Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

Article 19

$
0
0
Simu yako ni ya Kichina iwapo.......

1. Battery inajaa baada ya dk 3 ....
2. Simu ina Tv,microwave,torch,kikata kucha,mswaki,kiberiti cha sigara
3. Unaweza kuandika Msg kwa tooth pick 

4.Kuna matatizo ya kimaandishi yanayoitambulisha kwa mfano Nokla, Blackderry,Samvang n.k.
5.Ndege ikipita ,simu inaandika 1 missed
call 

6.Ukiwa karibu na lorry likawashwa kitu kinaandika "Charger Connected"
7.Nilazima iwe na Simu card Mbili na bettry mbili

8.Kukiwa hakuna umeme inaandika "insert sim card"
9.Ukipost status facebook ina post 10 nyingine bila wewe kujua

10. Ukipita karibu na mchina huku bluetooth ikiwa on ,simu inaonesha "new hardware found, please enter pairing code!"

Kampuni za simu za mkononi zaongoza kutangaza biashara nchini

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Push Observer, Rubelyn Alcantara akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisini mwa Push Observer, Kinondoni.
Baadhi ya maofisa kutoka makampuni mbali mbali wakielekezwa jinsi kampuni ya Push Observer inavyofanya shughuli zake kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo. 

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa kutoka nchini Norway amtembelea Waziri wa Nishati na Madini

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akimsikiliza Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa kutoka nchini Norway Mhe. Heikki Holmas wakati alipomtembelea ofisini kwake makao makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Tanzania na Norway. Kulia ni Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Ingunn Klepsivik.
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akimsikiliza Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa kutoka nchini Norway, Mhe.Heikki Holmas wakati alipomtembelea ofisini kwake makao makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.

TTCL YAZINDUA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA KARIAKOO

$
0
0
Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe. Jerry Silaa akizungumza wakati wa ufunguzi wa kituo cha huduma kwa wateja eneo la Kariakoo mtaa wa msimbazi na Makamba,jijini Dar es salaam leo.

Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) imezindua kituo cha huduma kwa wateja eneo la Kariakoo mtaa wa msimbazi na Makamba.

Akiongea wakati wa Uzinduzi huo, Mgeni rasmi ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Ilala Mheshimiwa Jerry Silaa amesema ni faraja kuona TTCL mkifanya huduma hizi za maendeleo hapa Dar es Salaam na kwingineko, kwani hii inazidi kuweka hai matumaini ya Watanzania kwamba kampuni yao hii bado ni imara na ipo mstari wa mbele kuchochea maendeleo ya sekta ya mawasiliano, na sekta nyingine za jamii na uchumi kwa ujumla.

Amesisitiza kuwa jambo la msingi zaidi kwa makampuni ya simu, ni kuongeza kasi ya kusambaza huduma hizi hadi vijijini ambako ndiko wanakoishi wananchi walio wengi.

‘Changamoto inayowakabili TTCL kama mhimili wa sekta hii hapa nchini kuongoza njia na wengine wafuate. Ongezeni juhudi, tuna imani kubwa na TTCL kwamba mnaweza, na tayari tunaona mwelekeo wa mafanikio mazuri kwa siku zijazo, ukizingatia kuwa mwezi huu pia TTCL imesaini mkataba na mfuko wa Mawasiliano (UCSAF) wa kufikisha huduma kwa mteja katika vijiji 103 katika maeneo mbalimbali nchini.’

Naye Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa TTCL Bw. Peter Ngota amesema Lengo la kuhamia Mtaa wa Makamba na Msimbazi ni kuwa karibu na wateja wetu, kama wote mnavyojua kauli mbiu yetu ni TTCL HULETA WATU KARIBU, vitendea kazi vimeboreshwa na tunatarajia wateja watapata huduma kwa haraka zaidi.

Aidha amesema, Kutokana na uwezo wa wafanyakazi, wigo wa mtandao na uzoefu wa kutumia mikongo na mikonga ya simu TTCL imekabidhiwa na Serikali ya Tanzania dhamana ya kuendesha, kusimamia na kuendeleza shughuli za Mkongo wa Taifa. Uwepo wa Mkongo wa Taifa uliojengwa na kuunganisha mikoa yote ya Tanzania, umesaidia kuwa na huduma bora zaidi ambapo kwa sasa wananchi tunaweza kupata huduma mbalimbali zikiwemo matibabu kwa njia ya mtandao, elimu kwa njia ya mtandao, biashara kwa njia ya mtandao na Serikali mtandao, Benki – Mtandao, Pesa - mtandao.

OFISI YA KIKUNDI CHA SANAA TARAB YATEKETEA KWA MOTO ZANZIBAR

$
0
0
Katibu wa kikundi cha Utamaduni cha Sanaa Tarab Daudi Shadhil (kulia) akitoa maelezo kwa Mwandishi wa habari Miza Kona kuhusu kuteketea kwa moto ofisi yao hapo Ngome kongwe, kushoto ni Muongozaji msaidizi wa Kikundi hicho Yazid Mawiya.
Vifaa vya muziki pamoja na pesa shilingi milioni 2.5 za Kikundi cha Utamaduni cha Sanaa Tarab vikiwa vimeteketea kwa moto pamoja na ofisi yao iliyopo Ngome Kongwe, Mjini Zanzibar usiku wa kuamkia jana.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

KINANA AFANYA MAZUNGUMZO NA KIONGOZI MZITO WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI, CHINA

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiwa katika mazungumzo na Mjumbe wa Tume ya Uongozi wa Taifa wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Liu Yunshan, kwenye Ofisi za chama hicho mjini Beijing China. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro.

Rais Kikwete amtembelea Mzee Kingunge Ngombale Mwiru Hospitali ya Taifa Muhimbili

$
0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliyepumzishwa katika chumba cha Dharura katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo.Mzee Kingunge alikimbizwa Hospitalini Hapo Baada ya Kujisikia Vibaya.jopo la Madaktari Bingwa linamfanyia uchunguzi Mzee Kingunga ili kubaini ugonjwa unaomsumbua.Aliyesimama Nyuma ya Rais ni mke wa Mzee Kingunge na kushoto ni Mtoto wa Mzee Kingunge Bwana Kinjekitile.(picha na freddy Maro)

Golden Bush FC Veterans VS Wahenga Veterans

$
0
0

Siku ya tarehe 31/03/2013 ambayo ni sikukuu ya pasaka timu yetu ya Golden Bush FC veterans itashuka uwanja wa TP Africa maeneo ya sinza ili kuonyeshana kazi na wazee wenzao Wahenga Veterans. Kutokana na historia ya upinzani wa jadi wa timu hizi mbili na kwa kutambua umuhimu wa mechi hii ya kusherekea sikukuu ya pasaka, uongozi wa timu zote mbili umelazimika kumualika mgeni rasmi ambaye ni mpenzi na mkereketwa wa michezo Afande Thobias Andegenye.

 Andengenye ndiye atakaye kagua timu hizi kabla kipute kuanza mnamo saa kumi na nusu jioni. Ni mechi inayovuta sana hisia za wapenda soka ambao wanatambua upinzani mkubwa kabisa pindi timu hizi zinapokutana. Golden bush ni timu inayoundwa na wachezaji wa zamani kama vile Onesmo Waziri “Ticotico” Athuman Machuppa, Nico Nyagawa, Waziri Mahadhi, Katina Shijja, Abuu Mtiro, Steven Marash, Said Sued, Majuto Komu, Wisdom Ndlovu, Majaliwa Mwaigaga, Yahaya Issa bila kusahau makocha wa timu ambao ni Madaraka Seleman na kocha mchezaji Herry Morris.

 Upande wa wahenga itakuwa na wachezaji maarufu kabisa wa zamani kama vile Mengi Matunda, Macocha Tembele, Baba Dimo, Mcameroun, Julius Mkemia, Deo Masanja “Mboma” Shomari Pengo na wachezaji wengine wengi waliotamba katika ligi ya Tanzania enzi hizo.

Timu zote ziko mafichoni kwasasa zikijufua sawasawa ili kumaliza ubishi wa nani zaidi kati ya vigogo hawa wa soka.

Tunajua uwanja utajaa sana hivyo tunaomba wapenzi wetu wawe watulivu na washangilie kwa utulivu kabisa kama ilivyozoeleka na mwisho wa siku mshindi apatikane katika dakika tisini. Wale watakao kuja na watoto, wanaombwa wawe wangalifu kwasababu uwanja uwa unajaa sana tena sana hivyo unaweza kumpteza mwanao na akawa tabu kumpta.

Golden Bush itaingia uwanjani mnamo saa kumi kamili alasiri na safari hii timu itaongozwa na mwenyekiti wetu Ally Mayay Tembele.

Karibuni sana

Msemaji wa timu na mchezaji mwandamizi.
Onesmo Waziri “Ticotico”

Msaada tutani

$
0
0
Ankal za leo,
Mie mdau wako wa looongi hapa Helsinki, Finland, ilikozaliwa Blogu ya Jamii mwaka 2005, kama sikosei. Tunashukuru bado unaendeleza libeneke kama umeanza jana vile. Hongera sana!

Mie sina kawaida ya kuomba msaada tutani toka enzi hizo, ila leo limenikaba kooni hivyo nikaona niombe msaada wa haraka nipumue. Maana dah! Nomaaaa!

Ni hivi ankal, mwanangu leo ni hepi besdei ya kuzaliwa kwake, nasi tumealika watoto wenzie kibao kusherehekea. Tatizo ni kwamba watoto hao waalikwa, ambao ni wa mataifa mbalimbali, wote wameweza kuimba wimbo wa "Happy Birthday" kwa kutumia lugha zao, lakini mwanangu kashindwa kuimba kwa Kiswahili ambacho anakifahamu vizuri tu.

Yaani hivi tunavyoongea analia sana baada ya mimi na mama yake kushindwa kumpa maneno ya Kiswahili ya wimbo huo. Nimepiga simu kila kona ya dunia, wapi. Nikaona hebu nijaribu wadau wa Blogu ya Jamii niombe msaada tutani.

Wadau nisaidieni wimbo huo kwa Kiswahili unaimbwaje????
Mdau Helsinki

WAZIRI NCHIMBI AWAPASHA WAFANYAKAZI WA WIZARA YAKE MJINI DODOMA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizunguma na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kabla ya kufungua mkutano wa siku mbili wa baraza hilo unaofanyika katika Hoteli ya St. Gasper mjini Dodoma. Wa pili kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Edson Nyinyimbe. Kulia ni Katibu wa Tughe Mkoa wa Dar es Salaam, Gaudensia Kadyango, anayefuata ni Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Hassan Kaumo. Katika kikao hicho Dk Nchimbi aliwataka wafanyakazi waashirikiane ili kuleta mafanikio ndani ya wizara hiyo muhimu katika maendeleo ya nchi.
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya kufungua mkutano wa wafanyakazi wa siku mbili unaofanyika katika Hoteli ya St. Gasper mjini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa tatu kutoka kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na Felix Mwagara.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa afungua mafunzo ya akina mama wajasiriamali wilayani humo

$
0
0
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa, Adolph Mapunda akifungua mafunzo ya akina mama wajasiriamali wilayani Kilwa yaliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Raphael Mwamoto akitoa maelezo ya utangulizi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu.
Mkurugenzi wa kitengo cha Uwezeshaji Wanawake katika Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Tabu Likoko akieleza jambo kwa washiriki wa mafunzo.

ZIFF Last Call for Films 2013

$
0
0

The 16th Zanzibar International Film Festival  is fast approaching and is encouraging all film makers and producers not to miss the opportunity to bring in their movies before the 31st of March for them to be showcased during the festival.

ZIFF which will take place in Stone Town, Zanzibar from the 29th of June to 7th July seeks to provide opportunity for filmmakers to showcase their films to an international audience. The festival’s official competition has four major categories which include Feature and short films, documentaries or short films, East African films and Short or Animation films. Entry fee for any of these categories is free and open to all African countries and the countries of the Indian Ocean Rim and Indian Ocean Islands and the deadline for submission is 31st of March.

The festival has also announced that they will give priority to films that depict the festival's theme - Global Images Meet in Zanzibar, which conveys the idea of merging realities in a global village, cultural encounter, engagement and exchange. Films in any genre - features, documentaries, short films, animation and music videos are welcome.

Zuku also announced that it will sponsor the film festival ZIFF to the tune of TSH 160 million this year. This year's sponsorship cost is part of Zuku 10 years agreement (2012-2022) to sponsor the annual event at a cost of $USD 1,000,000.

The festival aims to showcase African films, and the message from the organizers and sponsors is clear: African institutions must support their own stories in order for them to be told,” said Martin Mhando, adding “We therefore urge filmmakers to utilise this platform.”


This year the category of award will include: Best Short Film, Best Animation, Best Documentary, Best East Africa Film,  Best Features Film, Ousamane Sembene Film for Development  and the ,Verona award. In addition, Zuku sponsorship will also introduce new awards category at the festival. They include Zuku Film Award, Best Actor Award and the Best Actress Award, which will go to new players in the industry.

Ali Muruki, Chairman of Wananchi Group, said “Zuku is proud to once again be part of ZIFF a truly local festival and we continue to work closely with the festival to promote local talent in film and music and to develop the film, entertainment and media industry in East Africa. ZIFF has over the last 15 years been instrumental in growing the film industry in East Africa by providing a platform enabling and celebrating film making from our regions.

He added, “We at Zuku believe that there are several African works and stories that need to be shared to inspire, to entertain and to illuminate the world with the unique cultural offerings of the continent. And I encourage all filmmakers to take advantage of this and bring in their films for the world to learn and be entertained.

For details on what you will need to submit and how you can submit your film visit www.ziff.or.tz

KUMBUKUMBU

$
0
0
MAREHEMU SAMSON AMOS MITULA.

SITAWEZA KUISAHAU KAMWE TAREHE 22.03.2003 SIKU TULIPOKUWA SAFARINI NAWE TOKA DAR ES SALAAM KWENDA SINGIDA NA TULIPOFIKA CHALINZE TULIPATA AJALI MBAYA SANA UKANIACHA SIJITAMBUI.BAADA YA WIKI MBILI NIKIWA NAHOJI SANA KWANINI HAUJI KUNISALIMIA INGAWA PIA SIKUWA NIKIJUA NAUMWA NINI HADI JOPO LA MADAKTARI WALIPONIAMBIA KUWA HAUKO NASI TENA DUNIANI TANGU TAREHE 22.03.2003, KWAMBA TULIPATA AJALI MBAYA SANA CHALINZE NA ULIFARIKI DUNIA PALEPALE HAKIKA ILINIUMA SANA.

SIKU NILIPOPEWA TAARIFA HIZO NDIPO NILIPOJUA KUWA NAMI NINA BANDEJI NYINGI USONI.NI MIAKA KUMI(10) SASA TANGU UTUACHE KAKA YETU MPENDWA,MIMI ERASTO YOHANA SIMA NA FAMILIA YANGU TUNAKUKUMBUKA SANA TUTAZIDI KUYAENZI MEMA MENGI ULIYOTUACHIA.

UNAKUMBUKWA SANA NA MKE WAKO MPENZI MWL FAITH SAMSON KIDASHARI WATOTO WAKO WOTE HASA LILIAN ULIYEMWACHA AKIWA NA UMRI WA MWEZI MMOJA TU,WAZAZI WAKO BW & BIBI AMOS MITULA,FAMILIA YOTE YA MZEE KIDASHARI,DADA ZAKO,KAKA ZAKO,SHEMEJI ZAKO,WADOGO ZAKO,RAFIKI ZAKO WOTE NA WAFANYAKAZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA,HAKIKA TUTAKUKUMBUKA DAIMA KAKA SAM.

BWANA ALITOA NA BWANA AKATWAA JINA LAKE LIBARIKIWE AMEN

ERASTO YOHANA SIMA

MKUU WA WILAYA BARIADI-SIMIYU

Masheha Zanzibar wapewa somo

$
0
0
MRAJIS WA ARDHI ZANZIBAR,MWANAMKAA ABDULRAHMAN AKITOA MAFUNZO KWA MASHEHA WA MAENEO TEULE YA MANISPAA YA MJI WA ZANZIBAR KUHUSIANA NA USAJILI WA ARDHI KWA WANANCHI WANAOMILIKI VIPANDE VYA ARDHI KWA KUJENGA NYUMBA ZAO.WENGINE NI BAADHI YA MASHEHA WAKICHANGIA KATIKA MAFUNZO HAYO.MAFUNZO HAYO YALIFANYIKA UKUMBI WA MALARIA MWANAKWEREKWE ZANZIBAR.

MISS UTALII TANZANIA 2012/13 WATEMBELEA UKUMBI WA KIMATAIFA NA KISASA WA MAKUMBUSHO YA TAIFA

$
0
0

Picha Zote zinaonyesha Washiriki wa Miss Utalii Tanzania wakiwa wanatembelea Ukumbi wa Kimataifa wa Makumbusho ya Taifa(NATIONAL MUSIUM THEATRE).
Washiriki wa Fainali za Taifa za mashindano ya Miss Utalii Tanzania 2012/13,jana wametembelea Ukumbi wa kwanza na wa Kisasa na wa aina yake Tanzania ambao unamilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia kurugenzi ya mambo ya kale na makumbusho ya Taifa uliopo ndani ya Makumbusho ya Taifa jirani na Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM) karibu na maeneo ya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Wakiwa katika Ukumbi huo wenye uwezo wa kuchukua watu 470 kwa wakati mmoja, walishuhudia Viti,Mitambo na vifaa vingine vya kisasa vyenye uwezo wa kuendesha Matamasha na mashindano ya Urembo kwa kiwango cha hadhi ya nyota tano.



MULTICHOICE TANZANIA YAENDELEA KUIBUA MAMILIONEA; ALPHONCE MLEKWA OMARY AIBUKA NA KITITA CHA TShs MILIONI 5,000,000 KUPITIA DStv REWARDS

$
0
0

IMG_9695
Mshindi wa tano wa DStv Rewards, Alphonce Mlekwa Omary (wa pili kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu(kushoto), Meneja Mahusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (wa pili kutoka kulia)  na Meneja Muajiri wa MultiChoice Tanzania, Tike Mwakitwange(kulia), mara ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya Tshs Milioni 5 kuashiria ushindi alioibuka nao.

Wateja wa DStv ambao wanalipia malipo ya mwezi ya akaunti zao kabla ya kukatika wanaendelea kubahatika na kuibuka washindi wa mamilioni ya pesa kila wiki. Hiyo ni kupitia droo maalumu ya DStv ambayo imepewa jina la DStv Rewards.

Mteja ambaye amebahatika kuibuka na kitita cha Tshs Milioni 5 wiki hii na hivyo kuifanya idadi ya washindi kufikia watano ni Bw. Alphonce Mlekwa Omary.
IMG_9808
 Tabasamu la ushindi. Ndivyo inavyoonekana katika picha kwa mshindi wa 5 wa DStv Rewards akifurahia kitita cha Tshs 5,000,000. Waliomzunguka pembeni ni ndugu zake ambao walimsindikiza na kufurahia pamoja naye ushindi.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara yafanya ziara Mkoani Morogoro

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kushoto) akimsililiza Mwenyekiti wa Kamati  ya  Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara , Mahmoud Mgimwa ( kati kati),ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, ( CCM), bara baada ya kusomewa taarifa na Mkuu huyo wa Mkoa katika ukimbi uliopo kwenye jengo la Ofisi hiyo.
 Baadhi ya Wabunge ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Uchumi,Viawanda na Biashara walipokuwa katika ziara yao ya kutembelea viwanda mbalimbali Mkoani Morogoro.
 wajumbe wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara wakiwa kwenye Kiwanda cha Nguo cha 21 th Century cha Morogoro.
 Meneja Uendeshaji wa Kiwanda cha Nguo cha 21 th Century cha Morogoro , Clement Munisi, ( aliyenyoosha mkono) akitoa maelezo mbele ya baadhi ya wajumbe wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara , ikiongozwa na Mwenyekiti wake ,Mahmoud Mgimwa ( kati kati) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, ( CCM), na ( kulia ) ni Mbunge wa Viti Maalumu CCM wa Mkoa wa Geita, Vicky Kamata  na ( kushoto) ni mwezake wa viti maalumu kutoka Mkoa wa Tanga , Amina Mwidau, walipokitembelea kiwanda hicho juzi mjini.Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii,Morogoro.

Article 2

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Prince Nico Mbarga anakupa 'Sweet Mother'

NMB SASA YATOA MIKOPO YA PIKIPIKI ZA MIGUU MITATU

$
0
0
Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni ya Fair Deal Auto Private Limited pamoja Car & General Ltd zinazosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya TVS King leo zimeingia ubia wa kutoa mikopo ya pikipiki za miguu mitatu aina ya Bajaaj na TVS King kwa bei nafuu zaidi. Pikipiki hizi zitawawezesha wateja wa NMB kupata unafuu wa kujikimu kimaisha wakati huo huo wakiendelea na shughuli mbali mbali za kila siku.

Mkuu wa Kitengo cha wajasiriamali Wadogo Wadogo na wa kati wa NMB, Filbert Mponzi (pili kulia) akimpongeza Meneja Mauzo wa kampuni ya Fair Deal Auto LTD, Anil Dewan baada ya kuzindua mkopo wa pikipiki za miguu mitatu kwa ajili ya wateja wa NMB, wakishuhudia ni Meneja Masoko wa kampuni ya Car and General, Jonathani Masanja (pili kushoto) na Meneja wa NMB tawi la Mbezi, Leonard Ngaya.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa kitengo cha Wajasiriamali Wadogo na wa kati, Filbert Mponzi alisema, “Mikopo hii yenye masharti nafuu kabisa, inatolewa kwa mteja yeyote ambaye atatitimiza vigezo vilivyowekwa ili kupata mkopo huu. Mteja mwenye nia ya kupata mkopo huu atatakiwa kuwa na uwezo wa kulipia asilimia thelathini (30%) ya gharama au bei ya Bajaaj au TV’S kama inavyouzwa na wasambazaji wa pikipiki hizi nchini yaani kampuni ya Fair Deal Auto Private Ltd inayosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya Bajaj kwa sasa inauzwa kwa Sh. 5,450,000/= na kampuni ya Car & General Limited Ltd inayosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya TVS King Ltd inauzwa Sh. 5, 600,000/=”.

Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali Wadogo Wadogo na wa Kati NMB, Filbert Mponzi (kati) Meneja Mauzo wa kampuni ya Fair Deal Auto LTD, Anil Dewan (Kulia) na Meneja Masoko wa kampuni ya Car and General, Jonathani Masanja wakifurahia kuzinduliwa mkopo wa pikipiki za miguu mitatu kwa wateja wa NMB.

Mikopo hii ya Bajaj na TVS King kwa sasa inatolewa katika matawi tisa tu ya NMB yaliyopo jijini Dar es Salaam ambayo ni NMB Temeke, NMB Tegeta, NMB Ilala, NMB Airport, NMB Mlimani City, NMB Mwenge, NMB Mbezi, NMB Magomeni na NMB Msasani. Katika siku za usoni NMB ina mikakati ya kutoa huduma hii katika mikoa mingine ili kuwafikia wateja wengi zaidi.

Mkuu wa Kitengo cha wajasiriamali Wadogo Wadogo na wa kati wa NMB, Filbert Mponzi (pili kulia) akimpongeza Meneja Masoko wa kampuni ya Car and General, Jonathani Masanja (pili kushoto) baada ya kuzindua mkopo wa pikipiki za miguu mitatu kwa ajili ya wateja wa NMB, wakishuhudia ni Meneja Mauzo wa kampuni ya Fair Deal Auto LTD, Anil Dewan na Meneja wa NMB tawi la Mbezi, Leonard Ngaya.

Mkopo huu unaotolewa kwa muda wa miezi 24, ambapo kwa kipindi hiki chote, mteja ataendelea kurejesha makato yake ya kila mwezi kwa taratibu na makubaliano yatakayofanyika baina ya mteja na benki ya NMB. Mikopo hii pia inawekewa bima inayomletea unafuu mkopaji endapo atapata matatizo ya kiafya ambayo yatamfanya asiwe na uwezo wa kufanya shughuli zake za kila siku za kimaisha au kufariki, basi bima hii itachukua jukumu la kumalizia deni la mkopo huu na mteja ataendelea kumiliki pikipiki hii ya miguu mitatu kama kawaida.

Sasa, wateja wa NMB wanaweza kutimiza ndoto zao za kumiliki Bajaj au TVS King kwa kutumia mikopo hii. Benki ya NMB inatoa wito kwa wateja wake kutumia fursa ya kupata mikopo hii kwa unafuu zaidi na kupata fursa ya kumiliki pikipiki hizi za miguu mitatu ili kujikwamua kiuchumi.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images