Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 766 | 767 | (Page 768) | 769 | 770 | .... | 3272 | newer

  0 0

  The East African Legislative Assembly (EALA) resumes business next week by holding its Plenary in Bujumbura, Burundi. The Plenary which takes place from Monday, March 16, 2015, to Friday, March 27, 2015, is the Fifth Meeting of the Third Session of the Third Assembly.

  The President of the Republic of Burundi, H.E. Pierre Nkurunziza is expected to address a Special Sitting on Tuesday, March 17th, 2015.   The President of the United Republic of Tanzania and Chairperson of the Summit of EAC Heads of State, H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, is also expected to deliver the State of EAC Address on March 19th, 2015.

  The State of EAC Address is delivered annually by the sitting Chairperson of the Summit of EAC Heads of State and it reflects on matters of policies related to the Community.

  The Assembly is to be presided over by the Speaker, Rt. Hon Daniel F. Kidega. Top on the agenda during the two week period are key bills which are expected to be debated.

   The Bills include the EAC Customs Management (Amendment) Bill, 2015 the EAC Competition (Amendment) Bill, 2015, the EAC Cross Border Legal Practice Bill, 2014 and the EAC Electronic Transaction Bill, 2014.


  0 0

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetembelea wahanga wa mfuriko ya mvua katika wilaya ya kahama mkoani shinyanga kwa kuwapatia msaada wa mahitaji muhimu yanayoitajika kwa sasa. Zaidi ya watu 35 walifariki na kuwaacha mamia wakiwa hawana makazi ya kukaa kufatia mvua kubwa iliyonyesha mwanzoni mwa mwezi machi mwaka huu

  Akionge wakati wa makabithiano ya msaada huu, Meneja mauzo wa Airtel Shinyanga Bwana Ezekiel Nungwi alisema” Tunaungana kwa pamoja katika maafa haya na kutoa pole kwa familia zilizopoteza marafiki na wanafamilia kutokana na mafuriko haya.

  Tunatambua pia mafuriko haya yamewaacha wakazi wengi bila makazi, huku mazao yao kuharibiwa na mifugo yao kufa hivyo tunaungana kwa pamoja kutoa msaada kwa namna tutakayoweza . Leo kwa niaba ya Ofisi yetu ya kanda ya Shinyanga tunatoa msaada wa mabati, mablanketi, magodoro pamoja na chakula vyenye thamani ya shilingi milioni 3 na kuwaomba watanzania kuungana nasi kuwasaidia ndugu zetu wa kahama ili kuepuka milipuko ya magonjwa isitokee na kuwawezesha kurudi kufanya shughuli zao za kawaida mapema iwezekanavyo.

  Sambamba na mchango huu, tunapenda kuzindua namba maalumu itakayowawezesha watanzania kuchangia. Tunachukua fulsa hii kuwaomba wateja wetu kuchangia kwa kutuma ujumbe wenye neno MAAFA kwenda namba 15626 , ujumbe huu utalipiwa shiling 256 na pesa hiyo itaingia kwenye mfuko wa kuchangia wahanga wa mafuriko mkoani Shinyanga,

  Akiongea kwa niaba ya wakazi wa Kahama helen Benjamin Alisema” Tunawashukuru sana Airtel kwa msaada huu ulikuja wakati tunauhitaji zaidi, Tunawashukuru kwa kuanzisha namba itakayowapa fulsa watanzania kuchangia, napenda kuwaomba watanzania kushiriki kwa kuchagia na kwa makampuni mengine kujitolea na kutusaidia katika hali ngumu ambayo imetuweka kwenye hatari kupata milipuko ya magojwa na zaidi tumekosa makazi na shughuli zetu za kiuchumi zimeteketea. Tunawashukuru waliojitolea mpaka sasa na tunaomba muendelea na moyo huo wa kujitolea.
  Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Mh. Benson Mpesya akisalimiana na Muwakilishi wa kampuni ya Airtel mkoa wa Shinyanga,Ezekiel Nungwi wakati Kampuni hiyo ilipofika kuwaona wahanga wa mafuriko na kuwapelekea Baadhi ya Vitu mbali mbali.kampuni hiyo ya Airtel imetoa,sabuni ,mabati ,maharange ,mchele ,mafuta kwa Wahanga hao.
  Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Mh. Benson Mpesya akiwapongeza wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya Aitel kwa moyo wao wa kuwasaidia waathilika wa mafuriko katika kijiji cha mwakata ambapo Wilayani Kahama yaliyotokea hivi karibuni.Airtel imetoa msaada wa vitu mbali mbali kama vile sabuni ,mabati ,maharange ,mchele ,mafuta.
  Sehemu za Nyumba zilizoathiliwa na Mafuriko hayo.


  0 0


  0 0

  Wakati homa ya pambano la ubingwa wa dunia wa WBF kati ya mabondia, Mohamed Matumla na Wang Xin Hua wa China ikipamba moto, wadhamini wa pambano hilo wametoa nafasi kwa mashabiki wa ndondi kubahatisha 'kubeti' mshindi.

  Pambano hilo la raundi 12 la uzani wa Bantam limepangwa kufanyika Machi 27 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa pia na bingwa wa zamani wa dunia wa uzani wa juu, Francois Botha ambaye atakuwa mgeni rasmi.

  Promota wa pambano hilo, Jay Msangi alisema jana kuwa maandalizi yote yamekamilika na pambano litasimamiwa na Shirikisho la ngumi la dunia la WBF ambaye rais wake atawasili nchini Machi 21.

  Akizungumza jijini jana, Meneja Masoko wa Casino za Iplay 8, Le Grande na Palm beach, Ezekiel Lyal alisema wameamua kutoa nafasi ya bahati nasibu ya kushinda fedha 'Kubeti' kwa mashabiki wa ndondi kwenye pambano hilo.

  "Shabiki anachotakiwa ni kuingia kwenye tovuti ya www.iplay8casino.com ambapo kama ni mara ya kwanza atajisajili kwa kufuata maelekezo ambapo ni bure na atafungua akaunti ambapo ataanza kubeti na anaweza kufanya hivyo kwa wakala yoyote wa mtandao wa simu au benki na anaweza kuweka kiasi chochote cha fedha kuanzia elfu moja na kuendelea," alisema Lyal.

  Mbali na pambano la Matumla, siku hiyo pia mabondia wenye upinzani, Mada Maugo na Japhet Kaseba na Karama Nyilawila na Thomas Mashali watazichapa mapambano ya kumaliza ubishi nani mkali kati yao huku bondia wa uzito wa juu kutoka Zanzibar akizichapa na bondia kutoka Marekani.

  "Maandalizi yote yamekamilika na kuanzia wiki ijayo mabondia kutoka nje ya nchi na viongozi wa WBF sambamba na Botha wataanza kuwasili kwani tayari tiketi zao zimekamilika," alisema Msangi.

  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Profesa Juma Athumani Kapuya akizungumza na watendaji wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa nyumba za Serikali, wakati walipotembelea ofisi za Wakala jana jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli.
  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akieleza jambo kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu (hawapo pichani) kuhusuiana na mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa miradi mbalimbali na hatua zilizochukuliwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga akiongozana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Prof. Juma Kapuya, wakati Kamati hiyo ilipotembelea nyumba za watumishi wa Serikali eneo la Ada Estate jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Kampuni inayoongoza kwa huduma ya teknolojia ya mawasiliano, Push Mobile Media imezindua huduma ya ujumbe kwa njia ya mtandao wa internet ijulikanyo kwa jina la “Bulk Messaging” kwa lengo la kumwenzesha mtumiaji kufikisha ujumbe mmoja kwa watu wengi na katika muda muafaka.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Push Mobile Media, Freddie Manento alisema kuwa huduma hiyo itamwezesha mtumiaji kufikisha ujumbe muhimu kwa gharama nafuu ikiwa katika sekta mbalimbali na kwa mtu binafsi.

  Manento alisema kuwa lengo kubwa ya kuanzisha huduma hiyo ni kuwawezesha wafanyabiashara na sekta nyingine kufanya mawasiliano ya haraka zaidi na kujitangaza.

  “Kama ni mfanyabiashara, utaweza kujitangaza pia kwani wateja watapata taarifa muhimu utakazo wapa kwa muda muafaka na wao kuutumia katika maendeleo ya biashara zao,” alisema Manento. “Ili kupata huduma hiyo, unatakiwa kujiunga kupitia mtandao wetu, www.pushgw.com na kufungua akaunti yako,” alisema Manento.

  Alisema kuwa makampuni au taasisi yanaweza kutumia huduma hii kuwapa taarifa wafanyakazi, wateja wao kuhusiana na biashara na taarifa nyingine. “Kwa watu binafsi, unaweza kutumia huduma hii kutoa taarifa za shughuli mbalimbali ikiwa pamoja na harusi na hata kwa waandishi wa habari wanaweza kutumia taarifa hii kwa lengo la kuwasiliana na wahariri wao kwa kile wanachokifanya katika sekta hiyo,” alisema.

  Mkuu wa Idara ya Mauzo na Masoko wa Push Mobile Media Limited Ezekiel Mukundi alisema kuwa huduma hiyo ni rahisi kwani mtumiaji anaweza kutuma ujumbe kwa kiasi cha sh 16 kwa kutegemea na ukubwa wa ‘bando’ analotaka.

  Alisema kuwa kwa upande wa sekta ya afya, huduma hii inawezwa kutumiwa na madaktari kuwakumbusha wagonjwa kuhusiana na siku ya kupata matibabu. “Unachotakiwa kufanya ni kujiunga na huduma hii kwa njia ya mtandao na kuweka namba za simu ya mkononi kwa watu wanaotakiwa kupata taarifa na kutuma, watapata kwa haraka zaidi na kwa muda unaofaa,” alisema Mukundi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Push Mobile Media, Freddie Manento akifafanua jambo kuhusiana na huduma ya ‘Online Bulk Messaging’ inavyofanya kazi. Huduma hiyo itamwezesha mtumiaji kutuma ujumbe mmoja kwa watu wengi na katika muda muafaka.
  Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Push Mobile Media Limited, Ezekiel Mukundi (Kulia) akielezea umuhimu wa huduma ya “online bulk Messaging’ kwa sekta mbalimbali. Kushoto ni Daniel Buchafwe ambaye ni Mkuu wa Idara ya Ufundi.
  Mkuu wa Idara ya Ufundi wa Kampuni ya Push Mobile Media Daniel Buchafwe akielezea jinsi ya huduma ya “online bulk messaging” inavyofanyakazi. Kulia ni Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Push Mobile Media Limited, Ezekiel Mukundi.

  0 0  0 0

  Bobby Brown - Every Little Step

  0 0

  It is two years today since the sudden loss of our beloved Ibrahim Werrema John, who passed away on March 13, 2013 in Dar es salaam.

  Your wife Agatha Ibrahim John, your parents Mr & Mrs John Keraryo, brothers, sisters, nephews and nieces, inlaws and friends can’t forget your fond memories of kindness, friendship and amazing sense of humor. You were a wonderful leader on others and inspirational to every one of us. 

  With still remember that sad final moment when you left us with disbelief and tearful eyes. We have leant to remember you with smiles not tears as we believe we will see each other once again; When God call us we hope to be right by your side and reunite.

   “Whosoever believeth in Christ shall never perish, but have eternal life”.(John 3:16)
  As we remember you in this day, we promise to continue all the good things that you had already set for us to accomplish. In our hearts you will always stay.

  Your life was a blessing, your memory a treasure.
  You are loved beyond words and missed beyond measure.
  We hope to be re-united forever in eternity. 

  AMEN

  0 0

  Wajumbe kutoka Tanzania wanaohudhuria mkutano wa Benki ya Dunia kuhusu Mahitaji ya Stadi na Maendeleo kwa Sekta Muhimu katika Ukuaji wa Tanzania unaofanyika Washington, nchini Marekani wakiwa katika mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mh. Liberata Mulamula (kushoto) wakati walipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini humo. Wajumbe hao kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Prof. Yunis Mgaya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira, Bw. Eric Shitindi pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Mhandisi Zebadiah Moshi.

  0 0

  Katika picha hii ya maktaba anaoneka Mhe. Asha-Rose Migiro ( Mb) wakati huo akiwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa na baadhi ya askari wanawake kutoka JWTZ wanaoshiriki katika operesheni ya kulinda amani kupitia Umoja wa Mataifa huko Lebanon. Katika mchango wake, Mhe. Simba pamoja na mafanikio mengine ambayo Tanzania imeyapata katika miaka 20 tangu mkutano wa Beijing ni pamoja na askari wanawake kupata fursa za kushiriki katika operesheni za kulinza amani zinazoratibiwa na Umoja wa Mataifa.
  Mhe. Sophia Simba ( Mb) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akizungumza (alhamisi) katika majadiliano ya jumla katika mkutano wa Kamisheni 59 kuhusu Hadhi ya Wanawake. Mhe. Waziri anaongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwamo wajumbe kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.Tanzania ni kati ya nchi 13 zinazoiwakilisha Afrika katika Kamisheni hii inayoundwa na nchi 45.
  Sehemu ya ujumbe wa Mawaziri kutoka nchi za Afrika wakati wa mkutano wao uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Nchi za Afrika.
  Pamoja na kuzungumza katika majadiliano ya jumla, Mhe Waziri Sophia Simba pia alipata fursa ya kuhushiriki Mkutano wa Mawaziri kutoka Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Afrika karibu na UN. Mkutano huo ulikuwa wa kujadiliana na kupitisha maazimio mbalimbali kuhusu maudhui ya mwongo wa wanawake wa Afrika. Pichani Mhe. Waziri akiwa na Katibu Mkuu wake Bi. Anna Maembe wakifuatilia majadililano hayo.

  Na Mwandishi Maalum, New  York

  Ushiriki wa askari wanawake   katika Operesheni za Ulinzi wa Amani za  Umoja wa Mataifa,  ni baadhi ya  mafanikio ambayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inajivunia miaka 20 baada ya Mkutano wa Kihistoria wa wanawake uliofanyika Beijing, China mwaka 1995.

  Waziri wa  Maendeleo ya Jamii, Jinsia na  Watoto, Mhe. Sophia Simba ( Mb) ameyasema hayo  leo ( alhamis) wakati alipokuwa akitoa tathmini na changamoto za utekelezaji wa  maazimio muhimu yaliyofikiwa katika mkutano huo wa  wanawake Beijing. 

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mhe. Bernard Membe akiongoza Mkutano wa 45 wa Kikundi Kazi cha Mawaziri wa Jumuiya ya Madola, (Commonwealth Ministerial Action Group-CMAG) unaofanyika Mjini London, Uingereza tarehe 11 na 12 Machi, 2015. Waziri Membe ni Mwenyekiti wa Kikundi Kazi hicho ambaye aliteuliwa wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola uliofanyika nchini Sri Lanka mwaka 2013. Kushoto kwa Waziri Membe ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Bw. Kamalesh Sharma.


  0 0

  Wimbo “Najivunia” umetungwa na kurekodiwa Maryland, USA na kundi la wasanii wa Kitanzania waishio Marekani kwa ushirikiano na DMK Global Promotions. To be released on March 15th
  Wasanii wenyewe ni:
  DMV All Stars:
  Mr.Tz aka SanTz 
  Prince Herry
  Domi
  E-Breezy (Ibra. Max)
  AJ Ubao

  0 0

  Timu ya Vijimambo ikishiriana na Kwanza Production inapenda kwanza kutoa pongezi kwa Watanzania Houston kwa jitihada zao za kupambana na mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi Pia inaandaa kipindi cha video kuongelea hili swala kwa mapana zaidi na kuangalia jinsi gani ya kukomesha mauaji haya ambayo yanaleta fedheha na aibu  ikiwemo ukiukaji wa haki za binadamu.

  Kipindi kitarekodiwa siku ya Jumampili saa 8 mchana (2pm) mahali ni Extended Stay America chumba namba 224 anuani ni 2424 West Sam Houston Prkway, Houston, TX 77042. 

  Wadau kutoka New York katika moja ya vipindi vilivyorekodiwa.

  Wadau wa North Carolina wakiwa kwenye kipindi kilichopata kurekodiwa.

  Kwa maelezo zaidi wasiana na 301 335 6383 asante

  Ujumbe kutoka kwa ndugu zetu hapo chini.

  0 0

  DSC_0576
  Msimamizi wa mradi wa FAO kijiji cha Kiroka mkoani Morogoro, Ajuaye Sigalla, akitoa muhtasari wa maendeleo ya mradi FAO unaotekelezwa na wanakikundi wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI) mbele ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi walipofanya ziara ya kugagua miradi yao ya maendeleo mkoani Morogoro.(Picha na Zainul Mzige)

  Na Mwandishi wetu, Morogoro
  BALOZI wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi ametembelea skimu ya umwagiliaji ya Kiroka na kusema kwamba atahakikisha kwamba kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwamo serikali wataendelea kusaidia wananchi kujiinua kiuchumi.

  Akiwa katika skimu hiyo inayosaidiwa na Shirika la Chakula duniani (FAO) ametaka miradi ya maendeleo nchini kutowaacha nyuma wanawake na watoto kwani wao ndio msingi wa maendeleo ya kijamii kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa.

  Balozi huyo ambaye anatarajiwa kurejea Ulaya mwaka huu baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini amesema kwamba kuwapo kwa asilimia 60 ya wafaidika na mradi huo wa Mpunga kuwa wanawake kumesaidia sana kuamsha maendeleo ambayo yanatakiwa kuendelea kusimamiwa.

  "Wanawake wamefanikiwa kupeleka watoto wao shuleni. kuwapatia chakula kinachostahiki na kupata kipato na katika hili ni vyema wasiachwe nyuma kimaendeleo" alisema balozi huyo.
  DSC_0633
  Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi akizungumza na wanakikundi wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI) wanaofadhiliwa na FAO wakati wa ziara ya kutembelea miradi inayofadhiliwa na wadau wa maendeleo ambapo mradi wa Kiroka unafadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la FAO huku mradi wa makazi mapya kwa waathirika wa mafuriko Kilosa ukifadhiwa na Ubalozi wa Umoja wa Ulaya. Kushoto kwake ni Msimamizi wa mradi wa FAO kijiji cha Kiroka mkoani Morogoro, Ajuaye Sigalla.


  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi Mteule wa Japan Nchini Tanzania, Mhe. mashiro Yoshida kwenye Hoteli ya New Otani jijini Tokyo Machi 13, 2015 ambako Machi 14, 2015 anatarajiwa kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Mkutano Kuhusu namna ya kukabiana na maafa utakaofanyika Sendai.Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar,Mohamed Aboud Mohamed.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Ujumbe wake wakizungumza na Balozi Mteule wa Japan Nchini Tanzania, Mhe. Masahiro Yoshida kwenye Hoteli ya New Otani jijini Tokyo Japan Machi 13, 2015 ambako Machi 14, 2015 anatarajiwa kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Mkutano Kuhusu namna ya kukabiliana na maafa utakaofanyika Sendai.


  0 0

  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na wageni waliofika ofisini kwake kumjulisha kuhusu Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute litakalofanyika nchini Tanzania na kuhusisha nchi 18 tarehe 21 na 22 Machi mwaka huu. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, wakwanza kulia ni Bw. Ramadhani Madabida na anayefuata ni Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz.
  Bw. Ramadhani Madabida (kulia) akifafanua jambo walipokutana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara wakwanza kushoto kumpa taarifa ya Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute litakalofanyika nchini Tanzania tarehe 21 na 22 Machi mwaka huu na kuhusisha nchi 18. katikati ni Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz.
  Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz (wapili kulia) akielezea jinsi walivyojiandaa kufanikisha Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni litakalohusisha nchi 18 walipokutana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (wapili kushoto). Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, na kulia ni Bw. Ramadhani Madabida.

  0 0
 • 03/13/15--00:58: IN LOVING MEMORY
 • Heaven gained a beautiful angel on 13th March 2013, It’s been two years today bibi since you were suddenly called by the lord.

  Our hearts still bleed, but our love for you grows more with time.   
     
  Your memories remain fresh in our hearts and the love we still have for you no money could buy..
  You are fondly remembered by your kids, sisters, brothers, relatives, friends and grandkids. We will always remember you.

  A memorial mass is to be held at Kijitonyama Pentecostal Church on 15th March 2015 at 1030 hrs

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mkuu wa Misri, Ebrahim Mehlep, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Sharm El- Sheikh, kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa kuhusu maendeleo na Uchumi wa nchini Misri.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Misri, Ebrahim Mehlep, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Sharm El- Sheikh, jana kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa kuhusu maendeleo na Uchumi wa nchini Misri. Picha na OMR

  0 0

   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini (TBA), Arch. Elius Mwakalinga, akisoma taarifa ya mkutano wa Mameneja mikoa wa TBA nchini uliofanyika jijini Dar es salaam, katikati kulia ni Waziri wa Ujenzi  Dkt. John Magufuli, akisikiliza kwa makini taarifa hiyo.

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe (kulia), akifafanua jambo katika mkutano wa Mameneja wa mikoa wa TBA nchini, katikati ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli, (kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi wa TBA Dkt. Edward Ngwale.
   
   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (katikati), akitoa maelekezo kwa Mameneja wa mikoa wa TBA nchini waliohudhuria mkutano huo uliofanyika jijini Dar es salaam, Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TBA Dkt. Edward Ngwale.

   Baadhi ya Mameneja wa mikoa mbalimbali wa TBA nchini waliohudhuria mkutano huo, wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (hayupo pichani).

  Baadhi ya Mameneja mikoa wa TBA wakiangalia jengo la Ghorofa nane ambalo litakuwa na uwezo wa kuishi familia 16 katika eneo la Sida-Ada Estate jijini Dar es salaam


older | 1 | .... | 766 | 767 | (Page 768) | 769 | 770 | .... | 3272 | newer