Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 747 | 748 | (Page 749) | 750 | 751 | .... | 3272 | newer

  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali imepanga kuajiri walimu zaidi ya 35,000 kwa ajili ya shule za sekondari ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa walimu nchini.

  Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Februari 19, 2015) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya Kiwere, mara baada ya kukagua ujenzi wa maabara na kuzindua nyumba nne za walimu kwenye shule ya sekondari ya Kiwere, tarafa ya Kalenga, wilayani Iringa.

  Waziri Mkuu alisema walimu hao watagawanywa kwenye shule kulingana na mahitaji yaliyokwishawasilishwa na kwamba watakapopata mgao wao hawana budi kuziangalia kwanza shule zenye miundombinu iliyokamilika kama ilivyo kwa shule hiyo.

  Akifafanua kuhusu kasi ya ujenzi wa maabara Waziri Mkuu alisema: “Mkoa mzima wa Iringa unahitaji kuwa na maabara 318 na zilizo tayari mpaka sasa ni 108. Lakini kuna nyingine 141 ambazo zimekwishaanza kujengwa na zimefikia hatua nzuri. Nimeambiwa katika muda mfupi ujao kutakuwa na maabara 249 zilizokamilika,” alisema.

  “RC inabidi uwasukume watu wako ili hizi 69 ambazo bado hazijaanza kujengwa zikamilike kabla ya Juni mwaka huu kama ambavyo Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete alikuwa ameelekeza. Alisema hataongeza tena muda wa ujenzi,” aliongeza.

  Alisema elimu ni sekta ya msingi ambayo Serikali imeamua kuipa umuhimu wa kipekee na kuiweka katika moja ya maeneo sita muhimu ya kipaumbele chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa ya Haraka (BRN).

  Waziri Mkuu aliwataka wanafunzi wa shule hiyo wasome kwa bidii na wawe wasikivu ili waweze kufanya vizuri zaidi kwenye masomo yao.

  Mapema, akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Afisa Elimu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Leonard Msigwa alisema ujenzi wa nyumba hizo nne ambazo zina pande mbili (four duplex houses) umegharimu sh. milioni 323.2. Alisema nyumba hizo zenye vyumba vitatu vya kulala, sebule na jiko, zina uwezo wa kubeba familia nane.

  Bw. Msigwa alisema ujenzi wa nyumba ulifanywa shirika la DESWOS la Ujerumani kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa pamoja na wananchi. Pia walisaidiwa kujengewa tenki la maji na mabweni mawili yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 112 kila moja kwa ajili ya wasichana.

  Akifafanua kuhusu hali ya ujenzi wa maabara, Afisa Elimu huyo alisema hadi sasa wamekamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya Kemia na Baiolojia lakini bado viko kwenye hatua ya kupaka rangi. Alisema mfumo wa gesi na maji umekwishafungwa ndani ya vyumba vya maabara.

  “Ujenzi wa maabara hadi sasa umekwishagharimu sh. milioni 52.8/- na katika kipindi cha Februari 2015, tumefanikiwa kutengeneza baadhi ya samani za maabara yaani meza 24 na stuli 96 zenye thamani ya sh. 8,940,000/-,” alisema.

  0 0

   Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Profesa, Hasa Mlawa (kulia), akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia picha yenye nembo ya mfuko huo kwenye  hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya wadhamini ya mfuko wa LAPF na kuiaga bodi iliyomaliza muda wake iliyofanyika makao makuu ya mfuko huo Dar es Salaam jana. 
   Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Profesa, Hasa Mlawa (kulia), akimkabidhi Waziri wa Kazi na Ajira Gaudentia Kabaka picha yenye nembo ya mfuko huo kwenye  hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya wadhamini ya mfuko wa LAPF na kuiaga bodi iliyomaliza muda wake iliyofanyika makao makuu ya mfuko huo Dar es Salaam jana. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia.
   Wajumbe wapya wa bodi ya LAPF 
   Mgeni rasmi wa uzinduzi huo Waziri Hawa Ghasia (katikati mbele waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya zamani ya LAPF iliyomaliza muda wake. Kushoto kwa waziri Ghasia ni Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka ambaye wizara yake inasimamia mifuko hiyo ya kijamii.
   Mgeni rasmi wa uzinduzi huo Waziri Hawa Ghasia (katikati mbele waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wapya wa  bodi ya LAPF.
   Wajumbe wa bodi ya LAPF iliyomaliza muda wake.

  0 0

  TICKETS ON SALE NOW FOR $40 *** THEY WILL BE MORE AT THE DOOR $50
  SEATED 3 -COURSE DINNER
  FIRST CLASS SERVICE
  RED CARPET PAPARAZZI 
  DRESS READY FOR ACTION
  HIGH LEVEL SECURITY 
  @RICH RICH PALACE
  11019 ATLANTIC AVENUE RICHMOND HILL NY 11418
  **********************************************************
  PESA UNAYONUNULIA TICKET UNAPATA CHAKULA NA SOFT DRINKS KAZI KWAKO WAHI TICKET YAKO MAPEMA KWA $40 KWANI MLANGONI SIKU YA SHEREHE NI $ 50.
  MH. Ridhiwani Kikwete akiwa na wenyeji wake viongozi wa Tawi la CCM New York wakiongozwa na Mwenyekiti wa tawi Bwana Seif Akida Baada ya kumpokea Uwanja wa Ndege wa JFK tayari kwa Sherehe za Miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM kesho mambo ya meiva kazi kwenu Watanzania wote popote mlipo Mnaombwa kujitokeza kwa nguvu na umoja hiyo kesho  siyo Chadema wala  CUF  Utanzania kwanza kuanzia saa  12 jioni hadi majogoo kula kunywa na kucheza kwa Dollar 40 tu...
   Mh. Ridhiwani akifurahia jambo na wenyeweji wake uwanjani hapo baada ya kupokelewa. Kwa Picha zaidi nenda soma zaidi.
  Kwa picha Zaidi tembelea http://tembaphoto.com/

  0 0

  Tanzania inaunga mkono kwa dhati Ushirikiano wa Kikanda na muumini mkubwa wa Umoja wa Africa na Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). 
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo  jijini Nairobi mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa EAC na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye amekua mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita
   "Tunaamini kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyogawanyika, haitaweza kuchukua nafasi yake kamili na heshima katika familia ya Mataifa ya Afrika na dunia kwa ujumla" Rais amesema na kuongeza kuwa Tanzania inakua kuwa masoko yaliyogawanyika, miundombinu hafifu baina ya nchi, havina nafasi katika dunia ya leo wala ya baadaye. 

  Rais Kikwete amesema na kumpongeza Rais Kenyatta kwa kusimamia utekelezwaji wa maazimio na miradi ya pamoja ya Jumuiya wakati wa kipindi chake cha uenyekiti na kuahidi kuwa Tanzania haitawaangusha wana Afrika Mashariki katika kutekeleza azma yao ya pamoja ya kuendeleza Jumuiya ambayo inaundwa na nchi za Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda. 

  Rais Kikwete amesema katika utekelezaji wa ajenda ya EAC, biashara imeongezeka kwa kiasi kikubwa na kwamba nchi zote wanachama zinayaona matunda hayo. Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2013 biashara katika nchi za EAC imeongezeka kutoka dola za kimarekani 3, 722.9 hadi dola 5,805.6 ambapo kati ya mwaka 2012 hadi 2013 kumekua na ongezeko la asilimia 6. 
  "Kama biashara isiyo rasmi ingerasimishwa, kwa hakika, ongezeko hili la biashara lingekua juu zaidi ya hapa, hivyo imefikia wakati muafaka kurasimisha biashara isiyo rasmi katika ushirikiano wetu" Rais amesema na kuongeza kuwa " kwa njia hii serikali zitakusanya kodi na hivyo kuna umuhimu wa kuelekeza nguvu katika kusaidia biashara ndogo ndogo na zile zisizo rasmi kwa kuziwekea mazingira mazuri". 
  Rais Kikwete amerejea nyumbani mara baada ya mkutano huo ambao umehudhuriwa na Marais wa nchi zote tano za Jumuiya na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ambaye amehudhuria kama mualikwa maalum katika kipindi hiki ambapo mazungumzo ya awali ya kuijadili nchi yake kama inaweza kupata uanachama katika EAC yanaendelea. Pichani ni Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Profesa Mark Mwandosya akimkaribisha Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki , Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Rais kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea Nairobi Kenya ambapo alihudhuria mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi Jumuiya ya Afrika Mashariki.Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo Dkt.Shukuru Kawambwa
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pamoja na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakizungumza chemba kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa  Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya  katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa  Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya  katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Naibu Rais wa Kenya, Mhe. William Rutto na maafisa wengine wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa  Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015
   Kutoka kushoto ni mgeni mwalikwa, Rais wa Sudani Kusini, Mhe Salva Kiir, Rais wa Burundi, Mhe Pierre Nkurunziza, Rais Jakaya Mrisho Kikwete(Tanzania),Rais Uhuru Kenyatta(Kenya)Rais Yoweri Museveni (Uganda) Rais Paul Kagame (Rwanda) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Balozi Dk Richard Sezibera wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano kwenye  mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete(kushoto)akipokea bendera ya Afrika Mashariki(EAC)kutoka kwa Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta ikiwa ni ishara ya kumkabidhi rasmi Uenyekiti wa  EAC  kwenye  mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo Ijumaa Februari 20, 2015 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi. Picha na IKULU

  0 0


  EdExpo Tanzania 2015, the International Higher Education Exhibition will be happening in Dar es Salaam, Tanzania 9th and 10th March, 2015 at the New Africa Hotel, Dar es Salaam.
  EdExpo Tanzania 2015 will be a platform where prospective students can get information on available degree courses, scholarships and student life at different universities from around the world. EdExpo Tanzania will also provide information about how to access and succeed in international higher education.
  Participating universities include:
  Franklin University (USA), Acharya Institutes (India), Okan University (Turkey), University of Cattolica (Italy), Victoria University (Uganda), Girne American University (Cyprus), Student Enquiry (England), Swiss Hospitality Education – Les Roches (Switzerland), European Universities (Switzerland, Spain & Germany), International University of East Africa (Uganda)

  0 0

  Jeshi la Kujenga Taifa lilianzishwa Julai 10, 1963 na serikali kwa lengo la kuwaweka pamoja vijana wa nchi hii na kuwapa malezi kuhusu uzalendo na umoja ili kuondoa dalili za matabaka zilizoanza kujitokeza katika jamii baada ya uhuru.

  Baadhi ya sababu za kuanzishwa kwa JKT ni:

  Kubadili fikra za vijana wa nchi hii kutoka ile hali ya ukoloni kutegemea nchi nyingine kuleta maendeleo.

  Kukusanya nguvu za vijana wote wa nchi hii na kuzielekeza kwa umoja wao kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya taifa.

  Kuwafunza vijana kujenga mshikamano na umoja wa kitaifa, ili kulinda uhuru wa Taifa lao.

  Jeshi la Kujenga Taifa linaunganisha vijana bila kujali itikadi zao, dini, elimu, jinsia na mali ili kuwalea kuwa wazalendo kwa taifa lao na kupenda kuitumikia nchi yao.

  Pamoja na dhana ya kufunzwa uzalendo, pia stadi mbalimbali za kazi hufundishwa kwa vijana hao ili waweze kujiajiri, pindi wamalizapo mkataba yao ya kujitolea kwa miaka miwili.

  Serikali ilirejesha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa vijana wa kujitolea mwaka 2001, baada ya kusitishwa mwaka 1994.

  Masharti ya Kujiunga na JKT kwa vijana wa Kujitolea

  Kijana kabla ya kujiunga na JKT hutakiwa kuyajua masharti na kuzifahamu taratibu za kujiunga na kuelewa kuwa JKT halitoi ajira.

  Moja ya kipengele cha masharti ya kujiunga na JKT kinasema kuwa ‘Kwa kipindi chote nitakachokua ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa nitakuwa nafanya mafunzo ya kijeshi na ya stadi za kazi na maisha, na baada ya mkataba nitarejea nyumbani. Hivyo sitalidai Jeshi la Kujenga Taifa ajira, wala kulitaka linitafutie ajira/kazi’.

  Kipengele hiki kinaainisha masharti ya makubaliano kati ya Jeshi la Kujenga Taifa na kijana kabla ya kujiunga na kupatiwa mafunzo ya awali ya kijeshi.

  Aidha, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine mara kadhaa wamekuwa wakisisitiza kuwa, JKT halitoi ajira.

  Lakini hivi karibuni wakati nchi inaelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge mwaka huu, umezuka mtindo wa makundi ya vijana waliopitia JKT katika Operesheni mbalimbali kuomba kuandamana kwenda Ikulu kudai ajira.

  Madai yanayopingana na dhana ya JKT na kauli ya Mhe. Rais kuwa Jeshi la Kujenga Taifa haliajiri, bali vijana hujiunga kwa hiari kwa kujitolea na baada ya mkataba wa miaka miwili wanatakiwa kurejea walikotoka.

  Aidha, Mhe. Rais Kikwete, amewahi kutoa agizo kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, taasisi za Serikali na kuziomba zile zisizo za kiserikali kutoa ajira kwa vijana waliopata mafunzo ya JKT kulingana na sifa za kijana na nafasi zilizopo.

  Takwimu zinaonesha kuwa tangu kurejeshwa kwa mafunzo ya JKT mwaka 2001 hadi mwaka jana, jumla ya vijana 104,594 wamejiunga na JKT wakiwemo wavulana 76,832 na wasichana 27,762.

  Katika kipindi hicho, jumla ya operesheni 13 katika mafunzo ya JKT zimefanyika, Operesheni hizo ni pamoja na Operesheni Mkapa mwaka 2001, Miaka 40 ya JKT mwaka 2002, Utandawazi mwaka 2004 na Operesheni Jiajiri mwaka 2005.

  Zingine ni pamoja na Kasi Mpya mwaka 2006, Maisha Bora mwaka 2007, Uadilifu mwaka 2008, Kilimo Kwanza mwaka 2009 na Operesheni Uzalendo mwaka (2010), Miaka 50 ya Uhuru (2011), Sensa mwaka 2012, Miaka 50 ya JKT (2013) na Miaka 50 ya Muungano (2014).

  Vijana wa Kujitolea walioajiriwaTangu mwaka 2003 hadi 2014 jumla ya vijana 24,708 wameajiriwa katika vyombo vya ulinzi na usalama ambapo vijana 21,977 wakiwemo wavulana 17,307 na wasichana 4,670 wameajiriwa na Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ).

  Jeshi la Polisi vijana 3,965 wavulana wakiwa 2,943 na wasichana 1,022, Magereza vijana 2,139 wavulana 2,044 na wasichana ni 95, Zimamoto vijana 100 wavulana wakiwa ni 78 na wasichana ni 22 na taasisi zingine vijana 592 Vijana 1,622 wameajiriwa katika taasisi mbalimbali kama TANAPA, GEITA GOLD MINE, BANDARI na AFRICAN GOLD MINE.

  Ni vema vijana hao wakatambua kuwa tatizo la ajira sio kwao peke yao, ni tatizo la ulimwengu mzima Tanzania ikiwemo, wanashauriwa kutumia stadi za kazi kujiajiri wenyewe.

  Aidha, vijana hao watambue kuwa walikula kiapo cha UTII, wakati wa kuhitimu mafunzo ya JKT, hivyo suala la kuandamana ni kinyume cha kiapo chao. Vijana hao walitumikia Jeshi la Kujenga Taifa Operesheni za nyuma na kumaliza mkataba wa miaka miwili. Shinikizo lao la kulazimisha ajira kwa kuandamana ni kinyume cha sheria za nchi.

  Kwa maelezo ya hapo juu utaona kuwa Jeshi la Kujenga Taifa, halina dhamana ya kuajiri bali kufunza vijana wa taifa hili umoja, stadi za kazi na uzalendo baada ya hapo wenye sifa za kuajiriwa hupata ajira katika taasisi mbalimbali za serikari na binafsi.

  Taarifa hii Imetolewa na Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa.

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akizungumza na mwanamuziki mkongwe wa Bongo Flava, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA wakati mwanamuziki huyo alipokutana na Waziri huyo jijini Washington DC katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Waziri Chikawe yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani, na kwa upande wa Mwana FA yupo nchini Marekani kwa ajili ya matembezi yake binafsi hata hivyo alienda ubalozini hapo kwa ajili ya kumsalimia Balozi
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula wakiwa katika picha ya pamoja na mwanamuziki mkongwe wa Bongo Flava, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA wakati mwanamuziki huyo alipokutana na Waziri huyo jijini Washington DC katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Waziri Chikawe yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani, na kwa upande wa Mwana FA yupo nchini Marekani kwa ajili ya matembezi yake binafsi hata hivyo alienda ubalozini hapo kwa ajili ya kumsalimia Balozi. Kulia ni rafiki wa mwanamuziki huyo ambaye pia ni mfanyabiashara, Swalah Saidi. Picha zote na FelixMwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0


  0 0

  UNIVERSAL AUCTION CENTRE Kwa idhini waliyopewa na Ubalozi wa Netherlands, Norwegian, Sweden,  British Council na DFID  watauza kwa mnada wa hadhara  Magari & Fanicha za nyumbani na ofisi tarehe 21 Feb, 2015 Jumamosi saa 4.00 asubuhi. Mnada utafanyika Golden Resort Sinza,  Lion Street. MALI ZITAKAZOUZWA: Sofa sets, Dining table, Coffee table, Chest drawer, Vitanda,Magodoro, Meza za Computer, Book shelves,  Meza za ofisi na Viti, File cabinet, Fridge ,Majiko , TV sets, Radio call, Washer, Dryer, Computer, Printers, Heavy duty Ups 3KVA,Safe kubwa na ndogo,  A/c split units  Etc. MAGARI/PIKIPIKI ZITAKAZOUZWA:
  Idadi

  Aina

  Model

  Mwaka

  Ushuru

  1

  Nissan Patrol S/Wagon

  TD 42  T107CD112

  2005

  Bado

  1

  Nissan Safari S/Wagon

  VRGY60

  1995

  Umelipwa

  1

  Nissan Patrol S/wagon

  TK-520521-5G752

  1992

  Bado

  1

  Subaru Forester

  JFISF63

  2000

  Umelipwa

  1

  Suzuki  Carry P/Up

  DA32T

  2001

  Umelipwa

  1

  Leyland DAF FTG

  Truck (Horse)

  2003

  Bado

  1

  Suzuki Motorcycle

  TF125

  2006

  Bado

  2

  Daikin Air cooled water Chiller

  113KW

  2005

  Bado

  Mali zote zinaweza kukaguliwa Golden Resort Sinza,Lion Street tarehe 19 mpaka 20 Feb,  2015 kuanzia saa 4.00. asubuhi mpaka saa 10.00 jioni.

  MASHARTI YA MNADA:

  1. Mnunuzi  wa fanicha atatakiwa kulipa malipo yote pale pale. Na mnunuzi wa gari atatakiwa kulipa 25% pale pale na salio lilipwe ndani ya siku 7 ukishindwa kulipa kwa muda huo gari litauzwa tena na dhamana haitarudishwa. 
  1. Mali zote zitauzwa kama zilivyo.
  2. Mnunuzi atawajibika kulipa ushuru.
  3. Mali yote iliyouzwa itatakiwa kuondolewa siku hiyo hiyo  baada ya kulipia malipo yote pamoja na ushuru

  Kwa maelezo zaidi waone:
  UNIVERSAL AUCTION CENTRE

  NKRUMAH STREET
  MKABALA NA CO-CABS

  SIMU NA:  0754-284 926, 0767 284 926               
  Email : universalauction@hotamail.com  0 0

  Benki bora Tanzania (NMB) imekabidhi hundi ya udhamini wa shilingi milioni 10 kwa mfuko wa pensheni kwa jamii - PSPF kwa ajili ya kufanikisha mkutano mkuu wa mwaka wa wadau wa mfuko huo. 
   Mkurugenzi mkuu wa PSPF amewashukuru NMB kwa kuwa karibu Zaidi na wadau wao kwa vitendo tofauti na benki zingine, kwani hundi hiyo ni kielelezo tosha cha benki inayowajali wateja wake. 
   NMB ni benki bora Zaidi nchini ikiwa na matawi Zaidi ya 170 na mashine za ATM Zaidi ya 600 huku ikijivunia wateja Zaidi ya milioni 2 na ubunifu wa bidhaa zinazomlenga mteja Zaidi kama NMB Wakala, akaunti za Chap Chap na NMB Mobile. 
   Katika mkutano huo na PSPF, NMB imeweka mabanda yake ya maonyesho na kuonyesha huduma mbalimbali zinazotolewa na benki huku huduma yao Mpya ya NMB Wakala na Chap Chap Instant Account zikiwa ndizo huduma zilizopendwa Zaidi na washiriki wa mkutano huo.
   Afisa Mkuu wa kitengo cha biashara ya jumla wa NMB Ndugu Richard Makungwa, (Kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF - Adam Mayingu. Katikati ni Meneja Mwandamizi wa kitengo cha biashara za Kitaasisi   NMB Noela Kivaria.

   Afisa Mkuu wa kitengo cha biashara ya jumla wa NMB Ndugu Richard Makungwa (Kulia)  pamoja Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF -  Adam Mayingu, wakiashiria ushirikiano wa taasisi mbili kwa kugongesha  vinywaji  vyao  wakati wa hafla ya chakula cha jioni  iliyoandaliwa na NMB kwa wadau wa PSPF.

  Maofisa wa NMB wakifuatilia  jambo la muhimu wakati wa hafla hiyo ya PSPF iliyofadhiliwa na Benki ya NMB.


  0 0

  Mkaazi wa Kyela mkoani Mbeya Bwana Edom Dickson Mwansasu amekabithiwa gari aina ya Toyota IST na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel mara baada ya kuibuka mshindi kupitia droo ya wiki ya pili ya promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi iliyofanyika siku ya ijumaa iliyopita
   Bwana Edom Mwansasu mwenye umri wa miaka 40 anajishughulisha na shughuli za kilimo huko Ngonga Kyela Mkoani Mbeya ameibuka mshindi baada ya kununua na kujiunga na vifurushi vya siku vya huduma ya Airtel yatosha kila siku. 
   Akiongea baada ya kukabithiwa gari bwana Edom Mwansasu alisema ninafuraha sana kuwa mshindi na kutumiza ndoto yangu ya kumiliki gari. Nilipopigiwa simu sikuamini kuwa nimeshinda gari , nilifurahi sana nakupasha habari kwa familia yangu. Sijawahi kumiliki gari hivyo najisikia furaha sana Airtel kunizawadia mimi hii gari kupitia hii promosheni ya Airtel yatosha. Kwa kupitia gari hili sasa na uhakika wa usafiri mimi pamoja na familia yangu lakini pia litanisaidia katika kazi yangu ya kilimo na kuniwezesha kusafirisha mazao yangu kirahisi ukilinganisha na awali nilikuwa natumia baskeli au kukodi gari. 
   ‘Nawapongeza sana Airtel na nawashauri watanzania kuendelea kutumia huduma ya Airtel yatosha na kuamini kuwa nao wanaweza kubahatika na kushinda kama mimi” aliongeza Mwansasu Kwa upande wake Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mbeya Bwana Hemed Msangi alisema” kwanza kabisa napenda kuwapongeza Airtel kwa kuanzisha promosheni hii kabambe inayowawezesha watanzania kutoka sehemu mbalimbali kujishindia magari. 
  " Naamini kwa kupitia promosheni hii mtawawezesha watanzania wengi kujikwamua kiuchumi na kuwawezesha kufanya shughuli zao za kijamii na kiuchumi kirahisi na kwa ufanisi zaidi. Nawapongeza washindi wote waliopatikana mpaka sasa. Lakini natumia fulsa hii kuwaomba wananchi wadumishe amani maana kama sio amani tulionayo basi promosheni kama hizi zisingeweza kufanyika” 
   Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja biashara wa Nyanda za juu kusini Bwana Straton Mushi Alisema” promosheni hii ya Airtel yatosha zaidi ni mahususi kwa wateja wetu Tanzania nzima wanaotumia huduma hii ya Airtel Yatosha kuweza kujishindia gari aina ya Toyota IST kila siku . kujiunga na vifurushi vya Airtel yatosha mteja anatakiwa kupiga *149*99# au kwa kununua vocha vya Airtel yatosha au kununua kupitia huduma ya Airtel Money na kuunganishwa moja kwa moja kwenye droo itakayomwezesha kushinda.
   Mpaka sasa washindi 10 wamepatika ambapo kati yao wawili wanatoka kanda ya nyanda za juu kusini na leo tunamkabithi mshindi wetu wa Mbeya Bwana Edom Mwansansu gari lake na kisha tutamkabithi mshindi wa mkoa wa sumbawanga bwana Saidi Mashiko ambaye ni mganga wa tiba za jadi na mkazi wa Katavi hivi karibuni” 
   “Natoa wito kwa watanzania na wateja wetu kujiunga na vifurushi hivi vya Airtel yatosha na kupata nafasi ya kujishindia gari aina ya Toyota IST kila siku”. Aliongeza Mushi Washinde wengine waliojishindia Toyota IST toka promosheni hii ianze ni pamoja na Ramadhani Dilunga mkazi wa Pwani, Namtapika Kilumba Mkazi wa Mtwara, said Mashiko mkazi wa katavi, Hamim Yoyo mkazi wa Korogwe Tanga, Esther Mashauri Mkazi wa Mwanza, Ibrahim Kimondo mkazi wa Kondoa pamoja na Mwajabu Churian, Sakina Libwana na Justin Wilium wote wakazi wa Dar
  Mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Edom Dickson Mwansasu  mkazi wa Kyela Mbeya akitambulishwa  na Meneja biashara wa Airtel  Nyanda za juu kusini Bwana Straton Mushibaada ya kuibuka moja kati ya washindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi
   Kamanda mkuu wa polisi wa Mkoa wa Mbeya Bwana Hemed Msangi (wa pili kulia)  akimkabithi mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Edom Dickson Mwansasu  mkazi wa Kyela Mbeya baada ya kuibuka moja kati ya washindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi. pichani kulia  ni mke wa Edom Mwansasu na kushoto  ni Meneja biashara wa Airtel  Nyanda za juu kusini Bwana Straton Mushi
   Mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Edom Dickson Mwansasu  akiwasha gari mara baada ya kukabithiwa gari lake baada ya kuibuka moja kati ya washindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi.
   Mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Edom Dickson Mwansasu  akiwa ndani ya gari pamoja na mke wake baada ya kukabithiwa gari lake kufatia kuibuka kuwa mshindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi katika droo iliyofanyika ijumaa iliyopita
  Sehemu ya magari kibao yanayongoja kunyakuliwa na washindi wa kila wiki wa Airtel hatosha

  0 0

  Fainali ya kumsaka Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL), inatarajiwa kufanyika kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi kuanzia majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

  Awali mchezo huo wa fainali ulikuwa umepangwa kufanyika kesho kwenye dimba la Uwanja wa Taifa, lakini kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TTF imepelekea mchezo huo kuhamishiwa Chamazi.


  Mchezo huo wa fainali utaanza saa 10 kamili jioni, na utaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha Azam TV ili kuwapa nafasi wapenzi na wadau wa soka waliopo mbali na hasa mikoani kuweza kushuhudia mchezo huo.

  Bingwa wa Fainali ya Ligi Daraja la Kwanza atazawadiwa Kombe pamoja na medali, huku mshindi wa pili akipata kikombe na medali pia. Viingilio vya mchezo huo ni tsh.5,000 kwa jukwaa kuu na tsh. 3,000 kwa majukwaa ya mzunguko.

  Wakati huo huo, Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea leo (Jumamosi)  katika viwanja vitatu tofauti, Mgambo Shooting watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

  Ndanda FC ya Mtwara watawakaribisha Wagosi wa Kaya timu ya Coastal Union kutoka jijini Tanga katika mchezo utakaochezwa kwenye dimba la Ngwanda Sijaona.

  Huku wakata miwa wa Kagera Sugar wanaoutimia Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakiwakaribisha Maafande wa Jeshi la Polisi kutoka mjini Morogoro timu ya Polisi.

  Ligi hiyo ya Vodacom itaendelea tena kesho Jumapili katika viwanja vitatu   tofauti, Uwanja wa Chamazi wenyeji Azam FC wataikaribisha timu ya maafande wa Jeshi la Magereza nchini Tanzania Prisons, mchezo utakaonza majira ya saa 2 kamili usiku.

  Mjini Shinyanga wenyeji timu ya Stand United wataikaribisha Simba SC kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, huku wagonga nyundo wa jiji la Mbeya, timu ya Mbeya City wakicheza na timu ya Young Africans kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
    

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA 
  MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0


  0 0


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.) akimpokea Mwanzilishi wa Taasisi ya Maendeleo ya Aga khan Duniani,  Mtukufu Karim Aga Khan mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mtukufu Aga Khan yupo nchini kwa ziara binafsi ya siku nne, ambapo pia atatumia fursa hiyo kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ya taasisi hiyo hapa nchini.
  Mtukufu Aga Khan akisalimiana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Nchini  Dkt. Shukuru Kawambwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Dkt. John Pombe Magufuli amelaani vikali tukio la kikatili la kutekwa na kuuawa kwa mtoto Yohana Bahati pamoja na kujeruhiwa vibaya kwa mama mzazi wa marehemu na watu wasiofahamika.

  Akizungumza kwa masikitiko makubwa jijini Dar es Salaam, Dkt.Magufuli amewataka Watanzania kuishi kwa amani na upendo na kuacha dhana ya kutajirika kutokana na viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi(Albino).

  “Tukio hili ni la kinyama na halikubaliki popote Duniani, watu wanatakiwa waelewe kuwa mtu huwezi kutajirika kutokana na viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi kama alivyofanyiwa mtoto Bahati” Alisema Waziri Magufuli.

  Katika hatua nyingine, Waziri Magufuli ametoa msaada wake wa awali kiasi cha Shilingi milioni Moja kwa ajilili ya kumsaidia Ester Jonas mama mzazi wa mtoto huyo aliyeuawa na watu hao wasiofahamika.

  “Nimeona nitoe msaada wangu wa awali kiasi hichi cha fedha kwa ajili ya kumsaidia mama huyu aliyejeruhiwa vibaya kwa ajili ya mahitaji yake mbalimbali na hapo badae ntakapopata nafasi ntakwenda nyumbani kwake kutoa pole zaidi”

  Aidha, Waziri Magufuli ameishukuru Hospitali ya Wilaya ya Chato pamoja na Bugando kwa msaada mkubwa wa kumpatia matibabu mama huyo aliyejeruhiwa vibaya na watu hao wasiofahamika.

  Pia Waziri Magufuli aliipongeza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Geita kwa kazi kubwa ya kuwatafuta wale wote waliohusika na tukio hilo la kikatili.
  Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato mkoani Geita Dkt. John Pombe Magufuli(kushoto) akikabidhi msaada wa fedha Shilingi Milioni Moja kwa Mwandishi wa ITV Ndugu Emanuel Buhohela(kulia) kama mchango wake wa awali kwa ajili ya kumsaidia Ester Jonas aliyejeruhiwa vibaya na watu wasiofahamika wakati wa tukio la kutekwa kwa mwanaye mwenye ulemavu wa ngozi(Albino) Yohana Bahati aliyeuwawa katika Wilaya ya Chato Mkoani Geita. Mama huyo bado amelazwa katika katika Hospitali ya Bugando kwa ajili ya matibabu. Habari na Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi

  0 0

  Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa(kushoto) na Mkuu wa kitengo cha mazingira wa manispaa hiyo Themi Luther(kulia) wakipitia michoro ya usanifu ya majengo kwenye makutano ya mitaa ya Aggrey na Indragadhi ambapo ujenzi huo haujafuata michoro, Alipotembelea na kupima uzio wa mabati unaowekwa na wakandarasi wengi bila kulipiwa vibali, Katika ukaguzi huo majengo mengi yamekiuka michoro ya ujenzi na amesimamisha ujenzi huo mara moja hapo jana.
  Mkuu wa kitengo cha mazingira wa manispaa ya Ilala Themi Luther(katikati)akimpatia maelekezo .Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa(kushoto) kuhusiana na usanifu wa jengo kwenye makutano ya mitaa ya Aggrey na Indragadhi ambapo ujenzi huo haujafuata michoro,Meya huyo alitembelea na kupima uzio wa mabati unaowekwa na wakandarasi wengi bila kulipiwa vibali, Katika ukaguzi huo majengo mengi yamekiuka michoro ya ujenzi na amesimamisha ujenzi huo mara moja hapo jana.
  Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa(katikati mwenye miwani) akitaka ufafanuzi wa michoro ya majengo kwa mmoja wa waandisi wanaojenga majengo yaliyopo katika makutano ya mitaa ya Aggrey na Indragadhi ambapo baadhi ya majengo hayo hayajafuata michoro sanifu,Meya huyo alitembelea na kupima uzio wa mabati unaowekwa na wakandarasi wengi bila kulipiwa vibali, Katika ukaguzi huo majengo mengi yamekiuka michoro ya ujenzi na amesimamisha ujenzi huo mara moja hapo jana.
  Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa(wapili toka kushoto) na Naibu wake Khery Kessy Mohamed(katikati)wakipima michoro ya usanifu ya jengo kwenye makutano ya mitaa ya Aggrey na Indragadhi ambapo ujenzi huo haujafuata michoro halali ya ujenzi,Walipotembelea na kupima uzio wa mabati unaowekwa na wakandarasi wengi bila kulipiwa vibali, Katika ukaguzi huo majengo mengi yamekiuka michoro ya ujenzi na amesimamisha ujenzi huo mara moja hapo jana.
  Waandisi wanaojenga majengo yaliyopo katika makutano ya mitaa ya Aggrey na Indragadhi wakisisitizwa jambo na Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa(katikati mwenye miwani)wakati alipotembelea na kupima uzio wa mabati unaowekwa na wakandarasi wengi bila kulipiwa vibali na kukagua majengo mengi ambayo yamekiuka michoro ya ujenzi na amesimamisha ujenzi huo mara moja hapo jana.

  0 0

  Baadhi ya Viongozi wa juu wa Serikali, wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria maziko ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mjini Zanzibar, marehemu Salmin Awadh Salmin, huko Makunduchi mjini Zanzibar. Marehemu Salmin amezikwa leo Feb, 20, 2015 kijijini kwake Makunduchi Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohamed Ali Shein, akiweka udongo katika kaburi la marehemu Salmin Awadh Salmin, wakati wa shughuli za maziko yake zilizofanyika katika kijiji cha Makunduchi mjini Zanzibar jana Feb, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka udongo katika kaburi la marehemu Salmin Awadh Salmin, wakati wa shughuli za maziko yake zilizofanyika katika kijiji cha Makunduchi mjini Zanzibar jana Feb, 2015.


  0 0


  0 0
 • 02/21/15--02:58: TAARIFA KWA UMMA

 • UAMUZI WA BODI YA WAKURUGENZI KUHUSU MAOMBI YA TPDC YA  TOZO ZA HUDUMA ZA KUCHAKATA NA KUSAFIRISHA GESI ASILIA


  1.                  Tarehe 1 Septemba 2014, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilipokea ombi Na. TR-G-14-039 kutoka kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhusu kanuni ya kukokotoa tozo za huduma ya kuchakata na kusafirisha Gesi Asilia, na mapendekezo ya bei ya uchakataji na usafirishaji wa gesi asilia.


  2.                  Kati ya Septemba 2014 na Januari 2015, EWURA ilifanya uchambuzi wa kupitia gharama za ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia, muundo wa mtaji (capital structure)  na  faida ya mtaji, gharama za uendeshaji wa mradi, pamoja na tozo iliyoombwa na TPDC.  

  3.                  Kwa mujibu wa ombi husika, TPDC waliiomba EWURA kuidhinisha vipengele vifuatavyo:

  (a)      kanuni ya kurekebisha tozo za kuchakata na kusafirisha gesi asilia itumike kwa miaka 20 hadi mwaka 2034;

  (b)     tozo kwa huduma ya kuchakata na kusafirisha gesi asilia iwe Dola za Marekani 4.178 kwa uniti (MMBtu) kwa muda wa miaka mitatu ya kwanza;

  (c)      faida kwenye mtaji ya asilimia kumi na nane (18%) na muundo wa mtaji wa asilimia hamsini mkopo na asilimia hamsini fedha za TPDC (50:50); na

  (d)     mwezi Septemba kila mwaka wa tatu utakuwa ni mwezi ambao marekebisho ya tozo kwa miaka mitatu inayofuata yatawasilishwa kwa EWURA.

  4.                  Kwa mujibu wa kifungu 19(2)(b) cha Sheria ya EWURA (Sura ya 414 ya Sheria za Tanzania), tarehe 27 Novemba 2014, EWURA ilianza mchakato wa taftishi kukusanya maoni na hoja za wadau kuhusu uhalali wa ombi lililowasilishwa na TPDC. Wadau waliowasilisha maoni na hoja mbalimbali ni Baraza la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji (CCC), Baraza la Ushauri la Serikali kuhusu Huduma za Nishati na Maji (GCC), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Kampuni ya Saruji Tanzania (TPCC), PanAfrican Energy Tanzania Limited, Songas Limited, Maurel & Prom, Wizara ya Fedha, Wizara ya Maji, na Wizara ya Nishati na Madini. Aidha, hoja za wadau na ufafanuzi uliotolewa na TPDC vimezingatiwa na EWURA katika kutoa uamuzi wa ombi hilo.


  5.                  Tarehe  8 Januari na 6 Februari 2015, EWURA ilifanya mikutano na wadau wa karibu (Exit Conference) ambapo EWURA ilisambaza rasimu ya Agizo la EWURA (Draft Order) ili ijadiliwe na kupata maoni ya mwisho; na mkutano huo ulihudhuriwa na  wawakilishi wa Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Maji, Wizara ya Fedha, CCC, GCC, TANESCO, TPDC, PAT, Songas, na TPCC. Asasi zote hizo zilitoa maoni ya mwisho kwenye rasimu ya Agizo la EWURA. Kwa ujumla, EWURA imezingatia maoni yaliyopatikana katika mikutano hiyo na hatimaye kufikia maamuzi kwenye Ombi la TPDC.


  6.                  Katika kikao chake cha tarehe 19 Februari 2015, Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA, ilijadili Ombi la TPDC na kufikia maamuzi ya kipindi kifupi cha miezi mitatu (Interim Tariff) ambacho TPDC itakitumia kukamilisha ujenzi na kuwasilisha gharama halisi ambayo EWURA iliyahoji. Maamuzi yaliyotolewa ni kama ifuatavyo:

older | 1 | .... | 747 | 748 | (Page 749) | 750 | 751 | .... | 3272 | newer