Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 721 | 722 | (Page 723) | 724 | 725 | .... | 3278 | newer

  0 0

  The Minister is led into the EALA Chamber by Hon Shem Bageine, Minister for EAC, Uganda, Hon Dr. Nderakindo Kessy (right) and Hon Nusura Tiperu at the back.
  Administration of Oath. The new Minister takes the oath administered by Mr. Obatre Lumumba, the Deputy Clerk of EALA. He is flanked on right by the Minister for EAC, Republic of Uganda, Hon Shem Bageine and Hon Nusura Tiperu and Hon Dr. Nderakindo Kessy, partially hidden.

  CLICK HERE FOR MORE PHOTOS

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika hatua mbalimbali za mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika hatua mbalimbali za mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani,  Rais wa Mali Mhe Ibrahim Boubacar Keïta, Waziri Mkuu wa Norway Mhe. Erna Solbergna Mwenkekiti Mwenza wa Bill&Melinda Gates Foundation, Bw. Bill Gates, wakiwa jijini Berlin, Ujerumani, wakati wa chakula cha mchana cha mazungumzo baada ya kumalizika kwa mkubwa wa kuchangisha fedha katika mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.


  0 0
 • 01/28/15--09:14: FURSA YA AJIRA

 • 0 0  0 0
 • 01/28/15--19:00: ngoma azipendazo ankal

 • Ace of Base - All That She Wants

  0 0

  By Special Reporter, Addis Ababa

  The Heads of State and Government of the African countries participating in the APRM process will meet in Addis Ababa today on the margins of the 24th AU Summit. The theme of this year's meeting will be "2015 Year of Women Empowerment and Development towards Agenda 2063" which is in line with APRM's thematic objective of promotion of women empowerment and gender equality.

  Currently, there are 34 countries participating in the process and Ivory Coast is expected to sign the accession agreement making a total of 35 countries. These countries represent more than 80 percent of the African population. 

  Speaking in Addis Ababa, Ethiopia, the APRM Tanzania Executive Secretary, Rehema Twalib said after operating for about a decade, it has been found imperative to further improve the effectiveness, credibility and acceptability of the Mechanism through integration with the African Union structures.


  0 0

  Mkurugenzi wa Eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA) nchini, Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia akizungumza na Bw. Li Xuhang, Naibu Mkuu wa masuala ya Siasa katika Ubalozi wa China hapa nchini kuhusu mikakati ya Serikali ya Tanzanania katika kuhamasisha uwekezaji nchini katika Maeneo Maalum na kuimarisha ushirikiano na Serikali ya China katika masuala ya uwekezaji kwenye Maeneo Maalum. Mazungumzo yao yalifanyika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
  Ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na EPZA wakifuatilia mazungumzo kati ya Kanali Mstaafu Simbakalia na Bw. Li Xuhang. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Nathaniel Kaaya, Bw. Lamau Mpolo (kushoto), Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo wa EPZA na Bw. Iman Njalikai (kulia), Afisa Mambo ya Nje.
  Mazungumzo yakiendelea
  Kanali Mstaafu Simbakalia akiwaeleza jambo Bw. Li na Afisa kutoka Ubalozi wa China mara baada ya mazungumzo yao. Picha na Reuben Mchome

  0 0

  The Late Mr. Moses Tito Kachima
  Born: 27th January 1945 - Died: 29th January 2013. 

   You have gone too soon but we believe you are in a better place. We loved you but God loved you more. You've left us but your memory and spirit lives on. We will always remember and cherish the times spent with you. You have been a blessing in our lives. 

   Eternal rest grant to him, O Lord and let perpetual light shine upon him. May he rest in peace. Amen

  0 0


  0 0

  The EALA has late this afternoon enacted the EAC Cooperative Societies Bill 2014 giving the cooperative fraternity and stakeholders, something to smile about.  

  The Bill sailed through the third reading after Members debated and made amendments to a number of clauses to reflect relevancy and consistency.

  The object of the EAC Cooperative Societies Bill, 2014 is to provide a legal framework for Co-operative Societies in line with Article 128 of the Treaty for the Establishment of the EAC strengthening the role of private sector as an effective force for developing economies.

  The Bill is divided into ten parts. Clause 3 of the Bill lays down objectives of Cooperative Societies which include: solving problems collectively, co-ordinating knowledge and skills and promoting self- reliance amongst Members. 

  The rest of the areas contained in the Bill deal with the formation, rights and duties of members and privileges. Other areas include the assets and liabilities, settlement of disputes and winding up/dissolution of Societies. 
  Hon Dr. Nderakindo Kessy makes a point on the floor of the House.
  Hon Mike Kennedy Sebalu, the mover of the EAC Cooperative Societies Bill, 2014.


  0 0

  Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Kaskazini Brighthon Majwala akikabithi vitabu kwa Afisa Elimu wa shule za sekondari halimashauri ya Monduli Bwana Shaban Kasim Mgunya kwaajili ya shule ya sekondari Nanja iliyoko Monduli mkoani Arusha. wakishuhudia ni baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nanja.
  Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Kaskazini Brighthon Majwala akikabithi vitabu kwa Afisa Elimu wa shule za sekondari halimashauri ya Monduli Bwana Shaban Kasim Mgunya kwaajili ya shule ya sekondari Nanja iliyoko Monduli mkoani Arusha wakishuhudia kulia ni Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde na kushoto ni mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Nanja Yona Lukas.
  Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde akipitia kitabu na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nanja mara baada ya Airtel kukabithi msaada wa vitabu vya sayansi kwa shule hiyo chini ya mpango wake wa Airtel shule yetu.


  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi akimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Nd. Abdullah Juma Abdullah kuchukuwa hatua ya kuyapeleka TRA Makontena yote yaliyoshindwa kufuata tataribu ambayo yanaleta msongamano ndani ya Bandari hiyo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Nd. Abdullah Juma Abdullah akimkaguza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif baadhi ya maeneo yaliyowekwa makontena ndani ya Bandari hiyo. Balozi Seif alifanya ziara ya ghafla ndani ya Bandari hiyo ili kujionea hali halisi ya utendaji wa bandari ya Malindi,Zanzibar.
  Mrundikano mkubwa wa makontena unaoonekana katika Bandari ya Malindi ambapo baadhi ya wafanyabiashara wanashindwa kutoa makontena yao na kuleta usumbufu kwa watendaji wa Bandari hiyo.Picha na – OMPR – ZNZ.

  0 0

  Wageni mbalimbali wakiingia na kutoka Katika Banda la Watanzania kujione bidhaa za Watanzania Wanaoshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman.
  Msanii wa kuchora Fred Halla akifanya sanaa yake ya Uchoraji katika Katika Banda la Watanzania.Fred ni mmoja wa Watanzania Wanaoshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman. 
  Msanii wa Uchongaji Iddy Amana akiwahudumia wateja katika Banda la Watanzania. Iddy ni mmoja wa Watanzania Wanaoshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman. 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyo chini Wizara ya Fedha anautangazia Umma juu ya upimaji na uuzaji wa viwanja katika mji wa Chalinze (New Chalinze City). 

  Fomu za Maombi zinapatikana katika matawi ya Benki ya Posta ya Azikiwe, Metropolitan na Mkwepu kwa Mkoa wa Dar es Salaam na kwa Pwani zinapatikana katika tawi dogo la Benki ya Posta Bagamoyo na ofisi za Posta Chalinze. 

  Pia maombi yanaweza kufanyika kupitia tovuti yetu ya :
  Au

  Na kulipia katika tawi lolote la Benki ya Posta nchini. 

   Kwa maelezo zaidi soma hapa: ( Att)

  0 0

  Siku zote kumbukumbu za babu zinachekesha saana na mwisho wake unaona kama unaboreka na kumbukumbu zake . Fuatilia hii kupitia mtandao .......

  Kwa Kuangalia Filamu hii ya Kitanzania iitwayo Joti Sanduku la Babu au Kununua na iwe yako kupitia mtandao.

  Ili kuweza kuangalia au kununua kupitia Mtandao unachotakiwa kufanya ni kutembelea tovuti hii


  Pia unaweza kuangalia au kununua filamu nyingine kupitia mtandao huo huo

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akifafanua jambo kuhusiana na mshindi wa shilingi Milioni 100/-kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo ambapo Mkazi wa kilolo mkoani Iringa Bi.Uwezo Magedenge aliibuka na ushindi wa kitita hicho katika droo ya 14 iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam leo,Wengine ni Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania Mrisho Millao(Kushoto) na Afisa wa kampuni hiyo Pristin Lyatonga.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.


  0 0


  Tuzo za bodi yenye uongozi bora katika sekta ya kibenki na bima zijulikanazo kama Best Board Leadership Awards (BBLA) zinatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kesho, ambapo taasisi saba zitashiriki katika tuzo hizo.
  Akizungumza jijini Dar es Salaam hapo jana, Mratibu wa tuzo hizo, Bi. Neema Gerald, amezitaja benki zilizothibitisha kushiriki katika tuzo hizo kuwa ni pamoja na Benki ya Posta (TPB), Benki ya Exim na Benki ya CRDB.
  “Kwa upande wa makampuni ya bima, watakaoshiriki ni Heritage Insurance, Alliance Insurance Corporation, Alliance Life Assurance na Strategis Insurance (T) Limited,” alisema.
  Kwa mujibu wa Bi. Neema, tuzo hizo maalum kwa ajili ya sekta za kibenki na bima ni mpango pekee uliopo unaolenga kutambua mchango wa uongozi bora wa Bodi za Wakurugenzi katika sekta hizo mbili.
  “Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa makampuni yaliyoonyesha mwamko wa kushiriki. Tuzo hizi zinalenga kutambua mchango mkubwa unaotolewa na kundi la watu waliokabidhiwa dhamana ya kufanya maamuzi kwa niaba ya wanahisa,” alisema.
  Kwa mujibu wa mratibu huyo, Tuzo hizi zitatoa fursa ya ufahamu ni kwa jinsi gani bodi bora inaweza kusaidia taasisi kupata mafanikio na kufikia utendaji bora hususani katika eneo walilobobea kiutalaam.
  "Tumeona umuhimu wa kutambua na kuthamini mchango unaotolewa na wakurugenzi wa bodi katika taasisi zao. Tunaamini kuwa katika kila mafanikio ya taasisi ya kifedha, nyuma yake kuna bodi ya wakurugenzi imara na makini. Sasa, sifa hizi ambazo wajumbe wa bodi wengi wanakua nazo zinapaswa kutambuliwa na kuthaminiwa, " alisema.
  Akizungumzia tuzo hizo, Bw. Laurence Mwangoka, Meneja Mauzo wa Hoteli ya Serena, ambayo ni moja kati ya wadhamini, alisema kuwa tuzo hizo zimeanzishwa wakati muafaka nchini kipindi ambapo sekta za Bima na kibenki zinapitia mabadiliko makubwa katika ukuaji wake.
  Mbali na Hoteli ya Serena, wadhamini wengine wa tukio hilo la kipekee ni pamoja na Excel Management and Outsourcing, Fix Agency Ltd, IPP Media,Real PR Solutions, Lilacnshades, Afrimax Strategic Partnerships Limited na Capital Plus International huku wadhamini zaidi wakiaswa kujitokeza.

  0 0

  Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Alphayo J. Kidata akitoa hotuba katika Mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Wanataalum ya Uthamini, Uwakala wa Majengo na Haki za Ardhi, Usimamizi wa Miliki na Maendeleo ya Ardhi Tanzania (TIVEA), Kulia kwake waliokaa ni Kamishna wa Ardhi, Dr. Moses.M.Kusiluka na Makamu Rais wa TIVEA – Hamad Abdallah.Pamoja na mambo mengine, Ndg. Kidata alikemea tabia ya wathamini wanaotuhumiwa kufanya tathmini za nyumba hewa, au kuongeza kiwango cha thamani ya mali kwa kusukumwa na rushwa. Mkutano ulifanyika jana, tarehe 29-30, 2015, Blue Pearl Hotel – Dar es Salaam.
  Pro.Lusugga Kironde akisisitiza kwa Vijana wenye taaluma ya Uthamini kujiendeleza kuboresha fani yao kwa Maendeleo ya nchi, jana katika Mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Wanataalum ya Uthamini, Uwakala wa Majengo na Haki za Ardhi, Usimamizi wa Miliki na Maendeleo ya Ardhi Tanzania (TIVEA), uliofanyika jana, tarehe 29-30,2015, Blue Pearl Hotel – Dar es Salaam.


  0 0

   Balozi wa Tanzania kwenye Nchi za Nordic na Baltic, Mh. Dora Mmari Msechu (kulia) awasilisha Hati ya Utambulisho kwa Rais wa Lithuania,Mh.Dalia Grybauskaitė kwenye ikulu ya nchi hiyo leo.
   Balozi wa Tanzania kwenye Nchi za Nordic na Baltic, Mh. Dora Mmari Msechu akiwa pamoja na Rais wa Lithuania,Mh.Dalia Grybauskaitė mara baada ya kuwasilisha hati ya utambulisho wake,kwenye ikulu ya nchi hiyo leo.
  Balozi wa Tanzania kwenye Nchi za Nordic na Baltic, Mh. Dora Mmari Msechu awasilisha Hati ya Utambulisho kwa Rais wa Latvia,Andris Bērziņš kwenye ikulu ya nchi hiyo.
   Balozi wa Tanzania kwenye Nchi za Nordic na Baltic, Mh. Dora Mmari Msechu akiwa pamoja na Rais wa Latvia,Andris Bērziņš mara baada ya kuwasilisha hati ya utambulisho wake,kwenye ikulu ya nchi hiyo.

  0 0

  ·        Ben Paul, Grace Matata waongezeka kwenye burudani, Mrisho Mpoto na Weusi kusindikiza

  ·        Viingilio shilingi elfu 15 kwenye vituo na elfu 20 mlangoni

  Tamasha la miaka kumi ya THT litakalofanyika jumamosi hii katika viwanja vya Escape 1 Mikocheni, limekamilisha maandalizi yake na hivyo kuwataka wadau na wapenzi wake wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani kubwa ya mziki hapa nchini.

  THT, ambayo inasifika kwa kuzalisha wasanii mahiri nchini kama Linah, Barnaba, Mwasiti, Ditto, Mataluma, Vumi, Beka, Recho, Marlaw, Msami, Makomando na wengine wengi, imejipanga kutoa burudani kubwa ya mziki kwa mashabiki wake.

  Akizungumza kuhusu maandalizi hayo, Meneja Mkuu wa THT, Mwita Mwaikenda alisema maandalizi yanaenda vema na mashabiki wahudhurie kwa wingi kujionea namna kituo hicho kilivyoweza kufanya mapinduzi kwenye tasnia ya muziki.

  ‘Mpaka sasa wasanii wa THT watakaotoa burudani wako tayari, na kama mnavyojua THT utamaduni wake ni kupiga muziki kwa kutumia bendi lakini pia wasanii watakaotusindikiza ni kama Ben Paul, Mrisho Mpoto na Weusi’ alisema Mwita.

  Akizungumzia wadhamini waliojitokeza kwenye shughuli hiyo, Mwita aliwashukuru Mr. Price waliowavisha wasanii wote, Mziiki.Com ya Spice Afrika walionunua tiketi 500 za tamasha kwa ajili ya wateja wao, SanMoto Pikipiki waliotoa pikipiki, Tanzania Fashion and Design Limited, Darling Hair ambao wametoa nywele kwa waimbaji wote wa kike na Clouds Media Group.

  ‘Tunatoa shukrani za dhati kwa wadhamini wetu, kwa kutuunga mkono katika kuadhimisha miaka kumi ya kuleta mapinduzi katika burudani’ alisema Mwita.

  Tiketi za tamasha zinapatikana maduka ya Robby One Fashion Kinondoni na Sinza, Yahya Boutique Kinondoni, Born 2 Shine Mwenge, Ofisi za Clouds, Moca City Samora Avenue, City Sports Lounge, Mr Price na THT Kinondoni.

  Kiingilio ni 15,000/-  kwenye vituo hivyo na kwa wale wanaotaka za VIP ni 50,000/- na zinapatikana THT pekee yake.
  Siku ya onesho pale Escape One, mlangoni kiingilio kitakuwa ni Shs 20,000/=.

older | 1 | .... | 721 | 722 | (Page 723) | 724 | 725 | .... | 3278 | newer