Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

Tanzania Ijayo, Ufugaji Wa Kisasa Na Biashara Kubwa Ya Mazao Ya Mifugo Yetu - Profesa Muhongo


The exclusive launch of @AllyRehmtullah 2015 - Eleganza at the Dar es salaam serena hotel last night

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA MH. ZITTO KABWE WAKATI AKITANGAZA KUJIUNGA NA CHAMA CHA ACT-TANZANIA

NEWS ALERT: AFRICAN IN NEW YORK TV SHOW TAKES OFF NEXT FRIDAY

0
0
Deogratius Mhella,The Director and Producer of "African in New York", welcomes you to watch this new show every friday at 4:00 pm from March 27th, 2015 to June 19th, 2015 on the following channels depending on who your service provider is. 
 *Provider Channel: Times Warner Cable (TWC) 67 and 1998 FiOS 36 RCN 85 
 *To stream online: Tune to channel 4 @ www.MNN.org every friday at 4:00 pm.
Every week has a new show to expose the African and African American culture and heritage. 
 We look forward to providing you with great shwows! 
 Thank You and Stay Tuned!

Rais Kikwete akutana na Rais Uhuru Kenyatta mjini Windhoek, Alhaj Mwinyi na Mzee Mkapa waungana naye sherehe za kuapishwa rais mpya wa namibia

0
0
 .Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya jijini Windhoek Namibia ambapo walihudhuria sherehe za kuapishwa Rais mpya wa Namibia.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akikutana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya katika Hoteli ya Safari Court jijini Windhoek Namibia jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi(kulia) na Benjamin William Mkapa(kushoto) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hosea Kutako jijini Windhoek Namibia leo.Viongozi hao walihudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 25 ya Uhuru wa Namibia ambapo pia Rais wa awamu ya tatu  wa Namibia Dkt.Hage Geingob aliapishwa katika uwanja wa Independence jijini Windhoek.Chama cha ukombozi cha Namibia SWAPO kilizaliwa nchini Tanzania na kuendesha harakati za ukombozi mpaka mwaka 1990 ambapo nchi hiyo ilipata uhuru. Picha na Freddy Maro.

BREAKING NEWZZZZ: MAGARI YA KITALII YA TANZANIA RUKSA KUINGIA UWANJA WA JOMO KENYATTA, NA SAFARI ZA KENYA AIRWAYS KUENDELEA KUWA 42

0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu makubaliano ya pamoja yaliyofikiwa kati ya  Serikali za Tanzania na Kenya juu ya kuruhusu tena magari ya kitalii ya Tanzania kuingia Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta na kurudisha idadi ya awali ya safari za ndege za Kenya ambazo ni 42. 
Sehemu ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri Membe
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatlia mazungumzo kati ya Waziri Membe na Waandhishi wa Habari. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Bibi Rosemary Jairo, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Joseph Sokoine,  Bw. Innocent Shiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia na Bi. Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.
Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia mazungumzo ya Waziri Membe na Waandishi wa Habari ambao hawapo pichani. (Picha na Reginald Philip) ================================
JOINT STATEMENT BY FOREIGN MINISTERS OF TANZANIA AND KENYA FOLLOWING THE MEETING BETWEEN HIS EXCELLENCY JAKAYA KIKWETE, PRESIDENT OF TANZANIA AND HIS EXCELLENCY UHURU KENYATTA, PRESIDENT OF KENYA HELD IN WINDHOEK, NAMIBIA ON 21ST MARCH, 2015

His Excellency Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania and His Excellency Uhuru Kenyatta, President of the Republic of Kenya met in Windhoek, Namibia on 21st March, 2015 to discuss bilateral issues.

Both Presidents were in Windhoek to attend the 25th Independence Anniversary and Inauguration of the 3rd President of the Republic of Namibia, His Excellency Dr. Hage G. Geingob. Also in attendance were the Foreign Ministers Bernard K. Membe of Tanzania and Ambassador Amina Mohamed of Kenya as well as Engineer Michael Kamau, Kenya’s Transport and Infrastructure Minister. 

The main issues of the meeting revolved around transport and tourism sectors. In particular, the two Heads of State discussed the decision by the Ministry of Tourism of Kenya to bar Tanzania registered vehicles from accessing the Jomo Kenyatta International Airport. They also discussed the decision by Tanzania Civil Aviation Authority to reduce the frequency of Kenya Airways flights operating between Kenya and Tanzanian Airports.

On the two issues under deliberation, the two leaders agreed on the following actions:

1.  To reinstate the status quo. This means, with immediate effect, Tanzania registered vehicles will access the Jomo Kenyatta International Airport as before, while Kenya Airways will continue with its normal operations.

2.  Within four weeks, Ministers of Foreign Affairs will convene and chair a meeting of the parties including Ministers of Transport, Ministers of Tourism and Chiefs of Staffs in the two Presidencies to discuss and reach a mutual beneficial agreement. The first meeting will be held in Dar es Salaam on a date to be agreed by the conveners.

The meeting was held under a very cordial atmosphere with two Heads of State emphasizing the need to continue discuss openly issues affecting the brotherly and a long-standing bilateral relationship that exists between Tanzania and Kenya.

Done in Windhoek, Namibia on 21st March, 2015.

SHEIKH MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO SHEIKH ABDULKADIR MOHAMED RAMIYA ATOA TAMKO LEO

0
0
Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Sheikh Abdulkadir Mohamed Ramiya akiongea na mwandishi wa Azam TV Bw. Octaviana baada ya kutoa tamko lake (hapo juu) leo mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani

WARNING: Periods of heavy rains are expected to continue in some areas along the coastal sector of the country (Update).


TAHADHARI: Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa kuendelea katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani wa nchi (Mrejeo)

Maji week, Mara region 16th - 22nd March 2015

0
0
The Vice President of Tanzania Dr. Mohammed Gharib Bilal visiting WWF Tanzania pavilion in Mukendo grounds, Musoma on the peak day of Maji week (22nd March) celebrated nationally in Mara region for 2015.
WWF Tanzania's Mwasiti Rashid who coordinates the Freshwater Mara River Basin Management initiative holds high a certificate attained for participating in the Maji week in Musoma, Mara region 16th -22nd March 2015. Theme: Water for sustainable development.

Vita ya ujangili yaungwa mkono,Kikosi cha kupambana na Ujangili chapata zana za kisasa

0
0
Kikosi cha kupambana na ujangili nchini kimepata vitendea kazi kutoka kwa wadau wa sekta ya utalii vitakavyowezesha kukabiliana na matukio ya ujangili yaliyoshika kasi nchini na kuhatarisha kutoweka baadhi ya wanyama.

Miongoni mwa misaada iliyotolewa ni magari matano aina ya Land Cruser yenye thamani ya Sh 750 milioni,bunduki za kivita 50 aina ya Ak 47 na risasi 10,000 na Magazini 20 ambazo thamani haikutajwa kwa kwasababu za kiusalama.

Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu baada ya kukagua vitendea kazi hivyo kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) amesema vitasaidia kuongeza nguvu za kufanya doria na kupambana na ujangili kwenye mapori ya akiba nchini na kudhibiti utoroshwaji wa nyara za serikali.

Nyalandu amekiri kuwapo kwa changamoto ya mwingiliano wa maeneo yaliyohifadhiwa na makazi ya wananchi ambayo inatatuliwa kwa mujibu wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)lengo likiwa kuwa na uhifadhi endelevu ambao unaleta maendeleo endelevu kwa wananchi.

Naye Naibu Mkuu wa Kikosi cha kupambana Ujangili Kanda ya Kaskazini,Michael Msuka amesema vitendea kazi hivyo vitaongeza hari ya watumishi katika kulinda wanyamapori katika mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,Manyara na Tanga.

Alisema vita ya kupambana na ujangili ni kubwa kwani katika kipindi cha mwezi Septemba hadi Disemba mwaka 2014 jumla ya majangili 203 walikamatwa kwenye maeneo mbalimbali nchini na kuwa wamefikishwa mahakamani na baadhi yao kutozwa faini.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akikagua magari matano yaliyotolewa kwaajili ya kupambana na ujangili katika kanda ya Kaskazini kwenye uwanja wa ndege wa Kilimanjaro(KIA) yakiwa na thamani ya Sh 750 milioni.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akijaribu sehemu ya bunduki 50 aina ya AK 47 zilizotolewa kwaajili ya kupambana na ujangili katika kanda ya Kaskazini kwenye uwanja wa ndege wa Kilimanjaro(KIA)

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AMJULIA HALI MZEE ISRAELI ELLY NAWINGA KIJIJINI KWAKE MASAMA LOSAA WILAYANI HAI.

0
0
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipeana mkono na Bwa.Israel Elly Nawinga mapema leo asubuhi katika kijiji cha Masama Losaa,Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro,Pichani kulia ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Hai,Mh Anthony Mtaka.Bwa.Israel aliwahi kuwa Waziri wa Elimu na pia Waziri wa Mambo ya Nje kwa nyakati tofauti enzi za uongozi wa Mwal.Julius Kambarage Nyerere.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wapo mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku tisa ya kukagua,kuhimiza na kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya chama cha CCM ya mwaka 2010 ikiwemo pia kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi
Bwa.Israel Elly Nawinga akiuzungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana mapema leo asubuhi alipopita kumsabahi katika kijiji cha Masama Losaa,Wilaya ya Hai mkoani KilimanjaroBwa.Israel aliwahi kuwa Waziri wa Elimu na pia Waziri wa Mambo ya Nje kwa nyakati tofauti enzi za uongozi wa Mwal.Julius Kambarage Nyerere.

PICHA NA MICHUZI JR-HAI  MKOANI KILIMANJARO

SITA MBARONI KWA KUMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA, KULIMA BHANGI NA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI MKOANI DODOMA

0
0
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu sita (6) kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya kumiliki silaha kinyume cha sheria, kulima na kukutwa na bhangi pamoja na kuingia nchini bila kibali, kufuatia operesheni inayoendelea Mkoani Dodoma kusaka watuwanaojihusisha na uhalifu wa aina mbalimbali.

Akithibitisha matukio hayo kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME - SACP amewataja watu wanaoshikiliwa na Polisi kuwa ni ERASTO DIHELELA mwenye miaka 31, mkulima, mkazi wa kijiji cha Lukole aliyekamatwa na silaha aina ya Gobore isiyokuwa na namba pamoja na Golori zake 11 na vipande 17 vya nondo akilimiliki bila kuwa na kibali. Mtuhumiwa huyo pia alikutwa amelima bhangi kwa kuchanganya na mahindi katika shamba lake la hekari moja.

Mtu wa pili ni HAPPY GIBSON mwenye miaka 28, mkulima, mkazi wa Kijiji cha Lukole akiwa na silaha aina ya Gobole nyumbani kwake bila kuwa na kibali cha kumiliki silaha hiyo. Vile vile katika kupekuliwa nyumbani kwake mtuhumiwa huyu alikutwa na bhangi kilo tano (5) alizohifadhi ndani ya nyumba yake tayari kwa kusafirisha.

Kamanda MISIME amesema katika oparesheni hiyo pia amekamatwa HAMISI MWIKOLA mwenye miaka 28, mkulima, mkazi wa Kijiji cha Lukole akiwa amelima bhangi kwa kuchanganya ndani ya shamba lake la mahindi hekari mbili.

Watuhumiwa hawa wote wamekamatwa siku ya tarehe 21/03/2015 katika kitongoji cha shuleni mlimani kijiji cha Lukole kata ya Kingiti tarafa ya Kibakwe Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma na watafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu kukamilika.

Aidha Kamanda MISIME amesema wamekamatwa raia wawili kutoka Ethiopia katika eneo la Nala Dodoma Mjini wakiwa hawana kibali cha kuingia nchini na kuishi. Watu hao ni GETHGACHEW ANCHISO mwenye miaka 29, na KONJITI FEYSA mwenye miaka 23.

Vilevile huko katika kijiji cha Tubugwe juu kata ya Chamkoloma Tarafa ya Mlali Wilayani Kongwa amekamatwa mtu mmoja anayefahamika kwa jina la MWAJABU SALUM mwenye miaka 28, mkulima, mkazi wa Tubugwe juu akiwa amelima bhangi ndani ya shamba lake la mahindi la hekari mbili na nusu (2 ½).

Kamanda MISIME ametoa wito kwa wakulima kutolima mazao haramu na badala yake walime mazao yenye tija kwa maendeleo halali kwani hatima ya wahalifu wanaolima bhangi na kukutwa na silaha bila kibali ni kuishia jela na kuzitesa familia zao kwa vitendo wanavyofanya vya kihalifu. Aidha amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kuwafichua watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria, kulima na kumiliki au kuuza dawa za kulevya na kujihusisha vitendo vingine vya kihalifu katika maeneo yote ya Mkoa wa Dodoma kwa usalama wa wananchi kwa ujumla na kutokomeza uhalifu wa aina zote.
Bhangi ikiteketezwa baada ya kukamatwa katika shamba la mahindi.
Watuhumiwa waliokuwa wakilima Bhangi hiyo.

ICF na TIC Kuongeza Uwekezaji Nchini

0
0
Taasisi inayoshughulikia mazingira ya Uwekezaji Barani Afrika (ICF-Africa) na Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) leo wamesaini makubaliano ya kusaidia kuvutia na kuongeza uwekezaji wa ndani na nje hapa nchini. Makubaliano hayo yamesainiwa leo na Mwenyekiti Mwenza wa ICF ambaye pia ni Rais mtaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Mkapa na kwa upande wa serikali ya Tanzania yamesainiwa na Waziri wa nchi Uwekezaji na Uwezeshaji Mheshimiwa Christopher Kajoro Chiza.

Katika makubaliano hayo, kiasi cha fedha zipatazo Dola za Kimarekani 950,000 zitatolewa kwa ajili ya Mradi wa Dirisha la Uwekezaji Tanzania (Tanzania Investment Window) ambazo zitachangiwa kwa pamoja kati ya ICF na Serikali ya Tanzania kwa lengo la kurahisisha taratibu na kufanya huduma zote zinazotolewa na Kituo cha Uwekezaji kupatikana haraka, kwa ufanisi, na bila kupoteza muda na gharama kwa wawekezaji. Gharama hizo za Dola za Kimarekani 950,000 zitachangiwa kwa ICF kutoa Dola za Kimarekani 650,000 na Serikali ya Tanzania kupitia Kituo cha Uwekezaji (TIC) itachangia Dola za Kimarekani 300,000.

Chini ya makubaliano haya, ICF itakisaidia Kituo cha Uwekezaji (TIC) kukuza, kuinua na kulitangaza Dirisha la Uwekezaji na kuimarisha uwezo wake katika kuwezesha na kufuatilia uwekezaji nchini Tanzania. Ikumbukwe kwamba mnamo mwaka 2014 TIC ilianzisha huduma ya kimtandao ya Dirisha la Uwekezaji ambapo huduma mbalimbali zinazohusu uwekezaji zinapatikana kwa pamoja. Chini ya utaratibu huu wawekezaji wa ndani na wa nje wanaweza kutuma maombi ya huduma wanazohitaji kabla ya kufanya biashara Tanzania.

Hivyo basi, chini ya Mradi huu ambao Makubaliano yake yamesainiwa leo, Dirisha la Uwekezaji kupitia juhudi za kimawasiliano na kuimarisha uwezo wa utendaji kazi wa Kituo cha Uwekezaji zitafanyika. Mpango huu utasaidia kuzileta huduma zote zinazotolewa na Kituo cha Uwekezaji karibu zaidi na wananchi kupitia dirisha la moja (One Stop Shop) kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali kama vile TRA, Idara ya Uhamiaji, Wizara ya Ardhi, SSRA (Mamlaka ya Hifadhi za Jamii) na BRELA kwa kutumia mfumo wa kielectronikia ili kuleta ufanisi zaidi. Kwa sasa Kituo cha Uwekezaji kinao Maafisa Waandamizi kutoka TRA, Idara ya Uhamiaji, Wizara ya Viwanda na Biashara, BRELA, na Wizara ya Ardhi hivyo kwa kutumia Dirisha hili la Uwekezaji, maafisa hawa wataweza kutoa huduma zilizo bora na za kisasa, bila kuchelewa na kwa ufanisi mkubwa.

Matarajio ya Mradi huu ni kuimarisha mtazamo chanya kwa wawekezaji wa ndani na nje kuwa Tanzania ni sehemu iliyo bora kabisa kuwekeza na hii itasaidia kuongeza uwekezaji mwingi nchini na kutengeneza ajira nyingi zaidi kwa watanzania.

Akizungumza wakati wa kutiwa saini Makubaliano hayo kati ya ICF na TIC, Mwenyekiti mwenza wa ICF Benjamin Mkaapa alisema, “ICF ina furaha kubwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji nchini katika kukuza na kuimarisha huduma wanazohitaji wawekezaji. Biashara zote hususan zilizo ndogo zinahitaji kuwa na mazingira yaliyo mazuri watakayofanyia shughuli zao. Kwa kuwa na Dirisha la Uwekezaji, biashara nyingi zitaweza kukua, kuongezeka na kushamiri kwa haraka. Wafanyabiashara na wawekezaji hawa wataweza pia kuchangia sana katika kuzalisha ajira na hatimaye kuboresha kipato kwa watanzania hapa nchini”

Aidha, kwa upande wa Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Mheshimiwa Christopher Chiza alisema, “Mara Mradi huu wa Dirisha la Uwekezaji Tanzania utakapokamilika, utasaidia kuboresha mazingira ya biashara na ushindani nchini. Kwa muda wa miaka michache iliyopita nafasi ya Tanzania kimataifa katika kufanya biashara kwa mujibu wa ripoti mbalimbali imekuwa hairidhishi, ishara ambayo sio nzuri kwa wawekezaji na sekta binafsi. Kukamilika kwa mpango huu ambao utawezesha usajili mbalimbali wa biashara kufanyika kwa njia ya kielekroniki utafanya taratibu za biashara kuwa rahisi kabisa kwa kuondoa vikwazo na urasimu katika uwekezaji.
Rais mtaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (awamu ya tatu) na Mwenyekiti Mwenza wa ICF,Mh. Benjamin Mkapa akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya kusaidia kuvutia na kuongeza uwekezaji wa ndani na nje ya nchini baina ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) na Taasisi inayoshughulikia mazingira ya Uwekezaji Barani Afrika (ICF-Africa),iliyofanyika leo Machi 23,2015 kwenye ofisi ya TIC jijini Dar es salaam.Kulia ni Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji,Mh. Ing. Christopher Chiza.Picha zote na Othman Michuzi.
Rais mtaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (awamu ya tatu) na Mwenyekiti Mwenza wa ICF,Mh. Benjamin Mkapa (kushoto) na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji,Mh. Ing. Christopher Chiza (wa pili kulia) wakisaini wa makubaliano ya kusaidia kuvutia na kuongeza uwekezaji wa ndani na nje ya nchini,wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Machi 23,2015 kwenye ofisi ukumbi wa Mikutano wa TIC,jijini Dar es Salaam.Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Prof. Lucian Msambichaka (kulia),Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Juliet Kairuki pamoja na Mtendaji Mkuu wa Taasisi inayoshughulikia mazingira ya Uwekezaji Barani Afrika (ICF-Africa),William Asiko.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Juliet Kairuki (kulia) akibadilishana mikataba na Mtendaji Mkuu wa Taasisi inayoshughulikia mazingira ya Uwekezaji Barani Afrika (ICF-Africa),William Asiko mara baada ya kusainiwa.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

MKURUGENZI MKUU WA NHC AFANYA ZIARA MIKOA YA SINGIDA, TABORA NA SHINYANGA

0
0
Jana Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia kyando Mchechu ameanza ziara yake ya kutembelea Mikoa ili kuhimiza utendaji kazi wa viwango na kujionea utekelezaji wa miradi ya nyumba za gharama nafuu katika mikoa atakayotembelea ya Singida, Shinyanga, Tabora, Kigoma, Sumbawanga,Katavi na Mbeya. Picha na Muungano Saguya-Shinyanga
1
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukitembelea jengo la NHC lililoungua mwaka jana mjini Singida ambapo Shirika linajenga upya jengo jingine katika kiwanja hicho kilichoko katikati ya mji huo.
New Picture (2)
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la Unyankumi na kupewa maelezo ya mradi wa nyumba za gharama nafuu na Meneja wa NHC Mkoa wa Singida Bw. Ladislaus Bamanyisa ulipotembelea mradi huo kukagua ujenzi wake.
New Picture (5)
Meneja wa NHC Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo akitoa maelezo ya awali kwa ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu ulipotembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Igunga jana.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

KATIBA INAYOPENDEKEZWA

Article 17

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard K. Membe (Mb.) amezindua albamu mbili za nyimbo za injili zinazokwenda kwa majina ya "Pisha Mbele" na "Ni Ujumbe wa Bwana" za mwimbaji Mercy Nyagwaswa katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza uliopo Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Machi, 2015. 
Askofu Mstaafu na Baba mzazi wa Mercy Askofu Nyagwaswa (wa kwanza kulia) akiwa pamoja na Mchungaji David Mangoti (wa pili kulia) na  Balozi Mstaafu Costa Mahalu wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipokuwa akihutubia wakati wa uzinduzi huo.  
Sehemu ya Wachungaji walioudhuria  uzinduzi wa albamu hiyo.
Waziri Membe akikata utepe kuzindua  Albamu mbili za Bi Mercy Nyagwaswa.
Waziri Membe akimpongeza Bi. Mercy kwa kuandaag Albamu mbili kwa mara moja. 
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Wafanyakazi wa Airtel wadhamini ujenzi wa darasa la shule ya watoto wa mahitaji maalumu Pongwe Tanga

0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imesaidia ujenzi wa darasa kwa ajili ya watoto wenye ulemavu katika shule ya msingi Pongwe iliyopo nje kidogo ya Jiji la Tanga.Darasa hilo limejengwa ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kusaidia maendeleo ya elimu nchini kupitia mpango wa “ Tunakujali” unaohusisha wafanyakazi wake kuchangia katika shughuli za kijamiiMkurugenzi wa Huduma za jamii wa kampuni ya Airtel Bi Adriana Lyamba amefanya ukaguzi wa ujenzi huo na kuahidi kuendelea kusaidia mpango wa elimu kwa makundi yenye mahitaji muhimu hapa nchini.

Bi Lyamba amesema kuwa msaada huo umetokana na mahitaji ya miundombinu kwa jamii ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwenye shule hiyo ambayo kwa Jiji la Tanga ndiyo inatoa elimu kwa watu wenye ulemavu.“sisi Airtel tumeona umuhimu wa wanafunzi wenye ulemavu na tumetambua mahitaji yao ndio maana tumekuja na mpango huu wa ujenzi wa Darasa hapa Pongwe” alisema Bi Lyamba.

“ujenzi wa Darasa hili ni sehemu ya mpango wetu wa kusaidia ukuaji wa elimu hapa nchini kupitia kampeni yetu ya shule yetu na tunaamini utasaidia makundi yote ya jamii” aliongeza Bi Lyamba.Mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo Bw. Mfaume Kamba amesema, msaada huo wa ujenzi wa chumba hicho utasaidia sana kupunguza tatizo la wanafunzi wenye mahitaji maalumu kukosa sehemu ya kujifunzi.

Bw. Mfaume amesema, Jengo hilo ni msaada mkubwa kwa wanafunzi wa awali kwenye shule hiyo ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisomea nje kutokana na kutokuwepo kwa chumba cha kusomea.“msaada huu ni mkombozi kwetu kwani kwa sasa wanafunzi wetu wa awali watakuwa na mahala pazuri kwa kusomea na kuondokana na adha ya kujifunza wakiwa kwenye mazingira ya nje” alisema Bw. Mfaume.

Shule hiyo ya Mchanganyiko ya msingi ya Pongwe bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vyumba vya kutosha vya kujifunzi kwa watu wenye ulemavu na vifaa vyake.
Wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakiongozwa na Mkurugenzi wa Huduma kwa Jamii,Bi. Adriana Lyamba kubeba mabati kwa ajili ya kupaua darasa litakalotumiwa na wanafunzi wenye ulemavu kwenye shule ya msingi pongwe jijini tanga.
Mwalimu Mkuu msaidizi wa Shule ya Msingi Pongwe, Mfaume Kamba akitoa maelezo ya ujenzi wa darasa linalojengwa kwa msaada wa kampuni ya simu ya airtel Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa kampuni hiyo,Bi. Adriana Lyamba.

SERIKALI KILIMANJARO YAPONGEZA JITIHADA ZA WAFANYABIASHARA KUTANGAZA HIFADHI YA MLIMA KILIMANJARO

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akimvisha taji,mfanyabiashara mashuhuri katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro,Vicent Laswai mara baada ya kufanikiwa kufika katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akimkabidhi cheti mfanyabiashara mashuhuri,Vicent Laswai kwa niaba ya hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA ) mara baada ya kufanikiwa kufika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.
RC Gama akikabidhi zawadi za T-shirt kutoka KINAPA kwa mke wa mfanyabiashara ,Laswai ,Bi Marry Laswai wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Cheti kwa mfanyabiashara huyo baada ya kufanikiwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.wengine wanao shuhudia ni Mhifadhi mkuu KINAPA,Erastus Rufungulo,na kulia ni mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Nchi 19 zashiriki Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni nchini

0
0
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akiwahutubia washiriki wa Tamasha la Kimatafa la Lugha na Utamaduni lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute na kufanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jana Jijini Dar es Salaam na kuhusisha washiriki kutoka nchi 19 wakiwa na lengo la kuhamasisha matumizi ya lugha ya kiswahili.
Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz akizungumza na washiriki wa Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni jana katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akipokea zawadi kutoka kwa Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz wakati wa Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni jana katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images