Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 731 | 732 | (Page 733) | 734 | 735 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Juma Malemi akiongoza kikao wakati Viongozi wa Kikosi cha Zimamoto toka Jiji la Linz, Austria walipotembelea Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji cha Jiji la Linz, Austria Christian Puchner, akimkabidhi Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Juma Malemi mojawapo ya kofia za zimamoto zilizotolewa kama msaada kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji la Tanzania. Kushoto ni Diwani wa Jiji la Linz Bwana Deltef Wimmer.
  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Juma Malemi akijaribisha mojawapo ya kofia za zimamoto zilizotolewa na Jeshi la Zimamoto la Jiji la Linz, Austria kama msaada kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji la Tanzania.


  0 0

   Mtayarishaji wa Vipindi wa Radio FM, Zourha akimkabidhi zawadi ya Laptop mume wake mtarajiwa  ambaye pia ni Mtalaamu wa IT wa kituo hicho, George Zuri wakati wa sherehe ya kuagwa jana kwenye Ukumbi wa Quality Centre, Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Bibi Harusi mtarajiwa, Zourha akilia baada ya kuagwa na babake, Malisa kushoto
   Zourha akiwapatia keki wazazi wake wakati wa sherehe hiyo
   Wafanyakazi wenzie na baba wa Zourha, Mzee Malisa kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakiwa na furaha wakati wa sherehe hiyo
   Zourha na mpambe wake Mary Thomas wakicheza muziki. 

  0 0

    


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Duniani kwenye sherehe za uzinduzi wa Utume (MISSION EXTRAVAGANZA) zilizofanyika leo Februari 06,2015 uwanja wa Taifa jijini                 Dar es salaam.
   Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Duniani wakiwa kwenye maandamano wakati wa sherehe za uzinduzi wa Utume (MISSION EXTRAVAGANZA) wa kanisa hilo zilizofanyika leo Februari 06,2015 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
   Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Duniani wakiwa kwenye maandamano wakati wa sherehe za uzinduzi wa Utume (MISSION EXTRAVAGANZA) wa kanisa hilo zilizofanyika leo Februari 06,2015 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Duniani Dkt. Ted Wilson katikati, wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Dini mbalimbali kwenye uzinduzi wa sherehe za Utume (MISSION EXTRAVAGANZA) za kanisa hilo zilizofanyika leo Februari 06,2015 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Duniani Dkt. Ted Wilson baada ya kuzindua sherehe za Utume (MISSION EXTRAVAGANZA) za kanisa hilo zilizofanyika leo Februari 06,2013 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. (Picha na OMR)

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick akikata utepe kuashiria kukabidhi mashine wakati wa ufungwaji wa mafunzo ya ufyatuaji tofali na makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam kwa vikundi vya vijana. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akikabidhi mashine kwa viongozi wa vkundi vya vijana wa Dar es Salaam wakati wa ufungwaji wa mafunzo ya ufyatuaji tofali na makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam kwa vikundi vya vijana. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick akizungumza wakati wa ufungwaji wa mafunzo ya ufyatuaji tofali na makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam kwa vikundi vya vijana. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana.
  Mkuu wa wilaya ya Temeke akizungumza wakati wa ufungwaji wa mafunzo ya ufyatuaji tofali na makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam kwa vikundi vya vijana. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana. Picha zaidi BOFYA HAPA  0 0

  Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA, kimetaja makundi ya timu zitakazoshiriki kucheza hatua ya 18 bora (hatua ya pili) ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam,inayotarajia kuanza kutimua vumbi mapema mwezi huu.
  Katika kundi 
  (A) limepangwa kuwa na timu za Simba U20,Red Coast,Sifa UTD,Shababi,Ukonga UTD,Zakhem,Ugimbi,Beirahotspurs na Pan Africa.
  Katika kundi 
  (B) litakuwa na timu za Yanga U20,Stakishari,FFU,New Kunduchi,Sinza Stars,Changanyikeni,Tuamoyo,Sifapilitan na Azania Unga.

  Ligi hiyo ya mkoa wa Dar es salaam iliyokuwa na jumla ya timu 36, imeingia katika hatua ya pili,ambayo  itaanza Februari 11 mwaka huu katika viwanja mbalimbali.
  Kundi (A)
   Simba U20    vs    Red Coast       (Karume)
  Sifa UTD         vs   Shababi           (Mwl/Nyerere)
  Ukonga UTD  vs   Zakhem           (Airwing)
  Ugimbi           vs   Beirahospurs  (Bandari)

  KATIKA KUNDI (B) Februari 12
  Yanga U20    vs   Stakishari          (Karume)
  FFU                vs  New Kunduchi   (Benjamini Mkapa)
  Sinza Stars    vs  Changanyikeni   (Kines)
  Tuamoyo      vs  Sifapolitan          (Bandari)
  Viongozi wa DRFA bado wanatoa wito kwa viongozi wa vilabu mbalimbali,mashabiki na wakazi wa jiji pamoja na maeneo ya jirani,kujitokeza kwa wingi kushuhudia vipaji vya wachezaji.
   Imetolewa na DRFA

  0 0
 • 02/06/15--11:53: kutoka bungeni leo
 •  Mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji Taifa,George G.Bajuta kulia akiwa ameongozana na Mbunge wa Chalinze Mhe.Ridhiwani Kikwete katikati na Mbunge wa Mtera ,Mhe.Livingstone Lusinde wakati akielekea katika ukumbi wa Bunge kusikiliza ripoti ya kamati maalumu ya Bunge kuhusu Migogoro ya ardhi.
   Mhe. Ole Sendeka akipongezwa na jamii ya wafugaji kutoka Mkoa wa Manyara waliofika kufuatilia kikao cha bunge leo mara baada ya kumaliza kuwasiloisha ripoti ya kamati teule iliyo kuwa inashughulikia migogoro ya Ardhi hapa Nchini.
  Mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji Taifa,George G.Bajuta akiwa anazungumza na waandishi wa habari mara baada ya Bunge kusikiliza ripoti ya kamati maalumu ya Bunge kuhusu Migogoro ya ardhi iliyo wasilishwa na Mhe. Ole Sendeka.
  Picha na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii Kanda ya Kati

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (wa tatu kutoka kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Ujumbe wa Viongozi wa Makundi ya Chama cha SPLM cha Sudan ya Kusini

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (wa tatu kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya na Ujumbe wa Viongozi wa Makundi ya Chama cha SPLM cha Sudan ya Kusini   Ujumbe wa Viongozi wa Makundi ya Chama cha SPLM cha Sudan ya Kusini yalifanya mazungumzo  na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mjini Dar es Salaam jana.
  Mazungumzo haya yalilenga kuandaa utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa mjini Arusha  mwezi wa januari tarehe 21 ambayo yanalenga kuyaunganisha makundi matatu katika chama cha SPLM kurudisha Amani na kuunda Serikali itakayowajumuisha viongozi kutoka makundi yote.
  Katika mazungumzo ya jana makundi haya yamekubaliana kuendelea na mkakati  wa utekelezaji wa makubaliano ya Arusha kwa lengo la kuandaa utaratibu wa viongozi  wa makundi yote kurudi Sudan ya Kusini mapema iwezekanavyo.

  0 0


  0 0  0 0  0 0
 • 02/06/15--14:35: ubungo mataa


 • 0 0

  Na Othman  Khamis Ame,  OMPR – ZNZ.
  Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Peter Pinda aliwapongeza wanamichezo wa Timu za Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuliletea sifa kubwa Bunge hilo kwenye mashindano ya michezo mbali mbali ya Kitaifa na Kimataifa. 
   Mh. Pinda alitoa pongezi hizo katika Tafrija maalum ya kuukaribisha mwaka mpya zilizofanyika katika majengo ya Bunge la Jamuhuri Mjini Dodoma hafla iliyokwenda sambamba na kuwapongeza wanamichezo wa Bunge hilo baada ya kushinda michezo tofauti katika mashindano ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Mjini Arusha Tanzania. 
   Waziri Mkuu Pinda alisema kwamba michezo inatoa nafasi kubwa ya ushirikiano ambayo ni kielelezo cha msingi kinachozaa Viongozi bora wanaotokana na sekta ya michezo. 
   Aliishauri Kamati ya Uongozi wa Michezo ya Bunge hilo kufikiria umuhimu wa kuwashirikisha wawakilishi wa wanamichezo wa mabunge wanachama kwenye tafrija kama hizo kwa lengo la kusherehekea nao pamoja ili kudumisha ushirikiano pamoja na ujirani mwema. Alieleza kwamba michezo ina nafasi pana ya kupunguza joto la kisiasa, hitilafu au ugomvi unaotokea baina ya nchi na nchi na kupelekea watu wa pande zinazohitilafiana kurejea kwenye ushirikiano na mafungamano baina yao. 
   Mh. Pinda alifahamisha kwamba kwa kuwa mabunge mengi yana utaratibu mzuri wa kuandaa mashindano ni vyema kwa waheshimiwa wabunge kuzitumia fursa kama hizo katika kushiriki kwenye mazoezi na hatimae mashindano kwa lengo la kudumisha afya zao. 
   Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania aliwatakia mwaka mwema wa 2015 Waheshimiwa wote wa Bunge la Jamuhuri hasa mwezi Oktoba mwaka huu ambao kama wamefanya vyema majimboni mwao utawarejesha tena kwenye wadhifa wao. 
   Alisema kurejea kwa Wabunge hao kwa kiasi kikubwa kunaweza kuleta faraja kubwa kwa vile tayari wameshazoeana kutokana na kushirikiana pamoja katika vikao vya Bunge hilo kwa takriban miaka mitano. Mapema Mwenyekiti wa Bunge Sports Club Iddi Azan alisema ongezeko la michezo mbali mbali kwenye mashindano ya Timu za Mabunge ya Afrika ya Mashariki linatokana na azimio la Mabunge ya Jumuiya hiyo la kuzitaka Nchi Wanachama kuongeza michezo mengine kwenye mashindano hayo. 
   Mwenyekiti Azan alisema mshindano ya Mabunge hayo yalikuwa yakishirikisha michezo miwili tuu ile ya Kandanda na Pete ambapo kwa sasa ipo riadha, mbio za vijiti, kuvuta kamba, kufukuza kuku ikiwemo pia ile ya watu wenye mahitaji maalum { Walemavu }. 
   Mwenyekiti huyo wa Bunge Sports Club alielezea faraja yake kutokana na ushiriki mzuri wa wanamichezo wa Timu za Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye mashindano mbali mbali ya Mabunge na kuleta ushindi katika michezo tofauti. 
   Katika mashindano hayo ya mwaka 2014 ya Timu za Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyoshirikisha wachezaji 150 Timu ya Mpira wa Pete Wanawake ya Bunge la Tanzania ilitokea mshindi wa kwanza, Riadha wanawake washindi wa kwanza, riadha wanaume washindi wa Tatu, mpira wa miguu washindi wa Pili na kuvuta kamba Timu za wanawake na wanaume Tanzania zimeshika nafasi ya kwanza.
   Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiwa pamoja na Spika wa Bunge Mh. Anna Makinda na Baadhi ya Wabunge wakifurahia vikombe mbali mbali vilivyoibuliwa na Timu za Bunge la Jamuhuri katika Mashindano yha Mambunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
   Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wakiwa kwenye tafrija ya kuupokea mwaka mpya wa 2015 iliyofanyika katika majengo ya Bunge Mjini Dodoma sambamba na kuzipongeza Timu za Bunge hilo zilizoshinda kwenye mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki.
   Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwapongeza wachezaji wa timu za Bunge la Jamuhuri kwenye tafrija ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2015 katika majengo ya Bunge hilo Mjini Dodoma.
  OMPR – ZNZ.
  Waziri Mkuu akiwaongoza waheshimiwa wenzake kwenye mduara ulioporomoshwa na bendi ya Utalii katika tafrija ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2015 Mjini Dodoma. Picha na 

  0 0

  Miami Florida. The worlds largest education and learning company - Pearson, has featured Africa's Most influential Child - Zuriel Oduwole earlier today in her first US Commercial. It was first shown to 40,000 Pearson employees in their annual convention in Miami this morning, before it rolls out on other platforms and on TV. The commercial simply tells Zuriels incredible story in 2 minutes, as a Nigerian 12 year old, doing the most improbable things across the globe. She attends one of Pearson's online learning structured programs, via Connections Academy in California. She was chosen over millions of children, as her accomplishments were simply remarkable and heads and shoulders, above other students across the US in the area of supporting children's education, especially girls. Zuriel gave her first policy speech to the global media in London in May 2014, advocating e-learning as the best way to reach the continents uneducated and out of school kids. She has now taken the first tangible step, towards realizing this by way of this partnership of community service awareness with Pearson. A beautiful and distinguishing element in it all, is she is an African Girl Child. Africa indeed, Rises !!! VIEW TV COMMERCIAL HERE:

  0 0

  10945033_856755441041229_6165141623154796543_o

  UNFPA, UNICEF, Shirikisho la Kimataifa la Wakunga na Shirikisho la Kimataifa la Magonjwa ya Wanawake na Uzazi.
  Wito kwa wafanyakazi wa afya duniani kote ili kuhamasisha kukomesha ukeketaji.

  Kwa mwaka 2015, ujumbe wa kimataifa wa siku ya kupinga ukeketaji umewalenga wahudumu wa afya; “Uhamasishaji na ushirikishwaji wa wafanyakazi wa Afya ili kuharakisha kutokomeza ukeketaji”. Na hii ni kwa sababu asilimia 34 ya ukeketaji duniani hufanywa na wahudumu wa afya.
  Pamoja na ujumbe huu mahsusi kwa wahudumu wa afya, wadau wengine wote unawahusu.

  Ujumbe unasema hivi:
  Ukeketaji wa wasichana na wanawake unakiuka haki za binadamu na unadhoofisha afya na ustawi wa wasichana takriban milioni 3 kila mwaka. Zaidi ya wasichana na wanawake milioni 130 katika nchi 29 barani Afrika na Mashariki ya Kati ambapo hadi leo hii vitendo hivi vimekithiri wamekwisha fanyiwa aina fulani ya ukeketaji - na athari kwa maisha yao ni kubwa sana.


  0 0


  0 0
 • 02/07/15--00:59: rambirambi

 • Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Semamba Makinda (Mb), kwa niaba ya Bunge la Jamhuri ya Muungao wa Tanzania anatuma salaamu za rambirambi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Bwana Othman Rashid, kufuatia kifo cha mama yake mzazi, BI. TAJIRI ABDALLAH KITENGE, kilichotokea tarehe 5 Februari, 2015.

  Aidha, Spika Makinda anatuma salaamu za rambirambi kwa Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mhe. Augustino Ramadhani kufuatia kifo cha mama yake mzazi, BI. BRIDGET RAMADHAN, kilichotokea Februari 3, 2015.

  “Nimepokea taarifa za misiba hii kwa masikitiko makubwa na ninawapa pole familia, ndugu, jamaa na marafiki wote. Ninamwomba Mwenyezi Mungu awape faraja wafiwa katika kipindi hiki kigumu.

  BWANA  alitoa na BWANA  ametwaa, Jina la BWANA  lihimidiwe. Amina.”


  Imetolewa na Ofisi ya Bunge,

  Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na

  Uhusiano wa Kimataifa


  DODOMA


  0 0

  Ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya Diplomasia ya  uchumi, Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa uliandaa hafla maalum kwa ajili ya mawakala wa safari (Tour operators) iliyofanyika mjini Paris Ijumaa Februari 6, 2015


  Madhumuni ya hafla hii ni kuitangazia Tanzania na vivutio vyake vya utalii kwa mawakala wa safari (Tour operators) ambao ni wadau wakubwa kutokana na ushawishi wao kwa watalii wa Ufaransa wanaotaka kutembelea Tanzania.

  Baadhi ya wadau wa utalii wakimsikiliza Mh Balozi Begum Taj

  Wageni wakionja baadhi ya vyakula vya kitanzania

  Ukarimu kwa wageni ni tunu ya watanzania

  Picha ya jumla wa walioshiriki katika hafla ya kuitangaza Tanzania

  0 0  0 0
 • 02/07/15--01:08: Bei ya Madafu leo

older | 1 | .... | 731 | 732 | (Page 733) | 734 | 735 | .... | 3283 | newer