Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 777 | 778 | (Page 779) | 780 | 781 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Mpya wa Namibia Dkt.Hage Geingob wakati wa sherehe za kuapishwa kwake zilizofanyika katika Uwanja wa michezo wa Uhuru wa Namibia jijini Windhoek leo.Sherehe za kumuapisha Rais huyo wa tatu wa Namibia ziligongana na maadhimisho ya miaka 25 ya uhuru wa nchi hiyo.(picha na Freddy Maro)


  0 0

  Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Monduli,Amani Ole Torongei,akizungumza jambo mbele ya umati wa watu waliofika katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo huku akionesha fulana ya CHADEMA akieleza kuwa amechoka kuwa mtumwa.Amani alitangaza kukihama chama chake na kutangaza rasmi kuhamia chama cha CCM,ambapo pia alikabidhi kadi yake ya awali kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na kukabidhiwa kadi mpya ya chama hicho cha CCM.
  Aliyekuwa Mwenyekiti wa wilaya ya Ngorongoro kupitia chama cha CHADEMA,Revocatus Mpalampala,akizungumza jambo mbele ya umati wa watu waliofika katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo.Revocatusi alitangaza kukihama chama chake na kutangaza rasmi kuhamia chama cha CCM,ambapo pia alikabidhi kadi yake ya awali kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na kukabidhiwa kadi mpya ya chama hicho cha CCM.
  Aliyekuwa Katibu Mwenezi Kata ya Olorien,mkoani Arusha kupitiaa chama cha CHADEMA,Prosper Mfinanga akivua sare za chama chake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo,akiashiria kukihama chama hicho na kuhamia chama cha CCM,ambapo pia alikabidhi kadi yake ya awali kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na kukabidhiwa kadi mpya ya chama hivyo.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa mji wa Arusha na vitongoji vyake katka mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.Ndugu Kinana akiwa emeambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na wajumbe wengine leo wanahitimisha ziara ya siku nane mkoani humo ya Kuhimiza,kukagua na kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwemo sambamba na kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.

  Ndugu Kinana katika ziara yake ndani ya mkoa wa Arusha ametembea umbali wa kilometa 2671,Wilaya zote sita za mkoa huo yakiwemo na majimbo saba ya uchaguzi.Amefanya mikutano 69,mikutano nane ya ndani na mikutano 61 ya nje kwa kuzungumza na Wanachi kuyasikiliza matatizo yao na kuyatafutia ufumbuzi.Kama vile haitoshi Ndugu Kinana ametembelea miradi 49,miradi sita ya CCM katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi na miradi 43 ya serikali.

  Katika taarifu fupi ya Katibu wa NEC Itikadi na  Uenezi kuhusiana na wanachama wapya,ziara hiyo imejiongezea wanachama wapya wapatao 4290,ambapo wanachama 519 kutoka CHADEMA walijiunga na chama hicho cha CCM.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Arusha waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jioni ya leo.
  Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano huo.
  Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano huo,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia jioni ya leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid,wakati wa kuhitImisha ziara yake ya siku nane ndani ya mkoa huo.

  PICHA NA MICHUZI JR-ARUSHA


  0 0

   Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akimkabidhi fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni moja Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa ya Chama cha Albino Tanzania, Mohamed Chanzi kwa ajili kuunga mkono kampeni ya kupinga mauaji ya albino. Kushoto ni Mweka Hazina wa Chama hicho, Abdilah Omari na wa pili kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha la Pasaka, Hudson Kamoga. Mbali na fedha hizo Msama alikabidhi hundi ya sh. milioni moja. (Picha na Francis Dande)
   Msama akikabidhi hundi ya sh. milioni moja kwa Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa ya Chama cha Albino Tanzania, Mohamed Chanzi. Katikati anayeshuhudia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha la Pasaka, Hudson Kamoga. 
   Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msamaakifafanua jambo.
  Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa ya Chama cha Albino Tanzania, Mohamed Chanzi akitoa neno la shukrani. 

  Na Mwandishi Wetu

  KAMPUNI ya Msama Promotions, waandaaji wa Tamasha la Pasaka, kupitia kitengo chake cha maafa, imetoa msaada wa sh. milioni 2 kuunga mkono kampeni ya kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini (albino).

  Akitoa hundi ya fedha hizo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama, alisema anaungana na Rais Jakaya Kikwete katika hatua ya kupinga ukatili na mauaji ya albino.

  Alisema fedha hizo zitatumika kuongeza nguvu ya kuhamasisha juhudi za kupinga vitendo vya kikatili dhidi ya albino, kwani na wao ni binadamu kama walivyo watu wengine.

  “Nawaomba wadau na Watanzania kwa ujumla, wazidi kuunga mkono harakati hizi ili kukomesha mauaji yanayoendelea nchini pamoja na kutoa elimu kwa watu wenye dhana potofu ya kuamini kwamba viungo vya albino vinatajirisha,” alisema.

  Pia Msama aliiomba serikali itenge eneo maalumu lenye ulinzi mkali ili kuwaweka watoto albino, ambao hawana uwezo wa kujilinda dhidi ya vitendo wanavyofanyiwa.

  Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Albino Tanzania (TAS), Mohammed Chanzi, aliishukuru kampuni hiyo kwa kugundua umuhimu wa kulinda watu wenye ualbino nchini.
  “Hatuna pa kukimbilia zaidi ya kumuomba Mungu na wadau mbalimbali kutusaidia, kwani hata sisi tunatamani kuishi kama binaadamu wengine, pia tunaomba taasisi na Watanzania wasikie kilio chetu na kutuunga mkono katika hili,” alisema.

  0 0

  Kamanda Mpinga na kikosi chake cha Usalama Barabarani kweli wana kazi. Ankal kalishuhudia hili wakati akirejea kutoka Dodoma kikazi kurudi Dar es salaam ambapo wakati akisafiri barabara ya Morogoro alikutana na mambo ya kutisha yanayoelekea kuendelea katika barabara zetu na kupelekea ajali za kila siku. 
   Kwanza Ankal alishuhudia ajali za barabarani takriban tatu hivi katika siku moja tu ya Machi 20, 2015 ambapo alishuhudia lori la semi-trela za gari (zote) za Scania ambapo ya kwanza ilikuwa kukuta lori moja likiwa limeacha njia na kupinduka karubu na kijiji cha Mdaula. 
   Mbele kidogo, huku mvua ikinyesha kwa nguvu, Ankal na wenzie katika gari dogo walilokuwa wakisafiria wakajikuta uso-kwa-uso na mauti, pale lori semi-trela (la Scania) lililokuwa likitokea Dar es salaam likiacha msururu wa magari mengine na kulenga njia ya magari yajayo. 
  Hakika zilikuwa ni sekunde kama 10 hivi za kuogoya wakati lori hilo lililokuwa linataka kupita takriban magari saba, manne kati yake yakiwa ni ma semi-trela kama hilo, likijaribu kupita foleni hiyo kwa kasi. Dereva wa gari alilokuwemo Ankal alipiga honi, kisha akawasha ta azote, lakini bado semi-trela hilo liliendelea kuja. 
  Kiasi cha mita sita mbele yao ndipo dereva wa lori hilo akaweza kusimama, kwa mbinde na kuponea kugogana uso-kwa-uso na gari dogo la kina Ankal. Kamanda Mpinga na kikosi chake wana kazi kweli. Ni dhahiri kwamba dereva wa lori hilo aidha hana utaalamu wa kuendesha gari barabarani, ama alikuwa amelewa. Ukichanganya na mvua kubwa iliyokuwa unanyesha, usalama ulikuwa haupo kabisa barabarani. 
  Nini kifanyike? Swali zuri sana hilo. Sensa ama ukaguzi wa leseni za madereva wote nchi nzima ufanyike haraka iwezekanavyo. Na kama ikigundulika dereva ana leseni bila kupitia mafunzo katika Chuo cha Usafirishaji ama VETA awekwe kando. 
  Kubwa lazima kuanzia sasa hatua zichukuliwe, na zionekane kuchukuliwa, kila inapotokea jambo kama hili ama ajali kabisa. 
  Lori semi-trela likikaribia kugongana uso-kwa-uso na gari dogo alilokuwemo Ankal na wenzie baada ya lori hilo kuingia sehemu ya barabara isiyo yake...na kama si ustadi wa dereva wa kina Ankal, saa hizi hii habari ingekuwa ingine hapa...
  Uso-kwa-uso na lori
  Mbele kidogo kuna lori liloloacha njia bila shaka kwa tukio kama ambalo Ankal alikutana nalo huko nyuma


  0 0

  Watch The exclusive launch of @AllyRehmtullah 2015 - Eleganza LIVE online today 21st March 2015 - 8pm on WWW.AR.CO.TZ

  0 0   Licha ya kusemwa sana kwa muda mrefu juu ya kuhusishwa na chama kipya cha siasa cha ACT-Tanzania dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Ruyagwa Kabwe (pichani juu akisaini kitabu baada ya kupewa kadi) sasa yamekuwa kweli kwa Mbunge huyo baada ya jana  Jumamosi ya Machi 21, kupokelewa rasmi na chama hicho na kukabidhiwa kadi yake yenye namba 007194.

  Hili limetokea  siku moja tu baada ya Zitto kutangaza kuachia ubunge na kuandika barua rasmi ambapo sasa amekuwa mwanachama wa ACT-Tanzania na kuahidi kuendeleza mapambano ndani ya chama hicho.


   ACT-Tanzania: kirefu chake ni Chama cha Alliance for Change and Transparence Makao makuu ya chama hicho yapo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam, Tanzania.


  0 0

   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa  Benki ya NBC, Pius Tibazarwa (wa pili kulia) akishiriki michezo na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo katika warsha ya siku ya moja ya kujengeana uwezo na mshikamano mahali pa kazi iliyoandaliwa na kitengo cha masoko cha benki hiyo na kuwashirikisha wafanyakazi wa vitengo mbalimbali vya NBC.
   Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe akizungumza katika warsha hiyo.
   Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo.
   Baadhi ya wafanyakazi wa NBC walioshiriki warsha hiyo wakifanya mafunzo kwa njia ya michezo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Kivuko cha Mv Sengerema kikikaribia kuwasisili kwenye gati la Busisi wilayani Sengerema kikitoka Kkigongo Mwanza Machi 21, 2015. Kivuko hicho ni moja ya vivuko vitatu vinavyovusha magari na abiria katia ya Kigongo na Busisi mkoani Mwanza.

  0 0

    Baadhi ya mameneja wa matawi ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakijitolea kuosha magari ili kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia watu wenye ulemavu wa ngoz (albino) na kusaidia juhudi za  kupinga ukatili dhidi yao katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja wa NBC Kanda ya Dar es Salaam Rachel Mwalukasa na kulia ni Meneja wa Tawi la Sea Cliff, Mariam Kombo.
   Baadhi ya mameneja wa matawi ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakijitolea kuosha magari ili kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) na kusaidia juhudi za  kupinga ukatili dhidi yao katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja wa NBC Tawi la Muhimbili, Fatma Gulamsood,Meneja wa Tawi la Mnazi Mmoja, Osmund Kinunda  na  Meneja wa Tawi la Sea Cliff, Mariam Kombo.
   Baadhi ya mameneja wa matawi ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakijitolea kuosha magari ili kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) na kusaidia juhudi za  kupinga ukatili dhidi yao katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa NBC Tawi la Muhimbili, Fatma Gulamsood,Meneja wa Tawi la Mnazi Mmoja, Osmund Kinunda  na  Meneja wa Tawi la Kichwele, Frank Mwanga.
   Baadhi ya mameneja wa matawi ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakijitolea kuosha magari ili kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) na kusaidia juhudi za  kupinga ukatili dhidi yao katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa NBC Tawi la Muhimbili, Fatma Gulamsood,Meneja wa Tawi la Sea Cliff, Mariam Kombo na Meneja wa Tawi la Kichwele, Frank Mwanga.
  Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakiosha magari ili kutafuta fedha kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).

  0 0

  Mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha St.Joseph cha jijini Dar es Salaam ,Ibrahim.M.Ibrahim anayesomea fani ya uhandisi wa kusindika vyakula katika kampasi ya Songea leo amekabidhiwa kitita cha shilingi milioni 10/-alizojishindia kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania katika hafla iliyofanyika katika tawi la NMB benki house Jijini Dar es Salaam. 
  Ibrahim Ibrahim alikabidhiwa fedha zake na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu pamoja na Meneja Uhusiano wa NMB Bw. Vicent Mnyanyika mbele ya waandishi wa habari. 
  Akiongea muda mfupi baada ya kupokea fedha zake za ushindi Ibrahim alisema kuwa siku ya leo itabaki kwenye kumbumbukumbu za historia kwa kuwa ndoto yake ya kusoma shahada ya pili muda mfupi baada ya kuhitimu masomo ya shahada ya kwanza imetimia .“Vodacom kupitia promosheni hii wamefanya ndoto yangu ya kuwa mhandisi msomi kutimia kwa kutumia shilingi mia tatu tu na kuandika neno JAY kwenda namba 15544”.Alisema Ibrahim kwa furaha. 
   "Promosheni ya Jaymillions imelenga kuwakomboa kimaisha watanzania hususani wenye kipato cha chini na washindi wengi waliopatikana hadi sasa wametoka kwenye makundi ya watu katika jamii wanaohitaji kuwezeshwa kimaisha ili wajikwamue na kuinua hali zao kama vile wajasiriamali wadogo wadogo , wamachinga, mama ntilie,wanafunzi na wazee wastaafu. 
   Promosheni ya Jaymillions iliyoanza katikati ya mwezi Januari ambayo itadumu kwa muda wa siku 100 imeleta faraja na itaendelea kuleta faraja na mafanikio kwa wateja wa Vodacom kwa kuweza kujinasua katika hali duni ya maisha na maisha kuwa murua na hadi kufikia sasa ameishapatikana mshindi mmoja wa milioni 100/-,Washindi wanne wa Milioni 10 na washindi 38 wa Milioni 1/- Mshindi wa milioni 100/- ni Uwezo Madengenya kutoka Wilayani Kilolo mkoani Iringa. Washindi wa milioni 10/- ni – Hyness Petro Kanumba kutoka Rukwa , James Mangu (Mwanza),Zuena Rajabu (22) anayefanya kazi ya ususi mkazi wa Tabata Segerea na Deborah Stanley (23) ambaye naye pia ni msusi na mkazi Kimara kwa Komba jijini Dar es Salaam. Meneja Uhisiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu, akiongea katika hafla hiyo alimpongeza mshindi huyo na kusema kwamba fedha hizo zimeenda kwa mshindi sahihi kwani mshindi huyo ana malengo mazuri ya matumizi ya fedha zake kwa kujiendeleza kielimu. 
   Pia aliwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni ya Jaymillions ili wajishindie mamilioni ya fedha kwa kuhakikisha wanatuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza bahati zao za kushinda.
  Aliitaja njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-tu. Kwa upande wake Meneja wa Uhusiano wa benki ya NMB, Vicent Mnyanyika alimpongeza mshindi na kumshauri kuweka akiba ya fedha hizo benki ili kuhakikisha zinakuwa salama hadi utakapofikia muda wa kutaka kuzitumia kutimiza ndoto yake pia alimwakikishia mshindi huyo kuwa benki yao ipo tayari kwa kumpatia mafunzo yaliyo bora ya jinsi ya kuwekeza ili fedha zake ziweze kuongezeka zaidi ya hizo alizojishindia.
  Pia aliipongeza Vodacom kwa kubuni promosheni za aina hii zenye mwelekeo chanya wa kuinua maisha ya wateja wake na wananchi kwa ujumla.
   Meneja wa NMB tawi la Benki House jijini Dar es Salaam, Leon Ngowi(kushoto) akipanga kitita cha shilingi Milioni 10/- wakati wa hafla ya kumkabidhi kitita hicho Mwanafunzi wa chuo Kikuu cha ST. Joseph, Ibrahim M. Ibrahim(kulia) aliyejishindia kupitia Promosheni ya JayMillions  inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,katikati ni  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu. Hafla hiyo ilifanyika  jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
   Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akimkabidhi kitita cha shilingi Milioni 10/- Mwanafunzi wa chuo Kikuu cha ST. Joseph, Ibrahim M. Ibrahim(kulia) aliyejishindia kupitia Promosheni ya JayMillions  inayoendeshwa na kampuni hiyo.Katikati ni  Meneja Uhusiano wa NMB Vicent Mnyanyika. Hafla hiyo ilifanyika tawi la NMB House  jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki,Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
    Mshindi wa kitita cha shilingi  Milioni 10/- kupitia Promosheni ya JayMillions  inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Ibrahim M. Ibrahim ambaye ni Mwanafunzi wa chuo Kikuu cha ST. Joseph tawi la Songea(kulia)akiowaonesha kitita chake waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa hafla ya kukabidhiwa kitita hicho na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu(kushoto)Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, anayeshuhudia katikati ni Meneja Uhusiano wa Benki ya NMB Vicent Mnyanyika.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
   Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu(kushoto)akisisitiza jambo kwa waandshindi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla ya kumkabidhi cha shilingi Milioni 10/- Mwanafunzi wa chuo Kikuu cha ST. Joseph, Ibrahim M. Ibrahim(katikati)aliyejishindia kupitia Promosheni ya JayMillions  inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,kushoto ni  Meneja Uhusiano wa Benki ya NMB,Vicent Mnyanyika. Hafla hiyo ilifanyika  katika tawi la NMB benki house jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki,Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
   Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud”Jay Millions”(kushoto) akimpongeza kwa ushindi wa shilingi Milioni 10/- Mwanafunzi wa chuo Kikuu cha ST. Joseph, Ibrahim M. Ibrahim(kulia)alizojishindia kupitia promosheni hiyo na kukabidhiwa rasmi na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Matina Nkurlu(hayupo pichani)wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika tawi la NMB benki house jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

  0 0

  Kikosi cha Simba kimetoka kidedea kwa bao 5-4 kwenye match ya watani wa jadi Yanga katika mechi ya Nani Mtani Jembe huko Dubai.
  Mpambano huo uliokuwa mkali sana ulianza kwa Yanga kupata penalty 2 kwa mpigi lakini moja iliokolewa na goal keeper na nahodha wa Simba Ali Yusuf. 
  Magoli ya Simba yalifungwa na Matama Chesama (DJ Tama) 3, Tariq Mbarak 1,na Thani 1.magoli ya Yanga yalifungwa Yunus 2, Waleed 1, na Kulwa 1.Yanga imeendelea kuwa mteja wa Simba Sports club hadi huko Dubai.
  Kikosi cha Yanga Dubai
  Kikosi cha Simba Dubai
  Vikosi vya Yanga na Simba katika picha ya pamoja kabla ya gemu

  0 0

  Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe akinzungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutambulishwa kwake kujiunga na Chama cha ACT-Tanzania, katika mkutano wake na wanahabari uliofanyika mapema leo kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tawi la Tegeta wa Chama cha ACT-Tanzania, Mhe Lugano Mwaikenda.Picha zote na Othman Michuzi.
  Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe akionyesha kadi ya Chama chake kipya yenye namba 007184 mbele ya waandishi wa habari waliofika kwenye mkutano wa Chama cha ACT-Tanzania,uliofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena,jijini Dar es salaam leo.  Kluia kwake ni Mwenyekiti wa Tawi la Tegeta wa Chama cha ACT-Tanzania, Mhe. Lugano Mwaikenda
  Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe  na Msanii Afande Sele wakionesha kadi zao za wanachama wa ACT-Tanzania.Wengine ni Dickson Ng'ili pamoja na Adam Shanzy.
  Mwenyekiti wa Tawi la Tegeta wa Chama cha ACT-Tanzania, Mhe Lugano Mwaikenda akionesha vipeperushi vya chama chao wakati wa mkutano huo
   Sehemu ya Wanachama wa Chama ACT-Tanzania wakionyesha mabango ya kumkaribisha Mwanachama mwenzao Mhe. Zitto Kabwe.


  0 0

   Bingwa wa zamani wa dunia wa uzito wa juu, Francois Botha na rais wa chama cha ngumi cha dunia cha WBF, Howard Goldberg wanatarajiwa kuwasili nchini kesho Machi 23, tayari kwa  kusimamia pambano la Mohamed Matumla Jr na Wang Xiu Hua wa China. 

  Botha atawasili nchi kwa mara ya pili kwa mualiko maalumu wa Kampuni ya Hall Of Fame inayoandaa mapambano ya ngumi ndani na nje ya nchi. Nguli huyo wa masumbwi anatarajiwa kuwasili saa 12 jioni na ndege ya Shirika la ndege la Afrika Kusini sambamba na Goldberg wakiwa na mkanda wa dunia wa WBF wa uzani wa Super Bantam utakaowania na Matumla Jr na Hua Ijumaa hii kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee. 

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Hall of Fame, Jay Msangi alisema kuwa, baada ya kuwasili, Botha atashiriki katika programu mbalimbali za pambano hilo ambalo kama Matumla Jr akionyesha kiwango atakata tiketi ya kuzichapa pambano la Utangulizi kwenye lile la dunia kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao la Mei 2 jijini Las Vegas,Marekani.   Wakati huohuo, mpinzani wa Matumla anatarajiwa kuwasili saa saba mchana wa kesho akitokea China tayari kwa pambano lao la Ijumaa. Hua atawasili jijini akiwa ameambatana na kocha wake sambamba na viongozi wengine wa ngumi wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa Msangi, baada ya kuwasili bondia huyo ataendelea na mazoezi kabla ya kushiriki zoezi la kupima uzito na afya litakalofanyika Alhamisi hii. 

  Katika hatua nyingine, mabondia Ashraf Suleiman, Mada Maugo, Karama Nyilawila, Japhet Kaseba na Thomas Mashali wako katika maandalizi ya mwisho kuelekea kwenye mapambano yao ya Ijumaa. Mabondia hao watapanda ulingoni kuzichapa kabla ya Matumla Jr na Hua kupanda kuwania ubingwa wa dunia. 

  Mashali atazichapa na Nyilawila pambano lisilo la ubingwa la uzani wa super bantam wakati Maugo akizichapa na Kaseba kwenye uzani wa super heavy na Suleiman akionyeshana ubabe na bondia kutoka Marekani pambano la uzani wa juu siku hiyo. Kwa nyakati tofauti, mabondia hao kila mmoja alijinadi kumkung'uta mwenzake siku hiyo.

  0 0
 • 03/22/15--08:03: LEXUS RX 300 LINAUZWA
 • AINA YA GARI

  LEXUS RX 300

  BEI YA KUUZA

  Milioni 20 Tsh.

  MWAKA WA KUTENGENEZWA

  2004

  RANGI YA GARI

  PALE SUMMER BLUE METALLIC/

  KILOMETA ILIZOKWENDA

  160,234

  UWEZO/UKUBWA WA INJINI

  2.4-liters, V6

  MENGINEYO

  Gari lipo kwenye hali nzuri na kama, linavyoonekana kwenye picha

  MAWASILIANO

  Mnunuzi, nipigie kwenye namba +255 785 734 519
  0 0

  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza na mmoja wa wanufaika wa mkopo kwa akina mama na vijana uliotolewa kwenye Kata zote za Manispaa hiyo, Victoria Mboweto alipotembelea mradi wake wa duka la nguo, Kigogo Mbuyumi, Dar es Salaam juzi. Manispaa hiyo imetenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya kukopesha vikundi vya akina mama na vijana katika Kata zake.
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza na mmoja wa wanufaika wa mkopo kwa akina mama na vijana uliotolewa na Manispaa hiyo kwa Kata zote, Semeni Mahita ambaye ana mradi wa kuuza vitafunwa na mbogamboga sokoni alipotembelea mradi wake Kigogo Mbuyumi, Dar es Salaam juzi. Manispaa hiyo imetenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya kukopesha vikundi vya akina mama na vijana katika Kata zake. Wapili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana wa Manispaa hiyo, Mwajuma Magwiza.
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza na mmoja wa wanufaika wa mkopo kwa akina mama na vijana uliotolewa na Manispaa hiyo kwa Kata zote, Semeni Mahita ambaye ana mradi wa kuuza vitafunwa na mbogamboga sokoni alipotembelea mradi wake Kigogo Mbuyumi, Dar es Salaam juzi. Manispaa hiyo imetenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya kukopesha vikundi vya akina mama na vijana katika Kata zake. Kushoto ni mmoja wa wateja wa mwanamama huyo.
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kushoto) akikagua mradi wa kuchakata vikoi na mashuka wa mmoja wa wanufaika wa fedha za mkopo za akinamama na vijana wa Manispaa hiyo, Thresia Mazwazwa (kulia kwake) alipotembelea mradi wake, Sinza, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Manispaa hiyo imetenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya kukopesha vikundi vya akina mama na vijana katika Kata zake.


  0 0

  Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiwasalimia mamia ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu mkoa wa Dodoma, waendesha boda boda na wamachinga wa mkoa huo walioandamana hii leo hadi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma kumuomba pindi wakati ukifika kwa mujibu wa taratibu za chama cha Mapinduzi (CCM) asisite kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais. 

  Lowassa amesema anazidi kuhamasika kufuatia maombi ya watu wa makundi mbalimbali ya jamii wanao muomba kugombea urais mwaka huu.Aidha na yeye amewaomba vijana hao na makundi mengine kuwahimiza wenzao vyuoni na hata mitaani kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili siku ya uchaguzi wawe na sifa za kuweza kushiriki katika uchaguzi kwa kupiga kura.
   Wanafunzi hao zaidi ya 300 walifika nyumbani kwake hapo majira ya saa sita mchana na kuzungumza nae na kufikisha salamu zao ikiwa ni pamoja na kumchangia fedha za kuchukulia fomu.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

   Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akimtambulisha Mansour Yussuf Himid kwa wanachama wa Kiembesamaki na kuwaomba wamuunge Mkono leo Unguja
   Aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki (CCM) Mansour Yussuf Himid, akizungumza katika mkutano wa hadhara wa CUF uliofanyika jimboni humo.
   Wafuasi na wapenzi wa CUF wakifuatilia mkutano huo wa kumtambulisha Mansour.
  Wafuasi na wapenzi wa CUF wakifuatilia mkutano huo wa kumtambulisha Mansour.

  0 0


  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zanzibar, Mhe Salim Mwalim, akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Sengerema mjini humo mkoani Mwanza 
   Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zanzibar, Mhe. Salim Mwalim,
   Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zanzibar, Mhe. Salim Mwalim, akisisitiza jambo
  Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zanzibar, Salim Mwalim (kushoto) akimsikiliza kada wa Chadema Wilaya ya Sengerema, Hamis Tabasamu (kulia) akieleza nia yake ya kugombea Ubunge Jimbo la Sengerema katika Uchaguzi Mkuu 2015

  0 0

  Hussein Makame-MAELEZO, Musoma 
   MAKAMU wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohgamed Ghalib Bilal amesema kuwa kila ahadi ya Serikali iliyotolewa itatimizwa ili kuhakikisha kuwa inaacha kazi nyepesi kwa viongozi watakaokuja katika kuendeleza maendeleo ya Tanzania. 
   Dkt. Bilal aliyasema hayo kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Mara yakiwa na Kaulimbiu isemayo “Maji kwa Mandeleo Endelevu. 
   Katika kilele cha Maadhimisho hayo, Dkt. Bilal aliweka jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Ujenzi wa Uboreshaji wa Hudumu ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma ambao utagharimu Shilingi Bilioni 44 hadi kukamilika kwake. “Tumewaahidi kupata maji na hilo tutatekeleza.Kila ahadi ya Serikali itatimizwa swali ni muda na wakati lakini kwa kweli hatukusudii kuwaacha njiani, mambo tuliyosema tutayafanya ili tuwaachie watakaokuja kazi nyepesi ya kuendeleza maendeleo ya nchi yetu” alisema Dkt. Bilal. 
  Mradi huo mkubwa wa maji unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili, 2015 ambapo Dkt. Bilal alisema mradi huo utakapokamilika itaipatia Manispaa ya Musoma maji ya uhakika kwa asilimia 100. 
   Aliongeza kuwa mafanikio ya mradi huo pia ni kuongezeka kwa uzalishaji wa maji kutoka mita za ujazo 10,000 za sasa kwa siku, hadi mita za ujazo 36,000 kwa siku. Dkt. Bilal alitoa rai kwa wananchi wa Manispaa ya Musoma na mkoa wa Mara kutunza mradi huo na miradi yote inayoendelea kutekelezwa ili iendelee kuwasaidia wananchi na vizazi vijavyo. 
   “Na juu ya haya yote, ni msisitizo katika utunzaji endelevu wa mazingira yetu ili yaendelee kutuhifadhi. Aidha, teknolojia za uvunaji wa maji ya mvua na ujenzi wa mabwawa ni maeneo ambayo yatatuhakikishia kwamba tunakuwa na huduma endelevu ya rasilimali ya maji” alisema. 
   Alisema Tanzania haina budi kuwa na mikakati ya makusudi kukabiliana na changamoto hizo, jambo ambalo Serikali imeanza kulifanyia kazi. Alifafanua kuwa uhaba wa maji na kutopatikana kwake kwa uhakika kunaleta athari mbaya katika shughuli zote za kiuchumi. 
   “Majanga yanayohusiana na maji kama vile, mafuriko na ukame kwa kiwango kikubwa ni maafa yanayojitokeza mara nyingi katika sehemu mbalimbali duniani hivi sasa” alisema Dkt. Bilal na kupongeza kuwa: 
   “Vifo, uharibifu wa mali, makazi na miundombinu vina athari kubwa kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja, kikundi, jamii na hata Taifa” Hivyo, alitoa wito kwa wadau wote kuunganisha nguvu pamoja katika kukabiliana na athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa kwani, mabadiliko hayo yana athari kuanzia kwenye kupungua kwa misitu na vyanzo vya maji. 
   Alitaja athari nyingine kuwa ni kupungua kwa rasilimali za maji juu na chini ya ardhi; kuathirika kwa ubora wa maji ya kunywa; hadi kukua kwa utoaji wa gesi ya ukaa. 
   Hata hivyo alisema, Serikali ya Tanzania itaendeleza juhudi za kuhakikisha inawafikishia wananchi maji safi na salama katika maeneo ya nchi ambayo yamekosa huduma hiyo. 
   Aliwakumbusha wananchi kuwa wana jukumu kubwa la kutunza vyanzo vya maji popote pale vinapopatikana na kwamba wana kubwa kwenu wananchi ni kutoa mchango unaostahili katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji. 
   Akimkaribisha Dkt. Bilal, Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe alisema wizara yake itajitahidi na kufanya kila linalowezekana ili katika kipindi kisichozidi miezi mitatu maji yatoke mjini Musoma na wananchi wafurahie huduma hiyo. 
   Alisema katika kipindi cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji, viongozi mbalimbali walishiriki katika kukagua miradi ya maji na kutembelea wilaya zote za Mara na kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maji ambayo imekamilika. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma, (MUWASA) Mhandisi Said Gantala alisema mradi huo unajengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD). 
  Alisema mradi huo unajumuisha ujenzi wa chanzo kipya cha maji, chujio, mtambo wa kisasa wa kutibu maji na ujenzi wa matenki mapya mawili yenye mita za ujazo 5,500. 
  Aliongeza pia kuwa, ujenzi huo utajumuisha ujenzi wa mfumo mpya wa mabomba ya usambazaji maji na ujezni wa miundombinu mingine. 
  “Mheshimiwa mgeni Rasmi Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lake la AFD kwa kushirikiana na Benki ya Uwekezaji ya Jumuiya ya Ulaya (EAD) wamekubali kufadhili mradi wa kuondoa majitaka katika manispaa ya Musoma” alisema Mhandisi Gantala. 
  Naye Balozi wa Ufaransa nchini Melika Berak alisema kuwa amefurahishwa na ushirikiano anaoupata kutoka Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha wanapunguza tatizo la maji nchini. 
  Katika kilele cha maadhimisho hayo ya 27 ya Wiki ya Maji Duniani, washiriki wa maonesho katika maadhimisho hayo walipewa vyeti vya kushiriki na zawadi za vikombe kutokana na makundi washiriki.
   Makamu wa Rais, Dkt. Bilal akiweka jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Uboreshaji wa Hudumu ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma.Kushoto ni Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe  na katikati ni Balozi wa Ufaransa nchini Melika Berak.

   Mkurugenzi wa Idara ya Ubora wa Maji, Nadhifa Kemikimba akimuonesha Makamu wa Rais, Dkt. Bilal teknolojia ya kusafisha maji kwa kutumia mifupa.

   Baadhi ya washiriki wa maonesho ya Wiki ya Maji Kitaifa.

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mbogo Futakamba akizungumza na wananchi juu ya maadhimisho.

  Makamu wa Rais, Dkt. Bilal akimpa kikombe Mkuu wa Idara ya Rasilimali za Maji na Uhandisi wa Umwagiliaji wa Chuo cha Maji, Eng. Pantaleo Tumbo ikiwa ni moja ya zawadi zilizotolewa kwa washiriki wa maonesho ya maadhimisho ya wiki ya Maji.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 777 | 778 | (Page 779) | 780 | 781 | .... | 3286 | newer