Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109588 articles
Browse latest View live

Ziara ya Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC mikoani

0
0
New Picture (4) 
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu wakikagua eneo lililotengwa kwa ajili ya NHC kujenga nyumba za gharama nafuukatika Halmashauri ya Wilaya Serengeti-Mugumu. Eneo hili lina ekari 134 na miundombinu ya maji na umeme.
New Picture (5) 
Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mugumu Serengeti akimuonyesha Mkurugenzi Mkuu wa NHC ramani ya mpango Miji inayoonyesha eneo la NHC la kujenga nyumba za gharama nafuu.
New Picture (6)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akiongea na kikundi cha vijana Wilayani Serengeti waliyosaidiwa mashine na NHC kwa ajili ya kujiajiri kupitia utengenezaji wa matofali yanayofungamana
New Picture (7)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakikagua jingo la biashara lililojengwa na NHC eneo la Mukendo Musoma.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA.

DRFA yawataka mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi kuzishangilia timu za Dar

0
0
Uongozi wa chama  cha soka mkoa wa Dar es salaam, DRFA,umewaomba,mashabiki na wote wenye mapenzi mema ya kandanda,kujitokeza kwa wingi kuzishangilia timu za Dar es salaam zinazoshiriki ligi kuu,Daraja la kwanza na michuano ya taifa Cup wanawake ,ili kutoa hamasa kwa wachezaji.

Leo (januari 28) kutakuwa na mchezo mmoja wa ligi kuu kwa timu ya Simba ya Dar es salaam dhidi ya Mbeya City ya Mbeya,mchezo ambao utakaopigwa katika uwanja wa taifa jijini.

Itakumbukwa kwamba katika mechi mbili za ligi msimu uliopita,Simba na Mbeya City hakuna aliyefanikiwa kumfunga mwenzake,na kujikuta wakiambulia sare ya 1-1 kule uwanja wa Sokoine,na ule wa marudiano uliopigwa kwenye uwanja wa taifa nao kwenda sare ya 1-1.

Katika michuano ya taifa Cup,Temeke na Ilala zimefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali baada ya kupata ushindi kila moja katika mechi za robo fainali zilizopigwa leo (januari 27),ambapo Temeke imeiangamiza bila huruma Mbeya mabao 3-0,huku Ilala ikiizodoa Iringa kwa mabao 2-1.

Aidha DRFA imeipongeza timu ya Kinondoni ambayo haikufanikiwa kuingia katika hatua ya mtoano,kwa juhudi kubwa na ushindani iliouonesha licha ya kuondolewa katika hatua ya makundi.

Viongozi wa DRFA wamekuwa mfano kwa kujitokeza kushuhudia mechi hizo za Taifa Cup,Ligi kuu na zile za Daraja la kwanza,ili kuongeza chachu kwa timu za Dar es salaam kufanya vizuri.

IMETOLEWA NA AFISA HABARI- DRFA

BENKI YA NMB YAKABIDHI PIKIPIKI TANO KWA JESHI LA POLISI – DODOMA

0
0
Benki ya NMB jana ilikabidhi pikipiki 5 aina ya Honda kwa jeshi la polisi kwaajili ya kusaidia kazi za kila siku za jeshi hilo katika hafla iliyofanyika nje ya ukumbi wa St. Gasper katika mkutano wa maafisa wa polisi unaoendelea mjini hapa.

Pikipiki hizo zilizokabidhiwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani,Mh Mathias Chikawe na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB,Tom Borgols, zina thamani ya shilingi Milioni 10.

Waziri Chikawe alishukuru NMB kwa kuona umuhimu wa kusaidia jeshi la polisi na hivyo kuwataka wadau wengine kuiga mfano huo. “ Tunashukuru sana kwa hizi pikipiki, zitatusaidia sana kuboresha utendaji wa polisi, tutaendelea kuwa wadau wenu muhimu,” aliongeza Mh Chikawe.

Team ya NMB ipo Dodoma kwenye mkutano wa maofisa wa Polisi na kuonesha kuwa inawajali katika kipindi cha mkutano, NMB ina mabanda kadhaa ya maonyesho nje ya ukumbi wa St Gasper huku wakitoa huduma mbalimbali kama kutoa na kuweka fedha kupitia huduma ya NMB Wakala huduma mpya inayoshirikisha mawakala wa MaxiMalipo, Kufungua akaunti kupitia Chap Chap Instant Account pamoja na elimu kwa ujumla juu ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB,Tom Boghols akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani,Mathias Chikawe ufunguo wa pikipiki ambazo NMB imetoa kwa jeshi la polisi kwaajili ya kurahisisha kazi zao za kila siku. NMB ilikabidhi pikipiki 5 aina ya Honda mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini - Ernest Mangu na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Chiku Galawa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi – Mathias Chikawe akiwasha pikipiki iliyotolewa na benki ya NMB kwa jeshi la polisi ili kusaidia operation za kila siku huku akishuhudiwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB,Tom Boghols. NMB ilikabidhi pikipiki 5 aina ya Honda mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini - Ernest Mangu na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Chiku Galawa.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB,Tom Boghols akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,IGP Ernest Mangu wakati walipokutana mjini Dodoma kulikokuwa kukifanyika Mkutano Mkuu wa Maafisha waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini.

BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA AFANYA ZIARA MKOANI KAGERA KUKAGUA ENEO LA KUJENGA CHUO CHA KISASA CHA UFUNDI (VETA) NA KUONA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA MKOA

0
0
Balozi wa China nchini Tanzania,LU Youqing akicheza ngoma ya asili ya Mkoa wa Kagera wakati alipokuwa akilakiwa kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella .
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella akimkabidhi Balozi wa China nchini Tanzania,LU Youqing Hati na ramani eneo lililotengwa na serikali ya mkoa kwa ajili ya kujenga chuo cha Ufundi (VETA) cha Kitaifa kilichoahidiwa na serikali ya China wakati wa ziara ya Rais Kikwete nchini humo mwaka jana. 
Balozi wa China nchini Tanzania,LU Youqing akipokea zawadi ya ramani ya Afrika Mashari iliyochorwa kutoka kwa wanafunzi wa shule ya Mgeza Mseto. 

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

GROOVEBACK NIGHT

UNESCO YATAKA UBIA NA MWEDO

0
0
DSC_0005
Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Maendeleo ya wanawake wa Kimasai (MWEDO), Ndinini Kimesera (kushoto) akimkaribisha Mkurugenzi Mkazi wa Unesco nchini, Zulmira Rodrigues kwenye ofisi za asasi hiyo kwa ajili ya mazungumzo jijini Arusha.

Na Mwandishi Wetu, Arusha
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, limesema kwamba litaingia ubia na asasi ya Maendeleo ya wanawake wa Kimasai (MWEDO) ili kuimarisha mradi wa kijiji cha digitali cha Ololosokwan.

Mradi huo mkubwa unaoendeshwa na Unesco kwa kushirikiana na Samsung umelenga kuinua maisha ya jamii ya wafugaji wa kimasai kwa kuwawezesha kielimu, kitamaduni na kiujasirimali.

Kauli ya kutaka kuingia ubia imetolewa na Mkurugenzi Mkazi wa Unesco nchini, Zulmira Rodrigues wakati alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwedo, Ndinini Kimesera katika ofisi za Mwedo mkoani Arusha.

Alisema Unesco inataka kutumia uzoefu wa Mwedo katika ushirikishaji wananchi hasa katika uwezeshaji ujasirimali na elimu kufanikisha moja ya miradi mikubwa ya kisayansi katika kijiji cha Ololosokwan.
DSC_0031
Mkurugenzi Mkazi wa Unesco nchini, Zulmira Rodrigues (kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Maendeleo ya wanawake wa Kimasai (MWEDO), Ndinini Kimesera (katikati) alipotembelea ofisi hizo jijini Arusha. Kulia ni Mshauri wa kiufundi, usimamizi na tathmini wa MWEDO, Bw. Paul Wilson.

WASANII WATAKIWA KUTOA ELIMU YA UPIGAJI KURA

0
0
Na Mwandishi Wetu

Wasanii nchini wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kutoa elimu ya uraia kwa wananchi ili watambue umuhimu wa kupiga kura na kuwaweka madarakani viongozi wanaowataka.

Wito huo umetolewa mapema wiki hii na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa  (BASATA) Godfrey Mngereza wakati akichangia mada kuhusu Umuhimu wa Jamii kupiga kura kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika makao makuu ya BASATA Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.

“Kama taifa tunazungukwa na matukio mengi yanayohitaji wananchi kupiga kura katika kuamua. Tuna tukio la kupiga kura ya maoni juu ya katiba inayopendekezwa lakini pia uchaguzi mkuu. Wasanii tuna wajibu wa kuwajengea hamasa wananchi kushiriki matukio haya muhimu” alisisitiza.

 Aliongeza kwamba wasanii hawana budi kutambua kwamba wana nafasi kubwa kuhakikisha wanawaelimisha wananchi kuhusu nafasi waliyonayo katika kuamua hatma yao lakini pia kuwa katikati katika kuibua masuala mbalimbali yaliyoko katika jamii ili kuwapa wananchi uchaguzi sahihi linapokuja suala la kupiga kura.

“Wasanii hampaswi kuwa na upande mnapotoa elimu bali wajibu wenu ni kuibua na kuielimisha jamii kuhusu upigaji kura. Suala la nani apigiwe kura na wananchi linabaki kuwa mikononi mwa mwananchi mwenyewe ambaye ndiye mpiga kura” aliongeza.

Awali, wakitoa burudani kwenye Jukwaa hilo la Sanaa, wasanii kutoka kundi la Bongo Artists Foundation linaloongozwa na msanii wa maigizo Christian Kauzeni walitoa elimu mbalimbali kuhusu umuhimu wa wananchi kupiga kura huku wasanii hao wakionesha kwa hisia kali madhara yatokanayo na wananchi kutokupiga kura.

Kundi hilo lililovuta hisia za wadau takribani themanini waliohudhuria kwenye Jukwaa la Sanaa lilionesha madhara ya kutokupiga kura kuwa ni pamoja kupatikana kwa viongozi wabovu wasiyowajibika,kukosekana kwa huduma muhimu za jamii na changamoto nyingine nyingi ambazo zinakwamisha jitihada za wananchi kujikwamua kutoka kwenye ufukara.
Kiongozi wa Kundi la Bongo Artists Christian Kauzeni (Katikati) akizungumza na wadau wa Jukwaa la Sanaa (hawako pichani) wakati Kundi lake lilipotoa elimu kupitia Sanaa za Majukwaani kuhusu umuhimu wa wananchi kupiga kura mapema wiki hii. Kulia ni Afisa Habari wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Aristide Kwizela na Afisa Sanaa wa baraza hilo Ernest Biseko.
Moja ya wasanii wa Bongo Artists akiwauliza swali la Je kutokupiga kura ni uhayawani? Wadau wa Jukwaa la Sanaa wanaomtazama. Msanii huyu alikuwa kivutio kikubwa hasa kwa kuuliza swali hilo la Je Huu ni Uhayawani? Ambalo lilienda sambamba na maudhui ya igizo la kundi hilo.

EALA APPROVES SUPPLEMENTARY BUDGET OF USD 2 MILLION FOR EAC PROGAMMES

0
0
The Assembly late yesterday passed the EAC Supplementary Appropriation Bill 2015 providing a supplementary expenditure to the tune of USD 2,040,520 out of the budget for the Financial Year ending 30th June 2015.

Of the said amount, USD 99,840 will come from the EAC General Reserve Fund while USD 1, 940,680 is to be sourced from development partners.

The supplementary budget allocates USD 919,413 to undertake mediatory and confidence building activities prior to the upcoming May-June 2015 elections. The support from the European Union will assist the EAC/COMESA/AU Early Response mechanism (ERM) – African Peace Facility support to implement activities in the COMESA/EAC region.

It is part of on-going efforts by the regional economic communities to consolidate democracy and promote peaceful elections in the region.The Chair of the Council, Hon Dr. Abdalla Sadaala Abdalla presented the Supplementary Budget for the Financial Year 2014/2015 to the House.

Chair of the Council of Ministers, Hon Dr. Abdallah Sadaala Abdallah addressing the House.


Filamu: Pata Filamu ya KITENDAWILI kupitia Mtandao

0
0
MBAZI ni kijana aliyezaliwa kwenye familia ya kimasikini mkoani kilimanjaro, anakwenda mkoani kigoma huko anapendana na NYAMIZI binti mkimbizi wa kinyarwanda. Anaamua Kumtorosha na kurudi nae kijijini kwao, lakini Mambo yanapozidi kuwa magumu anaamua kwenda Dar Es Salaam Kutafuta maisha akiamuacha Nyamizi akiwa na mtoto mdogo. Akiwa Dar es Salaam anajikuta akiishia jela na kupoteza mawasiliano na familia yake kwa miaka mitatu anamaliza kifungo na kurudi kijijini na KITENDAWILI, mama yake na Mtoto wake walishafariki na mkewe anaishi na mwanaume mwingine na tayari nu majamizito.. Fuatilia hii kupitia mtandao .......

Kwa Kuangalia Filamu hii ya Kitanzania mtandaoni iitwayo KITENDAWILI au Kununua na iwe yako tembelea tovuti ya 


Pia unaweza kuangalia au kununua filamu nyingine kupitia mtandao huo huo

NEPAD YASAIDIA HARAKATI ZA KUTAFUTA CHANJO NA TIBA YA EBOLA - PROF. AMBALI

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb) kulia akiongea na mmoja wa viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Argentina walipokutana jijini Addis Ababa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika.

Na Ally Kondo, Addis Ababa

Nchi za Afrika zimehimizwa kuweka mazingira mazuri na wezeshi kwa ajili ya kufanya tiba na chanjo za maribio dhidi ya ugonjwa wa Ebola. Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu na Mshauri wa Kituo cha Sayansi, Teknolojia na Ubunifu cha NEPAD, Prof. Aggrey Ambali wakati alipokuwa anawasilisha mada kuhusu ugonjwa wa Ebola kwenye kikao cha Kamati ya Uongozi wa NEPAD jijini Addis Ababa siku ya Jumanne tarehe 27 Januari 2015.


Prof. Ambali alieleza kuwa mashirika mengi yanayohusika na udhibiti wa madawa barani Afrika yanakabiliwa na ugumu wa kushughulikia masuala ya kimaadili na kanuni zinazosimamia tiba za majaribio kwenye nchi wanachama.


Alitoa mfano wa masuala ya kimaadili na kisera ambayo yanahitaji ufumbuzi ili kuwezesha kukusanya na kusafirisha damu na plasma kwenye nchi zinazohusika.


Kwa kuliona hilo, NEPAD kupitia Programu ya Afrika ya Kuoanisha Kanuni za Udhibiti wa Madawa inafanya kazi kwa kushirikiana na Jumuiya za Kikanda pamoja na Mashirika ya Kitaifa ya Udhibiti wa Madawa ili kupata nguvu inayohitajika ya kusimamia tiba za majaribio na kushughulikia masuala ya kimaadili.


Kwa msaada wa NEPAD na Shirika la Afya Duniani, Jumuiya ya Afrika Mashariki inafanya tathmini ya pamoja ya chanjo ya Ebola ambayo itafanyika tarehe 02 – 04 Februari 2015. Nchi zinazolengwa kwa ajili ya majaribio hayo ni Tanzania, Uganda na Kenya lakini tathmini ya pamoja itafanywa na nchi zote za EAC.


Prof. Ambali alihitimisha mada yake kwa kusema kuwa tiba za majaribio kwa ajili ya chanjo mbili za Ebola yanafanyika huko Afrika Magharibi na majaribio mengine kadhaa yanatarajiwa kufanyika hivi klaribuni.

TANZANIA LAUNCHES TOURISM PROMOTION ROADSHOWS IN THREE CITIES OF US WEST COAST

0
0
Permanent Secretary, Ministry of Natural Resources and Tourism Dr. Adelhelm Meru delivering his speech during the launching of the tourism promotion campaign in the US West Coast at the Peninsula Hotel in Beverly Hills, California.
 Acting Managing Director of Tanzania Tourist Board Ms. Devota Mdachi giving her remarks during the launching of the tourism promotion campaign in the US West Coast at the Peninsula Hotel in Beverly Hills, California.
Permanent Secretary, Ministry of Natural Resources and Tourism Dr. Adelhelm Meru (right) presenting a Tanzanian wood carving to Vice Mayor of Beverly Hills Julian Gold of as an expression of appreciation on behalf of H.E. Jakaya Kikwete, President of the United Republic of Tanzania during the private VIP reception held at the Peninsula Hotel in Beverly Hills, California, where the tourism promotion campaign was launched.

FOR MORE PICTURES & STORY CLICK HERE

MJASIRIAMALI AJISHINDIA MILION 10 ZA PROMOSHENI YA JAYMILLIONS YA VODACOM

0
0
Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania Mrisho Millao(Kushoto)akihakiki namba ya simu ya mshindi wa promosheni ya JayMillions anayoonyeshwa na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(Katikati)wakati wa kuchezesha droo ya 13 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo Mkazi wa Magu James Mangu amejishindia kitita cha shilingi Milioni 10/-anaeshuhudia kulia ni Afisa wa kampuni hiyo Pristin Lyatonga.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (Katikati) akiongea na mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 10 kupitia promosheni ya JayMillions Mkazi wa Magu mkoani Mwanza James Mangu.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Mkurugenzi wa kampuni ya Mobile Solution,Dimitrios Lintis(katikati)akiwaonyesha namba ya mshindi wa Promosheni ya JayMillions Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania Mrisho Millao na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(Kulia) wakati wa kuchezesha droo ya 13 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo Mkazi wa Magu James Mangu amejishindia kitita cha shilingi Milioni 10/- Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

MGOMO WA WAFANYABIASHARA IRINGA BAADHI WAGOMA KUSHIRIKIA

0
0
Wananchi mbalimbali  wa mji  wa Iringa  wakiwa katika  soko  kuu mjini humo kupata  huduma  zao wakati sehemu mbali mbali huduma  zikiwa  zimesitishwa  kufuatia mgomo  wa wafanyabiashara  nchini, kushinikiza  jeshi la  polisi  kumwachia  huru mwenyekiti  wao  wa chama  cha  wafanyabiashara  nchini Bw  Johnson  Minja anayedaiwa  kushikiliwa na  jeshi la polisi kwa mahojiano.

Baadhi ya Maduka yakiwa yamefungwa kutokana na mgomo unaoendelea wa wafanyabiashara nchini.
Moja  kati  ya  maduka  mjini Iringa yakiendelea  kutoa  huduma  mbali ya  wafanyabiashara  wengine  kuwepo katika mgomo  kushinikiza  kuachiwa  huru kwa mwenyekiti wa  wafanyabiashara  Taifa  Bw  Johnson Minja.

BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI

January Makamba na ndoto ya vituo vya Michezo vya Kanda

0
0
Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa Bumbuli na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Habari na Masoko ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambaye hivi karibuni pia ametangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa January Makamba(Pichani juu)  hivi karibuni ameainisha adhma yake ya kuinua kiwango cha michezo nchini.

Azma hizo zimo katika  katika mazungumzo yake na Padre Privatus Karugendo ambayo yamechapishwa katika kitabu ambacho gazeti hili imekipata nakala yake ambapo ameainisha azma ya kujenga vitua vya michezo vya kanda vyenye hadhi ya kiolimpiki.

Kwenye kitabu hicho, Makamba amejibu swali kwamba kitu gani kifanyike ili Watanzania waweze kujivunia wanamichezo wao. Makamba alisema, “Inafedhehesha sana kuona kwamba asilimia 79 ya Watanzania walikuwa hawajazaliwa mara ya mwisho tumeshiriki katika fainali za kombe la mataifa ya Afrika.

Mwaka huo huo wa 1980 ndio mara ya kwanza na ya mwisho tuliweza kushinda medali za Olimpiki. Rafiki yangu Mzee Suleiman Nyambui na Mzee wetu Filbert Bayi ndio walitutoa kimasomaso kipindi kile. Ni muhimu kurekebisha hili.” 

RAIA WANNE (4) WA ETHIOPIA MBARONI KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI

0
0
Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikila watu wanne (4) raia wa Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini bila kuwa na kibali

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema watu hao wamekamatwa tarehe 26/01/2015 majira ya 15:55hrs katika eneo la Nala kwenye Mzani wa Magari (Weight Bridge) Kata ya Nala Tarafa ya Zuzu Manispaa ya Dodoma wakiwa kwenye basi la Prince Munaa lenye namba za usajili T. 788 CNK likitokea Mwanza Kuelekea Dar es Salaam.

Kamanda MISIME amewataja watu hao kuwa ni:-

1.    SULYAN S/O JEYLAN mwenye miaka 23, Mkazi wa Kolobi – Ethiopia.
2.    KIAR S/O TAHIR HUSSEN mwenye miaka 25, Mkazi wa Agerifa – Ethiopia.
3.    BELAYNEH S/O DANIEL LEMENGO mwenye miaka 22, Mkazi wa Durame – Ethiopia.
4.    GALASA S/O AHMED GELIL mwenye miaka 24, Mkazi wa Robe – Ethiopia wakiwa na hati za kusafiria (Passport) zilizogongwa muhuri wa mwisho mpakani mwa Ethiopia na Kenya eneo la Moyale Border tarehe 16/01/2015.

Pia Kamanda MISIME amesema katika tukio hilo amekamatwa wakala anayehusika na kuwasafirisha watu hao aliyefahamika kwa jina la SULTAN S/O SAID RAMADHANI @ KUSHARUNGA mwenye miaka 31, mkazi wa mtaa wa Mecco Jijini Mwanza ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Kusharunga Tarafa ya Kimani Wilayani Muleba Mkoani Kagera.

Wahamiaji hao walikuwa wanasafirishwa na wakala huyo kuelekea Afrika ya Kusini kupitia Mtwara – Msumbiji hatimaye kufikia Afrika ya Kusini. Aidha watuhumiwa wote wamekamatwa na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

ANKAL AKIWA NA WADAU WA BERLIN, UJERUMANI

0
0
Ankal (wa sita toka kushoto) akiwa na wadau wakubwa wa Globu ya Jamii wa jiji la Berlin alipokutana nao hivi karibuni katiuka jiji hilo. Ankal anasema anawapenda sana wadau wake popote walipo duniani na anawashukuru kwa kuendelea kumuweka pale pale juu ya orodha ya libeneke.

Launch of the European Union Supported "Usafi Iringa-Iringa Sanitation" Project

0
0
The Head of Delegation of the European Union to Tanzania, H.E. Ambassador Filiberto Ceriani Sebregondi and the Deputy Minister for Health and Social Welfare of the Government of Tanzania, Honorable Dr. Stephen Kebwe launched today the "Usafi Iringa - Iringa Sanitation" Project in Iringa region.

With funding from the European Union, ACRA-CCS Foundation, in partnership with Iringa Municipal Council, Iringa Urban Water and Sanitation Authority (IRUWASA), local (MAMADO, IDYDC) and international organisations (BOKU, cewas, CeTAmb and CUAMM) implement the project on integrated environmental sanitation concepts for poor, underserved and peri-urban areas of Iringa Municipality. Through the EU-ACP Water facility Initiative, the project has received more than 2.2 billion Tanzanian shillings (EUR 1.1 million) to increase access to sanitation services and safe drinking water by developing innovative, affordable and environmentally sustainable sanitation systems.

"Our objective is to help Tanzania achieving the water and sanitation MDG (7) which is to halve by 2015, the proportion of people without sustainable access to safe drinking water and basic sanitation; this means targeting the most vulnerable and needy people in rural and peri-urban areas, also leading to better health, education and socio-economic development.", said the EU Ambassador to Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi.

"The project has four result areas, which deal with the identification of sanitation provision systems, the strengthening of the sanitation supply chain, triggering of a behavioral change process in the target communities and finally increasing access to sanitation services and drinking water through construction activities, especially in schools and health facilities", explained Jörg Henkel, the Project Manager of Usafi Iringa Project.

The project is implemented in the four peri-urban wards of Kihesa, Kitwiru, Mtwivila/Mkimbizi and Nduli in Iringa Municipality, and aims to improve “health and hygiene conditions of poor communities living in the peri-urban areas of Iringa municipality, with great attention to environmental, social and economic sustainability of implemented solutions”, coupled with hygiene promotion activities.

VYUNGU VYA RUNGEMBA NI ZAIDI YA UTALII WILAYA YA MUFINDI

0
0
Mmiliki  wa mtandao wa matukiodaima akiwa ameshika kiatu cha michezo (njumu) ya asili  kilichotengenezwa kwa  udongo  ambacho  kinauzwa kati ya Tsh  150,000 kwa  kimoja na  pea moja ni Tsh 300,000.kiatu  hiki ni  moja kati ya  vivutio vya utalii katika  wilaya ya Mufindi  mkoani Iringa vinavyotengenezwa  eneo la Rungemba na kuvutia  watalii  wa ndani na nje.
Baadhi ya  vifaa mbali mbali  vilivyotengenezwa kwa udongo  eneo la  Rungemba  Mufindi  ni  zaidi ya  utalii.
Mmoja kati ya  wanahabari  mkoani Iringa  Mawazo Marembeka akitazama  vyungu eneo la  Rungemba Mufindi mkoani Iringa.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA BIASHARA YA KILIMO KWA NCHI ZA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI LEO

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa Biashara ya kilimo kwa Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki kwenye Hoteli ya serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa FMD yenye makamo yake Nchini Kenya Bw. Fergus Robley wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Biashara ya kilimo kwa Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki kwenye Hoteli ya serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa SUGECO CHAIR Dkt. Anna Temu alipotembelea mabanda ya maonesho ya Biashara ya kilimo kwa Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki kwenye Hoteli ya serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2015.

PROF. LIPUMBA APANDISHWA KIZIMBANI LEO

0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof Ibrahim Haruna Lipumba (katikati) akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo,alipofikishwa kujibu shitaka la kuhamasisha wanachama wa chama chake kufanya maandamano.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof Ibrahim Haruna Lipumba akiwatuliza wanachama na wafuasi wa chama hicho kuacha kelele katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo.
Wanachama na Wafuasi wa CUF wakiimba nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.Picha na Father Kidevu Blog
Viewing all 109588 articles
Browse latest View live




Latest Images