Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 728 | 729 | (Page 730) | 731 | 732 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Ndugu, Issa Wahichinenda  Mkurugenzi wa uendeshaji wa UTT AMIS akitoa maada kuhusiana na fursa za uwekezaji katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja kwa wafanyakazi wa ofisi ya Mkaguzi wa hesabu za serikali katika kikao cha baraza la wafanyakazi kilicho fanyika hivi karibuni  Mtwara.

  UTT AMIS ndiyo magwiji katika kuanzisha na kuendesha Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (Mutual Funds) hapa nchini. Mpaka sasa UTT AMIS inaendesha mifuko mitano ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi yenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 235.  Mifuko yote hii imeweza kukidhi vigezo  muhimu vya uwekezaji ambavyo ni Usalama,Ukwasi na Faida (Safety, Liquidity and Returns). Mifuko hii inayoendeshwa na UTT AMIS ni kwa ajili ya watanzania wote, vikundi, Saccos, taasisi, kampuni na mifuko ya hifadhi za jamii. Wawekezaji wote wananufaika  kwa kupata faida shindani, uwekezaji mseto ili kupunguza hatari za  uwekezaji,utalaamu wa meneja wa mifuko,unafuu wa mkubwa wa gharama na uwazi kwani bei halisi ya vipande vya mifuko hutangazwa kila siku za kazi.

   Baadhi ya washiriki wa kikao cha baraza la wafanyakazi la ofisi ya Mkaguzi  wa Hesabu za  Serikali wakifuatilia uwasilishwaji mada kuhusiana na fursa za uwekezaji katika mifuko ya Pamoja inayoendeshwa na UTT AMIS.

  0 0

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na mgeni wake Rais wa Ujerumani Mhe,Joachim Gauck mara alipowasili   katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar  leo akitokea Dar es Salaam akiwa katika ziara ya siku moja Nchini akifuatana ma Mkewe Daniela Schadt pamoja na viongozi mbali mbali wa Nchi hiyo. 
   Rais wa Ujerumani Mhe,Joachim Gauck  akisalimiana na  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (katikati) mara alipowasili   katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar  leo akitokea Dar es Salam akiwa katika ziara ya siku moja Nchini akifuatana ma Mkewe Daniela Schadt pamoja na viongozi mbali mbali wa Nchi hiyo (kulia) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein 
     Rais wa Ujerumani Mhe,Joachim Gauck akiwasili shada la mauwa na mtoto Salma  Issa mara alipowasili   katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar  leo akiwa katika ziara ya siku moja Nchini akifuatana ma Mkewe Daniela Schadt pamoja na viongozi mbali mbali wa Nchi hiyo.

  0 0

   Kamishna wa Kazi na Utumishi wa Umma Zanzibar Mr. Kubingwa Mashaka Simba akitoa nasaha na kufunga Mafunzo ya siku tu ya matumizi sahihi ya Mitandao ya kijamii (Social Media) yaliyofanyika Shule ya VIP mwanakwerekwe Mjini Zanzibar (kulia) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Elimu Zanzibar (ZEDO) Ussi Said Suleiman na (kushoto) Mjumbe wa kamati ya wazazi Ndugu. Makame Ameri Yusuf. 
   Kamishna wa Kazi na Utumishi wa Umma Zanzibar Mr. Kubingwa Mashaka Simba akimkabidhi Cheti mmoja wa wanafunzi wa (Social Media) Suhaila Humoud Hilal.
   Mgeni Rasmin Kamishna wa Kazi na Utumishi wa Umma Zanzibar Mr. Kubingwa Mashaka Simba (wakatikati) waliokaa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa Mafunzo ya siku tatu ya matumizi ya Mitandao ya kijamii (Social Media).
  Baadhi ya wahitimu wa Mafunzo ya siku tatu ya matumizi ya Mitandao ya kijamii (Social Media) wakionyesha veti vyao. 
   Mwenyekiti wa Jumuiya ya Elimu Zanzibar (ZEDO) Ussi Said Suleiman (kulia) akimkaribisha Kamishna wa Kazi na Utumishi wa Umma Mr. Kubingwa Mashaka Simba katika hafla ya ufungaji wa mafunzo ya siku tatu ya matumizi ya Mitandao ya kijamii (Social Media) yaliyofanyika Shule ya VIP mwanakwerekwe Mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

  0 0


  Mkuu wa wilaya Temeke, Sofia Mjema, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Kiislamu, Twayyibat, iliyopo Manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam, wiki iliyopita.

  Kuwapo kwa shule hizo kutazidi kuongeza idadi kubwa ya watoto wanaopata elimu ya msingi, sekondari na vyuo Vikuu kwa ajili ya kujikomboa katika maisha yao.

  Ukiacha mikoani ambako hakuna shule nyingi hususan maeneo ya vijijini, jijini Dar es Salaam kumefanikiwa kuwa na shule nyingi mno, zikiwamo za serikali na mashirika.

  Zipo shule za kidini ambazo wakati wote zimekuwa zikifundisha watoto elimu ya Dunia na ile ya kufahamu Mungu ni nani, nazumgumzia pale watoto wanapofundishwa kisawa sawa na kukolea kiimani kama njia ya kumjua Mungu na kutenda matendo ya kiungwana.

  Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema, alitembelea katika shule ya Twayyibat Islamic Seminary, iliyopo Temeke, jijini Dar es Salaam.

  DC Sofia alitumia muda huo kuikagua shule hiyo pamoja na kuzungumza na wadau wa elimu, walimu na wanafunzi wa shule hiyo kwa ajili ya kuona inakuwa kati ya shule bora wilayani Temeke na Dar es Salaam kwa ujumla.

  Miongoni mwa mambo yaliyomkosha DC Sofia ni pale alipoambiwa kuwa ada ya shule hiyo kwa mwaka mmoja ni Sh 200,000 tu, jambo ambalo ni agharabu kuliona wala kulikisia katika shule mbalimbali jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza shuleni hapo, Mkuu huyo wa wilaya ya Temeke, Sofia, anasema kwamba ameshangazwa na kuwapo kwa ada nafuu katika shule ya Twayyibat.
  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH) and Rosa Luxemberg-Stiftung Tanzania have signed an agreement to establish the Mwalimu Nyerere Resource Centre in Dar es Salaam.

  The Centre according to the Agreement inked in the city on Monday,is a semi-autonomous body under COSTECH with own organs of governance and full authority to run its programmes.

  The Agreement also stipulates that the Centre will provide a forum to organize conferences, seminars and other opportunities for discussions and debate to advance strategic thinking on the holistic development of the country and the continent, to honour the memory and advance the nationalist, socialist and Pan African legacy of Mwalimu Nyerere.
  Representative of the Rosa Luxemburg-Stiftung Mr Siegfried Schroeder(left),COSTECH Director General Dr Hassan Mshinda(Centre) and Founding Director of the Nyerere Resource Center Prof Issa Shivji sign Project Agreement about Mwalimu Nyerere Resource Centre


  0 0

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma 
           Leo tarehe 04.02.2015 majira ya saa 11:00 limetokea tukio baya na la kusikitisha la kuuawa kwa askari wa Polisi Mkoa wa Dodoma namba G.7168 PC JOSEPH ISACK SWAI.
            Chanzo cha kuuawa huyu askari ni kwamba alipigiwa simu na Mtendaji wa Mtaa wa chang’ombe juu hapa Dodoma Mjini akimjulisha kuwa amepokea taarifa ofisini kwake kutoka kwa OLIVER BALTAZARI, MIAKA 52, MKAZI WA CHANG’OMBE JUU kuwa kijana wake aitwaye TISI S/O SIRILI MALYA ana mtesa motto wake mdogo wa miezi nane aitwaye VALERIAN TISI MALYA na anahisi labda ameshamuua kwani motto huyo halii tena.
            Alichofanya mtendaji huyu ni kumpigia askari wetu huyo simu naye akaenda hadi katika Ofisi ya huyo Mtendaji wa Mtaa. Waliongozana wote wakiwa pamoja na kijana mmoja hadi anakoishi huyo TISI SIRILI MALYA. Walipofika askari aligonga mlango akijitambulisha kuwa yeye ni askari hivyo atoke nje.
            Alichofanya mtuhumiwa huyo ni kumnyanyua mtoto  wake mdogo wa miezi nane kwa mkono mmoja miguu juu kichwa chini na kutaka kumkata kwa panga na kusema namkata shingo na sitaki kuona mtu.
            Askari aliamua kumwokoa mtoto huyo na alipomrukia mtuhumiwa kwa bahati mbaya aliteleza na ndipo mtuhumiwa akamkata kichwani askari wetu na akadondoka chini kutokana na jeraha kubwa alilomsababishia. Hata hivyo mtuhumiwa huyo aliendelea kumkatakata na Mtendaji na kijana waliyekuwa naye ambaye ni maratibu wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu iliwabidi kukimbia huku wakipiga kelele kuomba msaada.
            Mtuhumiwa baada ya kufanya kitendo hicho cha kinyama alikimbia huku nguo zake zikiwa zimetapakaa damu akiwa na panga mkononi.
            Askari huyu muda mfupi kabla ya tukio hili alikuwa ametokea katika kituo cha Redio cha Dodoma FM kwa ajili ya kuandaa kipindi cha kuielimisha jamii juu ya ulinzi wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) tunapoelekea kipindi cha uchaguzi, kwani mbali na kazi anazofanya mojawapo ni kushiriki katika vipindi vya kutoa elimu ya Polisi Jamii hapa mkoani Dodoma.
            Msako bado unaendelea ili kuweza kumtia nguvuni mtuhumiwa huyu aliyesababisha kifo cha askari wetu wakati alipojitolea maisha ya ili kumwokoa huyo mtoto mdogo.
            Tuinazidi kuomba msaada wa wananchi popote pale watakapomuona TISI S/O SIRILI MALYA, MIAKA 29, MCHAGA ambaye ni maji ya kunde, mwembamba, siyo mrefu sana saizi ya kati alikuwa amevaa suruali rangi ya blue iliyopauka na T-Shirt rangi ya dark blue na kofia nyeupe yenye alama nyekundu ili tuweze kumkamata na kumfikisha mahakamani.
  Imetolewa na: 
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma 
  Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi - Misime D.A (SACP)

  0 0  0 0

   Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii

  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imezuia maandamano ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya Ilala (UVCCM) ya kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa chama hicho pamoja na kuacha kiporo  maandamano ya Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha).


  Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ,Kamishina wa Jeshi la Polisi ,Suleiman Kova ,amesema kuzuia kwa maandamano hayo inatokana na kuwepo kwa taarifa za Kiintelejensia za kuvuruga amani.


  Kova amesema maandamano ya UVCCM Wilaya ya Ilala yalitakiwa kufanyika kesho lakini kutokana na kuwepo kwa taarifa za kiintelejensia za Machinga ,Bodaboda ,Mama Lishe na Baba Lishe kushiriki maandamano na kufikisha malalamiko yaokupitia maandamano hayo.


  Amesema kumekuwepo kwa taarifa katika mitandao ya jamii wakihamasishana bodaboda na machinga ,mama lishe na baba lishe kushiriki maandamano pamoja na kutoa ujumbe wao kwa kupitia maandamano katika Mkoa wa Dar es Salaam.


  Kova amesema machinga ,Mama lishe,Baba,na Bodaboda watumie taratibu zingine za  kufikisha ujumbe kutokana na sheria zilizowekwa na sio kutumia mgongo katika vyama vya siasa.


  Kwa upande  Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) maandamano yao yalikuwa yanahusu kwenda tume ya Taifa ya Uchaguzi ni lini itaanza kuandikisha daftari la wapiga kura ,pamoja na wanafunzi watashiriki vipi upigaji kura ambapo Kamanda Kova amesema hilo wanaweka kiporo kwanza wanafanya uchunguzi wa taarifa mbalimbali.


  “Sisi tunachoangalia amani kwani maandamano ya amani yanaweza kufanyika lakini mwisho wa siku inakuwa sio amani kwa jeshi la polisi tunawajibu kuangalia hilo”amesema Kamanda Kova.

  0 0
 • 02/04/15--07:01: KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO
 •  Waziri wa Mambo ya Ndani,Mhe. Mathias Chikawe (kulia) akiwa ameongozana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu (katikati) na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,CGP John Minja wakati wakitoka katika ukumbi wa Bunge kujadili ripoti ya kamati ya Ulinzi na Usalama iliyowasilishwa Bungeni leo.
   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu (kulia) alijadiliana jambo na Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo.Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani,Mhe. Mathias Chikawe.
  Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Adam Malima akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu walipokutana nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo.Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani,Mhe. Mathias Chikawe.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  DSC_0100 

  Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (Katikati) akifafanua jambo kwenye mkutano na wanahabari (hawapo pichani), wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa king'amuziki kipya cha DStv HD leo jijini Dar. Kulia ni kwake ni Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo na kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog)

  Na Andrew Chale
  KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania wasambazaji wa ving’amuzi vya DStv, leo imezindua king’amuzi kipya cha DStv HD ambacho kitaanza kutumika kwa mara ya kwanza hapa Nchini. Akizungumza na wandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo, akielezea umuhimu wa huduma hizo alisema king’amuzi hicho kina ubora wa hali ya juu ikiwemo kuonyesha picha zenye ubora mzuri zaidi.

  Pia alieleza kuwa, DStv HD mteja atapata kuona picha zenye mvuto zaidi pamoja na kiwango cha juu cha sauti Dolby Digital 5.1. “Wateja wa DStv watafurahia ving’amuzi hivi kwa ubora wa hali ya juu hivyo ni wakati wa kuchangamkia ofa kwani ndio mara ya kwanza kuingia kwa Tanzania” alisema Ronald Shelukindo.
  DSC_0239
  Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akielezea ubora wa king'amuzi hicho cha DStv HD wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari leo jijini Dar.

  Ronald Shelukindo akielezea kwa kina, alisema DStv HD, mteja anaweza kufurahia vipindi mbalimbali ikiwemo mifumo na mipangilio ya kila vipindi kwa kupendekeza atazame kipi gani, muda gani na wakati gani?.

  King’amuzi cha “DStv HD, mteja anaweza kujipangia atazame kipindi gani ama kwa wakati autakao yeye, ambapo anachoweza ni kuseti hicho kipindi akipendacho na kisha anaweza kukiangalia kwa wakati wake, hata kama muda umepita kwa wakati huo kinarushwa kwenye chaneli husika” alifafanua Ronald Shelukindo.

  Kwa upande wake, Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu aliwahimiza watanzania kuchangamkia vinga’muzi hivyo vya DStv HD, ambavyo kwa sasa vipo karibu maduka yote ya Mawakala wa DStv, kwa bei rahisi kabisa vikiwa vinapatikana kwa sh 99,000/ kwa mteja mpya huku kwa wateja walio na ving’amuzi vya zamani vya DStv watakaotaka kubadilishiwa, watalipia sh 39,000/ tu.
  DSC_0140
  Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionesha king'amuzi kipya cha DStv HD kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).

  0 0  0 0

  Mshindi wa Milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Uwezo Magedenge ambaye ni mkazi wa Kilolo mkoani Iringa(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa hafla maalum ya kukabidhiwa kitita chake,Wengine katika picha Mkuu wa Idara ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Brigitta Stephen(kushoto) na Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Dar es Salaam,Selie Mlay.Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
  Mkuu wa Idara ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Brigitta Stephen(kushoto) na Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Dar es Salaam,Selie Mlay(kulia)wakimshuhudia Mshindi wa Milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Uwezo Magedenge ambaye ni mkazi wa Kilolo mkoani Iringa,akiowanyesha waandishi wa habari mamilioni yake aliyojishindia kupitia promosheni hiyo. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.


  0 0  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kulia akihutubia katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini Mkoni Rukwa leo tarehe 04/02/2015 katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga. Kaulimbiu ya maaadhimisho hayo ikiwa "Fursa ya kupata haki: Wajibu wa Serikali, Mahakama na Wadau". Katika hotuba yake hiyo alisema ipo haja kubwa kwa Serikali kubadili sheria zake ili lugha ya mahakamani na hukumu ziandikwe kwa kiswahili. Kwa upande wa wananchi aliwaasa kujiepusha na tabia ya kujichukulia sheria mkononi ili kudumisha amani nchini.
  Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. Jaji Sambo akipokea gwaride la heshima kutoka kwa kikosi cha Jeshi la Polisi wakati wa maadhimisho ya siku ya Sheria Mkoani Rukwa leo tarehe 04/02/2015.
  Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. Jaji Sambo katikati akisoma hotuba yake ya maadhimisho ya siku ya sheria Mkoani Rukwa ambapo aliwataka mahakimu wote Mkoani Rukwa kutimiza majukumu yao ipasavyo kwa mujibu miongozo ya mahakama ili kusaidia uharakishwaji wa utoaji haki kwa wananchi kwa wakati. Aliwaeleza pia wadau wote wa sheria wakiwepo mawakili wa kujitegemea kuwa mashauri yote ya kesi yatakua yakisimamiwa na kutolewa maamuzi na mahakama na sio mawakili kutaka kuingilia utendaji wa mahakama.
  Baadhi ya wadau na viongozi wa Sheria na Serikali katika meza kuu.
  Sehemu ya mahakimu, mawakili, wanasheria na wageni waalikwa katika maadhimisho hayo.
  (Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa@rukwareview.blogspot.com)

  0 0

  Baadhi ya washindi wa program ya Ndovu Golden Experience iliyokuwa ikiendeshwa na TBL kupitia bia yake ya Ndovu wakirejea jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzulu katika hifadhi ya Selous kwa siku mbili mwishoni mwa wiki.
  Baadhi ya washindi wa program ya Ndovu Golden Experience iliyokuwa ikiendeshwa na TBL kupitia bia yake ya Ndovu wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Kampi ya Lake Manze(katikati) walipokwenda kujionea vivutio mbalimbali katika mbuga hiyo mwishoni mwa wiki.
  Meneja wa Kambi ya Lake Manze akiwaelekeza jambo washindi wa wa program ya Ndovu Golden Experience iliyokuwa ikiendeshwa na TBL kupitia bia yake ya Ndovu walipokwenda kujionea vivutio mbalimbali katika mbuga hiyo mwishoni mwa wiki.

  0 0

  Rais Prof. Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akitoa salamu zake kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria kilichofanyika leo kwenye viwanja vya Mahakama vilivyopo kwenye mtaa wa Chimala,Jijini Dar es salaam.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
  Jaji Mkuu wa Tanzania,Mh. Mohamed Chande Othman akitoa hotuba yake katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria kilichofanyika leo kwenye viwanja vya Mahakama vilivyopo kwenye mtaa wa Chimala,Jijini Dar es salaam.


  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) akiwakaribisha ofisini kwake  Mkuu wa Taasisi ya Ujerumani iitwayo Hanns Seidel Foundation  kwa Afrika na ukanda wa Sahara Bw. Claus Liepert (wa pili kushoto) pamja na mwakilishi mkazi wa taasisi hiyo hapa Tanzania Bi. Julia Gabler (wa kwanza kushoto).

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) akiwa katika mazungumzo na wawakilishi wa Taasisi ya Hanns Seidel Foundation Bi.  Julia Gabler (wa kwanza kulia) na Bw. Claus Liepert (wa pili kulia).

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na ujumbe wa Taasisi ya Hanns Seidel Foundation ulioongozwa na Mkuu wa Afrika na Kanda ya Sahara  Bw. Claus Liepert.

   Mkuu wa Taasisi ya Hanns Seidel Foundation  kwa Afrika na kanda ya Sahara Bw. Claus Liepert akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma. 
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) akiagana na ujumbe kutoka Taasisi ya Hanns Seidel Foundation ulioongozwa na Bw. Claus Liepert (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake.  0 0


  0 0


  0 0

  Wapo Watanzania ambao ndoto zao ni kumiliki shule. Ninapoongelea shule simaanishi lazima  yawe yale mashule makubwa. Hata shule za awali ambazo zinaanzishwa na wajasiriamali wadogo mitaani nazo ni shule kwa  maana hii katika makala haya.

  Nyaraka kuu inayoongoza  taratibu za usajili wa shule binafsi huitwa fomu namba RS8. Huu ndio mwongozo mkuu wa usajili. 
  Kuna mambo ya msingi na ya kisheria ambayo  mtu hutakiwa kujiandaa nayo iwapo  anataka kuanzisha shule binafsi.
  Mambo haya huwa yanakamilishwa kwa wepesi na bila usumbufu  ikiwa yanapitia kwa wanasheria lakini pia mtu anaweza kufanya mwenyewe isipokuwa  hata   akifanya mwenyewe kuna document  za lazima ambazo lazima zisainiwe na kuthibitishwa na mwanasheria.

older | 1 | .... | 728 | 729 | (Page 730) | 731 | 732 | .... | 3272 | newer