Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 745 | 746 | (Page 747) | 748 | 749 | .... | 3272 | newer

  0 0


  0 0

  TIMU ya Coastal Union ya Tanga imeondoka mkoani hapa leo asubuhi kuelekea mkoani Mtwara kwa ajili ya mechi yao ya Ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda SC itakayochezwa Jumamosi wiki hii.

  Coastal Union ambayo mechi yao iliyopita dhidi ya Mbeya City iliyochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani haikupata matokeo mazuri sana baada ya kulazimishwa sare hivo itaingia kwenye mechi hiyo mithili ya mbogo aliyejeruhiwa msituni.

  Akizungumzia maandalizi ya kuelekea mchezo huo,Kocha Mkuu wa Coastal Union,Mkenya James Nandwa alisema kuwa kikosi chake kimeimarika zaidi baada ya kuyafanyia kazi kwa asilimia kubwa mapungufu yaliyojitokeza mechi iliyopita.

  Alisema kuwa dhamira yake kubwa ni kuhakikisha kikosi hicho kinaibuka na ushindi kwenye mchezo huo ambao unatazamiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na kila timu msimu huu kuonekana kujiimarisha vilivyo kwa ajili ya kupata matokeo mazuri.

  "Kikosi changu kipo imara kuweza kuwakabili Ndanda SC ikiwemo kuhakikisha tunapata matokeo mazuri hii inatokana na maandalizi kabambe tuliyoyafanya hasa kubwa kurekebisha baadhi ya maeneo kwenye kikosi hiki "Alisema Kocha Nandwa.

  Alisema kuwa mipango yake hivi sasa ni kukiwezesha kikosi cha timu hiyo kuweza kufanya vizuri kwenye mechi zao zijazo ili kuweza kusogea kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi kuu hapa nchini.

  Msafara wa Coastal Union uliondoka leo mkoani hapa kuelekea mkoani Mtwara unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ,Albert Peter ambapo baada ya kuwasili mkoani mtwara utafanya mazoezi.

  0 0  0 0

   Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd (wa pili kushoto) akiwa katika meza kuu pamoja na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI,Mh. Hawa Ghasia (kushoto),Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Mh. Said Meck Sadick (wa pili kulia),Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi,Prof. Joseph Sembojo (katikati) pamoja na Dkt. Remy Sietchiping kutoka UN-Habitat wakati wa Mkutano wa Kikanda uliojadili Ukuaji wa maisha ya baadae kwa miji ya Afrika,uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam. Picha na Emmanuel Masaka,Globu ya Jamii.
   Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi,Prof. Joseph Sembojo akizungumza wakati wa ufunguzi Mkutano wa Kikanda uliojadili Ukuaji wa maisha ya baadae kwa miji ya Afrika,uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam. 
   Muwakilishi kutoka Shirika la UN-Habitat,Dkt. Remy Sietchiping akifafanua jambo juu ya changamoto mbali mbali zinazoikabili miji mingi ya mikubwa Afrika Mashariki wakati wa Mkutano wa Kikanda uliojadili Ukuaji wa maisha ya baadae kwa miji ya Afrika,uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam. 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda ameupongeza uongozi wa NMB kwa kubuni bidhaa bora na zinazoendana na watanzania wa kada zote akitolea mfano wa akaunti za Chap Chap.

  Mh Pinda aliyasema hayo alipotembelea banda la NMB katika hoteli ya St. Gasper ya mkoani Dodoma ambapo PSPF wanafanya mkutano wao na NMB kama mdau mkubwa ameshiriki na kuweka mabanda ya huduma mbalimbali zikiwemo za NMB Wakala, NMB E- statement na Chap Chap Instant Account kwaajili ya washiriki wa mkutano huo.

  Akaunti za Chap Chap ni za haraka na kumchukua mteja takriban dakika 10 tu kufungua akaunti na kupata ATM card papo hapo. Tekinolojia hii ni ya kipekee na inaweza kumfanya mtu akafungua akaunti yake popote alipo na kuanza kufaidi huduma mbalimbali kutoka NMB kupitia matawi Zaidi ya 170 na ATM mashine Zaidi ya 600 nchini kote.

  Unangoja nini kuwa na akaunti ya NMB kama huduma zimerahisishwa kiasi hicho? NMB Karibu yako Zaidi.
  Waziri Mkuu Mhe.Mizengo Pinda  akipata maelezo kutoka kwa  Afisa Mkuu wa kitengo cha biashara ya jumla wa NMB Ndugu Richard Makungwa juu ya huduma zaChap Chap Instant Acount na NMB Wakala. Huduma ya NMB Wakala humuwezesha mteja kutoa na kuweka fedha kupitia mawakala wa MaxMalipo waliotapakaa nchi nzima.
  Maafisa wa NMB wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda na viongozi mbali mbali kutoka PSPF nje ya ukumbi wa Mkutano wa St Gasper ambapo Mkutano mkuu wa Nne wa wadau wa PSPF unafanyika.

  0 0

   
  Since 2006 DCMA has been receiving grants from the Andrew Scrivener family for the purpose of supporting students of DCMA

  The Andrew Scrivener Fund (UK) was established in memory of the late BBC Philharmonic Orchestra violinist to sustain the Music studies of young and talented students from all over Tanzania. Over the years, DCMA has had four intakes of students supported by the Andrew Scrivener Scholarship to study different instruments. This year three DCMA students will receive support from the Fund.

  The students receiving scholarship assistance are Rahma Ameir for her study of the violin, Amina Omar for her study of the oud and Said Bhai Said for his study of the qanun.

  The Andrew Scrivener Scholarship Fund covers the students' course fees, costs for all study materials, purchase of the student's instrument of specialization and a weekly transport allowance for each of the students. 

  This Scholarship has been greatly sought after, with many students applying and seeking the assistance of the award. The expressed criteria for receiving the award is the student's level of need and talent, gender equity and promotion of assisting individuals on learning some specific instruments.  The Dhow Countries Music Academy is a not-for-profit music institution based in Zanzibar that provides quality music education in various instruments as well as music related disciplines such as traditional African Dance, Music Theory as well as providing music courses in several schools.

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akitoa hotuba ya ufunguzi rasmi wa Taasisi ya Sheria za Kimataifa ya Afrika-AIIL yenye Makao Makuu yake Jijini Arusha hivi karibuni.
  Sehemu ya Wajumbe akiwemo Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju (wa pili kulia) wakimsikiliza Mhe. Maalim (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Taasisi hiyo.
  Mhe. Maalim (wa tano kushoto walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe waliohudhuria ufunguzi rasmi wa Taasisi ya Sheria za Kimataifa ya Afrika iliyopo Arusha.

  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa bodi ya udhamini wa mfuko wa kuwaenzi waasisi wa Taifa, Kanali mstaafu Kabenga Nsa Kaisi, akimkabidhi Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, sheria namba 18 ya mwaka 2004 ya kuwaenzi waasisi wa Taifa.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na Mwenyekiti wa bodi ya udhamini wa mfuko wa kuwaenzi waasisi wa Taifa, Kanali mstaafu Kabenga Nsa Kaisi nyumbani kwake Mbweni, huku wajumbe wengine wakishuhudia.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na Mjumbe wa bodi ya udhamini wa mfuko wa kuwaenzi waasisi wa Taifa, Mama Fatma Karume nyumbani kwake Mbweni.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya udhamini wa mfuko wa kuwaenzi waasisi wa Taifa, nyumbani kwake Mbweni. (Picha na Salmin Said, OMKR)

  0 0

  Serikali ya wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFMSO), kupitia
  msemaji wake mkuu ambaye ni Rais wa Serikali ya wanafunzi, ndugu
  Clinton Boniface inakanusha taarifa zilizotolewa na gazeti la NIPASHE
  toleo namba 0578395 la tarehe 19/02/2015, lenye kichwa cha habari
  “WANAFUNZI WA IFM WAMTAKA LOWASA URAIS” na kwamba habari hizo
  hazijatolewa na uongozi wa IFMSO, wala hakuna mkutano wowote
  uliofanyika katika eneo la chuo cha usimamizi wa fedha kati ya
  waandishi wa habari na uongozi wa serikali ya wanafunzi na kutoa tamko
  hilo. Pia, kulingana na Katiba ya IFMSO kifungu namba 3, ibara ndogo
  ya 1, Katiba inakataza serikali ya wanafunzi (IFMSO) kushiriki katika
  mambo yoyote ya kidini au kisiasa, hivyo basi IFMSO inasikitishwa na
  taarifa hizo na inaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza
  kutokana na taarifa hizo.

  Imetolewa na;

  …..........
  Clinton Boniface.
  Rais wa Serikali ya Wanafunzi.
  IFM-SO
  19/ 02/ 2015.

  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu na kufanya mazungumzo na Balozi wa Saudi Arabia anayemaliza muda wake Mhe. Hani Abdullah Mominah wakati balozi huyo alipokwenda ikulu kuagana na Rais leo.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Balozi wa Saudi Arabia anayemaliza muda wake Mhe. Hani Abdullah Mominah wakati balozi huyo alipokwenda ikulu kuagana na Rais leo.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Saudi Arabia anayemaliza muda wake Mhe. Hani Abdullah Mominah wakati balozi huyo mara baada ya kuzungumza nae alipokwenda ikulu kumuaga Rais leo (picha na Freddy Maro)

  0 0

  Kamanda mkuu wa polisi wa Mkoa wa Mbeya Bwana Hemed Msangi (wa pili kulia) akimkabithi mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Edom Dickson Mwansasu mkazi wa Kyela Mbeya baada ya kuibuka moja kati ya washindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi. pichani kushoto ni mke wa Edom Mwansasu na kulia ni Meneja biashara wa Airtel Nyanda za juu kusini Bwana Straton Mushi.
  mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Edom Dickson Mwansasu akiwa ndani ya gari pamoja na mke wake baada ya kukabithiwa gari lake kufatia kuibuka kuwa mshindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi katika droo iliyofanyika ijumaa iliyopita.
  Mkazi wa kyela mkoani Mbeya Bwana Edom Dickson Mwansasu amekabithiwa gari aina ya Toyota IST na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel mara baada ya kuibuka mshindi kupitia droo ya wiki ya pili ya promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi iliyofanyika siku ya ijumaa iliyopita

  Bwana Edom Mwansasu mwenye umri wa miaka 40 anajishughulisha na shughuli za kilimo huko Ngonga Kyela  Mkoani Mbeya  ameibuka mshindi baada ya kununua na kujiunga na  vifurushi vya siku vya huduma ya Airtel yatosha kila siku.

  Akiongea baada ya kukabithiwa gari bwana Edom Mwansasu alisema ninafuraha sana kuwa mshindi  na kutumiza ndoto yangu ya kumiliki gari.  Nilipopigiwa simu sikuamini kuwa nimeshinda gari , nilifurahi sana nakupasha habari kwa familia yangu. Sijawahi kumiliki gari hivyo najisikia furaha sana Airtel kunizawadia mimi hii gari kupitia hii promosheni ya Airtel yatosha. Kwa kupitia gari hili sasa na uhakika wa usafiri mimi pamoja na familia yangu lakini pia litanisaidia katika kazi yangu ya kilimo na kuniwezesha kusafirisha mazao yangu kirahisi ukilinganisha na  awali nilikuwa natumia baskeli au kukodi gari.

  ‘Nawapongeza sana Airtel na nawashauri watanzania kuendelea kutumia huduma ya Airtel yatosha na kuamini kuwa nao wanaweza kubahatika na kushinda kama mimi” aliongeza Mwansasu

  Kwa upande wake Kamanda mkuu wa polisi wa Mkoa wa Mbeya Bwana Hemed Msangi alisema”  kwanza kabisa napenda kuwapongeza Airtel kwa kuanzisha promosheni hii kabambe inayowawezesha watanzania kutoka sehemu mbalimbali kujishindia magari.  Naamini kwa kupitia promosheni hii mtawawezesha watanzania wengi kujikwamua kiuchumi na kuwawezesha kufanya shughuli zao za kijamii na kiuchumi kirahisi na kwa ufanisi zaidi. Nawapongeza washindi wote waliopatikana mpaka sasa.  Lakini natumia fulsa hii kuwaomba wananchi wadumishe amani maana kama sio amani tulionayo basi promosheni kama hizi zisingeweza kufanyika”

  Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja biashara wa Nyanda za juu kusini Bwana Straton Mushi Alisema”  promosheni hii ya Airtel yatosha zaidi ni mahususi kwa wateja wetu Tanzania nzima wanaotumia huduma hii ya Airtel Yatosha kuweza kujishindia gari aina ya Toyota IST kila siku .  kujiunga na vifurushi vya Airtel yatosha mteja anatakiwa kupiga *149*99# au kwa kununua vocha vya Airtel yatosha au kununua kupitia huduma ya Airtel Money na kuunganishwa moja kwa moja kwenye droo itakayomwezesha kushinda.

  Mpaka sasa washindi 10 wamepatika ambapo kati yao wawili wanatoka kanda ya nyanda za juu kusini na leo tunamkabithi mshindi wetu wa Mbeya Bwana Edom Mwansansu gari lake na kisha tutamkabithi mshindi wa mkoa wa sumbawanga bwana Saidi Mashiko ambaye ni mganga wa tiba za jadi na mkazi wa Katavi hivi karibuni”

  “Natoa wito kwa watanzania na wateja wetu kujiunga na vifurushi hivi vya Airtel yatosha na kupata nafasi ya kujishindia gari aina ya Toyota IST kila siku”. Aliongeza Mushi

  Washinde wengine waliojishindia Toyota IST toka promosheni hii ianze ni pamoja na Ramadhani Dilunga mkazi wa Pwani, Namtapika Kilumba Mkazi wa Mtwara, said Mashiko mkazi wa katavi, Hamim Yoyo mkazi wa Korogwe Tanga, Esther Mashauri Mkazi wa Mwanza, Ibrahim Kimondo mkazi wa Kondoa pamoja na Mwajabu Churian, Sakina Libwana na Justin Wilium wote wakazi wa Dar

  0 0

  Na Teresia Mhagama

  Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress na Ujumbe wake, wamekutana na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachewene, katika makao makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.

  Viongozi hao walikutana ili kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo miradi ya umeme inayofadhiliwa na Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC), mradi mkubwa wa umeme unaofadhiliwa na nchi ya Marekani ujulikanao kama Umeme Afrika (Power Africa) pamoja na suala la kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake ili kuongeza uelewa na hivyo kuleta ufanisi wa kazi.
  Waziri wa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachewene (kulia) akishikana mkono na Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress mara baada ya kumaliza mazungumzo yao jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachewene (kulia) akimsikiliza kwa makini Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress (wa tatu kushoto) wakati Balozi huyo na ujumbe wake walipokutana Waziri wa Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Sharon Pauling, Naibu Mkurugenzi anayeshughughulikia Ukuaji wa Uchumi katika Shirika la Misaada la Marekani (USAID), (wa pili kushoto) na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkaazi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia nchini, Scott Alexander.
  Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachewene (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress (wa tatu kushoto), wakati Balozi huyo na ujumbe wake walipokutana Waziri wa Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Sharon Pauling, Naibu Mkurugenzi anayeshughughulikia Ukuaji wa Uchumi katika Shirika la Misaada la Marekani (USAID), (wa kwanza kulia), Mkurugenzi Mkaazi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia nchini, Scott Alexander (wa kwanza kushoto) na Merrica Dominick, Afisa Uchumi na Biashara katika Ubalozi wa Marekani nchini.

  0 0

  Wanafunzi wa shule ya msingi ya Mwenge iliyopo mkoani Lindi wakimsikiliza kwa makini mwalimu wa masuala ya Afya na Uzazi wa Mpango Monica Mfaume, wakati wa kuwagawia wasichana pedi na kuwapatia elimu ya Afya na uzazi, mpango huu uko chini ya mradi wa Hakuna Wasichoweza unaoendeshwa na taasisi ya T-Marc na kudhaminiwa na USAID na Vodacom Foundation na unawalenga wanafunzi waliopo mashuleni na wasio mashuleni zoezi hili limeanza kufanyika katika mikoa ya  Lindi na Mtwara.
  Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi ya Mwenge iliyopo mkoani Lindi wakifurahia baada ya kugawia pedi za kujikinga wanapokuwa kwenye hedhi .Mpango kwa kuwagawia wasichana pedi na kuwapatia elimu ya Afya na uzazi uko chini ya mradi wa Hakuna Wasichoweza unaoendeshwa na taasisi ya T-Marc na kudhaminiwa na USAID na Vodacom Foundation na unawalenga wanafunzi waliopo mashuleni na wasio mashuleni zoezi hili limeanza kufanyanyika katika mikoa ya Lindi na Mtwara.


  0 0


  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Ofisi Bw. Michael Madembwe akizungumza na wazalishaji na watumiaji wa takwimu leo jijini Dar es salaam. Warsha hiyo imewakutanisha wadau hao kutoka maeneo mbalimbali nchini, kubadilishana uzoefu na kuangalia changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika usambazaji na ukusanyaji wa takwimu nchini.
  Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Hajjat Amina Mrisho Said akifungua warsha ya siku mbili ya wazalishaji na watumiaji wa takwimu kutoka Wizara, Idara za Serikali, Wakala, Taasisi za Elimu na Utafiti, Vyuo Vikuu pamoja na Wadau wa mbalimbali wa maendeleo leo jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya washiriki wa warsha ya siku mbili ya wazalishaji na watumiaji wa takwimu kutoka Wizara, Idara, Wakala na Taasisi za Serikali, Vyuo vya Elimu ya Juu, Taasisi za kiraia,Taasisi za Utafiti na Wadau wa mbalimbali wa maendeleo leo jijini Dar es salaam.


  0 0

  Viongozi wa vitengo mbalimbali wa Benki ya Standard Chartered wakipigiga mpira kwa pamoja kuashiria uzinduzi wa shindano la soka la “Kombe la Standard Chartered – Njia Kwenda Anfield” katika ofisi za Benki hiyo mapema leo. Kutoka kushoto kwenda kulia ni: Femi Alonge - Mkuu wa kitengo cha Wateja wa Makampuni Makubwa, Juanita Mramba – Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masoko, Mike Shio – Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na Ruth Zaipuna – Mkuu wa Kitengo cha Fedha.

  0 0

  Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma

  Watu wawili wamefariki dunia papo hapo katika ajali ya Basi kugongana na Lori ajali iliyotokea tarehe 19/02/2015 majira ya saa 13:15hrs huko eneo la Vikonje Kata ya Mtumba Barabara ya Dodoma – Morogoro.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema ajali hiyo imehusisha Basi lenye namba za usajili T. 663 AXL aina ya SCANIA Kampuni ya KIDIA ONE lililokuwa litokea Dar es Salaam kwenda Mwanza likiendeshwa na ADAM s/o ROBERT, 38yrs, kabila Mnyaturu, mkazi wa Tegeta Dar es Salaam, liligongana uso kwa uso na Lori namba T.469 CFG Scania lenye Tellar T. 756 AZX.

  Kamanda MISIME amewataja waliofariki dunia kuwa ni FADHILI S/O HAMIDU SAIDI miaka 36, Kabila Msukuma ambaye ni dereva wa Lori na utingo wa Bus aliyehafamika kwa jina la CHOGO S/O CHIGUNDA, miaka 30, Kabila Muha wote wakazi wa Dar es Salaam.

  Majeruhi katika ajali hiyo ni 45 kati yao 34 ni wanaume na 11 ni wanawake; wengine wametibiwa na kuruhusiwa. Waliolazwa ni 24 kati yao wanaume ni 17 na wanawake ni 7.

  Kamanda MISIME amesema chanzo cha ajali ni dereva wa Bus Kushindwa kuchukua tahadhali wakati wa kulipita gari lingine “over take”, na kusababisha ajali hiyo.

  Aidha Kamanda  MISIME ametoa wito kwa madereva kuwa na udereva wenye tahadhali na kuzingatia sheria za usalama barabarani, kwani dereva huyu wa basi angezingatia hilo ajali hii haingetokea na hatakama ingetokea madhara yake hayangekua makubwa kiasi hicho.

  0 0

  Balozi wa Japan nchini Tanzania Mheshimiwa Masaki Okada akizumgumza na Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete pamoja na uongozi wa Taasisi hiyo muda mfupi kabla ya kutiliana saini mkataba wa mradi wa kupanua Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama iliyoko Rufiji, Mkoani Pwani tarehe 19.2.2015.
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akitiliana saini na Balozi wa Japan hapa nchini Mheshimiwa Masaki Okada kwenye mradi wa upanuzi wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama utakaogharimu dola za kimarekani 498,738. Sherehe ya utiaji saini ilifanyika kwenye ofisi za WAMA zilizopo karibu na Ikulu ntarehe 19.2.2015.


  0 0

  Na  Bashir  Yakub

  Wapo watu ambao shida yao ni kuandaa wosia  lakini tatizo  ni  waanzeje.  Je waandike kama barua, je waandike  kama makala,  je waandike  kama maombi ya  zabuni, je waandike kama notisi,  waandikeje hasa. Wapo watu ambao wameshaandika wosia lakini wameandika hovyohovyo tu bila mpangilio maalum. 

  Ikumbukwe kuwa wosia mbovu usio katika taratibu na mpangilio wa kisheria ni wosia ambao baada ya kufa kwako unaweza kuleta ugomvi mkubwa na hatimaye inaweza kuamuliwa kuwa wosia huo si halali hata kama ni kweli uliuandika  na hivyo kusababisha yale yote uliyotaka yafanyike baada ya kufa kwako yasifanyike. 

  Aidha hili ni tatizo ambalo  makala  haya  yaweza kusaidia  kulimaliza kwa atakayesoma. Mfano huu au  sample hii hapa chini ni ya kitaalam  na  ya kisheria  hivyo  mtu anaweza kuinakili hivihivi ilivyo  na akaitumia  kuandalia wosia wake.older | 1 | .... | 745 | 746 | (Page 747) | 748 | 749 | .... | 3272 | newer