Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 727 | 728 | (Page 729) | 730 | 731 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Ulikuwa ni usiku wa manane majira ya saa nane na nusu, ambapo Mzee Jengo alikuwa amepumzika kitandani akiwa na mtoto wake wa kiume ambaye alikuwa anaitwa Rony.
  Alikuwa ni kijana mdogo mwenye umri  kati ya miaka nane au tisa, Usiku huo hali ya Mzee Jengo ilikuwa si nzuri kwani alianza kujisikia vibaya ghafla kiasi kwamba hata alipojaribu kunyanyuka alishindwa. Kutokana na maumivu makali aliyokuwa akiyasikia aliamua kumuamsha mtoto wake, taratibu alinyoosha mkono na kuanza kumvuta Ronyhuku akizungumza kwa sauti ya unyonge sana.   “Rony, Rony …..aaaaa…amka ukamwambie ….dada mimi naumwa, Rony mwanangu nenda kamwite dada yako najisikia vibaya sana” Alikuwa akizungumza kwa shida sana, lakini Rony alimsikia, na kwa haraka aliamka huku akiwa anafikicha macho yake kutokana na kushtuka kutoka usingizini, alimtizama baba yake, na moja kwa moja alishuka kutoka kitandani huku akiwa anamuuliza Baba yake, “Baba unaumwa nini,  nani atakupeleka hospitali Baba,”.   0 0

  Baadhi ya bidhaa zilizoteketezwa na Maofisa wakaguzi wa TFDA wilayani Sikonge.
  Maofisa wakaguzi wa TFDA kanda ya kati wakijiandaa kuteketeza bidhaa zilizoisha mda wake ikiwemo vinywaji wilayani Sikonge (picha na Allan Ntana).

  Na Allan Ntana, Sikonge

  MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati imefanikiwa kukamata na kuteketeza bidhaa mbalimbali za chakula, vinywaji, dawa za binadamu na mifugo, vipodozi na vifaa tiba vilivyoisha muda wake na vingine feki vyenye thamani ya zaidi ya sh mil.5 katika halmashauri ya wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.

  Akisoma taarifa ya ukaguzi mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo hapo juzi Afisa Mkaguzi wa Chakula Kanda ya Kati Sifa Chamgenzi alisema ukaguzi huo ulilenga kuangalia ubora na usalama wa dawa za binadamu na mifugo, uwepo wa vipodozi vilivyopigwa marufuku na bidhaa zingine zilizoisha muda wake wa matumizi. 

  Alisema lengo la TFDA ni kufuatilia utekelezaji wa sheria na.1 ya mwaka 2003 ya chakula, dawa na vipodozi kwa wauzaji na wasindikaji wa vyakula na dawa na kuongeza kuwa zoezi hili lililenga kutekeleza mpango kazi wa Mamlaka hiyo wa kufuatilia ubora na usalama wa bidhaa hizo kwa mtumiaji.


  0 0

  Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa(katikati)akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni (hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa Promosheni ya JayMillions,Wengine katika picha kushoto ni Balozi wa Promosheni hiyo Hilary Daud”Zembwela” na kulia ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.

  Uwezo Magendege, 22, ni mshindi wa kwanza wa zawadi nono ya siku ya pesa taslimu Sh. 100m/- za promosheni iliyozinduliwa siku 19 zilizopita na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.

  Hadi kufikia leo ni Sh. 126m/- pekee zilizokwisha kuchukuliwa na Uwezo, washindi wengine wawili – Hyness Petro Kanumba from Rukwa and James Mangu (Mwanza) – wa Sh. 10m/- na sita – Chiliphod Wanjala (Mwanza), Janeth Ngannyange (Njombe), Evarista A (Mwanza), Stanley Bagashe (Shinyanga), Ramadhani H. Maulid (Dodoma) and  Lucas M (Shinyanga) – wa Sh. 1m/-. Kiasi cha zaidi ya Sh. 5bn/- (ambazo ni sawasawa na magari madogo 428 ya muundo wa mgongo wa kobe) zingeweza kunyakuliwa na wateja iwapo wangetuma neno “JAY” kwenda 15544 kucheki kama wameshinda.

  Uwezo ni mkazi wa wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa. Mnamo Alhamis Januari 29, 2015, Uwezo alipokea simu ambayo ilipelekea maisha yake kubadilika milele alipotaarifiwa kuwa amejishindia Sh. 100m/- kutoka katika mamilioni ya shilingi yanayogawiwa kupitia promosheni ya JayMillions ya Vodacom Tanzania kwa siku hiyo.


  0 0

  Wanachama  wa  kikundo cha  VICOBA cha  Lukindo woman Group wakimvisha  mavazi ya uchif mbunge wa  jimbo la kalenga Bw Godfrey Mgimwa baada ya  kufurahishwa na jitihada zake  jimboni  humo
  Wanachama  wa  VICOBA  Tanangozi  Kalenga  wakimshangilia mbunge  wa  jimbo la kalenga Godfrey Mgimwa
  Mbunge wa   jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa katikati akipokelewa kijiji cha Tanangozi wakati  wa harambee ya  kuchangia VICOBA.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Ofisa Mkuu kutoka taasisi ya Uandishi wa Habari na Utangazaji EABMT Rosemary Mwakitwange akifafanua jambo katika Mdahalo juu ya uchaguzi mkuu ujao kuhakikisha haki na amani inatawala,mdahalo huo ulishirikisha wanasiasa kutoka vyama vya siasa CHADEMA,CCM,CUF,NCCR na vingine pamoja na taasisi binafsi na viongozi wa kiserikali,mdahalo huo umeandaliwa na shirika la TWAWEZA umefanyika jana jijini Arusha.
  Washiriki wa Mdahalo juu ya uchaguzi mkuu ujao kuhakikisha haki na amani inatawala wakifuatilia kwa makini mdahalo huo ulishirikisha wanasiasa kutoka vyama vya siasa CHADEMA,CCM,CUF,NCCR na vingine pamoja na taasisi binafsi na viongozi wa kiserikali,mdahalo huo umeandaliwa na shirika la TWAWEZA umefanyika jana jijini Arusha.Picha na Mahmoud Ahmad.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Maria Bilia akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya wadadisi 200 wa Sensa ya Viwanda itayofanyika nchi nzima mwezi huu. Mafunzo hayo yanafanyika chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo eneo la Changanyikeni jijini Dar es salaam.
  Mkuu wa chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo eneo la Changanyikeni jijini Dar es salaam Prof.Ngalinda Innocent akizungumza na wadadisi watakaokusanya takwimu za Sensa ya Viwanda mwezi huu wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku 14.
  Mkuu wa chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof. Ngalinda Innocent akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi. Maria Bilia (katikati) na Kamishna wa Sensa ya Watu na Makzi Bi. Hajjat Amina Mrsiho Said leo jijini Dar es salaam.


  0 0
 • 02/03/15--06:28: UJUMBE


 • 0 0  0 0

   Naibu Waziri wa Madini wa Wizara ya Nishati na Madini,Charle’s  Kitwanga akizungumza leo jijini Dar es Salaam  na wafanyabiashara wa Ujerumani wakitaka kujua fursa za uwekezaji katika sekta ya Nishati na Madini.


   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Ndosi Mwihava akitoa maelezo kwa wafanyabiashara wa Ujerumani wakitaka kujua mazingira ya uwekezaji katika sekta ya nishati na Madini walipotembelea wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
   Kiongozi wa Wafanyabiashara wa Ujerumani Mathias Maching akizungumza leo jijini Dar es Salaam juu ya msafara wao katika kujua mazingira ya uwekezaji katika sekta ya Nishati na Madini.

  0 0

   Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhandishi Athumani Mfutakamba akisoma taarifa ya kamati hiyo kwa niaba ya mwenyekiti wa kamati hiyo bungeni mjini Dodoma.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Jasson Rweikiza akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge yaMasuala ya Ukimwi Lediana Mng'ong'o akiwasilisha taarifa ya kamati yake.
   Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiuliza swali wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma.
   Baadhi ya wageni waliofika kwenye Bunge la Jamhuri wakifuatilia Bunge.
   Baadhi ya wabunge wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya wabunge nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma akiwemo Mbunge wa Morogoro Kusini Dkt. Lucy Nkya (kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Jasson Rweikiza.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mhe. Kapt (Mstaafu) George Mkuchika (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wabunge kwenye mlango wa Bunge mjini Dodoma.Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO,Dodoma

  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, akijibu hoja za kamati na wabunge mjini Dodoma.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akijibu hoja Bungeni kuhusu wizara yake.
  Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe akijibu hoja za kamati hoja za kamati.
  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Said Nkumba akiwasilisha taarifa ya kamati yake. Picha na Hussein Makame-MAELEZO,Dodoma.

  Hussein Makame-MAELEZO,Dodoma

  WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema Serikali itahakikisha inapambana na watu wote wanaoendesha vitendo vya dhuluma, matapeli na wanaonyang’anya viwanja, majengo, mashamba na ardhi za wanyonge.

  Waziri Lukuvi ametangaza azma hiyo wakati akijibu baadhi ya hoja za wabunge waliochangia Taarifa ya Kamati ya Bunge, ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyowasilishwa na kupitishwa Bungeni mjini Dodoma.

  Alisema anatambua kwamba hasa maeneo ya mijini kuna dhuluma nyingi zinafanyika ambapo masikini, mayatima na wajane wanadhulumiwa na kunyang’anywa ardhi na majengo yao.


  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank, Balozi Salome Sijaona (Katikati) akikabidhi kadi ya Bima ya Matibabu kwa Zaituni Zoro, ambae ni miongoni mwa wateja wa kwanza wa Huduma mpya ya Bima ya Matibabu ambayo zinawawezesha wateja wa Benki hiyo kupata Bima ya Matibahu kwa Shilingi 1000 kwa siku na kuweza kutibiwa hospitali Binafsi na za serikali pamoja na kununua dawa. Wanaoshuhudia (Kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja na Meneja Uendeshaji wa AAR. Majula Manyama.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank, Balozi Salome Sijaona (Katikati) akikabidhi kadi ya Bima ya Matibabu kwa Mary Temu, ambae ni miongoni mwa wateja wa kwanza wa Huduma mpya ya Bima ya Matibabu ambayo zinawawezesha wateja wa Benki hiyo kupata Bima ya Matibahu kwa Shilingi 1000 kwa siku na kuweza kutibiwa hospitali Binafsi na za serikali pamoja na kununua dawa. Wanaoshuhudia (Kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja na Meneja Uendeshaji wa AAR. Majula Manyama.


  0 0
 • 02/03/15--09:42: SAMAKI WA LEO LEO
 • Wakina mama wajasiliamali katika soko la Darajani,Mjini Unguja wakipanga samaki tayari kwa kuwauza kwa wateja sokoni hapo.

  0 0

  Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha mgeni wake Ikulu Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck ambaye ameongozana na mke wake Bibi schadt leo.
  Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete akimtambusha Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa waliojitokeza kumpekea leo tarehe.03.02.2015 katika viwanja vya Ikulu.
  Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mgeni wake Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck wakipata mapokezi kwa kuimbwa kwa nyimbo za taifa za mataifa hayo mawili.
  Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na kikosi cha jeshi la wananchi wa Tanzania kwa ajili yake leo katika viwanja vya Ikulu.  0 0
 • 02/04/15--01:29: BEI YA MADAFU LEO


 • 0 0

  Katibu Mkuu wa Divisheni ya Afrika Mashariki na kati wa Kanisa la Waadiventista Wasabato, Dkt. Nathaniel Walemba, akifungua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la kanisa la Waadiventista Wasabato Kigamboni jana mchana, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya extra vaganza yanayoendelea katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Divisheni ya Afrika Mashariki na kati wa Kanisa la Waadiventista Wasabato, Dkt. Nathaniel Walemba, (wa nne kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Kanisa la Wasabato kigamboni, wazee wa kanisa hilo na baadhi ya washiriki wa kanisa hilo, jana mchana mara baada ya kuweka jiwe la msingi. Wa nne kutoka kulia ni Katibu wa Union ya Kusini Mwa Tanzania, Mchungaji James Machage.

  Vijana wa Chama cha Watafuta Njia(PF), kutoka kanisa la Waadiventista Wasabato Kigamboni, wakimvalisha Skafu Mwenyekti wa Konference ya Kusini Mwa Tanzania, Mchungaji Mark Marekana (wa pili kutoka kulia), kabla ya kuweka jiwe la msingi katika kanisa la waadventista wasabato Kigamboni,jana mchana.


  Picha na Lisso Ibrahim Biseko    Katibu Mkuu wa Unioni ya Kaskazini mwa Tanzania, Mchungaji Davis Fue, akiangalia ramani ya jengo la kanisa la Waadventista Wasabato litakavyokuwa mara baada ya kumalizika, wakati wa uwekaji jiwe la msingi la kanisa hilo jana mchana, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Extra Vaganza, ambayo yanafanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
   Kwaya ya Kanisa la Waadventista Wasabato Kigamboni, wakiimba kabla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kanisa la Waadventista Wasabato Kigamboni. Jiwe hilo la msingi liliwekwa jana na Katibu Mkuu wa Divisheni ya Afrika Mashariki na kati wa Kanisa la Waadiventista Wasabato, Dkt. Nathaniel Walemba kwa niaba ya Mwenyekiti wa Divisheni ya Afrika Mashariki na kati wa Kanisa la Waadiventista Wasabato, Mchungaji, Dkt. Blasious Ruguri.

  0 0

   WADAU wa sanaa ndani na nje ya mkoa wa Mbeya wameombwa kutoa ushirikiano kwa wasanii wa filamu mkoani hapa kwa kununua kazi zinazofanywa na kuacha kasumba kuwa filamu bora zinaweza kutengenezwa na wasanii walioko Dra es salaam pekee.

  Mwongozaji wa filamu wa kampuni ya Pritauj Filim Prince Hekela alitoa rai hiyo jana alipokuwa akitambulisha Filamu mpya ya Vanilla iliyochezwa na wasanii kutoka mkoani Mbeya.


  Prince Hekela alisema kumekuwa na kasumba ya baadhi ya wadau kuamini filamu nzuri ni zile zinazochezwa na wasanii wa Dar es salaam jambo alilosema limekuwa likididimiza sana wasanii wa mikoani.


  Alisema ni wakati kwa wadau hao kutambua kuwa ubora wa filamu hautokanani na mahali anakofanyia kazi zake msanii,bali umakini na maandalizo bora ndiyo msingi wa kutengenezwa kwa filamu bora.


  Akizungumzia filamu ya Vanila aliyosema tayari imeingizwa sokoni,alisema imeandaliwa katika mazingira yenye kuzingatia staha hivyo haina vipande vyenye kuonesha aibu kiasi cha familia kushindwa kuitazama kwa pamoja.


  “Vanilla ni filamu ambayo hata ukienda kuonesha uwanjani hakuna kinachozuia.Kwa nyumbani hata awepo baba mama na watoto wanaweza kuiangalia kwa pamoja.Na ina mafundisho ya kila mtu kulinagana na umri wake”


  “Muhimu pia wadau watambue kuwa tumejipanga kuhakikisha tunaleta burudani nzuri kutokana na filamu zetu.Ndiyo sababu hata katika Vanila utaona tumechanganya wasanii wapya na wa zamani.Wasanii wapya ambao wamefanya vizuri sana katika filamu hii ni pamoja na Issa Ngoda,Regina Mwinyi, Kelvin Kaziyandege na Joachim Nyambo.Lakini pia tumemshirikisha mwanadada Riyama Ally ambaye ni mkongwe katika sanaa” alisisitiza Hekela.


  Kwa upande wake mmoja wa wasanii waliocheza filamu ya Vanila Joachim Nyambo alisisitiza kuwa filamu hiyo imekuja kuwadhihirishia wadau kuwa kazi nzuri ya sanaa inaweza pia kufanyika mikoani.


  Nyambo aliwasihi wadau kuendelea kushirikiana na wasanii mikoani wanaoonekana kukuza sanaa kwa kuwa michango ya hali na mali ili kuwezesha kukua kwa sanaa. 

  0 0  0 0

  IMG-20150203-WA0039
  Waziri wa maji profesa jumanne maghembe akielezea utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa BRN chini.
  ....................................................

  Waziri wa maji kupitia mpango wa BRN,kuanzia mwaka 2013 hadi sasa,imefanikiwa kuwafikishia maji wananchi milioni 4.3 wanaoishi maeneo ya mijini Aidha zaidi ya watu milioni 2 wanaoishi maeneo ya vijijini wamepatiwa huduma ya maji kupitia BRN.

  Waziri wa maji profesa jumanne maghembe ameyasema hayo Februari 3, 2015 mjini Dodoma alipokuwa akizungumzia utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa BRN chini ya wizara ya maji katika ukumbi wa Fr.Vicent uliyopo ndani ya hotel ya St.Gasper

  Profesa Maghembe amesema kuwa,mpango huo wa BRN umeonyesha kwa muda mfupi tofauti na ule mpango wa Taifa wa maji uliyonza mwaka 2017 hadi mwaka 2014,Amesema serikali kupitia mpango wa BRN itahakikisha inawafikishia wananchi maji katika maeneo mbali mbali ili kuwapunguzia kero ya maji.

  Kadhalika Maghembe amewataka wafanyakazi wa mamlaka za maji hapa nchini kufanya kazi kwa kasi kubwa na sio mazowea,Katika mkutano huo viongozi wa mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira za miji mikuu ya mikoa zimetia saini makubaliano ya miradi ya maji na mazingira kwa kutumia utaratibu wa BRN

older | 1 | .... | 727 | 728 | (Page 729) | 730 | 731 | .... | 3278 | newer