Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 749 | 750 | (Page 751) | 752 | 753 | .... | 3286 | newer

  0 0


  0 0

  Karibu Cultural Promotions Organization in collaboration with Legendary Music Entertainment and Promotions Company Limited are organizing the 2nd edition of the “Karibu Music Festival”, an annual Three (03) Days International cultural event aiming at African Culture Promotion to the world, as well as introducing other countries’ culture to Africa, and building up friendship/collaboration opportunities among all participants. In the aspects of music, dance, paintings, theater, crafts, and many others, all artists who can share our passion and goal together, you are welcomed to participate in this event to present your great talents and promote yourself!
  The festival involves International artists from Africa, Europe, America, and Asia who will perform at the main stage and conduct their unique Workshop classes. This will be 100% LIVE performance among 3 days!! It will also feature Musicians selling and showcasing their CDs (Albums), craftsmen and artisans selling unique products, cultural food and drink vendors, Also a Cinema and graffiti venues for more art adventures. The big Live performance stage with the high quality sound system from Legendary Music will be set nearby the College of Arts and Culture Bagamoyo-TASUBA, from 6th(Fri) to 8th (Sun) of November 2015.
   Let us share the wonderful moment on the stage!!!
  APPLICATIONS ONLINE www.karibumusic.org 

  0 0

  Bwa. Hashimu Lema, mfanyabiashara anayemiliki kampuni ya ujenzi ya Comfix, amemtembelea Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, ofisini kwake. Mhe. Mjenga amemfahamisha fursa nyingi zilizopo Dubai na Ukanda wa Ghuba kwenye sekta hii ya ujenzi, ambako kampuni kutoka Tanzania wanaweza kuwa ni mikataba ya ushirikiano nazo katika utekelezaji wa miradi mbali mbali Tanzania. Njia hii pia itasaidia kuwajengea uwezo na kupata mbinu za teknolojia mpya ( technological Transfer).

  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameutaka uongozi wa mkoa wa Iringa uangalie uwezekano wa kuanzisha Halmashauri mpya katika wilaya ya Kilolo kata ya Mahenge na tarafa ya Mahenge kwa sababu ya hali ya kijiografia ya eneo hilo. 
   “Makao makuu ya wilaya hii yako Kilolo kule milimani. Ukitaka kuja huku ni lazima upite kwanza mjini ndipo ufike huku. Hapana! Hatuwezi kuwasaidia wananchi hawa kujiletea maendeleo kwa staili hii,” alisema Waziri Mkuu. 
   Alikuwa akihutubia wakazi wa vijiji vya Nyanzwa na Igunda wilayani Kilolo, jana jioni (Jumamosi, Februari 21, 2015) mara baada ya kukagua mradi wa umwagiliaji wa Nyanzwa ambao ni maarufu kwa kilimo cha vitunguu. Vijiji hivyo viko umbali wa km. 120 kutoka Ipogoro ilipo njia panda ya kwenda Iringa mjini na km. 155 kutoka Kilolo mjini yalipo makao makuu ya wilaya hiyo. 
   Waziri Mkuu alisema kata za tarafa hiyo ni kubwa mno kwa mtendaji kuweza kusukuma maendeleo ya wananchi.
   “Kata hii imeanzia Kitonga hadi huku Nyanzwa. Hivi ni mtendaji gani anayeweza kuja kuhimiza shughuli za maendeleo akitokea huko?” alihoji Waziri Mkuu huku akishangiliwa. 
   Alisema mbali na idadi ya watu, suala la kijiografia huwa linaangaliwa wakati wa kuanzisha maeneo ya utawala. “Hili eneo ni zuri, fursa zipo lakini linakosa usimamizi ndiyo maana hata wilaya hii inaongoza kwa umaskini kuliko wilaya nyingine za mkoa huu. 
  "Acheni wilaya ibaki moja, mbunge abaki mmoja lakini Halmashauri ziwe mbili ili muweze kusukuma maendeleo ya eneo hili kwa sababu mtakuwa na madiwani wenu na bajeti yenu,” alisema. Mapema, akisoma taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Mtendaji wa Kijiji cha Nyanzwa, Bw. Hekima Masanula Katemo alisema skimu ya umwagiliaji ya Nyanzwa ilijengwa mwaka 1960 wakati huo kwa kutumia banio la miti na magunia ya mchanga. 
  Ilikuja kuboreshwa miaka ya 90 kwa ufadhili kutoka Jumuiya ya Ulaya na Serikali ya Sweden. 
   “Hata hivyo, skimu hii ambayo inahudumia wakulima 3,469 wakiwemo wanaume 1,662 na wanawake 1,807; inakabiliwa na uhaba wa maji kwani ni hekta 256 tu ambazo zinamwagiliwa kwa sasa wakati eneo lote la mradi ni hekta 940,” alisema Bw. Masanula. 
   Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake mkoani Iringa kwa kutembelea Manispaa ya Iringa ambako atakagua ujenzi wa maabara kwenye shule ya sekondari Kihesa, kuzindua kituo cha polisi cha Semtema, na kukagua huduma za afya kwenye hospitali ya manispaa ya iringa. 
  Pia atakagua mradi wa machinjio ya kisasa ya Ngelewela kabla ya kutubia mkutano wa hadhara kwenye viwanja wa shule ya msingi Ipogolo. 

   IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI
   MKUU, JUMAPILI, FEBRUARI 22, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wauguzi wa hospitali ya Manispaa ya Iringa iliyopo eneo la Frelimo baada ya kuitembelea na kuzungumza na wananchi hospitalini hapo akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 22, 2015
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wananchi na watumishi wa  Hospitali ya Manispaa ya Iringa iliyopo Frelimo baada ya kuitembelea akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 22, 2015.Wapili kulia ni Mkewe Tunu na kulia ni Mbunge wa Iringa, Mchungaji  Peter Msigwa
    Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akimpongeza, Gaudencia Malangalizi  ambaye amejifungua watoto mapacha wa kiume katika hospitali ya Manispaa ya Iringa iliyopo eneo la Frelimo  Februari 22, 2015. Mama Pinda aliambatana na Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda ambaye alitembelea hospitali hiyo.
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua Kituo cha Polisi cha SEMTEMA kilichopo Iringa Mjini ambacho kimejengwa na Mbunge wa Viti Maalum, Ritta Kabati (wapili kushoto) Februari 22, 2015. Mheshimiwa Pinda yuko katika ziara ya mkoa wa Iringa. Watatu kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Lediana Mng'ong'o.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwasalimia walimu wa Shule ya Sekondari ya Kihesa, Iringa mjini  kabla ya kukagua ujenzi wa Maabara na kuhutubia wananchi akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 22, 2015

  0 0


  0 0

  Na Othman Khamis Ame, OMPR
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa agizo kwa Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Zanzibar kuufutia hati ya matumizi ya ardhi Mfuko wa kuhudumia Watoto yatima Zanzibar { Zanzibar Children Fund } iliyopewa katika eneo la mawe mazito liliopo Vitongoji Chake chake Pemba. 
  Alisema eneo hilo la Hekta 20 ndilo pekee lililobakia Kisiwani Pemba linalotumiwa na Wizara ya Miundo mbinu na Mawasiliano kwa ung’oaji wa mawe mazito yanayotumiwa katika miundo mbinu ya ujenzi wa mawasiliano ya Bara bara.
  Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo wakati alipofanya ziara fupi ya kukagua eneo la Mawe mazito na kuiagiza Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati kufanya utaratibu mara moja wa kuupatia sehemu nyengine Mfuko huo ili uendelee na malengo yake iliyojipangia. 
  Alisema uamuzi huo wa Serikali umekuja baada ya eneo la Hekta 133 lililotengwa na Serikali kwa ajili ya shughuli ya uchimbaji mawe mazito Kisiwani Pemba kumalizika kwa rasilmali hiyo muhimu kwa ujenzi wa miundo mbinu ya bara bara. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza kwamba Ardhi ni Rasilmali ya Taifa. 
  Hivyo Serikali wakati wote ina haki na wajibu wa kulitumia eneo la Ardhi popote pale Nchini kwa maslami ya Jamii nzima. Mapema Afisa Mdhamini Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Pemba Nd. Hemed Salum alisema kwamba eneo hilo la Hecta 20 za ardhi walizopewa Mfuko huo wa Kuhudumia Watoto Yatima Zanzibar ni miongoni mwa Hekta 133 zilizotengwa maalum ya Serikali kwa kazi ya uchimbaji wa Mawe mazito. 
  Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipata wasaa wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa Bara bara ya Wete Gando na Gando Ukunjwi unaosimamiwa na Kampuni ya Mecco ambapo Mwakilishi wa Kampuni ya MECCO Bwana Abdullkadir Moh'Bujeti alimueleza Balozi Seif kwamba wahandisi wa ujenzi wa Bara bara hiyo wanaendelea na harakati za ujenzi katika kiwango cha kuridhisha.
   Eneo la Mawe Mazito la Hecta 20 liliopo Vitongoji  chake chake Pemba ndilo pekee lilopbakia Kisiwani humo kwa ajili ya upatikanaji wa rasimlali ya jiwe kwa ujenzi wa miundombinu ya bara bara.
   Afisa Mdhamini Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Pemba Nd. Hemed Salum wa pili kutoka kulia akimpatia maelezo Balozi Seif aliyefika kukagua eneo la mawe mazito ambalo liko chini ya dhamana ya Mfuko wa Kuwahudumia Watoto Yatima Zanzibar Hapo Vitongoji Chake chake Pemba.
  Wa kwanza kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Mwanjuuma Majid na Mwakilishi wa Kampuni ya Mecco Bwana Abdullkadir Mohamed Bujeti.
  Mwakilishi wa Kampuni ya ujenzi wa Miundombinu ya Bara bara ya Mecco Bwana Abdullkadir Moh’d Bujeti akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hatua iliyofikiwa ya kukamilika kwa ujenzi wa Bara bara Tatu zaMkoa wa Kaskazini Pemba. Picha na OMPR, ZNZ.

  0 0
 • 02/23/15--01:00: FOR SALE: LAND ROVER
 •  LAND ROVER   DISCOVERY 2/3  TD5         
  MODEL: 2004
  DIESEL 2.8 ,MANUAL, MILEAGE: 87000FULL A/C, POWER WINDOW, CENTRAL  LOCK, FOUR WHEEL DRIVE IN VERY GOOD CONDITION , JUST BEEN
   IMPORTED  FROM THE UK   
  CAR LOCATION : DAR ES SALAAM

   DUTY HAS BEEN DULY PAID             

   Front view
   Side view

  PRICE: TSH 30  MILLION  

    FOR MORE INFORMATION CONTACT : 

  0 0

   Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali,Dkt. Mohamed Ally Mohamed (katikati) akizindua rasmi Ripoti ya tafiti ya hali ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa Watu wa makundi maalum wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kuitambulisha Ripoti hiyo,uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Protea Courtyard,jijini Dar es salaam.Wengine pichani ni kutoka kulia ni Mraribu Idadi ya Watu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Makyao,Meneja Msaidizi wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP),Dkt. Robert Josiah,Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dkt. Fatma Mrisho pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa PSI-Tanzania,Romanus Mtung'e.
   Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali,Dkt. Mohamed Ally Mohamed (katikati) akimkabidhi Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dkt. Fatma Mrisho Ripoti ya tafiti ya hali ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa Watu wa makundi maalum mara baada ya kuzinduliwa rasmi leo kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Protea Courtyard,jijini Dar es salaam.Kulia ni Meneja Msaidizi wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP),Dkt. Robert Josiah.
  Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali,Dkt. Mohamed Ally Mohamed (katikati) akimkabidhi Meneja Msaidizi wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP),Dkt. Robert Josiah Ripoti ya tafiti ya hali ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa Watu wa makundi maalum mara baada ya kuzinduliwa rasmi leo kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Protea Courtyard,jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dkt. Fatma Mrisho .
  Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali,Dkt. Mohamed Ally Mohamed (katikati) akiwa pamoja viongozi wa taasisi mbali mbali za kupambala na Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) mara baada ya  uzinduzi rasmi wa Ripoti ya tafiti ya hali ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa Watu wa makundi maalum (walizozishika mikononi) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kuitambulisha Ripoti hiyo,uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Protea Courtyard,jijini Dar es salaam.viongozi hao ni pamoja na (kutoka kulia kwenda kushoto) Muwakilishi wa Sauti ya Watanzania,Hally Mahley, Mraribu Idadi ya Watu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Makyao,Meneja Msaidizi wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP),Dkt. Robert Josiah,Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dkt. Fatma Mrisho pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa PSI-Tanzania,Romanus Mtung'e.

  0 0

  Katika kuendeleza shughuli zake za huduma kwa jamii kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekabidhi simu za mkononi kama kitendea kazi kwa walemavu waliowezeshwa na Airtel kwa kupatiwa vibanda vya kisasa vya Airtel Money vyenye lengo la kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wajasiriamali na kuwa mawakala wa huduma ya Airtel Money na kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kuuza bidhaa za Airtel kupitia vibanda hivyo vilivyo katika sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.

  Simu hizo zilibabidhiwa kwenye muendelezo wa mafunzo yao ya ujasiriamali yanayofanyika katika ukumbu wa Machinga Complex .

  Akiongea wakati wa hafla ya makabidhiano, Afisa masoko wa Airtel Tanzania Haruna Ndyanabo alisema, “Airtel imeendelea kutoa mchango kwa jamii kwa kuhakikisha walemavu hao wanafikia ndoto zao, kwa kuendelea kuwapatia mafunzo mbali mbali ili kuhakikisha wanakuwa wafanyabiashara madhubuti na tunaamini msaada wetu utasaidia kuboresha maisha yao kwa kuwaongezea uwezo wakujiongezea kipato”.

  “Kwani watu wanaoishi na ulemavu wanakabiliana na hali ngumu ya uchumi kuliko makundi mengine katika jamii” ukizingatia kwamba ulemavu siyo kigezo chakutoweza kufanya kazi.

  Aliongeza kwa kusema “Shabaha ya kampuni ya Airtel hapa nchini sio tu biashara bali pia kuona maisha ya jamii zinazotuzunguka yananufaika na uwepo wetu kazi inayofanywa kupitia mfuko wa jamii wa Airtel na ndio maana tupo mstari wa mbele katika kusaidia nyanda tofauti hapa nchini.

  Simu hizo zilikabidhiwa mbele ya mwenyekiti wa Taasisi ya haki za binadamu na maendeleo ya kiuchumi bw. Abubakar Rakesh.

  Mwenyekiti huyo alisema,” tunayofuraha kuona baadhi ya wenzetu wakiwezeshwa ili kuweza kukidhi mahitaji yao na kuongeza kipato chao.

  Tutaendelea kuwashukuru Airtel kwa misaada yao endelevu na kwa kukiwezesha kikundi hiki kuweza kujiendeleza. Wito wangu kwa wanachama wenzangu ni kutumia nafasi hii vizuri, kuweka jitihada katika kazi zao ili kufanya vyema na kufanikiwa katika biashara zao.”
  Afisa masoko wa Airtel Haruna Ndyanabo (wa pili Kulia) akimkabidhi Rukia Salum (wapili Kushoto) mmoja kati ya walemavu waliowezeshwa na Airtel kwa kupatiwa vibanda vya kisasa vya Airtel Money ili kuweza kijipatia kipato na kuendeleza Maisha yao ya kila siku. Wakishuhudia ni baadhi ya walemavu wengine waliowezeshwa na Airtel katika mtaji huo.
  Afisa masoko wa Airtel Haruna Ndyanabo (kushoto) akimkabidhi Peter Gwikama mmoja kati ya walemavu waliowezeshwa na Airtel kwa kupatiwa vibanda vya kisasa vya Airtel Money ili kuweza kijipatia kipato.
  Afisa masoko wa Airtel Haruna Ndyanabo (Kulia) akimkabidhi Josephine John mmoja kati ya walemavu waliowezeshwa na Airtel kwa kupatiwa vibanda vya kisasa vya Airtel Money ili kuweza kijipatia kipato.

  0 0


  0 0

  Recently, a team of three visiting American art administrators from US State Department sponsored Centre Stage Cultural Exchange Program facilitated a workshop on marketing and branding for Tanzanian performing artists, producers and art administrators at the Alliance Francaise in Dar es Salaam.

  The one day workshop was organized by US Mission Dar es Salaam in Collaboration with Alliance Française in response to felt and expressed need by local artists for enhanced capacity to uplift themselves economically to be able to positively contribute to their communities’ social and economic wellbeing.

  Through brief presentations, plenary discussions and role plays, the team of American art administrators made of Ms. Adrianne Petrillo from New England Foundation for the Arts (NEFA), Deidre Valente from Lisa Booth Management, Inc.

  (LBMI) and Ruth Waalkes from Virginia Tech (Virginia Polytechnic Institute and State University) shared with the participants their experiences and expertise on best marketing and branding practices with a specific focus on the American art market. They also highlighted ways and means through which local artist can create and maintain local, regional and international linkages for them to learn from one another and improve their artistic and business profiles.

  Speaking after the workshop an art reporter and ethnomusicologist Iman Mani said; “The biggest thing we got as artists from this workshop is the need for performing artists to brand themselves. One of the problems facing music development in Africa and more so in Tanzania is that since music is an integral part of life, many people including musicians tend to take it for granted.

  This makes it difficult for them to see the business side of it and the need to brand themselves. This workshop has consolidated an understanding that there is a business side to performing arts and that for artists to succeed in the current competitive global market, they have to take the business side as seriously as they take the artistic side.”

  Attended by 27 Tanzanian artists, producers and art administrators, the workshop also sought to promote the goals of Center Stage Cultural Exchange Program and U.S cultural diplomacy in general amongst Tanzanian’s art practitioners.

  Center Stage is a cultural diplomacy initiative that connects foreign artists with American communities through the performing arts. Among other things, the program provides opportunities for international performing artists in dance, music and theater to tour the United States. U.S Embassy and Alliance Francaise have been working in partnership to promote art and culture in Tanzania with a view to promoting global understanding, peace and prosperity.
  Deirdre Valente from the U.S. State Department sponsored Center Stage Cultural Exchange Program and a Tanzanian Musician and Producer Enrico Figueredo in a role play on 45-seconds elevator pitch during a branding and marketing workshop for performing artists held at the Alliance Française in Dar es Salaam recently.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Mkuranga Mbenjamin Majoya (kushoto)akikabidhiwa msaada wa vifaa vya macho na Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute Eden Mahayo kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi 122 za Mkuranga ambapo wanafunzi hao watapata huduma ya kupima na kutibiwa macho bure.hafla hiyo ilifanyika katika hospitali ya wilaya ya mkuranga mkoa wa Pwani, wanao shuhudia ni Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dkt.Francis Mwanisi, Mratibu mradi Rebecca Kasika na Mratibu wa Taifa wa Huduma ya Macho Dkt.Nkundwe Mwakyusa(wapili kutoka kushoto)
  Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute Eden Mahayo (kushoto)akimuonyehsa mashine ya kutengenezea miwani baada ya kukmkabidhi msaada wa sanduku la vifaa vya kupimia macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4 Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Mkuranga Mbenjamin Majoya kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi 122 za Mkuranga ambao watanufaika na huduma ya kupima na kutibiwa macho bure.hafla hiyo ilifanyika katika hospitali ya Wilaya hiyo.kulia ni Mratibu huduma za macho mkuranga dkt.Gilbert Mrema.
  Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute Eden Mahayo (kushoto) akijaribu kumpima miwani matroni wa Hospitali ya Mkuranga Rosemary Magombola wakati wa hafla ya kumkabidhi wa msaada wa vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4 kwa ajili ya kuwahudumia wanafunzi wa shule za msingi 122 za mkuranga ambao watanufaika na huduma hiyo ya upimaji macho pamoja na matibabu bure. Mkurugenzi wa manispaa ya Mkuranga Kaimu Mbenjamin Majoya (kulia) Mganga Mkuu wa Wilaya ya hiyo Dkt,Francis Mwanisi.


  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Kiongozi wa madhehebu ya Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana akiongea baada ya kumkabidhi hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Kiongozi wa madhehebu ya Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongeqa kwa furaha na Kiongozi wa madhehebu ya Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana akiongea baada ya kumkabidhi hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Kiongozi wa madhehebu ya Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana baada ya kumkabidhi hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam. 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki na Kiongozi wa madhehebu ya Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana tayari kwa kumkabidhi hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU

  0 0

  Vijana wa Yamoto Band jumamosi iliyopita Walipiga Bonge moja la Show huko UK London katika Ukumbi wa Royal Regency na kuhudhuliwa na watu kibao wanaoishi huko, Hizi ni picha za matukio katika Show Hiyo.Pichani wakiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza,Balozi Peter Kallaghe pamoja na mwanadada Jestina George.
  Dogo Asley akifanya yake stejini.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali Kuu ya Mnazmmoja Dkt. Jamala Adam Taib akizungumza na Mkuu wa Chuo cha Biashara cha Dar es Salaam Prof. Emanuel Amani Mjema wakati wa hafla ya makabidhiano ya mashuka ya wodi ya akinamama na watoto ikiwa ni maadhimimisho ya miaka 50 tokea kuanzishwa chuo hicho.
  Mkuu wa Chuo cha CBE Prof. Emanuel Amani Mjema akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Maalim Abdalla Mwinyi msaada wa mashuka uliotolewa na chuo hicho kwa ajili ya Hospitali Kuu ya Mnazimmoja katika hafla iliyofanyika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja mjini Zanzibar.
  Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis katika picha ya pamoja na watendaji wakuu wa Chuo cha CBE na baadhi ya maafisa wa Hospitali ya Mnazimmoja.
  Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Maalim Abdalla Mwinyi Khamis akiagana na Mkuu wa Chuo cha CBE baada ya kukabidhiwa mashuka kwa ajili ya wodi ya wanawake na watoto Hospitali Kuu ya Mnazimmoja ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

  Gavana wa Benki Kuu nchini,Profesa Beno Ndulu amesema kazi milioni 885 za nchi ya jamhuri ya watu wa China wameshindwa kuziendesha,hivyo Tanzania inaweza kufaidika na kazi hizo katika kuongeza pato la taifa kwa sekta ya viwanda.

  Profesa Ndulu ameyasema hayo leo katika warsha ya kujadili chamgamoto na jinsi ya kukabiliana nazo kwa ukuaji wa Uchumi kutokana na rasilimali zilizopo nchini.

  Amesema pato  la taifa katika sekta ya viwanda limezidi kukua kwa dola  za Marekani milioni 1.3 hiyo ni tofauti  na miaka 10 iliyopita,hivyo kutokana na hali hiyo sekta ya viwanda itazidi kuongeza  pato la taifa kuliko ilivyo sasa.

  Amesema sekta nyingine inayoongeza pato la taifa ni sekta ya usafirishaji ambayo imechangia pato la taifa dola za Kimarekani milioni 8.6.

  Kwa upande wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (PAC),Zitto Kabwe amesema  uchumi umeshuka na uchumi uliopo unashikiliwa na watu wachache ambao ni wafanyabiashara 

  Amesema serikali iweke kipaumbele katika kilimo kutokana na kuwa na hali mbaya ya kiuchumi na wananchi wasifurahie kuwepo hali ya uchumi iliyopo sasa.


  0 0

  Na Ferdinand Shayo,Arusha.
  Wanahabari kutoka vyombo mbali mbali vya habari nchini wametembelea kituo cha watoto yatima cha Huruma Children  Center kilichopo Mtaa wa Morombo  na kuwafariji pamoja na kuwapeleka zawadi.

  Katika Ziara hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya jamii media ambao ni wamiliki wa  jamiiblog.co.tz  ililenga kuwakutanisha Wanahabari na makundi maalumu katika jamii ikiwa ni njia ya kujitoa kwa jamii na kuwa faraja kwa waliokosa faraja.

  Mkurugenzi wa Jamii media ,Pamela Mollel amesema kuwa mbali na kuripoti matukio mbali mbali yanayojiri nchini Wanahabari wana jukumu la kuisaidia jamii kwasababu wao ni sehemu ya jamii .
  Pamela Mollel ameeleza kuwa suala la kujitoa kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ni jukumu la kila Mtanzania ili kuwasaidia kuwa na maisha bora na kuisaidia jamii pia.

  Mwandishi wa Kituo cha TV 1 Mkoani hapa Jane Edward ameeleza kuguswa na watoto hao wenye vipaji lukuki ambavyo vikiendelezwa wanaweza kuwa tunu ya taifa na kuliletea taifa ushindi katika sanaa na michezo.
  “Watoto hawa licha ya kuwa yatima wana uwezo mkubwa ambao ukitumiwa vizuri unaweza kulisaidia taifa letu wengine ni wabunifu mashirika binafsi ,serikali na mtu mmoja mmoja kuwaunga mkono watoto hao” Alisema Jane Edward 

  Mmiliki wa blogu ya Wazalendo 25 Blog Bw. Gadiola Emmanuel anasema kuwa ni wakati sasa kwa wanahabari kuwa mfano wa kuigwa katika kuisaidia jamii na kuongoza mabadiliko wanayoyataka kuyaona badala ya kuwa wasemaji peke yake hususani katika masuala ya kijamii ushiriki wao utaleta mabadiliko chanya na ushawishi mkubwa.
   Waandishi wa Habari wa Arusha wakitoa Zawadi zao za "Valentine's day" kwa watoto wa kituo cha Huruma Children's Trust Kwa Morombo, Jijini Arusha, kama ishara ya Upendo na Kuwajali watoto yatima katika siku hii muhimu ya Wapendanao. Kushoto aliyesimama ni Mratibu wa Shughuli hiyo Bi. Jane Edward Kutoka TV1 -Arusha. Zawadi hizo zilitolewa Tarehe 14.02.2015 Jumamosi.
   Wakurugenzi wa Wazalendo 25 Blog Bw. Gadiola Emanuel na Jamii Blog Bi. Pamela Mollel tukitoa zawadi kwa mmoja wa watoto wa Huruma Children's Trust Centre Kwa Morombo, Jijini Arusha. kama ishara ya Upendo katika Sherehe ya siku ya wapendanao
   Mwandishi wa Habari wa Tanzania Daima Bw. Ferdinand Shayo na Mwandishi Huru na Mmiliki wa Blog ya Wazalendo 25 Blog Bw. Gadiola Emanuel Wakishusha mzigo ambao ni moja ya zawadi ya Upendo kwa Watoto yatima wa Kituo cha Huruma Children's Trust Centre, Kwa Morombo, Jijini Arusha. Tarehe 14/ 2/2015 Jumamosi.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu(AfCHPR)Jaji Augustino Ramadhani(kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Naibu Mwakilishi Mkazi wa taasisi ya kimataifa “La Francophonie” katika Umoja wa Afrika(AU)yenye makao yake Addis Ababa,Ethiopia,Cecile Folchini kwenye ofisi za Mahakama ya Afrika jijini Arusha leo.
  Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu(AfCHPR)Jaji Augustino Ramadhani(wa pili kulia)akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mwakilishi Mkazi wa taasisi ya kimataifa “La Francophonie” katika Umoja wa Afrika(AU)yenye makao yake Addis Ababa,Ethiopia,Cecile Leque Folchini(kulia)kushoto ni Msajili wa mahakama hiyo,Dk Eno Robert na Mkurugenzi wa Alliance Francaise d'Arusha,Gaelle Lapostolle.

  0 0

  Baada ya kugundua kuwa ujenzi wa nyumba hii iliyopo Bomang'ombe mkoani Kilimanjaro umeingia kwenye kiwanja chake ,mmiliki wa eneo hilo aliamua kujenga ukuta kuzunguka kiwanja chake na alivyofika katika nyumba hii alipitisha ukuta wake mlangoni.


  Ukuta ukapita sebuleni mwa nyumba hiyo na kutokea nyuma ya nyumba.Na Hii ndio waswahili wanasema dawa ya Kiburi Jeuri.


  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Mkuu Mpya wa Wilaya ya Kinondoni,Paul Makonda (kulia) akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Mh. Said Meck Sadick leo jijini Dar.

older | 1 | .... | 749 | 750 | (Page 751) | 752 | 753 | .... | 3286 | newer