Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 736 | 737 | (Page 738) | 739 | 740 | .... | 3272 | newer

  0 0  0 0

  Mbio za 13 za Kilimanjaro Marathon ambazo zimepangwa kufanyika Machi 1, 2015 mjini Moshi mkoani Kilimanjaro zimepata msisimko mpya baada ya wanariadha nyota wa Tanzania kuthibitisha kushiriki.

  Mkurugenzi wa Mbio hizo John Bayo jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliwataja baadhi ya wanariadha nyota kutoka Tanzania kuwa ni Andrew Sambu, Daudi Joseph, Mashaka Masumbuko, watachuana na wanariadha wengine kutoka nchini na kutoka nje ya nchi katika mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon kwa wanaume za kilometa 42.195.

  Kwenye upande wa marathon wanawake Fabiolla William, Sarah Maja and Banuelia  Katesigwa ni miongoni mwa nyota wa Tanzania watakaochuana na wenzao kutoka ndani na nje ya nchi katika kuwania tuzo mbalimbali kwenye Mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon kwa wanawake za Kilometa 42.195.

  Aidha, wanariadha Fabian Fabian Joseph, Alphonce Felix, Dickson Marwa wamethibitisha kushiriki Tigo Kili Half Marathon wanaume wakati Mary Naali, Natalia Elisante, Catherine Lange na Jacqueline Sakilu ni miongoni mwa majina maarufu katika riadha yaliyothibitisha kushiriki kupitia kundi la wanawake litakalochuana katika Mbio za Tigo Kili Half Marathon.

  Katika mbio za nusu marathon ambazo Tanzania ina historia ya kufanya vizuri, Fabian Joseph ana rekodi ya ushinda Kilimajaro Marathon mwaka 2010 ambapo alimaliza mbio katika muda wa 1:3;59 na vilevile ana rekodi ya kushinda Edmonton Marathon mwaka 2005 kwa muda wa 1:01:08.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Cuba Nchini Tanzania Jorge Luis Lopez Tormo leo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajiliya mazungumzo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Cuba Nchini Tanzania Jorge Luis Lopez Tormo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mgeni wake Balozi wa Jamhuri ya Cuba Nchini Tanzania Jorge Luis Lopez Tormo baada ya mazungumzo yao leo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar.Picha na Ikulu.

  0 0


  0 0

  “ Dr. Evans Rweikiza adressing the press during the official launching of Tanzania Financial services for Undeserved Settlements(TAFSUS) at Giraffe Hotel Dar es Salaam." .

  0 0

  Na Chalila Kibuda

  Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene amesema kushuka kwa bei ya mafuta kuendane na hali halisi ya vitu vyote vinavyotumia nishati hiyo.

  Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na wadau wa mafuta kupata mawazo katika uendeshaji wa sekta hiyo,Simbachawene amesema kuwa kushuka kwa mafuta hata nauli ya kusafiri kwa daladala pamoja na mabasi ya mikoani na nje ya nchi ni lazima zishuke.

  Simbachawene amesema watanzania wanataka kuona kushuka kwa mafuta kunaleta unafuu wa maisha na sio yanashuka katika soko lakini huduma zake zinabaki kama zilivyo,hata wale ambao wanasaga nafaka kwa kutumia nishati ya mafuta wanashusha bei zao kutokana na soko la mafuta kushuka na wananchi kuwa na imani mamlaka zinazoendesha soko hilo.

  “Imani yangu ni kuona watanzania wanapata mafuta bora na bei inashuka kwa pande zote na sio kushusha upande mmoja huku upande mwingine unapata huduma iliyo juu”amesema Simbachawene.

  Amesema wataendelea kufatilia uchakachuaji wa mafuta pamoja na umwagaji wa mafuta ili kuwe na uchumi imara na serikali kuendelea kupata mapato yake katika sekta hiyo,pia ataendelea kufatilia changamoto za wafanyabiashara wa mafuta ikiwemo suala la kodi kuwa kubwa.

  “Kazi yangu ni kuangalia mafuta yanaendelea kuwepo katika nchi kwani bila mafuta hakuwezi kuwepo uchumi imara”amesema Simbachawene.
  Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene akisisitiza jambo wakati akizungumza na wadau wa mafuta ili kupata mawazo yao katika uendeshaji wa sekta hiyo,leo kwenye ukumbi wa JB Belmonte,jijini Dar es salaam.Kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh. Charles Mwijage.
  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya MOIL,Mansoor Shanif akichangia mada katika mkutano huo.
  Sehemu ya wadau wa mafuta wakiwa kwenye mkutano huo.

  0 0

  Serikali imeanza kusambaza nakala milioni mbili za Katiba Inayopendekezwa nchini kote ili kuwawezesha wananchi kuisoma na kushiriki katika Kura ya Maoni iliyopangwa kufanyika tarehe 30 Aprili mwaka huu.

  Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro amesema leo (Jumatano, Februari 11, 2015) jijini Dar es Salaam kuwa kati ya nakala hizo zilizochapwa jijini Dar es Salaam, nakala 1,800,000 zinasambazwa Tanzania bara na nakala 200,000 zinasambazwa Tanzania Zanzibar.

  Kwa mujibu wa Waziri Migiro, hadi kufikia jana (Jumanne, Februari 10, 2015), jumla ya nakala 707,140 zilikuwa zimesambazwa katika mikoa 12 ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ambayo imepata nakala 200,000 na kuwa kazi hiyo inaendelea vizuri na inatarajiwa kukamilika katika muda mfupi ujao.

  Mikoa hiyo na nakala ziliozosambazwa katika mabano ni Katavi (15,640), Rukwa (27,040), Ruvuma (47,740), Mbeya (78,640), Simiyu (34,840), Mara (52,540), Tabora (58,540) na Kigoma (41,440). Mikoa mingine ni Kagera (54,340), Geita (36,940), Mwanza (57,040) na Pwani ambapo usambazaji umeanza kwa wilaya ya Mafia ambayo imepata nakala 2,400.

  “Idadi ya nakala ya Katiba Inayopendekezwa kwa kila mkoa inategemea na wingi wa kata katika mkoa, ndiyo maana baadhi ya mikoa unaona imepata nakala nyingi,” amesema Dkt. Migiro ofisini kwake wakati akiongea na baadhi ya waandishi wa Habari waliotaka ufafanuzi kuhusu hatua iliyofikiwa katika kazi ya uchapishaji na uasambazaji wa nakala za Katiba Inayopendekezwa.

  Kwa mujibu wa Waziri Migiro, kuna zaidi kata 3,800 nchini kote na lengo la Serikali ni kusambaza nakala 300 katika kila kata ambazo zitasambazwa kwenye vijiji, vitongoji na mitaa kupitia Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Miji, Manispaa na Majiji.

  Kuhusu taasisi za elimu na dini, Waziri Migiro amesema Serikali imepanga kusambaza nakala 658,400 kwa taasisi za elimu, dini, vyama vya siasa na asasi za kiraia na kuwa usambazaji huo utaanza hivi karibuni.

  Pamoja na usambazaji huo, Waziri Migiro amewakumbusha wananchi ambao bado hawajapata nakala za Katiba Inayopendekezwa, kuisoma kupitia tovuti ya Wizara ya Katiba na Sheria (www.sheria.go.tz) na tovuti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (www.agctz.go.tz).

  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na ujumbe wa mamlaka ya uwekezaji (Qatar Holding) mjini Doha, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne nchini Qatar.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa maendeleo ya biashara wa mamlaka ya uwekezaji ya Qatar Sheikh Faisal Bin Soud Al-Thani, baada ya mazungumzo yao mjini Doha.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akikabidhi zawadi kwa Mkurugenzi wa maendeleo ya biashara wa mamlaka ya uwekezaji ya Qatar Sheikh Faisal Bin Soud Al-Thani, baada ya mazungumzo yao mjini Doha.(Picha na Salmin Said, OMKR).

  0 0

  mengi2

  Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi.

  Na Andrew Chale wa modewjiblog.

  Mshindi wa Januari 2015 wa shindano la wazo la biashara 3N anatarajiwa kutangazwa siku ya Alhamisi ya Februari 12 kuanzia saa tano asubuhi jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa Dk. Reginald Mengi kupitia kurasa wake wa twitter, alitangazia umma kuwa Shindano hilo jipya lijulikanalo kwa kifupi -3N, ikiwa ni kifupisho cha ‘Nitabuni wazo la biashara, Nitatekeleza, na Nitafanikiwa’, ambapo mshindi wa kwanza wa mwezi Januari anatarajiwa kutangazwa siku hiyo ya alhamisi Februari 12. Dk. Mengi aliweka ujumbe huo twittter : “Kutokana na sababu zisizozuilika mshindi wa Januari wa shindano la 3N atatangazwa Februari 12 saa 5 asubuhi. Samahani kwa usumbufu wowote”.

  Kwa mujibu wa Dk. Mengi awali mshind I alitakiwa kutangazwa Jumatano ya leo ya Februari 11, kabla ya kusogeza mbele hiyo Februari 12. Shindano hilo litakuwa linafanyika kila mwezi kwa muda wa miezi sita kuanzia Januari Mosi 2015, hadi Juni 30, 2015, na mshindi wa kila mwezi atajishindia ruzuku ya shilingi milioni 10 atakazozitumia kutekeleza kwa vitendo wazo lake la biashara. 

  Shindano hilo, linawashirikisha Watanzania pekee, litaendeshwa kwa njia ya mtandao wa kompyuta ambapo mshiriki atatuma wazo lake la biashara kwa anuani ya twita @regmengi Shindano la Wazo la Biashara. Katika mchujo wa kwanza jopo la wataalamu litateua mawazo 10 bora Zaidi na waliotoa mawazo hayo watafanyiwa usaili kwa njia ya simu ili jopo hilo lijiridhishe kama mawazo waliyoyotuma ni yao binafsi, na kama wamejipanga vizuri kutekeleza kibiashara.

  Kutokana na mawazo hayo 10 teule, jopo litachagua wazo moja kuwa mshindi. Hii ni mara ya tatu kwa Dkt. Mengi kuendesha shindano kwa kutumia mtandao wa kompyuta wa twitter kwa kuamini kwake kuwa mitandao ya kijamii ina nguvu kubwa katika kuchochea ujasiriamali hasa kwa kizazi cha sasa.

  Shindano la kwanza na la pili lililoendeshwa mwaka jana lilikusudiwa kushawishi mawazo ya kuondoa umaskini katika taifa lenye utajiri mkubwa, lakini watu wake wengi wakiwa bado wametopea katika lindi la umaskini. Awali akizungumza katika uzinduzi wa shindano hilo, Dkt. Mengi alisema shindano hilo limelenga kuhimiza watu kuwa na upeo mkubwa wa kuona fursa za kibiashara na kuzitumia kujikwamua kiuchumi.

   Pia alisema shindano hilo ni mchango wake binafsi wa kuunga mkono jitihada za serikali na sekta binafsi za kuwakomboa wananchi kiuchumi kwa njia za ujasirimali, kwani amesema Sera zote mbili za kitaifa za Elimu ya juu na maendeleo ya viwanda vya kati na vidogo zina vipengele vya kuchochea na kuendeleza utamaduni wa ujasirimali wa mtu mmoja mmoja.

  “Kwa muda mrefu nimekuwa nikishawishi uwepo wa moyo wa ujasirimali miongoni mwa wa Watanzania na hasa kwa vijana. Ni ndoto yangu kuona uchumi wetu unakua kwa kasi kiasi cha kuzalisha zaidi ya mamilionea 100 kila mwaka wanaoendesha biashara halali,” alisema.
  Alisema kuwa na wazo sahihi la biashara, katika muda muafaka na eneo sahihi ni muhimu zaidi kuliko ruzuku ya fedha.

  “Nataka vijana watambue kwamba wanaweza kuanza na kitu kidogo na kukua kufikia kampuni kubwa kabisa ya kimataifa unayoweza kufikiria,” alisema na kusisitiza kwamba anaamini siku moja mazingira ya ujasirimali nchini Tanzania yakuwa miongoni mwa mazingira bora kabisa barani Afrika.

  Amesisitiza kuwa Shindano hilo liko wazi kwa watanzania wote na wanachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wanapeleka wazo lao la biashara kwa Dk Mengi kupitia mtandao wa kompyuta wa twita, kwa kumtag Dk Mengi kwenye @regmengi.

  Aidha amesema ni wale tu watakaomtag ndio watafikiriwa na jopo la wataalamu, na kusisitiza kuwa maamuzi ya jopo la Wataalamu yatakuwa ni ya mwisho.
  Washindi wa kila mwezi wataarifiwa kwa kutumiwa ujumbe mfupi kwa kupitia akaunti zao za twita (DM) na kupewa ruzuku yao katika sherehe fupi itakayohudhuriwa na waandishi wa habari.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongoza kikao cha Wizara ya Kilimo na Maliasili kilichozungumzia utekelezaji mpango kazi wa Wizara ya hiyo kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiongoza kikao cha Wizara ya Kilimo na Maliasili kilichozungumzia utekelezaji mpango kazi wa Wizara ya hiyo kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
  Waziri wa Kilimo na Maliasili Sira Ubwa Mamboya (katikati) akitoa taarifa ya utekelezaji mpango kazi wa Wizara ya hiyo kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi wakati wa kikao cha pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) Katibu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee na (kushoto) Naibu Waziri Mtumwa Kheir Mbarouk.Picha na Ikulu Zanzibar.

  0 0

  Na: Atley Kuni- Mwanza.

  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Magesa Mulongo
  Wazee katika Mkoa wa Mwanza, wamemshauri Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Magesa Mulongo kuanza kulima zao la alizeti ili kuuwezesha mkoa huo kuinuka kuichumi kutokana na hali mbaya ya mazao kama pamba kupoteza umaarufu kwenye sekta ya uchumi wa mkoa huo.

  Wakizungumza katika kikao kilicho wakutanisha wazee hao na mkuu wa mkoa hivi karibuni katika hoteli ya Mwanza, wazee hao walisema kutokana na hali isiyoridhisha kwa zao kama pamba ambalo ndilo lilikuwa zao kuu la uchumi wa mkoa huu kupoteza umaarufu ni vema sasa jamii ikabadilika na kuhamishia nguvu zake kwenye zao la alizeti.


  Akizungumza kwa niaba ya wazee wenzake, aliyekuwa Mkuu wa kwanza  wa wilaya ya Ilemela, Jared John Gachocha, alisema, haoni sababu ya mkoa wa Mwanza kushindwa kutilia mkazo zao la alizeti ambalo gharama zake za uzalishaji ni nafuu zaidi ukilinganisha na pamba.” 

  Mh. Mkuu wa mkoa mimi nadhani kipindi hiki tushughulike kufa na kupona kwenye alizeti, sioni kwa nini wenzetu wa Singida watupite katika hili, zao la alizeti ni rahisi mno kulilima halina usumbufu halihitaji mbolea nyingi, haliitaji maji mengi na maandalizi yake kwakweli ni rahisi lakini pia faida yake ni kubwa” alisema na kuongeza kuwa “hali hiyo itasaidia mkoa kujitosheleza kwa mafuta lakini pia kuweza kuuza kwa watu wengine.


  0 0


  Wachezaji wa Azam FC wakishangilia bao lao la tano dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Azama Complex jijini Dar es Salaam. Azam ilishinda 5-2. (Picha na Francis Dande)
   Mshambuliaji wa Azam FC, Salum Abubakar akimiliki mpira.
   Frank Domayo (shoto) akichuana na beki wa Kagera Sugar, Mussa Nampaka.
  Wachezaji wa Azam FC wakishangilia bao la kwanza la timu hiyo.
  Kipre Tchetche akimiliki mpira.
   Frank Domayo akishangilia bao lake.
   Kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohamed akiokoa moja ya hatari langoni mwake.

  0 0

   Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (Tanzania Bloggers Network - TBN ), Joachim Mushi (kulia) akitoa poe na kisha kukabidhi ubani wa fedha shilingi laki tano (500,000/-) jana zilizotolewa kwa mwanahabari wa Kitulo FM ya Njombe Bw. Conrad Mpila kama pole toka TBN baada ya kupoteza ndugu watano wa familia moja katika ajali ya moto iliyotokea hivi karibuni na kuua watu sita eneo la Kipunguni jijini Dar es Salaam. Katikati ni mmoja wa wajumbe wa TBN, Dotto Mwaibale. TBN ilishiriki katika mazishi ya marehemu hao sita waliozikwa jana katika makaburi ya Airwing, Dar es Salaam. Picha na Francis Dande.
   "Tupo nawe katika wakati huu mgumu..." anasema  Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (Tanzania Bloggers Network - TBN ) Bw. Joachim Mushi wakati anakabidhi ubani huo
  "Pole sana Conrad", Bw Mushi anamfariji mfiwa.

  0 0


  0 0   FOR HOTEL PROMO CODE NEXT TO THE VENUE CALL DMK GLOBAL @ 301-661-6207

  0 0


                                                                        http://europa.eu/about-eu/basic-information/symbols/images/flag_yellow_low.jpg

  EAST AFRICAN COMMUNITY - EUROPEAN UNION

  His Excellency Filiberto Ceriani Sebregondi, Ambassador of the European Union to Tanzania and to the EAC and his Excellency Dr. Richard Sezibera, Secretary General of the EAC signed today a Financing Agreement committing € 5 million in support to a Regional Electoral Support Programme (RESP).

  The European Union and the EAC share the principle of democracy, respect of fundamental rights and overall development, of which political elections are important milestones. The EAC Secretariat is committed to free, fair and peaceful elections in the region and support under this program is starting with Burundi and Tanzania in 2015.

  The RESP Programme, financed by the European Development Fund (EDF) will support the EAC capacity to follow-up the elections to be held in the Partner states between 2015 and 2018. It is intended to enhance democratic governance and political integration in the East African Community.

  The Programme will therefore support the EAC Secretariat in strengthening her capacities for electoral observation according to internationally recognized methodology.

  The EAC Forum of Electoral Commissions and other regional fora and knowledge-sharing platforms will be reinforced to encourage peer-learning among Partner States Electoral Management Bodies (EMBs), as well as to generate, share, disseminate and apply evidence and research-based electoral knowledge.

  EU Ambassador to Tanzania and the EAC, Filiberto Ceriani Sebregondi said: "Election observation is a vital component of European Union activities to promote democracy, human rights and the rule of law worldwide. Election observation can contribute to strengthening democratic institutions, build public confidence in electoral processes and help deter fraud, intimidation and violence.

  Through this project, the EU is partnering with the EAC Secretariat to achieve these shared goals in the region".

  The European Union will continue to support the East African Community, building on the achievements of a long-lasting engagement with a new Regional Programme between the EU and the EAC which will benefit the region for a total of 85 Million Euro from 2014 to 2020

  On his part the East African Community Secretary General Amb Dr. Richard Sezibera noted that  for the EAC to attain its Vision of  a prosperous, competitive, secure, stable and politically united East Africa; this support is important and timely.

  0 0

   Mdau mkubwa wa libeneke la Globu ya Jamii,Cheif Issa Kipande "Cheif Issa" (pili kulia) akiwa na kikosi kazi ya Michuzi Media Group wakati alipotembelea ofisi hizo zilizopo kwenye Jengo la Palm Residency (jirani na hospitali ya Ocean Road) Jijini Dar es saalam leo. Cheif Issa yupo nchini kwa mapunziko mafupi na siku si nyingi atarejea nyumbani kwake nchini Sweden.Wengine pichani toka kushoto ni Othman Michuzi,Ahmad Michuzi na Jonathan Msei a.k.a Gia Kubwa.
  Hapa Cheif Issa akiwa na Jonathan,Ahmad na Sam.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato (katikati) akifurahia jambo wakati akizungumza Balozi wa Japan Masaki Okada (kulia), pamoja na wawakilishi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya sherehe ya utiaji sahihi wa mkataba wa uwekwaji mashine ya kukamualia mafuta ya Alizeti wilayani Chato. Hafla hiyo ya utiaji saini umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Japan, Masaki Okada, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi ambaye ni Mbunge wa jimbo la Chato Mhe. John Magufuli kabla ya tukio la utiaji sahihi nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Na Teresia Mhagama 
   Wizara ya Nishati na Madini imepata Tuzo ya Ki¬mataifa ya mwaka ya Maende¬leo ya Udhibiti wa Sekta ndogo ya Mafuta na Gesi. Tuzo hiyo ya mwaka 2014 inayotolewa na Kampuni ya Kimataifa ya Wildcat International, ya nchini Marekani kupitia machapisho yake maarufu Duniani ya The Oil & Gas Year (TO&GY), imekabidhiwa rasmi jijini Dar es Salaam kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene ambaye alipokea Tuzo hiyo kwa niaba ya Wizara. 
   Tuzo hiyo, iliyotolewa na Mratibu wa Mahusiano kwa Wateja kutoka Jarida la TO&GY, Bi. Laura Carr inaitambua Wizara kutokana na mafan¬ikio yake katika kushughulikia changamoto za udhibiti wa sekta ndogo ya mafuta na gesi na hivyo kuchochea maende¬leo ya sekta hiyo. 
   Mafanikio hayo ni pamoja na kuwa na sera mpya ya gesi asilia, kuwa na muundo mpya wa makubaliano ya gharama za utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi (Production- Sharing Agreement), na kuwa na Rasimu ya Sera Uweze¬shaji na Ushirikishaji Wazawa (local content policy).
  “Hayo ni baadhi tu ya maendeleo yaliyofanya sekta hii kueleweka na kuku¬balika zaidi kwa wawekezaji na wadau,” imesema sehemu ya Jarida la TO&GY. 
   Pamoja na Tuzo ya Wiz¬ara ya T0&GY, Shirika la Umeme nchini kupitia Mkurugenzi wake, Mhandisi Felchesmi Mramba ameshinda Tuzo ya Mtu wa Mwaka (Person of the Year, 2014) kutoka¬na na mIpango yake ya Dola za Kimarekani Bilioni Sita zitakazowezesha TANESCO kuongeza uzalishaji umeme mara tatu zaidi ya sasa kutokana na vyanzo mbalimbali kama makaa ya mawe, gesi asilia na maji hivyo kuondokana na utegemezi wa uzalishaji umeme kwa ku¬tumia mafuta. 
   Aidha Shirika la Maende¬leo ya Petroli nchini (TPDC) limeshinda Tuzo ya transition of the year (2014) kutokana na kupiga hatua katika shughuli zake ambapo mbali ya kuwa kuwa mdhibiti wa sekta ndo¬go ya mafuta na gesi bali pia limekuwa mwekezaji baada ya kushinda tenda na kupata vitalu viwili kwa ajili ya utafiti wa mafuta na gesi nchini. 
   Usambazaji wa machap¬isho ya TO&GY hukaguliwa na Taasisi ya Marekani ya BPA Worldwide inayokagua machapisho maalum zaidi ya 2600 katika nchi 30 Duniani yakiwemo majarida maarufu ya Toronto Star, Wall Street Journal na Gulf News.
  Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia)  akipokea Tuzo ya Ki­mataifa ya mwaka ya Maende­leo ya Udhibiti wa Sekta ndogo ya Mafuta na Gesi inayotolewa na Kampuni ya Kimataifa ya Wildcat International, ya nchini Marekani kupitia machapisho yake maarufu Duniani ya The Oil & Gas Year (TO&GY). Anayemkabidhi Tuzo hiyo ni Mratibu wa Mahusiano kwa Wateja kutoka Jarida la TO&GY, Bi. Laura Carr.

  Mratibu wa Mahusiano kwa Wateja kutoka Jarida la TO&GY, Bi. Laura Carr (kushoto) akionyesha chapisho  maarufu Duniani la The Oil & Gas Year (TO&GY) linalotolewa na Kampuni ya Kimataifa ya Wildcat International, ya nchini Marekani. Chapisho hilo lina habari mbalimbali kuhusu masuala ya Nishati ikiwemo fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini kupitia sekta hiyo.Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.
  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Saleh M. Jidawi (wa kulia waliokaa) na Meneja wa Kampuni ya Simed International Services ya Uholanzi Nd. Michor Pleijzer wakitia saini mkataba wa uboreshwaji wa wodi ya wazazi na watoto Unguja na Pemba huku wakishuhudiwa na Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman na Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Mr. Jaap Frederiks katika hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Saleh M. Jidawi (kulia)na Meneja wa Kampuni ya Simed International Services ya Uholanzi Nd. Michor Pleijzer wakibadilishana hati za makubaliano ya uboreshwaji wodi ya wazazi na watoto za Unguja na Pemba katika hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
  Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Mr. Jaap Frederiks (wakatikati mbele walio simama)katika picha ya pamoja ya viongozi wa Wizara ya Afya ya Zanzibar wakiongozwa na Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman wa mbele kulia. Sherehe hiyo ilifanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

older | 1 | .... | 736 | 737 | (Page 738) | 739 | 740 | .... | 3272 | newer