Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

ajali ya moto yasababisha maafa ukonga Kipunguni usiku wa kuamkia leo jijini Dar es salaam

0
0
Majirani wakiondoa vitu kwenye nyumba iliyoungua moto usiku wa kuamkia leo na kusababisha watu sita kupoteza maisha huko Ukonga Kipunguni jijini Dar es salaam. Chini ni baadhi ya ndugu, jamaa na majirani wakiwa katika simanzi. Habari zaidi zitakuja baada ya kuthibitishwa na mamlaka husika.

MAHAKAMA: MACHA MNUNUZI HALALI NYUMBA YA BALENGA

0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imethibitisha kwamba mfanyabiashara Hans Macha alinunua nyumba kwa kufuata utaratibu na kihalali kutoka kwa Ramadhani Balenga.

Hayo yalithibitishwa leo kupitia hukumu iliyosomwa na Hakimu Mkazi Frank Moshi kwa niaba ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka, ambaye alisikiliza kesi ya kughushi inayomkabili Macha.

Katika kesi hiyo, Macha alikuwa akikabiliwa na mashitaka matatu ya kughushi hati ya umiliki wa kiwanja kilichopo eneo ya Kigogo, Dar es Salaam, kinachodaiwa kuwa mmiliki wake ni Ramadhani Balenga.

Pia alikuwa anadaiwa  kughushi mkataba wa mauziano wa eneo hilo kuonyesha kwamba Balenga alihamisha umiliki wa kiwanja hicho kwenda kwake na kuwasilisha nyaraka ya kughushi.

"Mahakama imepata muda wa kutosha wa kupitia ushahidi na vielelezo vyote. Makosa yote matatu hayajathibitishwa ipasavyo. Mlalamikaji  (Balenga), alimuuzia mshitakiwa eneo hilo kwa kufuata utaratibu na kihalali," alisema Hakimu huyo.

Alisema mahakama inamuachia mshitakiwa kwa mashitaka yote matatu na mlalamikaji ana nafasi ya kukata rufani.

Baada ya kusomwa kwa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali Nassoro Katunga, aliuliza iwapo nakala ya hukumu ipo tayari, ambapo Hakimu Moshi alimwambia haipo tayari na kama wanaitaka wafuate taratibu kwa kuwasilisha maombi mahakamani hapo.

Airtel yaitambulisha promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi kwa wakazi wa Arusha

0
0
Meneja Mauzo Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kanda ya kaskazini Bwana Brighton Majwala akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuitambulisha promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Mkoani Arusha , wakishuhudia (katika) Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akifatiwa na Afisa Masoko wa Airtel Bi Rebecca Mauma.
Meneja Mauzo kanda ya kaskazini Bwana Brighton Majwala (kulia) ,Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (katika) na Afisa Masoko wa Airtel Bi Rebecca Mauma kwa pamoja wakionyesha vipeperushi vya promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi wakati wa kuitambulisha promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Mkoani Arusha.

Wiki Ya Ulinzi Na Usalama Wa Mtoto

HOTUBA YA MHE. WAZIRI MKUU PINDA YA KUAHIRISHA MKUTANO WA 18 WA BUNGE

0
0
HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P.  PINDA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUHITIMISHA SHUGHULI ZA MKUTANO

WA 18 WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TAREHE 7 FEBRUARI, 2015


I:          UTANGULIZI 


(a)      Masuala ya jumla


Mheshimiwa Spika,

1.            Tumekuwepo hapa kwa takriban siku 12 katika shughuli za Mkutano wa 18 wa Bunge lako Tukufu. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutufikisha salama siku ya leo.


2.            Lakini tumekutana hapa tukiwa tumeshuhudia mabadiliko katika Baraza la Mawaziri na Wenyeviti wa baadhi ya Kamati za Kudumu za Bunge. Niruhusu nitumie nafasi hii ya awali kuwapongeza Mawaziri na Naibu Mawaziri wote ambao wameteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali katika mabadiliko hayo. Aidha, napenda niwapongeze Wenyeviti watatu pamoja na Makamu mmoja kwa kuchaguliwa kuongoza Kamati za Kudumu za Bunge ikiwemo Kamati ya Bajeti, Kamati ya Nishati na Madini na Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala. Tunawatakia afya njema Mawaziri, Naibu Mawaziri na Wenyeviti wote katika kutekeleza majukumu yao mapya.


Mheshimiwa Spika,

3.            Tangu tulipomaliza Mkutano wa 16 na 17 wa Bunge lako Tukufu, kumetokea majanga katika sehemu mbalimbali Nchini ikiwemo mafuriko na mapigano ya Wakulima na Wafugaji kule Morogoro, pamoja na ajali za barabarani. Naomba nitumie nafasi hii kuwapa pole wote walioathirika na majanga, maafa na ajali za barabarani.  Kwa wale waliopoteza maisha tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi Amina.


b)      Maswali


Mheshimiwa Spika,

4.            Katika Mkutano huu, Waheshimiwa Wabunge wamepata fursa ya kuuliza maswali ya kawaida na yale ya papo papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Jumla ya maswali 122 ya msingi na 313 ya nyongeza yaliulizwa na Waheshimiwa Wabunge na kujibiwa na Serikali.  Aidha, Maswali 15 ya msingi na 13 ya nyongeza yaliulizwa na kujibiwa kwa utaratibu wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.


(c)     Miswada na Taarifa Mbalimbali


Mheshimiwa Spika,

5.             Tunahitimisha Mkutano huu tukiwa tumekamilisha kazi kubwa ya kusoma na kujadili taarifa mbalimbli za Kamati za Bunge za Kisekta na zisizo za Kisekta. Kamati za Kisekta ambazo Taarifa zake zimewasilishwa na kujadiliwa na Waheshimiwa Wabunge ni zifuatazo:

i)             Kamati ya Miundombinu;

ii)            Kamati ya Nishati na Madini;

iii)           Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira;

iv)           Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji;

v)            Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala;

vi)           Kamati ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa;

vii)         Kamati ya Masuala ya UKIMWI;

viii)        Kamati ya Ulinzi na Usalama;

ix)           Kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa;

x)            Kamati ya Huduma na Jamii; na

xi)           Kamati ya Maendeleo ya Jamii.


6.            Aidha, Bunge Lako Tukufu lilipokea na kujadili Taarifa za Kamati zisizo za Kisekta zinazosimamia Fedha za Umma zifuatazo:

i)             Kamati ya Hesabu za Serikali;

ii)            Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa; na

iii)           Kamati za Bajeti.


Mbunge wa Kabete Nairobi, Mh. George Muchai auawa kwa kupigwa risasi

0
0

Kwa mujibu wa televisheni ya ntv ya Kenya.

Mheshimiwa ameuawa pamoja na dereva wake pamoja na walinzi wake wawili majira ya saa nane na nusu usiku wa kuamkia leo katkka barabara ya Kenyatta avenue wakati akiwa njiani kutoka katika sherehe.

Alisimama na ili kununua magazeti,na ndipo mtu aliyevalia mask alipojitokeza kutoka gari ndogo aina ya toyota pro-box na kuanza kuwafyatulia risasi vichwani kila mmoja,akitumia bunduki aina ya AK 47.

Pia alipora briefcase ya marehemu pamoja na bastola mbili za walinzi wake na kutokomea kusikojulikana akitumia gari hilo lililokuwa limefichwa namba zake.
Marehemu pia alikuwa ameambatana na mke na watoto wake wawili wa kike waliokuwa ndani ya gari la nyuma na walishuhudia mauaji hayo yakifanyika.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa Kenyatta hospital Nairobi.

R.I.P marehemu wote.


MAKALA YA SHERIA: NJIA YA KISHERIA YA KUKUEPUSHA KUNUNUA ARDHI YENYE MGOGORO.

0
0
Na Bashir Yakub
Makala zilizopita  nilieleza   mambo au taarifa muhimu  zinazopaswa kuwa kwenye  mkataba wako  unapokuwa unanunua  nyumba/kiwanja. 
Nikasema  katika niliyosema  kuwa mkataba  lazima uoneshe  ukitokea mgogoro  utatatuliwa vipi,  ueleze kuwa  utapotokea mgogoro  muuzaji  lazima  awajibike kuhakikisha anakupa ushirikiano  mnunuzi  ili kumaliza  mgogoro huo na kuwa muuzaji  kama ana  mke  basi  mke wake ni lazima  aandaiiwe  nyaraka iitwayo  ridhaa ya mwanandoa ambayo  ni  tofauti  na mkataba  na  aisaini  pamoja na kuweka picha yake.  
Nilieleza  mengi  lakini hayo ni baadhi tu. Kwa wale ambao  hawakubahatika kuyasoma hayo basi  waandike neno "MAKALA  SHERIA"  kwenye google watapata makala  hizo. 
Leo  tena naeleza hatua  muhimu sana au ya lazima  na lazima haswaa  kwa mnunuzi wa kiwanja/nyumba  ambayo anatakiwa  apitie  kabla ya kufanya manunuzi.
Hatua hii kwa  jina la  kitaalam huitwa OFFICIAL  SEARCH  kwa lugha rahisi tu waweza kuiita  utafiti,upekuzi,  upembuzi au upelelezi rasmi  ambayo hufanywa na wanasheria. Mi napenda niite upelelezi. 

Article 7

0
0
Na Lorietha Laurence-Maelezo,Dodoma 
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ametoa rai kwa wakulima na wafugaji nchini kujikubali kuwa wote ni Watanzania na wanahaki ya kuishi popote bila kuvunja sheria. 
 Amesema hayo Bungeni Dodoma alipokuwa akipokea na kukubali taarifa na mapendekezo iliyotolewa na kamati teule ya Bunge ya kuchunguza na kuchambua sera mbalimbali zinazohusu masuala ya Ardhi,kilimo,mifugo,maji na uwekezaji. 
“Nimepokea mapendekezo yote yaliyotolewa na kamati na ninaahidi yatafanyiwa kazi kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania” alisema Pinda 
Aliongeza kuwa kwa utekelezaji wa awali serikali itauunda tume maalum ya wataalum mchanganyiko na tume ya makatibu wakuu ili kuweza kupitia taarifa hizo na baadaye kuwasilisha kwa ajili ya utekelezaji. 
 Aidha alisema ni wajibu wa Wizara ya Ardhi kupima ardhi katika maeneo mbalimbali na kwa wale wanaokiuka taratibu wachukuliwe hatua madhubuti ya kuwawajibisha. 
Hata hivyo Waziri Mkuu Pinda alisema kuwa kuna umuhimu wa kutolewa kwa elimu ya kuwahamasisha wananchi umuhimu wa kulinda na kuitunza amani ya nchi yetu katika kuleta mabadiliko na kuondokana na mgawanyiko. 
Vile vile alizitaka Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kuwachunguza watendaji wake wanaokiuka sheria na taratibu za utendaji na baadaye kuweza kuwawajibisha. 
 Naye Mwenyekiti wa kamati hiyo teule Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka alisema kuna haja ya kuwatengea maeneo yaliyopimwa wafugaji na wakulima ili kuepusha vurugu kwa jamii hizo mbili. 
“Naiomba serikali iweze kushughulikia suali hili la wafugaji na wakulima ili kuepukana na migogoro inayojitokeza mara kwa mara katika maeneo hayo” alisema Ole Sendeka.
Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda akivunja Bunge mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge, Mhe Christopher Ole Sendeka, akijibu hoja za wabunge kuhitimisha mjadala.Kamati hiyo iliundwa kuchunguza na kuchambua Sera mbalimbali zinazohusu masuala ya Aridhi, Kilimo, Mifugo,Maji na Uwekezaji ili kubaini kasoro zilizomo katika matumizi ya Ardhi.
Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Mhe Sabrina Sungura aichangia hoja.

Mbunge waGando Mhe Khalifa Suleiman akichangia taarifa.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Mwijage, akisalimiana na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda(kulia) baada ya Bunge kuvunjwa.Katikati ni Mbunge waViti maalum (CCM) mkoa wa Singida Diana Mkumbo Chilolo.

MAISHA SUPERSTAR PREMIERES ON MAISHA MAGIC ON MONDAY!

nape atembelea magazeti ya Tanzania Daima na Jambo leo

0
0

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnuye akikutana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alipofika katika Ofisi za Free Media, wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima,  akiwa katika ziara katika vyombo vya habari ambayo aliianza jana, jijini Dar es Salaam.


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnuye akiagana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alipofika katika Ofisi za Free Media, wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima, akiwa katika ziara katika vyombo vya habari ambayo aliianza jana, jijini Dar es Salaam.


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana kwa furaha na Mhariri Mtendaji wa Free Media, Nevile Meena alipowasili kwenye kampuni hiyo akiwa katika ziara kwenye vyombo vya habari mjini Dar es Salaam


Nape akizungumza na baadhi ya viongozi wa kampuni ya Free Media wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima  jijini Dar es Salaam.

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA MAMA MZAZI WA JAJI AUGUSTINO RAMADHANI, DAR ES SALAAM

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Bibi Bridget Ramadhani, Mama Mzazi wa Jaji Augustino Ramadhani, wakati wa mazishi Ijumaa February 6, 2015 huko Kimara King'ongo jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakijumuika na waomboilezaji wengine katika mazishi ya Marehemu Bibi Bridget Ramadhani, mama Mzazi wa Jaji Augustino Ramadhani, wakati wa mazishi Ijumaa February 6, 2015 huko Kimara King'ongo jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Bibi Bridget Ramadhani, mama Mzazi wa Jaji Augustino Ramadhani, wakati wa mazishi Ijumaa February 6, 2015 huko Kimara King'ongo jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiweka shada kwenye kaburi la Marehemu Bibi Bridget Ramadhani, mama Mzazi wa Jaji Augustino Ramadhani, wakati wa mazishi Ijumaa February 6, 2015 huko Kimara King'ongo jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU

WAZIRI MEMBE ATOA RAI KWA MADHEHEBU KUOMBEA UADILIFU KWA VIONGOZI

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (wa pili  kulia), akiongozana na Rais wa Baraza Kuu la Makanisa ya Sabato Duniani,  Askofu Ted Wilson (wapili  kushoto),  Waziri wa Kilimo, Mhe. Stephen  Wassira (kushoto), pamoja  na  Mchungaji Blasius Luguri, Mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa la Utume  kuingia katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Mhe. Membe alikuwa mgeni rasmi katika Sherehe za ufungaji Kongamano la Kimataifa la Utume kwa Kanisa la Sabato  lililofanyika hapa nchini na kuyashirikisha Mataifa zaidi ya 20.
Waziri Membe akiwahutubia mamia ya Waumini wa Kanisa la Sabatoikiwa ni siku ya kilele cha Kongamano la Kimataifa la Utume kwa  Makanisa ya Sabato.  Wengine katika picha waliokaa ni Rais wa Kanisa hilo duniani, Askofu Wilson na Mkewe pamoja na Mhe. Wasira wakimsikiliza mmoja wa Viongozi akitafsiri kwao baadhi ya maneno ya Kiswahili yaliyokuwa kwenye hotuba ya Mhe. Membe.  

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Shamba la Bibi na Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam toka angani

0
0
Uwanja wa Uhuru Maarufu kama "Shamba la Bibi" ukiwa kushoto mwa Uwanja Mkuu wa Taifa ambao bado haujapewa jina rasmi unavyoonekana leo baada ya kuwekwa paa upande wa "Urusi".
Haijajulikana bado lini utaanza kutumika na kuupumzisha Uwanja wa Taifa ambao ndilo kimbilio la shughuli karibu zote za michezo  na za jamii.

SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII LAANZA MCHAKATO WA KUWASAKA WENYE VIPAJI VYA MPIRA WA MIGUU.

0
0
Itakumbukwa kuwa mnamo tarehe 26/01/2015 Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lilisaini mkataba maalum na timu ya Real Madrid ya Nchini  Hispania ya kuanzisha na kuendesha kituo cha michezo (NSSF- REAL MADRID Sports Academy) kwa lengo la kuibua, kuendeleza na kukuza vipaji kwa mpira wa miguu. 
Shirika la NSSF litajenga kituo hicho katika eneo la Mwasonga Kigamboni nje kidogo ya mji wa Dar es Salaam na wataalamu kutoka timu ya Real Madrid watatoa mafunzo kwa vijana wa umri wa miaka13 hadi 19 kwa madhumuni ya kukuza mpira wa miguu nchini, kupata wachezaji bora wanaouzika nje na ndani ya nchi pamoja na kulipatia mapato shirika na nchi kwa ujumla .

Akizungumza na Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya Habari Nchini, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dr. Ramadhani K. Dau alisema mradi huo ukiwa kama sehemu ya uwekezaji wa NSSF ulianza maramoja baada ya kusaini mkataba.  
NSSF imeanza utaratibu wa kuwabaini vijana walengwa ambapo kwa kuanzia utafutaji wa vipaji vya mpira wa miguu utaanzia mkoa wa Dar es Salaam kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 14. Utafutaji wa vipaji utafanyika kiwilaya kwa Wilaya za mkoa wa dar es salaam na utakuwa unafanyika  katika viwanja vya Karume. Zoezi hilo litakuwa linafanyika kati ya saa 1 asubuhi hadi saa 9 alasiri  kwa tarehe zilizoainishwa.

Uandikishaji  wa washiriki utakuwa unafanyika siku za mwisho wa wiki ili kutoathiri wanafunzi watakaopenda kushiriki na utaanza rasmi tarehe 14 na 15,na tarehe 22 na 23  Februari 2015, na kufuatiwa na michezo ya majaribio tarehe 28 Februari,na Tarehe 1 Machi 2015 kwa wilaya  zote za mkoa wa Dar es salaam ambapo kituo kitakuwa viwanja vya Karume kuanzia saa moja asubuhi hadi saa 9 alasiri.

 Zoezi la Uandikishaji halitahusisha gharama zozote kwa washiriki, na uandikishaji wa washiriki utafanyika kwa kujaza fomu maalum na kupewa namba ya ushiriki na kila mshiriki atapata fursa ya kucheza katika awamu mbili za dakika 30. Kwa kuanzia washiriki watatakiwa kuja na vifaa vyao vya michezo.


Zoezi la awali litafanywa na wataalam wa ndani ya nchi ambapo Vijana 500 kati ya wote watakaofanyiwa majaribio  wataingia katika awamu ya pili ya majaribio na  watadahiliwa na wataalamu kutoka Klabu ya Real Madrid na hatimaye kupatikana vijana 30 amabo ndio wataingia katika  shule maalum ya mafunzo kwa awamu ya kwanza. 

Wakati wa uandikishwaji washiriki watatakiwa kuja na wazazi/walezi wao wakiwa na vitambulisho vyao,na kijana husika awe na Cheti  halisi cha kuzaliwa  na kopi  yake pamoja na picha mbili za pasport  rangi ya blue.Muda wa uandikishaji na majaribio unaweza kuongezwa kulinagana na mahitaji.


Shirika la NSSF linatoa wito kwa vijana kujitokeza kwani ni fursa kwao ya kuweza kujiendeleza kimichezo na kujiajiri katika tasnia hiyo

WANAKWAYA WA CENTRAL MIRERANI WAKABIDHI MSAADA WA MIFUKO 34 YA SARUJI KUJENGEA CHOO CHA SHULE YA ENDIAMTU

0
0
Na Joseph Lyimo, Mirerani
Shule ya msingi Endiamtu ya Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, yenye upungufu wa matundu 19 ya choo, imepatiwa msaada wa mifuko 34 ya saruji iliyotolewa na kwaya ya Mirerani Central ya Kanisa la Wasabato SDA. Katibu wa Kanisa hilo, 
Benson Nyaura akizungumza jana wakati akikabidhi mifuko hiyo 34 ya saruji kwa Diwani wa kata ya Endiamtu Lucas Zacharia alisema kanisa ni taasisi inayojali mahitaji ya jamii hivyo wamejitoa ili kusaidia wanafunzi hao. 
 Nyaura alisema kila wakati Kanisa hilo linashirikiana na wananchi katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuhakikisha kwa namna moja au nyingine wanatatua matatizo yanayoizunguka jamii. 
 Kwa upande wake, Diwani wa kata ya Endiamtu Lucas Zacharia aliwapongeza wana kwaya hao kwa kujitolea kiasi hicho cha saruji, ambapo ikichanganywa na fedha zilizotengwa, zitawezesha kujengwa kwa choo kingine cha shule hiyo. 
 Zacharia alisema alipochaguliwa kuwa Diwani mwaka 2010 alikuta shule hiyo ina majengo ya madarasa mawili na wanafunzi wa kuanzia darasa la kwanza hadi la sita, ila sasa wameongeza madarasa mengine manne na ofisi ya walimu. 
 “Mimi kwa kushirikiana na jamii na halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, tumeweza kuiendeleza shule hii ambayo mwaka jana ifanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la saba hivyo kuonga kitaaluma,” alisema Zacharia. 
 Naye, Ofisa mtendaji wa kata ya Endiamtu Edmund Tibiita alipongeza jitihada za Diwani huyo kuipa kipaumbele shule hiyo ya msingi ambayo awali ilikuwa inadharaulika kuwa ipo porini na sasa imepiga hatua kubwa hasa kitaaluma. 
 “Sasa hivi shule hii ina vyumba sita vya madarasa, kutoka vyumba viwili vilivyokuwepo mwaka 2010 na Diwani Lucas amechangia fedha zake binafsi sh5 milioni kwa ajili ya kuendeleza shule hii na anafaa kupongezwa,” alisema Tibiita.
Wanakwaya wa Central Mirerani wa Kanisa la Wasabato SDA Songambele Mji mdogo wa Mirerani, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakisalimia jana na viongozi wa kata ya Endiamtu, baada ya kukabidhi mifuko 34 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa choo cha shule ya msingi Endiamtu ambayo ina upungufu wa matundu 19 ya choo
Diwani wa Kata ya Endiamtu Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Lucas Zacharia (wapili kulia) na viongozi wa shule ya msingi Endiamtu wakipokea mifuko 34 ya saruji iliyotolewa jana na wana kwaya wa Mirerani Central wa kanisa la Wasabato SDA.

BENKI YA NBC YADHAMINI SEMINA YA WAHARIRI WA BIASHARA NA UCHUMI

0
0
 Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Rukia Mtingwa akifungua semina ya wahariri wa habari za biashara na uchumi kutoka vyombo mbalimbali vya habari iliyodhaminiwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam
 Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe akizungumza wakati wa semina ya wahariri wa habari za biashara na uchumi iliyodhaminiwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam
 Meneja Mwenza wa Kampuni ya Auditax international,  Straton Makundi akiwasilisha mada kuhusu uelewa wa taarifa za fedha za taasisi mbalimbali wakati wa semina ya wahariri wa habari za biashara na uchumi iliyodhaminiwa na benki ya NBC jijini Dar es Salaam.
 Mhariri Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Mwananchi C          ommunications Ltd, Bakari Machumu akitoa mada kuhusu uandishi sahihi wa habari za biashara na uchumi   wakati wa semina ya wahariri wa habari za biashara na uchumi iliyodhaminiwa na benki ya NBC jijini Dar es Salaam
 Mhadhiri wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Salutary Orio aliwasilisha mada kuhusu sheria za mabenki na biashara za kibenki wakati wa semina ya wahariri wa habari za biashara na uchumi iliyodhaminiwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam 
Mmoja wa waendesha mikadala wakati wa semina ya wahariri wa habari za biashara na uchumi, Arden Kitomari mmiliki wa blogu ya kitomari banking & finance blog, akiweka mambo sawa wakati wa semina hiyo.  

MSANII WA KUNDI LA KAOLE AFARIKI DUNIA

0
0
MSANII wa maigizo aliekuwa kwenye Kundi la Kaole,Mwajuma Abdallah ‘Mama Mashaka’ (pichani) amefariki dunia siku ya Alhamis akiwa nyumbani kwake Yombo Reli,Kiwalani na baadae mwili wake kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Amana,Ilala jijini Dar es salaam.

Taarifa za msiba huo zilitolewa jana na Watoto wa Marehemu kwa ndugu na majirani wa eneo hilo,huku tetesi zikienea kwamba wamefanya hivyo ili kukwepa aibu kwa majirani kutokana na nyumba aliyokuwa akiishi mama yao huyo kuwa ni chakavu,hivyo waliutoa mwili kimya kimya na kuupeleka hospitali kuuhifadhi na wao wakarudi nyumbani kufanya ukarabati kidogo wa nyumba.walipomaliza ndio wakatoa taarifa ya msiba.

Mama Mashaka amezikwa leo asubuhi huko kijijini kwao,Vihingo wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMINA.

MKULIMA WA KATAVI ALIYEJISHINDIA MILIONI 10 ZA VODACOM AKABIDHIWA KITITA CHAKE, Ni kupitia promosheni ya JayMillions, Bilioni 24.3 zawasubiri wateja

0
0
Mmoja wa washindi wa milioni 10 kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania – Hynes Petro Kanumba mkazi wa Katavi mwishoni mwa wiki alikabidhiwa fedha zake katika hafla iliyofanyika mkoani humo. 
 Promosheni ya Jaymillions inayoendelea ikiwa katika wiki ya tatu na ambayo itadumu kwa muda wa siku 100 itaendelea kuleta faraja na mafanikio kwa wateja wa Vodacom kwa kuweza kujinasua katika hali duni ya maisha. 
 Hadi kufikia leo ni Sh. 126m/- pekee zilizokwisha kuchukuliwa na Uwezo Madengenya na washindi wengine wawili – Hyness Petro Kanumba kutoka Rukwa na James Mangu (Mwanza) – wa Sh. 10m/- na milioni 6m/- zimekwenda kwa – Chiliphod Wanjala (Mwanza), Janeth Nganyange (Njombe), Evarista A (Mwanza), Stanley Bagashe (Shinyanga), Ramadhani H. Maulid (Dodoma) na Lucas Masegese (Shinyanga) – wa Sh. 1m/-. 
Kiasi cha zaidi ya Sh. 5bn/- (ambazo ni sawasawa na magari madogo 428 ya muundo wa mgongo wa kobe) zingeweza kunyakuliwa na wateja iwapo wangetuma neno “JAY” kwenda 15544 kucheki kama wameshinda. 
Akizungumza wakati akikabidhiwa fedha zake za Ushindi, mshindi wa Shilingi Milioni 100 wa Promosheni hiyo, Hynes Kanumba, amewaomba Watanzania kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Kampuni ya Vodacom nchini katika kujenga na kuimarisha maisha ya Watanzania. "Promosheni ya Jaymillions naona inalenga kuwakomboa kimaisha watanzania hususani wenye kipato cha chini hasa wajasiriamali wadogo wadogo kama vile; wamachinga, mama ntilie, na wazee wastaafu ambapo kwa kiasi kikubwa tunajua watu wa aina hii wanahitaji msaada ili kujiendeleza kiuchumi. 
Kwa fedha ambazo baadhi ya washindi tayari wamezipata wengi zimewasaidia kujikwamua na kujiendeleza kimaisha," alisema Kanumba. 
 Aliongeza kuwa yeye ni mfano dhahiri wa Watanzania kuwa promosheni hii haina ujanja bali ya kweli kwa kuwa pamoja na kuishi kijijini ameweza kushinda na leo ameingiziwa fedha zake kwenye akaunti. 
"Sasa nimepata mwanga katika maisha yangu baada ya kujishindia fedha hizi kwa sababu sijapewa masharti wala utaratibu wowote wa matumizi ya fedha hizi, maisha niliyokuwa nayo yalikuwa duni sana ambayo yamewezeshwa na promosheni hii’’.Alisema. 
 Kanumba alisema ndoto yake ya kuwa mkulima stadi anayejimudu imetimia kwa kuwa kwa muda mrefu amekuwa akifanya kazi ya kilimo akiwa anakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile kutokuwa na pembejeo za kisasa ili niweze kuendesha kilimo cha kisasa 
“Kuanzia sasa kwa fedha nilizopata nitamaliza shughuli zangu za kilimo na nitanunua mifugo na kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili familia yangu. 
 Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu, akiongea katika hafla hiyo alimpongeza mshindi huyo na kusema kwamba fedha hizo zimeenda kwa mshindi sahihi kwani mshindi huyo ana malengo mazuri ya matumizi ya fedha zake kwa kuendeleza kilimo cha kisasa kwani kilimo ndiyo uti wa mgongo kwa Taifa letu. 
Pia aliwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni ya Jaymiilions ili wajishindie mamilioni ya fedha kwa kuhakikisha wanatuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza bahati zao za kushinda.Aliitaja njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/- 
“Tunaendelea kuwasisitizia wateja wetu wacheki kila siku ili kujua kama namba zao zimeshinda. Kama Kanumba asingetuma ujumbe siku ile angeendelea tu na maisha yake kama yalivyokuwa bila kujua kama namba yake ilichaguliwa kushinda. Hadi hivi sasa tuna washindi 10 wa zawadi za pesa taslimu Sh. 127m/- lakini kila siku wateja 111 wanachaguliwa kushinda. Bado kuna Sh. 24.3bn/- za kushindaniwa kwa siku 79 zilizosalia kwenye promosheni hii hivyo endeleeni kutuma “JAY” kwenda 15544 kila siku,” alisema Nkurlu. 
Pamoja na mambo mengine benki ya NMB imejitolea kutoa mafunzo ya ujasiriamali na matumizi sahihi ya fedha kwa Mshindi huyo ili kumuwezesha kuwa na matumizi yenye tija. 
 Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika tawi la benki ya NMB Katavi, Meneja wa tawi hilo Erick Luanda alisema kuwa benki yake imekuwa na ushirikiano mzuri wa kibiashara na hiyo hasa kupitia huduma yake ya M - pesa. 
 Luanda aliongeza kuwa mshindi wa Jaymilion pia ana akaunti na NMB hivyo kufanya benki kuamua kumpa ushirikiano mteja wao kwa kumkabidhi fedha zake kwenye ofisi za NMB. 
 "Kwanza ukiangalia huyu ni mteja wetu, pili sisi tumekuwa na uhusiano mzuri na kampuni ya Vodacom, Hivyo tumeona ni vyema kutumia fursa hii kutoa elimu kwa mshindi wa promosheni hii ili kumuwezesha awe na matumizi sahihi ya fedha yatakayo leta tija katika maisha yake,” alisema Luanda na kuongeza kuwa wataalamu wa benki watampatia elimu ya ujasiriamali ili aweze kujiendeleza kutokana na fedha alizopata.
 Mshindi wa kitita cha Shilingi Milioni 10/- kupitia promosheni ya JayMillions  inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hynes Kanumba  ambaye ni mkazi wa Inyonga Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya NMB tawi la Mpanda  baada ya kukabidhiwa fedha zake na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (kulia) Hafla hiyo ilifanyika  katika tawi hilo mkoani humo. Ili  kujua mteja  kama umeshinda  tuma neno Jay kwenda 15544.
 Meneja wa benki ya NMB  mkoa wa Katavi  Erick  Luanda  akimuonyesha taarifa za fedha ya benki (bank statement) Mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 10/- kupitia promosheni ya JayMillions  inayoendeshwa na Vodacom Tanzania , Hynes Kanumba  mkazi wa Inyonga Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi(wapili toka kushoto) wanao shuhudia ni Meneja mauzo  wa Vodacom kanda ya Kusini Petro Chinyama(kusho) na   Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu(kulia)Ili  kujua mteja  kama umeshinda  tuma neno Jay kwenda 15544.
003. Mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 10/- kupitia promosheni ya JayMillions  inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hynes Kanumba ambaye ni  mkazi wa Inyonga Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi akiwa anaondoka na mtoto wake mgongoni baada ya kukabidhiwa kitita chake rasmi na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(hayupo pichani) kwenye ofisi za  benki ya NMB tawi la Mpanda mkoani humo mwishoni mwa wiki. Ili mteja  kujua kama umeshinda   tuma neno Jay kwenda 15544.
  Hayawi hayawi yamekuwa  Haynes Peter Kanumba(20) na mwanaye akiwa haamini bahati yake baada ya kushinda  Milioni 10/- kupitia promosheni ya JayMillions  inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, akiwa mwenye furaha baada ya kukabidhiwa kitita chake na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi iliyofanyika mkoani Katavi.Ili mteja kujua kama umeshinda  unatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
   Hayawi hayawi yamekuwa  Haynes Peter Kanumba(20) ambaye ni mshindi wa Milioni 10/- kupitia promosheni ya JayMillions  inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, akiwa mwenye furaha baada ya kukabidhiwa kitita chake na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi iliyofanyika mkoani Katavi.Ili mteja kujua kama umeshinda  unatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
 Mshindi wa Milioni 10/- kupitia promosheni ya JayMillions  inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hynes Kanumba  mkazi wa Inyonga Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi akipongezwa  kwa kupigiwa makofi na Meneja Uhusiano wa Vodacom Matina Nkurlu (kulia) Meneja Mauzo wa kampuni hiyo wa  kanda za juu kusini na Meneja wa NMB mkoa wa Katavi Erick Luanda,mara baada ya kumkabidhi kitita chake wakati wa hafla fupi iliyofanyika mkoani Katavi mwishoni mwa wiki.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu(kulia) akimkabidhi kitita  cha shilingi Milioni 10/-Hynes Kanumba ambaye ni mkulima mkazi wa Inyonga  mkoa wa Katavi,alizojishindia kupitia promosheni ya JayMillions  inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika tawi la NMB Mpanda mkoani Katavi mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia katika picha kutoka kushoto ni Meneja wa NMB  mkoani  humo Erick Luanda,Meneja mauzo wa kampuni hiyo wa Kanda za juu kusini Petro Chinyama . Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

YANGA YAJICHIMBIA KILELENI LIGI KUU TANZANIA BARA

0
0
Mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima (kushoto) akichuana na beki wa Mtibwa Sugar,  David Luhende wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 2-0.
 Beki wa Mtibwa Sugar, Shaban Nditi akimdhibiti beki wa Yanga, Mbuyu Twite.
 Kocha wa Yanga, Hans Pluijm akitoa maelekezo kwa wacherzaji wakei.
Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe akichuana na kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohamed wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 2-0. (Picha na Francis Dande)
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

UBUNIFU WA KUVUTIA WATEJA katika MAONESHO YA Kimataifa MASCUT OMAN

0
0
Warembo kutoka Thailand wakiwa Wametulia nje ya Mlango wa Banda lao ikiwa ni ubunifu wa kuwavutia na kuwafurahisha Wateja wanaoingia katika Banda lao kujionea bidhaa mbalimnali za nchi yao katika Maonesho ya Kimatifa ya Sanaa,ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut-Oman
Bunduki ni miongoni mwa zana zinazotumika katika ngoma ya Asili kutoka nchini Moroko. Pichani Wasanii hao wakitumbuiza nje ya banda lao kuvutia wateja kujionea bidhaa mbalimbali za nchi yao katika maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,ubunifu na utamaduni. Picha na Faki Mjaka-Mascut Oman
Wasanii wa Ngoma za Asili kutoka Tanzania wakitumbuiza nje ya Mlangoni wa Banda lao la Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni Mascut nchini Oman. Utumbuizaji wa ngoma ni mfumo wanaoutumia katika kuwavutia na kuwafurahisha Wateja kuingia katika Banda la Tanzania kwenye Maonesho hayo. Pichani ni Ngoma ya Msewe yenye asili ya Zanzibar. Picha na Faki Mjaka.
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images