Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

In Ever-loving memory of our beloved Suzanna Mgwassa

0
0
Heaven gained a beautiful angel on 13th March 2013, It’s been two years today bibi since you were suddenly called by the lord
Our hearts still bleed, but our love for you grows more with time.     
Your memories remain fresh in our hearts and the love we still have for you no money could buy..
You are fondly remembered by your kids, sisters, brothers, relatives, friends and grand kids. We will always remember you


A memorial mass is to be held at Kijitonyama Pentecostal Church on 15thMarch 2015 at 1030 hrs

TAARIFA KUHUSU KUANZA KWA MKUTANO WA 19 WA BUNGE JUMANNE IJAYO

0
0
Mkutano wa Kumi na Tisa wa Bunge la Kumi ambao ni mahusisi kwa ajili ya Kushughulikia Miswada ya Sheria, unatarajiwa kuanza siku ya Jumanne tarehe 17 Machi 2015 na kumalizika tarehe 1 April 2015 Mjini Dodoma. Shughuli zitakazokuwepo katika Mkutano huo ni kama ifuatavyo:


1.0        MISWADA YA SHERIA:

1.1        MISWADA YA SHERIA YA SERIKALI:

a)   Kusomwa kwa mara ya Kwanza na hatua zake zote:

Katika Mkutano huo, Kwa mujibu wa Kanuni ya 93(3) ya Kanuni za Bunge Toleo la Aprili 2013  Jumla ya Miswada Sita (6) itawasilishwa Bungeni kwa Hati ya Dharura na inakusudiwa kupitishwa na Bunge katika hatua zake zote. Miswada hiyo ni:

(i)       Muswada wa Sheria ya kupata habari wa Mwaka 2015(The Access to Information Bill, 2015),

(ii)      Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari wa   Mwaka 2015 (The Media Services  Bill, 2015),

(iii)     Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ushindani wa Mwaka 2015 [The Fair Competitio (Amendment) Bill, 2015],

(iv)     Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao wa Mwaka, 2015(The Computer and Cyber Crimes Bill, 2015),

(v)      Muswada wa Sheria ya Miamala ya Kiektoniki wa Mwaka 2014 (The Electronic Transaction Bill, 2015),

(vi)     Muswada wa Sheria ya Gesi Asilia wa Mwaka 2015 (The Natural Gas Bill, 2015).

b)   Kusomwa kwa mara ya Pili na hatua zake zote:

Aidha, Jumla ya Miswada 15 itasomwa kwa mara ya Pili Bungeni na kupitishwa na Bunge katika hatua zake zote kwa mujibu wa Kanuni ya 86(1) ya Kanuni za Bunge. Miswada hiyo ni:

(i)       Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Ajira za Wageni wa Mwaka 2014 [The Non- Citizens Employment Regulation Bill, 2014];

(ii)      Muswada wa Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa  wa Mwaka 2015 [The National Payment Systems Bill, 2015],

(iii)     Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi wa Mwaka 2014 (The Tax Administration Bill, 2014.

(iv)     Muswada wa Sheria ya Takwimu wa Mwaka 2014 (The Statistics Bill, 2014),

(v)      Muswada wa Sheria ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI wa Mwaka 2014 [The Tanzania Commision for AIDS (Amendment) Bill, 2014],

(vi)     Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa wa   Mwaka 2014 [The Disaster Management Bill, 2014],

(vii)    Muswada wa Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Dawa za Kulevya wa Mwaka 2014 [The Drug Control and Enforcement Bill, 2014],

(viii)   Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Stakabadhi Ghalani wa Mwaka 2014 [The Wharehouse Receipts (Amendment) Bill, 2014],

(ix)   Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Uhamiaji wa     Mwaka 2014 [The Immigration (Amendment) Bill, 2014],

(x)       Muswada wa Sheria ya Kudhibiti Silaha wa Mwaka  2014 [The Firearms and Ammunition Control Bill, 2014],

(xi)    Muswada wa Sheria ya Wataalam wa Kemia wa    Mwaka 2014 [The Chemist Professionals Bill, 2014],

(xii)    Muswada wa Sheria ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa Mwaka 2014 [The Government Chemistry Laboratory Bill, 2014],

(xiii)   Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2014 [The Written Laws (Miscellaneous Amendements) (No. 2) Bill, 2014] ,

(xiv)  Muswada wa Sheria ya Bajeti wa Mwaka 2014 [The Budget Bill, 2014], na

(xv)   Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana Tanzania wa Mwaka 2015 [The Youth Council of Tanzania Bill, 2015],



1.2        MUSWADA BINAFSI WA MBUNGE:

kwa Mujibu wa kanuni ya 81 (1) ya Kanuni za Bunge, katika Mkutano ujao wa 19 kunatarajiwa kuwasilishwa Muswada Mmoja wa Mbunge Binafisi ambao ni Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana la Taifa wa Mwaka 2013 (The Nationa Youth Council Bill, 2013) wa Mheshimiwa John John Mnyika. Muswada huu utasomwa kwa mara pili na hatua zake zote.


2.0        MAAZIMIO NA ITIFAKI MBALIMBALI

Pamoja na Miswada hiyo, katika Mkutano wa 19, Bunge linatarajia pia kuazimia Maazimio Mawili kama ifuatavyo:

1.        Azimio la kuridhia Mkataba wa Msingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala Barani Afrika.

2.        Azimio la kuridhia Makubaliano ya Msingi ya Ushirikiano katika Bonde la mto Nile (Agreement on the Nile river basin Co-operative Framework- CFA).



3.0       MASWALI:

Aidha, katika Mkutano huu  wa 19 wa Bunge, Jumla ya Maswali ya kawaida 170 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa ambapo ni wastani wa Maswali 15 kwa siku na maswali 10 kwa siku za Alhamisi.

Aidha kutakuwa na kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu kwa Mujibu wa Kanuni ya 38 (1) ambapo jumla ya  Maswali 18 ya msingi yataulizwa na kujibiwa na Mhe. Waziri Mkuu. 
Ratiba Kamaili ya Mkutano wa Kumi na Tisa (19) na jinsi shughuli zitakavyowasilishwa itatolewa baada ya Kamati ya Uongozi kukutana Jumatatu tarehe 16 Machi, 2015 ambapo itatolewa na kuwekwa katika Tovuti ya Bunge ambayo ni  www.parliament.go.tz


Imetolewa na:

Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa,

Ofisi Ndogo za Bunge

DAR ES SALAAM


13 Machi,  2015

UDSM Students' Death Announcement

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA APONGEZWA KWA KUFUFUA KIWANDA CHA SABUNI GEREZA KUU RUANDA, MBEYA

0
0
Na Lucas Mboje, Mbeya

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja amepongezwa kwa kukifufua Kiwanda cha utengenezaji Sabuni za aina mbalimbali Gereza Kuu Ruanda, Mbeya.

Pongezi hizo zimetolewa na Maofisa na Askari wa Magereza Mkoani Mbeya kutokana na kukiwezesha Kiwanda hicho vifaa na malighafi za utengenezaji sabuni hivyo kukifanya Kiwanda hicho kizalishe sabuni za kutosha kwa Wafungwa waliopo Magerezani Tanzania Bara.

"Tunampongeza sana Kamishna Jenerali Minja hususani kwa kukiwezesha Kiwanda chetu vifaa vya utengenezaji sabuni. Tunaamini kutokana na kasi ya utendaji wake wa kazi ataendeleza juhudi za kukiunga mkono Kiwanda hiki ili kiweze kukidhi mahitaji halisi ya soko la ndani na nje." Walisikika wakisema.

Kiwanda cha Uzalishaji sabuni cha Gereza Kuu Ruanda, Mbeya ni miongoni mwa miradi 23 iliyopo chini ya Shirika la Magereza(Prison Corporation Sole) ambapo mradi huu ulianza shughuli zake za Uzalishaji sabuni mnamo Mwaka 1978.

Madhumuni ya kuanzishwa kwa mradi huu yalilenga zaidi kutimiza majukumu ya msingi ya Jeshi la Magereza hususani utekelezaji wa Programu ya Urekebishaji wa Wafungwa kwa kuwafundisha utengenezaji wa sabuni pia kiwanda hicho kinajiendesha kibishara hivyo kuchangia pato la Taifa.

Kiwanda hicho kinatengeneza Sabuni za aina mbalimbali zikiwemo Sabuni za kufulia zenye miche minene na mifupi, sabuni za kuongea, sabuni za maji kwa ajili ya usafi majumbani pamoja na sabuni za chenga chenga(flex soap).

Malighafi zinazotumika katika Kiwanda hicho ni caustic soda, mafuta ya mawese na mafuta ya mise ambayo hupatikana kwa wingi Wilayani Kyela, Mkoani Mbeya. Kwa wastani Kiwanda hicho kinauwezo wa kuzalisha katoni za sabuni 150 hadi 200 kwa siku.

Tangu kuanzishwa kwa mradi huu kwa kiasi kikubwa kimechangia utoaji elimu ya Ufundi Stadi kwa vitendo kwa Wafungwa katika fani ya za utengenezaji wa sabuni ambapo kuna Wafungwa wengi wamenufaika kupitia mradi huu na wameweza kuanzisha shughuli zao baada ya vifungo vyao kukoma.
Fundi Mkuu katika Kiwanda cha Sabuni cha Gereza Kuu Ruanda, Mbeya Sajin wa Magereza, George akitoa maelezo ya aina za Sabuni zinazotengenezwa katika mradi wa Sabuni Gereza Kuu Ruanda, Mbeya kama zinavyoonekana katika picha(Picha zote na Lucas Mboje).
Muonekano wa Sabuni ya kufulia ikiwa bado haijawekwa kwenye mashine maalum ya kukatia vipande vyenye ukubwa tofauti tofauti. Kwa wastani Kiwanda hicho kinauwezo wa kuzalisha katoni 150 hadi 200 kwa siku.
Sabuni za kufulia zenye miche minene mirefu(Big Bars) zinazotengenezwa katika Kiwanda cha Sabuni cha Gereza Kuu Ruanda, Mbeya zikiwa tayari kupelekwa kwa watumiaji.

MAAFISA WA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA MAFAO YA UZEENI KENYA (RBA) WAFURAHISHWA NA HUDUMA ZA PPF

0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Vupe Ligate, (kulia), na Meneja Miundombinu ya IT wa Mfuko huo, Gilbert W. Chawe, (katikati), wakimsikiliza afisa mwandamizi kutoka Mamlaka ya Usimamizi Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Rehema Kabongo, wakati wa ziara ya Maafisa kutoka Mamlaka ya Usimamizi Mafao ya Uzeeni, nchini Kenya, (RBA), kwenye makao makuu ya PPF barabara ya Samora/Morogoro jijini Dar es Salaam.
Maafisa toka Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Tanzania, (SSRA) na wenzao kutoka Kenya (RBA), wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa na mameneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakati maafisa hao walipotembelea makao makuu ya PPF kwa nia ya kujifunza shughuli za uhifadhi wa mafao na pensheni.
Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakifuatilia kwa makini wakati wa mkutano baina ya viongozi wa PPF na maafisa waandamizi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Mafao Ya Uzeeni kutoka Kenya, (RBA), walioongozwa na wenyeji wao SSRA kwenye ziara yao ya kujifunza walioifanya makao makuu ya Mfuko huo barabara ya Samora na Morogoro jijini Dar es Salaam.

Mh. Binilith Mahenge aendelea na ziara yake Mkoani Mbeya

0
0
Na Victor Mariki – Ofisi ya Makamu wa Rais.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Binilith Mahenge ameishauri Halmashauri ya Jiji la Mbeya kutafuta wawekezaji watakaotumia taka kama malighafi katika shughuli uzalishaji viwandani ili kukabiliana na uchafuzi wa mazingira jijini humo.

Ushauri huo aliutoa, akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani humo wakati alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya na kuzungumza na Idara ya Usafishaji na Mazingira jiji humo jana.

Aliongeza kusema kuwa taka ni mali, zinaweza kutumika katika uzalishaji wa bidhaa nyingine huku akitolea mfano Kiwanda cha Falcon, kinachozalisha milango pamoja na chemba za vyoo kwa kutumia taka huko jijini Mwanza.

Pia katika ziara hiyo Mh. Mahenge, alitembelea Mtaa wa Ntungi, Kata ya Nsalaga ili kuona ujenzi wa dampo jipya lenye mita za ujazo 454,000, linaloweza kutumika ndani ya miaka sita ambalo ujenzi wake umewezeshwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya shilingi bilioni 3.8.

Wakati huo huo pia, alitembelea hifadhi ya Safu ya Mlima Mbeya ili kujionea mikakati ya utunzaji mazingira inayotekelezwa katika hifadhi hiyo, ikiwemo upandaji miti kwa ajili ya kutunza vyanzo vya maji pamoja na ugawaji wa mbegu ya miti ya kuni bure kwa wananchi waishio karibu na hifadhi ili kuhepusha vitendo vya ukataji miti katika hifadhi hiyo.

Katika majumuisho ya ziara yake mkoani Mbeya, Mh. Mahenge alitembelea kiwanda cha saruji cha Mbeya Ciment, ambapo aliridhishwa na uendeshwaji wa shughuli za uzalishaji kiwandani hapo nakuupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuzingatia Kanuni za Mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Injinia Binilith Mahenge (katikati), akitoa majumuisho wakati akimalizia Ziara yake ya Siku mbili iliyofanyika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya nakumalizikia katika Kiwanda cha Saruji kilichopo eneo la Songwe, Mkoani humo jana. (Picha na OMR)

Polisi waendelea na uchunguzi dhidi ya Mlinzi wa Katibu Mkuu wa CHADEMA

0
0
Na Chalila Kibuda ,Globu ya jamii

Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linaendelea na uchunguzi dhidi ya Mlinzi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk.Wilbrod Slaa anayedaiwa kufanya njama ya kumuua kwa sumu, Bw. Khalid Kagezi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo,Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova amesema wamechukua maelezo kwa Katibu Mkuu Dk.Wilbrod Slaa pamoja na maelezo ya mlizi wake Khalid Kagezi.
Kamishina Kova amesema Chadema walichukua hatua mbalimbali na kujiridhisha kuhusika kwa mlinzi wa Dk.Slaa kufanya mikakati ya kumuua kwa sumu kwa kuiweka katika maji au chakula.
Amesema kwa maelezo ya Mlinzi huyo alidai kuteswa na baadhi ya watu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa kuwataja kwa majina.
 Kamishina Kova amesema Kagezi alidai kutekwa na kushambuliwa katika mwili wake na jeshi la Polisi likampa fomu namba tatu (PF3)kwa ajili ya matibabu
“Jeshi la Polisi limefanya jitihada kwa kupata maelezo kwa watu wote ambao wamehusika kwa mlizi na Dk.Slaa”amesema Kamishina Kova.
Amesema baada ya uchunguzi watapeleka kwa wakili wa serikali na yeyote atakayehusika sheria itashika mkondo wake.
Wakati huo huo, Haroub Mtopa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kufanya utapeli katika ofisi ya Rais kwa kudai kuwa yeye ndiye Katibu wa Rais  Bw. Prosper Mbena.
Mtopa amekamatwa jana baada ya kutegeshewa mtego wa sh.250,000 za jeshi la polisi kwa mtu anayedaiwa kutapeliwa kutaka kumuongeza fedha kwa mara ya pili.
Kamishina Kova amesema Mtopa alikuwa kila siku anapita Ikulu kwa matatizo mbalimbali kumbe ndio alikuwa akiwatega watu na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Amesema watu wanaofika katika ofisi zote bila kuwa na taarifa zao wawafatilie kutokana na kufanyia utapeli kupitia ofisi hizo
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake leo.

KAMATI YA BUNGE YA UKIMWI NA MADAWA YA KULEVYA YATEMBELEA MAKAO MAKUU YA PSPF, WAFURAHISHWA NA MAFANIKIO YALIYOFIKIWA

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya Mhe. Lediana Mg'ong'o
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu akitoa taarifa kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya inayoshughulikia masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya walipotembelea Makao Makuu ya PSPF, jijini Dar es salaam.Kushoto ni viongozi wa Kamati hiyo Mhe. Diana Chilolo, Makamu Mwenyekiti na Lediana Mg’ong’o, Mwenyekiti wa kamati hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya Mhe. Lediana Mg'ong'o akisisitiza jambo wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakati kamati anayoiongoza ilipotembelea makao makuu ya mfuko huo leo jijini Dar es salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, Bw. George Yambesi na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu.
Wajumbe wa Kamati ya ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa mfuko wa Pensheni wa PSPF mara baada ya kuhitimisha ziara yao makao makuu ya mfuko huo jijini Dar es salaam.  

Tanzania na China kuendeleza ushirikiano kwenye Sekta ya Uwekezaji na Viwanda

0
0
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akizungumza wakati wa mkutano kati yake na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Balozi Liu Songtian  (hayupo pichani). Balozi Liu na ujumbe wake wapo nchini kwa ajili ya kufuatilia masuala ya uwekezaji na maendeleo ya viwanda Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi tatu za Afrika zilizochaguliwa na China kwa ajili ya kuwa mfano katika uwekezaji na maendeleo ya viwanda. Nchi zingine ni Ethiopia na Kenya. Wengine katika picha ni Balozi Mbelwa Kairuki (kushoto kwa Bal. Gamaha), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Mhe. Abdulrahman Shimbo (mwenye tai nyekundu), Balozi wa Tanzania nchini China na Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa EPZA.
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Balozi Liu Songtian akizungumza wakati wa mkutano kati yake na Balozi Gamaha na ujumbe wake. Kulia ni Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Lu Yoqing.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Pazi ReUnion USA. Mabo yazidi kupamba moto Houston Texas

0
0


Mdau Richard Kasesela ( Wapili kulia) alipokua akiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa George  Bush Intercontinental uliopo Houston, Texas nchini Marekani kwa ajili ya Pazi Reunion itakayofanyika siku ya Jumamosi March 14, 2015 katika uwanja wa mpira wa kikapu wa Pilgrim uliopo katika kanisa la Lutheran lililopo Houston. Wengine katika picha ni wenyeji wake waliompokea,  kutoka kushoto ni Willy Crrusa, Aika na Flora Mochiwa maarufu kama Madikodiko. Mchezaji mwingine anayekuja kwenye maadhimisho hayo ya Pazi toka nje ya Marekani ni Atiki Matata anayekuja siku ya Ijumaa March 13, 2015 akitokea Uingereza. Picha na VIJIMAMBO
 Richard Kasesela akitest uwanja wa mpira wa kikapu mara tu alipowasili uwanjani hapo mara tu baada ya kutoka uwanja wa ndege kushoto ni Davis mchezaji mwingine wa mchezo huo, Flora Mochiwa na Willy Crrusa wakiangalia kama bado wamo. Richard Kasesela richa ya kuwa mchezaji wa Pazi pia aliwahi kuwa Rais wa chama cha mpira wa kikapu Tanzania.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Tangazo la msiba wa Robert John Ndege Makilagi wa pugu kajiungeni

0
0
Familia ya Mr Robert Makilagi ya Pugu Kajiungeni inasikitika kutangaza kifo cha baba yao mpendwa Robert John Ndege Makilagi kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 11/3/2015 katika hospital ya Hindu Mandal, Dar es salaam.

Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki wote popote pale walipo.

Marehemu Mzee Makilagi ataagwa nyumbani kweke pugu kajiungenikesho Jumamosi  asubuhi tarehe 14/3/2015 ikifuatiwa na ibada itakayoanza saa 8 mchana katika kanisa katoliki la Pugu lililopo Pugu Sekondari.

Baada ya kumalizika Ibada, Marehemu atazikwa saa tisa (9) katika makaburi ya Wakatoliki Pugu.

Bwana ametoa, na Bwana ametwaa.
 Jina la Bwana lihimidiwe.
AMINA

TANZANIA AND COLONIAL WAR DEBATE IN DAR ES SALAAM ON MARCH 19, 2015

0
0


 Thursday 19 March 2015
18.00 – 21.00

At the British Council
Corner Samora Machel Avenue and Ohio Street
Dar es Salaam 

It’s remembered as a European conflict, but one hundred years ago the British and German Empires also fought the First World War in East Africa.  The struggle over present-day Tanzania left an untold legacy that this debate will uncoverThe BBC’s Audrey Brown will be joined by some of the world’s greatest experts in World War One: The South African historian Bill Nasson and the India historian Santanu Das are coming to Tanzania and will be joined by Oswald Masebo from Dar es Salaam University.  He will present an essay on the Tanzanian Memory of The Great War. 

Make history with the British Council and the BBC: come and join the debate and take part in the BBC recording.  The event will be in English.

You must register in order to attend this event.  Attendance is free of charge.

Should you have any further queries or are having difficulties in registering, please contact us by email WW1info@britishcouncil.org or telephone +255 (0) 22 2165 300         

YAMOTO BAND WAELEKEA NEW YORK CITY BAADA YA KUPAGAWISHA UINGEREZA

NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA LIVE Katika Africa Unite Party Jumamosi 14 March 2015 MJINI STUTTGART, UJERUMANI

0
0
The Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni

Bendi hiyo inatarajiwa kutumbuiza katika onyesho maalumu la AFRICA UNITE PARTY litakalofanyika katika ukumbi wa VTS uliopo mtaa wa Augusburger Str.442 D-70327 mjini Stuttgart,nchini Ujerumani.

Onyesho hilo limeandaliwa na shirika la Afrikaktiv e.V wakishirikiana na  shirika la Cabaret du Monde,
Ngoma Africa band iliyozoeleka kwa kuwatia kiwewe washabiki wake kila kona duniani wataporomosha muziki moto moto na mdundo wao maarafu kama " Extraordinary Bongo Dansi" mdundo unaotingisha bila ya kuwa na mpinzani huko ughaibuni. Bendi hiyo inadumu katika medani ya muziki kwa muda wa miaka 23 na kufanikiwa kujizolea washabiki kila kona.

Ticket za onyesho hilo zinapatikana kwa simu ( booking): Call9+49 0)152 12091242 au +49(0)152 106106137 Mnakaribishwa wote,pia usikose kuwasikiliza
FFU-Ughaibuni at www.ngoma-africa.com

ngoma azipendazo ankal - kindly sponsored by isumba lounge...live in action every friday and saturday with dj jd & fast eddie on the one and two!


MAFUNZO YA AWALI YA UASKARI MAGEREZA KOZI NA. 27 YAENDELEA VYEMA CHUONI KIWIRA, TUKUYU, MBEYA

0
0
 Askari Wanafunzi(Recruits) wa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza Kozi Na. 27 wakiendelea na masomo kwa vitendo katika Gwaride la silaha kama wanavyoonekana kikakamavu wakiwa na Walimu wao uwanjani huku silaha zao zikiwa begani.
 Askari Wanafunzi wa Mafunzo ya Uaskari Magereza Kozi Na. 27 wakiendelea na somo la Gwaride la Salaam ya Utii wakiwa na silaha kama inavyoonekana katika picha.
 Bango Kuu linaloonyesha unapoingia Chuo cha Mafunzo ya Uaskari Magereza kilichopo Kiwira, Mkoani Mbeya.
Askari Wanafunzi wa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza wakiendelea na masomo ya Darasani. Katika Mafunzo hayo hujifunza masomo mbalimbali ikiwemo Utawala na Uendeshaji wa Magereza, Sheria zinazoongoza Jeshi la Magereza, Ustawi wa Jamii, Afya, Uraia na Utawala na Uongozi(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

TAMKO LA RSA KUHUSU AJALI ZA BARABARANI

ufunguzi wa Msikiti Mpya wa Ijumaa wa Kijiji cha Bandamaji Mvumoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.

0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya kuendeleza ujenzi wa Misikiti na Madrasa Zanzibar Rais Mstafu wa Tanzania Al-Hajj Ali Hassan Mwinyi akitoa salamu wakati wa hafla ya ufunguzi wa Msikiti Mpya wa Ijumaa wa Kijiji cha Bandamaji Mvumoni Mkoa wa Kaskazini Unguja. Kulia ya Mzee Mwinyi ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mfadhili wa Ujen zi wa Msikiti huo Sheikh Muhoma.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu wa Kijiji cha Bandamaji Mvumoni mara baada ya kuufunguwa rasmi Msikiti wa Ijumaa wa Kijiji hicho kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al-Hajj Dr. Ali Mohammed Shein.
 Balozi Seif akigawa Misahafu kwa ajili na Madrasat Taawun na Masjid Bilal wa Kijiji cha Bandamaji Mvumoni mara baadsa ya kuzindua Msikiti na Madrasa hiyo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na Mke wa Mfadhili wa Ujenzi wa Msikiti Bilal wa Bandamaji Mama Fatma nje ya msikiti huo. Kati kati yao ni Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Mkoa wa Kaskazini Unguja Sheikh Khamis Abdulhamid.
Picha na –OMPR – ZNZ.

GAPCO YAIPIGA TAFU MAENDELEO YA MICHEZO YA RIADHA NCHINI

0
0
Mkurugenzi mkuu wa GAPCO Afrika Mashariki Macharia Irungu akimpongeza Simon Mlewa mshindi wa kwanza mbio za walemavu kwa upande wa wanaume wanaotumia tricycle.
Mkuu wa wilaya ya  Moshi Novatus Makunga akimkabidhi zawadi Joseph Mungure mshidi wa kwanza mbio za walemavu kwa upande wa wanaume wanaotumia wheelchair. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa GAPCO Tanzania Vijay Nair, Meneja Masoko Caroline Kakwezi na Mkurugenzi Mkuu wa GAPCO Afrika Mashariki Macharia Irungu. Kulia ni Katibu Mkuu wa kamati ya michezo ya walemavu Tanzania (Paralympic) Peter Sarungi.
Mkuu wa wilaya ya Moshi Novatus Makunga akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza mbio za walemavu kwa upande wa wanawake Linda Macha. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa GAPCO Tanzania Vijay Nair na Meneja Masoko Caroline Kakwezi.

KIPINDI CHA DIRA YA DUNIA KUTOKA BBC IDHAA YA KISWAHILI, LONDON, LEo

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images