Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

DC Temeke aipongeza shule ya Twayyaibat kwa ada nafuu

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKUU wa wilaya Temeke, DC Sophia Mjema, ameipongeza shule ya Sekondari ya Kiislamu inayojulikana kama Twayyaibat Islamic Seminary Secondary School kwa kufanya ada nafuu inayoweza kuwafanya wazazi na walezi wamudu gharama za kusomesha watoto kwenye shule binafsi.

mwanafunzi kutoka Twayyibat Islamic Seminari akisoma Quraan katika shule hiyo walipotembelewa na Mkuu wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, hayupo pichani.

DC Mjema aliyasema hayo alipofanya ziara katika shule hiyo na kukuta uongozi wa Twayyaibat, ukitoa ada ya Sh 200,000 tu kwa mwaka, jambo ambalo ni agharabu mno hususan kwa shule za kulipia na zinazomilikiwa na taasisi za kidini.

Akizungumza kwa mshangao mkubwa mbele ya wadau wa elimu, DC Mjema alisema ameshangazwa na shule hiyo kufanya ada nafuu, hivyo ni jukumu la wazazi na walezi kujitokeza kuwasomesha watoto wao kwa nguvu zote.

Mkuu wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, kulia akimkabidhi cheti Mr Yakubu kwa kutambua mchango wake kwa maendeleo ya shule ya Twayyibat Islamic Seminary, iliyopo Temeke, jijini Dar es Salaam jana.


RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS UFARANSA FRANCOIS HOLLANDE JIJINI PARIS

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Ikulu ya Ufaransa maarufu kama Champs L’Elysee jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015 kuonana na mwenyeji wake Rais Francois Hollande.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mwenyeji wake Rais Francois Hollande katika Ikulu ya Ufaransa maarufu kama Champs L’Elysee jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake kuonana na mwenyeji wake Rais Francois Hollande Ikulu ya Ufaransa maarufu kama Champs L’Elysee jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015 kuonana na mwenyeji wake Rais Francois Hollande. PICHA NA IKULU

SAUTI ZA BUSARA WAMTANGAZA WAMTAMBULISHA RASMI ALI KIBA

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi wa Busara Promotions, wandaaji wa tamasha la Sauti za Busara, Simai Mohammed (katikati) akiongea na wandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wanahabari Jijini Dar es Salaam, juu ya tamasha la 12 la Sauti za Busara, litakalofanyika, Februari 12 hadi 15, mwaka huu, Ngome Kongwe, Zanzibar. Wengine (kushoto) ni Meneja wa tamasha hilo, Journey Ramadhani. na upande wa kulia ni Mkurugenzi wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud 'Dj Yusuf, akifuatiwa na msanii wa bongo fleva nchini, Ali Kiba (kulia).
Ali Kiba katika pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotions, Simai Mohammed, muda mfupi baada ya utambulisho wa msanii huyo juu ya kupiga shoo kwenye tamasha la 12 la Sauti za Busara, litakalofanyika Februari 12 hadi 15, Zanzibar.
Simai, Dj Yusuf na Kiba wakiwa wameunganisha mikono kwa kusalimiana ikiwa ni ishara ya Umoja na Amani, kama Kauli mbiu ya mwaka huu ya tamasha hilo inavyohimiza amani.

Evaluation of IFAD programme in Tanzania points to major strides but also areas for improvement

$
0
0
Targeted investments in Tanzanian agriculture contributed to increasing yields for crops such as paddy, maize, or tomato in a range of 60 to 120 per cent in those areas where irrigation and extension activities were carried out at a substantial level, a new country programme evaluation by the Independent Office of Evaluation of the International Fund for Agricultural Development (IFAD), presented today in Dar es Salaam, reveals.

Tanzania has the second-largest IFAD portfolio (in terms of volume of lending) in the East and Southern Africa region, after Ethiopia. Since the beginning of IFAD's operations in the country in 1978, IFAD has financed 14 loan-funded investment projects of US$360 million, and has mobilized more than US$700 million in support to agricultural development projects. 

The government has provided cofinancing of US$72 million, or about 10 per cent of total portfolio costs. Additional contributions were provided by other donors, notably the African Development Bank, the World Bank and the governments of Belgium, Japan and Ireland.

The evaluation recommended that IFAD support the next phase of the Agricultural Sector Development Programme – a governmental programme that aims to improve farmers' access to and use of agricultural knowledge, technologies, marketing systems and infrastructure, in Mainland and Zanzibar.READ MORE HERE

FNB KATIKA MAONESHO YA ZANA ZA KILIMO 'AGRI BUSINESS EAST AFRICA' JIJINI DAR

$
0
0
Meneja wa Biashara na Masoko wa Benki ya First National Bank (FNB), Adam Yusuf (aliyesimama ndani ya banda) akiwaeleza wateja namna benki hiyo inavyojitahidi siku hadi kukidhi matakwa ya wateja wake, ambapo kwa sasa imeongeza matawi na huduma za ATM, katika muktadha wa retail, SME, Comercial and Corporate Banking, Visa Debit Cards, InContact Mesaging, Online and Cellphone Banking, katika maonesho ya zana za kilimo maarufu kama ‘Agri Business East Africa’ yanayoendelea hotel ya serena Dar es Salaam.

Naibu Waziri Kitwanga afungua semina kuhusu matumizi ya gesi asilia nchini

$
0
0
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga akifungua rasmi semina kuhusu matumizi ya gesi asilia iliyofanyika hivi karibuni katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Japan Tanzania, Masaki Okada akizungumza na wadau na wataalamu wa gesi asilia (hawapo pichani) waliohudhuria semina ya matumizi ya gesi asilia iliyofanyika hivi karibuni katika Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam.
Wataalamu na wadau wa gesi asilia kutoka Japan na Tanzania wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya matumizi ya gesi asilia iliyofanyika hivi karibuni katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje amwakilisha Rais Kikwete kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa NEPAD

$
0
0
Meza Kuu wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa NEPAD uliofanyika leo jijini Addis Ababa. Wakuu wa Nchi pamoja na mambo mengine walisomewa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya NEPAD kwa kipindi cha mwaka 2014. Kubwa lilihusu uanzishwaji wa Mpango wa Kilimo unaozingatia mabadiliko ya tabianchi ambao unawalenga wakulima wadogo zaidi ya milioni 25 watakaokuwa wanalima kwa kutumia teknolojia isiyokuwa na athari katika tabianchi ifikapo mwaka 2025.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Makamishna wa Jeshi la Polisi waifagilia NMB Wakala

$
0
0
Makamishna wa Jeshi la Polisi wanaohudhuria mkutano wa mwaka wa maofisa waandamizi wa jeshi la polisi mjini Dodoma wamefurahishwa na matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma za kifedha.

Makamishna wengi waliofika kwenye banda maalumu la NMB lililopo nje ya ukumbi wa mikutano wa St.Gasper mjini Dodoma ambapo kikao cha mwaka cha maafisa wa polisi kinaendelea, walifurahishwa na uharaka wa kutoa na kuweka fedha kupitia NMB wakala ambapo kupitia teknolojia ya Max Malipo, mteja anaweza kutoa na kuweka fedha na pia kupata huduma zingine za kibenki ambazo angeweza kuzipata katika tawi lolote la NMB.

Wajumbe wa mkutano huo wa polisi walifarijika kuona kuwa siyo lazima kwenda kwenye matawi ya NMB ili kupata huduma za kutoa na kuweka fedha na kufagilia kuwa huduma hizo zilizowekwa nje ya ukumbi wa mkutano zimewapunguzia adha ya kwenda mjini kutafuta huduma za kifedha.
Makamishna wa Jeshi la Polisi,Paul Chagonja na Thobias Andengeye wakijaziwa form maalumu itakayowaruhusu kupata taarifa fupi za akaunti zao za NMB kupitia mtandao wa E-mail kutoka kwa Meneja Mwandamizi katika kitengo cha wateja binafsi,Suzan Shuma huku Daudi Sanga kutoka NMB Dodoma kitengo cha Chap Chap Instant Account akijiandaa kutoa maelezo juu ya huduma ya kufungua akaunti ya chap chap.
Meneja Mwandamizi katika kitengo cha wateja binafsi,Suzan Shuma akimjazia Kamishna wa Polisi kutoka makao makuu ya jeshi la Polisi,Paul Chagonja fomu itakayomruhusu kupata taarifa fupi za akaunti yake ya NMB kupitia mtandao wa E-mail (E-statement).

Jinsi matajiri wanavyotajirika zaidi, na masikini wanavyokuwa fukara zaidi

KATIBU MKUU WA CCM,KOMREDI KINANA AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU 15 KISIWANI UNGUJA NA PEMBA LEO.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Vuai Ali Vuai wakielekea kushiriki upandaji wa mboga mboga na kutia mbolea katika shamba la Wajasiliamali lenye ekari nne na nusu la ushirika wa Jambo Group Cooperative Society,lenye jumla ya washirika wapatao 15,katika kijiji cha Wambaa Kwaanzani,wilaya ya Mkoani ,Kusini Pemba.


Kinana amemaliza ziara ya siku 15 katika visiwa vya Unguja na Pemba Zanzibar ambapo amekagua na kushiriki ujenzi katika miradi 40 mikoa 12. 

Katika ziara hiyo,Ndugu Kinana alijionea mafanikio makubwa ya kimaendeleo yaliyofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais Dk. Ali Mohamed Shein, zikiwemo barabara, hospitali, elimu na maji pamoja na kusambazwa umeme karibu kila kona. 

Katika ziara hiyo ,Ndugu Kinana amewataka viongozi wa dini na Serikali kukemea kitendo cha CUF kuwaita wanaohamia CCM makafiri. Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alimpongeza Ndugu Kinana kwa ziara yake, kwamba imekuwa ya mafanikio makubwa na imewapa somo na moyo wa kuimarisha chama visiwani.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki upandaji wa mboga mboga na kutia mbolea katika shamba la Wajasiliamali lenye ekari nne na nusu la ushirika wa Jambo Group Cooperative Society,lenye jumla ya washirika wapatao 15,katika kijiji cha Wambaa Kwaanzani,wilaya ya Mkoani ,Kusini Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki upandaji Migomba katika shamba la Ushirika  la Utandawazi Cooperative Society katika kijiji cha Chokocho,jimbo la Mkanyageni,wilaya ya Mkoani,Kusini Pemba.Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na mmoja wa viongozi wa Ushirika huo alieleza mbele ya Kinana kuwa Ushirika huo una jumla ya watu 25,na wanajishughulisha na ufugaji wa Kuku wa Kienyeji,Mboga mboga pamoja na Migomba katika shamba lenye ekari mbili na nusu.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akitoka kushiriki upandaji wa Mboga mboga na kutia mbolea katika shamba la Wajasiliamali lenye ekari nne na nusu la ushirika wa Jambo Group Cooperative Society,lenye jumla ya washirika wapatao 15.

Baadhi ya wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM<ndgu Kinana alipokuwa akiwahutubia leo katika uwanja wa mpira wa Mjimbini,wilaya ya Mkoani,Kusini Pemba.Ndugu Kinana amehitimisha ziara yake ya siku 15 ndani ya Kisiwa cha Pemba  jioni ya leo,Kuhimiza na kukagua uhai wa chama cha CCM.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza mbele ya Wananchi na wafuasi wa chama cha CCM,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika uwanja wa mpira wa Mjimbini,wilaya ya Mkoani,Kusini Pemba.Ndugu Kinana amehitimisha ziara yake ya siku 15 ndani ya Kisiwa cha Unguja na Pemba  jioni ya leo,ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.

PICHA NA MICHUZI JR-WILAYA YA MKOANI KUSINI PEMBA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Baraza la madiwani Wilaya ya Arusha mjini lakutana kujadili bajet ya halmashauri hiyo kwa mwaka 2015/16

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi,Goodluck Ole Medeye akifafanua jambo katika kikao cha Baraza la madiwani kilichojadili bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha mjini kwa mwaka 2015/2016 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 42.7 zimetengwa kusaidia upatikanaji wa huduma za maji,afya na elimu kama vipaumbele vikuu.Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Arusha,Fidelis Lumato,Mwenyekiti wa Halmashauri Saimon Saning`o na kaimu Mwenyekiti Anna Agatha Msuya.Kikao hicho kilifanyika jana katika ukumbi wa Halmashauri.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Arusha Fidelis Lumato akielezea juu bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha mjini kwa mwaka 2015/2016 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 42.7 zimetengwa kusaidia upatikanaji wa huduma za maji,afya na elimu kama vipaumbele vikuu.pembeni yake ni Mwenyekiti wa Halmashauri Saimon Saning`o. Kikao hicho kilifanyika jana katika ukumbi wa Halmashauri.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha mjini wakiwa katika kikao cha Baraza la madiwani kilichojadili bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha mjini kwa mwaka 2015/2016 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 42.7 zimetengwa kusaidia upatikanaji wa huduma za maji,afya na elimu kama vipaumbele vikuu. hicho kilifanyika jana katika ukumbi wa Halmashauri.Picha na Ferdinand Shayo.

JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 52

McDowall amaliza mafunzo ya Siku mbili na Maafisa Mawasiliano mjini Mtwara

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano toka Wizara ya Nishati na Madini Bi. Badra Masoud akitoa somo kwa Maafisa Mawasiliano mara baada ya Mafunzo kutoka kwa Mkufunzi toka Uingereza Bw. Simon McDowell leo Mjini Mtwara
Afisa Mawasiliano wa Ofisi ya Rais Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Kassim Nyaki akitoa somo kwa Maafisa Mawasiliano mara baada ya Mafunzo kutoka kwa Mkufunzi toka Uingereza Bw. Simon McDowell leo Mjini Mtwara
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akimshukuru Mkufunzi toka Uingereza Bw. Simon McDowell mara baada ya kumaliza mafunzo yake ya Siku mbili kwa Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakati wa kikao kazi cha Maafisa Ha oleo Mjini Mtwara.Picha na Hassan Silayo

MKURUGENZI MKUU WA NHC AENDELEA NA ZIARA YAKE MIKOANI

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akiongea na kikundi cha vijana cha Mshikamano Wilayani Muleba alipokitembelea kuona namna kinavtumia mashine zilizotolewa na NHC ili kuongeza ajira kwa vijana. Bw. Mchechu amezitaka Halmashauri za Wilaya nchini kuunga mkono juhudi za NHC kwa kuwapatia vijana maeneo ya kufanyia kazi zao.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akikagua viwanja vya NHC Wilayani Chato vinavyokusudiwa kujengwa nyumba za gharama nafuu ikiwa ni program ya NHC ya kuzifikia Wilaya zote nchini.

PROF. MBWETTE RAIS MPYA WA BARAZA LA CHUO KIKUU CHA PAN AFRICAN

$
0
0

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Tolly Mbwette amechaguliwa kuwa Rais wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afrika (Pan African University) katika uchaguzi uliofanyika jijini Addis Ababa siku ya Jumatano tarehe 28 Januari 2015. Prof. Mbwette ambaye atahudumu nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo, aliwashinda wagombea wengine wanne katika kinyang’anyiro hicho.
Aidha, Bw. Ekwabi Mujungu amechagulikuwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Umoja wa Afrika inayoshughulika na mapambano dhidi ya rushwa kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.
Uteuzi wao unatarajiwa kuthibitishwa na Walkuu Nchi na Serikali wa AU katika mkutano wao utakaofanyika Addis Ababa tarehe 30 na 31 Januari 2015. Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atashiriki mkutano huo.
Seikali kupitia Ubalozi wake wa Addis Ababa chini ya Balozi Naimi Azizi, ulipiga kampeni kuhakikisha kuwa wagombea hao wanashinda nafasi hizo

RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI MAJENGO YA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UFARANSA

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Pamoja naye ni Mama Salma Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Msauni na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Mhe Begum Taj.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha wageni baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wafanyakazi wa ubalozi baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Pamoja naye ni Mama Salma Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Msauni na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Mhe Begum Taj.




ngoma azipendazo ankal

$
0
0

Guns N' Roses - Knocking on heaven's door

MAKALA YA SHERIA: MNUNUZI WA GARI JIHADHARI NA UTAPELI HUU WA KIMKATABA

$
0
0
Na   Bashir  Yakub 

1.KUTAPELIWA  KATIKA  UNUNUZI  WA  GARI.

Ununuzi wa magari sawa na biashara nyingine yoyote unahitaji umakini. Lakini ununuzi wa  gari unahitaji umakini mkubwa zaidi pengine kuliko  mali nyingine yoyote inayohamishika kwa sasa. Hii ni kutokana na kukua kwa biashara ya bidhaa hiyo kulikoleteleza kujipenyeza  kwa matapeli hasa mijini. Utapeli  wa magari ni mkubwa kuliko watu wanavyofikiria na idadi ya wanaotapeliwa kwa siku inaelekea kulingana na idadi ya magari yanayouzwa kwa siku. Si  rahisi kulijua hili kama hufuatilii mambo haya. Uzuri au ubaya, wanaofanya matukio haya ni walewale. Nafasi kubwa wanayotumia ni ulaghai wa kimkataba na wanatumia mapungufu ya mkataba kumtapeli mtu halafu wanaendelea kuwapo na huna la kufanya sababu  mkataba wako una mapungufu ambayo uzito wake kisheria ni kama huna  mkataba. Aliyekutapeli atakuwapo na hutakuwa na la kufanya kwasababu ya msemo wa kisheria usemao “Buyer Be Aware”(Mnunuzi kuwa Makini). Umakini wako ni katika kufanya mkataba utakaolinda manunuzi yako. Lau ukifanya kosa  sheria imeshasema hivyo imemaliza. 

2.MKATABA SALAMA WA KUNUNULIA GARI  LAKO HAKIKISHA  UNA  TAARIFA   HIZI.

( a ) Lazima uwe na majina ya wahusika ambayo yatakuwa yameandikwa kwa urefu  na kwa kueleweka.Mfano jina liwe Aloys Mayenge Archard. Epuka kuandika vifupi  mfano A.M. Archard. Jina linatakiwa liwe katika ukamilifu wake na hasa pawe na majina matatu kamili. Pia majina  ya pande zote mbili yaani muuzaji na mnunuzi yatokee hivyohiyvo  si tu majina ya upande mmoja. Yawezekana mkataba mwingine unahusisha watu wengi zaidi  pia ni muhimu  majina matatu ya kila mmoja yaonekane hata kama  wako ishirini.

MPANGO MZIMA WA RATIBA YA HARAKATI ZA VALENTINE NDANI YA VILLA PARK JIJINI MWANZA

$
0
0
Mpango mzima wa 'Harakati za Valentine ndani ya Villa Park Mwanza, utakao anza rasmi Alhamisi ya tarehe 12/02/2015 ambapo Mfalme Mzee Yusufu na Bendi yake ya Jahazi Mordrn Taarab kuhusika, kiingilio nishilingi 10,000/=

Kisha Jumamosi ya tarehe 14/02/2015 Valentines Day bendi ya Super Kamanyola kutambulisha safu ya waimbaji wake wapya, Kiingilio Sebuleni Tshs 5,000/= na Tshs10,000/= utazama hadi Disco ambako kutakuwa na mpambano wa Ma-Dj NANI MKALI KATI YA DJ TASS (MAGIC FM) V/s DJ EDDY (RFA)
Crew ya bendi yako Super Kamanyola yenye maskani yake Villa Park Kirumba jijini Mwanza.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

BENKI YA CRDB YAZINDUA KAMPENI YA UTUMIAJI WA SimBanking NA FAHARI HUDUMA WAKALA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB imezindua kampeni maalum ya utumiaji wa huduma zake kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’  kupitia kwa mawakala  wa ‘FahariHuduma’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kampeni hiyo ijulikanayo kama ‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei alisema lengo la kuanzisha kampeni hiyo ni kuwakumbusha wateja wake na watanzania wote kwa ujumla umuhimu wa kutumia njia hizo mbadala ili kupata huduma kwa urahisi na uharaka.

Alisema kampeni hiyo inatarajiwa kutoa magari kumi na mbili ambapo kila mwezi mshindi mmoja atazawadiwa gari hilo, pamoja na zawadi ya gari la wateja watakaotumia huduma hizo pia wataweza kujishindia zawadi nyingine mbalimbali zikiwemo solar power, tables na simu za kisasa za mkononi.

“Tunataka kuwavutia wateja wetu kuziamini na kuzitumia zaidi huduma hizi kwani ni sawa kabisa na kupata huduma kupitia matawi yetu,”.

Akielezea namna ya kushiriki  na jinsi mshindi atakavyopatikana, Dk. Kimei alisema kuwa shindano hilo ni la wateja wote wa CRDB watumiao huduma hizo na mshindi atakuwa ni yule mwenye miamala mingi zaidi kwa mwezi husika.

“Mshindi ni yule atakayekuwa amefanya miamala mingi zaidi kwa kutumia SimBanking au FahariHuduma katika mwezi husika, iwe ni kutumia fedha kwenda kwenye akaunti nyingine, au kwenda kwenye mitandao ya simu au kulipia Ankara,” alisema.

Kwa upande wake ,Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi CRDB, Martin Mmari alisema ubunifu ndio njia pekee itakayotatua changamoto, ni muda muafaka kwa Watanzania kuchangamkia fursa hiyo na kujishindia zawadi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari, akikata utepe wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’,  kupitia kwa mawakala wa ‘FahariHuduma’, ijulikanayo kama ‘Tuma pesa na simBanking shinda Passo’ uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, ambapo mtumaji wa miamala mingi katika benki hiyo atapata zawadi ya gari aina ya Passo. Kulia ni mjumbe wa bodi, Celina Mkoni.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei kuzungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’,  kupitia kwa mawakala wa ‘FahariHuduma’, ijulikanayo kama ‘Tuma pesa na SimBanking shinda Passo’ uliofanyika jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi huo.

Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images