Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 750 | 751 | (Page 752) | 753 | 754 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Balozi wa promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hillary Daud ‘Zembwela’na Claudia Mapunda(kulia)ambaye aliibuka mshindi wa kitita cha shilingi milioni 1/-kupitia promosheni hiyo wakihesabu fesha hizo kabla ya Balozi huyo kumkabidhi rasmi kitita chake katika hafla iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
  Balozi wa promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hillary Daud ‘Zembwela’akimkabidhi kitita cha shilingi Milioni 1/-mshindi kupitia promosheni hiyo Claudia Mapunda(kulia) katika hafla fupi iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
  Balozi wa promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hillary Daud ‘Zembwela’akisalimiana na wateja wa Vodacom Tanzania walifika kupata huduma mbalimbali katika duka la kampuni hiyo lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumkabidhi kitita cha shilingi milioni 1 mmoja wa washindi wa Promosheni hiyo Claudia Mapunda(hayupo pichani).
  Mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 1/= kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Bi.Claudia Mapunda(kulia) akifurahia kwa kuonesha kitita chake cha fedha alizoshinda baada ya kukabidhiwa na Balozi wa promosheni hiyo Hillary Daud ‘Zembwela’(kusho) anaeshuhudia katikati ni mpambe wa Balozi huyo Maria John.Hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  0 0

  Baadhi ya wakazi wa mji wa Moshi wakiashangaa lori la mafuta lilotembea bila ya kuwa na dereva likitoka kituo cha mafuta cha Puma lilipokuwa limepaki kwa ajili ya kushusha mafuta.tukio hilo limetokea mchana wa leo mjini Moshi jirani na ofisi za TTCL.
  Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa lori hilo baada ya kukata kona ya ghafla ambayo ilisaidia madhara zaidi yasitokee baada ya tanki kukata na kurudi upande wa barabarani na kisha kusimama.


  0 0

  Mgeni rasmi kwenye mafunzo ya stadi za kazi na utambuzi wa fursa za kiuchumi zilizopo mkoa wa Lindi Naibu waziri wa kazi na ajira mhe.Dr. Makongo Mahanga (MB) amewataka vijana wa mkoa wa Lindi kuyageuza mafunzo watakayoyapata ya stadi za maisha sanjari na kuzitambua fursa zilizopo ndani ya mkoa, waweze kujiajiri na kujikomboa kiuchumi,wakati wa  uzinduzi wa mafunzo hayo ambapo jumla ya vijana 360 kutoka halmashauri sita zilizopo mkoani Lindi wameudhuria kwenye ukumbi wa kanisa katoliki Mt.Kagwa. Vijana 360 kutoka kwenye wilaya za Kilwa,Ruangwa,Liwale,Nachingwea,Lindi Mjini na Vijijini ambao ni washiriki wa mafunzo wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi naibu waziri wa kazi na ajira Mhe.Dr.Mkaongoro Mahanga hayupo pichani.
  Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe.Mwantumu Mahiza akiwaeleza washiriki wa mafunzo ya stadi za maisha sambamba na kufahamu fursa za kiuchumu ambapo mpango wa kuendesha mafunzo hayo umebuniwa na yeye mwenyewe,mbele ya mgeni rasmi,wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.


  0 0

  Na  Bashir  Yakub

  Kawaida unapokuwa umeingia katika mkataba au makubaliano katika jambo lolote lile kunakuwa na masharti ambayo unapaswa kuyatimiza au kutimiziwa. Na hapa nazungumzia mikataba yote uwe wa kuuza mbuzi au ule wa kujenga ghorofa mia, yote ni mikataba. Masharti hayo huwa ndio makubaliano yenyewe au twaweza kusema kuwa ndio mkataba wenyewe. Kila upande unawajibika  juu ya utekelezaji wa masharti hayo. Yeyote anayefikia hatua ya kukiuka masharti hayo  au hata kukiuka sharti moja tu, hana namna ila kukubaliana na  hatua na utaratibu wa kisheria kuhusu  uvunjwaji au ukiukwaji wa mikataba. 

  1.KUKIUKA  MKATABA   AU   MAKUBALIANO.

  Uvunjaji wa mkataba unaweza kutokea katika njia nyingi. Moja ni ile ya kawaida ambapo mtu huamua kujitoa  kwa kusema,kutamka au kuandika kuwa sasa sitafanya hili na lile hata kama lipo katika makubaliano yetu.  Pili njia nyingine  ya kuvunja mkataba ni pale ambapo mtu hasemi kwa kutamka kwamba sasa sitafanya hili wala lile isipokuwa hatimiza wala hatekelezi kile mlichokubaliana. Ifahamike kuwa mtu anapoingia mkataba na mtu mwingine  au kampuni na kampuni  au kampuni na mtu sheria inalazimisha kutekeleza kwa usahihi yale yote yaliyokubaliwa  katika mkataba huo. Utekelezaji wa baadhi ya masharti na kuacha mengine au kutotekeleza yote kabisa ni uvunjaji au ni kujitoa katilka mkataba kwa mujibu wa sheria. Aidha nasisitiza kuwa ili mtu ajitoe katika mkataba sio lazima aseme kuwa nimejitoa katika mkataba. Kitendo cha kutofuata makubaliano  kama yalivyokubaliwa  ni kujitoa katika mkataba moja kwa moja.

  2.KUMDAI  FIDIA    ALIYEKIUKA  MKATABA  AU  MAKUBALIANO. 

  Si  vyema  mtu akafanya  makubaliano  na mtu mwingine  halafu  akapotea  bila  kutekeleza  kile  kilichokubaliwa. Ni  sababu  hii inayonifanya kuwaambia  watu  kuwadai  fidia  wale  wanaokiuka  masharti. Kudai kulipwa  fidia  baada ya  kuvunjwa  mkataba  ni takwa la  kisheria  na  hivyo  si  ukorofi  kama ambavyo  mtu anaweza kufikiri. 

  3.AINA  ZA FIDIA  UNAZOWEZA  KUDAI  UKIVUNJIWA  MKATABA.

  ( a ) Fidia zipo za aina nyingi.  Kwanza kuna fidia ambayo utatakiwa kulipa kutokana na makubaliano yenu ya awali wakati mnaingia mkataba. Hii ni aina ya fidia ambayo wahusilka katika mkataba hukubaliana  awali kabisa wakati wanaingia katika mkataba  ambapo hupanga kiasi cha fidia ambacho watalipana iwapo mmoja kati yao atakiuka au kujitoa katika mkataba. Kwa kuwa fidia hii huwa  imeandikwa na ipo ndani ya mkataba basi aliyekiuka au kujitoa katika mkataba hutakiwa kulipa fidia hiyo  kulingana na makubaliano yao mara moja. 

  ( b ) Fidia  nyingine ni ile ambayo mtu hutakiwa kulipa iwapo wakati wanaingia mkataba hakuna fidia yoyote waliyokuwa wamekubaliana kulipa iwapo mmoja wao atakwenda kinyume.  Hii ni aina ya fidia inayotathminiwa na mahakama.  Mahakama hutathmini fidia hii kwa kuangalia mambo mawili yaani  kiwango cha ukiukwaji wa mkataba na hasara  zilizotokana na ukiukwaji huo. Kupitia hayo mahakama huweza  kutangaza kiwango cha fidia anachotakiwa kulipwa mtu ambaye amevunjiwa mkataba.


  0 0

  The Oscar viewing party was held at the historic Warner Brothers Mansion which also the home Daphna Edwards Ziman who is the founder of Children Uniting Nations.
  Daphna Ziman launched CUN in 1999 with Honorary Chair and former First Lady and Secretary of State, Hillary Rodham Clinton and former President Bill Clinton to benefit at-risk youth in the foster care system (President Clinton was a foster child). This event has become one of the most prestigious celebrations of the Awards season, honoring supporters and celebrities, who have shown compassion and commitment to improving the lives of at-risk youth and children in foster care.
  Fashion Designer Linda Bezuidenhout was invited by Daphna Ziman to attend and contribute one of her dress designs that was auctioned to benefit Children Uniting Nations.
  The Children Uniting Nations Gala draws some of the biggest names in Hollywood. Past guests of the gala have included Prince, Halle Berry, Sharon Stone, Harrison Ford, Tom Hanks and Rita Wilson, Pierce Brosnan, David Bowie & Iman, Jeff Bridges, The Black Eyed Peas, Megan Fox, Mel B, Isiah Thomas, Dennis Quaid, Rob Reiner, Susan Sarandon, Tim Robbins, Carly Simon, Chris Tucker, Paris Hilton, Christina Milian, Metta World Peace, Magic Johnson, Russell Simmons, Alyssa Milano, Gladys Knight, Wyclef Jean, Ice-T, Lil Kim and others.
  For additional information on fashion designer Linda Bezuidenhout, please visit http://www.lbapparel.com           
  For additional information about Children Uniting Nations, please visit http://www.childrenunitingnations.org,  Fashion Designer Linda Bezuidenhout being interviewed on the red carpet as she arrived at the 16th ANNUAL OSCAR VIEWING PARTY AND AWARDS GALA TO BENEFIT CHILDREN UNITING NATIONS IN BEVERLY HILLS , CA  Linda with Daphna Ziman on the Red Carpet at the 16th ANNUAL OSCAR VIEWING PARTY AND AWARDS GALA TO BENEFIT CHILDREN UNITING NATIONS IN BEVERLY HILLS , CA

  Linda with Model and Entrepreneur Renee Knorr (Wearing a Black Ornamental LB Dress) and Skip Martin of COOL AND THE GANG.

  0 0

  Naibu waziri wa viwanda na biashara Mheshimiwa Janet mbene katika siku yake ya kwanza ya ziara ya kikazi nchini Uingereza, amekutana na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara na wawekezaji kupitia Chama chao cha East African Association, yenye lengo la kuvutia uwekezaji katika viwanda na kuongeza thamani bidhaa zinazozalishwa Tanzania. 
  Mheshimiwa Mbene amewaeleza wafanyabiashara hao hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kuboresha mazingira ya kufanya biashara, hasa kwa kufanya marekebisho ya mifumo ya utoaji huduma za kiserikali kwa wafanyabiashara na wawekezaji nchini kupitia kitengo kilichoko katika Ofisi ya Rais kijulikanacho kama “Presidential Delivery Bureau” kinachoongozwa na Mtendaji wake Omari Issa. 
  Aliwaambia wafanyabiashara hao kuwa licha ya kurekebisha mifumo hiyo pia kinalenga kuondoa migongano ya kisheria na ya kiutendaji iliopo miongoni mwa Taasisi za Serikali kama za Mamlaka mbalimbali kama ya Mapato (TRA) na zinginginezo kama BRELA, na TIC, na zingine zinazohusika na utoaji wa huduma mbalimbali kwa wafanyabiashara. 
  Aliwaambia kuwa kupitia PBD, kulipendekezwa sekta kipaumbele ambazo zimewekwa katika Mpango wa utekelezaji wake wa Matokeo Makubwa Sasa au “BIG Result Now”. Alizitaja Sekta hizo kuwa ni za Nishati, Kilimo, Maji, Miundombinu, Elimu na utaratibu wa upatikanaji wa Rasilimali. Alisema kuwa watendaji katika sekta hizo walipewa malengo ya utekelezaji na kwamba baada ya tathmini ya mwaka mmoja sasa, hali inaonyesha kuwa utekelezaji wa programu hiyo unaenda vizuri na umeonyesha pia kwamba kumbe hatua za kurekebisha mifumo ya utendaji kazi wa serikali zinawezekana. 
  Aliongeza kusema kuwa kutokana na mafanikio hayo ya muda mfupi, Wizara yake ya Viwanda na Biashara nayo pia imeingizwa katika Mpango huo ili kuharakisha urekebishaji wa mifumo ya utoaji Leseni, Vibali na huduma nyingine za biashara. Lengo likiwa ni kuwezesha utoaji huduma hizo katika mifumo ya kigitali kupitia Mtandao ili kuondoa tuhuma za rushwa na kuharakisha utoaji wa maamuzi. 
  Mheshimiwa Mbene ametumia pia fursa hiyo kuwahamasisha wawekezaji kuwa wakati Serikali inaendelea kurekebisha mifumo yake ya utoaji huduma, waje kuwekeza nchini hasa katika viwanda vya kusindika mazao ya kilimo na bidhaa nyingne kama madini kupitia Maeneo maalum ya uzalishaji (yaani EPZs na EFTAs), ambayo yametengwa tayari katika mikoa kadhaa ambayo ni muhimu katika kufanikisha malengo ya kiuchumi. 
  Ameyataja maeneo hayo kuwa yapo katika mikoa ya Mtwara, Dar es Salaam, Bagamoyo, Tanga, Ruvuma, Kigoma, Arusha na Kagera. Licha ya kuyataja maeneo hayo, Mheshimiwa Naibu Waziri aliwaeleza wafanyabiashara hao kuwa pia zipo fursa za kutosha za uwekezaji nchini Tanzania katika sekta mbalimbali kama miundombinu, nishati (hasa nishati mbadala za jua na upepo), kilimo hasa cha mazao ya nafaka kama mchele, mahindi, miwa, n.k. 
  Alizitaja sekta zingine kuwa ni za utaoaji huduma kama za Utalii (katika ujenzi wa Mahoteli), Hospitali na Shule (katika kuboresha elimu). Kesho Mheshimiwa Naibu Waziri anatarajia kukutana na watendaji wa Kampuni ya SACOMA inayoagiza bidhaa za mbogamboga, matunda na Maua kutoka Afrika
  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mama Janeth Mbene (pili kulia), kwenye picha ya pamoja na Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Bwana Msafiri Marwa, msaidizi wa Naibu Waziri Dada Magdalena , pamoja na Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London Bwana Yusuf Kashangwa mara baada ya Mhe. Waziri Mbene kuwasilini London, Uingereza kwa ziara ya kikazi.
  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mama Janeth Mbene, akiongea na Wafanyabiashara na Wawekezaji katika katika Mkutano ulioandaliwa na Jumuiya ya East African Association na Kituo cha Biashara, London. Mkutano huo uliokuwa na lengo la kuwakutanisha Wawekezaji hao wenyenia ya kuwekeza na kufanyabiashara na Tanzania katika sekta mbalimbali kama vile, Kilimo, Umeme, Madini, Elimu na Afya.
  Naibu Waziri Janeth Mbene (pili kushoto), Naibu Balozi wa Tanzania, Uingereza, Bwana Msafiri Marwa (wa kwanza kushoto ), Dada Magdalena (Msaidizi wa Naibu Waziri) na Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara, London, Bwana Yusuf Kashangwa, wakiwa kwenye Mkutano wao na Wafanyabiashara na Wawekezaji. Mkutano huo uliofanyika jana jumatatu, tarehe 23 Februari 2015. Picha na Ally Dilunga

  0 0

  Msanii wa kizazi kipya Mwana FA (kushoto) wakipata chai katika moja ya mgahawa New York City kujaribu kukabiliana na kipupwe kinachopuliza jiji la wasiolala wengine katika picha kutoka kushoto ni Dj Rich Maka. NY Ebra na Salah Said.

  0 0  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Chalinze  na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya  Chama cha  Mapinduzi Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa  katika picha ya   pamoja na  Muwakilishi wa Kudumu wa Jamburi ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako  Manongi  (kushoto) na  Naibu Mwakilishi wa  Kudumu,  Balozi Ramadhan Mwinyi. Mhe Ridhiwani Kikwete ( Mb)  alikuwa Jijini New York kwa ziara ya kikazi ambapo pia  alikuwa mgeni  rasmi  katika  hafla ya  miaka 38 ya  kuzaliwa kwa  Chama cha Mapinguzi iliyoandaliwa na Tawi la CCM New York na vitongoji vyake.
  Mhe. Ridhiwani Kikwete ( Mb) akiwa  katika picha ya pamoja na  Mabalozi   na  baadhi ya  maafisa wa Uwakilishi wa  kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa. Mhe.  Ridhiwani Kikwete  pamoja na  kuhudhuria hafla ya   CCM kutimiza miaka 38 pia alipata fursa ya kufika katika Ofisi za Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika  Umoja wa Mataifa, fursa aliyoitumia  kubadilishana  mawazo  na   Maafisa wa Uwakilishi.  

  0 0

  Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia mauaji ya Kimbari ya Rwanda (UN-ICTR) yenye makao yake makuu mjini Arusha imekabidhi msaada wa vifaa vya ki-eletronic vinavyosaidia kuongeza ufanisi wa kazi za kimakahakama kwa Jaji Mkuu wa Mahakama Tazania Mhe. Othman Mohamed Chande katika sherehe fupi iliyofanyika mahakamani hapo Arusha. 
  Vifaa hivyo ni pamoja na mashine 19 ziitwazo Dictaphone Machines na mashine nyingine 19 ziitwazo Transcribers. 
  Viffaa hivyo vilikabidhiwa na Kaimu Mkuu wa Utawala wa UN-ICTR Bwana Emmanuel Kodwo Bartels. Vifaa hivyo vilikuwa vikitumiwa na UN-ICTR katika kazi zake za kila siku. Mahakama hiyo inamaliza kazi zake mwaka huu. 
  Vifaa hivyo vikiwa vipya hununuliwa kwa US$ 5000 (Sh 9 millioni) kila kimoja. UN-ICTR imebakiza kesi moja tu ambayo itamaliziwa kabla ya mwisho wa mwaka huu. Kesi dhidi ya watuhumiwa 93 zimeshamalizwa na mahakama hiyo. 
  Kesi hizo zilijumuisha watu wazito nchini Rwanda wakiwemo mawaziri akiwamo waziri mkuu, wakuu na makamanda wa majeshi, wakuu wa mikoa na wilaya, waandishi waandamizi, wakuu wa madhehebu ya dini na wafanyabiashara wakubwa.
  Jaji Mkuu Mhe.Mohamed  Chande Othman akipokea kifaa kimoja kutoka kwa Bw. Bartels (menye miwani). Wanaoshuhudia ni viongozi wa mahakama hizo mbili wakiwemo (kutoka kushoto) Bw. Danford Mpumilwa, Afisa Habari wa UN-ICTR na Bw. Saidou Guindo, Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa UN-ICTR. Kutoka kulia ni Mama Margaret Shaidi-Ngatunga akifuatiwa na Bw. Richard Lipscombe, kutoka kitengo cha Ugavi cha UN-ICTR. Mwingine ni Bw. Jerry Mburi, Afisa Sheria wa UN-ICTR ( wa nne kulia). 
  Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. John Kahyoza akiweka saini kupokea vifaa hivyo.

  0 0

   Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akiongozana na Mhe. Robert Makaramba alipopokelewa mapema leo katika Uwanja wa Ndege Mwanza, nyuma ni baadhi ya Maafisa wa Mahakama wa Mkoani Mwanza waliofika kumpokea Mhe. Jaji Mkuu.
   Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania (kushoto). akifurahia jambo na Mhe. Jaji Robert Makaramba, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, katika chumba maalum cha wageni (VIP room) alipofika mkoani Mwanza mapema leo tayari kwa ziara ya Kutembelea Mahakama mkoani Tabora atakayoanza rasmi kesho.
   Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, akisaini kitabu cha wageni ktk chumba maalum cha wageni (VIP) katika Uwanja wa Ndege jijini Mwanza. (Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania). 
  Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, akisalimiana na mmoja wa Maafisa wa Polisi Mkoani Mwanza alipowasili katika Uwanja wa Ndege Mwanza mapema leo kwa ajili ya safari ya kuelekea mkoani Tabora kwenye ya KIKAZI,ikiwa ni pamoja na kukagua utendaji kazi wa Mahakama mkoani humo.

  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bibi Amina Masenza aandae orodha ya watumishi wa mkoa huo ambao wamekaa kwenye nafasi za ajira kwa zaidi ya miaka 10 na kumpelekea ili wafanyiwe utaraibu wa kuhamishiwa vituo vingine.

  Ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatatu, Februari 23, 2015) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Iringa waliofika kusikiliza majumuisho ya ziara ya siku sita ya Waziri Mkuu kwenye mkoa huo. Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ulioko Mafinga, wilayani Mufindi.

  “Tafuta wote waliokaa zaidi ya miaka 10. Ni lazima tuwabadilishe... niletee orodha mapema iwezekanavyo,” alisema Waziri Mkuu. Alisema nia ya zoezi hilo ni kuongeza ufanisi kwani watumishi wakikaa sehemu moja kwa muda mrefu wanakuwa butu kwa kukosa ubunifu kwenye kazi zao, wanaota mizizi na kugeuka kuwa chanzo cha matatizo katika baadhi ya sehemu.

  Alimtaka pia Mkuu huyo wa mkoa pamoja na timu yake wasimamie vizuri ukusanyaji wa mapato ili kuongeza kiwango cha mapato cha mkoa huo. “Na siyo hilo tu, simamieni vizuri matumizi ya fedha zilizopangwa kwenye miradi mbalimbali ili kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi mnaowaongoza,” alisisitiza. Alisema mkoa wa Iringa ni wa pili kwa kuwa na kiwango cha juu cha pato la mwanachi wa kawaida baada ya Dar es Salaam ambao ndiyo unaongoza nchini. “Katika taarifa ya Mkuu wa Mkoa, tulielezwa kwamba pato la mwananchi wa Iringa katika mwaka 2013 lilikuwa ni wastani wa shilingi 1,660,532/- ambazo ni sawa na shilingi 138,377/- kwa mwezi au shilingi 4,612/- kwa siku”.

  Alisema pato la mwananchi wa Iringa linakua vizuri ikilinganishwa na mwaka 2006 ambapo pato hilo lilikuwa shilingi 589,607/- na limeongezeka hadi kufikia shilingi 1,660,532/- mwaka 2013. Alivitaja viashiria vya kukua kwa uchumi kuwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba za kisasa zenye umeme, elimu bora, afya bora na upatikanaji wa vifaa vya mawasiliano kwenye ngazi ya kaya.

  Alisema kulingana na taarifa ya Shirika la Fedha Duniani (IMF), Tanzania imeondolewa kutoka miongoni mwa nchi 10 barani Afrika zenye umaskini mkubwa na kwamba sasa Tanzania ni miongoni mwa nchi 20 duniani ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kubwa. “Kukua kwa pato la mkoa kumechangiwa hasa na kuwepo kwa mashamba makubwa ya tumbaku, chai, viwanda vya chai, misitu na viwanda vya mbao. Tukitumia vizuri fursa hizi, na tukijipanga vizuri tutaweza kuongeza pato la mkoa kuzidi hapa tulipo,” alisema.

  Aliwataka watendaji wote katika ngazi zote, wawe na dhamira ya kuwaletea wananchi maendeleo na hivyo kuwaondolea umaskini na kuongeza pato lao kwa kila mmoja. “Ninawasihi sana viongozi wa mkoa tutangulize maslahi ya wananchi na siyo maslahi yetu binafsi. Tukifanya hivyo, wananchi wataona kweli tunawasaidia na tunastahili kuwaongoza,” aliongeza.

  Waziri Mkuu amemaliza ziara ya siku sita katika mkoa wa Iringa na leo anakwenda Makambako, Njombe kuzindua uandikishaji wa Daftari la Mpiga Kura. Baadaye mchana, ataelekea Mbeya kuanza ziara ya kikazi ya siku sita kukagua shughuli za maendeleo katika mkoa huo.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMANNE, FEBRUARI 24, 2015.

  0 0

  Balozi wa Tanzania kwenye nchi za Nordic na Baltiki, Mhe. Bibi Dora Mmari Msechu akiwa na Naibu Mkuu wa Itifaki Bi Annete Lassen, baada ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa  Mtukufu Malkia  Margrethe II wa Denmark tarehe 20 Februari 2015. 
   Picha ya pamoja na Mkuu wa Kasri la Malkia  baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho.    


  0 0

  TA1
  TA2
  Mkuu wa Idara ya Cartels (Makubaliano yanayodhirisha ushindani) kutoka Tume ya Ushindani Dar es Salaam,Shedrack Nkelebe akisisitiza jambo kwenye semina hiyo iliyohusisha wataalamu wa manunuzi na ugavi kutoka taasisi mbalimbali juu ya manunuzi yanayozingatia thamani (Value for Money) iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort mjini Tanga.
  Habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0  0 0

   Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava.
  Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
  Matokeo ya utekelezaji wa utoaji wa ruzuku kwa wachimbaji Madini wadogo nchini Awamu ya Pili yanatarajiwa kufanyiwa tathmini na ufuatiliaji kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

  Hayo yamebainishwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava wakati akiongea katika Kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa kupitia Televisheni ya Taifa TBC1 mapema leo, ambapo amefafanua kuhusu taratibu za maombi ya namna ya kupata ruzuku kwa wachimbaji wadogo wa madini Awamu ya Pili.

  Mhandisi Mwihava ameeleza kuwa, ili kupata matokeo bora ya namna ruzuku hiyo itakavyotumiwa na wachimbaji wadogo watakaokidhi vigezo vya maombi na kunufaika na ruzuku hiyo, mpango wa BRN utatumika ipasavyo kuhakikisha kwamba fedha hizo zinatumika kama ilivyopangwa.

  “BRN itatumika kufuatilia utekelezaji wa ruzuku. Wizarani tuna Sehemu ya Ukaguzi wa Migodi, lakini pia tuna Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), hawa wote watashirikiana kufanya tathmini yenye matokeo tunayotarajia,” amesisitiza Mhandisi Mwihava.

  Ameongeza kuwa, kiwango cha ruzuku kwa wachimbaji wadogo Awamu ya Pili kimeongezwa kufikia Dola za Marekani 100,000/-, ruzuku ambayo inalenga katika kuendeleza uchimbaji mdogo ili uwe na tija; kuwakwamua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuongeza pato la taifa.

  Aidha, ameeleza kuwa malengo mengine ya ruzuku hiyo kwa wachimbaji wadogo wa Madini kuwa ni kuendeleza mkakati wa kurasimisha shughuli za uchimbaji mdogo wa madini na kutoa mitaji ili kusaidia ukuaji wa tasnia ya uchimbaji mdogo wa madini.

  Malengo mengine ni pamoja na uongezaji thamani ya madini wenye Matokeo Makubwa Sasa.

  Ameongeza kuwa, Serikali imedhamiria kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini kuwawezesha kuwa wachimbaji wa kati, jambo ambalo limefanya Serikali kuzifanyia kazi changamoto zilizojitokeza katika utoaji ruzuku na mikopo awamu ya kwanza.

  “Tunataka kuwasaidia mitaji, kuwapatia vifaa na kuhakikisha wanapata uelewa wa namna ya kufanikisha shughuli zao kupitia wataalamu wetu. Tunalenga kuwafanya wakue hadi kuwa wachimbaji wakubwa”, ameongeza Mwihava.

  Aidha, Mhandisi Mwihava ametumia fursa hiyo kuwataka wachimbaji wadogo kuzitumia ofisi za madini zilizoko mikoani kwa ajili ya kuchukua fomu za maombi kuanzia tarehe 2 Machi na kuwataka kuzirejesha fomu hizo katika ofisi hizo ifikapo tarehe 27 Machi, 2015, zikiwa na viambatanisho vyake.

  Katika hatua nyingine, Mhandisi Mwihava amesema kuwa, migodi inayoshirikisha watoto wadogo katika shughuli za uchimbaji madini watanyanga’nywa leseni zao endapo itabainika kuwa, migodi hiyo inawashirikisha watoto, na hivyo kuwataka wachimbaji kufuata sheria na taratibu.

  “Watoto kushiriki katika shughuli za uchimbaji ni makosa. Watakaobainika watanyang’anywa leseni zao. Wizara inapinga si haki kwa watoto kufanya shughuli za uchimbaji madini”, alisisitiza Mwihava.


  Awamu ya pili ya utoaji ruzuku kwa wachimbaji wadogo nchini, inatekelezwa kupitia Wizara ya Nishati na Madini, chini ya Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), unaopata fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia.


  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu mapambano ya kukomesha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino),Said Ndonge akiwa na wajumbe wa kamati hiyo, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maandamano wanayotarajia kuyafanya Machi 3 Mwaka huu jijini Dar es Salaam. (Picha Emmanuel Massaka).
  NA Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii.

  Kamati ya kuratibu mapambano ya kukomesha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino)umepingana na kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ulemavu Ngozi Taifa, Bw. Ernest Kimaya kuwa kamati iliyoandaa matembezi ya hisani ni ya watu wahuni.


  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw, Said Ndonge amesema kauli ya mwenyekiti wa Taifa  ni ya ubaguzi na inatoa nafasi ya adui kuendelea kwa mauaji ya jamii yetu.


  Amesema tangu mwaka 2006  waliouwawa ni 76 na 15 kubaki na ulemavu wa kudumu "Hivyo sisi wanaharakati wa kupambana na kukomesha udhalimu huu tunaendelea kulaani vitendo wanavyotutendea baadhi ya jamii yenye imani potofu za kishirikina.


  Kamati hiyo imesema haiutambi umoja wa chama cha AlbinoTanzania kutokana na viongozi wake kushindwa kusimamia majukumu yake na badala yake kutaka kuleta mfumo wa kubaguana na kumfanya adui apate nafasi kutushambulia. 
  Hata hivyo, Bw. Ndonge amesema maandamano yako palepale kutokana na Jeshi la Polisi kutoa ulinzi kwa siku ya maandamano  yanayotarajiwa kufanyika Machi 2 mwaka huu.

  Kamati hiyo imetaka wadhili wajitokeze kufadhili maandamano hayo katika kuokoa watu wenye ulemavu wa ngozi.


  0 0

   DJ Tee (19) ni kijana mwenye ndoto kubwa katika maisha yake. Baada ya kuona mahangaiko ya vijana kuelekea kwenye mafanikio, wengi wakiwa wamemaliza shule na vyuo bila kupata kazi, ameamua kuunda redio stesheni ghetoni kwake aliyoipa jina la Shujaaz, ili aweze kushea ideas na vijana wote nchini Tanzania kuhusu mbinu mbalimbali za kuingiza pesa, kuwapa stori za vijana wanaochakarika katika maisha yao pamoja na kuwaburudisha. 

  "Nimeamua kuiita Shujaaz kwa sababu, naamini kuwa kijana ambaye anajituma na kuweka mfano bora kwenye jamii ni shujaa". Alisema DJ Tee. "Ndoto zangu zinakaribia kuwa kweli".

  Story ya kijana huyu inapatikana kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kupitia kijarida cha Shujaaz, kitakachokuwa kinasambazwa kupitia gazeti la Mwanaspoti, kuanzia JUMAMOSI HII ya tarehe 28. Kwenye kijarida hicho, utapata ideas mbali mbali ambazo vijana wanaweza kuzifuata na kujiingizia kipato. Pia, kutakuwa na stori za vijana wengine kama Pendo, Semeni na Pepe ambao ni mashabiki wakubwa wa DJ Tee na redio show yake ya Shujaaz.

  Kijana huyu ameamua kujiita DJ Tee ili asijulikane na watu wake wa karibu, kwa kuwa ana-hack airwaves za redio stesheni ili aweze kusikika. Sikiliza redio stesheni uipendayo kuanzia wiki ijayo, huwezi jua, inawezekana DJ Tee akawa hewani!

  Wewe pia USIKOSE kuwa sehemu ya mafanikio na harakati za kijana huyu kwa kujiunga naye. Pata nakala yako ya Shujaaz kuanzia Jumamosi hii (28/02/2015) kupitia gazeti la Mwanaspoti. Pia, jiunge naye kwenye ukurasa wake wa Facebook kwa jina DJTee255 ili upige naye story na wewe uweze kushea idea zako za hustle. Unaweza pia ukampata Instagram na Twitter kwa jina@djtee255  0 0

  Heineken Tanzania Country Manager Michael Mbungu (third from left in grey suit) looks on as Mrs Jackie Mlatie pops a bottle of champagne to signify the official launch of Club 777, in Kawe Dar es salaam. He is flanked by Mr. Femin Mabachi (extreme right), the group CEO of Club 777. Looking on from left are Heineken Brand ambassodors Irene Jackson and Nuru.
  Heineken Tanzania Country Manager Michael Mbungu (first from left in grey suit) is all smiles as Mr. Mlatie Assey gives a toast to signify the launch of a new hotspot in town Club 777 which located in Kawe, Dar es Salaam.


  0 0


older | 1 | .... | 750 | 751 | (Page 752) | 753 | 754 | .... | 3286 | newer