Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 756 | 757 | (Page 758) | 759 | 760 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb) akizundua kampeni ya Mpe riziki si matusi yenye lengo la kuondoa lugha chafu na matusi kwa wanawake wa sokoni na wanaofanya shughuli zao katika sekta zisizo rasmi. Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Belinda Jijini Dar es salaam tarehe 27 Februari 2015.
  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Dkt. Pindi Chana akizungumza mara baada ya kuzindua kampeni ya Mpe riziki si matusi yenye lengo la kuondoa lugha chafu na matusi kwa wanawake wa sokoni na wanaofanya shughuli zao katika sekta zisizo rasmi.
  Baadhi ya wanawake kutoka masoko mbalimbali ya Jijini Dar es salaam wakiwa katika uzinduzi huo.
  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb) (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Mradi huo (mwenye suti Nyeupe) Bibi. Jane Magigita na baadhi ya wanawake kutoka masoko mbalimbali ya Jijini Dar es salaam baada ya uzinduzi huo.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko mkubwa na huzuni nyingi taarifa za kifo cha ghafla cha Mheshimiwa Kepteni John Damian Komba, Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM na msanii hodari sana wa kizazi chake.

  Katika salamu zake za rambirambi kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda na Katibu Mkuu wa CCM, MheshimiwaAbdulrahman Kinana, Mheshimiwa Kikwete amesema: “Nimepokea kwa mshtuko mkubwa na huzuni nyingi taarifa za kifo cha ghafla cha Mheshimiwa Kepteni John Komba, ambacho nimejulishwa kuwa kimetokea mchana wa leo, Jumamosi, Februari 28, 2015, kwenye Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam.”

  “Kwa hakika, sina maneno ya kutosha kuelezea kwa fasaha hasara ambayo taifa letu na chama chetu kimepata kutokana na kifo cha Kepteni Komba. Taifa letu limepoteza hazina kubwa na mtu muhimu. Nimejua Kepteni Komba kwa muda mrefu sana, nimefanya naye kazi. Alikuwa msanii ambaye kiwango chake cha usanii kilikuwa hakipimiki, alikuwa na sifa kubwa za uongozi, alikuwa mpenzi, mzalendo na mtu mwaminifu sana kwa taifa lake na katika jambo lolote aliloliamini.,” 
  amesema Rais Kikwete katika salamu hizo na kuongeza:

  “Akiwa mwalimu, lakini hasa akiwa Mlinzi wa Taifa katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kepteni Komba alithibitisha sifa zake kama mlinzi wa taifa kwa kipaji chake cha kutunga na kuimba nyingi za kuhamamisha wanajeshi wetu katika ulinzi wa nchi yao. Alikuwa na uwezo mkubwa wa kisanii kutunga nyimbo za aina zote – ziwe za maombolezo, ziwe za kutoa hamasa, ziwe za makaribisho, ziwe za kampeni za kisiasa na kijamii ama ziwe za kampeni maalum.”

  “ Mheshimiwa Komba alikuwa Mbunge hodari sana na wananchi wa Nyasa wamepoteza mtetezi wa uhakika. Mheshimiwa Komba alikuwa mcheshi, aliyependa sana utani na alikuwa na uongozi mkubwa wa kutambua na kulea vipaji vya sanaa na wasanii kama alivyothibitisha katika kuanzisha na kulea Kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT) na kabla ya hapo .”

  “Kupitia kwenu Waheshimiwa, naomba mnifikishie salamu zangu za dhati kabisa kwa Wabunge wote ambao wameondokewa na mwenzao na wananchi wa Jimbo la Nyasa na Mkoa wote wa Ruvuma ambao wamepoteza mwakilishi na kiongozi wao. Ndani ya Chama chetu, naomba salamu zangu ziwafikie wanachama wetu wote kwa kupoteza mwanachama mwenzao, ziwafikie viongozi na hasa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ambayo imepoteza mwakilishi mwenzao na wasanii wote wa Tanzania One Theatre (TOT) ambao Kiongozi wao ameondoka duniani,” amesema Rais na kumalizia:

  Naungana na wanafamilia kuomboleza kifo cha rafiki yetu, ndugu yetu na kiongozi mwenzetu. Napenda wanafamilia wajue kuwa natambua uchungu wao katika kipindi hiki na tahayari yao ya  kuondokewa na mhimili wa familia. Niko nao katika maombolezo na katika kumwomba Mwenyeji Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Kepteni John Damian Komba. Amen.”


  0 0

  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akifunua kitambaa kwenye jiwe la msingi kuashilia uzinduzi rasmi wa "Duty Free Shop" ya Magereza Mkoani Tabora leo februari 28, 2015. Kamishna Jenerali Minja amesema kuwa Huduma hiyo itatolewa pia kwa Maafisa na Askari wa Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama Mkoani Tabora(kulia) ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Transit Military Shop, Bw. Sadrudin Virji.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akiangalia bidhaa mbalimbali zinazouzwa katika "Duty Free Shop" ya Magereza Mkoani Tabora mara tu baada ya uzinduzi rasmi leo februari 28, 2015 katika Viwanja vya Gereza Kuu Uyui, Tabora.


  0 0

  Hayati John Komba enzi za uhai wake
  Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kepteni John Komba amefariki dunia jioni hii katika hospitali ya TMJ jijini Dar es salaam, mtoto wa Marehemu Bw. Herman Komba amethibitisha.

  0 0

  Muonekano wa Daraja jipya la Salenda litaakalopita baharini kuanzia Coco Beachi (Oysterbay) kwenda Hospitali ya Aga Khan (Maeneo ya Ocean Road/ Baraka Obama Road). Daraja hilo pamoja na barabara zake, litakuwa na urefu wa kilomita 7.2 na uwezo wa kupitisha magari zaidi ya 61,000 kwa siku huku likiwa na njia nne za magari pamoja service road njia za waenda kwa miguu kila upande
  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kulia akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Chung Il wapili kushoto kuhusiana na mambo mbalimbali kuhusu sekta ya Ujenzi pamoja na mchakato wa Ujenzi wa Daraja jipya la Salenda litakalopita baharini. Wa kwanza kushoto ni mke wa Balozi huyo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe kushoto akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Korea Chung Il kulia. Katikati ni Eng. Consolata Ngimbwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi nchini (CRB).


  0 0

  Waziri mkuu, Mizengo Pinda akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mkwajuni wilayani Chunya akiwa katika ziara ya wailaya ya Chunya Februari 28, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo PInda akizungumza na wananchi wa mji mdogo wa Makongorosi Chunya waliofunga njia na akalazimika kuzungumza nao akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya Februari 28, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameendelea kukemea tabia za utoro na mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Chunya baada ya kupewa taarifa kwamba watoto 4,420 walitoroka shule na wengine 201 kupata mimba.

  Februari 26, mwaka huu, Waziri Mkuu aliwaagiza Mkuu wa Wilaya ya Kyela pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuwasaka na kuwakamata wale wote waliohusika na utoro na ujauzito wanafunzi na kuwafikisha mahakamani mara moja ili liwe fundisho kwa wengine baada ya kuelezwa kwamba wanafunzi 94 walipata ujauzito na wengine 645 kuacha shule kwa sababu ya utoro.

  Akizungumza na maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana (Jumamosi, Februari 28, 2015) kwenye uwanja wa Saba Saba wilayani Chunya, Waziri Mkuu alisema haiwezekani kuiacha hali hiyo iendelee huku watoto wa wilaya hiyo wakiharibiwa maisha kwa kukosa masomo.

  “Utoro kwenye shule za msingi, taarifa ya wilaya inaonyesha watoto 1,979 waliacha shule kati ya mwaka 2010 na 2014 ambao ni wastani wa watoto 395 kila mwaka na katika suala la mimba, taarifa hiyo inasema watoto 161 waliachishwa shule kwa sababu ya ujauzito,” alisema.

  “Haiwezekani kabisa! Hivi akinababa kuamua kutembea na mtoto shule ya msingi ni lipi hasa unalolitaka kwake… unamwachisha shule mtoto kwa lipi hasa, hapana. Nimeshatoa agizo wahusika wakamatwe. Wa zamani tunaweza tusiwapate, lakini hawa wa mwaka jana kwa shule za msingi wako 28, RC na watendaji wako fuatilieni na muwapeleke kwenye vyombo vya sheria,” alisisitiza.

  Akichanganua takwimu za sekondari, Waziri Mkuu alisema kati ya mwaka 2010 na 2014 wanafunzi 2,251 waliacha shule kwa sababu ya utoro na wengine 40 waliachishwa kwa sababu ya ujauzito.

  “Ninawasishi wazazi  na uongozi wa wilaya na mkoa tufanye jitihada kuhakikisha jambo hili linakomeshwa mara moja. Huwezi kununua madaftari an kumlipia ada tu halafu usitake kuona mwanao anamaliza shule. Kila mzazi ana jukumu la kuhakikisha mtoto wake anamaliza shule ili awe na maisha bora hapo baadaye,” alisema Waziri Mkuu.

  “Nirudie kuwakumbusha wazazi kwamba mtoto wa mwenzio ni mtoto wako, huwezi kukubali maisha yaharibike hivi hivi. Tuungane pamoja kuhakikisha tunashinda vita hii,” alisisitiza.

  Waziri Mkuu leo anaendelea na ziara yake mkoani Mbeya kwa kutembelea wilaya ya Mbozi ambapo mbali ya kuzungumza na wananchi, atazindua maabara Vwawa sekondari, atakagua ghala la nafaka la NFRA na kupokea taarifa ya uzalishaji na usambazaji wa miche ya kahawa kwenye kituo cha TACRI - Mbimba.

  0 0

  Katibu Tawala wa jiji la Mbeya, Quip Mbeyela(katikati) akimkabithi mshindi wa Safari Nyama Choma 2015, John Mushi kitita cha Shilingi 1,000 000/= mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano hayo yaliyofanyika katika Chuo cha TIA mwishoni mwa wiki.
  Mpishi Mkuu wa Bar ya Tumaini ya jijini Mbeya, John Mushi(kushoto) akishangilia na kikombe mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya Safari Nyama Choma 2015 yaliyofanyika katika Chuo cha uhasibu(TIA) mwishoni mwa wiki.Kulia ni Meneja wa bia ya Safari Lger, Edith Bebwa na Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya, Quip Mbeyela.
  Mpishi Mkuu wa Bar ya Tumaini ya jijini Mbeya, John Mushi(kushoto) akiaonyesha kitita cha pesa tasliomu Shilingi 1,000 000/= mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya Safari Nyama Choma 2015 yaliyofanyika katika Chuo cha uhasibu(TIA) mwishoni mwa wiki.Kulia ni Meneja wa bia ya Safari Lger, Edith Bebwa na Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya, Quip Mbeyela.

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0


  Rais Jakaya Mrisho kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda yeye Mama Salma Kikwete kutoa pole na kuifariji familia ya Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo walipokwenda yeye na Rais Kikwete kutoa pole na kuifariji familia ya Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015.
  Rais Jakaya Mrisho kikwete na mkewe Mama Salma kikwete wakimfariji familia ya Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015.
  Rais Jakaya Mrisho kikwete na mkewe Mama Salma kikwete wakiwafariji wasanii wa Tanzania One Theatre kufuatia kifo cha kiongozi wao, Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015.PICHA NA IKULU

  0 0

         MODEL: 200 ,DIESEL 2.8 
  ,MANUAL, MILEAGE: 87000FULL A/C, POWER WINDOW, CENTRAL 
  LOCK, 
   FOUR WHEEL DRIVEIN VERY GOOD CONDITION , JUST BEEN 
   IMPORTED
    FROM THE UK   CAR 
  LOCATION : DAR ES SALAAM ,
   DUTY HAS BEEN PAID             
  PRICE: TSH 
   30 
   MILLION  
   FOR MORE INFORMATION CONTACT :
  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akijumuikana Viongozi na waislamu katika kisomo cha Hitma ya Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa Mwakilishiwa Jimbo la Magomeni (CCM) iliyosomwa leo jioni katika Msikiti wa Mushawal Mwembeshauri Mjini Unguja hitma hiyo ilihudhuriwa na Waumini na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi.
  Baadhiya Waislamu na Viongozi mbali mbali na wananchi wakiwa katika kisomo cha Hitma ya kumuombea Dua Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa Mwakilichi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Mjini Unguja aliyefariki hivi karibuni Hitma hiyo ilisomwa leo jioni katika Msikiti wa Mushawal Mwembeshauri.
  Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akitoa mawaidha baada ya kisomo cha Hitma ya Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa Mwakilichi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Mjini Unguja aliyefariki hivi karibuni Hitma hiyo ilisomwa leo jioni katika Msikiti wa Mushawal Mwembeshauri.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akitoa shukurani kwa Viongozi mbali mbali Waislamu na Wananchi na wapenzi wa CCM baada ya kisomo cha Hitma Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa Mwakilichi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Mjini Unguja iliyosomwa leo katika Msikiti wa Mushawal Mwembesahauri Marehemu alifariki hivi karibuni na kuzikwa Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja,[Picha na Ikulu,Zanzibar.]

  0 0

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Eng. Mussa Natty akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa kwanza kushoto) ambapo alisema miradi ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari katika wilaya hiyo itagharimu zaidi ya sh. bilioni 2. na kuwa ujenzi wake unasimamiwa na waataalamu waliobobea katika shughuli hiyo.
  FUPA uliomshinda Waziri wa zamani wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka kuhusu migogoro ya ardhi iliyokithiri katika Manispaa ya Kinondoni Mkuu mpya wa wilaya hiyo Paul Makonda ameahidi kuutafuna.
  Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Mussa Natty alisema miradi hiyo yote ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari katika wilaya hiyo itagharimu zaidi ya sh. bilioni 2. na kuwa ujenzi wake unasimamiwa na waataalamu waliobobea katika shughuli hiyo.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Eng. Mussa Natty aakimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda jinsi maabara hiyo ilivyojengwa kwa ubora wa hali ya juu.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa kwanza kushoto) akiongea na baadhi ya madiwani wa Wilaya.


  0 0

  Ankal akiwa na Mkurugenzi Mkuu MD wa Michuzi Media Group Mama Sellah (kulia kwake) pamoja na kikosi kazi cha Team Michuzi Production chini ya Production Manager Barbra Kilugira (wa tatu kushoto) ambayo ilipata heshima ya kurekodi mnuso wa kihistoria wa Tanzania Bloggers Network (TBN) Meet and greet Party katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia March 1, 2015. Mnuso huu ulifanikiwa sana kwa udhamini mkubwa wa VODACOM TANZANIA (wadhamini wakuu), NMB, COCACOLA, RAHA.COM, AIM GROUP na SERENA HOTEL. 

  0 0  NA.

  MUDA

  TUKIO

  MHUSIKA


  1.

  12:00 - 01:00


  Familia na Waombolezaji kupata chai nyumbani


  Kaimu Katibu wa Bunge

  2.

  01:00 - 04:00

  Misa ya kuaga mwili wa Marehemu


  Kanisa Katoliki,

  Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa


  3.

  04:00 - 04:30

  ·         Ndugu, Jamaa na Wananchi kuwasili katika Viwanja vya Karimjee


  ·         Viongozi wa Vyama vya Siasa, Waheshimiwa Wabunge, Manaibu Waziri, Mawaziri kuwasili na kuketi katika nafasi zao


  Katibu wa Bunge


  4.

  04:33

  Kiongozi wa Upinzani Bungeni  kuwasili


  Kaimu Katibu wa Bunge

  5.

  04:36

  Mhe. Naibu Spika kuwasili


  Kaimu Katibu wa Bunge

  6.

  04:39

  Mhe. Spika kuwasili


  Mhe. Naibu Spika

  7.

  04:42

  Mhe. Waziri Mkuu kuwasili


  Mhe. Spika

  8.

  04:50

  Mhe. Makamu wa Rais kuwasili

  Mhe. Spika


  9.

  05:00

  Mhe. Rais kuwasili


  Mhe. Spika

  10.

  05:00

  Mwili wa Marehemu kuwasili  kwa gwaride maalum la Sergeant-At-Arms


  Katibu wa Bunge

  11.

  05:00 - 05:15

  Sala fupi

  Kanisa Katoliki,

  Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa

  12.

  05:15 - 05:20

  Wasifu wa Marehemu


  Kaimu Katibu wa Bunge

  13.

  05:20 - 05:30

  Salamu na Rambirambi za Chama cha Mapinduzi (CCM)


  Katibu Mkuu, CCM

  14.

  05:30 - 05:35

  Salamu na Rambirambi kutoka kwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni


  Kiongozi wa Upinzani Bungeni

  15.

  05:35 - 05:45

  Salamu na Rambirambi za Serikali


  Waziri Mkuu

  16.

  05:45 - 05:55

  Salamu na Rambirambi za Uongozi wa Bunge


  Mhe. Spika

  17.

  05:55 - 06:00

  Neno la Shukrani toka kwa familia


  Mwakilishi wa Familia

  18.

  06:00 - 06:15

  Utaratibu wa safari


  Kaimu Katibu wa Bunge

  19.

  06:15 - 07:15

  Kuaga Mwili wa Marehemu kulingana na Itifaki


  MC

  20.

  07:15

  Mwili wa Marehemu kuondoka uwanjani kuelekea Uwanja wa Ndege


  MC

  21.

  07:20 - 07:25

  Viongozi wa Kitaifa kuondoka kulingana na Itifaki


  MC

  22.

  07:40

  Mwili wa Marehemu kuwasili Uwanja wa Ndege


  Kaimu Katibu wa Bunge

  23.

  08:00

  Mwili, Familia na Waombolezaji kuondoka kuelekea Songea


  Kaimu Katibu wa Bunge

  24.

  10:00

  Mwili wa Marehemu kuwasili Uwanja wa Ndge Songea na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa


  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

  25.

  10:00 - 10:15

  Mwili wa Marehemu kuelekea Uwanja wa Majimaji


  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

  26.

  10:15 - 11:00

  Mkuu wa Mkoa kuongoza wakazi wa Ruvuma kuaga mwili wa Marehemu


  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

  27.

  11:00 - 01:00

  Mwili wa Marehemu kuondoka Uwanja wa Majimaji kuelekea Lituhi, Nyasa


  ·         Ofisi ya Mkuu wa Mkoa


  ·         Kaimu Katibu wa Bunge

  28.

  01:00

  Mwili kuwasili nyumbani na taratibu za kifamilia kuendelea


  MC


  0 0

  Marafiki wa Wafanye Watabasamu Jumamosi iliyopita waliwatembelea tena watoto wanaoendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, ambapo waliwapa zawadi mbali mbali kisha kuchora nao ikiwa ni sehemu ya sanaa tiba (art therapy). 
   Akizungumza na blogu hii, mratibu wa programu hiyo ambaye pia ni mchora vibonzo maarufu nchini, Nathan Mpangala, alisema, ziara hiyo iliyokuwa na lengo la kutumia sanaa tiba kukabiliana na msongo wa mawazo, kusahaulisha maumivu na kuwapa nafasi watoto waweze kufanya shughuli walizokuwa wakifanya majumbani. 
  Ziara hiyo imewezekana kutokana na michango ya marafiki wa ndani na nje ya nchi ambao walichangia fedha na vitu mbali zikiwamo sabuni, dawa za meno, miswaki, mafuta ya kupakaa, toilet papers, matunda, vifaa vya kuchorea nk. “Tiba sanaa ni sanaa mpya nchini, baadhi ya nchi inatumika mahospitalini, magerezani, makambi ya wakimbizi, mashuleni, kwenye vituo vya kulelea watoto wenye mazingira magumu, majumbani nk. Si kwa watoto tu hata watu wazima inawahusu pia,” Alisema Mpangala. 
   Mpangala alisema programu hiyo imepokelewa vizuri na watoto hospitalini hapo na inaratibiwa kupitia mitandao ya kijamii. 
  Kwa watakaopenda kuungana na programu hii watembelee ukurasa wa Wafanye Watabasamu katika facebook. 
   Mpangala amewashukuru, wasanii wenzake, marafiki wa Wafanye Watabasamu, Hospitali ya Taifa Muhimbili, ndugu jamaa na marafiki kwa kuwezesha zoezi hili kufanyika. Pia vyombo vya habari kwa kupaza sauti za watoto hao.
   Mratibu wa programu ya Wafanye Watabasamu na mchora vibonzo maarufu nchini, Nathan Mpangala, akimwonesha mtoto Maurine jinsi ya kuchora katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Jumamosi iliyopita. Mpangala na wenzake walitembelea watoto wanaotibiwa saratani ili kuchora nao na kuwapa zawadi mbalimbali. Zaidi kuhusu programu hii tembelea: https://www.facebook.com/wafanyewatabasamu
   Nguvu ya sanaa tiba kama inavyooneshwa na Clara.
   Sanaa tiba ikawasahaulisha maumivu, wakajihisi wako nyumbani. Baadhi ya watoto wakijiachia na marafiki wa Wafanye Watabasamu waliokwenda kuwatabasamisha katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Jumamosi iliyopita.
   Mtoto Nico akienda sambamba na marafiki wa Wafanye Watabasamu. Kutoka kulia ni Sia Marupa, Masoud Junior na Cloud Chatanda.
   Ha ha ha haaaaaa. Hili ndilo lengo hasa la Wafanye Watabasamu. Mungu akupe nafuu ya mapema Nico. 
  Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Wafanyakazi wa Uhuru FM, Redio ya wananchi wakiongozwa na Dj Fast Edie (kushoto) wakishow love wakati wa tafrija yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika Februari 27, 2015 katika ukumbi wa Tukuyu katika Hoteli ya Land Mark jijini Dar es Salaam. 

  Tafrija hiyo iliyoongozwa na Kaimu Mkurugenzi wao Angela Akilimali ilifana na kupongezwa na kila mfanyakazi kwa jambo hilo jema la kuwakutanisha wafanykazi na kufurahi pamoja. 
  Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM, Angela Akilimali akizungumza machache wakati wa tafrija hiyo. Pamoja na mambo mengine aliwaasa wana Uhuru FM, Redio ya Wananchi kuzingatia weledi katika utekelezaji wa majukumu yao hasa katika kipindi hiki cha Kura ya maoni ya katiba mpya pamoja na Uchaguzi mkuu.
   Picha ya pamoja ya wafanyakazi na wageni waalikwa katika tafrija hiyo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0
 • 03/01/15--17:47: BWAWA LA MAINI OYE!
 •  Philippe Coutinho (kushoto)  baada ya kupiga  bao kali wakati  Liverpool walipotia pancha matairi ya gari la kutetea ubingwa la Manchester City katika mtanange wa   Premier League uwanja wa  Anfield jana.

  Bwawa la maini walifungua dimba kwa bao la Jordan Henderson  (picha ya chini) kabla ya Edin Dzeko kusawazisha kwa City. Lakini kiungo Mbrazil   Coutinho alimaliza ubishi kwa bao la mita 25 lililowaacha kina Yaya Toure Midomo wazi.Matokeao hayo yanawaacha City wakiwa nyumba ya   Chelsea kwa pointo tano, huku Liverpool tukipanda hadi nafasi ya tano. Bwawa la Maini Oye!


  0 0

  Kampuni ya ACACIA kupitia mgodi wake wa Buzwagi uliopo kwenye halmashauri ya mji wa Kahama,imeipatia ushuru wa asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato ghafi halmashauri hiyo,ikiwa ni ushuru kwa kipindi cha miezi sita (Julai - Disemba,2014) ambayo ni zaidi ya shilingi za kitanzania millioni 800,uliokabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama.
  Kaimu Meneja Mkuu wa mgodi wa Buzwagi  ulio chini ya Kampuni ya ACACIA,Ing. Mutereko Muganda (wa pili kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania millioni 800 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Bw. Felix Kimaryo (kulia) nje ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Mh. Benson Mpesya (wenye tai).

  0 0


  0 0

   
  Kikosi cha Timu ya Benki ya Exim Tawi la Babati katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wa kirafiki kuanza kati ya timu hiyo ya Benki na timu ya Babati Citizens FC wakati wa Bonanza la michezo lililofanyika mwishoni mwa wiki Babati. Bonanza hilo liliandaliwa na ofisi ya mkuu wa mkoa mkoani Manyara lilikiwa na lengo la kukuza michezo mkoani hapo.

  0 0

  Napenda Kuchukua Fursa hii Kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma na Mwenye Kurehemu kwa kunijaalia Uhai na afya njema hadi kufikia siku hii ya leo,ambapo ninayo furaha kubwa sana kwa kuongeza namba moja katika umri wangu, kwani bila yeye hakuna kitu chochote kinachoweza kufanyika.
  pia nitakuwa ni mchoyo wa Fadhila iwapo sitotoa shukrani za kipekee kwa ndugu zangu woote (wakiwemo wazazi wangu wawili na akina  Ankal Issa Michuzi, Ahmad Michuzi, Karim Michuzi, Ramadhan Michuzi, Ismail Michuzi, Ankal Macheka, Ai Michuzi,Rashid,Amir, Fadhil, Zahra, Tatu, Sellah, Bobby, Noreen, Adam, Saleh,Timu nzima ya Michuzi Media Group na wengine wengi ambao sijawataja majina yenu hapa ila moyoni ninayo, na bila kumsahau mtarajiwa wangu wa ubani Bi. Farida) kwa kuwa pamoja nami katika makuzi yaliyo mema hadi leo hii kufikia hapa nilipo.


  Tanzania Bloggers Network (TBN) pia naomba mpokee shukrani zangu za dhati kwa kuwa pamoja nami kama mwanachama hai siku zote na bila kunitupa, pia nichukue fursa hii kutoa pongezi kwa uongozi wa TBN na wanachama wenzangu kwa kuungana pamoja katika tafrija ya kihistoria  iliyotukutanisha pamoja. Kwa kweli ile ilikuwa ni siku muhimu sana kwetu kwa kutukutanisha pamoja na kufahamiana zaidi. Ile ilikuwa ni bonge la heko kwani kuna wengine wanatamani kuwa na umoja kama wetu lakini hawafanikiwi.
  Pia nawashukuru marafiki, jamaa zangu pamoja na Wadau woote popote pale mlipo ambao kwa namna moja ama nyingine mmekuwa ni mchango mkubwa katika maisha yangu na kunifanya kila siku niwe bize kuhakikisha libeneke halilali mpaka kieleweke. Nawashukuruni sana tena sana na Mungu awabariki nyoote. Nawapenda sana wote na tuko pamoja sana.

  TEMBELEA BLOG YA MTAA KWA MTAA Inayomilikiwa na Besdei boy Othman Michuzi kwa kufuata link hii.
  http://othmanmichuzi.blogspot.com

older | 1 | .... | 756 | 757 | (Page 758) | 759 | 760 | .... | 3270 | newer