Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 751 | 752 | (Page 753) | 754 | 755 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Wananchi wa mji wa Ilula katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa leo wamezua tafrani dhidi ya Askari Polisi baada ya mwanamke mmoja kupoteza maisha kwa kudaiwa kusababishwa na Askari hao waliokuwa kwenye msako wa kukamata watu wanaokunywa pombe wakati wa kazi.

  Kutokana na tukio hilo, mwanamke huyo aliyepoteza Maisha aliyetambulika kwa jina la Mwanne Mtandi awali aliamua kukimbia kwa lengo la kukwepa kukamatwa na Polisi hao Kabla ya kukutwa nyuma ya jengo la kilabu hicho cha pombe za kienyeji kilichopo mtaa wa Ilala Mjini Ilula akiwa amekufa.

  Taarifa za awali zinaeleza kuwa,Tukio hilo lilitokea majira ya saa 5 asubuhi leo na kudumu hadi Majira ya saa 10 jioni huku kituo cha Polisi kilichopo kwenye mji huo kudaiwa kuvunjwa na kuchomwa moto kwa magari matatu na Pikipiki Moja ya polisi.
  Baadhi ya wananchi wa mji wa Ilula katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wakiwa wameizunguka moja ya gari linalodaiwa kuchomwa moto na baadhi yao kufuatia vurugu kubwa iliyotokea mapema leo.
  Moto ukiendelea kuwaka barabarani.
  Vurugu hizo zilisababisha wasafiri wanaotumia barabara ya Kuu ya Mikoa ya Nyanda za juu kusini kukwama kwa zaidi ya masaa 6.

  0 0

  Na Tinah Reuben, Globu ya Jamii
  VIJANA sita waliokuwa katika mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wanaodaiwa kupanga kuandamana mpaka kwa Rais Jakaya Kikwete kudai ajira,wamefikishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam.
  Wakisomewa mashtaka yao na mwendesha mashtaka wa serikali,Tumaini Kwema mbele ya Hakimu Mkazi ,Frank Mushi alidai  kuwa,washtakiwa hao wanadaiwa kufanya fujo,kufanya mkusanyiko usiokuwa wa halali ili kuilazimisha serikali kuwapatia kazi na kushawishi kutenda makosa ya jinai kwa kuandamana mnamo Februari 15 mwaka huu eneo la Msimbazi Centre jijini Dar es salaam.
  Washitakiwa hao ni George Gagris,Linus Immanuel,Pharas  wera,Emmanuel Richard,Ridhwan Brayson na Jacob Joseph.  Baada ya kusomewa mashtaka na mwendesha mashtaka,Tumaini Kwema,watuhumiwa hao wote kwa pamoja walikana mashtaka hayo.
  Washtakiwa hao wamerudishwa tena rumande kutokana na kutokidhi masharti na vigezo vya dhamana,kesi hiyo itatajwa tena Machi 6 mwaka huu.
   Baadhi ya vijana waliokuwa katika mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wanaodaiwa kupanga kuandamana mpaka kwa Rais Jakaya Kikwete kudai ajira,wakiwa chini ya ulinzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,jijini Dar es salaam leo.
   Watuhumiwa hao wakipandishwa kwenye gari ya polisi.
  Picha na Emmanuel Massaka.

  0 0


  0 0

   Kijitonyama
   Kawe
  Mbezi

  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amezindua zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo wa Biometric Voter Registration (BVR) na kuwataka viongozi wa siasa wawahimize wanachama wao wajitokeze kwa wingi bila kujali tofauti za kiitikadi. 
   Ametoa wito huo leo mchana (Jumanne, Februari 24, 2015) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali na wananchi waliofika kushuhudia uzinduzi huo uliofanyika kwenye kata ya Lumumba, Halmashauri ya Mji wa Makambako, mkoani Njombe. 
   “Ninawasihi viongozi wa siasa tuwahimize wanachama wetu waende kujiandikisha kwa wingi. Tuache kauli za kukatisha tamaa, tuache kauli za kejeli sababu zoezi hili ni jema na lina nia ya kuwawezesha Watanzania wote kutumia haki yao ya kupiga kura,” alisema. 
   Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaomba Watanzania wenye vitambulisho vya uchaguzi vya zamani na wale wasio na vitambulisho wajitokeze kwa wingi kushiriki zoezi hilo. 
   “Wale waliokwishafikisha miaka 18, na wale ambao watatimiza miaka 18 ifikapo Oktoba, mwaka huu wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwa sababu wasipofanya hivyo hawataweza kupiga kura kama hawatajiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura,” aliongeza. 
   Akiwa uwanjani hapo, Waziri Mkuu alishuhudia uandikishaji wa wakazi watatu wa kata hiyo ambapo zoezi zima lilidumu kati ya dakika tatu na dakika tano. Kisha alikabidhi kadi kwa mpigakura wa kwanza kuandikishwa ambaye alitumia dakika tatu kamili. 
   Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema amefurahishwa na taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva kwamba zoezi la uandikishaji lililoanza jana katika mji wa Makambako lilizidi matarajio ya Tume ya kuandikisha wapigakura 1,850. “Nimefarijika sana na taarifa ya Mwenyekiti... Mlianza na kata tisa zenye vituo 54 na mlitarajia kuandikisha watu 1,850 lakini badala yake mmepata watu 3,014. Hili limenipa faraja sana. Ninawapongeza sana kwa hatua hiyo,” alisema. 
   Mapema, akitoa taarifa kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu kufanya uzinduzi huo, Jaji Lubuva alisema ana imani wadau mbalimbali wataendelea kuhamasisha wananchi washiriki zoezi la uboreshaji daftari la wapiga kura. 
  Alisema uboreshaji wa daftari hilo utafanyika kikanda na kwamba wamepanga kutumia siku saba kwa kila kituo huku akisisitiza kwamba hakuna mtu atakayebakizwa bila kuandikishwa wakati ameshafika kituoni. 
   Aliwataka watu wanaokwenda kujiandikisha wawe na vitambulisho vyao vya zamani vilivyotolewa na Tume ya taifa ya Uchaguzi kwani tayari vina taarifa zao kwa hiyo vitapunguza muda wa mtu kuandikishwa. 
  “Kadi za Tume (NEC) au za NIDA kwa wale wachache ambao wanazo, wakija nazo zitapunguza muda wa uandikishai sababu zina taarifa kwenye kanzidata,” alisema. Akitoa ufafanuzi kuhusu mfumo wa uandikishaji wa BVR, Jaji Lubuva alisema mfumo huo siyo sawa na mfumo wa upigaji kura wa kielektroniki (e-voting) kama ambavyo wengi wanadai bali mfumo huo unafanya kazi kwa kutumia alama muhimu za mpigakura. 
   “Mfumo huu unatumia alama zaidi kwanza ikiwa ni picha na zaidi ni macho ya mhusika, pili ni alama za vidole na tatu ni saini ya mhusika. Mfumo huu unaweza pia kuchukua alama za mtu mwenye ulemavu wa kuona ama ulemavu wa mikono,” alisema. 
   Alisema uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura ni hatua ya kisheria na kwamba Tume itajitahidi kuhakikisha inafuata hatua zote wakati wa zoezi hilo. 
   Waziri Mkuu ameondoka Makambako na anaelekea Mbeya kuanza ziara ya kikazi ya siku sita kukagua shughuli za maendeleo katika mkoa huo.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua  Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la Wapigakura  katika mji mdogo wa Makambako Februari 24, 2015.Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva na Katikati ni Katibu wa Tume hiyo, Ndugu Malaba. 
     Waziri Mkuu Mizengo Pinda   na Naibu Katibu Mkuu  ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CHADEMA  Mhe John 
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mwenyekititi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva (kushpoto) , Naibu Katibu Mkuu  na Katibu Mwenezi wa CHADEMA, John Mnyika (kulia), Yusufu Mbungiro ambaye ni Afisa Uchaguzi na Mafunzo taifa wa Chama cha CUF (wapili kushoto) na Allan Bujo ambaye ni Mkuu wa Ulinzi wa CHADEMA baada ya kuzinua Uborereshaji wa Daftari

    Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama kazi ya uandiskishaji wapiga kura baada ya ya kuzinua Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la Wapigakura  katika mji mdogo wa Makambako Februari 24, 2015.

  0 0

   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama mafunzo kwa vitendo yaliyokuwa yakifanywa na wanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari ya Igomelo wilayani Mbarari akiwa katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoani Mbeya Februari 24, 2015. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


  0 0

  Sauti Sol toka nchini Kenya mwishoni mwa wiki (21/02/2015) wamepiga show ya kufufuka mtu ndani ya kiota cha burudani chanye hadhi ya kitalii Jembe Beach ndani ya party lililopewa jina la JEMBEKA, likiandaliwa na Kituo kipya cha redio jijini Mwanza Jembe FM 93.7.
  Mashabiki walitoa ushirikiano wa kila htua zilizokuwa zikiendelea stejini.
  Hapo vijEee....!!
  Kenyan Afro Pop (2014 MTV EMA Best Worlwide Act Nominees) walifanya kazi ya ukweli...
  Stage kama screen vile unawochi kitu cha LIVE....
  Picha zaidi na G. Sengo BOFYA HAPA

  0 0

  Trevo ni nini?

  ·         Bidhaa kutoka Marekani ambayo ndani yake kuna virutubisho 174

  ·         Trevo imethibitishwa na ORAC,Cap-e ,Halal,Kosher,Vegetarian,na TFDA

  Trevo Inaimarisha

  ·         Ufahamu wa kiakili-mental focus

  ·         Kudhibiti uzito- weight management

  ·         Afya ya moyo- Blood pressure and Heart health

  ·         Afya ya seli

  ·         Afya ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula - digestion system

  ·         Afya ya mfumo wa neva za fahamu - nervous system

  ·         Afya ya mfumo wa kinga ya mwili -immune system

  ·         Afya ya mifupa na viungo

  ·         Afya ya mfumo wa damu - blood circulation

  ·         Afya bora ya mwili mzima

  ·         Nishati ya kutosha mwilini

  ·         Kuongeza nguvu mwili

  ·         Afya ya sukari damuni- Blood sugar level

  ·         Kuongeza CD4 kwa wagonjwa wa HIV/Aids

  ·         Kusaidia wenye vidonda vya tumbo na magonjwa ya kina mama

  Fursa ya Biashara

  ·         Fursa ya biashara ya kimataifa bila mipaka ya nchi

  ·         Gharama ya kuanza biashara ni sh 389,200

  ·         Kwa kila Msambazaji mpya unamuingiza kwenye mtandao unalipwa kati ya sh 100,000 na Sh 800,000

  ·         Kuna njia nane za kutengeneza hela na Trevo

  ·         Trevo ina miezi mitatu tu nchini Tanzania na inapata umaarufu kila kukicha. Hivyo fursa ya biashara ni nzuri sana

  ·         Nafasi ya kufikia ndoto zako kuwa mfanyabiashara wa kimataifa na kufikia malengo ya kweli


  Jipatie Trevo Leo na Uimarishe Afya Yako.Tembelea tovuti ya Trevo www.trevo.co.tz.     
  AU  Tupigie simu kupitia +255 767 059 211 .
  Unaweza acha ujumbe mfupi SMS...UTAJIBIWA


  Bidhaa inasambazwa popote Tanzania NA nje ya nchi, Kujiunga na Biashara hii tupigie simu hapo juu au tuandikie email: kemikoku@gmail.com  0 0

  For the first time in Tanzania, the Dar Choral Society and Orchestra proudly presents to you a Symphonic night experience. The unforgettable evening of music mastery will feature a special performance of Tchaikovsky Symphony no.5 in E minor and Beethoven Egmont. Limited number of seats available for the two nights at the Dar es Salaam Serena Hotel on 28-29th March 2015, from 06:30 PM 

  Book your ticket now via our email: info@darchoralsociety.org. Tickets will be available at selling points from 1st of March 2015. Karibuni sana.

                                                 Dar Choral Society and Orchestra
  dar coral.jpg

  0 0


  BONDIA Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' 


  ametamba kumsambalatisha Fadhili Majiha 'Stopper' katika raundi za awali za mpambano wao utakaofanyika siku ya jumamosi ya feb 28 katika uwanja wa ndani wa taifa mpambano huo wa raundi nane unasubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki mbalimbali wa mchezo wa masumbwi nchini ususani vitongoji vya Kinondoni, Manzese, mabibo na Mwananyamala ambapo ndio maeneo yao yenye wapenzi wao wa ngumi na sehermu mbalimbali


  akizungumza na mwandishi wa habari hizi Miyeyusho ametamba kuwa atokuwa na mzaha siku hiyo itakuwa kazikazi mana yeye ni bondia mkubwa sana hapa nchini na akuna mtu wa kumbabaisha kwa sasa katika uzito wake

  mbali na mpambono huo wa utangulizi kutakuwa na mpambano wa ubingwa wa U.B.O Africa utakaowakutaniosha mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Cosmas Cheka kutoka Morogoro ambao watatanguliwa na mapambano mengine yatakayowakutanisha Shomari Mirundi zidi ya Mwinyi Mzengela wakati Shedrack Ignas atapambana na Husein Mbonde, na Godfrey Slive atamenyana na Sadick Abdulazizi


  siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi  mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Alina wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

  0 0
 • 02/24/15--18:10: Article 4


 • 0 0


  0 0


  Come and eat different tastes of Chicken Wings, Chicken Sausages, Grilled Chicken etc.
  We will have:-
  Dj Music | Professional Dancers Beach Soccer Kids ZonesSwimming 
  Venue: Azura Beach Club Kawe Mwai Kibaki Rd, Dar es salaam
  Date: 28th February 2015 
  Time: 12pm to Midnight
  For Sponsorship or advertising your products
  Call: +255 755 048 362 or +255 658 289 737
    
  chicken wings.jpg

  0 0

  Natanguliza shukrani zangu mbele ya Mwenyezi Mungu ambaye ameendelea kunipigania kila kukicha, lakini pia niwashukuru wazazi wangu Abdalah Mbaruku na Eustela Massatu kwa malezi mema ambayo mmekuwa mkinipatia hadi leo kijana wenu nimefikia katika umri huu.
  Furaha niliyo nayo leo ni sawa na ile ambayo wanayo wadogo zangu wapendwa Jane, Judi, Juma Busagaga , Ashura Mbaruku  na mtoto wangu mpendwa Jesca Dixon pamoja na ndugu zangu kaka, Dada, wajomba ,mashangazi, marafiki na wengine wote tuendelee kufanya maombi ili Mwenyezi Mungu atusimamie katika kila jambo.


  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Paul Makonda baada ya kuwasili katika Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar e salaam leo tayari kwa kukagua ujenzi wa maabara na pia kupokea na kugawa vitabu vya sayansi vilivyochapishwa  na Watu wa Marekani.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua maabara katika Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar e salaam ambako  pia alipokea na kugawa vitabu vya sayansi vilivyochapishwa  na Watu wa Marekani. Wa kwanza kulia ni Dkt Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, akifuatiwa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma kikwete, Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress, na viongozi wengine wakiangalia jinsi somonla sayansi likifundishwa katika darasa la Kidatu cha pili Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar e salaam ambako  pia alipokea na kugawa vitabu vya sayansi vilivyochapishwa  na Watu wa Marekani
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma kikwete, Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress, Dkt Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,na viongozi wengine wakisalimia wanafunzi katika   darasa la Kidatu cha pili Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar e salaam ambako  pia alipokea na kugawa vitabu vya sayansi vilivyochapishwa na Watu wa Marekani
   Rais  Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress, wakiongea na mkandarasi wa maabara ya  Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar e salaam ambako  pia alipokea na kugawa vitabu vya sayansi vilivyotolewa na Watu wa Marekani

   Rais  Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete  na Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress wakiwa na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar e salaam wakiwa na vitabu walivyogawiwa vya sayansi vilivyochapishwa  na Watu wa Marekani.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Na Abdulla Ali, Maelezo-Zanzibar 
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Mhe. Said Ali Mbarouk amesema zaidi ya shilingi milioni 100 za Kitanzania zinahitajika ili kukamilisha ujenzi wa kituo kipya cha kurushia matangazo cha Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC). 
   Hayo ameyasema wakati wa ziara yake ya kutembelea kituo hicho kilichopo Bungi Wilaya ya Kati Unguja. Amesema lengo la ziara hiyo ni kuangalia ufanisi wa kazi kwa watendaji wa kituo hicho na kusisitiza kuwa ni jukumu la Wizara kufanya hivyo ili kuimarisha dhana ya uwajibikaji kwa watendaji wake. 
   Amesema kwa sasa Serikali inaweza kuendesha mitambo ya kurushia matangazo iliyopo kituoni hapo bila ya kutegemea mafundi kutoka nje ya Nchi kama vile China kwani ina mafundi wa kutosha wenye uweledi katika fani ya uhandisi wa mitambo ya Redio na Televisheni. 
   Aidha ametanabahisha kuwa Serikali ina jukumu la kuwaongezea ujuzi baadhi ya mafundi hao kwa kuwapeleka kusoma nje ya Nchi ili waende sambamba na mabadiliko ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya Umma. 
   Waziri huyo amewataka mafundi wa kituo hicho kurekebisha matatizo madogo madogo yaliyopo kituoni hapo ikiwemo kufunga mafeni pamoja na viyoyozi (Air Condition) ili kuzifanya mashine hizo zidumu kwa muda mrefu na kupunguza hasara ya kuungua mara kwa mara kutokana na joto kali linakuwemo katika vyumba hivyo vya kurushia matangazo. 
   Waziri Mbarouk amewataka wafanyakazi kuwa wabunifu katika utendaji wao wa kazi na kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa lengo la kuliimarisha shirika hilo kwani matangazo yake ni muhimu ndani na nje ya Nchi ikiwemo mwambao wa Kenya ambao wanategemea kwa kiasi kikubwa matangazo ya ZBC. 
   Nae fundi mkuu wa kituo hicho Nd. Ali Aboud Talib amesema wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo uchakavu wa nyaya za kurushia matangazo (Cable) kutokana na kutumika kwa muda mrefu, kuwepo kwa msitu mkubwa kutokana na kukosekana kwa wafanyakazi wa kusafisha eneo hilo. Vilevile amesema tatizo la usafiri ni usumbufu mkubwa kwao kwani hadi sasa kituo hicho kina gari moja ambayo haitoshelezi kwa kazi za kila siku pamoja na Taa za Mnara wa kurushia matangazo kuwa haziwaki. 
   Aidha amesema mashine za kurushia matangazo (Transmitter) hazina uwezo mkubwa ukilinganisha na vyomo vyengine vya habari vilivyopo Nchini kwani hadi sasa ZBC inatumia mashine yenye uwezo wa masafa ya 1 kilowatts ambapo vyombo vyengine vinatumia mashine zenye uwezo wa masafa hadi 4 kilowatts. 
   Fundi huyo amewataka wananchi kuwa wazalendo kwa kuangalia Televisheni yao ya nyumbani (ZBC) ili kuipa thamani ndani na nje ya Nchi jirani kwa kuwa na watazamaji wengi.
  Chumba cha mitambo ya kurushia matangazo (Transmitter) kilichopo katika Kituo cha Bungi, Unguja.

  Fundi mkuu wa kituo hicho Nd. Ali Aboud Talib akitoa maelezo ya kiufundi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Mhe. Said Ali Mbarouk wa kushoto.
  Aliyenyoosha mkono ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Nd. Hassan Abdalla Mitawi akitoa maelezo kwa Waziri wa Habari Zanzibar. 

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Mhe. Said Ali Mbarouk akikagua Jenereta linalotumika pindi umeme utakapokosekana kituoni hapo. 

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Mhe. Said Ali Mbarouk akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali mara baada ya kumaliza ziara yake kituoni hapo. 
  Picha zote na Miza Othman, Maelezo-Zanzibar

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EY, Bw. Mark Otty, amesema Tanzania ina rasilimali nyingi ambazo zinahitaji watu kuwekeza, hasa katika sekta ya miundombinu, kilimo, huduma za Kifedha ,mawasiliano,madini pamoja na gesi asilia .
  Otty ameyasema hayo leo wakati wa alipokutana na waandishi wa habari kwenye ofisi ya kampuni hiyo hapa nchini,yenye makao yake makuu nchini Uingereza,amesema kutokana na rasilimali zilizopo zitavuta uwekezaji na uchumi wa nchi unaweza kukua.
  Mkurugenzi huyo amesema kazi kubwa ya kampuni hiyo ni ushauri wa uchumi ,biashara pamoja na ukaguzi kwa sekta za serikali na sekata binafsi.
  Amesema katika ziara yake nchini ni pamoja na kukutana na Rais Jakaya Kikwete na kujadili masuala mbalimbali likiwemo la ujio wake nchini na jinsi kampuni yake na serikali wanavyoshirikiana katika shughuli mbalimbali za biashara.
  Kwa upande wa Meneja Mkazi wa Kampuni ya EY, Bw. Joseph Sheffu amesema kuna maeneo mengi wameayatafiti na kuona kuna fursa ya uwekezaji kutokana na taratibu bora zilizopo nchini katika sekta ya uwekezaji.
  Bw. Sheffu amesema kampuni hiyo ina wahasibu,wataalam wa kodi pamoja na wakaguzi ambao wameweza kupata ujunzi katika mataifa mbalimbali  hivyo huduma inayotolewa na taasisi hiyo imekuwa ni bora.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EY,Mark Otty akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokutana nao Februari 24,2015 kwenye ofisi za kampuni hiyo,jijini Dar es salaam.
  Meneja Mkazi wa Kampuni ya EY, Bw. Joseph Sheffu (kushoto) akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati walipokutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EY, Bw. Mark Otty (kulia) kuzungumzia ujio wake hapa nchini. Picha na Othman Michuzi.

  0 0

  Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii 

  ‘Usilolijua ni sawa na usiku wa giza’ msemo huu una maana kwani kitu usichokijua huwezi ukajadili kutokana na kutokielewa.

  Katika pitapita mitaani hasa katika maeneo ya masoko katika jiji la Dar es Salaam kuna mtu aliyejitambulisha kwa jina la Julius Methew alienileza kuwa hakuna sehemu yeyote katika nchi za Afrika ambayo takataka zake zinatoka mashambani na kupelekwa mijini isipokuwa Tanzania ambayo ameitaja kuwa ni nchi ya kwanza kwa Afrika inayopokea takataka za mashambani kuingiza mijini.

  Mathew anasema taka nyingi zinazozalishwa vijijini zinakuja katika jiji la Dar es Salaam ambapo kila sehemu ya masoko utakuta uchafu na mwingine kuingia katika mitaa mbalimbali kutokana na kuchukua huduma katika masoko hayo.

  Anasema kuwa na uchafu katika jiji la Dar es Salaam ni kutokana na kutokuwa na mfumo wa kutunza mazingira na mwisho wa siku watu wanailaumu serikali kwa kushindwa kukusanya taka katika mitaa.

  Aidha anasema vijiji ambavyo vinazalisha bidhaa mbalimbali vina kuwa na usafi kutokana na takataka zao kuleta mijini.

  Julius anasema kuwa ndizi mbivu zinapoletwa katika jiji la Dar es Salaam zinakuja zikiwa zimefunikwa na majani ya mgomba lakini mwisho wa siku majani yanabaki sokoni,hapo ndipo utakuta ni tatizo la kuwa na taka nyingi katika jiji letu.


  “Mfumo huu wa kuchukua taka vijijini utafanya jiji kuendelea kuwa na uchafu miaka yote na hakuna suluhu itakayowezesha kuondokana”anasema Methew.


  Mathew anasema nyanya nazo zinazalishwa zinakuja katika tenga zikiwa zina majani lakini mwisho wa siku nyanya zinaondoka majani yanabaki sokoni hili ni tatizo katika jiji la kuweza kuondokana na uchafu wa masoko na mitaani.

  Aidha anaeleza kuwa teknolojia imezidi kukua lakini bado watu wanatumia tenga ,majani ya migomba ,majani ya mpunga kusafirishia bidhaa na mwisho wa siku bidhaa zinaisha lakini mwisho wake ni kupata majani.tenga na majani ya mpunga katika mitaa.

  Anasema suluhu yake ni serikali kupiga marufu uingizaji wa bidhaa ambazo zinakuwa na takataka kwa kutumia mfumo wa kuweka katika boksi ambapo boksi inaweza ikaondolewa bidhaa na boksi kuendelea kuwa bidhaa na kuzalisha bidhaa nyingine.

  0 0

  Mwishoni mwa wiki iliyopita vijana machachari wa Yamoto Band walifanya ziara maalum kutembelea ubalozi wetu a jijini London, Uingereza, na kupata fursa ya kukutana na Balozi Peter Kallaghe na kujadili nae kuhusu tasnia ya muziki Tanzania. Aidha Mh Balozi Kallaghe aliwapongeza kwa kazi zao nzuri na kuwaasa kuwa waendelee kujituma kwa moyo zaidi, huku akiwatahadharisha wasilewe sifa na kuwa nguvu ya soda, bali wawe mfano wa kuigwa kwa kudumu pamoja kwa muda mrefu. Bendi ya Yamoto iko nchini Uingereza kwa ajili ya kufanya maonyesho maalum.
   Mh Balozi Kallaghe akiongea na vijana wa Yamoto Band katika ubalozi wa Tanzania jijini London
   Mh Balozi Kallaghe akipata picha ya kumbukumbu na  vijana wa Yamoto Band 
  Promota wa safari ya Yamoto Band jijini London, Jestina George, akiwatambulisha Yamoto Band kwa balozi

  0 0

  Na   Bashir     Yakub.

  Mara nyingi  nimeandika  kuhusu  mirathi  lakini  zaidi  nimegusia habari ya usimamizi  wa mirathi . Leo  nimeona  ni muhimu  kueleza  mgao  wa mirahi  kwa kuangalia nani anapata  nini kupitia  Sheria ya mirathi ya serikali. Fuatana  nami.

  ( A ) MGAO UKOJE  IKIWA  MUME  AMEFARIKI  AKAACHA  MJANE, WATOTO  NA  NDUGU ZAKE.

  Kama mume  amefariki  na akaacha mjane na watoto basi moja ya tatu ( 1/3) ya mali  za marehemu  zilizo kwenye mirathi anatakiwa apewe mke wake. Mbili ya tatu( 2/3)  ya mali hizo itaenda kwa watoto wake.

  ( B ) MGAO UKOJE KAMA MAREHEMU HAKUACHA WATOTO  LAKINI   KUNA  MJANE.
  Kama hakuna watoto walioachwa  na marehemu katika familia husika  lakini kuna mjane ,mali ya marehemu hugawanywa katika mtindo ambao ndugu hupewa nusu (1/2), na mjane  hupewa nusu ya mirathi ya marehemu(1/2). Hii ni sawa kwa sawa.

  (C)MGAO UKOJE IWAPO MAREHEMU HAJAACHA NDUGU WALA   MTOTO ISIPOKUWA MJANE TU.

  Kama marehemu hajaacha ndugu wala  mtoto  au watoto  basi mali yote huchukuliwa  na  mjane.Ndugu  kwa maana  ya hapa ni  kaka, dada, mama  mzazi  wa marehemu au baba n.k. 
  ( D ) KAMA  MKE AMEFARIKI  NA KAMUACHA  MUME  NA  WATOTO JE   MGAO  UKOJE.

  Hapo juu tumeona mume akifariki akamuacha mke  na watoto mke huchukua  moja ya tatu na watoto au mtoto mbili ya tatu. Hali  iko hivohivo kwa mume naye ana haki kama alizo nazo mke wake yaani kupata mirathi kutoka katika mali za marehemu.Kwa maana hiyo mume hupata moja ya tatu(1/3)  ya  mali  za marehemu mkewe na mbili ya tatu (2/3) huenda kwa watoto.


older | 1 | .... | 751 | 752 | (Page 753) | 754 | 755 | .... | 3283 | newer