Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad awasili nchini Qatar kwa ziara ya siku nne ya kiserikali.

0
0
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Seif Sharif Hamad, akiwa na ujumbe wa SMZ mjini Doha kwa ajili ya kuanza ziara ya kiserikali nchini Qatar.
 Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mama Awena Sinani Massoud (kushoto), akiwa na viongozi wengine wa SMZ tayari kwa kuanza ziara nchini Qatar.
Waziri wa Nchi, ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej, akibadilishana mawazo na maofisa wa mambo ya nje, tayari kwa kuanza ziara nchini Qatar. (Picha na Salmin Said, OMKR)

Na: Hassan Hamad, Qatar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Seif Sharif Hamad, amewasili mjini Doha nchini Qatar kwa ajili ya ziara rasmi ya kiserikali.

Katika ziara hiyo ya siku nne, Maalim Seif anaambatana na viongozi mbali mbali wa SMZ wakiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Ali Juma Shamuhuna na mwakilishi wa jimbo la Kwamtipura Mhe. Hamza Hassan Juma.

Viongozi wengine ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dr. Omar Dadi Shajak na Katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, wanawake na watoto Bi. Asha Ali Abdallah.

Akiwa nchini Qatar, pamoja na mambo mengine Maalim Seif atatembelea mamlaka ya uwekezaji nchini humo pamoja na kuona na watanzania waishio nchini Qatar.

TANZANIA YASAINI MAKUBALIANO NA UINGEREZA YA KUKOMESHA NDOA ZA UTOTONI NA UKEKETAJI KWA WATOTO KIKE

0
0
 Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Bi Sophia Simba (katikati) akisaini makubaliano ya pamoja baina ya Tanzania na Uingereza ya kukomesha ndoa za utotoni na ukeketaji wa watoto wa kike. kutoka kushoto ni Kamishna Mkuu wa Uingereza nchini,Bi.Dianna Melrose kulia ni Mwakilishi wa UNFPA,Dr.Natalia Kanem, leo katika ofisi za Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto.

Picha ya pamoja baada ya kusaini makubaliano ya pamoja baina ya Tanzania na Uingereza  kukomesha ndoa za utotoni na ukeketaji wa watoto wa kike.
 Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Bi.Sophia Simba (pichani) akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano ya pamoja baina ya Tanzania na Uingereza ya kukomesha ndoa za utotoni na ukeketaji wa watoto wa kike,leo katika ofisi za Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto jijini Dar.
PICHA NA EMMANUEL MASSAKA.

MWALIMU WA KISWAHILI JIJINI PARIS, UFARANSA, AZIZA MOHAMED ABUBAKAR

JK AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA TANZANIA 2015

Ziara ya naibu waziri wa Maji Mhe Amos Makalla wilayani Hanang leo

0
0
Naibu waziri wa maji Amos Makalla amefanya ziara ya kikazi wilayani Hanang leo kwa kutembelea mradi wa maji kijiji cha Ishponga na kuagiza Generator lifungwe haraka kurejesha huduma ya maji iliyosimama kwa miezi mitatu 
Amekagua mradi maji Kateshi na kuhaidi kushughulikia tatizo la nishati ya umeme linalopelekea mamlaka kushindwa kumudu gharama za uendeshaji 
Ameweka jiwe la msingi mradi mkubwa wa maji kijiji cha Simbay kata na tarafa ya Simbay Aidha ameagiza mradi wa mradi wa maji wa Endasak utakaohudumia vijiji vitatu wiki ijayo halmashauri itangaze zabuni za kumpata mkandarasi kwani tayari wizara imeshatuma shilingi milioni 300 Ameagiza watu 39 waliovamia chanzo cha maji Endasak wapewe notisi waondoke eneo la chanzo
Naibu waziri wa maji Mhe. Amos Makalla akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Sumaye huko Hanang leo
Naibu waziri maji Amos makalla akiweka jiwe la msingi mradi maji kijiji cha Simbay- Hanang
Naibu waziri maji kushoto na mbunge wa Hanang wakiwasikiliza viongozi wa kijiji cha Ishponga

Naibu waziri Amos Makalla akizungumza  na mbunge wa Hanang na waziri ofisi ya Rais (Mahusiano)  Dr Mary Nagu
Naibu waziri maji akikagua tanki la maji mji wa Katesh

Meya Manispaa ya Kinondoni aagiza Wenyeviti kusimamia Watendaji kutekeleza Miradi

0
0
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akikata utepe kuzindua Daraja la Mabwepande, Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Eng. Mussa Nati akizungumza wakati wa kikao cha wenyeviti wa Serikali za Mitaa,uliofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza na wenyeviti wa Serikali za Mitaa.
Wenyeviti wa Serikali za mitaa, manispaa ya Kinondoni wakimsikiliza Meya Yusuph Mwenda.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (wa pili kushoto), Naibu Meya, Songoro Mnyonge (wa pili kulia), Afisa Utumishi wa Manispaa, Mgomi (kulia) wakifuatilia kikao hicho.

PRESIDENT KIKWETE SALUTES Islamic Republic of Iran on the occasion of celebrating 36th Anniversary of the Islamic Revolution

0
0
H.E. Hassan Rouhani, President of Iran

His Excellency Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to His Excellency Hassan Rouhani, President of the Islamic Republic of Iran on the occasion of celebrating 36th Anniversary of the Islamic Revolution of Iran. The message reads as follows;



“Your Excellency

Hassan Rouhani,

President of the Islamic Republic of Iran,

TEHRAN

Your Excellency and Dear Brother,

On behalf of the Government and People of the United Republic of Tanzania and indeed on my own behalf, I would like to take this opportunity to extend to Your Excellency and through you, to the Government and People of the Islamic Republic of Iran our profound congratulations and best wishes on this historic occasion of celebrating the 36th anniversary of the Islamic Revolution of Iran.

The People of Tanzania and Iran enjoy cordial relations cemented by historic and cultural bonds dating back long ago. These relations provide a strong foundation for fraternal relations between our two countries that have been nurtured and developed by successive leadership in our two countries. In that regard, Tanzania and Iran maintain close cooperation in a number of important areas such as health and education. We wish to consolidate further and expand these relations to include other sectors such as transport, trade, investments, technology, oil, gas and communication.  

Your Excellency,

I would like to assure you of my personal commitment as well as that of my Government to continue working closely with your Government at bilateral and international levels. It is my sincere hope that our traditional cooperation through NAM and the UN aimed at enhancing peace and security as a basis for socio-economic development not only in our countries but also at global level.

While wishing you continued personal good health, happiness and prosperity for the people of Iran, please accept, Your Excellency the assurances of my highest consideration”.



Issued by: The Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam

10th February, 2015

leo ni hepi besdei ya kuzaliwa mtoto Benedickt wa mdau ernest makulilo - waraka toka kwa baba mtu

0
0
 HAPPY BIRTHDAY BENEDIKT FULBRIGHT MAKULILO
 HAPPY BIRTHDAY BENEDIKT FULBRIGHT MAKULILO
 HAPPY BIRTHDAY BENEDIKT FULBRIGHT MAKULILO
My dearest son, Benedikt
Today is your 4thBirthday. It is another February 10th of the year. You were born at 5:42pm Pacific Standard Time. Your birth is a blessing and that’s why you are Benedikt. You have helped us to be better human beings by reflecting our lives as parents. Both Marie and I are thankful to God every day to have such a wonderful little guy.
For the past four years we haven’t settled into one area for a long time. You know it was because of job change. I am proud of you whenever we moved you adopted quickly and enjoyed the area. There is a big possibility to have another move this summer. If I get accepted into my PhD studies, obvious we will move to another state. You will enjoy more to the new area, play with snow which you’ve not experienced in your four years. We’ll have so much fun.
On your first birthday’s letter, I promised one thing. I promised to take you to Tanzania when you are older enough so that you can meet all my family members and know my roots. I remember you had a dream and said we were together in Tanzania and you milked a cow….yes, when we are there you will milk cow. I think this year we can work out and take you to Tanzania. Unfortunately you will not meet Babu (your grandfather). He is already in heaven with his three children; Scolastica, Stanslaus and Vincent. Though you’ll not meet him, you will get opportunity to see his legacy which I am very much proud of his accomplishments as a committed father, a non-corrupt personnel, religious and above all the only person who valued education to his children than any person I have ever seen in this world.
Recently we have not been able to play soccer and run many times as we used to. We have to go back to our routine of going to the park and have more fun. I know when you go to school you will learn other kind of sports. I have no problem with any sport of you and enjoy playing. What I promise is: I will support you in any sport, take you to practice and attend your games. The most important thing is have fun and enjoy the talents you have been given by God. But if you want to be professional in any sport, remember hardworking and prayers will take you to another level. Talent is nothing if you don’t work hard on it. Always remember to pray and ask for God blessings no matter what, whether you are in success or hard time.
Nothing in this world comes easy. You will face so many challenges. You will fail and loose so many things. The best thing is to learn from your failures and challenges you face to make you a better person and a winner. This is one of the reason when you and I compete on running I don’t let you win every time. I give you opportunity to work harder. This is what Carl Brashear said “It is not a sin to be knocked down; it’s a sin to stay down”. Always get up and do it again. Don’t allow failure and challenges steal your dreams and achievements.
For the past year, you started saving some money (pennies and quarters) in your pig bank for ice-cream. You didn’t touch a single coin, you were determined to have enough money for ice-cream. You managed to have like $20 for such a period. I’m very much proud of you son in that accomplishment. To me is not about how much money you have collected and saved. It is about discipline, commitment and long term goals you have. Many of us hard time to have such discipline. 
You and I have our own tradition for your birthday. We are going to the bus ride as we have been doing in all other birthdays. And this letter is another gift for you. I have kept all letters I have written to you. I’m going to publish it into a book titled “THE BENEDIKT FACTOR”. You are the really factor of my life. You are the game changer. You have given me opportunity to look life into a different angle as a father and husband. You’ve helped me to know how important mothers are to children. As most men we take things for granted. But being in the labor room for your birth and see how mothers go through, I have different and most positive perspective on women and mothers. I know without you, things would be different.

You are the best my little crazy guy.

Nakupenda Sana
HAPPY BIRTHDAY BENEDIKT FULBRIGHT MAKULILO
Your loving Baba

Ernest

JK afungua jengo la upasuaji katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro

0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua jengo la upasuaji katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro muda mfupi baada ya kulifungua leo.Kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt.Steven Kebwe.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Mawenzi mjini Moshi muda mfupi baada ya kufungua jengo la upasuaji na kuweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa wodi ya mama na watoto katika hospitali hiyo leo.(wanne kulia ni Naibu waziri wa Afya Dkt.Steven Kebwe,wanne kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama,Kushoto ni Mbunge wa Vunjo Agustino Lyatonga Mrema,na wapili kushoto ni Mbunge wa Moshi Vijijini Dkt.Cyril Chami.

introducing Wimbo mpya wa msanii Dakee - "Rest In Peace"

BREAKING NEWZZZZZ:MOTO MKUBWA UMEZUKA KATIKA MOJA YA JENGO MTAA WA LIBYA/MOSQUE JIJINI DAR

0
0
Na Chalila Kibuda.

MOTO umezuka mapema leo na kuteketeza majengo matatu ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika makutano ya Mtaa wa Libya na Mosque jijini Dar es Salaam.


Moto huo ulioanza majira ya saa tatu asubuhi kwa kuanza kufuka moshi na baadae kuwaka na kuteketeza eneo lote la juu ya majengo hayo.



Akizungumza leo na waandishi wa habari katika eneo la tukio Kamanda wa Kanda Polisi Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova amesema vikosi vya uokoaji na Zimamoto vimefanya ushirikiano katika kuzima moto huo baadhi ya maeneo na kuokoa maduka katika majengo hayo.


 ‘’Vikosi vya zimamoto vimefanya ushirikiano kwa kuleta magari sita ya kuzima moto na kufanikisha kuuzima moto ambao ulikuwa mkubwa sana’’amesema Kova.


Kova amesema kuwa vikosi vya ukoaji vya zima moto vimefanya kazi kwa ushirikiano ambavyo ni  Zimamoto za Uwanja wa Ndege,Zimamoto ya Kampuni ya Ulinzi ya Ultimate,Night Support ,pamoja  na Kikosi cha Zimamoto ya Jiji.


Amesema kuwa  chanzo cha moto bado hakijafahamika mpaka sasa na uchunguzi wa kubaini chanzo cha moto huo bado unaendelea.

Naye Kamishna msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Kanda Maalum ya Dar es salaam,Jeswald Nkongo amewataka wananchi kutoa taarifa mapema pindi waonapo matukio ya moto na sio kudharau kwa kuamini kuwa moto ni mdogo na wanaweza kuudhibiti.
Moto Mkubwa umezuka mapema leo kwenye moja ya nyumba pichani iliopo mtaa wa Libya na Mosque jijini Dar es salaam na kuteketeza  mali kadhaa. Kikosi Kazi cha Globu ya Jamii kipo eneo la tukio kwa sasa kikiendelea kukusanya kila kinachojiri,lakini kwa taarifa kutoka kwa mashuhuda waliopo eneo la tukio wanaeleza kuwa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika rasmi,Jeshi la Polisi limefika eneo la tukio kuhakikisha amani na utulivu vinakuwepo huku magari ya zimamoto nayo yakiendelea kuwasili kupambana na moto huo..
Mmoja wa wapiga picha akitazama kwa mshangao moto mkubwa uliokuwa ukiendelea kuwaka kwa nguvu na kuteketeza baadhi ya mali zilizomo ndani ya jengo hilo lililopo mtaa wa Libya na Moski-Kariakoo jijini Dar.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalim ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova akizungumza na vyombo vya habari.
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Jeswad Nkongo akizungumza na vyombo vya habari juu ya walivyofanikiwa kuudhibiti moto huo.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI NA HAMIS MAKUKA

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

NYUMBA TATU ZAUNGUA MOTO KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

MAKAMU WA RAIS AONGOZA MAELFU KATIKA MAZISHI YA WATU SITA WA FAMILIA MOJA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MOTO

0
0


 Baba wa watoto wawili waliokufa katika ajali ya moto, Emmanuel Mpila akiweka shada la maua katika kaburi la mmoja wa watoto wake, Pauline
.

 Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akiweka shada la maua.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akiweka shada la maua.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya akiweka shada la maua.
 Jaji Mkuu mstaafu, Agustino Ramadhani akiweka shada la maua.

Dar es Salaam Institute of Technology VACANCIES

CHONDE CHONDE WATUMIAJI WA INTERNETI TUMIENI TEKNOLOJIA HII KUPATA MAARIFA-VODACOM TANZANIA

0
0
Watumiaji wa teknolojia ya interneti nchini wametakiwa kutumia teknolojia hii kutafuta taarifa mbalimbali za maarifa na zenye  mwelekeo wa kuleta maendeleo badala ya kutumia teknolojia hii kutafuta taarifa zisizo na faida na zenye mwelekeo wa kupotosha kizazi cha sasa kimaadili.
Wito huu umetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (pichani) katika siku ya matumizi ya interneti duniani iliyoadhimishwa leo duniani kote ambako alisema kuwa Vodacom kama kampuni ya mawasiliano siku zote itakuwa mstari wa mbele kuwaelimisha wananchi juu ya matumizi  bora na sahihi ya mtandao wa interneti.
“Tukiwa kampuni inayoongoza kutoa huduma za mawasiliano nchini siku zote tutashirikiana na serikali na wadau wengine wa masuala ya mawasiliano  kuhimiza matumizi bora na sahihi ya mtandao wa internet.Matumizi ya intaneti yamekuwa siyo anasa tena kama ilivyokuwa ikichukuliwa na wengi hapo awali ambapo watu hujiunga kwa ajili ya kuwasiliana na watu walio nje ya nchi au kwa burudani nyinginezo. Hivi sasa  utumiaji wa intaneti umekuwa kutoka watu kuwasiliaina mpaka kwa matumizi ya biashara ambapo watu wa mataifa mbali mbali hukutana mtandaoni kuuza ama kununua bidhaa na huduma,”.Alisema.
Mbali na biashara alisema kuwa interneti imejaa maarifa ya kielimu ya taaluma mbalimbali ambazo zinafanya dunia kuwa kijiji kimoja hivyo matumizi mazuri ya interneti yanaweza kumfanya mtu popote alipo kupata taarifa na maarifa ya fani  anayohitaji au taarifa anazotaka kujua kwa haraka na kwenda na wakati na kuna vyuo vingi duniani vinatoa elimu kwa njia ya mtandao. “Inashangaza kuona baadhi ya watu hususani katika nchi zetu zinazoendelea wanatumia muda wao mwingi kuangalia taarifa zisizo na manufaa kwenye mitandao ya interneti”.Alisema.
Aliwaasa vijana wanaojiita wa kizazi cha Dot.Com hususani wanafunzi ambao wako mashuleni na vyuoni kuachana na kutumia muda wao kutafuta taarifa za kuwapotosha na zisizoendana na utamaduni wa kitanzania badala yake watumie teknolojia hii kupata maarifa na taarifa zenye manufaa kwao na kwa maisha yao ya baadaye.
Alimalizia kwa kuwahimiza watanzania  kuwa makini na neno la siri ”Password” na kuendelea kutumia mtandao wa Vodacom ambao hivi sasa unatoa huduma ya interneti yenye kasi kubwa na viwango vya gharama nafuu lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha idadi ya watumiaji wa interneti nchini inaongezeka ili kwenda na nchi zilizopo katika ukanda wa Afrika Mashariki.
“Katika kuhakikisha lengo hii linatimia hivi karibuni tuliingiza kwenye soko simu za smartphone za gharama nafuu ambazo zimewalenga watu wenye vipato vya chini hususani wanaoishi maeneo ya vijijini na tuna imani watazipenda na kuzifurahia kwa kuwa mbali na kuwapatia interneti kwa gharama  nafuu wakizinunua wanakuwa wameunganishwa na mitandao maarufu duniani kama vile Facebook, Whatsap, Twitter, Viber, Instagram na mingineyo”.Alisema.

JK afungua jengo la NSSF la kitega uchumi Moshi

0
0
  NSSF Kilimanjaro Commercial Complex mjini Moshi,Mkoani Kilimanjaro 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Kazi na ajira Mh.Gaudensia Kabaka(watano kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhani Dau(wapili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama(wapili kushoto) pamoja na viongozi na wadau wengine wakikata utepe kufungua rasmi jengo la kitega uchumi la NSSF Kilimanjaro Commercial Complex mjini Moshi,Mkoani Kilimanjaro leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhan Dau pamoja na wadau wengine wakitazama ramani ya jengo jipya la kitega uchumi la NSSF mjini Moshi Kilimanjaro Commercial Complex wakati wa hafla ya ufunguzi leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na chipikizi wa Tanzania Girl Guides wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la NSSF mjini Moshi leo.Tanzania Girl Guides,UMATI,Tanzania Red Cross ni wadau wa NSSF katika mradi huo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhani Dau baada ya hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la kitega uchumi la NSSF mjini Moshi leo.Katikati ni Waziri wa Kazi na Ajira Mh.Gaudensia Kabaka(picha na Freddy Maro)

CHRISTIAN BELLA 'KING OF THE BEST MELODIES' AAHIDI MAKUBWA SHOO YA VALENTINE'S DAY, DAR LIVE

0
0

Bella akiwa na Mhariri wa Gazeti la Risasi Jumamosi, Erick Evarist.
X-Bass Babu Bomba na Bella katika pozi na Mpiga Picha wa GPL, Musa Mateja.
X-Bass Babu Bomba na Bella wakiwa katika picha ya pamoja na Mhariri Mwandamizi wa GPL, Walusanga Ndaki.
X-Bass Babu Bomba na Bella wakipozi na Shafii Mohamed wa GPL.
X-Bass Babu Bomba na Christian Bella katika pozi ndani ya GPL.

PREZIDAA wa Bendi ya Malaika Music, Christian Bella 'King of the Best Melodies' amewaahidi shoo kali mashabiki wake watakaohudhuria katika Ukumbi wa Kisasa wa Dar Live, Jumamosi ijayo ambayo ni Siku ya Wapendanao 'Valentine's Day'.
Staa huyo ameyasema hayo hivi punde wakati wa mkutano na wanahabari wa vyombo mbalimbali uliofanyika katika ofisi za Global Publishers.
Bella amesema atakuwepo ndani ya kiwanja hicho mapema kuanzia saa 7 mchana na atapiga picha za red carpet na mashabiki wake watakaohudhuria sambamba na kuzungumza nao mawili-matatu.
Mbali na kuwahi ukumbini, Bella amewaandalia nyimbo zake zote kali za mapenzi kama vile Msaliti, Safari Siyo Kifo, Nakuhitaji pamoja na wimbo bora uliofunga mwaka wa Nani Kama Mama.
Kuonyesha kuwa utakuwa Usiku wa Wapendanao, Bella amewaandalia mashabiki wake zawadi ya wimbo mpya uitwao NASHINDWA ambao atauchia kwa mara ya kwanza huku video akienda kuifanyia nchini Afrika Kusini wiki ijayo.
Mbali na Bella usiku huo ambao ni maalum kwa wapendanao, mkali wa muziki wa Mwambao, Mfalme Mzee Yusuf naye atakuwepo katika kuwaburudisha mashabiki wote watakaokuwepo ukumbini hapo.
Usiku huo Mzee Yusuf atashuka na kundi lake la Jahazi Modern Taarab na kuangusha ngoma zake zote kali za mapenzi kama vile My Valentine, Wapendanao, Tiba ya Mapenzi,  Wasiwasi Wako pamoja na hii ambayo ni habari ya mjini kwa sasa ya Mahaba Niue.

hepi besdei ya kuzaliwa shadya shaibu chapuchapu leo

0
0
 Shadya Shaibu, akilishwa kipade cha keki na Baba yake mzazi Shaibu Chapuchapu, katika hafla yake ya kuzaliwa iliyofanyika nyumbani kwa wazazi wake Kigamboni Dar es Salaam usiku huu. 
(PICHA NA KHAMISI MUSSA)
  Shadya Chapuchapu (kulia) akimlisha baba yake mzazi Shadya Shaibu keki
 Shadya Chapuchapu (kulia) akimlisha mama yake mzazi Marim Tindwa ,keki katika Hafla ya kuzaliwa iliyofanyika Kigamboni Dar es Salaam
 Mama mzazi wa Shadya Chapuchapu  Marim Tindwa (kushoto), akimlisha keki mwanaye katika Hafla iliyofanyika nyumbani kwao Kigamboni Dar es Salaam leo
Kaka wa Shadya,  Sheni Shaibu , akila keki katika hafla fupi ya siku ya kuzaliwa dada yake
Shadya chapuchapu (wapili kushoto) walio chuchuma katika Picha ya pamoja akiwa ameshika keki na kaka yake Shamte chapuchapu, wakishika keki kwa pamoja katika hafla ya kupongezwa kwake katika hafla ya kuzaliwa iliyofanyika usiku huu Kigamboni Dar es Salaam.

Cuban Ambassador visits SUZA

0
0
An official visit of Cuban Ambassador to Tanzania His Excellency Mr. Jorge Luis Lopez Tormo (with white shirt in the centre) at the State University of Zanzibar (SUZA) on Wednesday 11th February, 2015. On the Ambassador’s left is his host, Prof. Idris A. Rai, the SUZA Vice Chancellor. During this official visit, Prof. Rai and his guest discussed on various issues including how Cuban government through her higher learning institutions collaborate with SUZA in education related matters. The Cuban government through the Zanzibar Ministry of Health currently provides academicians teaching at the School of Health and Medical Sciences of the State University of Zanzibar.

WASHINDI AIRTEL YATOSHA ZAIDI WAKABIDHIWA MAGARI

0
0
Mkurugenzi wa masoko wa Airtel bw. Levi Nyakundi (kushoto) akimkabidhi mmoja kati ya washindi wa promosheni ya Yatosha Zaidi bi. Mwajabu Omary leo katika makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel Tanzania. Anayeshuhudia (katikati) Mkurugenzi wa kitengo cha Mawasiliano bi Beatrice Singano Mallya .Airtel imekabidhi magari matatu katika hafla hiyo.
KAMPUNI Ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo asubuhi imekabidhi magari kwa washindi watatu wa kwanza wa promoseni ya Yatosha Zaidi.

Hafla hiyo fupi ya kuvutia ilifanyika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na waandishi wa habari, wafanyakazi wa Airtel na wageni waalikwa kadhaa.

Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Levi Nyakundi aliwaomba washindi kuendelea kutumia mtandao wa Airtel kwani kwa sasa wao ni sehemu ya familia ya kampuni hiyo.

Washindi hao ni mkazi wa mkoani Pwani, Ramadhan Dilunga (53) ambaye ni mkulima, mwalimu mstaafu na anayeishi Mtwara, Namtapika Kilumba (60) na mfanyabiashara mkazi wa Dar es Salaam, Mwajabu Churian (27).

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi Mawasiliano Bi Beatrice Singa Mallya  alisema: “Tukio hili la leo linaweza kuchukuliwa kama mwanzo wa mipango mingi iliyopo kwenye kampuni yetu. Kuna mambo mengi yanakuja na madhumuni yetu makubwa ni kushiriki katika kubadilisha na kuboresha maisha ya Watanzania kadhaa wenye bahati.

Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images