Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 760 | 761 | (Page 762) | 763 | 764 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

   Imeelezwa kuwa nchi ya Afrika Kusini katika bara la Afrika ndio inayoongoza kwa kuwa na njia nyingi za usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya Cocaine na Heroine .

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Afisa Habari wa Kituo Cha Habari wa Umoja wa Mataifa (UNIC),Stella Vuzo alisema kuwa hilo limetokana na ripoti ya Bodi ya Kupambana na Dawa za Kulevya ya Umoja wa Mataifa imeweka mkazo katika kwa nchi mwanachama kuweka mikakati katika kupambana na dawa za kulevya.

  Alisema alisema nchi zilizo katika pwani za bahari zinatakiwa kuwa na uangalizi katika maeneo hayo kutokana na watu wanatumia njia hizo katika kupitisha dawa za kulevya.

  Naye Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Komputa wa Tume ya kudhibiti  Ukimwi DCC,January Ntisi ,amesema wanashirikiana katika kupambana na dawa za kulevya kutokana na maambukizi yake yanatokana na utumiaji wa dawa.

  Alisema mwaka jana walikamata dawa tani 2.3 ambazo zingeingia nchini kungekuwa na kundi kubwa ambao wanatumia dawa hizo.
  Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Komputa wa Tume ya Taifa ya kudhibiti  Ukimwi (DCC),January Ntisi akizindua kitabu cha ripoti ya Bodi ya Kupambana na Dawa za Kulevya ya Umoja wa Mataifa,uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa idara ya habari- Maelezo,jijini Dar es salaam.Kushoni ni Afisa Mipango wa Umoja wa Mataifa,Immaculata Malyamkono-Nyoni na katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Kupambana na Watumiaji wa Madawa ya Kulevya,Very Kunambi.Picha na Emmanuel Massaka.

  0 0

  Kaimu Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa wa Airtel Bwana David Wankuru akimkabithi gari aina ya Toyota IST bwana Kijiji Gweso ambaye ni Mvuvi na mkazi wa wilaya ya Sengerema Mwanza mara baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi akishuhudia ni Afisa Uhusiano wa Airtel,Bi. Jane Matinde.
  Mshindi wa gari kupitia promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Bwana Kijiji Gweso akifungua gari mara baada ya kukabidhiwa gari na Airtel mara baada ya kuibuka mshindi, Bwana Gweso ni Mvuvi na mkazi wa wilaya ya Sengerema Mwanza. akishuhudia ni Kaimu Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa wa Airtel David Wankuru.
  Mshindi wa gari kupitia promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Bwana Kijiji Gweso akiwa ndani ya gari yake mara baada ya kukabidhiwa gari na Airtel mara baada ya kuibuka mshindi, Bwana Gweso ni Mvuvi na mkazi wa wilaya ya Sengerema Mwanza.


  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama (kulia) akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusiana na maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 5, 2015. (Picha na Francis Dande)

  Na Mwandishi Wetu
  MWIMBAJI wa nyimbo za injili kutoka Zambia, Ephraem Sekereti yu miongoni mwa nyota wa kimataifa watakaopamba Tamasha la Kimataifa la Pasaka litakaloanzia Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam hapo April 5, kabla ya kuhamia mikoani.
  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo linalofanyika chini ya uratibu wa kampnuni ya Msama Promotions, Alex Msama, Sekereti anakuwa mwimbaji wa kwanza wa kimataifa kuthibitisha ushiriki. 
  Alisema mbali ya Sekereti ambaye mara kadhaa aliwahi kushiriki tamasha hilo na kuwa baraka kwa wapendwa na wadau wa Tamasha hilo, tayari ameanza maandalizi ya nguvu ili kuwa fiti katika tamasha hilo ambalo litabeba pia maadhimisho ya miaka 15.
  “Kwa upande wa waimbaji wa kimataifa, safari hii watakuwa wengi zaidi kutokana na ukubwa wa tukio lenyewe. Lakini hadi sasa Sekereti ndie wa kwanza kuthibitisha, wengine mazungumzo yanaendelea,” alisema Msama.
  Kwa upande wa waimbaji wazawa, Msama alisema nao wameongezeka na kufikia wawili kwani mbali ya Upendo Nkone aliyethibitishwa wiki iliyopita, mwingine ni Jesca Honoli na kusema wengine watazidi kujulikana kwa siku za usoni.
  Katika hatua nyingine, Msama alisema kwa vile ni tamasha linalokwenda na maadhimiosho ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000, makundi maalumu katika jamii kama walemavu, yatima na wajane watashiriki katika kufurahia tukio ambalo ni faraja kwao.
  “Tamasha la Pasaka limekuwa pia baraka kwa makundi maalumu katika jamii kama walemavu, yatima na wajane, katika kuadhimisha miaka 15, makundi hayo yatakuwa na wawakilishi ili kuleta maana kamili ya nafasi yao katika tukio hilo la kimataifa,” alisema.
  Kuhusu mikoa ambayo itafikiwa na tamasha la mwaka huu, Msama alisema suala hilo bado linafanyiwa kazi na kamati yake kutokana na wingi wa maombio yaliyowafikia hadi sasa kwani ni mingi kuliko walivyotarajia kiasi cha kuipa kamati yake kazi ya ziada.

  0 0

  Na Geofrey Tengeneza - Berlin 
  Maonesho ya Utalii ya kimataifa ya ITB ya siku tano yameanza leo jijini Berlin. Maonesho haya yanayofanyika kila mwaka na ambayo ni makubwa kuliko yote duniani yanahudhuriwa na waoneshajio zaidi ya 10000 kutoka nchi 190 duniani. Tanzania katika maonesho haya inawakilishwa na waoneshaji 160 kutoka katika makampuni 60 kutoka sekta ya umma na binafsi . 
  Taasisi za serikali zinazoshiriki maonesho haya ni Idara ya Utalii ya Wizara ya Maliaslili na Utalii, Bodi ya utalii Tanzania (TTB) ambao ndio waratibu wa ushiriki wa Tanzania katika maonesho haya. 
  Nyingine ni Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Shirika la hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya hifadhi ya ya Bonde la Ngorongoro (NCAA), Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na Jumuia ya Afrika Mashariki. 
  Kwa mujibu wa Geofrey Meena Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania idadi ya makampuni na taaisi yanayoshiriki kutoka Tanzania katika onesho la ITB imekuwa ikiongezeka kila mwaka ambapo mwaka huu washiriki ni sitini (60) wakati mwaka jana jumla ya makampuni yalikuwa hamsini na tatu (53). Miongoni mwa matukio muhimu yanayotarajiwa ni pamoja na tukio la siku ya Jumuia ya Afrika Mashariki katika maonesho haya litakayofanyika tarehe 6/2/2015 ambapo Tanzania kama mwenyekiti wa jumuia hiyo itakuwa mwenyeji wa tukio hilo litafanyika katika banda la Tanzania. 
  Mawaziri wa Utalii kutoka nchi wanachama, mabalozi wa nchi hizo hapa Ujerumani na wageni wengine mbalimbali waalikwa wanatarajiwa kujumuika na mwenyeji wao Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu katika hafla hiyo katika banda la Tanzania.
    Waoneshaji kutoka Tanzania wakiwa katika mazungumzo ya Kibiashara na wenzao kutoka nchi mbalimbali katika sikuu ya kwanza ya maonesho ya ITB jijini Berlin Ujerumani.
  Waoneshaji kutoka taasisi za umma wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mweneshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi (wa tatu kulia) na Meneja Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena (wa Kwanza kulia) wakiwa katika kaunta ya banda la Tanzania katika maonesho ya ITB Ujerumani.

  Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mh. Philip Marmo (wa nne toka kulia)  katika picha ya pamoja na mabalozi wenzake wanaowakilisha nchi za jumuia ya Afrika Mashariki nchini Ujerumani sambamba na maafisa kutoka Bodi ya Utalii Tanzania na Jumuia ya Afrika Mashariki muda mfupi baada ya kumaliza kikao cha pamoja kujadili imaandalizi ya ‘siku ya jumuia ya Afrika Mashariki’ katika maonesho ya ITB itakayo fanyika tarehe 6/2/2015.


  0 0  0 0
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikatiza kwenye moja ya mtaro alipokwenda kukagua na kushiriki kulima katika shamba la mkulima bora wa mwaka 2014,Bi.Anna Mlewa katika kijiji cha Berege,wilaya ya Mpwapwa. Kinana ameanza ziara ya siku 9 mkoani Dodoma ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua,kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010 pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
   Pichani Kati ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameongoza na Mkulima bora wa mwaka 2014,Bi.Anna Mlewa na Mumewe pichani kulia,ambapo Ndugu Kinana alikwenda kukagua na kushiriki kulima katika shamba la mkulima huyo katika kijiji cha Berege,wilaya ya Mpwapwa.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (wa tatu kushoto) akishiriki kulima shamba la karanga la Mkulima bora wa mwaka 2014 mkoa wa Dodoma,Bi.Anna Mlewaka katika kijiji cha Berege Wilayni Mpwapwa mkoani Dodoma.Mkulima huyo alieleza mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuwa 2012/13 alifanikiwa kulima ekari 30 na kuzalisha kiasi cha gunia 300 za mtama,mnamo mwaka 2014 alihamasika kuongeza eneo kufikia ekari 130 ambazo alizalisha gunia 650.Mkulima huyo alisema kuwa mpaka sasa amefanikiwa kununua power tiller 1,ameanzisha biashara ya duka na mashine ya kusaga,anasomesha watoto shule ya msingi,sekondari na chuo
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa Mpwapwa mapema leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mashujaa mjini Mpwapwa.Kinana ameanza ziara ya siku 9 mkoani Dodoma ya Kuiarisha uhai wa chama,kukagua,kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010 pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
  Wakazi wa Mpwapwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mapema leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa mjini Mpwapwa.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi-Taifa,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Mpwapwa mapema leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mashujaa mjini Mpwapwa mkoani Dodoma.
   Baadhi ya Wananchi na wanachama wa CCM,wakishangilia jambo walipokuwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia kwenye uwanja wa Mashujaa,wilayani Mpwapwa leo jioni .

  PICHA NA MICHUZI JR-MPWAPWA

  0 0

  Mkurugenzi na mmiliki wa kampuni urban and rular engineering ndugu Awadh Zuberi ,pamoja na wasaidizi wake walipomtembelea balozi mstaafu Mustafa nyang'anyi nyumbani kwake Washington, kuanzia kushoto ni Awadh Zuberi, Shemuni Halahala,Balozi Nyang'anyi, Zuberi Athumani.

  0 0

  Angelina Mziray Katibu Mkuu wa Women and Poverty alleviation in Tanzania  , Akiwakaribisha wageni Mbalimbali waliofika katika Sherehe za Kuazimisha Siku ya Wanawake Duniani ambapo wao wameadhimisha mapema,Katika Ufunguzi Alisema kuwa Shirika lisilo ka Kiserikali la Waupata wakishirikiana na OXFAM wamesaidia Kijiji hicho katika kuleta maendeleo mbalimbali Tangu mwaka 2006 ikiwa ni pamoja na Kilimo cha mpunga, Matumizi Bora ya Ardhi, Ambapo Pia aliwashukuru OXFAM kwa kuleta ufugaji bora wa kuku wa kienyeji, na ujenzi wa masoko mawili ya kisasa, Pia kusaidia wanawake kupata hati milili za Ardhi ambapo wanawake 186 watapata Hati hizo. Mwisho alishukuru taasisi zengine zisizo za Kiserikali ikiwemo Mviwata,Ungo,Tupawaki pamoja na Mwayodeo kwa jitihada zao za kusaidia wanawake na wanakijiji cha Gongoni katika maendeleo ya kijiji hicho.
   Mmoja wa Mashuhuda Juliana Bi. Salum ambaye amepata haki Miliki ya Ardhi akielezea Jinsi gani ambavyo itamsaidia katika Maendeleo yake na jamii kwa ujumla.
  Mshereheshaji MC Chadieli G. Senzighe akiendelea kutoa Mwongozo katika Sherehe hizo.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lenye dhamana ya kufufua, kukuza na kuendeleza Sanaa kwa kushirikiana na taasisi ya Ako’mungoma Poverty Alleviation Organization (APAO) linaendesha programu ya wiki tatu ya Sanaa kwa watoto katika Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam. 

  Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Utamaduni ya mwaka 1997 sura ya 9.6.16 Baraza linaelekezwa kushirikiana na wadau katika kuendesha matukio mbalimbali ya sanaa  kama programu hii ya watoto. 

  Programu hii ya Sanaa kwa watoto ambayo kilele chake kitakuwa tarehe 07/03/2015 na kuhusisha  maonesho, inatarajia kushirikisha watoto 215 ambapo 100 wanaishi katika mazingira magumu eneo la Mbutu - Kigamboni na wengine 100 kutoka shule za Msingi Gomvu na Mbutu. Aidha, watakuwepo wanafunzi waalikwa 15 kutoka shule ya msingi Msimbazi iliyopo wilaya ya Ilala. 

  Programu hii ambayo mwaka huu inadhaminiwa na Kampuni ya Mohamed Enterprises na Haakneel production (T) Ltd inalenga kukuza vipaji vya watoto katika fani za uchoraji, maigizo hususan majigambo na ngoma za asili. Pia tunatarajia udhamini toka wadau na makampuni mengine. 

  Kilele cha programu hii yenye kauli mbiu ya “Amani na Uchaguzi 2015” kitapambwa na burudani ikiwemo mpira wa miguu kutoka kwa watoto wa Kituo cha APAO na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka jimbo la Kigamboni Mheshimiwa Faustine Ndugulile.

  Aidha programu hii ni mwendelezo wa programu ya Sanaa kwa watoto ya Baraza iliyoanza tangu miaka ya 80 ambayo ilipata kuibua na kukuza vipaji vya wasanii kama Mrisho Mpoto na Masoud Kipanya ambao hadi sasa wanafanya vizuri. 

  Kwa mwaka 2014 programu hii iliendeshwa katika wilaya ya Ilala kwa kushirikisha shule tano (5) ikiwemo ya Buguruni Viziwi na ilidhaminiwa na kampuni ya Msama Promotion. 

  Baraza linachukua fursa hii kuwaalika wananchi na wadau wote wa sanaa kufika kwa wingi kushuhudia vipaji vya sanaa walivyonavyo watoto.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard K. Membe (Mb.) akifanya mazungumzo na Balozi wa Oman hapa nchini, Mhe. Saoud Al Ruqaishi alimpomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kuzungumzia masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Oman.
  Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (kushoto) akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bi. Mindi Kasiga (kulia) pamoja na Bi. Asha Mkuja, Afisa Mambo ya Nje.
  Mazungumzo yakiendelea
  Picha na Reginald Philip

  0 0

  Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Stephen Masatu Wasira amefanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe Mark Childress ofisini kwake.

  Mhe Wasira katika mazungumzo yake na Balozi Childdress alibainisha changamoto zinazokabili kilimo nchini kuwa ni pamoja na zana duni zinazotumiwa na wakulima wadogo katika kilimo kuwa ni jembe la mkono. Alisema kwa kutumia jembe la mkono itakuwa ni ngumu kuondoa umaskini kwa wakulima wadogo katika maeneo ya vijijini.

  Aliongeza kuwa jembe la mkono hutumiwa wakulima wengi wa vijijini katika uzalishaji wa mazao katika Taifa letu. ’’ Wakulima wadogo ndio tegemeo kubwa katika kuzalisha kilimo hapa nchini karibu asilimia 90 ya chakula hapa nchini inazalishwa na wakulima wadogo” alifahamisha Mhe Wasira katika mazungumzo yake.

  Soko nalo ni tatizo lingine linalokabili mazao ya wakulima wetu wadogo waishio vijijini, alitoa mfano wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini katika mikoa ya Mbeya na Iringa ambako kuna mazao mengi na hasa mahindi ambayo yamekosa soko.

  Pia ameiomba serikali ya Marekani kusaidia kuwekeza zaidi katika viwanda vya kilimo ili kuongeza thamani ya mazao ya wakulima wetu ili waweze kufaidika na juhudi zao na mwishowe waondokane na umasikini Uwekezaji katika viwanda vya kilimo utasaidia kuepukana na tabia ya kusafirisha malighafi na hivyo kutaongeza thamani ya mazao ya wakulima wetu, aliongeza Mhe Wasira.

  Aidha, kitu kingine kilichosisitizwa na Mhe Wasira ni mkakati wa serikali kuwashirikisha vijana katika kilimo ili kuondokana na tabia ya sasa kwa vijana kukimbilia mjini na hasa Jijini Dar es Salaam kutafuta kile wanachokiita na kuamini kuwa maisha bora hupatikana mjini.

  “ Kilimo cha Bustani ni muhimu kwani kinaweza kuwasaidia vijana kupata kipato cha haraka kwa kuwa mazao ya aina ya bustani huchukua muda mfupi kupata mafao yake, “ aliongeza Mhe Wasira.

  Mhe. Wasira pia alisema serikali imejipanga kuhakikisha kuwa inaboresha kilimo cha umwagiliaji na akaiomba serikali ya Marekani kusaidia katika hili kwani itaongeza uzalishaji kwa wakulima wadogo kwa kuwa watazalisha mara mbili kwa msimu mmoja wa kilimo.

  Wakulima wanasafirisha mazao ghafi nje ya nchi kama korosho bila kuongezwa thamani yake na hivi kuwakosesha kupata faida kubwa katika mazao yao. Naye Mhe Childress aliahidi kuwa serikali ya Marekani itafanyakazi na serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa inasaidia kilimo hapa nchini.

  0 0


  0 0

   Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Ayoob Omary akizindua vilabu vya wanafunzi vya Sumatra. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Oscar Kikoyo na kulia ni Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatan.
   Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Oscar Kikoyo akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
   Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano akizungumza.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nchi za Nje,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Mh. Dianna Melrose aliyefika ofisini kwake leo kwa mazungumzo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nchi za Nje,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Mh. Dianna Melrose ofisini kwake,jijini Dar es salaam leo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nchi za Nje,Mh. Edward Lowassa akiagana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Mh. Dianna Melrose mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

  0 0

  Katibu wa Mbunge wa Viti Maalum, Al Sheimar Kweigyir (Semeni Kingaru) mwenye shati la mikono mirefu, akiwa kwenye mazishi ya mama yake mzazi Bi Kibibi Haji Pembe, aliyezikwa Machi 3, kijiji cha Misugusugu, Kibaha, mkoani Pwani.

  "Nashukuru Watanzania wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kufanikisha msiba na mazishi ya mama yetu kwa kutufanyia mambo mengi yenye kuleta ushirikiano kwa jamii kwa rambimbari zilizoonyesha kuguswa na msiba huu. Familia haina cha kuwalipa, isipokuwa kwa Mungu pekee.


  0 0

  Naibu Waziri wa Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kassim Majaliwa (katikati) pamoja ya Wakuu wa Shule za Sekondari za Serikali na Binafsi- walioshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo yanayoratibiwa na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu nchini ‘ADEM’ wilayani Bagamoyo, jana.
  Wakuu wa shule wakifuatilia nasaha za -Naibu Waziri wa Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kassim Majaliwa, wakati akifunga mafunzo ya uongozi na usimamizi wa shule wilayani Bagamoyo jana.
  Naibu Waziri wa Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kassim Majaliwa, akizungumza na wakuu wa shule za sekondari za Serikali na Binafsi- kitaifa wilayani Bagamoyo, walioshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo yanayoratibiwa na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu nchini ‘ADEM’ kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa ADEM, Dk. Siston Masanja Mgullah.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Kamishina Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya, wakati walipokutana baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Burn Ltd, Malaczynski Burn, baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015.


  0 0

  Southern Sun Hotel Sales Manager, Punim Kanabar (2nd L) speaking to journalists on her hotel sponsorship towards this year Dar Charity Goat Races scheduled for May 30th this year in Dar es Salaam. It was during a press launch in Dar es Salaam today. From left are, Kilimanjaro Premium Lager Brand Manager, Pamela Kikuli (sponsors), Regent Tanzania General Manager, Ryan O’Sullivan (sponsors) and Dar Charity Goat Races Chair, Karen Stanley.
  Dar Charity Goat Races Chair, Karen Stanley (4th L) addressing a media conference during a function to launch the 2015 charity goat races scheduled for 30th May in Dar es Salaam. A brief occasion was held in Dar es Salaam yesterday. Looking on are representatives from companies sponsors a charity event.

  0 0

  Na Grace Michael, Tabora

  WAGONJWA waliofika na kupata huduma za Madaktari Bingwa ambao wapo kwenye mpango unaoendeshwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wamefurahia huduma hizo na kusema kwamba zimeokoa fedha nyingi ambazo wangetakiwa kuzitumia kusafiri kufuata huduma hizo.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika Hospitali ya Mkoa wa Tabora, Kitete, walisema kwamba ujio wa Madaktari hao umewasaidia kupata huduma nzuri na zinazohitajika bila ya usumbufu wa aina yoyote na wala kutumia gharama kubwa.

  “Kwa upande wangu nashukuru mno kwani nilifika hapa nikiwa na hali mbaya sana, nilikuwa siwezi hata kula wala kutembea, lakini nipofika na kuonwa na daktari Bingwa na kunipa huduma nina nafuu kubwa mno kwani naweza kula na kuzungumza vizuri,” alisema Bw. Shukuru Jumanne (33) Mkazi wa Ipuli mkoani Tabora.

  Mgonjwa huyo alipata huduma ya kutolewa maji kwenye kuta za moyo ambayo yalikuwa yakimsabishia maumivu makali na kushindwa kupumua vizuri. Mgonjwa mwingine ambaye naye alipata huduma hiyo, Bi. Halima Juma (49) mkazi wa Ipuli, Tabora alisema kuwa ana faraja kubwa baada ya kupata huduma ya kutolewa maji ambapo sasa anaweza kupumua vizuri ikilinganishwa na mwanzo.

  “Sikuwa na uwezo wa kufuata huduma hizi mbali hivyo ujio wa hawa wataalam kwangu ni kama muujiza, namshukuru sana Mungu kwa kuwaonesha NHIF mpango kama huu,” alisema Bi. Halima.

  Mbali na wagonjwa hawa, pia ndugu wa wagonjwa ambao walikuwa na ndugu zao wakiwa kwenye chumba cha upasuaji, waliupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kuona umuhimu wa kuleta wataalam hao mkoani Tabora. Walisema kuwa huduma kama za upasuaji na huduma zingine ambazo walitakiwa kuzifuata Muhimbili au Bugando wamezipata hospitalini hapa bila ya usumbufu wowote.

  Wamesema kuwa kitendo cha madaktari bingwa kuja mkoani hapo kimewapunguzia gharama ambazo wangetakiwa kuzitumia, hivyo wameuomba Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuendelea na utaratibu huo ili kukomboa maisha ya Watanzania wengi wanaoishi katika mikoa ya pembezoni.

  Mpaka sasa jumla ya wagonjwa…..wameonwa na Madaktari Bingwa huku wagonjwa ……wamefanyiwa upasuaji tangu zoezi hili lilipoanza siku ya Jumatatu.
  Wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakihakikiwa nyaraka zao kabla ya kuingia kupata huduma za Madaktari Bingwa.
  Wahitaji wa huduma za kitaalam wakisubiri kuwaona madaktari bingwa.


  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Masuala ya Kimataifa wa Chama cha Wafanyabiashara cha Luxembourg Bwana Jean Claude Vesque. Bwana Claude alimtembelea Balozi Kamala leo ofisini kwake Brussels. Kushoto ni Bwana Jofrey Kabakaki afisa wa masuala ya uchumi Ubalozi wa Tanzania Ubeligi.

older | 1 | .... | 760 | 761 | (Page 762) | 763 | 764 | .... | 3348 | newer