Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 746 | 747 | (Page 748) | 749 | 750 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Kwa heshima na taadhima mnakaribishwa kwenye hadhara ya kuadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad Allah amuiye radhi.

  Hadhara itafanyika siku ya Jumamosi sawa na tarehe 21/02/2015  kwenye anuani ifuatayo ‘4O GOLDSMITH ROAD NN8 3RU’ kuanzia saa nane mchana hadi saa moja usiku.

  Masheikh kutoka sehemu mbalimbali wamealikwa kwa malengo ya kuilezea historia ya Mtume Muhammad (SAW) kwa kina. Sheikh Muhammadul Eid (Abu Eid) ataongoza shughuli hiyo kama mgeni rasmi.  Pamoja na mambo mengine hadhara ina malengo ya kuikutanisha jamii, kuwakumbusha watu wazima na kuwafundisha watoto tabia za Mtume (SAW) kama vile uaminifu ukweli na nyinginezo ili waweze kujifananisha nae. 

  Itakumbukwa kwamba sheikh Abu Eid yuko nchini Uingereza karibu wiki mbili sasa ktk ziara ya kida’wa na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzidisha mshikamano khususan ktk jamii zinazozungumza Kiswahili.

  Kwa wakazi wa Uingereza na hasa maeneo ya jirani mnahimizwa kujitokeza kwa wingi ili muweze kufadika na nasaha kutoka kwa masheikh mbalimbali. Kwa mawasiliano kuhusu shughuli unaweza kupiga na zifuatazo 07529302674 au 07986142485. 

  Wote mnakaribishwa.


  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wauguzi wa Kituo cha Afya cha Mlowa katika jimbo la Ismani kabla ya kuzindua kituo hicho akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 19, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipima mapigo ya moyo ikiwa ni ishara ya kuzindua kituo cha afya cha Mlowa katika jimbo la Isimani akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 19, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa kwenye kituo cha afya cha Mlowa katika jimbo la Isimani akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 19, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua matrekta madogo maarufu kwa jina la Power Tiller yanayotumika katika shamba la kilimo cha umwagiliaji la Magozi katika jimbo la Ismani wakati alipolitembelea shamba hilo akiwa katika ziara ya mkoawa Iringa Februari 19, 2015. Watatu kulia ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza.


  0 0

   Mshauri mkuu wa mradi wa NewsRadar, Romana Gersuni kutoka Ujerumani akielezea jinsi teknolojia hiyo mpya na ya kisasa ya ukusanyaji taarifa mbalimbali ya Push Observer inavyofanyakazi zake.
   mkuu wa mikakati wa kampuni ya Six Telecoms ambayo ni kampuni mama ya Push Observer, Rashid Shamte akielezea faida ambazo watazipata kampuni mbalimbali nchini, husasani za kibiashara kwa kujiunga na huduma ya NewsRadar waliyoianzisha nchii.
  Mkurugenzi Mtendaji wa  Kampuni ya Push Mobile Fred Manento akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ufanisi wa mradi wa NewsRadar ambao utawawezesha wafanyabiashara kupata taarifa mbalimbali kwa kutumia mradi huo mpya na wa kisasa nchini
   Afisa Mawasiliano wa kampuni ya Push Observer, Tunu Makamula akiteta jambo na wadau wa kampuni hiyo waliohudhuria semina elekezi na uzinduzi rasmi wa mradi wa NewsRadar ambao utawawezesha wafanyabiashara kupata taarifa mbalimbali kwa kutumia mradi huo mpya na wa kisasa nchini.

  Sekta zote Nchini sasa zinaweza kupata taarifa mbali mbali zilizorushwa kwene vyombo vya habari kupitia teknolojia mpya ya usambazaji taarifa ijulikanayo kwa jina la NewsRadar ya kampuni ya Push Observer.

  Push Observer Limited ni kampuni ya Tanzania inayomiliki vyombo vya kiinteligencia na teknolojia ya sanaa ya kufuatilia, kukamata na kuchuja vyombo vya habari - magazeti, matangazo (radio & televisheni), Internet na uchambuzi, ripoti ya ushindani kwa ajili ya biashara, serikali na wateja wengineo wa mashirika yasiyo ya kiserikali.

  Hivi sasa, Push Observer wanachunguza vituo vya redio 90+, vituo vya televisheni 15+, magazeti (magazeti, majarida, magazeti na majarida) 70+ na machapisho online ikiwa ni pamoja na blogs na mitandao maudhui. Observer ni kampuni ya kiTanzania inayoongoza kidigitali, kwa viwango vya kimataifa na ushirikiano wa kimataifa katika data na uanachama na vyombo kama FIBEP, Nudge, Vision Critical, na Harvard Innovation Labs.

  Kwa mujibu wa Mkuu wa Mikakati wa Six Telecoms, Kampuni mama ya Push Observer, Rashid Shamte alisema kuwa kupitia teknologia hii ya usambazaji ya kisasa, wateja wao wataweza kupata habari taarifa muhimu na mpya masaa ishirini na nne ya wiki. Aliongeza kuwa,tumezindua teknolojia hii kwa wateja wetu kutokana na teknologia ya uchunguzi wa vyombo vya habari kubadilika sana miaka ya karibuni”.

  “Huduma hii ya kusambaza taarifa imekuwa ya kisasa, rahisi na ya ubora wa hali ya juu kutokana na uwekezaji wetu katika teknolojia hii. Wana vifaa vya kisasa ambavyo vinaweza kupata taarifa kupitia televisheni, magazeti, mitandao ya kijamii na redio kwa muda muafaka, vifaa hivyo vinauwezo wa kupata taarifa had 350,000 kutoka vyombo mbali mbali. Kwa kutambua mahitaji ya wateja wetu kupata habari na taarifa za muhimu tumeamua kuzindua huduma hii na ili kuwahakikishia wateja wetu upatikanaji wa taarifa muhimu na taarifa zinginezo za kwene vyombo vya habari kwa muda muafaka” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Push Observer, Tom Kyalo.

  0 0

   Baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi Tanzania wakitoa heshima mbele ya jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Mzee Andrew Michael Kumalilwa ambae alikuwa mstaafu wa jeshi la Polisi kwa ngazi ya DCP
   Ndugu wa marehemu akijadiliana jambo na Mmoja wa Askari wa Jeshi la Polisi wakati wa Kutoa Heshima za mwisho kabla ya kwenda kuupumzisha mwili wa Mzee Andrew Kumalilwa ambae alizikwa nyumbani kwake Tabata Segerea tarehe 14 Februari 2015.
  Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi Tanzania, DCP Simon Siro akitoa maneno mafupi kabla ya kwenda kuupumzisha Mwili wa marehemu Mzee Andrew Kumalilwa katika nyumba yake ya Milele. Marehemu Andrew Kumalilwa alizikwa mnamo tarehe 14 February 2015 huko Nyumbani Kwake Tabata Segerea.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Afrika, Karibiani na Pasifiki (ACP) Alhaji Muhammad Mumuni (kushoto) akiwa  katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania Ubeligiji Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala baada ya kumaliza mazungumzo naye ofisini kwake Brussels. Alhaji Mumuni alifika ofisi za Ubalozi wa Tanzania kuishukuru Tanzania kwa kumuunga mkono toka alipoteuliwa miaka miwili iliyopita hadi anapomaliza kipindi chake cha miaka miaka miwili ya kutumikia Sekretarieti ya ACP.

  0 0

  Afisa Mkuu wa kitengo cha biashara ya jumla wa NMB Ndugu Richard Makungwa, (Kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF - Adam Mayingu. Katikati ni Meneja Mwandamizi wa kitengo cha biashara za Kitaasisi   NMB -oela Kivaria. 

   Afisa Mkuu wa kitengo cha biashara ya jumla wa NMB Ndugu Richard Makungwa (Kulia)  pamoja Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF -  Adam Mayingu, wakiashiria ushirikiano wa taasisi mbili kwa kugongesha  vinywaji  vyao  wakati wa hafla ya chakula cha jioni  iliyoandaliwa na NMB kwa wadau wa PSPF.
   Maofisa wa NMB wakifuatilia  jambo la muhimu wakati wa hafla hiyo ya PSPF iliyofadhiliwa na Benki ya NMB.  0 0

  Taarifa iliyotufikia mapema leo,inaeleza kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la ‘Chamber Squad’, Moses Bushagama ‘Mez B’, amefariki dunia leo asubuhi huko Mkoani Dodoma baada ya kusumbuliwa na Homa ya mapafu kwa muda mrefu. Taarifa ya kifo cha Mez B zimethibitishwa na mama yake mzazi, na kwamba alikuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Mwananchi.

  Mez B amewahi kulazwa na kuruhusiwa mara kadhaa katika hospitali ya Dodoma na hivi karibuni alizidiwa na kulazwa mkoani humo mpaka umauti ulivyompata.

  Baadhi ya nyimbo alizowahi kuimba Mez B ni pamoja na ‘Fikiria’, ‘Kama Vipi’, ‘Kikuku’, ‘Shemeji’ ‘Nimekubali’ pamoja na ‘Ghetto langu’ aliyoshirikishwa na Marehemu Albert Mangwea.

  Huyu ni msanii wa pili kufariki kutoka kundi la chamber squad. Miaka miwili iliyopita kundi hilo liliomboleza kifo cha mwenzao Albert Mangwea ‘Ngwea’ huku Mez B akiwa mstari wa mbele wakati wa mazishi yake.

  Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu (aliyenyoosha mkono), akimwonyesha Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, jinsi maji ya bahari yalivyoathiri eneola MnaziBay, karibu na kampuni ya kuzalisha umeme ya Maurel & Prom.

  Athari ya mmomonyoko wa ardhi katika eneo la MnaziBay inavyoonekana pichani. Mmomonyoko huo umetishia usalama wa Kiwanda cha kufua umeme unaotumiwa na wakazi wa Lindi na Mtwara cha Maurel & Prom.

  Na Veronica Simba aliyekuwa Mtwara Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu ameushukuru uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini kwa ushirikiano ilioonyesha katika zoezi linaloendelea kudhibiti kasi ya maji Pwani ya Mnazi Bay, yaliyosababisha mazingira ya hatari kwa bomba la gesi na kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Maurel & Prom.

  Alitoa shukrani hizo hivi karibuni wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene mkoani humo kukagua miradi mbalimbali inayosimamiwa na Wizara yake hususan Mradi wa bomba la gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.

  “Kazi iliyofanyika imewezesha kudhibiti kasi ya maji kuendelea kumega sehemu ya ardhi iliyobaki. Kazi ya kudhibiti kingo za bahari inaendelea vizuri na tunashukuru uwezeshaji wa haraka uliofanywa na Wizara na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),” alisema Dendegu.

  Akielezea hali halisi iliyopo sasa baada ya jitihada zilizofanywa kukabiliana na janga hilo, Dendegu alisema kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Mnazi Bay kinachoendeshwa na kampuni ya Maurel & Prom, kinaendelea kuzalisha gesi na Mikoa ya Lindi na Mtwara inaendelea kupata umeme.

  Kwa upande wake, Waziri Simbachawene alipongeza jitihada zilizofanywa na uongozi wa Mkoa wa Mtwara kusimamia zoezi zima la kuzuia mmonyoko wa ardhi katika kingo za bahari, Pwani ya Mnazi Bay. “Nawapongeza wenzetu, mmejitahidi. Mmefanya kazi kubwa kuokoa mali ya taifa,” alisema.

  Janga hilo la mmomonyoko wa ardhi, Pwani ya Mnazi Bay lilitokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na kusababisha kujaa kwa maji katika Pwani hiyo tofauti na hali ilivyo siku zote.

  Kujaa huko kwa maji kulisababisha mazingira ya hatari kwa bomba la gesi la inchi 16 ambapo ilibakia mita nne tu maji hayo kulifikia bomba hilo. Aidha, hali hiyo ya kujaa maji pia ilisababisha mazingira ya hatari kwa kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Mnazi Bay kinachoendeshwa na kampuni ya Maurel & Prom Tanzania (M&P) ambapo zilibaki mita 29 tu maji kufikia kiwanda hicho.

  Kiwanda hicho ndicho kinachochakata gesi inayoendesha mitambo ya Tanesco iliyopo Mtwara Mjini na umeme wake kutumiwa na wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara.

  Makundi ambayo yamekuwa mstari wa mbele kushirikiana kukabiliana na janga hilo ni pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, na Jeshi la Magereza.

  Mengine ni Kampuni ya Dangote, Kampuni ya Maurel & Prom Tanzania, Shirika la Petroli Tanzania (TPDC), Wizara ya Nishati na Madini na Wataalam kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

  0 0

  Rais wa Marekani, Barack Obama akitoa hotuba yake katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani uliofanyika katika Ukumbi wa Loy Henderson, Wizara ya Mambo ya Nje, jijini Washington DC nchini humo leo. Mkutano huo uliowashirikisha Mawaziri wanaoshughulika na masuala ya usalama kutoka mataifa mbalimbali duniani, Maafisa Waandamizi wa Umoja wa Mataifa (UN), Vyama vya Kiraia na Sekta Binafsi ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupambana na ugaidi pamoja na vurugu mbalimbali dunaini. Katika hotuba yake, Obama alisema mapambano dhidi ya watu wenye msimamo mkali hayawezi kulinganishwa na mapambano dhidi ya waislamu. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe aliiwakilisha Tanzania katika mkutano huo.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akimsikiliza kwa makini Rais Barack Obama (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba yake katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani uliofanyika katika Ukumbi wa Loy Henderson wa Wizara ya Mambo ya Nje, jijini Washington DC nchini humo leo. Mkutano huo uliowashirikisha Mawaziri wanaoshughulika na masuala ya usalama kutoka mataifa mbalimbali duniani, Maafisa Waandamizi wa Umoja wa Mataifa (UN), Vyama vya Kiraia na Sekta Binafsi ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupambana na vurugu na ugaidi dunaini. Katika hotuba yake, Obama alisema mapambano dhidi ya watu wenye msimamo mkali hayawezi kulinganishwa na mapambano dhidi ya waislamu, hivyo hakuna dini yoyote inayowajibika kwa ugaidi, isipokuwa watu ndio wanaowajibika kwa vurugu na ugaidi.
  Rais wa Marekani, Barack Obama akitoa hotuba yake katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani uliofanyika katika Ukumbi wa Loy Henderson, Wizara ya Mambo ya Nje, jijini Washington DC nchini humo leo. Mkutano huo uliowashirikisha Mawaziri wanaoshughulika na masuala ya usalama kutoka mataifa mbalimbali duniani, Maafisa Waandamizi wa Umoja wa Mataifa (UN), Vyama vya Kiraia na Sekta Binafsi ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupambana na ugaidi pamoja na vurugu mbalimbali dunaini. Katika hotuba yake, Obama alisema mapambano dhidi ya watu wenye msimamo mkali hayawezi kulinganishwa na mapambano dhidi ya waislamu. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe aliiwakilisha Tanzania katika mkutano huo.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto-mstari wa pili), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula (nyuma ya waziri) wakimsikiliza kwa makini Rais Barack Obama (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba yake katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani uliofanyika katika Ukumbi wa Loy Henderson wa Wizara ya Mambo ya Nje, jijini Washington DC nchini humo leo. Mkutano huo uliowashirikisha Mawaziri wanaoshughulika na masuala ya usalama kutoka mataifa mbalimbali duniani, Maafisa Waandamizi wa Umoja wa Mataifa (UN), Vyama vya Kiraia na Sekta Binafsi ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupambana na vurugu na ugaidi dunaini. Katika hotuba yake, Obama alisema mapambano dhidi ya watu wenye msimamo mkali hayawezi kulinganishwa na mapambano dhidi ya waislamu, hivyo hakuna dini yoyote inayowajibika kwa ugaidi, isipokuwa watu ndio wanaowajibika kwa vurugu na ugaidi. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi, akitoa mada, kuhusu benki hiyo inavyoweza kuwasaidia wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kutokana na ushikiano wa kibiashara baina ya taasisi nhizo mbili, wakati wa mkutani mkuu wa nne wa wanachama na wadau wa PSPF mjini Dodoma. Mkutano huo wa siku mbili umefungwao Alhamisi Februari 19, 2015.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akisikiliza kwa makini majadiliano ya wanachama na wadau wa Mfuko huo wakati wa mkutano mkuu wa nne wa wanachama na wadau wa PSPF mjini Dodoma ,leo Alhamisi Februari 19, 2015.
  Kaimu mkurugenzi wa fedha na utawala wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Yahaya Ally, akitoa taarifa ya fedha ya Mfuko huo wakati wa mkutano wa nne wa wanachama na wadau wa PSPF, mjini Dodoma. Mkutano huo ulioanza Februari 18, umefungwa leo Alhamisi Februari 19, 2015.


  0 0

  Na Bakari Issa,Dar es Salaam

  Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetoa agizo kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) kuzingatia kanuni za ushindani pamoja na kuiarifu EWURA kila TPDC inapofanya manunuzi ya thamani yanayozidi dola za Marekani 5 Milioni.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam,Mkururugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),Felix Ngamlagosi amesema agizo hilo litaanza kutekelezwa kuanzia tarehe 1 Aprili mwaka huu.

  Aidha,Ngamlagosi amesema EWURA ilifanya uchambuzi na faida ya mtaji,gharama za uendeshaji mradi,pamoja na tozo iliyoombwa na TPDC.
   Mkururugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),Felix Ngamlagosi akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) uliifanyika leo kwenye ofisi za EWURA jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.


  0 0

  Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel leo imemtangaza rasmi mshindi wa shindano la Airtel Trace Music star, shindano lilidumu kwa muda wa miezi mitatu maalum kwa wasanii chipukizi kuweza kuimba na kutuma nyimbo zao kwa kutumia simu zao za mkononi kama studio kwa lengo la kusaka na kuibua vipaji kwa wanamuziki chipukizi nchini.

  Akiongea na waandishi wa habari Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga alisema"Leo tunayofuraha kubwa kumtangaza mshindi wetu wa shindano la Airtel Trace Music Stars mara baada ya kuchaguliwa na majaji na kupigiwa kura na watanzania.

  "Washiriki watano ni kati ya wengi waliothubutu kuonyesha uwezo wao wa kushiriki kwa kupiga simu, kuimba na kutuma nyimbo zao na hatimae majaji wamesikiliza vipaji vyao kama walivyoimba na kuwachagua kuingia tano bora (top 5)" alifafanua Muga.

  Washiriki waliokuwa wamebahatika kuingia tano bora ni Nalimi Mayunga mwenye namba ya ushiriki (55100182), Christopher Kihwele (5510050), Tracy Eminence (55100420), Beautus Henry (55100106) na Rose Mbuya (55100366).

  Mshindi wetu ni Nalimi Mayunga mwenye namba ya ushiriki (55100182) ambae amechaguliwa na majaji wetu pamoja na kupigiwa kura nyingi na wananchi.

  Zawadi yake ni milioni Tshs 50mil, na pia atapata fursa ya kwenda kuiwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Airtel Trace Stars ya Afrika Nairobi Kenya yanayoshirikisha nchi 13 barani Afrika ambapo pia mshindi atakaepatikana atarekodiwa nyimbo zake katika studio za kimataifa nchini uingereza, na kupewa mafunzo toka kwa msanii nguli wa Afrika Akon.

  Nchi nyingine zinazoshiriki mashindano haya na zitakazotoa jumla ya vijana 13 barani Afrika ni pamoja na Kenya, Uganda Zambia, Madagascar, Malawi, Nigeria, Ghana, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, The Democratic Republic of Congo (DRC), na Gabon.
  Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga (kushoto) akimkabidhi mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga hundi ya mfano yenye dhamani ya sh. 50mil baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya Airtel Trace Music Stars, pia atapata fursa ya kwenda kuiwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Airtel Trace Stars ya Afrika yatakayofanyika Mjini Nairobi Kenya mwezi machi, anaeshuhudia ni Afisa Uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki.
  Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga akifurahia zawadi yake baada ya kuibuka mshindi wa mashindano hayo yaliyofanyika hivi karibuni. Mshindi huyo pia atapata fursa ya kwenda kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace Stars ya Afrika yatakayofanyika Mjini Nairobi Kenya mwezi machi.
  Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga (kati) akiwaimbia waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika hafla ya makabidhiano ya zawadi yake hundi ya sh. Milioni 50 kushoto yake ni Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki (kushoto) na Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga (kulia).

  0 0

   Mwanamitindo,Tausi Likokola akiwasili leo wa uwanja wa Ndege Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akitoke nchini Marekani kwa ziara ya siku 10 kushoto ni mama mdogo,Beatrice Likokola
   Mwanamitindo,Tausi Likokola akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo Jijini Dar es Salaam.
  Mwanamitindo Tausi Likokola akishiriki kucheza ngoma ya asili ya kundi la wanne Star mara baada ya kuwasili wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo Jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka)
                 
   Na Chalila Kibuda
  Mwanamitindo wa Kimataifa (Mtanzania) aishiye Ughaibuni, Tausi Likokola amesema Watanzania wanajitahidi mno katika tasnia ya mitindo, hivyo wanatakiwa  kuwa na ubunifu wa  kipekee kutokana kuwepo kwa ushindani katika tasnia hiyo.

  Tausi ameyasema hayo mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,amesma kwa miaka aliyoishi katika nchi za Ujerumani na Marekani, kwa sasa ndio ameona watanzania wakionesha ubunifu wao  ni mwanzo mzuri na wanaweza kufika mbali.

  Tausi amesema anatarajia kufanya ushiriki wa shughuli za kijamii, kwani ndio wajibu wake kama mwanamitindo kutokana na kuwa mchango wake unahitajika katika jamii zenye mahitaji maalum.
  Katika ujio wa Mwanamitindo huyo,Tausi anatarajia kutembelea  shirika lisilo la Kiserikali linaloshughulikia  watu wanaoishi na virusi (WAMATA) kutokana na kuwasaidia kwa kila hatua pamoja na kuzuru visiwa vya Zanzibar.

  ‘’Nimekuja katika ziara yangu hii nitafanya masuala ya kijamii lakini na uzinduzi wa mafuta ya marashi hapa nchini na nimeona uzinduzi huu ni ufanyie nchini kwetu iwe ni fahari yangu’’amesema Tausi .

  0 0

  Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Lowasa akiingia katika ukumbi wa baraza la wawakilishi kuuwaga mwili wa aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Marehemu Salmin Awadh Salmin aliefariki ghafla jana.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakiingia katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi kuuwaga mwili wa Marehemu Salimn Awadh.
  Mwili wa Marehemu Salmin Awadh ukiingizwa katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani kwa ajili ya kuagwa rasmi.
  Viongozi mbali mbali wakijumuika na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakitoa heshma za mwisho kwa marehemu Salmin Awadh Salmin katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani.


  0 0


  0 0

  Mkurugenzi wa Mradi wa "AIDS free", Bw. Samson Kironde(wa pili kushoto) akitoa maelezo mafupi namna mradi huo utakaotekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza na Polisi katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwa Kamishna Jenerali wa Magereza leo februari 20, 2015(wa pili kulia) ni Mkurugenzi wa Operesheni na Fedha, Bw. Mike Hames(wa kwanza kushoto) ni Afisa Mwandamizi anayeshughulikia masuala ya UKIMWI kutoka USAID, Bw. Erick Mlang'ha.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akisisitiza jambo katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwake leo februari 20, 2015 kati ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza, Polisi na Wasimamizi Wakuu wa Mradi wa "AIDS - free" utakaotekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza.
  Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza walioshriki katika mazungumzo rasmi kuhusu Mradi wa "AIDS - free" unaotarajiwa kutekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza(wa kwanza kulia) ni Kamishna Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa pili kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kushoto) ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Gedion Nkana(wa kwanza kushoto) ni Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Nsajigwa Mwakenja.
  Maofisa Wasimamizi wa Sekta ya Afya kutoka Jeshi la Polisi wakifuatilia mazungumzo rasmi kuhusu Mradi wa "AIDS - free"(wa kwanza kushoto) ni Dkt. Nyanda Lushina(katikati) ni Mrakibu wa Polisi, Husein Yahya.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(meza kuu) akiongoza mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwake leo februari 20, 2015 kati ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza na Wasimamizi Wakuu wa Mradi wa "AIDS - free" utakaotekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza.(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0


  Kituo cha kukuza soka la vijana cha Future Stars Academy(FSA) cha jijini Arusha  kinataraji kushiriki  katika  michuano ya Uganda Junior League inayotaraji kutimua vumbi jijini Kampala mnamo Aprili 24 hadi 26 mwaka huu.


  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi na mwanzilishi wa kituo hicho,Alfred  Itaeli alisema kuwa kituo chao kinataraji kupeleka timu ya watoto ya U-15 katika michuano hiyo kwa lengo la kushindana na kisha kunyakua ubingwa.


  Alisema kuwa  ushiriki wao umefuatia kupitia mwaliko walioupata kutoka nchini Uganda kutokana na  nchi hiyo kutambua jitihada za kituo chao za kukuza soka la vijana hapa nchini pamoja na ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki.


  Hatahivyo,mkurugenzi huyo alisisitiza ya kwamba katika kuhakikisha wanashriki mashindano hayo kituo chao kimeanza mkakati wa kusaka fedha za nauli na matumizi wakiwa nchini wakati wote wa mashindano kwa kusaka udhamini kutoka kwa wadu mbalimbali wa soka mkoani Arusha na nchini kwa ujumla.
  Alisema kuwa wameanzisha tamasha la soka liitwalo “Quiz Night” ambalo linataraji kufanyika mnamo febuari 28 mwaka huu katika viwanja vya TGT jijini Arusha ambapo wanataraji kukusanya fedha za ushiriki katika tamasha hilo ili ziweze kuwasaidia katika safari yao nchini Uganda.


  Itaeli,aliwataka wadau mbalimbali wa soka mkoani Arusha ana nchini kwa ujumla kuwapa sapoti katika safari yao kwa kuwa hadi sasa wamekusanya kiasi cha sh,2 milioni  ambapo kwa safari yote nchini humo kinahitajika kiasi cha sh,7 milioni.

  HABARI kwahisani ya libeneke la kaskazini blog

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika ibada ya mazishi ya Askofu Mstaafu wa Jimbo la Tunduru/ Masasi, Magnus Mwalunyungu yaliyofanyia kwenye kanisa la Tosamaganga mkoani Iringa Februari 20, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, na Askofu wa Jimbo la Iringa, Mhashamu Ngalalekumtwa (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza baada ya mazishi ya Askofu Mstaafu wa Jimbo la Tunduru Masasi, Mhashamu Magnus Mwalunyungu yaliyofanyika kwenye Kanisa la Tosamaganga mkoani Iringa Februari 20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Na Victor Mariki – Ofisi ya Makamu wa Rais

  Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, limetoa amri ya kfungwa shughuli za uzalishaji katika Kiwanda cha nguo cha 21st Century Limited kilichopo Kihonda Mkoani Morogoro leo ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira.

  Hatua hiyo imechukuliwa kufuatiwa na kupuuzwa kwa maelekezo na maagizo ya mazingira yaliyokuwa yakitolewa nyakati tofautit tofauti na Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Morogo .

  Kiwanda hicho chenye wafanyakazi 1779 kiliagizwa na kuelekezwa tangu mwaka 2006 mamlaka hizo kutumia mitambo ya kutibu majitaka yake kabla ya kuyatiririsha kwenye Mto Ngerengere ili kuhepusha jamii inayotumia vyanzo vya maji hayo na madhara ya kiafya.

  Aidha Taarifa ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ilifafanuwa kuwa mitambo ya kutibu sumu ya majitaka kiwandani hapo haina uwezo wa kutosha kutibu sumu zinazozalishwa na shughuli za uendeshaji wa kiwanda hicho.

  Taarifa hiyo iliongeza kuwa kufungwa kwa kiwanda hicho ni sehemu ya Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira Na. 20 ya mwaka 2004 pamoja na Kanuni za Mazingira ya mwaka 2007 ambazo zinavitaka viwanda kutibu majitaka yake hadi kufikia viwango vilivyowekwa kabla ya kumwaga au kutiririsha maji hayo kwenye mazingira.

older | 1 | .... | 746 | 747 | (Page 748) | 749 | 750 | .... | 3278 | newer