Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 729 | 730 | (Page 731) | 732 | 733 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakifuatilia mafunzo ya sheria inayomlinda mtoto pamoja na masuala mengine ya jinsia yaliyokuwa yakitolewa kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo na Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Kinondoni, Inspekta Prisca Komba (hayupo pichani).
  Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Kinondoni, Inspekta Prisca Komba akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakati alipokuwa akitoa elimu juu ya sheria inayomlinda mtoto kwenye mwendelezo wa semina za mafunzo ya jinsia zinaoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wafanyakazi wake iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.
  Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Umma na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (aliyesimama) akimuuliza swali Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Kinondoni, Inspekta Prisca Komba (hayupo pichani) wakati wa mafunzo juu ya sheria inayomlinda mtoto kwenye mwendelezo wa semina za mafunzo ya jinsia zinaoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wafanyakazi wake iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Pamoja na kuwepo kwa changamoto za kushuka kwa bei ya mafuta duniani, Tanzania bado imeendelea kuvutia wawekezaji kutoka pande zote za Dunia kuja kuwekeza katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi nchini.

  Akiongea katika mkutano wa mwaka wa GE Oil & Gas, Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene (MB) aliwaalika wawekezaji wakubwa kutoka pande zote za dunia kutembelea Tanzania na kuona nafasi za uwekezaji zilizopo.

  Mkutano huo uliofanyika Florence, Italy uliwakutanisha wadau wakubwa wa Mafuta na Gesi duniani kujadili changamoto katika sekta hiyo na namna ya kuzikabili. Kauli mbiu ya mwaka huu ililienga zaidi kuangalia namna ambavyo sekta hii itachochea maendeleo ya dunia nzima kwa kuhakikisha kuwapo kwa nishati endelevu na yenye kujali mazingira.

  Tanzania iliwakilishwa pia na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dr. James Matargio ambaye alipata fursa ya kuitangaza Tanzania kwa kuonyesha fursa zilizopo katika sekta ya Mafuta na Gesi nchini.

  Dr. Mataragio alisema “ pamoja na kuwa bei za mafuta zinaendelea kushuka, bado kuna fursa ya kutumia gesi kusaidia upatikanaji wa nishati endelevu na yenye kulinda mazingira kwa vizazi vya sasa na baadae”
  Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. George Simbachawene (MB) akihutubia wadau mbalimbali wa mafuta na gesi duniana katika mkutano wa mwaka ulioandaliwa na GE Oil & Gas uliofanyika Florence, Italy.
  Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. George Simbachawene (aliesimama katikati) akibadilishana mawazo na CEO wa Exxonmobil (Moja ya Kampuni kubwa ya Mafuta na Gesi duniani). Aliesimama sambamba na Waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dr. James Mataragio na aliekaa ni Rais na CEO wa GE Oil & Gas, Lorenzo Simonelli.
  Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. George Simbachawene (MB) akisikiliza kwa makini wakati Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dr. Mataragio (Hayupo pichani) akiongea kuitangaza Tanzania kwa wadau na wawekezaji wakubwa wa Mafuta na Gesi duniani, aliekaa kushoto kwa Waziri ni Rais na CEO wa GE Oil & Gas, Lorenzo Simonelli.
  Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dr. James Mataragio akiongea katika mkutano wa mwaka wa GE Oil & Gas uliofanyika Florence, Italy 

  0 0

  "Participants gather at the inaugural Great Lakes to Great Lakes Initiative on the shores of Lake Tanganyika in Kigoma, Tanzania".
  "‎The North American and African Great Lakes systems hold nearly half of the world's surface freshwater resources.‎"

  The United States Special Envoy for the African Great Lakes and the Democratic Republic of the Congo (DRC) Russell Feingold, in collaboration with the Lake Tanganyika Authority (LTA), launched a unique initiative this week to bring together experts from the North American Great Lakes with counterparts from the African Great Lakes to address sustainable management of these trans boundary waters. ‎ Together the North American and African Great Lakes systems hold nearly half of the world's surface freshwater resources.‎

  Over three days (February 2-4) on the shore of Lake Tanganyika in Kigoma, Tanzania, scientists, academics and policymakers from the United States and Canada engaged in an in-depth exchange with colleagues from countries around one of the African Great Lakes‎, Lake Tanganyika, including Burundi, DRC, Rwanda, Tanzania, and Zambia. ‎


  0 0


  0 0

  Kampuni ya Ms Shimoja  yenye Makao Makuu yake katika Jimbo la Michigan  Nchini Marekani iko mbioni kutaka kuanzisha kituo cha Matangazo ya Televisheni Mjini Dar es salaam Nchini Tanzania kitakachotoa huduma ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki.

  Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ambae pia ni Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani Dr. Robert Shumake alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake katika Jengo la Msekwa ndani ya viunga vya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.

  Dr. Shumake alisema licha ya kwamba matangazo ya Televisheni yanachukuwa sehemu kubwa ya burdani lakini Kituo hicho kitalenga zaidi kutoa vipindi wa Elimu vitakavyowasaidia wananchi na hasa wanafunzi wa elimu ya msingi, sekondari na vyuo vikuu Afrika Mashariki.

  Alisema mipango inaandaliwa na Kampuni hiyo katika kuyashirikisha Makampuni ya Mitandao ya Mawasiliano Duniani ya Google na Microsoft ili kuona Elimu inayokusudiwa kufikishwa kwa umma kupitia matangazo ya Kituo hicho yanafanikiwa kwa kiwango kikubwa.

  Dr. Shumake alifahamisha kwamba mpango huo unakusudiwa kwenda sambamba na ule utakaoandaliwa na Kampuni hiyo wa kuwapatia mafunzo vijana wapatao 50,000 kutoka Bara la Afrika katika Jimbo la Michigan Nchini Marekani.

  Alisema hatua hiyo inakusudia kuwajengea uwezo wa ajira vijana hao katika fani ya  ujasiri amali utakaowapa fursa nzuri ya kufanya kazi katika taasisi na mashirikia yoyote ya Kitaifa na Kimataifa.

  “ Tumejipanga kuwapatia mafunzo maalum viiana wa Bara la Afrika ili kusaidia kupunguza wimbi la vijana wasio na ajira ndani ya Bara hili “. Alifafanua Balozi huyo wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani Dr. Shumake.

  Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alimshukuru Dr. Robert  Shumake pamoja na Kampuni yake kwa uamuzi huo wa busara utakaowezesha kuisaidia pia Serikali katika mapambano dhidi ya uhaba wa ajira Nchini.

   Balozi Seif alisema Serikali zote mbili ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeweka milango wazi kwa taasisi na mashirika ya Kitaifa na Kimataifa kuwekeza miradi yao kwa kutumia rasilmali zilizopo nchini ili  kusaidia nguvu za kiuchumi na kupunguza ukali wa maisha.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimshauri Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Ms Shimoja ya Nchini Marekani kuangalia fursa nyingi zaidi  za uwekezaji zilizopo Nchini Tanzania ambazo Kampuni yake inaweza kuongeza uwekezaji zaidi.
  Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani ambae pia ni Murugenzi wa Kampuni ya Ms Shimoja ya Nchini Marekani Dr. Robert Shumake akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake iliyopo katika Jengo la Msekwa ndani ya Viunga vya Bunge la Jamuhuri nya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibadilishana mawazo na Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani ambae pia ni Murugenzi wa Kampuni ya Ms Shimoja ya Nchini Marekani Dr. Robert Shumake Bungeni Mjini Dodoma. Picha na – OPMR – ZNZ.

  0 0


  0 0
 • 02/05/15--04:51: Article 18


 • 0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akikabidhi
  funguo za trekta kwa Mwalimu wa Shule ya msingi Kwadelo Bw. Hamza Haji,matrekta saba yalikabidhiwa leo kwa wakulima chini ya usimamizi wa
  Diwani wa Kwadelo Alhaji Omari Kariati.(Picha na Adam Mzee)
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akikabidhi funguo za trekta kwa Dk. Edmund Mndolwa ambaye ni Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa ikiwa sehemu ya matrekta saba yaliotolewa na Alhaji Omari Kariati Diwani wa Kwadelo.
   Moja ya matrekta waliokabidhiwa wakulima ,Alhaji Omari Kariati ameshatoa matrekta 100 mpaka leo tarehe 5 februari 2015.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi matrekta saba kwa wakulima yaliyotolewa na Diwani wa Kwadelo Alhaji Omari Kariati ambapo aliwataka viongozi kushiriki shughuli za wananchi (Picha na Adam Mzee).

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma Februari, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Februari 5, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimaa John Kwegyir, kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Februari 5, 2015.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na wananchi kutoka wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe walitembelea Bunge mjini Dodoma kwa mwaliko wa Mbunge wao wa jimbo la Njombe Magharibi, Gerson Lwenge ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi Februari 5, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wananchi kutoka wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe waliotembelea Bunge mjini Dodoma kwa mwaliko wa Mbunge wao wa jimbo la Njombe Magharibi, Gerson Lwenge ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi Februari 5, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga akiwaonyesha wananchi wa kijiji cha Sanya Stesheni Rejesta ya wakazi kama moja ya vitendea kazi vya wenyeviti wa vitongoji.
  Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga akimkabidhi rejesta ya wakazi mmoja ya wenyeviti wa kitongoji katika kijiji cha Sanya Stesheni.
  Mmoja ya wazee wa kabila la Wamaasai akimtawaza Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga kwa miongoni mwa viongozi wa jamii hiyo maarufu kama Laigwanan kwa kumkabidhi rungu.


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim, Bw. Baddal Calikusu akitoa maelezo mafupi kabla ya Ufunguzi wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya Mradi wa Ubia wa Kilimo cha Umwagiliaji unaotarajiwa kuanza rasmi kutekelezwa katika eneo la Magereza, Gereza Kigongoni Bagamoyo(kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Green Park iliyoko Bagamoyo.
  Wajumbe wa Bodi ya mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji kutoka Jeshi la Magereza wakisikiliza maelezo ya utambulisho kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim Bw Baddal Calikusu (hayupo pichani)
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim, Bw. Baddal Calikusu (aliyesimama) akitoa utambulisho kwa wajumbe wapya wa Bodi kabla ya Ufunguzi wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya Mradi wa Ubia wa Kilimo cha Umwagiliaji unaotarajiwa kuanza rasmi kutekelezwa katika eneo la Magereza, Gereza Kigongoni Bagamoyo.
  Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Gideon Nkana akiwa na Wajumbe wengine wa Bodi ya mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji Gereza Kigongoni wakikagua eneo la Mradi utakapotekelezwa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim, Bw. Baddal Calikusu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji Gereza Kigongoni mara baada ya Kikao cha kwanza kilichofanyika katika Hoteli ya Green Park iliyopo Mjini Bagamoyo (wa kwanza kulia) ni Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Gideon Nkana(wa tatu kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Magereza,Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza John Masunga.

  0 0

  Na Sylvester Onesmo wa 
  Jeshi la Polisi Dodoma. 
   Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kama Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema kama alivyotoa taarifa jana tarehe 04/02/2015 kuhusiana na kuawa kwa Askari  Namba G. 7168 PC JOSEPH ISACK SWAI huko Chango’ombe ya juu Mkoani Dodoma na mtu aliyefamika kwa jina la TISSI S/O SIRIL MALYA.
  Jeshi la Polisi Mkoa wa Dododoma lilianza msako wa kumtafuta mtuhumiwa huyo baada ya kufanya kitendo hicho cha kinyama cha kumkata kata kwa panga kichwani na mikononi Askari huyo. Kamanda MISIME amesema majira ya saa 23:00hrs usiku wananchi walimuona maeneo ya Mti Mkavu Mailimbili Mkoani Dodoma akiwa bado na lile panga alilotumia kumuua Askari. 
   Hata hivyo walichukua sheria mkononi na kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake, Polisi walifika eneo la tukio na kumchukua kisha kumkimbiza Hospitali ya Mkoa lakini daktari akagundua ameshafariki. 
   Aidha Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa huyo katika kumbukumbu tulizonazo ni kwamba mwaka 2006 aliwahi kufungwa miaka mitatu (3) kwa kosa la kujeruhi, Pia mwaka 2009 alifungwa tena miezi sita (6) kwa kosa la kutishia kuua. 
   Ametoa pongezi kwa wananchi kwa kuonyesha kuchukizwa na kitendo alichomtendea Askari wetu lakini waache kujichukulia sheria mkononi. 
  Pia ametoa wito kwa wananchi tuanze kuchukua hatua kurekebisha maadili kuanzia ngazi ya familia kwani tumeelezwa kuwa mtuhumiwa alikuwa ni mvutaji bangi kiasi kwamba ilimfanya awe anafanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadili na sheria za nchi.
  Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu akiongoza leo waombolezaji katika kutoa heshima za mwisho kwa Askari  Namba G. 7168 PC JOSEPH ISACK SWAI aliyeuwawa huko Chango’ombe ya juu Mkoani Dodoma na mtu aliyefamika kwa jina la TISSI SIRIL MALYA.
  Wasifu wa marehemu ukisomwa 
  Maombolezo wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa askari huyo shujaa


  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kamugisha Kazaura (Kulia) akimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa(TTCL) Justine Mwandu(Kushoto) baada ya kukamilisha mradi wa kuunganisha Makao Makuu ya NIC na matawi 24 nchi nzima kwenye mtandao wa TTCL(MPLS-VPN). Tukio hilo limefanyika katika ofisi za Shirika la Bima la Taifa (NIC).
  Meneja wa Mradi wa TTCL Ngayalina Mihayo akitoa ufafanuzi kuhusu Shirika la Bima la Taifa jinsi lilivyounganishwa katika mtandaowa TTCL wa MPLS- VPN.
  NIC and TTCL wakiwa katika picha ya pamoja.

  BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI

  0 0

  MHE. JOHN MICHAEL HAULE


  0 0

   Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki ambaye pia ni mkazi wa Mbweni, Mhe. Shy Rose Bhanji akiwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mbweni-Malindi, jijini Dar es Salaam, Bariki wakisimamia ukarabati wa barabara yao leo.
   Mbunge wa Bunge kla Afrika Mashariki ambaye pia ni mkazi wa Mbweni, Shy Rose Bhanji akielekeza jambo kwa mkandarasi.
  Barabara ya Mbweni-Malindi inavyonekana baada ya kuanza kufanyiwa ukarabati.

  0 0
 • 02/05/15--08:10: msiba reading, uingereza
 • Jumuiya ya Watanzania Reading tunaendelea kwa majonzi makubwa kuomboleza na kuhani msiba wa mwanafamilia mwenzetu Mama Anna Goodchild (pichani), na kuifariji familia nyumbani kwake ktk anuani hii:-


         56b St Peter's Road
         Reading (Wokingham Rd area)
         RG6  1PH
  Marehemu Anna Goodchild ataagwa kwa Heshima ya Mwisho-

  Siku:      Ijumaa ya 06/02/2015.
  Muda:   Saa Nane Mchana
  Anuani: Kanisa la "Our Lady of
               Peace"
               Wokingham Rd, RG6 7DA  Mazishi:Makaburi ya Early, Reading

  Bwana Aliyetoa ndiye  Ametwaa.
  AMINA
  Jumuiya ya Watanzania Reading.

  0 0

    
  Dear Esteemed Customer,


  We sincerely apologize for not being able to provide services to you, our esteemed customers and the public in general on the evening of February 4, 2015. This was due to a technical failure on one of the features on our network.

  As a result of this you were unable to make voice calls, use the internet and do money transfers. We understand the inconvenience that this outage caused you and would like to once again apologize and thank you for your patience, loyalty and support while we worked to restore our services.

  Our engineers were able to fix the problem and restore full services within 23 minutes of the failure.

  I would like to assure you, our esteemed customers that we at Vodacom remain committed to continue providing you with world-class services.

  Thank you for your support, patience and understanding throughout this period.


  Managing Director

  Rene Meza

  0 0  0 0

  Kupitia mtandao huu wa jamii,  ninayoheshima kuwakaribisha watu wote kutoka jiji hili la Dallas na vitongoji vyake katika TAMASHA  KUBWA LA UIMBAJI  litakalofanyika katika mji wetu.Tamasha hili litatanguliwa na chakula cha pamoja saa kumi na moja kamili mpaka saa kumi na mbili jioni.
  Karibuni sana.
  Pastor Absalom

  0 0

   Mwandishi wa habari wa Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar Leo Nd. Abdi Shamna akiuliza swali kuhusiana na Tenzi Dume wakati wa maadhimisho hayo.

   Naibu Waziri wa Afya Mhe. Mahamoud Thabit Kombo akizunguza na wajumbe na waandishi wa habari jinsi ya kuwaelimisha wananchi juu ya kupambana na ugonjwa huo.

   Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wanaoishi na Saratani Zanzibar Bi. Mwanahamisi Moh’d Abdalla ambae pia ni muhanga wa ugonjwa wa Saratani akitoa ufafanuzi jinsi alivyopambana na ugonjwa huo na hatimaye kupona kabisa  katika siku ya maadhimisho ya siku ya Saratani Duniani kwa upande wa Zanzibar.

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wanaoishi na Saratani Zanzibar Dkt. Msafiri Marjani akitoa elimu juu ya ugonjwa wa Saratani katika mkutano wa maadhimisho ya siku ya Saratani Duniani uliofanyika ofisini kwao Mpendae Zanzibar. PICHA NA ABDALLA OMAR - MAELEZO, ZANZIBAR


older | 1 | .... | 729 | 730 | (Page 731) | 732 | 733 | .... | 3284 | newer