Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 748 | 749 | (Page 750) | 751 | 752 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Karume huko Pemba na kupokewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Ndugu Mwanajuma Majid Abdalla tarehe 20.2.2015. Mama Salma alialikwa Pemba kama Mgeni Rasmi kwenye sherehe ya Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) iliyoandaliwa na Al-Madrasat Jabal- Hiraa.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kumpokea wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Karume huko Pemba kwa ziara ya kikazi ya siku moja kisiwani humo tarehe 20.2.2015.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi kwa kuvishwa shada na wasichana wa Almadrsat Jabal-Hiraa mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Shule ya Utaani huko Wete Pemba ilikofanyika sherehe ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) ambapo Mama Salma Kikwete alikuwa mgeni rasmi tarehe 20.2.2015.


  0 0

  Balozi wa kinjwaji cha Baileys katika Usiku wa Warembo ndani ya Kiota cha Samaki Samaki,Vanessa (mwenye nguo nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na warembo katika kiota cha Samaki Samaki mtaa wa Samora Jijini Dar es Salaam,ikiwa ni muendelezo wa kuwaleta pamoja warembo wote hapa mjini.
  Wateja waliofika katika kiota cha Samaki samaki katika siku ya warembo wakiwa wanawaangalia warembo hawapo pichani.
  Balozi wa Baileys,Rahma Zumba (wa tatu kulia) akiwahudumia wateja waliofika katika kiota cha Samaki Samaki Mtaa wa Samora Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya "Bongo Flava, Shilole na wacheza show wake, wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka msanii mwenzao wa Bongo Flava, Mez B, mzaliwa wa Dodoma, wakati wa bonanza lililoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Februari 20, 2015. Bonanza hilo lilipambwa na michezo mbalimbali kama vile, soka, netibole, voliboli na muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiongozwa na balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto wa Mjomba band. Wasanii wengine ni pamoja na Chege na Temba na Mr. Blue. Mez B, ni mzaliwa wa mkoa wa Dodoma, ambaye alifariki leo saa tano kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma, alikokuwa akipatiwa matibabu. Anatarajiwa kuzikwa Jumatatu ijayo Februari 23.
  Mrisho Mpoto, a.k.a Mjomba, ambaye pia ni balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akiburudisha wanachuo na watu wengine waluohudhuria bonanza hilo 
  Chege(kulia) na Temba
  Wanachuo na watu wengine wakipagawishwa na muziki uliokuwa ukiungurumishwa kwenye bonanza hilo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI 

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kuufungua Msikiti Mpya wa Kijiji cha Kiongoni Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja na kuanza rasmi shuhuli za Ibada (kulia) Mkuu wa Mkoa Kusini Dk.Idriss Muslim Hijja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa nne kushoto) pamoja na Mashekhe na Viongozi na Waislamu mbali mbali wakiitikia dua iliyoombwa baada ya Swala ya Dhuhuri iliyoongozwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji (kulia) baada ya ufunguzi wa Msikiti Mpya katika Kijiji cha Kiongoni Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.


  0 0

  Trevo ni nini

  ·         Bidhaa kutoka Marekani ambayo ndani yake kuna virutubisho 174

  ·         Trevo imethibitishwa na ORAC,Cap-e ,Halal,Kosher,Vegetarian,na TFDA

  Trevo Inaimarisha

  ·         Ufahamu wa kiakili-mental focus

  ·         Kudhibiti uzito- weight management

  ·         Afya ya moyo- Blood pressure and Heart health

  ·         Afya ya seli

  ·         Afya ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula - digestion system

  ·         Afya ya mfumo wa neva za fahamu - nervous system

  ·         Afya ya mfumo wa kinga ya mwili -immune system

  ·         Afya ya mifupa na viungo

  ·         Afya ya mfumo wa damu - blood circulation

  ·         Afya bora ya mwili mzima

  ·         Nishati ya kutosha mwilini

  ·         Kuongeza nguvu mwili

  ·         Afya ya sukari damuni- Blood sugar level

  ·         Kuongeza CD4 kwa wagonjwa wa HIV/Aids

  ·         Kusaidia wenye vidonda vya tumbo na magonjwa ya kina mama

  Fursa ya Biashara

  ·         Fursa ya biashara ya kimataifa bila mipaka ya nchi

  ·         Gharama ya kuanza biashara ni sh 389,200

  ·         Kwa kila Msambazaji mpya unamuingiza kwenye mtandao unalipwa kati ya sh 100,000 na Sh 800,000

  ·         Kuna njia nane za kutengeneza hela na Trevo

  ·         Trevo ina miezi mitatu tu nchini Tanzania ,hivyo fursa ya biashara ni nzuri sana

  ·         Nafasi ya kufikia ndoto zako kuwa mfanyabiashara wa kimataifa na kufikia malengo ya kweli


  Jipatie Trevo Leo na Uimarishe Afya Yako.Tembelea tovuti ya Trevo www.trevo.co.tz.     AU  Tupigie simu kupitia +255 767 059 211 .Unaweza acha ujumbe mfupi .


  Bidhaa inasambazwa popote Tanzania NA nje ya nchi .Kujiunga na Biashara hii tupigie simu hapo juu au tuandikie kemikoku@gmail.com


  0 0

  Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Sita ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Saada Mkuya akitoa hotuba kwa wahitimu hawapo pichani ambapo mewataka wajiajiri wenyewe badala ya kutegemea Serikali.
  Baadhi ya Wahitimu wa Fani ya Upishi wakiwa wanamsikiliza Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Saada Mkuya hayupo pichani wakati wa sherehe ya Mahafali ya Sita ya Chuoni hapo.
  Mwanafunzi Bora Chuoni hapo wa Fani ya Mapokezi ya Wageni “Front Office”Said Shaame Khamis akipokea Zawadi kutoka kwa Mgeni Rasmi Waziri wa fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Saada Mkuya katika Mahafali hayo Yaliyofanyika Maruhubi mjini Zanzibar.


  0 0

  Umati mkubwa wa waombolezaji leo Jumamosi February 21, 2015 wamejumuika na familia ya Mzee Geofrey Gondwe katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele Marehemu Faith Catherine Gondwe, dada yetu aliyeaga dunia ghafla Jumanne iliyopita nyumbani kwao Baahari  Beach jijini Dar es salaam. Ujumbe wa sauti wa kurekodiwa kutoka kwa Mzee Gondwe ambaye yuko India kwa matibabu kuliwaliza wengi na wakati huo huo uliwafariji pale aliposema "Kufariki dunia kwa Faith ni mapenzi yake Mungu"
  Ibada ya mazishi ikiendelea
  Shada maalumu kwa Faith
  Mke wa Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathia Chikawe, Profesa Amandina Lihamba akiweka shada la maua kwa niaba ya familia yao ambao ni ndugu wa karibu na familia ya Gondwe
  Wanachama wa Jambo Group ambao ni marafiki wa karibu wa baba wa marehemu wakiweka maua kaburini
  Marafiki waliosoma na Marehemu Faith nchini India wakiweka maua kaburini

  0 0

  FAITH CATHERINE GONDWE
  FAMILIA YA BW. GEOFFREY GONDWE INAPENDA KUWASHUKURU WATU WOTE WALIOSHIRIKI KWA NAMNA MOJA AMA INGINE KATIKA KUHITIMISHA SAFARI YA MWISHO YA MTOTO WAO FAITH CATHERINE GONDWE ALIYEFARIKI DUNIA GHAFLA SIKU YA JUMANNE FEBRUARY 17, 2015 JIJINI DAR ES SALAAM, NA KUPUMZISHWA KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE SIKU YA JUMAMOSI FEBRUARY 21, 2015 KATIKA MAKABURI YA JUMUIYA YA MADOLA, KINONDONI.

  FAMILIA YA BW. GEOFFREY GONDWE INATAMBUA KWAMBA SI RAHISI SANA KUMSHUKURU MTU MMOJA MMOJA KWA MSAADA WA HALI NA MALI ALIOTOA KWAO KATIKA WAKATI HUU MGUMU, ILA NI MUHIMU KUTAMBUA MCHANGO MKUBWA ULIOTOLEWA NA KANISA LA ST. GASPER LA MBEZI BEACH, NDUGU, JAMAA, MARAAFIKI NA JIRANI WA FAMILIA, BILA KUASHAU USHIRIKIANO WA KARIBU SANA ULIOTOLEWA NA MWAJIRI WA MAREHEMU FAITH (TANESSCO) PAMOJA NA WANACHAMA JAMBO BROTHERS WA KUNDUCHI JIJINI DAR ES SALAAM.

  BABA WA MAREHEMU FAITH CATHERINE GONDWE, GEOFFFREY GONDWE, AMBAYE YUKO NCHINI INDIA KWA MATIBABU NA MKEWE PAMOJA NA FAMILIA NZIMA YA GONDWE KWA UJUMLA WANATOA AHSANTE NYINGI SANA KWA KILA ALIYESHIRIKI NAO KATIKA MSIBA WA BINTI YAO KIPENZI, FAITH.

  KWA PAMOJA FAMILIA YA GONDWE WANASHUKURU KILA MTU NA KUSEMA KWAMBA MUUMBA WA YOTE MWENYEZI MUNGU AWAJAALIE NA KUWAONGEZEA WALIPOPUNGUKIWA.

  FAMILIA YA GONDWE WANASEMA KUONDOKA KWA FAITH NI KUDURA ZAKE BWANA KWANI NDIYE ALIYELETA NA NDIYE ALIYETWAA. HIVYO KUDURA ZAKE NA ZIHIMIDIWE.

   - AMINA

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla jana alifanya ziara katika Jimbo lake hilo kwa kutumia usafiri wa pikipiki kufika kitongoji cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha Mvomero ambacho kwa historia hakijawahi kufikiwa na kiongozi yeyote tangu uhuru.

  Mbunge huyo ambaye amesifika na kuweka rekodi ya kutembelea vijiji vyote 130 vya Jimbo lake hilo,aliona umuhimu kuwafikia wananchi na wana CCM wa Ifumbo kwa njia ya pikipiki ili ajionee changamoto na kuchukua hatua stahiki ili kukabiliana nazo.

  Makalla alifika kwenye kitongoji hicho cha Ifumba na kulakiwa kwa shangwe na wananchi wa kijiji hicho ambao walifurika kwa wingi kumpokea, na amehaidi kutuma watalaam wa halmashauri wafike na kuiona barabara na kuingiza katika mipango.

  Aidha alikagua ujenzi wa shule ya msingi Ifumbo na kuchangia mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo,pia amesaidia timu ya Ifumbo Star jezi na mpira na kuwahamasisha kujiandikisha kwenye daftari la wapigakura pindi litakapoanza.
  Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiwa amepakiwa kwenye pikipiki (Bodaboda) wakati akielekea kwenye kitongoji cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha Mvomero. 
  Msafara wa Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla kuelekea kitongoji cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha Mvomero. 
  Walifika kwenye kitongoji hicho muda muafaka kabisa na kuandaliwa chai na magimbi.
  Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akikabidhi baadhi ya vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya kitongoji cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha Mvomero.
  Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya vijana wa kitongoji cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha Mvomero.


  0 0

  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (katikati)akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa (NACTE) Dkt. Primus Nkwela,Kamishina wa Elimu Profesa Uestella Bhalalusesa,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara wa wizara hiyo Consolata Mgimba na Mwenyekiti wa barabaza la Taifa la Elimu ya Ufundi Mhandisi Steven Mlote.Hafla hiyo ya Uzinduzi ilifanyika katika makao makuu ya ofisi hizo Mikocheni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Consolata Mgimba wakizinduzi jengo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) uzinduzi huo ulifanyika makao makuu ya NACTE Mikocheni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto)akimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwela wakati alipokuwa akimfafanulia jambo alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani lililopo makao makuu ya ofisi hiyo Mikocheni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


  0 0

   Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Chalinze Bw. Idd Swala (mwenye kanzu), ambaye alimwakilisha mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Ridhiwani Kikwete akikabidhi kwa  wakaazi wa Chalinze misaada ya chakula baada ya  nyumba zao kuharibiwa vibaya kutokana  na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni.


  0 0

  HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni imepitisha Bajeti ya shilingi bilioni 50.1 kwa mwaka 2015/2016 ikiwa ni mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya Manispaa hiyo.

  Akiwasilisha taarifa ya bajeti hiyo mbele ya wajumbe wa mkutano wa maalum wa Baraza la Madiwani Dar es Salaam,Meya wa Manispaa wa Kinondoni, Yusuph Mwenda alisema kuwa mbali ya fedha hizo ambazo ni makusanyo ya ndani pia wanatarajia kupokea shilingi bilioni 128.6 ikiwa ni ruzuku kutoka Serikalini ambayo jumla yake ni shilingi bilioni 180.01.

  Akielezea mchanganuo wa fedha hizo Meya Mwenda alisema kuwa kati ya shilingi bilioni 128.6 za ruzuku ya Serikali, bilioni 101.4 ni kwa ajili ya mishahara, bilioni bilioni 5.9 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida ikiwemo bilioni 1.4 ya fidia ya vyanzo vilivyofutwa.

  Aidha, shilingi bilioni 11.3 ni fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo toka Hazina na shilingi bilioni 9.9 ni ruzuku ya mfuko wa matengenezo ya Barabara kutoka mfuko wa barabara (Tamisemi).

  Meya Mwenda alisema kuwa mpango huo umelenga kufikia dhima ya dira ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa kutekeleza malengo ya Huduma ya Ukimwi na maambukizi mapya kupunguzwa, uboreshaji, uendelezaji na utekelezaji kikamilifu wa Taifa wa kupambana na ukimwi.

  Malengo mengine ni kuimarika kwa upatikanaji na ubora wa huduma za jamii, kuongezeka na kuboreka kwa huduma za kiuchumi na miundombinu ya Halmashauri, Kuimarika kwa utawala bora na utoaji wa huduma, kuimarika kwa uwezo wa kiuchumi na kijinsia na ustawi wa jamii.

  Pia kuimarika kwa uwezo wa kiuchumi na jinsia na ustawi wa jamii, Kuimarika kwa usimamizi wa kujikinga na maafa na milipuko ya magonjwa na Kuimarika kwa usimamizi wa maliasili na mazingira.

  Mwenda alisema kuwa makadirio ya shilingi bilioni 180.01 ni ongezeko la kiasi cha shilingi bilioni 44.5 ambayo ni sawa na 33% ya Bajeti ya 2014/2015, pia shilingi bilini 128.6 za fedha za ruzuku ya Serikali sawa na ongezeko la asilimia 32 na shilingi bilioni 51.2 ni sawa na ongezeko la asilimia 45.

  Hata hivyo Meya Mwenda aliwataka vijana na akina mama wenye sifa za kukopesheka ikiwa ni pamoja na kutimiza masharti ya mikopo wajitokeze kwa ajili ya kukopeshwa fedha zitakazoelekezwa katika kila Kata ambazo ni zaidi shilingi milioni 100 katika shilingi bilioni 3.4 za mkopo wa benki ya DCB.
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akisawilisha Bajeti ya mwaka 2015/2016 ya Manispaa hiyo kwa wajumbe wa mkutano maalum wa Baraza la Madiwani, uliofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Naibu Meya, Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, En. Mussa Nati.
  Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni wakifuatilia kwa makini mkutano wa Bajeti ya mwaka 2015/2016 ya Manispaa hiyo, uliofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wakifuatilia kwa makini wakati wa mkutano wa Bajeti ya mwaka 2015/2016 ya Manispaa hiyo, uliofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  0 0

  Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma (Mabodi) akifungua Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya wawekezaji wa sekta ya Utalii Zanzibar (ZATI) katika Hoteli ya Double Tree by Hilton Shangani Mjini Zanzibar.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya wawekezaji wa sekta ya Utalii Zanzibar (ZATI) Bi. Pamela Mattheuu (aliesimama) akielezea hali ya Utalii ilivyo kwa sasa na kupanga mikakati ya kuitangaza zaidi sekta hiyo, huko Hoteli ya Double Tree by Hilton Shangani Mjini Zanzibar.
  Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya wawekezaji wa sekta ya Utalii Zanzibar Nd. Abdulsamad Said akizungumza na wanachama kuhusu mafanikio na changamoto zinazokabil sekta ya Utalii nchini katika Mkutano Mkuu uliofanyika Hoteli ya Double Tree by Hilton Shangani Mjini Zanzibar.


  0 0

  Na Freddy Maro Chalinze,Bagamoyo.

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana aliwafariji na kuahidi kuzisaidia kaya 40 ambazo nyumba zao ziliharibiwa vibaya na mvua mkubwa iliyoambatana na upepo mkali wiki iliyopita huko Chalinze,wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

  Katika ziara hiyo Rais Kikwete ambaye alikuwa amefuatana na mkewe mama Salma Kikwete alikagua Shule ya msingi Chalinze, Ofisi ya CCM, na nyumba kadhaa za wanakijiji ambazo ziliharibiwa vibaya na mvua hizo na kujeruhi baadhi ya wanavijiji walioangukiwa na nyumba zao.

  “Nimepata taarifa ya maafa yaliyotokea, sikuwepo kwahiyo nimekuja kuwapa pole.Poleni sana Kwa wale ambao nyumba zimeharibika serikali inao utaratibu wa kusaidia.Mkurugenzi akipata taarifa atajua jinsi gani ya kuwasaidia.

  Lakini kuna misaada tunayoweza kutoa.Nasikia Mbunge ametoa msaada wa chakula na dawa pamoja na matibabu.Lakini Kwenye serikali tunao wajibu wetu.Mkurugenzi yupo taarifa zipilekwe kwake kwa uhakika ilitujue la kufanya.Poleni sana tutaendelea kusaidiana,” alisema Rais Kikwete ambaye pia ni Mkazi wa kijiji cha Msoga, kata ya Chalinze.

  Mvua mkubwa iliyoambatana na upepo mkali wiki liyopita iliharibu kabisa majengo nane katika kata ya Chalinze ambapo kuta zilibomoka mabati kuezuliwa na upepo mkali na miti kuangukia nyumba na kujeruhi wana kijiji kadhaa ambao walitibiwa katika hospitali ya Tumbi.Kaya 47 kutoka vijiji vya Msoga na Tonga ziliathirika na mkasa huo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakiwasili kwa helikopta katika kata ya Chalinze wakitokea jijini Dar es Salaam jana, kukagua uharibifu ulioletwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na kuharibu makazi ya watu na kujeruhi ambapo kaya 47 zikiathirika katika vijiji vya Msoga na Tonga.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete pamoja na viongozi wa kata ya Chalinze wakikagua baadhi ya nyumba zilizoharibiwa vibaya baada ya kuangukiwa na miti kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha katika kata ya Chalinze na kuathiri kaya 47.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakizungumza na wananchi wakazi wa kata ya Chalinze waliopatwa na mkasa wa kuharibikiwa nyumba zao baada ya kuangukiwa na miti kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha katika kata ya Chalinze na kuathiri kaya 47. 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwafariji wana vijiji hao na kuahidi kuwasaidia katika janga hilo.(picha na Freddy Maro).

  0 0

  Chama cha kandanda mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimeeleza kusikitishwa kwake na kifo cha mchezaji kiungo wa zamani wa klabu ya simba na timu ya taifa-Taifa Stars,Christopher Alex  maarufu kama Masawe,kilichotokea leo (februari 22 mwaka huu),katika Hospitali ya Mirembe Dodoma.

  Mwenyekiti wa DRFA,Almas Kasongo,amemuelezea marehemu Christopher kuwa ni mchezaji aliyevuma enzi za uhai wake na kuiletea heshima kubwa klabu yake ya Simba na Taifa Kwa ujumla,pale walipofanikiwa kuisukumiza nje ya michuano ya afrika klabu ya Zamalek na kuivua ubingwa miamba hiyo ya soka ya kaskazini mwaka 2003.

  Kiungo huyo aliyeanza kuvuma katika miaka ya 2000,amefariki dunia kutokana na kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kifua kikuu (TB).

  Marehemu Christopher Alex, alizaliwa Septemba 12 mwaka 1975,na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Uhuru na kumaliza katika shule ya Chamwino huko Dodoma mwaka 1993,na alianza kucheza mpira kwenye timu ya Daraja la nne Chamwino UTD na baadaye daraja la tatu akiwa na kikosi cha Aston Villa nayo ya Dodoma.

  Mwaka 1999-2001 ameitumikia klabu ya CDA ya Dodoma,kabla ya kutimkia klabu ya Reli mwaka 2002 na baadaye kujiunga na wekundu wa msimbazi Simba,Marehemu ameacha mtoto mmoja aitwaye Alex.

  Kasongo,kwa niaba ya kamati ya utendaji ya DRFA,wametoa ubani wa shilingi laki mbili (200,000/=) kwa familia ya marehemu,na kuwataka mashabiki wa soka na watanzania kwa ujumla kuungana pamoja katika kuifariji familia hiyo kwenye kipindi hiki kigumu cha majonzi.

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi tuzo na fedha taslim kijana Mohammed Suleiman Khalfan baada ya kuwa Mwanafunzi Bora wa Fani ya Hesabu katika chuo cha Elimu ya Biashara Pemba.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi akimzawadia Tuzo na Fedha Taslim Mwanafunzi Bora wa Fani ya Mawasiliano ya Umma wa Chuo cha Elimu ya Biashara Pemba Nassor Mussa Khamis kwenye mahafali ya chuo hicho hapo Vitongoji Chake Chake Pemba.
  Wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Pemba wakiwa tayari kuthibitishwa kukamilisha mafunzo yao na kupewa vyeti vyao kwenye mahafali yao ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.


  0 0


   MH. Ridhiwani Kikwete akiongea kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi CCM sherehe zilizofanyika New York na kudhuliwa na wageni mbalimbali kutoka kila sehemu yenye tawi la CCM hapa Marekani.
   Mwenyekiti wa tawi la CCM New York akiongea kwenye sherehe hizo
   Bwana Isaac Kibodya akiongea kwa niaba ya katibu mwenezi wa tawi la CCM New York

  Hapa ni Joyce akiongea wasifu wa Mh.Ridhiwani Kikwete historia yake kwa ufupi
  Mh.Ridhiwani akiwa kwenye meza pamoja  na mabalozi wa umoja wamataifa, viongiozi wa tawi na Jumuhia ya Watanzania New York.
  Kwa picha zaidi kujionea mambo yalivyo kuwa yamenogo BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Chifu wa Wahehe , Mtwa Adam Mkwakwa wa II wakati alipokwenda nyumbani kwa Chief huyo, Kalenga Iringa Februari 20, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akishiriki katika dua mbele ya kaburi la marehemu Chifu Abdu Adam Sapi Mkwawa wakati alipokwenda nyumbani kwa Chifu huyo, Kalenga Iringa kuhani Februari 20, 2015.

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Chief wa Wahehe,Mtwa Adam Mkwawa wa II wakati alipokwenda nyumbani kwa Chifu huyo, Kalenga Iringa Februari 20, 2015 kuhani msiba wa baba yake Chifu huyo, Marehemu Chifu Abdu Adam Sapi Mkwawa uliotokea hivi karibuni.


  0 0

  Mkutano wa kikanda juu ya ukuaji na maisha ya baadae ya miji ya Afrika mashariki ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI INSTITUTE) umefungwa rasmi leo na Naibu waziri wa Nyumba na maendeleo ya makazi Mhe.  Angela Kairuki katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.

  Mkutano huo wa siku mbili uliohudhuriwa na wawakilishi wa ngazi za juu kutoka serikalini, mashirika ya kikanda na kimataifa, miji mikubwa, wasomi, sekta binafsi na asasi za kiraia umeweza kujadili na kuainisha mipango kabambe katika kutatua changamoto mbalimbali za ukuaji wa miji na jinsi gani tungependa kuishi mwaka 2050. 

  “Tatizo la ukuaji wa miji ni moja ya changamoto katika ukanda wa Afrika mashariki na nchi kwa ujumla. Ninaimani kuwa mkutano huu umeweza kujadili changamoto mbalimbali tunazokabiliana nazo kama nchi na ukanda mzima wa Afrika mashariki” alisemaMhe.Kairuki.
  Aliongeza kuwa matatizo ya foleni na kubanana kwa makazi ni kutokana na mipangilio mibovu ya nyumba na makazi jijini Dar es salaam. Hivyo basi kwa kutatua changamoto hizi wakazi wa Dar na wa miji mbalimbali ya Afrika kwa ujumla wataweza kufurahia mahitaji yao muhimu na kuongeza kasi ya maendeleo.

  Mhe. Kairuki pia aliweza kutambua mchango mkubwa wa Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI INSTITUTE) kwa kuleta mijadala yenye tija yenye lengo ya kustawisha uongozi bora na maendeleo kwa nchi za Afrika na dunia kwa ujumla.

  Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute, Prof. Joseph Semboja aliwashukuru watoa mada na washiriki wote walioweza kufika na kuhakikisha kuwa mkutano huu unafana.
  “Lengo kuu la mkutano huu limekuwa ni kujadili juu ya ukuaji na maisha ya baadae ya miji ya Afrika na tumekubaliana wote kuwa ili haya yaweze kutimia ni lazima basi miji iongeze nguvu ya ukuaji wa uchumi ili kuongeza ajira iliyawezekudumukwamudamrefu, lakini pia kufikia maono na malengo haya basi ni lazima kuwe na utawala bora na tumeainisha mabadiliko ya kifikra na maridhiano katika kutekeleza majukumu haya”.

  Washiriki wa kongamano hilo wametoka nchi mbalimbali ikiwemo Burundi, Ethiopia, South Afrika, Sudan, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan ya Kusini, Tanzania na  Uganda.
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya makazi,Mhe:Angela Kairuki, akiongea na Viongozi na watunga Sera kutoka Nchi za Afrika Mashariki wakati wa kufunga Mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI INSTITUTE) uliozungumzia changamoto za ukuaji wa miji na jinsi gani tungependa kuishi ifikapo 2050. Mkutano huo ulifanyika katika hoteli ya Hyatt Regency zamani Kilimanjaro-jijini Dar es Salaam.
  Afisa mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa maendeleo Endelevu “Uongozi Instutite” Prof.Joseph Semboja, kushoto, akiteta jambo na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya makazi, Mhe:Angela Kairuki (kulia) wakati waziri huyo alipoalikwa kufunga mkutano wa siku mbili wa viongozi na watunga Sera kutoka nchi za Afrika Mashariki uliozungumzia changamoto za ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadae ya miji ya Afrika ifikapo 2050 uliofanyika katika hotel ya Hyatt Regency zamani Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
  Meya wa jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi (kulia) akitamtambulisha , Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya makazi, Bi. Angela Kairuki, wa pili kushoto kwa balozi wa Finland nchini , Sinikka Antila, wa kwanza kushoto wakati wa kufunga mkutano wa siku mbili wa Viongozi na watunga Sera kutoka Nchi za Afrika Mashariki uliozungumzia changamoto za ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadae ya miji ya Afrika ifikapo 2050. Wa pili kushoto ni Afisa mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa maendeleo Endelevu “Uongozi Instutite”, Prof.Joseph Semboja. Mkutano huo ulifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency zamani Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

  0 0


older | 1 | .... | 748 | 749 | (Page 750) | 751 | 752 | .... | 3282 | newer