ya Lindi mjini,ambapo aliwataka kutambua na kuchangamkia fursa ya kujiunga na mfuko huo kwani ni wa gharama nafuu,utakaowawezesha kupata huduma za matibabu na familia zao kwa kuchangia mara moja kwa mwaka mzima,elimu hiyo ilifanyika kwenye Uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi.
  Mwalimu Fikiri ambaye ni mweka hazina wa chama cha mpira wa miguu Manispaa ya Lindi akiuliza jambo kwa mtoa mada ambaye ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Lindi,Fortunata Raymond (hayupo pichani) wakati wa utoaji elimu kwa viongozi hao uliofanyika hivi karibuni kwenye viwanja vya mpira wa miguu ilulu lindi.

  0 0

  Wananchi wa Bomang'ombe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipowahutubia jioni ya leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapo wilayani Hai,mkoa wa Kilimanjaro.
   katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akipita kwenye moja ya daraja maarufu sana wilayani Hai,Dara la MNEPO (la zamani) lililopo katika kitongoji cha Kiyungi kijiji cha Mijongweni,wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua ujenzi wa daraja jipya la MNEPO ambalo lipo katika hatua za mwisho kukamilika,lililopo katika kitongoji cha Kiyungi kijiji cha Mijongweni,wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya wakazi jamii ya kimasai kutoka kijiji cha Mtakuja,wilayani Hai,mara baada ya kusikiliza mgogoro wao wa ardhi na kampuni ya KADCO,ambapo Ndugu Kinana ameahidi kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka mingi.
   Baadhi ya wakazi jamii ya kimasai kutoka kijiji cha Mtakuja,wilayani Hai,wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwa staili ya aina yake,alipokuwa akiondoka kijijini hapo mara baada ya kuzungumza nao kusikiliza mgogoro wao wa ardhi na kampuni ya KADCO,ambapo Ndugu Kinana ameahidi kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka mingi. SOMA HAPA KUHUSIANA NA MGOGORO HUO
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiongozwa kukagua chumba kipya cha mionzi,pichani nyuma ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Mh.Leonidas Gama.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akifanya majaribio ya uchunguzi juu ya mkono wake kupitia mashine mpya ya mionzi,iliyowekwa katika chumba hicho cha mionzi.

  PICHA NA MICHUZI JR-HAI KILIMANJARO 


  0 0

  Na Bakari Issa,Dar es Salaam

  Kampuni ya Ask Indus (T) Limited yenye lengo la kuunganisha kati ya Tanzania na India katika nyanja ya Afya,elimu pamoja na masuala ya biashara hususan katika sekta binafsi imezinduliwa rasmi leo,nchini Tanzania.

  Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam,Balozi wa India nchini,Mhe. Debnath Shaw amesema Watanzania watafaidika na Kampuni hiyo kwa kuwa itatoa msaada zaidi katika matibabu bora,Elimu bora kwa wanafunzi pamoja na huduma bora zaidi za kibiashara kwa Wafanyabiashara.

  Aidha,Shaw ameishukuru nchi ya Tanzania kwa ushirikiano mpaka kuanzishwa kwa Kampuni hiyo ambayo itawasaidia Watanzania,pamoja na kuunganisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

  Naye,Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ask Indus,Bw.Abhilash Puljal amemshukuru Balozi wa India nchini kwa kukubali wito wa kuja ili kufanya uzinduzi wa Kampuni hiyo itakayowasaidia Watanzania kupata huduma bora ya Afya,Elimu pamoja na biashara nchini India.

  Kampuni ya Ask Indus (T) Limited ina matawi mengine katika nchi za India,Kenya,Mauritius pamoja na Nigeria.
  Balozi wa India nchini,Mhe. Debnath Shaw (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kampuni ya Ask Indus itakayojihusisha na masuala ya utoaji huduma za Afya,Elimu pamoja na biashara,uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ask Indus,Bw.Abhilash Puljal.
  Balozi wa India nchini,Mh. Debnath Shaw (aliyesimama) akizungumza jambo kwa wadau kuhusu Kampuni ya Ask Indus ambayo itajihusisha na utoaji huduma za Afya,Elimu pamoja na biashara,iliyozinduliwa rasmi leo jijini Dar es salaam.Wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Ask Indus,Bw. Abhilash Puljal (katikati) na kulia ni Msimamizi wa Tawi la Tanzania,Bw. Prakash.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ask Indus,Bw.Abhilash Puljal (kulia) akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Kampuni yake hiyo yenye lengo la kuunganisha kati ya Tanzania na India katika nyanja ya Afya,elimu pamoja na masuala ya biashara hususan katika sekta binafsi uliofanyika jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya wadau wakisikiliza kwa umakini juu ya tukio la uzinduzi wa Kampuni ya Ask Indus (T) Limited.Picha na Emmanuel Massaka.

  0 0
 • 03/23/15--20:54: BBC DIRA YA DUNIA

 • 0 0

  Dear Fellow Tanzanians and Friends,

  Tanzania Global Prayer Movement (TGPM) is delighted to present to you Chicago Prayer Summit that will take place in Chicago on April 11th  from 8am to 5pm as part of the Global Day of Prayer. For more information, please visit our website at www.tgpm.organd click on the link about the Prayer Summit. 
  April 11th is the Global Day of Prayer when Tanzanians and Friends worldwide will be praying for our beloved country Tanzania and its beautiful people. Those who live in America or Canada have the privilege to come together in Chicago at the Prayer Summit and cry out to God to intervene, to heal our country Tanzania. The beauty is that Jesus Christ is the healer! 
  This Prayer Summit is not a prayer workshop, a prayer seminar or a prayer conference where you come and sit all day long to learn about prayer. This is a Prayer Summit. Whoever is coming to Chicago for the Prayer Summit should know that he/she is coming to give in prayer, to be on their knees and standing in the gap in prayer for the country we love, Tanzania and its people wherever they are. The prayer will be an 8-hour run from 8am to 4pm and then from 4pm to 5pm for snacks/refreshments/light meal. We will have short breaks between sessions. Everyone coming to Chicago is coming to war, a  spiritual war. It’s an 8 hour run on empty tummies. How about that? You need to come fully prepared with full armor of God (Ephesians 6:10-18) so that you can fight the good fight of faith with diligence and endurance.

  All TGPM members are asked to fast for seven (7) days before the Prayer Summit. So starting from Easter Sunday on April 5th to Saturday April 11th. The Prayer Summit will be the climax of the 7-days fast.

  Please make sure you register for the Prayer Summit to help us as we organize the event.  Register at www.tgpm.org.

  Visit www.tgpm.org for more information about Hotel reservation, and ground transportation for pickups for those coming by air, bus or train.

  Should you have any questions about the Prayer Summit after reading the information online, please contact us atsummit@tgpm.org.

  Your Humble Servant,

  Frank Mwakasisi, Ph.D.
  Founder
  Evangelist, Pastor, Teacher, and Preacher
  Tanzania Global Prayer Movement - "Praying for the Power of the Resurrected Jesus Christ, our Lord to Transform Tanzania and spring forth Personal Renewal and Community Revival."
  Chicago, Illinois
  USA


  0 0

  Leo Jumanne 24.March 2014 ni siku ya kuzaliwa mdau Hamisi Ally Hamisi tunamuombea kila la heri,Afya njema na maisha marefu,Kijana Hamisi Ally Hamisi
  alizaliwa siku kama ya leo 24 March, mtaa wa Mchikichi/Kongo st.18 Kariakoo jijini Dar es salaam,
  akiwa mtoto wa kiume wa aliyekuwa mchezaji kandanda wa timu za Benfrika, Kongo United "Shetani Wekundu" marehem Bw.Ally Hamisi Ally(RIP) aka De Stefano.

  Hongera sana kijana Hamisi Ally Hamisi kwa siku yako ya Kuzaliwa na endeleza kipaji chako cha kandanda

  wadau mnaweza kuungana nae at www.facebook.com/hamisi.ally.7?fref=ts

  0 0

  Mratibu wa mradi wa ruzuku kwa waandishi wa habari wa mfuko wa waandishi wa habari nchini (TMF) Danstan Kamanzi akizungumza jana mjini Dodoma na kikundi cha waandishi wa habari wanaoandika habari za wasiosikika (Sauti ya mnyonge) kwenye mafunzo ya siku tano ya kuandika habari za mitandao ya jamii yanayofanyika Dodoma hotel.
  Miongoni mwa waandishi wa habari 17 wa kikundi cha waandishi wa habari wanaoandika habari za wasiosikika (Sauti ya mnyonge) wakiwa mjini Dodoma kwenye mafunzo ya siku tano ya kujengewa uwezo wa kuandika habari kwa njia ya mitandoa ya kijamii (social media) yaliyoanza jana.
  Mratibu wa mradi wa ruzuku kwa wanaandishi wa habari wa mfuko wa waandishi wa habari nchini (TMF) Danstan Kamanzi (kushoto) akimkabidhi mjini Dodoma, Mwenyekiti wa kikundi cha waandishi wa habari wanaoandika habari za wasiosikika (Sauti ya mnyonge) Ramadhan Msangi moja kati ya kompyuta ndogo (tablet) jana kwa ajili ya kufanya shughuli za kikundi hicho.

  0 0

  DSC_0036
  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akipitia kijarida cha maelezo kazi zinazofanywa na taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15. Kulia ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Doris Mollel wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi hiyo uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

  Na Mwandishi wetu
  NAIBU Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi, Mahmoud Thabit Kombo ameitaka jamii kubadili utamaduni na kumshikirisha mwanamme wakati mke wake akienda kujifungua ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha usalama wa mtoto na mama.

  Alisema wanaume wengi hasa wanawake wao wanapokuwa wajawazito na wanakaribia kujifungua wanakosa amani na wengine hukimbia nyumbani au humkimbiza mke na mtoto wao kwa ndugu na jamaa baada ya kujifungua kutokana na kukosa ushauri unaompa ujasiri kuhusu familia yake hiyo mpya.

  Naibu waziri huyo alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel mwishoni mwa wiki.
  Alisema yeye anaamini kwamba moja ya vitu vinavyoweza kupunguza idadi ya vifo kwa watoto wa njiti ni ushiriki wa wanaume na kuwataka watu wa Doris Mollel Foundation kufanya kampeni kubwa ya kubadili tamaduni na wanaume kukalishwa chini kuelekezwa.
  DSC_0069
  Muuguzi wa wodi ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mariana Makanda akitoa somo na elimu ya makuzi kwa watoto njiti wanaozaliwa nchini kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi hiyo.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Meneje Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Gary Chapman, akizungumza kwenye hafla ya awamu ya pili ya utoaji tuzo za umahiri mwaka 2014 (Excellence Awards 2014), iliyofanyika Jumanne usiku Machi 23, 2014, kwenye mgodi huo ulioko Nyamongo, wilayani Tarime mkoa wa Mara.
  Meneja mkuu wa mgodi wa North Mara, Gary Chapman, (kushoto), akishuhudia wakati Le Poer Trench, (katikati) na Albert Rudman, wakionyesha tuzo za umahiri za mwaka 2014, (Excellence Aawards 2014), walizopokea kwa niaba ya idara ya huduma za kiufundi ya mgodi huo, kwenye hafla ya awamu ya pili ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika kwenye mgodi huo ulioko Nyamongo wilayani Tarime mkoa wa Mara, Jumanne usiku Machi 23, 2015
  Stanley Harding, Meneja wa Liability, mgodi wa North Mara, (kushoto), akimkabidhi tuzo ya umahiri ya mwaka 2014, Adam Charles, kwa niaba ya idara ya operesheni ya mgodi huo, kwenye sherehe za awamu ya pili ya utoaji tuzo hizo (Excellence Awards 2014), zilizofanyika Jumanne usiku Machi 23, 2015, kwenye mgodi huo ulioko Nyamongo, wilayani Tarime mkoa wa Mara. Tuzo hizo utolewa kila mwaka kwa mfanyakazi binafsi au idara, kutokana na umahiri katika kutekeleza majukumu yao kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu.


older | 1 | .... | 779 | 780 | (Page 781) | 782 | 783 | .... | 3272 | newer