Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109594 articles
Browse latest View live

Home shopping centre yakabidhi shule mpya ya msingi mabwepande

0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua shule mpya ya msingi ya Mabwepande jijini Dar es salaam leo iliyojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya Home Shopping Cenrre
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni kabla ya kuzindua shule mpya ya msingi ya Mabwepande jijini Dar es salaam leo iliyojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya Home Shopping Cenrre
 Rais Kikwete akimsikiliza Mkurugenzi wa Home Shopping Centre wakati akikabidhi shule hiyo
Rais Kikwete akimshukuru Mkurugenzi wa Home Shopping Centre kwa kujenga shule ya msingi Mabwepande yenye majengo na samani za kisasa. Picha na Raqey Mohamed

NYUMBANI LOUNGE 2nd Anniversary

ngoma azipendazo ankal

0
0
Wakaja London beat na ngoma yao "I've been thinking about you" na kutamba sana

Ajali asubuhi hii karibu na Exective Pub, Mbezi Chini, Dar

0
0
  Wasamaria wema wakijitahidi kumtoa Jamaa nje ya gari baada ya kupata ajali ya kupindukia mtaroni miguu juu sehemu za Mbezi chini karibu na Executive Pub jijini Dar es salaam asubuhi hii. Haikuweza kujulikana mara moja chanzo cha ajali hii

Traffic akikomaa na dereva asimame asubuhi hii Dar

0
0
Askari wa Usalama Barabarani akipambana na dereva asiyetaka kutii amri halali ya kusimama asubuhi hii katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es salaam...

JARIDA LA KATUNI LA NATHAN ‘NATHAN CARTOONS MAGAZINE’ KUWA HEWANI KILA ALHAMISI

0
0

Jarida la katuni linaloandaliwa na mchoraji katuni, Nathan Mpangala, limeanza kurushwa leo, Alhamisi, likiwa na sura mpya kwa kusheheni katuni kibao ili kukidhi haja ya wapenzi wa katuni wa ndani na nje ya nchi.

Jarida hilo ambalo litakuwa likipatikanakwenye link; www.nathanmpangala.blogspot.com, linatambulikwa kwa jina la ‘Jarida la Katuni la Nathan’ au kwa kidhungu; ‘Nathan Cartoons Magazine’ linalenga kuongeza wigo wa matumizi ya katuni nchini kwani kwa miaka mingi, katuni zimekuwa zikitumika zaidi kwenye zaidi kuliko njia zingine.

Jarida hilo litakuwa likipambwa na katuni za kisiasa, uchumi, michezo na karakta maarufu zilizokuwa zikitoka magazetini siku za nyuma kama; Kijasti, Mzungu Mtaani, Daladala Laivu nk. Pia litakuwa na katuni mahsusi kwa ajili ya anga za kimataifa.

Mbali na katuni pia litakuwa na habari mbalimbali za mashindano ya katuni yanayoendelea ulimwenguni ili kuwawezesha wachoraji wa Kitanzania kushiriki.

Hatimaye Abiria wa Precision Air wasafiri kutoka Dar kwenda Mtwara

0
0
Baada ya ndege ya Precision air PW 0403 kubuma hapo jana jioni na abiria wote kulazimika kulala Dar, asubuhi hii wamebadilishiwa ndege na kupanda PW 0401 kwenda mtwara. Jamaa wanasema hii haibumi.

Balozi Seif Ali Idd azindua rasmi safari za ndege za kitalii moja kwa moja kutoka Afrika Kusini hadi Zanzibar.

0
0

 Rubani wa Ndege ya Shirika la Mango Airlines Kepteni Kevin Viljoen akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Zanzibar kuanza safari za kuleta abiria kati ya Afrika Kusini na Zanzibar. Nyuma ya Kepteni Kevin ni Kaimu Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Juma Dunia Haji.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akimaliza kuzindua safari za ndege za shirika la Mango Airlines kati ya Afrika Kusini na Zanzibar katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar uliopo Kisauni. Kulia yake ni Kaimu Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Juma Duni Haji na Kushoto yake ni Mwakilishi wa Shirika la Mango Airlines hapa Zanzibar Bw. Javed Jaffery.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisoma hotuba ya uzinduzi rasmi wa safari za watalii kutoka moja kwa moja Afrtika kusini hadi Zanzibar kwa usafiri wa shirika la Mango Airlines katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar Kisauni Nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Baadhi ya Watalii 175 waliotua uwanja wa ndege wa Zanzibar kwa kutumia ndege ya shirika la Mango Airlines wakifurahia ukarimu wa kinywaji cha dafu mara tu baada ya kutua uwanjani hapo.Picha na Hassan Issa-Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
--
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema asilimia 80% ya mapato ya fedha za kigeni zinazoingia Nchini kupitia Sekta ya Utalii inaweza kubakia kuwa ndoto kama suala la amani na utulivu halitazingatiwa  na kupewa nafasi yake chini ya usimamizi wa Jamii kwa mashirikiano na Serikali Kuu.

Amesema hakutakuwa na mgeni wala Mtalii atakayekuwa na shauku ya kutaka kuingia Nchini sambamba na kufifia biashara ya Utalii endapo amani na utulivu uliopo utachezewa na hatimae kutoweka kabisa.

Balozi Seif Ali Iddi ameeleza hayo wakati akizindua rasmi safari za ndege za shirika liitwalo Mango Airlines kati ya Afrika Kusini na Zanzibar, kufuatia ushawishi uliofanywa na Kampuni ya utembezaji watalii Zanzibar ya Gallery Tours, hafla iliyofanyika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar uliopo Kisauni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Amesema Taasisi, Jumuiya na hata watu wanaohudumia wageni na watalii wanapaswa  kuendeleza zaidi ukarimu uliopo Nchini ambao ni miongoni mwa utamaduni unaoikuza Zanzibar Kiutalii katika Mataifa ya Nje.

“ Hakika vivutio tulivyokuwa navyo mfano Utamaduni, fukwe, bustani za ndani ya Bahari, Mambo ya kale, wanyama adimu ni mali kubwa, lakini mali zaidi katika vyote hivyo ni amani na utulivu”. Alisisitiza Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba  Serikali kwa upande wake  itajitahidi  kutunza na kuidumisha amani na wale  wanaotishia usalama wa wananchi na mali zao watachukuliwa hatua zinazostahiki kwa mujibu wa sheria bila ya kumuonea mtu.

Ameipongeza Kampuni ya Gallery Tours kwa uratibu wake uliofanikisha Kampuni ya Mango Airlines kuanzisha safari zake kati ya Afrika ya Kusini na Zanzibar na kuyataka Makampuni mengine popote pale yalipo kuanzisha safari kama hizo baina ya mataifa mbali mbali duniani na Zanzibar.
Balozi Seif ameyahakikishia  makampuni yatakayotumia fursa hiyo kuwa Serikali itayapatia mashirikiano ya hali ya juu lengo likiwa ni kurahisisha uingiaji wa watalii ili kuimarisha sekta hiyo muhimu kwa sasa.

Amefahamisha kwamba safari za ndege zitakazofanywa na Kampuni ya Mango Airlines  kati ya Afrika Kusini na Zanzibar ni miongoni mwa kishawishi kitakachoongeza idadi ya watalii wanaotoka Nchini humo kutembelea Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema  soko hilo la Afrika Kusini ni kubwa na ni lazima kwa makampuni yanayohusika na sekta hiyo kujiimarisha ili kupata watalii wengi zaidi.
“ Mwaka 2012 idadi ya watalii kutoka Afrika Kusini ni kubwa na ilifikia watalii elfu 11,145 na kuchukuwa nafasi ya Tano miongoni mwa Nchi zilizoleta watalii wengi hapa Zanzibar”. Amefafanua Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iiddi aliipongeza Wizara ya Habari, Utamaduni ,Utalii na Michezo Zanzibar kwa juhudi zake zilizopelekea kufanikisha harakati hizi za kukuza utalii nchini.

Akimkaribisha mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Kaimu Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Juma Duni Haji alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini moyo na juhudi za Makampuni hayo kwa uamuzi wao wa kuekeza katika sekta ya Utalii ambayo ni sehemu ya muhimili wa Uchumi wa Taifa.

Mh. Juma Duni alifahamisha kwamba Serikali inaelewa  kwamba vipo vivutio vingi vya ushawishi wa Utalii katika Mataifa mbali mbali Duniani lakini kampuni hizo zikaonelea kufanya biashara zao Zanzibar.

Kaminu Waziri huyo wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo alieleza kuwa muelekeo wa utoaji  wa huduma za Utalii zitaongeza kiwango cha mchango wa fedha  za kigeni kupitia Sekta hiyo.

Mapema Mwakilishi wa Kampuni ya Mango Airlines hapa Zanzibar Bw. Javed Jaffery alisema safari za ndege za Kampuni hiyo kati ya Afrika Kusini na Zanzibar zilianza Disemba mwaka uliopita lakini zikasitishwa kutokana na upungufu wa abiria kati ya pande hizo mbili.

Bw. Jaffery alieleza kwamba kuanza tena kwa safari hizo kumekuja kutokana na ongezeko la idadi ya makampuni yanayoshughulikia sekta ya Utalii kushawishi abiria kutumia kituo cha Zanzibar kama kiunganishi kwa safari zao katika Mataifa mengine Duniani.

Jumla ya abiria mia moja na Sabini na Tano wameteremka kutoka ndani ya  ndege hiyo ya Mango Airlines ikitokea moja kwa moja Afrika Kusini chini ya usimamizi wa Rubani wa Ndege hiyo Kepteni  Kevin Viljoen na wana anga wenzake.

ALEXANDER FORBES TANZANIA LIMITED REBRANDS TO ARIS

0
0
 The Finance Minister William Mgimwa takes a group photo with the African Risk and Insurance Services Limited (ARIS) management staff
 The African Risk and Insurance Services Limited (ARIS) Board Chairman Sir Andy Chande (second left) and the Finance Minister William Mgimwa (second right) display signed documents during a function that saw Alexander Forbes Tanzania Limited re-brand to ARIS. Left is the Commissioner of Insurance, Tanzania Insurance Regulatory Authority (TIRA) Israel Kamuzora. 
 The African Risk and Insurance Services Limited (ARIS) Board Chairman Sir Andy Chande (second left) hands over a present to the Finance Minister William Mgimwa (right) during a re-branding event that saw Alexander Forbes Tanzania become African Risk and Insurance Services Limited (ARIS) with effect from Tuesday. 
 The Finance Minister William Mgimwa (right) and the Commissioner of Insurance, Tanzania Insurance Regulatory Authority (TIRA) Israel Kamuzora (centre) sign documents during a re-branding event that saw Alexander Forbes Tanzania become African Risk and Insurance Services Limited (ARIS) with effect from Tuesday.
 The Finance Minister William Mgimwa gives a speech on behalf of the Prime Minster Mizengo Pinda who was supposed to be the Guest of Honor for the event. 
 The Mohamed Enterprises Tanzania Ltd (METL) Managing Director, Mohammed Dewji shares a light moment with the Minister for Home Affairs, Dr Emanuel Nchimbi during the event
 The Exim Bank Board Chairman Yogesh Manek interacts with some of the invited guests during the event.

R.I.P John Baptiste da Silva – 1937 - 2013

0
0

John da Silva passed away yesterday March 20, 2013 at the age of 76, with his family by his side, leaving many wondering: Who, now, will pick up where the renowned historian left and continue to tell the story?

Da Silva, who died of heart complications, some related to diabetes, had been ill for some time and leaves behind his devoted daughters Donna, Valerie and Cecilia, his adored nieces Bernadine, Presilda, Lucas, Lorna, Francesca, Lorraine, Ulrica, Roselee and Ramona, and three brothers Santana, Abel and Cajetan. His wife Carmen, who he had met and married in Zanzibar, died in 1993 and his late brother Rudolph had passed away recently.

Not least, he leaves an island, which is in mourning today for a man universally loved, admired and cherished for his gentle, generous and gregarious soul, his sharp wit, intellectual brilliance and tenacious dedication to the integrity of Zanzibar and its people. All it’s people. Those from every community he so lovingly sought to be preserved in their intertwined intricacies of their diverse histories. 

Da Silva’s funeral mass will take place today Thursday   21st March  at 3.30pm at St Joseph's Cathedral, Stone Town, Zanzibar  followed by his interment at Mwanakwerekwe Cemetery. 

The historian, artist and family 
father was Zanzibar’s living memory. 


Article 9

Airtel yazindua gharama nafuu zakupiga simu mitandao mingine

0
0
Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akielezea huduma mpya ya Airtel yatosha  yaani Simu kadi moja, taifa moja, bei moja inayomwezesha mteja wa Airtel kuwasiliana na mitandao yoyote nchi na kupata kifurushi cha muda wa maongezi, sms, na internet kwa bei nafuu hadi shiling 349/= pichani (katikati) ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel  Bi, Beatrice Singano Mallya akifatiwa na Meneja masoko Airtel Anethy Muga
 Mkurugenzi mkuu wa Airtel bwana Sunil Colaso akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma ya Airtel yatosha inayomwezesha mteja wa Airtel kupata dakika za muda wa maongezi,sms na kifurushi cha internet.

Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel  Bi, Beatrice Singano Mallya akiongea
wakati wa uzinduzi wa huduma mpya  ya Airtel Yatosha inayomwenzesha mteja wa Airtel kupata kifurushi cha maongezi , sms na internet na kuwasiliana na mitandao yoyote nchini, huduma hii imebeba ujumbe wa  simkadi moja, taifa moja, bei moja.

==========  ==========  =========

Airtel yazindua gharama nafuu za kupiga simu mitandao mingine

*         Airtel yadhihirisha simu kadi moja, taifa moja, bei moja -
Wateja nchini kufaidika na kiwango cha chini cha hadi 75% kupiga simu
popote bila kikomo

*          Piga simu muda wowote usiku and mchana

Dar Es Salaam  Jumatano 20 Marchi 2012.  Airtel Tanzania leo imezindua 
huduma mpya ijulikanayo kama "AIRTEL YATOSHA" itakayowawezesha wateja wake  nchi nzima kupiga simu kwenda mtandao wowote kwa kiwango nafuu cha hadi asilimia 75 bila kuwa na  sababu kubadili simu laini kwa kuhofia gharama.

Huduma ya AIRTEL YATOSHA inadhihirisha simu kadi moja, taifa moja, bei
moja  inayoendeleza dhamira ya Airtel ya kutoa huduma bora na nafuu
ambapo wateja wa Airtel sasa watapata ofa ya kifurushi kitakacho wapa
muda wa maongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet ambacho
kinaweza kutumika kwa siku au kwa wiki kulingana na mahitaji ya wateja

Akiongea wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa huduma hiyo iliofanyika
katika makao makuu ya Airtel Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw
Sunil Colaso Alisema"  Huduma ya Airtel YATOSHA ni maalum kwa kila
mtanzania, hii itawarahisishia watanzania wote kupata mawasilino
nafuu kwa kupiga bila kikomo kwenda mitandao mingine nchini. 

Kupitia
kifurushi cha Airtel YATOSHA wateja wa Airtel watafurahia kiwango cha
chini cha hadi shilingi 349/=, hii inamaana kwamba  mteja atapata
dakika 10 za kupiga simu kwenda mtandao wowote muda wowote, pia SMS
100 (ujumbe mfupi wa maneno) pamoja na kifurushi cha intenet cha 25MB
ofa itakayotumika masaa 24 kwa siku

Faida za AIRTEL YATOSHA kwa mteja zinadhihirisha dhamira yetu Airtel
ya kutoa huduma za mawasiliano bora na nafuu nchini. Airtel
tunazingatia kuwa wateja wetu wanamahitaji tofauti na ndio sababu
kubwa inayotufanya tuwe wabunifu kwa kuwapatia huduma zinazogusa kila
aina ya wateja na kuleta mabadiliko halisi kwa kuwapa wateja wetu nchi
nzima thamani ya pesa zao

Kwa Upande wake  Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel  Bi,i Beatrice
Singano Mallya alisema " Airtel YATOSHA  ni huduma inayopatikana kwa
SIKU au kwa WIKI hivyo mteja anapewa nafasi ya kuchagua anachokata.
Katika mpango wa WIKI mteja atatozwa shilingi 1,999  na kupata dakika
70, sms 700 na kifurushi cha interneti cha 175MB.

Kujiunga na huduma hii mteja anatakia kupiga *149*99#  na kuunganisha
moja kwa moja kwenye orodha ya huduma hii na kuchangua kifurushi
anachokipenda na kuweza kujipatia dakika za maongezi, ujumbe mfupi na
kifurushi cha internet.  Dakika za maongezi zitatumika kupiga simu
kwenda mtando wowote nchini kwa massa 24 na gharama za kupiga simu
zitatozwa kwa sekunde.

Kuhusu muda wa kujiunga na Airtel YATOSHA mteja anaweza kujiunga
wakati wowote  kati ya 0500hrs to 2359hrs,

Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma zenye
ubora na ubunifu nchini. Na hii ni njia nyingine ya kudhihirisha jinsi
Airtel inavyotoa huduma za mawasiliano yenye ubora na gharama za
ushindani kwa watanzania. Airtel itaendelea kuwa chachu ya maendeleo
kwa kutoa huduma  bora zenye gharama nafuu.

KAMATI YA BUNGE YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA BORA YATEMBELEA OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA

0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala Bora Dk.Pindi Chana (wa tatu kutoka kulia)akizungumza na viongozi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakati wa ziara ya kamati yake katika ofisi hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi Rasilimaliwatu Serikalini Bw.Emmanuel Mlay (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala Bora.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.HAB Mkwizu (aliyesimama)akiwasilisha kazi za ofisi yake kwa Kamati ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala Bora ilipofanya ziara ofisini hapo.
Wajumbe wa Kamati ya Katiba,Sheria na Utawala Bora wakiangalia jinsi Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara Serikalini (HCMIS)unavyofanya kazi kupitia mtandao katika ziara waliyoifanya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Mwenyekiti Msaidizi wa Kamati ya Bunge ya Katiba ,Sheria na Utawala Bora Mh.William Ngeleja (MB)(wa pili kulia) akichangia mada wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Naibu Spika aongoza kikao cha Kamati ya Mazingira cha Wabunge wa Afrika, Carribbean na Pacific

0
0
Mhe.Naibu Spika Job Ndugai akijadiliana jambo na Katibu Mkuu Msaidizi wa Umoja wa Mabunge ya Nchi za Afrika, Carribbean na Pacific (ACP) muda mfupi kabla ya kuongoza kikao cha Kamati ya Mazingira na Masuala ya Jamii cha Umoja huo katika mkutano unaoendelea jijini Brussels, Ubelgiji.Kulia ni mjumbe wa Tanzania Mhe.Dr Mary Machuche Mwanjelwa.
Mhe.Naibu Spika Job Ndugai akiwasilisha ripoti ya Kamati ya Mazingira na Masuala ya Jamii ya Mabunge ya ACP kwenye mkutano wa pamoja (Joint Assembly) wa Wajumbe toka kamati zote za Umoja huo.Katika ripoti yake Mhe.Ndugai alizungumzia changamoto kadhaa zinazokabili nchi za ACP katika sekta ya Mazingira na Masuala ya Jamii ikiwemo ongezeko kubwa la watu na uhaba wa rasilimali za kuwahudumia pamoja na mambo mengine. Picha zote na Saidi Yakubu wa Ofisi ya Bunge.

SERIKALI KUKUTANISHA VIONGOZI WA DINI, NGOs NA VYAMA VYA SIASA MWEZI UJAO - PINDA

0
0

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali itaitisha kikao cha wadau mbalimbali kutoka taasisi za dini, mashirika yasiyo ya Kiserikali pamoja na vyama vya siasa ili kujadili mustakabali wa Taifa la Tanzania na hasa suala la amani na utulivu.
 
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana mchana (Jumatano, Machi 20, 2013) wakati wa mahojiano maalum na kituo cha Redio Vatican kilichopo Vatican City, mjini Roma, Italia.
 
“Serikali inatarajia kuitisha kikao cha wadau wote kutoka vyama vya siasa, mashirika ya dini, NGOs, ili kutafakari nini kifanyike ambacho kitasaidia kuendeleza amani na utulivu... tutaitisha kikao hiki tarehe 4 Aprili,” alisema Waziri Mkuu wakati akihojiwa na Padri Richard Mjigwa, Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.
 

US Ambassador Donates Four Trucks to Tanzanian People's Defense Force on Behalf of American People

0
0
United States Ambassador Alfonso E. Lenhardt (center) with Chief of Defense Forces of the Tanzanian People's Defense Force (TPDF) General Davis Mwamunyange (left) and TPDF's Chief of Staff Lieutenant General Samuel Ndomba. Ambassador Lenhardt presided over a ceremony where he officially handed over four Toyota trucks to TPDF. The trucks were donated by the American people, through the U.S. Department of State's African Contingency Operations Training and Assistance Program (ACOTA). The event was held at the Ministry of Defense in Dar es Salaam on March 20, 2013. (Photo courtesy of the American Embassy)

Balozi Kamala ajitambulisha rasmi kwa Rais wa Mahakama ya Dunia ya Makosa ya Jinai (ICC)

0
0
Balozi wa Tanzania katika nchi za Ubelgiji, Uholanzi na Luxembourg Balozi Dkt. Diodorus B Kamala akiwa na Rais wa Mahakama ya Dunia ya Makosa ya Jinai (ICC) H.E Sang Hyun Song. Balozi Kamala alienda ofisini kwa Rais wa ICC kwa nia ya kujitambulisha rasmi. Balozi Kamala anaratibu mahusiano ya Tanzania na mahakama ya ICC.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA SIKU 3 WA MABADILIKO YA TABIANCHI JIJINI DAR

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia washiriki wa Mkutano wa kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, wakati akifungua mkutano huo wa siku tatu ulioanza leo Machi 21,2013 kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Fatma Fereji, wakionyesha moja vitabu vya Mabadiliko ya Tabianchi, baada ya kuzinduliwa na Makamu wa Rais wakati alipokuwa akifungua rasmi mkutano wa Kimataifa wa siku tatu wa Mabadiliko ya Tabinchi, ulioanza leo Machi 21, 2013 katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam. Wa pili (kushoto) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa (kushoto) ni Makamu Katibu Mtendaji wa UNFCC, Richard Kinley.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mwakilishi wa Balozi wa Denmark, Hanne Fritzen,wakionyesha moja vitabu vya Mabadiliko ya Tabianchi, baada ya kuzinduliwa na Makamu wa Rais wakati alipokuwa akifungua rasmi mkutano wa Kimataifa wa siku tatu wa Mabadiliko ya Tabinchi, ulioanza leo Machi 21, 2013 katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa (kulia) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Fatma Fereji.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Kitwanga, wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo leo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akiwahutubia wakati akifungua rasmi mkutano wa kimataifa wa siku tatu wa Mabadiliko ya Tabianchi, jijini Dar es Salaam leo. Picha na OMR

Ridhiwani Kikwete awa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa kitega uchumi klabu ya Yanga

0
0

MWENYEKITI  wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji leo amemtambulisha  Ridhiwani Kikwete kuwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa kitega uchumi katika eneo la klabu lililopo makutano ya Mafia/Nyamwezi eneo la Ilala jijini Dar es salaam.
 
Akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu yaliyopo mtaa wa Twiga na Jangwani, Manji alisema uteuzi wa Ridhiwani umezingatia uwezo wake kwa taaluma yake ya uwakili, na moyo alionao katika kujitolea katika kazi mbali mbali za klabu ya Yanga.
 
"Wote tunamfahamu Ridhiwani amekua ni mwanachama wa Yanga kwa muda mrefu, amekua akijitoa katika kazi mbali mbali za maendeleo ya klabu, hivyo tumeona ni vizuri kumpa fursa hiyo ili aweze kusaidia katika kuleta maendeleo ya klabu" alisema Manji
 
Katika kamati hiyo ambayo Ridhiwani ameteuliwa , amepewa fursa ya kuteua/kuchagua wajumbe atakaoshirikiana nao katika ujenzi wa kitega uchumi hicho katika mtaa wa mafia, pia atakua na uwezo wa kuongeza wajumbe au kupunguza kulingana na mahitaji kwa kipindi hicho.
 
Mara baada ya kutambulishwa kwa wanachama na waandishi wa habari, Ridhiwani alisema anashukuru kwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga Manji kumteua kushika nafasi hiyo na kuahidi kuwa atajitahidi kadri ya uwezo wake kuhakikisha ujenzi huo unafanikiwa.
 
"Nitakaa na kuangalia ni wajumbe gani ambao tutaweza kukaa pamoja na wajenzi (wakandarasi) ili kuweza kufanikiwa katika ujenzi wa kitega uchumi, kwani napenda eneo hilo liwe sehemu ambayo litasaidia katika uchumi wa klabu" alisema Rdihiwani 
 
Aidha Ridhiwan aliendelea kusema kuwa Kiwanja cha mafia kimekuwepo kwa mda mrrefu bila ya kufanyiwa muendelezeo, ila naamini tutajitahidi ili kuweza kuhakisha historia inajengwa kwa kubadili eneo hilo na kuwa sehemu ya kivutio na ya kuiingiza pesa klabu.
 
Ridhiwani mwisho alimalizia kwa kusema hawataishia katika ujenzi wa kiwanja cha mafia tu bali wataweka mipango kuhakikisha kuwa hata katika matawi ya Yanga sehemu mbali mbali wanaweza kuwekeza na kujenga majengo ambayo yatasaidia katika kuendeleza uchumui wa klabu.

maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Miti Duniani (World Wood Day) yafana jijini Dar

0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (kulia) akifurahia kinyago kilichochongwa na raia wa Afrika Kusini, Azwimpheleli (mwenye fulana nyeupe) huku Makamu wa Rais wa Chama cha Kimataifa cha Utamaduni wa Miti, Haward Rosen (mwenye tai) akimtazama,wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Miti (World Wood Day)yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee Dar es Salaam.
Mmoja wa wananchi aliyetembelea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Miti (World Wood Day) kwenye Viwanja vya Karimjee Dar es Salaam akijaribu mkanda.
Moja ya kinyago kilichopo kwenye moja ya Mabanda ya maonyesho ya Siku ya Kimataifa ya Miti (World Wood Day) kwenye Viwanja vya Karimjee Dar es Salaam.
Viewing all 109594 articles
Browse latest View live




Latest Images