Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 730 | 731 | (Page 732) | 733 | 734 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Rais wa Mahakama ya Afrika ya  Haki za Binadamu(AfCHPR)Jaji Augustino Ramadhani akitoa hotuba yake fupi mbele ya Rais wa Shirikisho la Ujerumani,Mheshimiwa Joachim Gauck leo jijini Arusha.
   Rais wa shirikisho la Ujerumani,Joachim Gauck akizungumza na wafanyakazi wa  Mahakama ya Afrika ya  Haki za Binadamu(AfCHPR)

  Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani,Philipo Sanka Marmo(katikati)akibadilishana mawazo na Afisa Habari Mwandamizi wa Mahakama ya  Afrika ya  Haki za Binadamu(AfCHPR) Bw. Sukhdev Chatbar(shoto) na Mwandishi wa habari wa gazeti la The Citizen, Bw. Zephania Ubwani.

  0 0

   Vikosi vya Simba iliyokuwa Simba enzi hizo...


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya  Kiislamu ya Iran Mohammed Javad  Zarif alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)  akizungumza na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya  Kiislamu ya Iran Mohammed Javad  Zarif (wa pili kulia) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)  akizungumza na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya  Kiislamu ya Iran Mohammed Javad  Zarif (kulia kwa Rais ) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao. Picha na Ikulu, Zanzibar

  0 0

  Na Annastazia Rugaba, PDB habari
  Mtendaji mkuu wa Ofisi ya Rais, usimamizi wa utekelezaji wa miradi (PDB) Bwana Omari Issa, leo amekabidhi rasmi taarifa ya mkakati wa kuboresha sekta ya afya chini ya BRN kwa jumuia ya wahisani wa maendeleo. 
  Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za PDB ambapo jumuiya ya wahisani ilipata fursa ya kusikiliza kwa kina namna BRN inavyofanya kazi ya kuleta matumaini mapya kwa watanzania kupitia sekta za kipaumbele. Sekta ya afya imekuwa ikijaribu kuboresha utendaji wake lakini kuingia katika BRN kutaleta tija Zaidi. 
  BRN inaamini katika misingi mikuu ambayo ni kuweka vipaumbele, kuwa na adabu ya utekelezaji, uwajibikaji na uaminifu, ufuatiliaji wa kina na wa mara kwa mara na Mawasiliano thabiti kati ya watoa huduma na wapokea huduma. 
  Hizi ni nguzo muhimu zitakazotufikisha katika dira ya maendeleo ya taifa ya Mwaka 2025. Awamu ya kwanza ya BRN iliziangazia sekta sita ambazo ni Kilimo, Elimu, Maji, Uchukuzi, Nishati na ukusanyaji wa mapato ambapo sekta za Afya na Uboreshaji wa mazingira ya Biashara zimeanza rasmi Mwaka huu. 
  Sekta sita za mwanzo zimedhihirisha mafanikio anuwai ambayo yaliwavutia jopo la wataalamu wa maendeleo wakiongozwa na Rais Mstaafu wa Botswana Bw Mogae. Ripoti kamili ya utekelezaji wa BRN kwa Mwaka wa kwanza itazinduliwa rasmi mapema mwezi Machi Mwaka huu. 
   Sekta ya afya inakusudia kutekeleza vipaumbele vine ambavyo ni mosi; ugawanyaji sawia wa wahudumu wa afya wenye ujuzi takikana kuanzia ngazi ya chini ya afya ya msingi, pili; utoaji huduma wenye ubora wa nyota tatu katika ngazi zote, tatu; upatikanaji wa dawa na bidhaa muhimu za afya katika ngazi zote, nne; kuimarisha afya ya uzazi na usalama wa mama na mtoto ili kupunguza vifo vya kundi hili muhimu kwa angalau asilimia 60 ifikapo Mwaka 2018. 
   Jumuiya ya wahisani wamepongeza uamuzi wa kuiingiza sekta ya afya katika BRN na wakithibisha utayari wao wa kufanikisha mkakati huu, wametoa wito kwa wizara ya afya, PDB, Sekta binafsi na jamii ya kitanzania kwa ujumla kuhakikisha kuwa mkakati huu utafanikiwa. 
   Malengo haya yote yanahitaji juhudi kubwa na ya pamoja kutoka kwa jamii, wizara na taasisi zake zote hadi ngazi ya kijiji, wahisani wa maendeleo na sekta binafsi. 
  “Tusingoje nani aanze, sote tuwajibike, kila mmoja ajitazame kama anawajibika ipasavyo. Dira ya maendeleo ya Taifa tunayotaka itupeleke kuwa nchi yenye uchumi wa kati haiwezi kufikiwa tusipofanya kazi kwa pamoja bila kunyoosheana vidole. 
  BRN ni treni iliyoanza safari tayari, kila mmoja anawajibika kuingia kwa wakati na kwa nia Chanya, ukichelewa ukakuta imeondoka bado una fursa ya kuikimbilia kituo kinachofuata ili twende pamoja” Bw Omari Issa ametoa wito huo kwa wahisani wa maendeleo na jamii kwa ujumla.
   Mtendaji Mkuu wa PDB Bw. Omari Issa akielezea umuhimu wa sekta ya Afya kuingia BRN kuungana na sekta nyingine zilizotangulia zinazoendelea kuzaa matunda
   Dr Linda Ezekiel ambae ni Mkurugenzi wa sekta za jamii (Afya, Elimu na Maji) PDB akiwasilisha mada kuhusu malengo ya kipaumbele sekta ya afya kwa miaka
   Bw. Omari Issa akimkabidhi mwakilishi wa wahisani wa maendeleo mkakati wa sekta ya Afya chini ya BRN. 


  0 0

   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mkandarasi pamoja na Mhandisi Mshauri wa barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye jumla ya  km 89.3 inayojengwa kwa kiwango cha lami. Mradi huu utakapokamilika na kupokelewa na Serikali Mkandarasi atakaa site miaka mitatu kwa ajili ya uangalizi na kufanya marekebisho yoyote yatakayojitokeza kwa gharama zake mwenyewe.

   . Sehemu ya barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye jumla ya  km 89.3 inayojengwa kwa kiwango cha lami. Barabara hii imekamilika kujengwa kwa asilimia 97.

   Sehemu unapojengwa mzani utakaotumika kupimia magari makubwa yatakayopita kwenye barabara hiyo.

   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Itigi waliofika kumpokea kabla ya kuwahutubia wananchi kuhusu maendeleo ya mradi huo wa barabara. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  exim1 
  Mkuu wa matawi wa Benki ya Exim, Bi. Elizabeth Mayengoh, akikabidhi vitabu kwa mmoja wa watoto waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwenye wodi maalum ya watoto wanaougua ugonjwa wa saratani katika kuadhimisha siku ya saratani duniani. Wanaoshudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim na wazazi wa watoto hao. Benki hiyo ilikabidhi vifaa mbalimbali vikiwemo vyakula, vifaa vya kuchezea, sabuni, vifaa vya shule nk, lengo likiwa ni kujenga uelewa kuhusiana na ugonjwa wa saratani mpango unaoendana na kauli mbiu ya mwaka huu ya Siku ya Saratani Duniani inayosema kuwa tatizo la saratani “lipo ndani ya uwezo wetu”.
  exim2 
  Meneja masoko msaidizi wa Benki ya Exim, Bi. Anita Goshashy akishikana mikono na Dr. Livin Mumbari  Daktari wa watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, muda mfupi baada ya benki hiyo kukabidhi vifaa mbalimbali kwa watoto waliolazwa hospitalini hapo kwenye wodi maalum ya watoto wanaougua ugonjwa wa saratani katika kuadhimisha siku ya saratani duniani. 


  Wanaoshudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim na wazazi wa watoto hao. Benki hiyo ilikabidhi vifaa mbalimbali vikiwemo vyakula, vifaa vya kuchezea, sabuni, vifaa vya shule nk, lengo likiwa ni kujenga uelewa kuhusiana na ugonjwa wa saratani mpango unaoendana na kauli mbiu ya mwaka huu ya Siku ya Saratani Duniani inayosema kuwa tatizo la saratani “lipo ndani ya uwezo wetu”.

  0 0

  Na Bashir Yakub
  Yapo mambo  ambayo huwaumiza  watu vIchwa  yumkini  yakiwa   ni mambo madogo na ya kawaida.  Tatizo mara nyingi  huwa ni taarifa. Taarifa  zikimfikia  mtu ndipo huhisi jambo  ambalo alikuwa halijui  kuwa ni jepesi. 

  Lakini kabla  ya taarifa mtu  huendelea kufikiria jambo hilo kwa ugumu. Katika kipindi kama hiki kuwa na kitu kama pasipoti si jambo la  anasa  au ufahari tena isipokuwa ni jambo  ambalo limeishaingia katika matumizi ya kawaida   ya kila siku ya walio wengi. 
  Hii ni kutokana na kukua kwa  biashara za kimataifa, mawasiliano, utalii,usafirishaji  na kila kitu ambacho husababisha  watu kutoka nchi moja hadi nyingine.  Kwasasa kuwa na pasipoti  hata kama huna safari ya hivi karibuni ni jambo muhimu sana. 
  Yumkini  usisubiri ikutokee safari ya ghafla halafu ndio uanze kukimbizana  na  pasipoti. Pasipoti inayo manufaa mengi  lakini moja ni kuwa pasipoti  ni mali kama mali nyingine. Pasipoti inaweza kumdhamini mtu kama  mali nyingine inavyoweza kumdhamini  mtu.Pasipoti  ni amana tena amana ya kuaminika. Ni  kutokana na umhimu huu nikaona leo nieleze  pasipoti na namna ya kupata pasipoti.Kusoma Zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Mkurugenzi mkuu  wa TFDA, Hiiti Sillo (katikati), akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Halima Dendegu (wa kwanza kulia), katika ziara yake ya  kikazi mkoani Mtwara ikiwa ni harakati za awali za TFDA kufungua ofisi ya Kanda ya Kusini kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi. Kushoto ni Mfamasia wa mkoa wa Mtwara Bw. Musa Nasoro.

  0 0

   WAZIRI wa Uchukuzi, Samuel Sitta ameelezea kufurahishwa na waandaaji wa Tamasha la Pasaka na kusema kuwa katika miaka 15 ya tamasha hilo wana mengi ya kujivunia.
   
  Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na kusainiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa kamati yake imepokea salamu kutoka kwa Waziri Sitta akizungumzia maandalizi ya miaka 15 ya tamasha hilo.
   
  “Ni tamasha lenye tija kwa Watanzania, mimi mwenyewe nimekuwa shahidi wa namna mnavyosaidia yatima, wajane na makundi mbalimbali ya kijamii.
   
  “Nimesikia mwaka huu mna tamasha kubwa la miaka 15 tangu muanze kufanya Tamasha la Pasaka, niwatakie kila la heri katika maandalizi na naamini litakuwa tamasha la aina yake,” alisema Msama katika taarifa yake akimnukuu Sitta.

  Alisema wamekuwa wakipokea salamu kutoka kwa wadau mbalimbali wakizungumzia kuhusiana na maandalizi ya Miaka 15 ya Tamasha la Pasaka na wakielezea pia mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kwa kipindi hicho.

  Baadhi ya walioguswa na maandalizi ya tamasha hilo ni waimbaji mahiri wa muziki wa Injili kutoka Afrika Kusini Solly Mahlangu ‘Obrigado’ na Rebecca Malope.

   Wasanii hao wamewahi kwa nyakati tofauti kuja nchini katika Tamasha la Pasaka, ambapo mwaka huu waandaji wamepanga kufanya sherehe ya Miaka 15 ya Tamasha la Pasaka.

     

  0 0

  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi na Mwenyekiti wa Chadema Manispaa ya Moshi Jafary Michael akiwahutubia wakazi wa mji wa Moshi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Manyema mjini Moshi.
  Baadhi ya wakazi wa mji wa Moshi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa Meya wa Manispaa ya Moshi ,Jafary Michael katika viwanja vya Manyema ,Meya Jafary alikuwa akizungumzia vitendo vya Uporaji wa Viwanja vya Umma pamoja na tatizo la wafanya biashara ndogo ndogo  maarufu kama wamachinga.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya M uungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisaini kitabu cha kumbukukmbu kufuatia kifo cha mama mzazi wa Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani nyumbani kwake Kimara leo Februar 06, 2015 alipofika kwa ajili ya kumfariji.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya M uungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwafariji wana familia ya Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani alipomtembelea nyumbani kwake Kimara leo Februar 06, 2015, kutokana na kufiwa na mama yake mzazi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Jaji Mkuu mstaafu Augustino leo alipomtembelea nyumbani kwake kimara leo Februar 06, 2015 kwa ajili ya kumfariji kutokana na kufiwa na mama yake mzazi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani Baada ya kumfariji kutokana na kufiwa na mama yake mzazi alipomtembelea nyumbani kwake Kimara leo Februar 06, 2015. (Picha na OMR)

  0 0


  Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungia kati ya mechi tatu na nane wachezaji Juma Nyoso wa Mbeya City na Aggrey Morris wa Azam kutokana na makosa ya kinidhamu waliyoyafanya wakiwa uwanjani.


  Nyoso ambaye alilalamikiwa na TFF kwa kumfanyia vitendo vya udhalilishaji mshambuliaji Elias Maguri wa Simba amefungiwa mechi nane za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL). Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Ibara ya 57 na Ibara ya 11 (f) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012.

  Akiwa mbele ya Kamati hiyo jana (Februari 5 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Nyoso alikiri kufanya na kujutia kosa hilo, pia amemuomba radhi mchezaji Maguri kwa kitendo hicho.

  Akisoma uamuzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili Jerome Msemwa alisema kitendo kilichofanywa na Nyoso ni kosa kubwa, kudhalilisha utu wa mtu, na ni mfano mbaya kwa watoto na jamii nzima ya mpira wa miguu.

  Naye Morris amefungiwa mechi tatu za VPL baada ya kutiwa hatiani kwa kumpiga mshambuliaji Emmanuel Okwi wakati timu hizo zilipopambana kwenye mechi ya ligi iliyochezwa Januari 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Kabla ya kusoma uamuzi, Wakili Msemwa alisema mlalamikiwa Morris alikiri kugongana na Okwi, kwa maelezo kuwa aliingia kwenye 'reli' ndiyo ukatokea mgongano huo.


  Kamati baada ya kupitia malalamiko ya klabu ya Simba, ripoti za Brain CT scan kutoka Besta Diagnostic Centre na nyingine kutoka Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), taarifa za madaktari zilionyesha Okwi aligongwa kichwani akiwa anacheza mpira na kuzimia kwa dakika tano, pia mkanda wa video uliowasilishwa na TFF imeona kulikuwa na kugongana kati ya wachezaji hao.

  Hivyo, Kamati ikamtia hatiani Morris kwa kutumia Ibara ya 48(1)(d) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012 kwa kumfungia mechi hizo tatu na kumpa onyo kali.

  Pia Kamati hiyo imemfungia miezi sita na kumpiga faini ya sh. 200,000 Meneja Vifaa (Kit Manager) wa timu ya Polisi Mara, Clement Kajeri kwa kuhamamisha vurugu na kuwapiga waamuzi kwenye mechi dhidi ya Mwadui iliyochezwa Uwanja wa Karume mjini Musoma. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 40(2) ya Ligi Daraja la Kwanza.

  Wachezaji watatu wa Friends Rangers; Mahmoud Othman, Khalid Twahil na John Alexander wamefungia miezi sita na faini ya sh. 500,000 kila mmoja kwa kumpiga mwamuzi kwenye mechi ya Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Majimaji.

  Licha ya wachezaji hao kuitikia mwito wa Kamati, wachezaji hao walizuiwa na viongozi wa kuingia ukumbini wakati malalamiko dhidi yao yalipoanza kusikilizwa. Hatua hiyo iliifanya Kamati ifanye uamuzi baada ya kuusikiliza upande wa walalamikaji pekee.

  Shauri dhidi ya mchezaji George Michael wa Ruvu Shooting kwa kumchezea ubabe Amisi Tambwe wa Yanga, Kamati imeliahirisha baada ya mlalamikiwa kupata udhuru uliosababisha asiwepo.

  Pia Kamati ya Nidhamu imeelekeza malalamiko ya timu ya Friends Rangers kupinga refa kuchezesha mechi yao dhidi ya Majimaji kwenye mvua kubwa, kutoa maamuzi yasiyo halali na kutokuwepo na ukweli kwenye ripoti ya Kamishna yakasikilizwe na Bodi ya Ligi kwa vile si masuala ya kinidhamu.
    
  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Ibraline ,Ibrahim Shayo.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Moshi.  SIKU chache baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kutangaza punguzo la bei ya Mafuta Kampuni ya kutoa huduma ya usafirishaji wa ndani na nje ya nchi ya Ibraline imetangaza kushusha nauli kwa nusu ya bei elekezi ya SUMATRA.

  Hatua hiyo inakuja wakati baadhi ya wananchi kulalamika kutokuwepo na ahueni yoyote licha ya kwamba serikali imetangaza kushusha bei ya bidhaa ya Mafuta kwa nchi nzima kufuatia  bidhaa hiyo kushuka bei katika soko la dunia.

  Akizungumza ofisini kwake mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ibrahimu Shayo alisema Kampuni imefikia hatua hiyo ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa wateja wake ambao wamekuwa wakitumia huduma ya usafiri inayotolewa na Ibraline.

  “Tumeamua kufanya hivi lengo ni kuwashukuru wateja wetu wanao tumia huduma ya usafiri unaotolewa na kampuni yetu ya Ibraline…ningewajua mmoja mmoja ningeweza kuwapa mkono lakini kwa kuwa wanaishi maeneo tofauti ndio sababu tumeamua kurudisha kile tunachopata kwa njia ya kuwapunguzia bei.”alisema Shayo.


  0 0

  Mtaalam wa Kutoa Damu wa Kitengo cha Damu Salama, Kanda ya Mashariki, Daudi Mkawa akimtoa damu Mfanyakazi wa Airtel Tanzania, Amitin Mbamba wakati wa zoezi la kuchangia damu lililofanywa na wafanyakazi wa vitengo mbalimbali vya Airtel, jijini Dar es Salaam jana. Kitengo cha Damu Salama kina upungufu mkubwa wa damu ambapo kiasi cha ujazo wa unit 350,000 zinahitajika kwa ajili ya dharura za kitabibu kila mwaka.
  Wafanyakazi wa Airtel Tanzania (kutoka kushoto), Adam Suleiman na Frank Munale wakitolewa damu kwa ajili ya kuchangia katika Kitengo cha Damu Salama, Kanda ya Mashariki, wakati wa zoezi la kuchangia damu lililofanyika katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana. Kitengo cha Damu Salama kina upungufu mkubwa wa damu ambapo kiasi cha ujazo wa unit 350,000 zinahitajika kwa ajili ya dharura za kitabibu kila mwaka.
  Mtaalam wa Kutoa Damu wa Kitengo cha Damu Salama, Kanda ya Mashariki, Judith Goshashy akimpima shinikizo la damu Mkurugenzi wa Raslimali Watu wa Airtel Tanzania, Patrick Foya wakati wa zoezi la kuchangia damu lililofanywa na wafanyakazi wa vitengo mbalimbali vya Airtel, jijini Dar es Salaam jana. Kitengo cha Damu Salama kina upungufu mkubwa wa damu ambapo kiasi cha ujazo wa unit 350,000 zinahitajika kwa ajili ya dharura za kitabibu kila mwaka.


  0 0

   Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Kamishina wa Polisi Mussa Ally Mussa akiwa na mkuu wa jeshi la polisi mstaafu Philimon Mgaya akikata utepe wa kuashiria kuzindua magari mapya Zaidi ya ishirini ya kampuni ya ulinzi ya Security Group Africa ambayo yataanza kutumika katika kazi mbalimbali za kampuni hiyo hivi karibuni.Katikati yao ni mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Eric Sambu.
   Mwakilishi wa Mkuu wa jeshi la polisi nchini Kamishina wa Polisi Mussa Ally Mussa  akipokea msaada wa pikipiki mbili aina ya Boxer toka kwa mwenyekiti wa bodi wa kampuni ya Security Group Africa ambae pia ni mkuu wa  jeshi la polisi mstaafu Philimon Mgaya kwaajili ya kusaidia jeshi hilo katika oparasheni mbalimbali za kupambana na uhalifu,Katikati yao ni mkurugenzi mkuu wa kampuni ya SGA nchini  Eric Sambu.
   Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya SGA nchini  Eric Sambu akizungumza kwenye hafla ya kuzindua magari mapya Zaidi ya ishirini ya kampuni ya ulinzi ya Security Group Africa ambayo yataanza kutumika katika kazi mbalimbali za kampuni hiyo hivi karibuni.Hafla hiyo imefanyika katika ofisi za kampuni hiyo Mbezi Beach jijini Dar Es Salaam.
   Mwakilishi wa Mkuu wa jeshi la polisi nchini Kamishina wa Polisi Mussa Ally Mussa  akikagua gwaride maalum la kuashiria kuanza kwa shuguli ya kuzindua magari mapya Zaidi ya ishirini ya kampuni ya ulinzi ya Security Group Africa ambayo yataanza kutumika katika kazi mbalimbali za kampuni hiyo hivi karibuni.Kulia kwake ni mkuu wa kitengo cha mafunzo cha SGA bwana Rogers Lumwaji.
   Mwakilishi wa Mkuu wa jeshi la polisi nchini Kamishina wa Polisi Mussa Ally Mussa  akipeperusha bendera kuashiria kuanza kutumika kwa magari magari mapya Zaidi ya ishirini ya kampuni ya ulinzi ya Security Group Africa ambayo yataanza kutumika katika kazi mbalimbali za kampuni hiyo hivi karibuni.Katikati yao ni mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Eric Sambu.

  0 0

  Naibu kamanda wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi wilaya ya Moshi vijijini ambae pia anatajwa kutakiwa kuwania ubunge jimbo la vunjo Innocent Melleck shirima leo 06/02/2015 ni siku yake ya kuzaliwa. Kwa niaba ya vijana na wananchi wa jimbo la vunjo tunamtakia afya njema na Mwenyezi Mungu ambariki kuwa na umri mkubwa mara dufu.Tupo nae katika kutekeleza ndoto za maisha yake mwaka huu 2015.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge kwenye jengo la utawala la Bunge mjini Dodoma Februari 6, 2015. Kutoka kushoto ni Yahya Kassim Issa wa Chwaka, Jerome Damas Bwanausi wa Lulindi, Muhammad Amour Chombo wa Magomeni na Mussa Hassan Mussa wa Aman.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wabunge kwenye jengo la utawala la Bunge mjini Dodoma Februari 6, 2015. Kutoka kushoto ni Yahya Kassim Issa wa Chwaka, Jerome Damas Bwanausi wa Lulindi na Muhammad Amour Chombo wa Magomeni .
  Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa TLP akiteta na Mbunge wa Kuteuliwa na Mwenyekiti wa NCC MAGEUZI,James Mbatia (kushoto) bungeni mjini Dodoma Februari 6,2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Mwenyekiti wa kamati teule ya Bunge iliyokuwa inashughulikia matatizo ya Ardhi hapa Nchini Mhe. Christopher Ole Sendeka akiwasilisha Ripoti ya kamati yake katika kikao cha Bunge mjini Dodoma mapema leo.
  Wadau wa Ardhi Kutoka jamii ya wafugaji na wakulima wakiwa wamekaa ndani ya Ukumbi wa Bunge wakifuatilia wakati Mwenyekiti wa kamati teule ya Bunge iliyokuwa inashughulikia matatizo ya Ardhi hapa Nchini,  Mhe. Christopher Ole Sendeka akiwasilisha Ripoti ya kamati yake katika kikao cha Bunge mapema leo. 
  Watumishi wa kampuni ya Masu Entertrade wakiwa wabebeba makabrasha yenye ripoti ya kamati teule ya Bunge iliyokuwa inashughulikia migogoro ya Ardhi hapa nchini wakiwa wanaelekea ndani ya ukumbi wa Bunge.Picha na Deusdedit Moshi Globu ya Jamii Kanda ya Kati.

  0 0
 • 02/06/15--06:21: TAARIFA KWA UMMA TOKA TCRA

 • 0 0

  HEAD OF PERSONAL BANKING
  Qualifications: Bachelors/Masters degree in relevant professional qualification in banking and Accounting or Finance from a reputable institution
  Apply: www.pwc.com/tz/en/executive-search/index.jhml
  Details: Daily News Febr 04,2015
  Deadline: February  10,  2015

  HEAD OF OPERATIONS AND SERVICE DELIVERY
  Qualifications: Bachelors/Masters degree in relevant professional qualification in banking and Accounting or Finance from a reputable institution
  Apply: www.pwc.com/tz/en/executive-search/index.jhml
  Details: Daily News Febr 04,2015
  Deadline: February  10,  2015

  DRIVER  II  -  4  POSITIONS
  Qualifications: Certificate of Secondary Education with passes in Kiswahili and English,a valid class “C” driving licence of not less than three years without causing accident
  Apply: Director General
  Tanzania Tobaco Board
  Box 227, Dar es Salaam
  Details: Mwananchi Febr 05,2015
  Deadline: March  02,  2015

  READ MORE HERE

  0 0

  Meneja wa bia ya Safari Lager, Edidh Bebwa(kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa masindano ya Safari Nyama Choma kwa mwaka 2015 uliofanyika Dar es Salaam leo.Kushoto ni Jaji Mkuu wa mashindano hayo, Manase Mwasha.
  Jaji Mkuu wa mashindano Safari Nyama Choma, Manase Mwasha(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa masindano ya Safari Nyama Choma kwa mwaka 2015 uliofanyika Dar es Salaam leo.Kulia ni Meneja wa bia ya Safari Lager, Edidh Bebwa.
  Meneja wa bia ya Safari Lager, Edidh Bebwa(kulia) akimkabidhi kikombe Jaji wa mashindano ya Safari Nyama Choma 2015 wakati wa uzinduzi uliofanyika Dar es Salaam leo.

  BOFYA HAPA KWA BARI KAMILI

older | 1 | .... | 730 | 731 | (Page 732) | 733 | 734 | .... | 3272 | newer