Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 734 | 735 | (Page 736) | 737 | 738 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Meneja Mauzo wa Hyundai, Bw. Alen Nkya (kushoto) akijadiliana na Meneja Mradi wa Dangote Industries, Mhandisi Markus Abayo (kulia) kuhusu mitambo ya ujenzi ya kisasa katika Mkutano wa Kimataifa wa Teknolojia uliofanyika Nairobi. Anayeshuhudia (katikati) ni Afisa Mikopo wa Hyundai, Bw. Manase Mpayo. Dangote Industries wanatumia mitambo ya Hyundai Excavator, Wheel Loader na Forklift katika miradi ya cement, n.k.

  0 0

  Wataalam wa Sekta ya Umeme kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Shirika la Umeme nchini (Tanesco), wakiongozwa na Kamishna Msaidizi wa Umeme Mhandisi Innocent Luoga (wa kwanza kushoto), wakiwa katika mazungumzo na wawakilishi wa Kampuni ya Sunshine Group Ltd (Kulia). Mazungumzo yalifanyika hivi karibuni Makao Makuu ya Wizara, jijini Dar es Salaam na yalihusu uanzishwaji wa Kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme za zege kwa ajili ya kusambaza umeme nchini.
  Ujumbe kutoka Kampuni ya Sunshine Group Ltd, ukiwa katika mazungumzo na wataalam wa Sekta ya Umeme kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Shirika la Umeme nchini – Tanesco (hawapo pichani). Kampuni hiyo iliwasilisha mapendekezo (proposal) ya kuanzisha Kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme za zege kwa ajili ya matumizi ya hapa nchini.
  Mtaalam wa Sekta ya Umeme kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Leonard Masanja (wa kwanza Kulia) akichangia hoja katika kikao baina ya Wataalam wa Wizara na wawakilishi wa Kampuni ya Sunshine Group Ltd, Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Majadiliano yalihusu uwezekano wa Kampuni hiyo kuanzisha Kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme za zege kwa matumizi ya kusambaza umeme nchini. Wa kwanza Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga.
  Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga (Kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sunshine Group Ltd, Bw. Sun Tao aliyekuwa akitoa ufafanuzi wa jambo fulani, mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina ya Wataalam wa Wizara na wawakilishi wa Kampuni hiyo kuhusu uwezekano wa kuanzisha Kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme za zege kwa ajili ya kusambaza umeme nchini.


  0 0


  0 0

  By Joett
  In a text message after the February 7, 2015 competition, I wrote... "Mayunga, I have waited YEARS to meet someone like you. It has been an honor to work with you. I feel truly blessed. With YOU I know Tanzania has found a TRUE star who will carry the Tanzanian flag to the WORLD. You are the next Michael Jackson, and what REALLY delights me is that you are TANZANIAN. The doors to my studio are open to you for ALWAYS. Now let's go out there and show the world what we Tanzanians are made of. I'm truly proud of you!"


  In all honesty, Mayunga thrilled the crowd with his soaring vocals with the BBMak hit single More Than Words from 1999, a cover of the original version by Extreme (1990). I selected this song for him, and trained him to deliver. He did me proud. I'm SO very excited.

  I'm a huge fan of the late Luther Vandross, and I think Henry who emerged runner up, is quite frankly Luther Vandross reincarnated. His delivery of the hit Vandross classicAlways And Forever -- which I selected for him -- a cover of the original version byHeatwave, left everybody spellbound. I'm VERY proud of Henry. You're going to be seeing a lot of this guy. Just watch this space.


  0 0

  Performance ya Julio Batalia kwenye Show iliyofanyika escape 1 tarehe 7 february j'mosi kwenye Utambulisho wa Video mbili Kaunyaka ya Chege na Temba na Vuvula ya Madee ali.video zilizotengenezwa na director Adam Juma...Julio aliperfom ngoma zake mbili "Haina Noma" na "Special for you" na pia kuwapa kionjo cha ngoma yake mpya inayoitwa (Tetemesha) ambayo imefanyika wakati wa safari ya South Africa akiwa na Chege,Madee na Temba na kufanikisha kurekodi na producer mkubwa Dj maphorisa wa UHURU UHURU..Ngoma mpya ya Julio (Tetemesha) inategemewa kutoka March ama April mwanzoni ikiambatana na video.

  0 0

   Zainab Rajab Mwinyijuma akiwa anasubiria kuitwa kupokea nondozzz yake ya   "BACHELOR OF SCIENCE IN NURSING" katika  Chuo Kikuu cha The University Of Northampon Uingerezea akiwa na wahatimu wenziwe wikiendi hii
    Zainab Rajab Mwinyijuma akiwa na mai hazbendi wake Mbegu Diego na familia yao baada ya kulamba nondozzzz yake
   Zainab Rajab Mwinyijuma akiwa na mama yake mzazi baada ya kulamba nondozzzz yake

  0 0

   MWAKILISHI WA JIMBO LA MAKUNDUCHI MH. HAROUN ALI SULEIMAN AKIFUNGUA TAMASHA HILO HUKO KOBA MAKUNDUCHI.
   MSHINDI WA KWANZA MBIO ZA BAISKELI  ABDALLAH ABOUBAKAR


   MHE. HAROUN AKIZINDUA RESI ZA NGALAWA KIGAENI MAKUNDUCHI
   MASHINDANO YA KUOGELEA KIGAENI MITA 100. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  0 0

   Kutoka kushoto Enock, Maromboso, Beka na Aslay wakiwa wameshikilia ticket zao za ndege  ambazo walikabidhiwa rasmi na mkurugenzi wa Zurii house of Beauty Jestina George Meru.
  Yamoto Band wanatarijiwa kufanya Live show kwenye jiji London siku ya tarehe 21.02.2015 katika ukumbi wa Royal Regency Banguet Hall 
   Zuri House of Beauty CEO Jestina George Meru akiwa kwenye picha ya pamoja na timu nzima ya Yamoto Band 
  Kama kawaida Ukitembelea Zurii House of Beauty huondoki mkono mtupu
  UK na Europe yote Siku ya Jumamosi tarehe 21 Feb 2015 tukutane pale kwenye ukumbi wa Royal Regency Manor Park London Kwani Hiyo ndio sehemu pekee kwenye jiji la London utapopata Burudani ya kukata na shoka kutoka kwa No1 band ya Tanzania Hakuna wengine ni wale wale vijana wetu wanne machachari wanaoitikisha East Africa sasa hivi YAMOTO BAND aka MKUBWA na WANAWE. Tickets are on sale now Standard ticket £25, VIP £35 kama unahitaji Meza ya watu 10 basi wasiliana nasi  kwenye number hizi  07853482158 @bongodeejays or whatsapp +447557304940 

  Also if you are in
  Northampton,you can get your tickets 

  Kass's Grill 01604621567/07527283219 
  And for people in Milton Keynes you can Get your tickets by 

  Calling  Cobby ...07448416240 London Chris Chagula 07405889880 /Hakim 07931 526622

  VjOj on 07940 679201and Exposed Uganda on  07931 119346 


  0 0

  Bw. Elia Yobu wa Dar es Salaam anasikitika kutangaza kifo cha Mama yake Mzazi EDINECK ELIAMEN YOBU (pichani) kilichotokea leo tarehe 9.2.2014 hapa Dar es Salaam. 

  Mipango ya Mazishi inafanywa nyumbani kwa mtoto wa Marehemu Tegeta Mivumoni Dar es Salaam. 

  Habari ziwafikie Marko Ruwaichi Lyimo na nduguze wa Kilombero Morogoro, Vera na Jessie Mpanda wa Mwanza , Filex na Ajuae Lyimo wa Marangu Moshi na Eliwangu Jamhuri wa Arusha. Ukoo wa Yobu Lyimo, Shoo wa Machame, Mbuya, Mtui, Makundi ndg jamaa na Marafiki

  0 0

  Ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa mabadiliko ya Tabia nchi mjini Geneva pamoja na Balozi wa Tanzania anaetuwakilisha nchini Uswiss na Vienna. Mh Modest Mero (kati mbele). Wengine mbele kushoto mkurugenzi msaidizi ofisi ya makamu wa raisi mazingira bw. Richard Muyungi,kulia Afisa mazingira mandamizi kutoka ofis ya Makamu wa Rais Bw. Fred manyika,nyuma kulia ni injia Ladslaus Kyaruzi kutoka ofisi ya Makamu wa Rais,kushoto ni Bi Emelda Teikwa afisa mazingira kutoka ofisi ya Makamu wa Rais. Picha na Everlyn Mkokoi


  0 0


  0 0

   George Lwakatare, with  H.E Dr Jakaya Kikwete, at the Annual African President's meeting held in Addis Ababa last week. Mr Lwakatare attended the prestigious & Africa's most powerful meeting,  as a special guest of the African Union Commission
  George Lwakatare, with H.E Jacob Zuma  in Addis Ababa last week. Mr Lwakatare is the Vice Chairperson of Business Link Africa PLC  (BLA), head quartered in Nairobi and also is the Managing Director of Hygiene & Pests Management Ltd based in Dar es salaam.

  Mr Lwakatare advocated for De-fragmenting Africa by deepening Regional Trade Integration, emphasizing  on removing trade barriers and inefficiencies in transport & logistics within the continent.Often citing, while a Tanzanian does not need a Visa to get into Hong Kong, one must  get an Ethiopian entry Visa  through its Kenyan Embassy. Also, insists Mr Lwakatare, air travel  costs more to travel within the continent than to go to Middle East!

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati  wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Sheria sherehe zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja (kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande (kushoto) na Waziri wa katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary. 
  sh7Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu alipokuwa akisema machache na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ali azungumze na Wananchi, Mahakimu na Wanasheria katika sherehe za Kilele cha Siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.sh2Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mohamed Othman Chande (mbele) wakiongoza maandamano wakati wa kilele cha siku ya Sheria Zanzibar sherehe zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Zanzibar.sh3Mahakimu na Wanasheria wakiwa katika maandamano wakati wa kilele cha siku ya Sheria Zanzibar sherehe zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Zanzibar ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
  PICHA ZAIDI INGIA HAPA

  0 0

  Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akiongea na waandishi wa habari ( pichani hawapo) wakati wa kuzindua promosheni ya Airtel yatosha Zaidi jijini Mwanza, Promosheni ya Airtel yatosha inawawezesha wateja wa Airtel kujishindia gari Aina ya Toyota IST moja kila siku. kushoto Afisa Masoko wa Airtel Rebecca Mauma na Kulia ni Afisa Mauzo kanda ya Ziwa Emmanuel Raphael.
  Afisa Masoko wa Airtel Rebecca Mauma (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kuzindua promosheni ya Airtel yatosha Zaidi jijini Mwanza, Promosheni ya Airtel yatosha inawawezesha wateja wa Airtel kujishindia gari Aina ya Toyota IST moja kila siku. katikati ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akifatiwa na Afisa Mauzo kanda ya Ziwa Emmanuel Raphael.
  Wanahabari wa kutoka vyombo vya habari Mwanza wajadili kuhusu promosheni ya Airtel yatosha Zaidi wakati wa kuzindua promosheni ya Airtel yatosha Zaidi jijini Mwanza, Promosheni ya Airtel yatosha inawawezesha wateja wa Airtel kujishindia gari Aina ya Toyota IST moja kila siku.


  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwaongoza viongozi wa Kanisa la Anglican kutembelea shamba lake la zabibu lililopo Zuzu Dodoma Februari 9, 2015. Baadhi ya viongozi hao ambao walikwenda kujifunza kwa lengo la kuanzisha shamba linalofanana na hilo Dodoma ni Askofu Dickson Chilongani wa Dayosisi ya Dodoma (kushoto), Askofu Maimbo Mndolwa wa Dayosisi ya Tanga (wapili kushoto) na kulia ni Re. Canon, Johnson Chinyongole ambaye ni Katibu Mkuu wa Kanisa hilo.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwaongoza viongozi wa Kanisa la Anglican kutembelea shamba lake la zabibu lililopo Zuzu Dodoma Februari 9, 2015. 
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwaongoza viongozi wa Kanisa la Anglican kutembelea malisho ya ng'ombe kwenye shamba lake lililopo Zuzu Dodoma Februari 9, 2015. Baadhi ya viongozi hao ambao walikwenda kujifunza kwa lengo la kuanzisha shamba linalofanana na hilo Dodoma ni Askofu Dickson Chilongani wa Dayosisi ya Dodoma (wapili kushoto), Askofu Maimbo Mndolwa wa Dayosisi ya Tanga (kulia kwake) na kulia ni Re. Canon, Johnson Chinyongole ambaye ni Katibu Mkuu wa Kanisa hilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Idhaa ya Kiswahili ya BBC inataka kuwatahadharisha wasikilizaji na watumiaji wa mtandao wake wa bbcswahili.com dhidi ya wahalifu wanaotumia jina la BBC kuwahadaa na kutaka kuwatapeli watu.

  Kumezuka mtandao bandia unaotumia jina la BBC SWAHILI NEWS kuandika habari za uzushi na kulaghai wananchi kwa habari zisizokuwa na ukweli wala uhusiano na shirika hili la habari.

  BBC inapenda kuwakumbusha wasikilizaji na wasomaji wake wote wanaofuatilia habari zake kuwa makini. BBC inaufahamisha umma wa wazungumzaji wa Kiswahili kuwa haina blog ya aina hiyo na kwamba habari zote rasmi zinapatikana kupitia bbcswahili.com au bbc.co.uk/swahili na kupitia Facebook katika facebook.com/bbswahili– kinyume na hapo jihadhari sana.

  Matapeli hawa wanaandika habari za uongo kuhusu watu maarufu, lakini lengo lao ni kutaka kulaghai watu watoe fedha au watoe maelezo yao binafsi ambayo yatatumiwa kwa uhalifu.

  Tayari mamlaka husika zimepewa taarifa za vitendo hivyo, BBC haitahusika kwa hasara au athari itakayotokana na mtu kutapeliwa kwa njia iliyoelezwa au nyingineyo kinyume na kazi zinazofanywa na BBC.

  Yoyote atakayehisi mwenendo wa aina hii atoe taarifa kupitia swahili@bbc.co.uk  au piga simu 0222 701752.

  BBC Tanzania

  0 0

  Waziri wa Ushirikiano Afrika Mashariki, Dkt. Harrison Mwakyembe (kati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya swala la serikali ya Kenya kuzuia magari ya kitalii ya yaliyosajiliwa nchini Tanzania kuingia kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta nchini Kenya.Kulia ni Naibu Waziri wa Ushirikiano Afrika Mashariki,Dkt Abdallah Juma Saadala na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Joyce Mapunjo. 

  0 0


  Baadhi ya vijana wanaofanya utapeli kwa kutumia vipande vya sabuni wakikimbia baada ya kunaswa na kamera ya bloger wetu wakiwa katika jitihada za kumwibia mmoja wapita njia katika mtaa wa Uhuru Dar es Salaam leo asubuhi. 

  Kwa Mujibu wa shuhuda vijana hao huwa kundi na baadhi huangalia mwenzao akitekeleza uhalifu wakati wao wakihakikisha wanampa ishara ya kufuatiliwa na kutoa ishara waonapo mazingira ya mchakato kushindikana ama hali kuwa tete kwa mwenzao iwapo mnunuzi wa simu atakuwa ameshtukia njama zao mbovu za kutaka kutenda uhalifu. 

  Mmoja wa wakazi wa Dar es Salaam alikumbwa na mkasa wa kuibiwa shilingi laki moja alivutiwa na mhalifu mmoja kwa kumwonesha simu yenye gharama ya sh 200,000 huku akimsihi anunue kwa sh 100,000. 

  Alipokubali kununua simu hiyo, walimbadilishia wakati akitoa hela na alipoikabidhi na kwenda hatua chache aligundua kuwa amepewa kipande cha sabuni kwenye bahasha wakati mhalifu huyo na wenzake wameshatokea kusikojulikana. 

  Jambo la kusikitisha ni kwamba askari polisi wameshapokea malamiko ya mikasa kama hiyo lakini hakuna jitihada za makusudi zilizochukuliwa kuwanasa na kuwatia hatiani wahalifu hao.Tahadhari inatolewa kwa wananchi kutonunua bidha kama hizo mkononi kwa watu hasa katika mazingira ya ushawishi mkubwa na kufanya manunuzi kwenye maduka yenye kutoa risiti kwa bidhaa walizonunua.
  HABARI ZAIDI INGIA HAPA

  0 0

    Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiongea na viongozi wa CCM wa Tawi la Ufukoni katika Kata ya Rahaleo huko Lindi Mjini tarehe 9.2.2015.  Mama Salma Kikwete yupo wilayani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku 5 
   Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Lindi Mjini Dkt. Zulfa Msami wakati Mama alipotembelea kituo hicho tarehe 10.2.2015.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimwangalia mtoto mwenye umri wa siku 2 aliyeshikwa na Mama yake Sharifa Ali,19, wakiati Mama Salma alipotembelea kituo cha Afya cha Lindi Mjini tarehe 10.2.2015. 
  Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiwa amempakata mtoto Adaita Hamis mwenye umri wa siku 1 aliyezaliwa katika Kituo cha Afya cha Lindi Mjini tarehe 9.2.2015 huku akiongea na mama wa mtoto huyo Bibi Zanida Ismail,42, anayeishi Mtaa wa Benki huko Lindi Mjini wakati Mama Salma alitembelea kituoni hapo tarehe 10.2.2015. PICHA NA JOHN  LUKUWI.   

older | 1 | .... | 734 | 735 | (Page 736) | 737 | 738 | .... | 3272 | newer